text
stringlengths
0
4.5k
Mkutano utajadili ni kwa jinsi gani Tanzania inajipanga kufaidika na rasilimali ya gesi asilia. Kwa kifupi masuala ya yanayohusu uwekezaji katika gesi asilia, usimamizi na jinsi ya kutumia rasilimali na menejimenti ya mapato yatokanayo na gesi, pamoja na ushiriki wa wananchi katika fursa mbalimbali zinazotokana na ujio wa gesi hiyo. Utayarishaji wa wataalam katika eneo hilo la gesi husani vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na kadhalika.
Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Mkutano wa mwisho wa mwaka wa maafisa mipango ulifanyika mkoani Morogoro tarehe 12 Machi 2010 ambapo uliandaliwa na Wizara ya Fedha. Mada nne zilizowasilishwa na kujadiliwa zilikuwa ni;
i. Wajibu wa wataalamu wa mipango katika Maendeleo ya Uchumi: Mipango ya Kiuchumi, Utekelezaji na Uandaaji wa Taarifa;
ii. Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki;
iii. Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Wafanyabiashara Wadogo na Wakati; na
iv. Ufanisi wa Uwekezaji kutoka nje katika Uchumi wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake leo Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Swahili Time: Katika Hifadhi ya Wanyama Mikumi
Hii ndio picha iliyopata like nyingi Instagram kwa siku moja
Tazama picha ambayo imeweza kupata umaarufu mkubwa sana katika kurasa ya Instagram kwa muda wa siku moja.
Imepata like zaidi ya milioni 8 na comment zaidi ya laki 4.
Mpaka sasa imekaa kwa muda wa siku moja.
Hii ni picha inayomuonesha mwanadada maarufu duniani kwa kazi yake ya muziki pia ni mke wa rapa Jay Z; Anaitwa Beyonce. Hii ndio picha inamuonesha akiwa na ujauzito wa watoto mapacha ambao dunia inataji kuwapokea.
KILIMO CHA MKATABA KUONGEZA UZALISHAJI WA PAMBA
WAKULIMA wa pamba nchini, wamehimizwa kujiunga na kilimo cha mkataba kwa kuwa kina faida na mafanikio kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimba, alisema kilimo cha mkataba kimesaidia kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba na matumizi ya mbegu bora aina ya UK M08.
Pia, alisema kilimo hicho kimesaidia katika usambazaji na matumizi ya viuadudu na upatikanaji wa huduma za ugani.
“Kilimo cha mkataba kimewafanya wakulima wa ukanda wa Magharibi unaojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Tabora, Singida, Kagera na Kigoma, kupata usimamizi mzuri wa sheria na sera za kilimo kupitia maofisa ugani walioko kwenye halmashauri zao za wilaya.
“Kilimo hicho pia kimesaidia kuongeza eneo la uzalishaji wa pamba, matumizi makubwa ya mbegu za kupanda, ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuhakikisha wakulima wengi zaidi wanajiunga na kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba.
“Kwa sasa pamoja na kwenda vizuri, kuna changamoto ambayo bodi ya pamba inaendelea kukabiliana nayo kwa kutoa elimu ya kilimo cha mkataba ambapo tunawaelimisha namna ya kulima kwa kuzingatia vipimo na maelekezo yanayopendekezwa na wataalamu.
“Lakini pia, tunawahimiza wang’oe na kuchoma moto miche ya pamba baada ya kuvuna kwa kuwa wakiiacha inakuwa mazalia ya wadudu waharibifu wa pamba.
“Hivyo basi, lazima iwepo mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji kwa kushirikiana na wakulima, wachambuaji wa pamba, viongozi wa ngazi ya wilaya na Serikali Kuu,” alisema.
Kanuni hizi zipo kila kituo cha polisi, kama kuna wengine hawazisomi huko naomba wasome hapa. Kanuni za maadili za Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wa Arusha anazijua, Mkuu wa Polisi wa wilaya anazijua, na Mkuu wa Upepelezi ambaye kwa namna ya pekee alinikasirikia nisihojiane naye bila shaka naye anazijua.
Haya si maneno yangu, ni ya baadhi ya wakazi wa Arusha, pamoja na hao ambao nimewataja hapo juu. Wanahoji utendaji wa Jeshi la Polisi jijini Arusha lilivyojiaibisha. Lilivyotumika kisiasa bila kutumia akili yake.
Sisi askari wa upande wa polisi jamii wenye nia na mapenzi mema kwa nchi yetu turudie kuzisoma kanuni hizi na maadili yao.
Kanuni hizi zinasema: “Nikiwa ofisa wa polisi nina wajibu wa kutekeleza sheria, wajibu wangu ni kuwahudumia watu, kulinda maisha na mali.
“Kuwalinda wasio na hatia dhidi ya udanganyifu, dhaifu dhidi ya ugandamizaji au vitisho na utulivu dhidi ya vurugu au fujo, kuheshimu haki za kikatiba za raia wote katika uhuru usawa na haki.
“Nitatunza heshima yangu binafsi kama mfano kwa wote, kuwa jasiri wakai wa utulivu na wakati wa hatari. Sitakuwa na dharau au dhihaka, kuwa na uvumilivu na kujali ustawi wa wengine.
“Nitakuwa mwaminifu kimawazo na kimatendo katika maisha yangu binafsi na ya kijamii. Nitaonyesha mfano wa kufuata sheria za nchi na kanuni ya idara yangu. Chochote nitakachoona au kusikia ambacho ni siri au ambacho nimeaminiwa kutokana na wadhifa wangu kitakuwa siri isipokuwa tu pale itakapobidi kufichuliwa katika kutekeleza wajibu wangu.
“Sitatumia kamwe nguvu za ziada bila sababu, ninatambua kuwa beji yangu ni ishara ya uaminifu wangu kwa umma, nitakuwa mwadilifu kwa umma na kwa maadili ya kazi za polisi. Nitajitahidi muda wote kufikia malengo hayo na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, kwa chaguo la kazi ya kutekeleza sheria.”
Je, mbunge huyu angeweza kutoroka kwa sababu ya kauli ya kumwambia Mkuu wa Mkoa kuwa anakuja kama anaenda kwenye “Send Off”? Kama mbunge anakamatwa kwa vitisho hivi, hizo kanuni tunazotaja hapo juu zilizingatiwa?
Maneno haya kwamba: “Sitaingilia au kuruhusu hisia binafsi, chuki, uhasama au urafiki viathiri uamuzi wangu, sitakubaliana na uhalifu.
Je, hapa kulikuwepo na chuki au uhasama katika maamuzi yaliyofikiwa katika kumkamata mbunge huyo?
Kwanini jeshi letu litumike kwa mambo ya aibu hivi? Jeshi letu linazidi kushuka hadhi siku hadi siku sio kwa kuwa kanuni zao ni mbovu, kanuni zao ni nzuri isipokuwa hazifuatwi, na viongozi wakubwa wa jeshi ndio viongozi wa kuvunja kanuni hizi.
Nimeombwa niulize hivi polisi hawakujua suala hili? Kama Lema alikosea sana wakati akiwa Chuo cha Uhasibu kwanini Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) na makachero wote hawakumkamata pale pale? Alifanya kosa hilo baada ya kuondoka?
Hakuna uwezekano wowote kukubali kuwa jeshi letu halitumiki vibaya. Kila tendo lina gharama zake, hili la kumkamata Lema limegharimu heshima ya Jeshi la Polisi. Huo ndio ujumbe niliotumwa niwaambie. Si maneno yangu, mtapima kama mpo tayari kubadilika au la.
MAOMBI YA NAFASI YA KAZI: ANAHITAJIKA MENEJA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA MKURANGA MKOANI PWANI. _ MTANDA BLOG
Home / Uncategories / MAOMBI YA NAFASI YA KAZI: ANAHITAJIKA MENEJA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA MKURANGA MKOANI PWANI.
MAOMBI YA NAFASI YA KAZI: ANAHITAJIKA MENEJA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA MKURANGA MKOANI PWANI.
ANAHITAJIKA Meneja wa Kijiji cha kulea watoto yatima kilichopo maeneo ya Mkuranga, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Awe mwenye uzoefu wa kufanya kazi na watoto wenye umri kuanzia miaka 0 mpaka 22 na awe amepitia ualimu na ustawi wa jamii, awe tayari kuhamia katika eneo la kulea watoto na awe na uwezo wa kuongea lugha za kishwahi na kiingereza kwa ufasaha.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarahe 25/6/2013.
HABARI NA MATUKIO: KAMISHNA MKUU TRA AFANYA ZIARA YA KIKAZI TBL
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati alipoongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi wa taasisi hiyo katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries Limited, kilichopo Ilala jijini Dar e Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (aliyesimama) akielezea ujumbe wa Kamishna Mkuu wa TRA utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Meneja wa Afya na Usalama sehemuya kazi wa TBL Group, Renatus Nyanda (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA (Kulia) na ujumbe wake utekelezaji wa kanuni za usalama wa kampuni kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda ,wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Roberto Jarrin.
Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake wakipata maelezo ya mchakato wa kutengeneza bia kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala-Calvin Martin.
Mtaalam wa kuonja bia wa TBLGroup, Rebecca Semoka, (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake mchakato wa kuonja ubora wa radha ya bia kabla ya kuingia kwenye masoko.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin ( wa nne kulia) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) Charles Kichere ( wa tatu kushoto ) wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa TBL na TRA wakazi wa ziara ya kikazi ya watendaji wa TRA katika kiwanda hicho.
Wiki iliyopita Nchini Marekani idadi wa watu waliokuwa wamejisajili kwenye orodha ya wanaohitaji mshaara wa kutokuwa na kazi ilikuwa ni 234,000. Kiwango ni kikubwa kabisa kupata kurekodiwa ndani ya miezi 6.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wizara ya kazi ya nchi hiyo, kwa mara ya kwanza idadi ya waliojiandikisha kuhitaji mshaara wa wasiokuwa na kazi katika wiki inayoishia Novemba 24 ukilinganisha na wiki iliyotangulia iliongezeka kwa watu 10,000 kufanya idadi kufikia 234,000.
Kuanzia mwezi Mei mpaka hivi sasa Idadi kubwa ya walijisajili kutokuwa na kazi wanaosubiri soko la ajira ilikuwa ni 220,000. Kufikia wiki iliyopita wastani wa watu waliokuwa wakijiandikisha kuhitaji mshahara wa kutokuwa na kazi ilikuwa 4,750 hivyo kufanya idadi kufikia 223,250
Kufikia Novemba 17 jumla ya idadi waliojiandikisha kwenye orodha ya wanaohitaji mshahara wa wasiokuwa na kazi ilifikia milioni 1 laki saba na kumi elfu imefahamishwa.
Rapa Kutoka Marekani, Future Adata na Hip Hop ya Afrika...Afunguka Haya
Hata hivyo, Rapa Future baada ya kunogewa na midundo ya kiafrika amethibitisha kuwa tayari amefanya kolabo na WizKid kutoka Nigeria .
Vanessa Mdee anaendelea kushambulia kwa kasi na haoneshi dalili za kupumzika.
Akiwa anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Nobody But Me’ aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O, Vee Money amesema tayari mkononi ana video ya wimbo mpya.
Serikali ya Mali yatangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge - Afrika - RFI
Serikali ya Mali yatangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge
Raia huyu anajiandaa kupiga kura katika kituo cha uchaguzi cha mjini Bamako katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Mali Agosti 12, 2018 (picha ya kumbukumbu). ISSOUF SANOGO / AFP
Serikali ya Mali imetangaza tarehe ya uchaguzi ujao wa wabunge. Duru ya kwanza ya uchaguzi itafanyika tarehe 28 Oktoba na duru ya pili mnamo Novemba 18.
Tangazo ambalo linakuja siku chache baada ya Ibrahim Boubacar Keita kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 12, hali ambayo ilizua mgogoro wa baada ya uchaguzi.
Katika taarifa iliyotumwa Jumanne kwa jumuiya ya kimataifa, upinzani unasema kuna kesi za wafuasi wake wanaoendelea kukamatwa nchini humo.
Tarehe hiyo ya uchaguzi wa wabunge ilitangazwa na baraza la mawaziri Jumanne wiki hii, kikao ambacho kiliongozwa na Waziri Mkuu, Soumeylou Boubèye Maïga. Na kulingana na sheria, kampeni ya uchaguzi ya duru ya kwanza ya uchaguzi itafanyika kuanzia Oktoba 6 hadi 26.
Tangazo hili linakuja katika mazingira ya kutatanisha, baada ya kiongozi wa upinzani Soumaila Cisse kushindwa katika uchaguzi wa urais kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Mahakama ya Katiba.
Hii ndiyo Ngoma Mpya iliyofanywa na watu wawili; Roma Mkatoliki a.k.a Roma2030 na Bob Junior
Ni ngoma ya pekee inayoonesha ushirikiano wa hatari na wa namna yake kati ya Bob Junior na Roma. kazi imesimamiwa na Sharobaro music
kuonyesha moyo wa dhati kwa Kazi hii NUNUA HAPA
Burundi yatangaza muda wa mwisho wa kutumia mifuko ya plastiki - E.A.C - RFI
Burundi Pierre Nkurunziza Mazingira Uchafuzi wa hali ya hewa
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametoa amri inayopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo na kutoa muda wa mwisho wa kutumia mifuko hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu, kulingana na agizo la rais.
Kwa mujibu wa amri hiyo iliyosainiwa na Rais Nkurunziza utengenezaji, uagizaji, kuhifadhi, uuzaji na matumizi mengine ya mifuko ya plastiki vitapigwa maarufuku kufikia kipindi hicho.
Aidha amri hiyo itatoa ruhusa maalum ya mifuko ya plastiki na malighafi nyingine za plastiki kutumika katika huduma za ufungishaji dawa katika viwanda nchini humo kwa lengo la kukabiliana na uaharibifu wa mazingira
"Kipindi cha miezi 18 kinatolewa, kuanzia baada rais kutia saini nakala hii, ili kuweza kuuza na kutumia mifuko ya plastiki iliyokuwa imehifadhiwa na ile ambayo ilikua iliagizwa nje ya nchi," nakala hiyo imebaini.
Lakini mifuko ya plastiki, vifaa vya plastiki vinavyotumiwa katika huduma za matibabu, katika viwanda na maduka ya dawa" vitaendelea kutumiwa kwa masharti, imeongeza nakala hiyo.
Nchi nyingine za Afrika tayari zimeanza kupikabiliana na uchafuzi wa vifaa na mifuko ya plastiki, kama vile Morocco, Rwanda na Kenya, ambazo zilipiga marufu matumizi ya mifuko ya plastiki.