text
stringlengths
0
4.5k
MKUTANO WA BIASHARA
▪ Je Ungependa Kupata Mualiko Maalum Kuhudhuria Kwenye Mafunzo Makubwa Ya Ujasiriamali Kama Haya Bureee? Yatakayo Kukutanisha Na Wafanyabiashara Na Wamiliki Wa Biashara Kubwa Na Wadogo.
▪ Nikupe Maelezo Zaidi Ya Namna Ya Ushiriki Wako Wa Event Hii.
Labels: MKUTANO WA BIASHARA
Lakini inakubaliwa hadhi ya "dini" katika nchi ya Marekani, Australia na nyingine chache, kwa sababu toka mwanzo imehusishwa na makosa mbalimbali ya jinai, hususan ujasusi, utapeli na kuathiri hali ya nafsi ya wafuasi wake.
Kadiri ya hesabu yake, hao mwaka 2005 walikuwa milioni 8, lakini watu wa nje wanakadiria kuwa ni nusu milioni tu.
Makao makuu ya Scientology yako Marekani, katika kijiji cha Clearwater.
Jina linatokana na neno la Kilatini "scio" (yaani "najua" kwa maana pana), na neno la Kigiriki "logos" (yaani "somo").Historia ya Scientology inaendana kabisa na maisha ya mwanzilishi wake ambaye tangu miaka ya 1930 aliandika vitabu vya ubunifu mkubwa, mpaka alipojingiza katika masuala ya saikolojia akipinga kabisa misingi na maelekeo ya sayansi hiyo.
Kisha kupata umaarufu wa muda mfupi, akaelekea upande wa roho, aliyoiona haitegemei mwili wala akili, ila inavitumia ili kutenda ulimwenguni.
Kuanzia miaka ya 1960 alifukuzwa na nchi mbalimbali na kuhukumiwa na mahakama tofautitofauti.
Scientology imeitwa "dini ghali" kuliko zote duniani. Kila huduma inatolewa kwa bei iliyopangwa na uongozi wa juu.
Kuna kitu unafahamu zaidi?
MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MARCH 24,2018 - HABARI ZA JAMII
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umetangaza kusitisha maandamano waliyokuwa wamepanga kuyafanya Jumatano hii ili kuunga mkono juhudi na kazi inayofanywa na Rais Dk John Magufuli.
Umesema kuwa umepokea majibu ya barua yao kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu inayowataka kuacha kufanya maandamano yao kwa sababu polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na maandamano nchi nzima.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka, ilisema mbali na barua hiyo pia wamefikia uamuzi huo unatokana na utii, nidhamu na kuzingatia utaratibu wa mamlaka za juu ndani ya chama.
Home burudani Headlines mpya za mtoto wa pili wa Diamond Platnumz Instagram
Headlines mpya za mtoto wa pili wa Diamond Platnumz Instagram
Siku chache baada ya star mwimbaji Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari kupata mtoto wa pili ambaye alizaliwa December 6 2016 tayari mtoto huyo ameanza kuzichukua headlines baada ya kupewa jina na kufunguliwa akaunti ya Instagram ambayo mpaka kufikia leo imefikisha followers zaidi ya 26.5 elfu.
Zari alijifungua saa 10:35 alfajiri katika Hospitali ya Netcare Pretoria South Africa, Pamoja na kuwaomba mashabiki wake kumsaidia kupata jina la mtoto wake ambaye ni wa wakiume, Diamond na Zari wameamua kumuita mtoto huyo jina la Riaz Nasib Abdul huku ikisemekana kuwa ni kinyume cha jina la Zari “Riaz”.
Ikumbukwe kuwa mtoto wa kwanza Diamond na Zari, Princes Tiffa amefikisha followers zaidi ya milioni 1 na kuwa mtoto wa kwanza barani Afrika kuweka rekodi hiyo.
VIDEO: Diamond alichojibu kuhusu stori za mtoto kuwa sio wake na watoto aliowakuta na Zari.
Msanii wa muziki nchini Nigeria D’banj amepata pigo mara baada ya mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja, Daniel iii aliyezaa na mke wake Didi kufariki dunia.
Vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa mtoto huyo amefariki dunia mara baada ya kuzama kwenye maji siku ya kuamkia jana.
Bado D’banj hajazungumza jambo lolote juu ya kifo cha mtoto wake Daniel, aidha katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram amepost picha nyeusi iliyosindikzwa na maneno yaliyosema
Mungu aipumzishe roho ya malaika Daniel iii mahali pema peponi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Dr. Nabil Elaraby. Mazungumzo yao yametawaliwa na hali inayoendelea nchini Syria, Libya na hali nzima ya mchakato wa amani Mashariki ya Kati.
Kwa pamoja wamesisitiza haja ya kukomesha umwagaji damu nchini Syria haraka iwezekanavyo pia kushughulikia haraka mahitaji muhimu ya kibinadamu nchini humo.
Katibu Mkuu amekaribisha hatua zilizopigwa na amehimiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa.
WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WAKIFURAHIA MANDHARI YA MKOA WA DODOMA.... - Boss Ngasa Official Website
Home burudani WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WAKIFURAHIA MANDHARI YA MKOA WA DODOMA....
WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WAKIFURAHIA MANDHARI YA MKOA WA DODOMA....
Marekani imeutaja ushuru wa forodha uliowekwa na China kwenye bidhaa zake kama “sio haki”, baada ya China kuweka ushuru wa bidhaa 128 zenye thamani ya dola bilioni 3, zinazoingizwa na Marekani nchini humo.
Bidhaa, zilizowekewa ushuru na China, ni pamoja na matunda na nyama ya nguruwe, ikiwa ni hatua za karibuni zaidi za ulipizaji kisasi kufuatia Marekani kupandisha ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na bati kutoka China.
Aidha, hatua hiyo ya China imekuja baada ya mvutano mkali kati ya nchi hizo kutokana na masuala ya kibiashara, ambapo hofu kubwa ilikuwa ni kutokea kwa vita ya kibiashara kati ya mataifa hayo yenye nguvu za kiuchumi duniani.
Serikali ya Rais Donald Trump imesema ushuru wake ulilenga bidhaa za chuma cha pua na bati zinazoingizwa nchini Marekani ambazo ilizichukulia kama tishio dhidi ya usalama wa taifa hilo.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Taro Kano akiwa mjini Tokyo ameelezea wasiwasi wake kwa kuhusiana na hatua hizo za kisasi kati ya Marekani na China, na kusema kwamba zinaweza kuwa na matokeo makubwa kiuchumi.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mhe Peter Msigwa amewekwa ndani kwa saa chache na kupigwa marufuku na jeshi la polisi wilayani Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kuzungumza na wananchi wa jimbo la Iringa iliyoanza jana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Msigwa alipata kibali cha kufanya mikutano ya kuhamasisha maendeleo, kusikiliza kero za wananchi wa Iringa na kuzitafutia ufumbuzi.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimlisha chakula Narsa Ramadhan (2) akiwa na mama yake Tatu Saleh (kushoto) wakati wa hafla ya chaku...
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KUTOKA SERIKALINI MAY 27
Kula kabla ya adhaana baada ya jua kuzama
Je, mambo haya yanafaa kwa mfungaji?
DALADALA namba T274 DEX,(pichani), lililokuwa likisafiri kutoka Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke jijini Dar es Salaam, limeanguka mita chache kutoka kituo cha Daladala Sabasaba-Mbagala leo asubuhi Agosti 11, 2016 na kujeruhi watu kadhaa.
Polisi wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya kuliondoa gari hilo zilianza.
Abiria wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.
Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
Polisi wa usalama barabarani, akikagua mazingira ya ajali hiyo huku akizungumza na simu yake ya mkononi
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela ameungana na wananchi katika zoezi la kutoa mwili wa mchimbaji madini kwenye mgodi wa Nyakavangala wilayani humo.
Mkuu huyo wa wilaya aliwatahadharisha wachimbaji hao kuchukua tahadhari wakati wa kufanya shughuli zao ili kuepuka ajali kama hiyo iliyomkuta mchimbaji huyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu muda.
Nape akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya katiba"alisisitiza Nape.
Lakini Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya helkopta.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa UWT wa wilaya ya Kisarawe mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Kisarawe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye leo amefanya ziara kwenye wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa wilaya ya Kisarawe waliojitokeza kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Kisarawe.
Daktari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Dk.Happiness Ndosi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye hospitali ya wilaya ya Kisarawe .
Daktari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Dk.Happiness Ndosi akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye hospitali ya wilaya ya Kisarawe .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pole wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya kisarawe ambapo alijionea maendeleo katika kuboresha huduma za kinana mama na watoto.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Manerumango sokoni ambapo alisisitiza CCM ndio chama pekee kinachozungumzia maendeleo ya mtanzania kwa sasa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akijibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Maneromango sokoni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa na viongozi wengine wa CCM kwenye meza kuu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Maneromango sokoni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma kadi ya aliyekuwa Katibu Kata wa Chadema Shaban Juma Some aliyerudi CCM, zaidi ya watu 30 wamejiunga na CCM leo wakitokea CUF na CHADEMA.
Uingizaji Data Utangazaji wa Facebook Utangazaji kwa Makundi ya Kijamii Msaidizi wa Mtandao Tafuta Mtandaoni
Kutangaza Kwa Wingi Utangazaji wa biashara ukitumia Barua Pepe Utangazaji wa Biashara Mtandaoni Utangazaji wa bidhaa
OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKABIDHI VIFAA VYA KUTAMBUA GESI ZINAZOHARIBU NA ZISIZOHARIBU TABAKA LA OZONI (REFRIGERANT IDENTIFIERS) KWA CHUO CHA VETA NA SHIRIKA LA VIWANGO TBS.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto) akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kwa Afisa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bwana Arnold Mato, wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akipeana mkono na Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Chuo cha ufundi Stadi VETA-Chang'ombe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya vinavyotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu tabaka la ozoni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bibi Magdalena Mtenga akijadiliana jambo na Wawakilishi toka TBS na VETA-Chang'ombe mara baada ya makabidhiano hayo.
Mfanyabiashara Said Lugumi akiongozwa na Ofisa wa Polisi kuelekea ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola baada ya kutoka Makao Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.(Picha na Jeshi la Polisi)
Ujuzi: Android, Kujaribu Kitufe cha Simu, Ujenzi wa Software
Hapa ndipo wanapopikia chakula wakati wa usiku kwakweli ni hali ya hatari sana
Hapa wakinawa kutokana na hali ya uchafu waliokuwanayo baada ya kumaliza kufanya usafi nyumba yao
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda kata ya Iyela Jijini Mbeya akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi mitano bila huduma za msingi ikiwemo chakula na sare za shule.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka huu eneo la nyumbani kwake alikokuwa amewatelekeza watoto hao.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria dhidi yake baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili kesi iliyombele yake.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa uchunguzi unafanyika ili kesi iweze kufunguliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vikomeshwe.
Wakati huo huo maisha wanayoishi kwa sasa watoto hao Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila huduma za msingi wasamaria wema wameombwa msaada wao wa hali na mali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada kutoka kwa walimu na baadhi ya watu ambao huwapa unga na maharage na wao hulazimika kutafuta fedha za kununulia mahitaji mengine kama mafuta ya kula na taa.

Swahili: CC-100: Monolingual Datasets from Web Crawl Data

This is a Swahili corpus obtained from CC-100: Monolingual Datasets from Web Crawl Data

Downloads last month
120

Space using mwitiderrick/swahili 1