input
stringlengths
5
25.1k
label
stringclasses
6 values
NEW YORK, Marekani MSHAURI wa  Usalama wa Taifa nchini hapa, John Bolton ameionya Serikali ya Syria akisema isidhani kuwa hatua inayosubiriwa ya kuondosha majeshi kutoka nchini humo kama ni ruhsa ya wao sasa kutumia silaha za kemikali. Mshauri huyo aliyasema hayo juzi na kwamba msimamo wa serikali ya nchi hii hauna mabadiliko dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali ambazo zinatumiwa na serikali ya Syria. “Hakuna kabisa mabadiliko juu ya msimamo wa Marekani dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali zinazo tumiwa na utawala wa Syria. “Hakuna mabadiliko kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali yatakabiliwa na hatua kali sana, kama tulivyokuwa tumefanya mara mbili hapo awali,” Bolton aliwaambia waandishi akiwa katika ndege yake muda mfupi kabla ya kutua mjini Tel Aviv nchini  Israel. “Kwa hiyo utawala wa Assad usijidanganye juu ya suala hilo, wakati tukifafanua jinsi utaratibu wa kuondoa majeshi utakavyo kuwa na mazingira yake, hatutaki utawala wa Assad kuangalia hatua hii kuwa inapunguza shinikizo letu dhidi ya matumizi ya silaha za maangamizi ya umma,”aliongeza Bolton.
KIMATAIFA
NA ESTHER GEORGE MSANII wa Bongo Fleva, Athumani Mwingereza ‘Tanzanite’, ameibuka na kudai kwamba wimbo wa ‘Mbagala’ wa msanii, Nasib Abdul ‘Diamond’, umemuweka katika wakati mgumu tangu alipourudia na kuuita ‘Kafara’. “Wimbo ule nilitumia mdundo wa wimbo wa ‘Mbagala’ nikauita ‘Kafara’, wimbo huo umenisababishia changamoto nyingi sana ikiwemo ya kutokuaminika kwa wadau wengi wa muziki na hata mashabiki wangu hata ninapotoa wimbo mpya. “Kwa sasa nafanya muziki wangu lakini katika wakati mgumu kwa kuwa nimekosa kabisa watu wa kusaidia kunirudisha kama nilipokuwa, wengi wao hawaamini kama nina uwezo na kipaji cha kutunga na kuimba mwenyewe lakini pia baadhi ya waliokuwa wakinisaidia wapo kwa msanii huyo hivyo tangu niimbe wimbo huo wamesitisha msaada kwangu,” alieleza kwa masikitiko. Hata hivyo, Tanzanite amewataka mashabiki wake wamsamehe na wasahau yaliyopita kwa sasa ameamua kusimama mwenyewe bila kutumia mgongo wa mtu kuwa juu kisanii.
BURUDANI
LONDON, ENGLAND KOCHA wa timu ya Arsenal, Mikel Arteta, ameweka wazi kuwa, kwenye kikosi chake kuna shida ya mchezaji kiongozi ndani na nje ya uwanja. Mshambuliaji wa timu hiyo Pierre Aubameyang kwa sasa ndio wa nahodha wa timu hiyo akichukua nafasi ya Granit Xhaka tangu Oktoba mwaka jana baada ya mashabiki wa timu hiyo kumzomea wakidai hana mchango wowote na timu. Wakati timu hiyo ipo chini ya kocha Unai Emery, alikuwa anabadilisha nahodha, hivyo jumla alitumia watano ambao ni Aubameyang, Xhaka, Hector Bellerin, Alexandre Lacazette na Mesut Ozil. Lakini baada ya wachezaji kupiga kura mwanzoni mwa msimu huu jina la Xhaka likajitokeza sehemu nyingi kabla ya Aubameyang kuja kuchukua nafasi hiyo. Kutokana na mwenendo wa timu hiyo, Arteta amedai timu hiyo inahitaji nahodha ambaye atakuwa anafanya majukumu yake ndani ya uwanja na kuleta mafanikio makubwa. “Lazima tuwe na nahodha mwenye mchango mkubwa ndani ya kikosi, aweze kuwa na ushawishi kwa ajili ya timu, hata mashabiki wamekuwa wakihitaji nahodha wa namna hiyo. “Kuna sababu nyingi za mchezaji kuwa nahodha, zingine zinakuwa ngumu kuzifikia, lakini kwa sasa ninaamini hakuna shida hiyo ya nahodha kwa kuwa mambo yanakwenda sawa, hivyo hakuna sababu ya kubadilisha nahodha wakati kuna mambo mengine mengi ya msingi ya kuyaangalia, ila ukifika wakati nitafanya maamuzi hayo. “Nimewahi kuwa kwenye klabu ambayo ina manahodha watano. Hiyo inakuwa moja kati ya timu yenye viongozi wengi kuliko nahodha. Lakini mwisho wa siku mmoja ndiye ambaye anavaa kitambaa na wengine wanabaki kama wachezaji viongozi,” alisema kocha huyo. Aliongeza kwa kusema, anaamini nahodha ana umuhimu mkubwa sana ndani ya kikosi, lakini muda bado haujafika wa kufanya mabadiliko, kitu cha msingi nahodha aliyopo kuhakikisha anatekeleza wajibu wake.
MICHEZO
KENYA sasa inaweza kuuza maparachichi nchini Afrika Kusini. Nchi hiyo imefungua soko la matunda hayo lililolifungwa kwa takribani miaka 11 iliyopita.Hatua hiyo, imetokana na mazungumzo yaliyofanywa na wawakilishi wa serikali za nchi hizo mbili wakiwemo mawaziri wanaohusika na kilimo na biashara.Mamlaka ya udhibiti wa bidhaa nchini Afrika Kusini iliweka zuio la kufanyabiashara ya maparachichi na Kenya baada ya kugundulika kuwepo kwa mdudu anayejulikana kama Bactrocera Invadens).Mdudu huyo anayeaminika kutokea katika nchi za Asia, alionekana kwa mara ya kwanza nchini Kenya mwaka 2003 na kusambaa na kuathiri mazao mengi ya matunda nchini humo.Soko hilo jipya la maparachichi baina ya nchi hizo mbili, lilifunguliwa rasmi Julai 24, mwaka huu na mamlaka nchini Afrika Kusini kwa kuandika barua kwa Waziri wa Kilimo na Biashara nchini Kenya.Mapema, katika jitihada za kufungua soko hilo Kenya ilitakiwa na Afrika Kusini kuitengeneza maeneo ya mashamba yasiyoathiriwa na wadudu na kuyatengeneza mazingira ya ubaridi.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Sera kutoka Wizara ya Kilimo, John Mwaniki Kenya ilibidi ikitane na mamlaka nchini Afrika Kusini kuzungumzia suala hilo la kufungua soko la maparachichi ambapo mazungumzo hayo yalifikia muafaka.
UCHUMI
WATU 10 kutoka vijiji mbalimbali vya Kata ya Ruhembe na Kidodi Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wanadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.Hadi sasa wamefikisha siku 21 tangu Aprili 2, mwaka huu baada ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Watu hao wote wakiwa ni wanaume wanadaiwa walikwenda katika shughuli za kilimo katika mashamba yao yaliyopo Kitongoji cha Kitope kilichopo mpakani mwa Hifadhi yaTaifa Mikumi, ambapo hawakurejea tena nyumbani kwao tangu siku hiyo walipoondoka.Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Ruhembe wilayani Kilosa, Salum Mponzi akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili jana, alidai watu hao walikwenda shambani kulima.Kwamba baada ya kumaliza shughuli zao, waliacha vifaa vyao na kisha kuvuka mpaka kuingia hifadhini kuokota kuni na tangu siku hiyo hawajaonekana tena. Alisema mara baada ya kupatikana kwa taarifa za kupotea kwao, walitoa taarifa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Ruhembe na kwa kushirikiana na polisi walienda Ofisi ya Hifadhi Mikumi, lakini hawakuwaona.Diwani huyo alisema watu hao, walitumia usafiri wa pikipiki tatu na baiskeli mbili walipoenda shambani siku ya tukio hilo. Kwamba baada ya kupotea, timu ya kuwatafuta ilifanikiwa kukuta pikipiki mbili, kati ya tatu, zikiwa zimechomwa moto na baiskeli mbili.“Hakijulikani kilichowapata kwa vile hakuna ushahidi uliopatikana, hadi sasa haijulikani walipo na juhudi za kuwatafuta zinaendelea,” alisema Mponzi. Alisema taarifa iliyowasilishwa kwake na Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Ruhembe, Afrodisius Kashaba ilitaja majina ya watu waliopotea kuanzia Aprili 2, mwaka huu kutoka kijiji hicho na vingine kuwa ni Adamu Majambo na Kaimu Majambo ( familia moja).Wengine ni Said M. Mrisho, Elia Haongo, Gabriel Matei, Luka Oswad na Hemed Sawaya. Wengine waliotambuliwa kwa jina moja moja ni Sadick, Johnsen na Chaumwe.Awali, wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara Aprili 18, mwaka huu kijijini hapo ambao uliitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, Diwani wa kata hiyo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruhembe, Mohamed Kapyale walisema wao hawajui watu hao wapo wapi hadi hivi sasa. Kamanda Mutafungwa alienda katika kijiji cha Ruhembe na kuwaeleza wananchi juu ya jitihada ambazo jeshi hilo linafanya, kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa Mikumi na viongozi wa serikali.Alisema jeshi la polisi linajitahidi kuwatafuta watu hao, tangu zilipotolewa taarifa za kutokea kwa tukio hilo. “Tangu Aprili 3 mwaka huu tulipopata taarifa kidogo za kusikitisha na za kushitua kwa watu 10 hawaonekani ...nilipokea taarifa hii kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya na mara moja nilielekeza lifunguliwe jadala na kuanza kufanya msako wa kuwatafuta watu hawa,” alisema Mutafugwa kwenye mkutano na wananchi.Kamanda Mutafungwa alisema katika kufanikisha kazi hiyo, waliwasiliana na kushirikiana na askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Mikumi, baada ya kutolewa kwa kibali cha kuendesha msako wa pamoja wa kuwatafuta watu hao.“Nawaomba wananchi muwe na subira kipindi hiki msako unapoendelea,” alisema Mutafungwa. Aliwaonya wananchi wote wanaoishi jirani na hifadhi za taifa, kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kukata mkaa, kilimo na ujangili. Alisisitiza kwamba atakayekamatwa, atachukuliwa hatua za kisheria.“Wananchi acheni tabia ya kwenda ndani ya hifadhi ya wanyamapori bila kupata kibali maalumu kutoka mamlaka husika kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za nchi,” alisema Mutafungwa. Kata ya Ruhembe ina jumla ya vijiji vinne vya Ruhembe, Kidogobasi, Kielezo na Kitete Msimbazi. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, kata hiyo ina ya wakazi 16, 492.
KITAIFA
*Uteuzi wake wapingwa, viongozi wagawanyika Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM UTEUZI wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo. Mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uteuzi huo, ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa jumuiya hiyo wamedai kuwa haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo. Vyanzo vya kuaminika kutoka katika umoja huo vimeliambia MTANZANIA kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa UVCCM hawakushirikishwa katika uteuzi huo uliofanywa na kigogo mmoja wa umoja huo. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa uteuzi huo haukushirikisha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wala Baraza Kuu la UVCCM, ambalo halikukutana kumthibitisha Jokate kama kanuni zinavyoelekeza. Kwa mujibu wa kanuni za jumuiya hiyo, wajumbe wa kamati ya utekelezaji hawazidi 10, ambapo miongoni mwao ni Mwenyekiti wa umoja huo Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na mjumbe mmoja kutoka makao makuu ya chama. Wajumbe wa baraza kuu ni wenyeviti na makatibu wa mikoa na mjumbe mmoja kutoka katika kila mkoa. SHAKA ATOA NENO Kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni mvurugano ndani ya umoja huo, MTANZANIA lilimtafuta Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka,  ambaye alikiri Jokate kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo na kusema kuwa uteuzi huo ulifuata taratibu zote za chama. “Ni kweli amekaimishwa kwa kufuata taratibu zote za chama, kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilikutana Aprili 18, mwaka huu, Dar es Salaam na ndicho kimewakaimisha wakuu wa idara watano akiwamo Jokate. “Hao wanaolalamika hawajui kanuni na taratibu za jumuiya yetu, huwezi kupata nafasi kama kikao cha Kamati ya Utekelezaji hakijakaa,” alisema Shaka. Hata hivyo alikiri kutoitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kuthibitisha uteuzi huo, akisema ni gharama kubwa kuitisha kikao hicho. “Kwa kawaida Baraza Kuu huwa linakutana kila baada ya mwaka mmoja, kuita baraza kuu ni gharama sana hivyo ikitokea kuna nafasi wazi Kamati ya Utekelezaji ina mamlaka pia ya kumthibitisha,” alisema. JOKATE AZUNGUMZA Akizungumza na MTANZANIA, Jokate alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuifanya jumuiya hiyo iwe karibu zaidi na vijana wa Kitanzania. “Nashukuru kwa imani waliyoonyesha viongozi wangu ila zaidi kuona nina uwezo wa kuongoza idara hiyo nyeti na muhimu kwenye jumuiya. “Kikubwa ni kuifanya jumuiya iwe karibu zaidi na vijana wa Kitanzania na kurudisha tumaini na kusimamia changamoto wanazozikabili vijana katika kujiletea maendeleo,” alisema Jokate. Jokate pia alikuwa miongozi mwa wanachama 450 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Jokate alianzia kwenye mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambapo aliibuka mshindi wa pili. Hivi sasa anajishughulisha na sanaa na ujasiriamali ambapo anamiliki Lebo ya Kidoti Fashion inayojihusisha na uuzaji wa nywele na mavazi. MADAI YA MALIMBIKIZO Katika hatua nyingine, baadhi ya watumishi wa jumuiya hiyo wamelalamikia madai ya malimbikizo ya uhamisho na likizo. Miongoni mwa watumishi hao wamo makatibu wa wilaya na mikoa ambao wamekuwa wakihamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao. Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina gazetini, watumishi hao walisema wana hali ngumu kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu, hali inayotishia utendaji wao. Katibu mmoja wa wilaya ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema anadai malimbikizo ya zaidi ya Sh milioni 20 kutoka mwaka 2010 tangu alipoanza kuhamishwa vituo mbalimbali vya kazi. Mtumishi alisema hatua hiyo ni kinyume na maazimio ya Mkutano Mkuu wa UVCCM wa nane uliofanyika Oktoba 2012 mkoani Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine uliazimia kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi wake wote yanayohusu gharama za uhamisho, posho ya likizo, matibabu na nyingine. “Malimbikizo ni mengi mimi nadai zaidi ya Sh milioni 20, wapo wanadai milioni 30 na wengine hadi milioni 50, unapewa barua ya uhamisho bila kulipwa stahiki zako, huko unapoenda utaishi vipi? “Watumishi wanajiingiza kwenye mikopo ili kupata fedha za kujikimu na wengine wanakua ombaomba, tena ukikuta mtumishi kama ni mwanamke anaambiwa nenda kule utamwona kamanda, hiyo ni sawa na kumuuza huyu mtumishi,” alisema. Alipouliwa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka alisema malimbikizo hayo ya watumishi yanalipwa kadiri fedha zinavyopatikana. “Hii ni taasisi ya chama ina taratibu zake, kuna utaratibu mzuri na malimbikizo yote yanalipwa kutokana na hali ya kifedha iliyopo…hivyo ni vitu vya kawaida hata serikalini mfumo huo upo. “Kama sasa hivi tunakabiliana na chaguzi mbalimbali, tunapunguza malimbikizo lakini wakati huo huo tunajiandaa na uchaguzi,” alisema Shaka.
KITAIFA
Na NORA DAMIAN -DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, ameyaomba mashirika na taasisi za fedha duniani kusaidia nchi zinazoendelea kwakusimamisha kwa mwaka mmoja malipo ya madeni ili fedha zinazookolewa zitumike kukabili virusi vya corona. Pia ameshauri watu wote ndani walio katika hatari ya ugonjwa wa corona, wapimwe kuzuia kusambaa kwa maambukizi.  Akizungumza jana, alisema iwapo mashirika ya kimataifa yatakubali, fedha zitakazookolewa zitasaidia kujenga mfumo wa afya utakaosaidia watu masikini na kurejesha hali ya uchumi katika hali ya kawaida.  “Mataifa mengi hasa ya Afrika yanatumia fedha nyingi kuhudumia madeni yao hasa ya nje. Iwapo taasisi kama Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)na nchi zilizoendelea zitasimamisha kutaka kulipwa riba ya madeni haya, nchi zetu zinazoendelea zitapata nafuu na kupata fedha za kusaidia kukabiliana na virusi vya corona,” alisema Maalim Seif. Maalim Seif pia alishauri Serikali zote kuchukua hatua za dharura za kupunguza makali ya kiuchumi kwa wananchi.  “Kila mmoja wetu anayejiita kiongozi ana wajibu wa kumlinda mwananchi maskini anayeteseka na kadhia hii. “Ipo haja kubwa ya kujipanga, kwamba iwapo tutafikia kipindi cha kuwataka watu wabaki majumbani je, tutawasaidia vipi kujikimu kwa angalau mahitaji yao ya msingi hasa chakula?” alihoji. Kwa mujibu wa Maalim Seif, kwa Zanzibar theluthi moja ya pato la taifa inategemea utalii na asilimia 80 ya mapato ya fedha za kigeni yanatoka kwenye sekta hiyo ambayo sasa imeathiriwa na corona. Alisema watu wengi hasa vijana waliokuwa wanategemea kuongoza watalii ili kupata vipato vyao kwa sasa hawana shughuli ya kufanya.  “Wafanyakazi wa hoteli na migahawa wapo nyumbani hawana kazi, wasafirishaji kuanzia madereva wa taxi,  daladala na hata marubani wa ndege za watalii sasa wapo nyumbani kwa sababu shughuli zimesimama,” alisema. Alisema licha ya kuwapo mipango ya kupunguza msongamano wa wafanyakazi katika ofisi za Serikali, alihoji iwapo kuna sera ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya kuwashawisha watu kubaki majumbani na kuepuka misongamano au mikusanyiko isiyo na ulazima. “Nchi kubwa duniani zinapoteza maelfu ya raia wao kutokana na kuzidiwa uwezo kwa mifumo yao ya afya na hospitali, ikiwa hali ni hivyo kwa nchi hizo tajiri zenye fedha itakuwaje ugonjwa huu ukifikia katika nchi kama yetu?” alihoji.  UPIMAJI KWA JAMII Maalim Seif alisema kufunga mipaka ya bandari na uwanja wa ndege ni hatua moja lakini kuna haja ya kuanza kufanya upimaji kwa jamii.    “Kwa wenzetu mashirika yote ya kimataifa ya afya watusaidie Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kuanzisha mifumo bora na ya haraka ya kuwapima wale walio katika hatari ya ugonjwa wa corona.  “Mifano ya nchi za wenzetu waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa hadi sasa kukabiliana na corona imeonyesha upimaji katika jamii ni msingi mkubwa wa kupambana na adui huyu corona,” alisema Maalim Seif. Pia aliwaasa wananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu kwa kuepuka mikusanyiko na kupunguza watu wanaokutana nao. “Nawaomba sana msipuuze ushauri wa watalaamu wa kukaa umbali wa angalau mita mbili kutoka mtu na mtu.  “Hata kama corona haitokuathiri wewe, ukishindwa kufuata ushauri wa wataalamu utakuwa ndani ya hatari ya kuwadhuru wenzako, marafiki, ndugu, jamaa, wazee, watoto, mke, au mume. “Jiulize, utakwenda kusema nini mbele ya muumba wako pale itakapodhihirika kuwa wewe ndiye uliyekuwa chanzo cha madhila na misiba ya wenzako? Tuchukue tahadhari na tufuate tunayoelekezwa,” alisema. Aliwasihi wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu ili kuzuia nchi kupata maambukizo makubwa kwani uwezo wa kuyakabili ni mdogo, hivyo ufumbuzi ni kujikinga.  “Kama kila Mzanzibari na kila Mtanzania atafuata maelekezo ya wataalamu wa afya kwa usahihi tutapunguza maambukizo kwa kiasi kikubwa na kuushinda ugonjwa huu.  “Tukifanya uzembe hospitali zetu ambazo hali yake tunaijua wenyewe hazitakuwa na uwezo wa kukabiliana na wingi wa wagonjwa na hivyo, watu wetu wengi watapoteza maisha yao,” alisema. 
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU-DODOMA  NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka Watanzania waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) huku wakimtanguliza Mungu. Ametoa kauli hiyo juzi jioni wakati akizungumza na viongozi wa dini mbalimbali walioshiriki maombi maalumu ya kitaifa kwa Mkoa wa Dodoma dhidi ya Covid-19 yaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Veta, Dodoma. “Hakuna njia nyingine yoyote isipokuwa kunyenyekea chini ya mkono wa Mungu. Tuendelee kuchukua tahadhari wakati bado tunaendelea kumtumainia Mungu. Ni heri kumwishia Mungu, na Roho Mtakatifu atatupa njia ya kutoka hapa tulipo,” alisema Dk. Mwanjelwa. Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inaongozwa na Rais Dk. John Magufuli ambaye ana hofu ya Mungu na ndiyo maana aliomba Watanzania kwa imani zao wafanye maombi kwa siku tatu. Dk. Mwanjelwa alisema Serikali inatambua mchango wa viongozi wa kiroho na akawataka waliombee taifa kwani mwaka huu linajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.  “Mwaka huu tunatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu, kwa hiyo tunaomba tumtangulize rais wetu, tumwombee sana kwa yale anayoyafanya kwa nchi yetu,” alisema Dk. Mwanjelwa.  Akizungumza wakati wa kufungua maombi hayo, Rais wa Chama cha Maaskofu na Wachungaji (Tanzania Pastors’ Association – TPA), Askofu Samson Mlawi alitoa maombi akimwomba Mungu aifute Covid-19 kwenye mipaka ya Tanzania. Naye mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Kisusu Mvumbo alisema dunia huwa inaandika historia kila kunapotokea tukio kubwa akitolea mfano wa vita kuu ya dunia.  “Vita ya kwanza ya dunia iliandika historia, ikaja vita ya pili ya dunia nayo ikapita. “Sasa hivi, tishio juu ya mdudu huyu corona pia inaendelea. Dunia haiendi, imesimama, imekwama kiuchumi sababu ya mdudu corona. Tumsihi Mwenyezi Mungu atuepushe na hili janga,” alisema Sheikh Mvumbo katika maombi yake. Kwa upande wake, mwakilishi kutoka madhehebu ya Khoja Shia Mkoa wa Dodoma, Ustaadh Haidary Bakari alisema anamwomba Mungu aiponye Tanzania na pia akaombea Uchaguzi Mkuu ujao uwe wa heri na amani. Akimalizia maombi hayo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Maombezi wa Wanawake Barani Afrika, Profesa Margareth Kilimali alisema anamshukuru Mungu kwa kuwakutanisha viongozi hao wa dini wa Mkoa wa Dodoma bila kujali tofauti zao za dini. “Tunamshukuru Mungu kwa kuwa ana uwezo wa kutokomeza janga hili kwa nchi yetu ya Tanzania na bara zima la Afrika. Asante kwa fursa ya Uchaguzi Mkuu kwani umeshapanga ni jinsi gani utaendeshwa kwa amani wakati ukifika,” alisema Profesa Kilimali. Alisema Tanzania haitaaibika na janga la corona kwa sababu imemtumaini Mungu.  “Tanzania haitaaibika kwa sababu tumekujua wewe ni Mungu na unaweza kutuponya, Afrika haitaaibika kwa sababu nao wamekukimbilia wewe,” alisema Profesa Kilimali. Wakati huohuo, Mratibu wa TPA, Askofu Gerald Nzwalla alisema neno kuu la maombi hayo ya kitaifa limetoka nyakati wa pili, sura ya saba mstari wa 14 na wa 15 (2Nya.7: 14-15) na waliona ni muhimu maombi hayo yafanyike jijini Dodoma kwa sababu ni makao mkuu ya nchi na ndipo mahali anaishi Rais wa nchi. Maombi hayo maalumu yaliandaliwa na TPA kwa kushirikiana na Bakwata, Shia, Hamadia, Hindu, Aga Khan, KKKT, EAGT, FPCT, Menonite na Morovian.
KITAIFA
NA GEORGE KAYALA MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, Lucy Masha, amewaonya waimbaji wenzake kuishi maisha matakatifu na kuwa kielelezo kizuri katika jamii badala ya kufanya mambo yaliyokinyume na kile wanachokiimba kwenye tungo zao. Akizungumza na MTANZANIA jana, Lucy, anayetamba na albamu yake aliyoipa jina la ‘Tetea Maisha Yangu’, alisema anaumizwa anapoona waimbaji wenzake wanafanya matendo yenye machukizo mbele za Mungu na kwa mtu asiyewajua huwachukulia kama wapagani, wakati wakiwa kwenye madhabahu huigiza kama wacha Mungu wa kweli. “Waimbaji wengi wa nyimbo za injili wamekuwa wakifanya usanii katik huduma hiyo, maisha wanayoishi yako tofauti na ujumbe wanaoimba kwenye albamu zao, wengi ni waasherati, wazinzi, waongo, wasengenyaji, walevi, jambo ambalo ni chukizo mbele za Mungu, hivyo wanatakiwa kubadilika kwa kuwa wao ni kioo kwa jamii,” alisema Lucy. Aidha, mwimbaji huyo amewataka wasanii hao kuchagua njia moja, ya kumtumikia Mungu ama kuwa wapagani ili kuepuka suala la kuendelea kuitukanisha huduma ya uimbaji.
BURUDANI
Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM KIKOSI cha timu ya Yanga, leo kinatarajia kuelekea mkoani Njombe,  kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa  keshokutwa kwenye Uwanja wa Sabasaba. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara  watawavaa Njombe  Mji wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC, kwenye mchezo wao wa ufunguzi uliopigwa kwenye Dimba la Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten, alisema kikosi chao kitaondoka kuelekea Njombe kikiwa na wachezaji 26. “Timu itafanya mazoezi yake ya mwisho leo (jana) jioni na kesho (leo) itaondoka kuelekea Njombe. Msafara utakuwa wa wachezaji 26  isipokuwa Amiss Tambwe, Beno Kakolanya na Baruhani Akilimali ambao bado wanaendelea na matibabu,” alisema. Alisema wanatarajia mchezo huo utakuwa ni mgumu ukizingatia watakuwa ugenini, lakini watahakikisha wanavuna pointi tatu muhimu. Wakati huo huo daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, alisema wachezaji wao,  Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya wanaendelea na mazoezi mepesi huku wakitarajiwa kuungana na wenzao kwenye msafara utakaoelekea Njombe. “Kwenye mazoezi ya leo (jana) jioni ntaendelea kuwaangalia hawa majeruhi, lakini hali zao hadi sasa zinaendelea vizuri isipokuwa Tambwe, Akilimali na Kakolanya ambao watabaki Dar es Salaam kwa matibabu zaidi,” alisema.  
MICHEZO
NAIROBI, KENYA NANCY ni miongoni mwa walionusurika katika shambulio la kigaidi kwenye majengo ya Hoteli ya Dusit D2, iliyopo Riverside, baada ya kukaa ndani kwa saa 12 huku akisubiri msaada wa kuokolewa. “Shambulizi lilitukuta tukiwa tunamalizia mkutano katika ofisi zetu zilizopo Riverside siku ya Jumanne, Januari 15, ilikuwa kama saa 9 alasiri. Kichwani nilikuwa na jambo moja tu, kukimbilia nje na kuendesha gari kwa kasi bila kujali taa za barabarani na kufika nyumbani ili kuwahi kumpokea mwanangu getini baada ya kushushwa na gari la shuleni kwao. “Tulikuwa tunaagana na wenzetu wakati tuliposikia mlipuko kutoka upande wa pili wa mto. Uamuzi wa haraka uliochukuliwa na wenzangu ni kukimbilia dirishani. Lakini kutokana na mafunzo yangu ya ulinzi, niliwaonya juu ya tabia kama hiyo ya kukimbilia dirishani.” Mmoja wa wafanyakazi wenzake alisema ana mtoto anayesoma Shule ya Consolata, ambayo ili kuifikia ni lazima kuvuka mto huo na alitakiwa kuhakikisha kuwa mtoto wake yuko salama. “Tuliamua kutoka nje ya chumba cha mikutano na kuondoka. Lakini walinzi walituonya kuwa watu wanakimbilia nje ya jengo.” Shambulizi “Hapo ndipo nilipogundua kuwa tumeshambuliwa. Nilikimbia tena ndani na kuchukua mkoba wangu, lakini wakati nakimbilia kule juu, kulikuwa na sauti isiyo ya kawaida, kulikuwa na mkanganyiko. Vijana na wazee, wagonjwa na wenye afya njema walikuwa wanasukumana wenyewe kwa wenyewe ili kupata upenyo wa kujiokoa na kukimbilia nje ya majengo. “Upesi nilianza kupiga kelele, kuwaomba watu wasisukumane na wala wasikimbie. “Tutatoka nje sote pamoja, niliwaambia. Tukaweka mkakati wa namna ya kutoka nje, kwanza tulikubaliana kuwatanguliza wazee na wanawake wajawazito. “Kutoka kwenye ghorofa ya pili tuliona magaidi wawili kupitia dirishani. Walishika silaha nzito sana. “Nikawaonyesha: “Haya, ndiyo wale hebu waone. “Ilitokea kama ajali tu, gaidi mmoja aliangalia kule juu na macho yetu yakakutana ana kwa ana. Akaelekeza bunduki yake kwenye kundi tulilokuwepo na kushambulia. Risasi zilitoboa dirisha na kuvunja kabisa.” Maombi “Wote tulisambaratika. Nilijikuta nimejificha chini ya meza wakati risasi zikirushwa hewani zikipasua madirisha. Ilikuwa hatari sana. “Nilimpigia simu mama yangu na kumwambia tunashambuliwa na magaidi na nikamwomba atuombee. Nikaanza kujifikiria mwenyewe nikiwa nimezungukwa na ndugu zangu na nikagundua kuna soketi ya umeme. Bahati nzuri nilikuwa na chaja ya simu. Haraka nikachomeka na kutoa mlio kwenye simu yangu. Nikaanza kutuma meseji kwenye makundi mbalimbali ya WhatsApp kuwaambia watu kuwa tunashambuliwa na magaidi. “Muda huo huo nikasikia mlio wa risasi na mlipuko ukatokea. Wakati mwingine sauti ya mlipuko ilikuwa karibu sana, nikajisemea mwenyewe, sasa nimepatikana. Lakini nilikuwa napokea meseji nyingi za kunipa pole na kunipa moyo.” Kuokolewa “Tuliendelea kufanya mawasiliano na kwa kiasi kikubwa maofisa usalama waliwasiliana nami kutaka kujua eneo halisi nililokuwepo. Niliwaelekeza eneo nililokuwepo na walinihakikishia kuwa watakuja kuniokoa. Walituomba tusiwe na papara, wakataka tuwe watulivu. “Ilipofika saa 4 usiku, umeme ulikatwa. Nilipiga simu kwa mmoja wa maofisa usalama kuuliza kwanini umeme umekatwa na kwa mara nyingine alinihakikishia nisiwe na wasiwasi na akasema watatumia giza hilo kutuokoa wote. “Ilipofika saa 5 usiku, nilisikia sauti na kujaribu kujificha ndani zaidi kwa nafasi iliyobaki, nilifikiria kuwa watakuwa karibu yangu tayari kuniua. Lakini nikasikia, polisi, polisi, polisi, hapo ndipo nami nikatoka nje na kuamini kuwa wamenifuatilia kwa mawasiliano yangu. Kitu cha kwanza walichosema: “Jitambulishe mwenyewe,” hilo nililifanya bila wasiwasi. Waliniuliza idadi ya watu waliokuwa nami na kama naweza kuwabaini wote. Kisha walinichukua na kunizunguka wakati wakinisaidia. “Walikuwa na silaha zilizokokiwa kabisa na kuzielekeza kila kona, wakati naelekea kuwaonyesha maeneo mengine waliyojificha wenzangu. “Baada ya hapo walituhamisha na kutuweka katikati ya jengo na kusema tubaki hapo pamoja na kukaa mbali na madirisha ya jengo hilo na watakuja tena kutuondoa baada ya kuhakikisha usalama wa majengo yote. “Tulikaa hapo kwenye maficho kwa masaa manne, lakini kikosi cha maofisa usalama kiliendelea kuwasiliana na sisi, kutuambia tuwe wavumilivu na watulivu, pale tutakaposikia mlipuko wowote au sauti za risasi kwa sababu watakuwa ni wao polisi wakipambana na magaidi kuhakikisha wanakomboa jengo zima. “Kikosi kingine tofauti kilikuja kutuokoa saa 9:45 alfajiri. Hapo ndipo nilipokuja kuelewa hali halisi. Maofisa hao walitueleza kwa ufupi kilichotokea. “Walituambia kuwa kama tungekuwa tunapita sehemu yenye dirisha, tuhakikishe tunapita kwa kasi, kisha tupunguze mwendo baada ya kupita na kujificha katika nafasi na kutoka nje kwa kasi kubwa. “Askari hao walitembea kwenye ghorofa ya pili kwenda ya chini katika mlango wa dharura, huko ndiko waliegesha magari yaliyokuja kutuokoa. “Walituzingira kwa bunduki kwa kila upande na walitembea na kukimbia wakiwa wameinama. Pia walituambia kuhakikisha kuwa tusiwe na papara. “Hata pale tulipokuwa ndani kusubiri kuokolewa, wakati wote walituonya kuacha papara. Tulifanikiwa kutoka nje tukiwa pekupeku. Sikujua kama nakimbia kwenye sakafu ambayo ilijaa vipande vya vioo, kwani sikujisikia maumivu yoyote. “Tulichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo cha Msalaba Mwekundu na kupewa ushauri kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani. “Tulikutana na ndugu na familia zetu nje wakitusubiri, hatimaye nikafanikiwa kufika nyumbani asubuhi. Nilichojifunza katika shambulizi hilo ni umuhimu wa kuwa na mtandao mkubwa wa watu kimawasiliano. Nilikuwa na marafiki na ndugu zangu ambao walikesha usiku wote kuniombea. “Wengine walikuwa wanatoa taarifa kila baada ya muda kuelezea kinachoendelea baada ya kutazama runinga na kutuona tukikimbia kutoka upande mmoja kwenda mwingine katika tukio halisi. Wengine walikuwa wanawasiliana kwa meseji ili kuhakikisha wanapata taarifa zangu na kuchukua tahadhari kwa kuandika jina langu ‘Nancy’ na hayo yote yalinisaidia kuokolewa na kuwa watulivu.”
KIMATAIFA
 WINFRIDA MTOI  RAIS Dk. John Magufuli (JPM), ametangaza kurejea kwa michezo yote, ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili, kuanzia Juni Mosi, mwaka huu.  Michezo yote nchini ilisimamishwa na serikali tangu Machi 17, mwaka huu kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya corona.  Wadau wa soka nchini walikuwa wakisubiri kwa hamu kauli hiyo Rais Magufuli, ikiwa ni baada ya awali kusema anafikiria kuruhusu shughuli za michezo kuendelea kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virus vya corona.  Akizungumza jana wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, Rais Magufuli, alisema anafahamu kila mmoja anapenda michezo.  Alisema uamuzi huo unatokana na kuona michezo inasaidia katika kupambana na janga la corona kwa sababu hata katika taaarifa ya waliopata ugonjwa huo, hakuna uhakika kama yupo mwanamichezo aliyefariki.  “Nafahamu kila mmoja anapenda michezo, hata wabunge wanaenda kwenye michezo, kuna Ligi Daraja la Kwanza, Daraja la Pili, michezo ya Majeshi na mingine, ni lazima watu wafanye michezo.  “Taratibu za kushangilia na kuangalia zile zinaweza kupangwa na Wizara ya Afya pamoja na Wizara husuka ya michezo ili utaratibu wa nafasi (distance) ukaendelea kuwepo,” alisema Rais Magufuli.  Baadhi ya viongozi wa klabu za Ligi Kuu Bara, wamepokea kwa mkono miwili tamka hilo la JPM, wakisema wapo tayari kurudi uwanjani kwani walikuwa wakijindaa.   “Tupo tayari muda wowote kurudi uwanjani, tunasubiri utaratibu utolewe wachezaji warudi kambini, hapa tunapozungumza mafundi wapo katika uwanja wa mazoezi Chuo cha Sheria wanafanya marekebisho,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli. Alisema wiki hii walikuwa wanawatembelea wachezaji kuangalia hali zao, wakijiridhisha kila mmoja yupo fiti na sasa wanafanya mipango ya usafiri kwa kocha wao Luc Eymael aliyepo nchini kwao, Ubelgiji. Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa klabu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, alisema hawana tatizo lolote, kila kitu kinakwenda vizuri. “Tumepokea kwa furaha kauli ya Rais, tunafanya utaratibu wa wachezaji wetu waliopo nje ya nchi pamoja na makocha warudi, lakini utaratibu wa kambi ukitolewa, tunaweza kuanza na hawa waliopo Dar es Salaam,” alisema.  Aidha, Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas, imesema ni ruksa timu kuanza mazoezi. “Tumepokea kwa unyenyekevu agizo la Rais la ligi na michezo kurejea, huu uamuzi umekuja wakati mwafaka. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumepokea kwa tabasamu na timu zote za ligi za soka ni ruksa kuanza mazoezi rasmi. Taratibu za kuzingatiwa kiafya zitatolewa,” alisema.
MICHEZO
BAADA ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kufi ka mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kujibu tuhuma za kulidhalilisha Bunge kuwa ni dhaifu, wanasheria na wasomi wamefunguka kuhusu suala hilo.Ndugai alivieleza vyombo vya habari jijini Dodoma juzi kuwa CAG pamoja na Mbunge wa Kawe jijini Dar e s Salaam, Halima Mdee (Chadema) ambaye aliunga mkono kauli ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu, wanapaswa kufika mbele ya Kamati hiyo Januari 21 na 22, mwaka huu. Gazeti hili jana liliripoti kuwa Desemba 30 mwaka jana, Profesa Assad wakati akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alisema kuwa Bunge la Tanzania ni dhaifu, kwa kuwa limeshindwa kuzifanyia kazi ripoti za ufisadi, zinazotolewa na ofisi yake.Kauli hiyo ya CAG, ilimuibua Spika Ndugai aliyedai kuwa CAG ndiye anayepotosha, kwa kuwa haiwezekani aiseme nchi yake vibaya anapokuwa nje ya nchi, hivyo kuagiza CAG na Mdee kufika kuhojiwa na wasipotekeleza wito huo, hatua nyingine zitachukuliwa dhidi yao. Kutokana na hali hiyo, Wakili wa Kujitegemea, Albert Msando, alilieleza gazeti hili jana kuwa wakati CAG anatekeleza wajibu wake kisheria, hawezi kuhojiwa kwa jambo lolote na mtu yeyote, kwa kuwa sheria inamlinda.Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine wa shilingi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, inaeleza kuwa mtu yeyote, bila kujali nafasi yake, hapaswi kulidharau au kulikashifu Bunge na akifanya kosa hilo, Spika anaweza kumuita ili kuhojiwa na kamati hiyo. Ili kujua nguvu aliyonayo CAG ya kulindwa na sharia, lakini pia na nguvu iliyonayo Bunge ya kumhoji mtu yeyote anayelidharau, gazeti hili lililazimika kutafuta tafsiri ya kisheria na utawala bora juu ya muktadha huo.Msando alisema katika suala hilo la Spika na CAG, kilichotakiwa kuangaliwa kwanza ni tafsiri ya neno ‘dhaifu’ kama ni kweli neno hilo linalidhalilisha Bunge au la. Alisema kama tafsiri ambayo ilipaswa kuangaliwa, ingethibitisha ni kweli neno hilo linalidhalilisha Bunge, basi ndipo Bunge lingekuwa na sababu ya kumwita CAG kwa mahojiano.“Sasa swali ni kwamba nani mwenye mamlaka kisheria ya kutafsiri neno ‘dhaifu’ kama linalidhalilisha Bunge au la? Hapa kingepaswa kiundwe chombo kingine huru cha kutoa tafsiri na si Bunge lenyewe ambaye ni mlalamikaji kufanya kazi hiyo. Bunge haliwezi kuwa mlalamikaji na mwamuzi lenyewe, na katika kipengele hiki, sheria iko kimya”alieleza Msando. Kwa mujibu wa Msando, kwa kuwa CAG alitoa kauli hiyo wakati ambao hakuna Bunge linaloendelea, hajalidhalilisha Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 24 cha Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.“Spika alipaswa kulipeleka jambo hili kwenye mamlaka iliyomteua CAG yaani Rais na kulalamika kuwa amelidhalilisha Bunge katika vyombo vya habari, ndipo mamlaka iliyomteua CAG ingepima na kutoa uamuzi,” alieleza Msando. Wakili huyo alisema kuwa Spika alipaswa kumfikishia wito huo CAG kimaandishi, akiweka hoja zote ambazo CAG anatakiwa kuzitolea ufafanuzi katika utetezi wa kauli yake ; na si kueleza jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Alisema hata kama CAG atakwenda kuhojiwa, bado Bunge haliwezi kisheria kumshauri Rais atengue uteuzi wake, ila linachoweza kufanya ni kutoa karipio tu.Msando alisema kwa kuwa Bunge na CAG wanafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana, kama itaonekana jambo hilo linaleta ukakasi katika kutimiza majukumu yao, ndipo sasa Rais mwenyewe anaweza kuamua ama aendelee naye au amtoe au yeye CAG mwenyewe, aamue kwa hiari yake kujiuzulu kutokana na hali ya kutoaminiana kati yake na Bunge. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa, Dk Benson Bana, alisema kuwa uamuzi wa Bunge kumwita CAG na kutaka kumhoji ni sahihi, kwa kuwa kauli yake ya kwamba Bunge ni dhaifu, aliitoa akiwa nje ya ofisi yake.Alisema CAG anapaswa kuwa makini na kauli zake, kwa kuwa yeye ni sehemu ya serikali, hivyo ana wajibu wa kuhakikisha mwenendo, kauli na tabia yake vinaendana na dhana ya utawala bora, ikiwemo kuheshimu mihimili mingine ya dola. Mihimili ya dola ni Mahakama, Bunge na Utawala (Serikali). “Kwa kweli kauli ya kusema Bunge ni dhaifu inachefua. Kauli kama hii inapaswa kutolewa mahali sahihi na si hadharani kama hivyo, kwa hiyo ni sahihi kwa Spika Ndugai kumwita ili ahojiwe ili kujua kauli yake ina mwelekeo gani, na CAG si kiongozi wa kwanza kuitwa na Bunge kwa sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alishawahi kuitwa na kuhojiwa na Bunge,”alieleza Dk Bana.Majukumu ya Kamati ya Haki na Maadili ya BungeKanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016 Nyongeza ya Nane Kifungu cha 4 (1) (a) na (b), kinaeleza kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itatekeleza majukumu yake kwa: Kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge, yatakayopelekwa na Spika ; na kwamba itashughulikia mambo yanayohusu maadili ya Wabunge yatayaopelekwa na Spika.Kamati hiyo itakapokamilisha kushughulikia jambo husika, Mwenyekiti wa Kamati atamjulisha Spika kwa maandishi kwamba Kamati imemaliza kujadili jambo husika na Spika baada ya kupokea taarifa hiyo, ataagiza iwekwe kwenye Orodha ya Shughuli za Bunge kwa ajili ya kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni.Kinga ya CAG kikatibaHali ikiwa hivyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 143 (6) inasema kwamba, katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali.Lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo, hayataizuia Mahakama kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.Katiba inavyoweza kumwondoa CAGKwa mujibu wa Ibara ya 144 (1), CAG atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote, utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.Na Ibara ya 144 (2) inaeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu anaweza kuondolewa katika madaraka ya kazi yake, kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya 4 ya ibara hii.Nafasi ya Rais katika kumwondoa CAGRais ana mamlaka kikatiba ya kumwondoa CAG kwa mujibu wa Ibara ya 144 (3)(a) (b). Ibara hiyo inasema kuwa iwapo Rais ataona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii linahitaji kuchunguzwa, basi atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Kwa mujibu wa ibara hiyo, Mwenyekiti na walau nusu ya wajumbe wa Tume hiyo wanapaswa kuwa watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.Ibara hiyo inafafanua kuwa Tume hiyo itachunguza shauri lote na kisha kutoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hiyo kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinashangazwa na mwenendo wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuhusu uchunguzi inaoufanya kuhusu chama hicho kinyume na sheria. Kutokana na hilo, kimeitaka Takukuru kueleza rasmi makosa ya chama hicho na si kuchukua kauli za kisiasa na kufanyia uchunguzi. Mwishoni mwa Mei mwaka huu, Takukuru ilisema imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha ya Chadema, ikiwemo wabunge wa chama hicho kukatwa mishahara yao. Baadaye wabunge 69 na viongozi wengine wa chama hicho pamoja na waliowahi kuhudumu kupitia chama hicho, walihojiwa na Takukuru. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema pamoja na kwamba walitoa ushirikiano tangu mwanzo wa nyaraka mbalimbali za matumizi ya fedha na wabunge kuhojiwa, lakini taasisi hiyo imewaandikia barua nyingine mbili. Mnyika alisema katika barua hizo mbili Takukuru inawataka kuwasilisha nyaraka zingine za vikao na mipango ya chama kuanzia mwaka 2014-2020. “Sasa barua yao hii ni wazi kwamba Takukuru imeingia kutekeleza kauli iliyowahi kutolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kuwa watatumia vyombo vya dola kubaki madarakani,” alisema Mnyika. Alisema wanashangazwa kwa mwenendo huo wa Takukuru kwa sababu katika barua zao hakuna uchunguzi wa kosa kama vifungu vya sheria vinavyoelekeza ikiwa kuna kosa. Mnyika ambaye pia ni Mbunge Kibamba, alisema kutokana na hali hiyo, wameiandikia barua Takukuru ambayo imejibu kile walichotaka.  “Sasa tumewajibu na tumewasilisha barua yetu leo (jana) kuwa watujulishe rasmi kwa mujibu wa sheria kuhusu kile wanachokichunguza ili tuendelee kuwapa ushirikiano, tunataka watupe majibu rasmi na kwenye barua tumewaeleza bayana kuwa tunaona jambo hili lina mwelekeo wa kisiasa wa kuokoteza makosa. “Pia tumeitaka Takukuru izingatie kwamba hadi sasa haijaeleza kosa au makosa jambo ambalo Chadema tulishaweleza awali. “Hadi sasa Chadema imeshatoa nyaraka na michango ya wabunge, viongozi na wabunge wamefanyiwa mahojiano kuhusu fedha za wabunge, pia tumewaeleza wigo wa hicho inachodaiwa kuwa uchunguzi hauonyeshi ukomo wala makosa,” alisema Mnyika. Aidha alisema kutokana na mazingira ya kisiasa hapa nchini na kwa kuwa wako kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, wanapata wakati mgumu kuendelea kutoa ushirikiano bila kufahamu ukomo wa uchunguzi au jambo au kosa mahususi ambalo wanachunguzwa. “Chadema inatatizwa zaidi kwa Takukuru kutumia kauli za kisiasa zinazotolewa na watu na sasa tunaitaka Takukuru iongozwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Mnyika.
KITAIFA
FAMILIA ya Naomi Marijani, mwanamke anayedaiwa kuuawa na mumewe Khamis Luongo kisha kuchomwa moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, imesema bado haina imani kama ndugu yao huyo kuteketezwa kwa moto wa mkaa.Kauli yao hiyo imekuja baada ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kigamboni, Thobias Walelo kubainisha kuwa Naomi ameuawa na mumewe huyo ambaye baada ya tukio hilo alichimba shimo na kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia mkaa magunia mawili.Walelo alisema, Jeshi la Polisi lilimhoji Luongo aliyekiri kutekeleza mauaji hayo na kuwa aliuchomea mwili nyumbani kwake Gezaulole Kigamboni, hatua iliyowafanya wataalamu kutoka Jeshi la Polisi kufuatilia mabaki ya mwili wa marehemu Kigamboni ili kuchukua mabaki ya mwili kwa uchunguzi ili kubaini ukweli kama mabaki hayo ni mwili wa Naomi.Jana gazeti hili liliwasili nyumbani kwa dada wa marehemu, Salma Marijani aishiye, Mbweni- Ubungo, Dar es Salaam na kuzungumza na Msemaji wa familia Wiseman Marijani ambaye alibainisha kuwa hawana imani kama ndugu yao amechomwa moto kweli. Hata hivyo alisema kuwa familia itaendelea kusubiri majibu ya Polisi. Alisema mtuhumiwa huyo amedanganya wanafamilia kuwa ndugu yao amesafiri nje ya nchi baada ya kupata mwanaume mwingine huku akijua fika kuwa amemuua.
KITAIFA
NA MWANDISHI WETU VANESSA Mdee ni miongoni mwa wasanii tisa wa muziki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, watakaowakilisha katika mkutano wa kiuchumi wa dunia kwa Afrika na wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika wakati watakapozindua wimbo wa ‘Strong Girl’ unaohamasisha kampeni inayojulikana kama “Poverty is Sexist”. Licha ya wimbo huo kuja kuzinduliwa rasmi katika mkutano huo utakaofanyika nchini Afrika Kusini, kwa sasa unaendelea kuzinduliwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Nigeria, Msumbiji na Zimbabwe. Wasanii wengine walioshiriki katika wimbo huo ni Victoria Kimani (Kenya), Judith Sephuma (Afrika Kusini), Waje (Nigeria), Arielle T (Gabon), Gabriela (Msumbiji) na Selomor Mtukudzi (Mtoto wa Oliver Mtukudzi wa Zimbabwe), Blessing Nwafor na Yemi Alade (Nigeria). Vanessa alisema kampeni hii inawataka viongozi wa dunia kuwaweka wasichana mbele kwa mwaka huu 2015 kutokana na malengo mapya ya maendeleo yatakayoazimiwa na viongozi wa dunia katika Umoja wa Mataifa. Alisema pia wimbo huo umeanza kuonekana sehemu mbalimbali ukiwa na ripoti ya kampeni ya ONE inayojulikana kama “Poverty is Sexist’ ikimaanisha umasikini unaaumiza zaidi jinsia moja. “Ndani ya ripoti hiyo inaonyesha namna wasichana na wanawake wanavyotakiwa wawe na moyo wa mapambano ya umasikini uliokithiri huku ikionesha namna ambavyo wataweza kufungua fursa za uchumi kwa wanawake kunavyoweza kuwasaidia kwa jamii,’’ alisema. Kampeni hiyo inaunga mkono wito wa viongozi wa dunia wa kupambana na ukosefu wa usawa wa kijinsia kwa kuwekeza zaidi kwa wanawake na wasichana ili kumaliza umasikini uliokithiri ifikapo 2030.
BURUDANI
UELEWA wa wajawazito juu ya uzazi salama bado uko chini huku wanawake wanaohudhuria kliniki katika zahanati na vituo vya afya uelewa wao ukielezwa uko chini zaidi. Hilo lilibainika katika utafiti uliofanywa na Daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Norman Jonas kuhusu uelewa wa wajawazito Wilaya ya Biharamulo, Kagera.“Utafiti huu ulifanywa ndani ya miezi sita Biharamulo kuangalia vijijini uelewa wao ukoje juu ya jambo hilo. Tulibaini uelewa wao mdogo, jambo ambalo linaongeza vifo vya kina mama na watoto, chini ya asilimia 50 ya kina mama hawana uelewa wa maandalizi haya,” alisema.Utafiti huo ulihusisha wajawazito 379 wenye mimba za umri tofauti wanaohudhuria kliniki vituo vya afya, zahanati na hospitali ya wilaya. Alisema wanawake waliomaliza shule ya msingi uelewa wao ilikuwa asilimia 13, walioingia sekondari lakini hawakumaliza ni asilimia 33, waliomaliza sekondari ilikuwa asilimia 46. Alipoangalia kwa kufuata umri wa mimba, wale walio na mimba ya chini ya wiki 13 uelewa wao ilikuwa asilimia 22 na wale wenye wiki 13 hadi 27 ilipanda hadi asilimia 29 ya waliohojiwa.“Hospitali ya wilaya uelewa wao ulionekana ni mkubwa kwa sababu watoa huduma ni wengi na akina mama hawa wanaishi wilayani wana elimu zaidi, lakini wale wa kijijini zaidi, watoa huduma ni wachache na wengi hawajasoma, hawa kina mama, vitu vingi vinachangia,” alisema.Alisema Shirika la Afya Duniani (WHO) limeweka mpango maalumu kuwaelimisha wajawazito ni namna gani wajiandae na uzazi na wafanye nini ikitokea dharura. Alisema huo ni Mpango Maalumu wa Uzazi na Utayari wa Kukabiliana na Changamoto (BBCR) ambapo Tanzania pia unatumika.Katika mpango huo watoa huduma za kliniki kwa wanawake wajawazito wanapaswa kutoa uelewa dalili hatari katika ujauzito, wakati wa uchungu na wa kujifungua. Pia wanatakiwa kuelimishwa wachague wapi pa kujifungulia.
KITAIFA
Mtandao wa Skysport imeripoti uongozi wa Manchester United wamesema fedha hiyo ni kiduchu kwao pia bado wana mipango na mchezaji huyo kwa msimu ujao wa ligi kuu na klabu bingwa ulaya.August 2015 Degea alibakiza dakika tu kujiunga na matajiri hao wa Hispania kabla ya dirisha la usajili kufungwa , lakini Manchester United waliwachezea shere tena Real Madrid kwa kumsainisha mlinda mlango huyo kandarasi ya miaka miwili ikiwa na muda wa ziada wa miezi 12 .Licha ya Real Madrid kuja na ofa kubwa zaidi kuwahi kuweka kwa upande wa walinda milango ya paundi milioni 60 mara tatu zaidi ya mkwanja wa paundi milioni 18 ambazo Manchester United waliwapa Atletico Madrid mwaka 2011 lakini wameigomea ofa hiyo na kuwajibu bado wanamuhitaji .
MICHEZO
Na CHRISTINA GAULUHANGA DAR ES SALAAM WAANDISHI wa habari, wametakiwa kujikita kusoma ripoti mbalimbali na kuandika kwa kina habari’ zinazohusu ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kutoa  elimu kwa umma na kufahamu maendeleo ya taasisi zao mbalimbali. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na mkaguzi kutoka ofisi ya CAG, Lenatus Mnyangabi wakati wa ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habari na namna ya kuripoti taarifa za ofisi hiyo. Alisema ofisi yao, imekuwa ikitoa hati za aina nne ambazo baada ya kufanya ukaguzi wa hesabu katika idara na taasisi za serikali ambazo ni inayoridhisha, isiyoridhisha, yenye shaka na hali mbaya kulingana na utunzaji nzuri wa hesabu. Alisema hati za ukaguzi zilizotolewa kwa mwaka wa fedha 2017/18, ulioishia Juni, mwaka jana pia ilifanya kaguzi 255 za Serikali kuu, mashirika ya umma 122, halmashauri 185 na miradi ya maendeleo 469. “Katika mwaka wa fedha  huo,CAG ametoa hati za ukaguzi 1,031, kati ya hati hizo zinazoridhisha ni 989, zenye shaka 19, zisizoridhisha 17 na hali mbaya sita,”alisema Mnyangabi. Mkaguzi Mkuu wa Nje,   Alestidia Ngalaba alisema ni vema waandishi wakatumia taaluma yao kuwaelewesha wadau na wananchi kwa ujumla namna ya kusimamia rasilimali na fedha kwa maendeleo. “Ninaamini kupitia vyombo vyenu, mtatusaidia kuchambua kwa ufasaha kwa kutumia lugha nyepesi ambayo kila mwananchi ataweza kuielewa vizuri na kufanya uamuzi sahihi wa kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za taifa,”alisema. Alisema uhusiano baina ya ofisi yao na wanahabari,  umesaidia kuleta maendeleo ya nchi kwa sababu kila mmoja amejifunza jinsi ya kutumia na kulinda rasilimali zinazotokana na Kodi. Ofisa kutoka ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Elias Malima alisema vyombo vya habari, ni mawakala wa umma  na amani, vina kila sababu ya kuisaidia Serikali kutangaza fursa zilizopo na jitihada zinazofanyika. Alisema wakati huu nchi ikiwa kwenye vita ya kiuchumi, mapambano ya rushwa na kulinda rasilimali ipo haja wananchi nao wakajitokeza kushirikiana na Serikali ili iweze kufikia malengo yake. “Ni vema ofisi ya CAG, ikawapa fursa wanahabari ya kusoma ripoti zinapotolewa na masuala muhimu ya kuzingatia,”alisema Malima. Alisema wanahabari wanapaswa kubadilika kwa kuzibeza  taafsiri za kisiasa na kujenga mazoea ya kusoma taarifa za kitaaluma. Mwishooo
KITAIFA
KAMISHNA Msaidizi wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathew Nhonge ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steel Group na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50) alipata kihalali hati 70 za viwanja.Aidha, alidai kuwa mshitakiwa huyo anayedaiwa kutoa rushwa ya Sh milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipata hati hizo kihalali na kwamba hakuwahi kumshawishi kwa kutoa rushwa ili kusaidia upatikanaji wa hati hizo. Nhonge ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashitaka, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Samweli Obas.Akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo, shahidi huyo alidai kuwa Kampuni ya Kiluwa iliomba kumiliki ardhi maeneo ya Kikongo Kibaha na kwamba ilipewa hati 73 za viwanja ili azisaini. Alidai katika hati hizo, tatu hazikusainiwa na Msajili wa hati, kwa sababu ya mapungufu yaliyokuwepo.“Baada ya hati hizo kusainiwa, Julai 13, mwaka huu nilipigiwa simu na Waziri Lukuvi akanieleza kuwa nimfahamishe Kiluwa kwamba aende ofisini kwake akiwa na hati zake,” alidai Nhonge. Alidai kwa kuongeza kuwa, “nilifikisha ujumbe kwa Shabani na Kiluwa aliupata, Julai 16 mwaka huu Kiluwa alienda ofisini kwa Waziri ambaye aliagiza hati hizo ziongezewe masharti hasa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.”Shahidi huyo alidai alifahamu kama mshitakiwa huyo alifika kwa Waziri Lukuvi, baada ya kukutana naye mapokezi ya kwenda ofisini kwa waziri kati ya saa nne mpaka saa sita. Pia, alidai hakufahamu kilichoendelea baada ya maongezi yao, isipokuwa alisikia kwa watumishi wa wizara kuwa Kiluwa amekamatwa kwa rushwa. Alidai kutokana na suala la rushwa lililomkabili Kiluwa, hati zote alizosajiliwa zilifutwa katika usajili chini ya Kifungu Namba 178 cha Sheria ya Ardhi Namba Nne.
KITAIFA
Juzi Yanga iliifunga Stand United mabao 3-1 katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, matokeo ambayo yaliiweka Yanga jirani kabisa na ubingwa baada ya kufikisha pointi 68. Kwa matokeo ya juzi, Yanga ilikuwa ikihitaji pointi nne tu ili iwe bingwa kwani ingefikisha pointi 72 ambazo hakuna timu ambayo ingeweza kuzifikia.Lakini kutokana na matokeo ya jana, Yanga sasa inahitaji pointi tatu tu kuibuka bingwa, kwani itafikisha pointi 71 ambazo hakuna timu itakayozifikia. Azam inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 60, kama itashinda michezo yake iliyosalia itafikisha pointi 69, wakati Simba inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 58 ikishinda michezo yake minne iliyosalia itafikisha pointi 70.Yanga imebakisha mechi zote ugenini dhidi ya Mbeya City ya Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara na Majimaji ya Songea. Pia matokeo ya jana, yameisaidia JKT Ruvu ambayo imefikisha pointi 26 na kupanda nafasi moja ikitoka ya 14 hadi ya 13 katika timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo.JKT Ruvu imebakisha michezo mitatu. Katika mchezo wa jana, Azam ilipata bao la kwanza dakika ya 31 mfungaji akiwa Michael Balou baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa wapinzani wao.Dakika saba baadaye Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Mudhathir Yahya. JKT Ruvu ilipata bao la kwanza dakika ya 57 mfungaji akiwa Saad Kipanga kwa penalti baada ya beki Gadiel Michael kuushika mpira katika eneo la hatari. JKT Ruvu ilisawazisha bao dakika ya 71 mfungaji akiwa Mussa Juma kwa shuti baada ya kipa Aishi Manula kuutema mpira.
MICHEZO
NAHODHA John Mikel Obi amesema fainali za mwaka huu ni za mwisho kwake akiamini kuwafanya Wanigeria kumkumbuka na kuamini uwepo wake kwenye kikosi ni moja ya kufanya kikosi hicho kuwa na mafanikio.“Ni safari ya kufurahisha kwangu kwenye timu ya taifa,” Mikel mwenye umri wa miaka 32 aliiambia BBC Sport. “Hakuna shaka kuwa kushinda taji Afrika Kusini ni jambo kubwa sana na ndio ninalotaka kuwasaidia kuwasaidia vijana wadogo kwenye timu kufikia ndoto zao,” alisema. “Miaka 13 nadhani inatosha, nimeshinda mataji, nimekuwa na wakati mzuri, nadhani ni wakati kwa vijana wote kuendelea.”“Nipo hapa Misri kuwasapoti vijana, na kuhakikisha wanakuwa kwenye mstari sahihi.” “Nadhani uwepo wangu mara zote ni muhimu kwao, ninaamini naweza kumaliza na taji.” Mikel amecheza mechi 89 kwa Nigeria, akicheza kwenye kombe la dunia mara mbili na kuisaidia Super Eagles kushinda taji la Afrika mwaka 2013. Pia aliisaidia Nigeria kumaliza ya tatu kwenye michuano ya Afcon mwaka 2006 na 2010.Amecheza mara mbili kwenye michuano inayoendelea sasa Misri lakini alikosa mechi ya hatua ya 16 kutokana na kuwa majeruhi ambapo Nigeria ilikata tiketi ya kucheza robo fainali na Afrika Kusini kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cameroon. Sasa Mikel anawania kuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria kinachowania taji la nne. “Kama nipo fiti ningependa kucheza robo fainali, lakini alihitaji kufanya haraka,” aliongeza.“Ninaamini kama tunaweza kucheza nusu fainali, nitakuwa tayari na kuisaidia timu kama nitahitajika.” Mchezaji huyo aliyecheza fainali ya kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2005, mchezaji wa zamani wa Chelsea anaamini ana mchango wake katika mafanikio ya taifa hilo la Afrika Magharibi.“Kama tutakuwa tayari kushinda hapa, nitafurahi sana, kisha wanaweza kuendelea kutoka hapa.” Alikuwa pia miongoni mwa wachezaji watatu wa Nigeria waliozidi umri walioshinda medali ya shaba kwenye michezo ya Olimpiki Rio mwaka 2016.
MICHEZO
MAJERUHI saba, kati 32 wa ajali ya lori la mafuta ya petroli, lililoanguka na kulipuka mkoani Morogoro, waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam, wamepoteza maisha.Hii ina maana kuwa waliofariki kutokana na ajali hiyo iliyotokea Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro hadi kufikia saa 5.30 asubuhi ya jana ni 89. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha akitoa tarifa jana alisema kwa sasa wamesalia majeruhi 25, kati ya 46, waliopokelewa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.Aligaesha alisema kati ya majeruhi hao 25, 16 wapo Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU). Wengine tisa wanaendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya Sewahaji namba 22, ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya majeruhi hao.Alisema madaktari wanaendelea kufanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya majeruhi waliobaki. “Madaktari na wauguzi wanafanya kila jitihada kwa weledi kuhakikisha majeruhi wanapatiwa matibabu kunusuru maisha yao,” alisema. Aliwataja waliopoteza maisha usiku wa kuamkia jana ni Shaban Makunganya (40), Ramadhani Mdoe (50), Shabani Ayub (34), Khalifa Idd (26), Omary Abdala Omary (34), Omary Abdallah (24) na Aloyce Kiponzi (36).Ofisa Uhamasishaji wa Damu Salama Hospitali ya Muhimbili, Dk John Bigambalaye alisema mpaka sasa kiasi kilichokusanya cha unit 400, hakitoshelezi mahitaji. Dk Bigambalaye alisema kwa kawaida MNH pekee inatumia chupa 120 kwa siku, ukichanganya na Mloganzila jumla ya chupa 150 zinatumika kwa siku. Alifanya alisema idadi hiyo ni ya kawaida kama hakuna dharura. Lakini, kwa kipindi hiki cha dharura wa majeruhi wa moto, wanahitaji chupa 200 mpaka 250 kwa siku.“Kwenye damu kuna majimaji ambayo tunayatenganisha na damu, maji hayo uitwa Plazma, na hata huhitajika sana kwa wagonjwa wa moto,” alisema.Aliongeza kuwa mpaka sasa wamekusanya unit 400 za damu. Alisema kiasi hicho kimeongezeka, tofauti na siku za nyuma, ambazo walikuwa wakikusanya unit 70, zikizidi sana 80.“Mahitaji ya damu ni makubwa, tunaomba watu binafsi, makampuni na taasisi binafsi zije kuchangia damu tuokoe maisha ya wenzetu, na pia benki ya damu ibaki na akiba,” alisema Bigambalaye.Aidha, alisema leo Ijumaa wanatarajiwa kukusanya damu si chini ya lita 400 kutoka kwa wafanyakazi 500 wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao leo watachangia damu.
KITAIFA
['Kuigeuza Everton kuwa klabu ya kugombea nafasi ya kucheza Champions League si jambo ambalo halitawezekana, anaeleza kocha mpya wa klabu hiyo Carlo Ancelotti.', 'Ancelotti, 60, ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na AC Milan ametia saini mkataba wa kuwanoa Everton mpaka mwaka 2024.', 'Kocha huyo mwenye mafanikio lukuki anaichukua timu hiyo ikiwa nafasi ya 15 kwenye jedwali la Ligi ya Primia, wakiwa na alama nne tu juu ya mstari wa kushuka daraja. ', '"Champions League ni mpango wetu wa muda mrefu," amesema na kuongeza. "Hakuna kisichowezekana katika mpira wa miguu."', 'Everton hawajamaliza katika nafasi nne za juu toka mwaka 2005, na kabla ya hapo ilikuwa mwaka 1988. ', 'Klabu pekee ambazo Ancelotti amefundisha na kukosa uwiano wa ushindi wa kufikia 50% ni klabu za Italia za Reggiana na Parma mwishoni mwa miaka ya 1990.', 'Ancelotti amesema kilichomvutia kujiunga na klabu hiyo ni: "Historia na utamaduni wa klabu. Ni moja ya klabu kubwa zaidi England."', 'Ancelotti ameshinda Champions League mara tatu kama kocha - mara mbili akiwa na AC Milan na mara moja na Real Madrid.', 'Pia ametwaa ubingwa wa Ligi ya Primia na Kombe la FA akiwa na Chelsea mwaka 2010 na ametwaa mataji wakiwa na Bayern Munich na Paris St-Germain.', 'Ancelotti ametua Everton siku chache baada ya kutimuliwa katika klabu ya Napoli ya nchini kwao Italia.', '"Ni kweli nimefunza klabu kubwa," amesema, "Mipango ya Paris St-Germain ilikwa mizuri. Naamini itakuwa hivyo na hapa pia. ', 'Nimeenda uwanja wa mazoezi jana. Mambo yalikuwa mazuri.', 'Mipango ya klabu kujenga uwanja mpya inaonesha kuwa klabu inataka mafanikio. ', '"Kukusanya mapato ni jambo kubwa katika mpira wa kisasa. Everton wanataka uwanja wao mpya ili uwasaidie kukusanya mapato na kuwa na ushindani mkubwa. ', '"Kwangu, itakuwa ni jambo zuri kuwepo hapa wakati uwanja mpya ukifunguliwa." ']
MICHEZO
TAMASHA la Urithi litakalofanyika kwa siku tatu jijini hapa maarufu Rock City linatarajia kuvutia maelfu ya wananchi wanaotarajia kuungana na wasanii, wadau wa utalii na viongozi wa nchi kunadi vivutio tele vilivyojaa Mwanza na vitongoji vyake.Tamasha la Urithi likiwa ni kipeperushi cha bendera ya Tanzania kwa ulimwengu wa utalii, na toleo la pili la utamaduni linaloendeshwa kwa azma ya kisiasa ya kutangaza utalii, kupanua wigo wa mazao ya utalii kupitia utamaduni na kauli mbiu yake, inasisitiza Sherehe, Urithi na Utalii.Baada ya kufunguliwa jijini Dar es Salaam Septemba 21, na kushirikiana na JAMAFEST kuanzia 21-28 Septemba, Urithi liliangazia zaidi utofauti wa bidhaa za utalii na ubunifu katika mikoa mingine 10 kabla ya kutinga mjini hapa kukamilishwa ngwe ya mwaka huu. Likiwa mjini tamasha limesheheni maonesho na shughuli nyingi tofauti zinazoitambulisha Mwanza na nyingine ambazo zinaongezewa nguvu kwa kuoneshwa kwa ufundi zaidi hapa Mwanza.Matukio yanayofanyika Mwanza ni pamoja na mashindano ya kwaya mbalimbali zilizopo mkoani Mwanza na mikoa mingine, mashindano ya mieleka kwa wanaume, mashindano ya mbio za mitumbwi na mashindano ya mbio za baiskeli zisizo na gia na mashindano ya bao.Vilevile kutakuwepo na sanaa za maonesho za vikundi vya ngoma za asili za makabila ya Kanda ya Ziwa, na maonesho ya shughuli mbalimbali za utalii na utamaduni wa Mkoa wa Mwanza. Zaidi ya hayo kutakuwa na burudani ya muziki wa asili kwa wageni na wananchi watakaotembelea tamasha hili.Kama kawaida katika shughuli za tamasha la Urithi muziki wa kisasa nao unasherehekewa na Mwanza watakuwepo wanamuziki kama Saida Karoli, Mrisho Mpoto, Mauwa Sama na wengine wengi.Kutakuweko pia maonesho ya mapishi vyakula vya kiasili vya makabila makuu yanayopatikana mkoani Mwanza na wananchi wataweza kuonjeshwa nyama choma ya porini ambayo imekuwa kichocheo kikubwa cha tamasha hili. Tamasha hili ni nafasi moja kubwa ya sanaa na utamaduni kutangaza utalii hapa nchini na papo hapo kupanua wigo wa bidhaa za utalii Tanzania.
KITAIFA
Hadija Omary, Lindi Wajawazito na wagonjwa mbalimbali katika Zahanati ya Rondo Junior Seminary, iliyopo Kitongoji cha Ngara, kijiji na Tarafa ya Mnara, mkoani hapa wameondokana na adha ya kutumia vibatari wanapolazwa au kupatiwa matibabu usiku katika hospitali hiyo baada ya kuwekewa umeme wa  nishati ya jua (Solar) kwa ufadhi wa Shirika la Maendeleo la Umoja   wa Mataifa (UNDP). Hayo yameelezwa na muuguzi wa zahanati hiyo, Judith Mbaya alipokuwa akitoa maelezo ya zahanati hiyo mbele ya ujumbe kutoka UNDP, ulipotembelea chuoni hapo, kuona misaada waliyoifadhili namna inavyofanya kazi. Judith amesema tangu kupatikana kwa nishati hiyo kumerahisisha upatikanaji wa huduma ndani ya seminari hiyo na kwa wakazi wa jirani na hasa kwa akina mama wajawazito wanaokwenda kupata huduma. “kabla ya kupata nishati hii tulikuwa tunalazimika kutumia vibatari au tochi wakati wa kumsaidia mama mjamzito wakati wa kujifungua jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa mtoto na mama mwenyewe,” amesema Judith. Aidha, amesema licha ya zahanati hiyo  zahanati kuhudumia wafanyakazi wanaoishi katika seminari hiyo pia hutoa huduma kwa wakazi wengine zaidi ya 700 wanaoishi katika vijiji jirani. Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, amepongeza namna ya fedha waliyoitoa kwa ajili ya kuteleleza miradi katika zahanati hiyo inavyotumika ipasavyo ambapo pia amewaasa wahudumu wa zahanati hiyo kutunza miundombinu hiyo.
AFYA
Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM WAKILI wa msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu, Peter Kibatala, ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,   Dar es Salaam,   kuomba kujitoa kumwakilisha katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili. Wakati huo huo mahakama imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumwakilisha msanii huyo katika kesi hiyo. Msando  aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi. Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema   alipokea barua hizo juzi   na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya. Inadaiwa    Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema yaliyopo Kunduchi Ununio  Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipande vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Naye Wema  anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka jana katika  eneo lisilojulikana  Dar es Salaam,  alitumia bangi.
KITAIFA
['Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito - via Metro)', 'Chelsea sasa wanamlenga mlinzi wa West Ham Issa Diop na wanatazamiwa kutuma dau la usajili la pauni milioni 40 kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 22. (Express)', 'Manchester United wanaaminika kutaka kumsajili beki wa klabu ya Hellas Verona ya Italia na raia wa Albania Marash Kumbulla, 19. (Star)', 'Tottenham, Arsenal na Manchester United wanapigana vikumbo kutaka kumsajili beki wa kati Samuel Umtiti, 26, na klabu ya Barcelona inaonekana imedhamiria kumsajili Mfaransa huyo. (El Desmarque - in Spanish)', 'Ajax wanapanga kumrudisha beki Matthijs de Ligt, 20, kwa mkopo licha ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kumuuza Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. (A Bola - in Portuguese) ', 'Chelsea inaonekana haipo tayari kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, huku meneja Frank Lampard akiona mchezaji huyo haendani na kikosi chake. (90min)', 'Crystal Palace wamekataa kumuuza Zaha kwa vigogo wa Ujerumani Bayern Munich. (Guardian)', 'Tottenham wamejiunga kwenye mbio za kutaka kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24, huku Milan wakitaka dau la pauni milioni 30. (Guardian)', 'Spurs hawana mpango wa kutafuta mbadala wa haraka wa kiungo Moussa Sissoko, 30, ambaye ni majeruhi na hatarajiwi kurudi dimbani mpaka Aprili. Hata hivyo, watalazimika kununua kiungo mwengine endapo watawauza Victor Wanyama, 28, na Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)', 'Everton wanataka kumsajili kiungo wa Juventus, Mfaransa Adrien Rabiot, 24, kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)', 'Arsenal haitarajiwi kufanya usajili wa moja kwa moja mwezi Januari na badala yake watajikita kwenye mikopo. (Goal)', 'Kocha Ole Gunnar Solskjaer amesema wachezaji wengi wa Man United wanacheza kwa ajili ya kesho yao. Kiungo wa England Jesse Lingard, 27 amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake pamoja na kiungo Mserbia Nemanja Matic. Beki wa Mholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22 na beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 25 watamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)', 'Manchester City wanawania kumsajili winga wa Wolves Mhispania Adama Traore, 23. (Calcio Mercato, via Manchester Evening News)', 'Wakala wa kiungo wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 32, atafanya mazungumza na Manchester United kuhusiana na uwezekano wa mchezaji huo kuhamia United mwezi huu. (Corriere Della Sera, via Mirror)', 'Inter Milan inaripotiwa kumfuatilia nahodha wa Manchester United Ashley Young, 34. (Manchester Evening News)', 'Aston Villa wako kwenye mawasiliano na Crystal Palace kuhusu kumrejesha mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 29. (Telegraph, via Birmingham Mail)', 'Villa wamepewa fursa ya kumsajili kipa mkongwe Pepe Reina, 37, kutoka AC Milan. (Mail)']
MICHEZO
NA JESSCA NANGAWE MKALI wa muziki wa RnB nchini, Bernad Paul ‘Ben Pol’, anatarajia kufanya kazi na mkali wa muziki huo nchini Marekani, Trey Songz. Mipango ya kufanya kazi pamoja imetokana na wimbo mpya wa Ben Pol, ambao unajulikana kwa jina la ‘Tatu’ aliomshirikisha Darasa, wimbo huo unaonekana kuvuka mipaka na kuongeza idadi kubwa ya mashabiki. Ben Pol amesema anafurahi kuona wimbo wake huo ukipokelewa vizuri ndani na nje ya nchi, huku baadhi ya wasanii wakijitokeza kutaka kufanya naye kazi. “Nina ‘collabo’ nyingi zinakuja kutoka kwa wasanii wa Nigeria, Marekani, ngoma yangu mpya ya Tatu imenifungulia njia, ninaamini bado nina nafasi ya kuendelea kuwa na mafanikio makubwa,” alisema Ben Pol. Alisema miongoni mwa wasanii wa kimataifa anaotarajia kufanya nao kazi ni pamoja na Chidinma wa Nigeria na Trey Songz kutoka Marekani.
BURUDANI
Na Elias Simon Msanii wa kizazi kipya ndani ya mziki wa bongo fleva Tanzania, Elderado baada ya kushirikiana na Mr blue kupitia wimbo wa chechema kwa sasa ameachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Christian bella katika wimbo wa ‘Nimekuwa’ Akizingumza na Papaso la Burudani jana, Elderado alisema Chechema ndio wimbo uliomtambulisha kwenye game ya bongo fleva kupitia Mr blue lakini wimbo huu mpya wa “Nimekuwa” amemshirikisha Christian bella. “Chechema imefanya vizuri sana maana Mr blue ni msanii mkubwa ndani ya Tanzania lakini huu wimbo wa sasa ndio balaa tosha kupitia Christian Bella  maana Christian bella anajua sana sio msanii wa kawaida hapa nchini,” alisema Elderado.
BURUDANI
LEO Waziri wa Madini, Angela Kairuki ataongozana na wafanyabiashara 180 kutokea kampuni 44 za madini nchini, kuelekea nchini China kuhudhuria kongamano la madini. Wakiwa kwenye kongamano hilo la siku tano, watajifunza masuala mbalimbali kuhusu madini ikiwa pamoja na kutafuta wawekezaji kwa kuzunguka na kuhudhuria mijadala mingine mbalimbali, lengo likiwa ni kuiwezesha nchi kunufaika na sekta hiyo.Kongamano hilo litakaloanza rasmi kesho jijini Beijing ni wazi litakuwa na tija kwa nchi hii, hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa Tanzania ipo kwenye harakati za kukuza uchumi kufikia uchumi wa kati huku sekta ya madini ikiwa na mchango mkubwa.Hii ni fursa ya Tanzania kunufaika na uwekezaji wenye tija kutokea China, hasa kipindi hiki ambacho Rais Dk John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali zao.Ni muda muafaka wa kufungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya madini kutokea China na tena siyo kwenye miradi ya kawaida, ila miradi mikubwa mikubwa. Mrejee na wataalamu wabobezi wa kwenye utafiti, uchimbaji, uuzaji wa madini na biashara na huduma nyingine ziendanazo na sekta hiyo muhimu.Kwa kuwa ziara hiyo inahusisha wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wa kati ni muda muafaka wa wafanyabiashara hao kila mmoja kwa nafasi yake kutafuta fursa za kibiashara. Uamuzi wa wizara ya madini kwenda China na wafanyabiashara wa ngazi hizo ni uamuzi wenye tija, unaoweza kubadilisha mwenendo wa biashara hiyo nzima, kwa kuwa wanaweza kunufaika moja kwa moja kutokea kwa wenzao wa China.Kwa kuwa China kuna soko kubwa la madini, huku kukiwa na wataalamu na wawekezaji wa uhakika, zaidi hivyo ni uhakika kuwa kwa kushiriki kongamano hilo, sekta ya madini itapata mwanga.Ni vema mtakaporejea muwe mmepata wawekezaji wakubwa kwenye uchimbaji wa madini, ambao wataifanya kazi ya uchimbaji hapa nchini kwa ajili ya kukuza uchumi na kuwawezesha watanzania kunufaika zaidi. Kwa kuwa nchini ipo miradi mikubwa inayoweza kutumika kuzalisha umeme, kama vile madini ya makaa ya mawe ya Kiwira, ni vema pia nayo itafutiwe uwekezaji mkubwa zaidi ili izalishe kiwango kikubwa cha umeme.Kwa kuwa kwenye ziara hiyo, watakuwepo wataalamu kutoka Chuo cha Madini, Shirika la Taifa la Madini(Stamico), Chama cha Wachimbaji wa Madini na wadau wengine, wanapaswa kuwa washauri wakubwa kwa wafanyabiashara hao wa kati na wa chini juu ya namna bora ya kupata wawekezaji au kwenye uimarishaji wa miundombinu za kuwekeza kwenye migodi yao.Ziara hiyo ifungue milango kwa wawekezaji kutokea nje ya nchi, kuja kuwekeza nchini. China ni mwekezaji mkubwa nchini na kila kukicha serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), imekuwa ikipata mawazo na mikakati ya maendeleo ya uwekezaji nchini kwa kushirikiana na China.
KITAIFA
NAIROBI, KENYA TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imetangaza kuwa robo ya vituo vyote vya kupigia kura nchini hapa havina huduma nzuri ya mtandao wa simu wenye kasi wa 3G au 4G. Tume imesema maafisa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo hivyo watalazimika kusogea hadi maeneo yenye huduma nzuri ya mtandao ndipo waweze kurusha matokeo. Taarifa ya tume hiyo inasema kuna jumla ya vituo 11,155, ambavyo havina huduma nzuri ya mtandao wa 3G kati ya jumla ya vituo 40,883 kote nchini humo. “Maafisa wasimamizi wa uchaguzi watatafuta mahala penye huduma nzuri ya mtandao au watumie simu za setelaiti kurusha matokeo,” tume hiyo imeandika kwenye Twitter. Vituo hivyo visivyo na huduma nzuri ya simu vinapatikana katika kaunti 45 kote nchini humo. Ni kaunti za Nairobi na Mombasa pekee ambazo hazijakumbwa na tatizo hilo. Takwimu kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya zinaonesha maeneo mengi nje ya miji nchini humo hayana huduma ya 3G. Ripoti kuhusu huduma ya simu na mtandao nchini Kenya ya mwaka jana inaonesha huduma ya 3G inapatikana kwa asilimia 17 pekee ya ardhi ya Kenya. Hata hivyo, tofauti katika wingi wa watu maeneo mbalimbali, huduma hiyo huweza kufikia asilimia 78 ya wananchi nchini humo.
KIMATAIFA
Kwa sasa, kuna watumiaji wa huduma ya M-Pesa zaidi ya milioni saba nchini Tanzania ambao hufanya miamala ya zaidi ya trilioni mbili kila mwezi. Ushirikiano huo mpya utawawezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutuma fedha moja kwa moja kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini ambao ni wateja wa M-Pesa kwa njia rahisi, inayofaa, salama na haraka zaidi.Hatua hiyo itafungua uwezekano wa kukuza utumaji pesa kuja Tanzania, ambao kwa sasa ni umefikia dola za Marekani bilioni 1.2. Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo pia ulihudhuriwa na Herve Chomel, Makamu wa Rais wa MoneyGram Upande wa Mauzo Kanda ya Afrika na Jacques Voogt, Ofisa Mkuu wa wa Idara ya biashara ya huduma za M-Pesa wa Vodacom Tanzania.“Kampuni ya MoneyGram inafurahi sana kufanyakazi na Vodacom katika kutoa huduma ya haraka, uhakika na salama kwa mamilioni ya wateja watakaotuma na kupokea pesa,” alisema Chomel.
UCHUMI
ISTANBUL, UTURUKI MKANDA wa sauti uliorekodi dakika za mwisho za uhai wa mwandishi wa habari raia wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, unadaiwa kufichua namna alivyouawa katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini hapa Oktoba 2 mwaka huu. Kwa mujibu wa Gazeti la Middle East Eye (MEE), mkosoaji huyo mkubwa wa Saudia aliburuzwa kutoka ofisi ya Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Mohammed al Otaibi kwenda katika meza ya chumba jirani cha kujisomea. Kuwapo  ushahidi kuwa Khashoggi, ambaye pia ana asili ya Uturuki aliuawa, kulifichuliwa mapema na wachunguzi wa Uturuki MEE linasema sauti ya Balozi al Otaibi mwenyewe inasikika katika kanda hiyo iliyonasa kifo cha Khashoggi. Chanzo kimoja cha habari chenye uhusiano wa karibu na serikali kilimnukuu balozi huyo akidai kuwa Saudi Arabia ilituma majasusi  Istanbul: ‘Msiseme hili. Mtanitia mashakani.’ Otaibi alirejea   Riyadh Jumanne wiki hii. Sauti za mkoromo wa kutisha zilisikika, kwa mujibu ya walioshuhudia waliokuwa kwenye chumba vya chini, chanzo cha habari kimesema. “Balozi mdogo mwenyewe aliondolewa kutoka chumba hicho. Hakukuwa na jaribio la kumhoji. Walikuja kumuua,” chanzo hicho kililiambia MEE. Sauti   zenye kelele ya kuogofya zilisimama wakati Khashoggi, ambaye mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi huyo Oktoba 2, alipochomwa sindano yenye kimiminika kisichofahamika. Salah Muhammad al-Tubaigy, ambaye ametambuliwa kama mkuu wa kitengo cha Ushahidi wa Alama za Vidole, Idara ya Usalama wa Jumla Saudi Arabia, ameelezwa kuwa mmoja wa kikosi cha watu 15, walioingia Ankara mapema siku hiyo kwa ndege binafsi. Magari kadhaa ya Saudi Arabia yenye nambari ya usajili ya diplomasia yalinaswa kwenye kamera za usalama za CCTV yakiingia ubalozini chini ya saa mbili baada ya  Khashoggi kuingia humo siku hiyo. Tubaigy anadaiwa alianza kuukata mwili wa Khashoggi ukiwa mezani wakati akiwa bado hai, chanzo hicho kilidai. Mauaji hayo yalichukua dakika saba, chanzo hicho kilisema. Wakati akianza kuukata kata mwili, Tubaigy aliweka spika ya masikio ‘earphones’ masikioni na kusikiliza muziki. Aliwashauri wenzake kumuiga. “Wakati nikifanya kazi hii, huwa nasikiliza muziki. Nanyi mnapaswa kufanya hivi pia,” Tubaigy alirekodiwa akisema, kwa mujibu wa chanzo hicho kwa MEE. Sehemu ya mkanda huo ilipatiwa gazeti la Sabah la hapa ambalo bado halijautoa. Chanzo hicho cha habari pia kililiambia gazeti la New York Times kuwa Tubaigy alikuwa ameshikilia msumeno wa kukatia mifupa. Maofisa wa Saudi Arabia wamekana vikali kuhusika na kutoweka mwandishi huyo wakidai aliondoka ubalozini hapo kwa mlango wa nyuma muda mfupi tu baada ya kuwasili. Hata hivyo, wameshindwa kutoa ushahidi kuunga mkono madai yao na wanadai kuwa kamera za video hazikuwa zikirekodi wakati huo. Jumanne baada ya awali kuionya Saudi Arabia, Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo walijitokeza kuikingia kifua Saudi Arabia, mshirika wao muhimu Mashariki ya Kati. Kutokana na sababu hiyo, kupotea kwa Khashoggi kumeuweka utawala huo katika hali ya kutatanisha. Lakini akizungumzia mkanda huo, Trump alisema hawezi kuamini hadi watakapopatiwa na kuuchunguza. Trump alidai kuzungumza na Mrithi wa Ufalme, Prince Mohammed bin Salman na amekana kufahamu tukio hilo. Akiendelea kuutetea ufalme huo, Trump alisema amehakikishiwa kutakuwa na uchunguzi wa kina na wa haraka kuhusu suala hilo. Rais Trump aliwaambia wanahabari Ikulu ya Marekani  kuwa, “Tumeomba kupatiwa nakala ya kanda hiyo, kama kweli ipo.”   Akigusia sauti iliyorekodiwa na ambayo inadaiwa kuwa na ushahidi wa mauaji ya Khashoggi, Trump aliongeza: “Sina uhakika wa kuwapo   sauti hiyo, lakini huenda ni kweli ipo.” Trump alisema anatarajia ripoti kutoka kwa Waziri wake, Pompeo ambaye alikuwa   Saudi Arabia na Uturuki. Rais Trump alisema ukweli kuhusu suala hilo utajulikana kufikia mwisho wa wiki. Jumatatu iliyopita, Televisheni ya  Marekani ya CNN liliripoti kuwa maofisa wa Saudi Arabia wanajiandaa kutoa ripoti itakayoonesha kifo cha Khashoggi kilitokana na mahojiano ya uchunguzi yaliyoenda mrama.
KIMATAIFA
Na CHRISTOPHER MSEKENA BAADA ya kutoka kwenye kifungo kilichotokana na kukiuka taratibu za mashindano ya urembo, shindano la Miss Tanzania lilirejea kwa kishindo mwaka jana likiwa limebeba matumaini mapya kwa Watanzania. Jamii ilichoka kushuhudia vibweka ambavyo vilionekana dhahiri ukiukwaji wa taratibu za mashindano kiasi kwamba Serikali ililiona hilo na kufikia uamuzi wa kulifungia shindano kwa lengo la kurudisha hadhi yake. Kiu kubwa ya wadau wa tasnia ya urembo ilikuwa ni kuona jukwaa la Miss Tanzania linakuwa daraja la kuzalisha ajira kwa warembo makini wenye haiba kama ya kina malkia wa nguvu, Hoyce Temu. Warembo kama hao walipatikana kutokana na taratibu za mashindano ya urembo kufuatwa vizuri na kama tunavyojua haki ikitawala basi hakuna jambo linaloharibika. Sasa shindano lilipofungiwa na baadaye kufunguliwa nilitamani kuona mabadiliko makubwa ndani ya Miss Tanzania hasa katika mambo yaliyolitia doa na kupunguza kasi ya kulifikia taji la urembo wa dunia. Turudi kwenye hoja yangu, wiki hii mrembo aliyeibuka mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka jana, Diana Edward, aliweka wazi kutokabidhiwa zawadi zake kama ilivyotakiwa. Kwanini hakupewa zawadi licha ya jamii kuaminishwa kuwa mshindi wa shindano hilo angepata zawadi ya gari na kiasi flani cha fedha. Leo mrembo wetu anaibuka na kudai hajapata zawadi zake, hii ni aibu. Ikumbukwe kuwa, Diana ndiye aliyekwenda Marekani kwenye shindano la urembo wa dunia kuiwakilisha Tanzania. Alifanya vizuri kwenye shindano hilo na kama asingefanyiwa hujuma na yule mrembo wa Kenya basi angekuwa kwenye nafasi nzuri. Mpaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) linaibuka na kuwataka waandaaji wa shindano hilo kumkabidhi mrembo wetu zawadi zake ni jambo la aibu. Tukio hili linaweza kuwa dogo lakini linapunguza heshima ya shindano. Siyo kila mtu anaweza kuwaelewa waandaaji wa Miss Tanzania, wapo watu watakaosema ubabaishaji umeingia kwenye kamati ya shindano, kitu ambacho hakipendezi na si jambo la afya kwa uhai wa tasnia ya urembo nchini. Nimalize kwa kusema kuwa shindano kubwa kama Miss Tanzania halipaswi kuchukuliwa poa hasa katika udhamini, ingawa waandaaji wa shindano hawajaweka wazi sababu za kutompa mrembo wetu zawadi zake ila inaonyesha wazi kuna tatizo nyuma ya pazia baina yao na wadhamini. Mpeni Diana zawadi zake tuijenge pamoja tasnia.
BURUDANI
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro ameagiza askari wawashughulikie wanaume wanaopiga au kuwanyanyasa wake zao.IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizindua Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto Serengeti mkoani Mara.Amesema kuna namna nyingi za ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto ukiwemo ubakaji, ulawiti, ndoa za utotoni, na mfumo dume kwenye jamii.“Mfumo dume ndugu zangu wana Mara ndio unaotusumbua, hatubadiliki, hatubadilishi fikra, hatuendani na wakati, dunia inakwenda mbele sisi tunabaki palepale” amesema Sirro.Amebainisha kuwa, suala la wanawake kupigwa au kunyanyaswa ni kubwa kwa jeshi hilo, na kwamba, mwaka jana kulikuwa na matukio 43, 487 ya kijinsia na watoto na mwaka huu yamepungua hadi 41,416.“Na nimewaambia askari ukipata mtu amempiga mke wake, kamnyanyasa mke wake na wewe mshughulikie, narudia, mshughulikie kwa nguvu ya kadri, la msingi tutakushughulikia kwa nguvu ya kadri” amesema Sirro.Amesema, wanaume wakishughulikiwa itasaidia jamii kubadilika kwa kuwa sasa imekuwa vigumu hata kupata wachumba.“Sio mtu wako, sio mtoto wako, mnakorofishana ugomvi wa kawaida, unampiga, unampiga nini, unamfundisha nini, wewe ni nani kwake. Yule mmekubaliana tu, kama unaona ndoa imekuwa na matatizo achana nae tafuta mwingine. Unamkata sikio, unampiga wewe ni nani, upo juu ya sheria? Hizo nguvu umezipata wapi, mamlaka amekupa nani kufanya hivyo” amesema Sirro.
KITAIFA
NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, (Mawasiliano), Atashasta Nditiye ametoboa siri ya kampuni za simu kwenda kinyume na bei elekezi ya serikali ya kupiga simu kwa Sh 10.40 kwa dakika moja na badala yake kutoza kwa sekunde, kinyume cha mwongozo wa watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano.Kutokana na wizi huo kwa wananchi, Naibu Waziri huyo ameagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzichukulia hatua kampuni hizo mara moja. Alitoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Sira Ubwa Mamboya alipotembelea TCRA.Dk Mamboya alifanya ziara hiyo katika mamlaka hiyo ambayo ni miongoni mwa taasisi za mawasiliano nchini ili kujifunza utendaji kazi wake kwa kuwa mawasiliano ni suala la Muungano.Nditiye alisema, mwishoni mwa mwaka jana, serikali ilitoa bei elekezi kwa kampuni za simu za mkononi wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kwamba ifikapo Januari Mosi, mwaka huu, gharama za kupiga simu lazima zipungue na kuwa Sh 10,40 kwa dakika moja wala si kwa sekunde.“Kampuni zimekuwa zikitoza tofauti wakati makubaliano yalikuwa gharama ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine itakuwa shilingi 10.40 kwa dakika moja na si kwa sekunde kwa kuwa tulikuwa tumetoka kupiga kwa shilingi 15.60 kwa dakika moja,” alisema.Nditiye alisema, hadi sasa anasikia matangazo kutoka kampuni za mawasiliano za simu wanajinadi kuwa kupiga simu mtandao wowote ni Sh moja kwa sekunde hiyo ina maana ukipiga sekunde 60 ni Sh 60 na inakuwa imezidi mara tano ya gharama ambayo ni mwongozo wa serikali kwa kampuni ya simu.“Nawataka TCRA sasa waanze kufuatilia kampuni yoyote ambayo imekwenda kinyume na bei elekezi ya serikali, kwanza, wachukue hatua za kinidhamu na wawapige faini.“Lakini pia TCRA wahakikishe fedha yetu ambayo hizo kampuni zimekuwa zikichukua isivyo halali, irudi kwa sababu mpango wa serikali ni kwamba inapofika mwaka 2022 iwe Sh mbili kwa dakika kupiga mtandao wowote wa simu.”Nditiye pia aliipongeza TCRA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakuwa juu nchini, kwani sekta ya mawasiliano kupitia wadau kama TCRA kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikichukua nafasi tatu za mwanzo kuchangia pato la serikali.
KITAIFA
['Ni likizo ya kimataifa na wachezaji wenzake wengi wapo katika zamu ya kimataifa lakini nahodha wa timu ya Taifa Stars na KRK Genk Mbwana Samatta alikuwa na mipango mingine kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania. ', 'Mshambuliaji huyo matata alitumia wakati wake mzuri wa likizo hiyo siku ya Alhamisi kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Neima Mgange.', 'Sherehe ya harusi yake iliofanyika katika kijiji cha kijichi mjini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars akiwemo Himid Mao na Thomas Ulimwengu kulingaa na gazeti hilo.', 'Ilikuwa sherehe ya kufana miongoni mwa watu wa familia ya Mgange walipokutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya.', ' Alhamdullilah.🙏 @thomasulimwengu📷 @hanya30', 'A post shared by Mbwana Samatta (@samagoal77) on Oct 11, 2019 at 2:21am PDT', 'Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa samagoal77', ' Dab 🤦\u200d♂️😂 Kanzu by @islamicfashiontz Picha by @hanya30', 'A post shared by Mbwana Samatta (@samagoal77) on Oct 11, 2019 at 3:42am PDT', 'Mwisho wa ujumbe 2 wa Instagram wa samagoal77', 'Maelezo kuhusu uhusiano wa Mbwana na Neima yalikuwa ya siri kubwa na ni watu wa familia zote mbili pekee waliokuwa wakielewa kilichokuwa kikiendelea hadi siku ya Alhamisi.', 'Mshambuliaji huyo hakushirikishwa katika mechi ya kimataifa ambayo Taifa Stars inacheza dhidi ya Uganda wikendi hii.', 'Alikuwa akiugua jeraha lakini akashirikishwa katika kikosi cha timu ya Genk kilichopoteza 6-2 dhidi ya klabu ya Salzbourg kutoka Austria katika michuano ya kombe la mataifa bingwa Ulaya. ', 'Pia aliisaidia Tanzania katika michuano ya kimakundi ya kufuzu kwa kombe la dunia Qatar 2022.', "Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema.", 'Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley.', "Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji.", 'Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya.', 'Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao.', 'Samatta, mwenye kimo cha futi 5 inchi 11, amefunga mabao sita katika ligi ndogo ya klabu barani Ulaya, Europa League, na ni hapo ameanza kuonekana na klabu za England.', "Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga 'hat-trick' dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5-2.", 'Everton wametatizika kumpata mshambuliaji wa kutegemewa tangu nyota wao Romelu Lukaku alipowaacha na kuhamia Manchester United kwa £75 mwaka 2017.', 'Wamekumbwa na ukame wa mabao msimu huu na zaidi wamesaidiwa na mawinga au viungo wa kati badala ya washambuliaji wao ambao wameonekana butu.', 'Ndio maana si ajabu wanavutiwa na mchezaji ambaye ameibuka stadi wa kutikisa nyavu.', 'Walijaribu kujaza pengo kwa kumchukua mchezaji wao wa zamani Wayne Rooney lakini mshambuliaji huyo hakuvuma sana na mwishowe alihamia Marekani.', 'Mshambuliaji wao wa sasa Oumar Niasse, kwa mujibu wa msn.com anatarajiwa kuihama klabu hiyo ya Merseyside, na inaarifiwa meneja wao Marco Silva anatafuta mchezaji wa kujaza nafasi hiyo.', 'Cenk Tosun alikuwa amenunuliwa na klabu hiyo Januari lakini baada alianza vibaya kisha akaimarika kabla ya kudidimia tena. Mturuki huyo amewafungia bao moja pekee msimu huu. Alikuwa kwenye benchi mechi yao dhidi ya Leicester City Jumamosi.', 'Klabu nyingine za Ligi Kuu ya England - West Ham United, Burnley na Brighton - pia zinadaiwa kumfuatilia kwa karibu mchezaji huyo kutoka Afrika Mashariki.', 'Gazeti la Daily Mirror Jumamosi liliripoti kwamba West Ham wanamfuatilia mchezaji huyo ingawa walisema Everton wanaonekana kuwa na uzito zaidi wa kumtafuta ikizingatiwa kwamba Niasse anatarajiwa kuuzwa Januari.', 'Everton tayari wana uhusiano na Afrika Mashariki kupitia mdhamini wao SportPesa, na waliibuka kuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kuchezea Afrika Mashariki walipocheza dhidi ya mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia katika Kombe la SportPesa Super Cup mwaka jana.', 'Watakuwa pia klabu ya kwanza ya England kuwa mwenyeji wa klabu ya soka ya Afrika Mashariki watakapowakaribisha nyumbani Gor Mahia uwanjani Goodison Park mwezi ujao.', 'Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20.', 'Amesalia na miezi 20 hivi kabla ya mkataba wake kumalizika.', 'Samatta alihamia Ubelgiji mwaka mmoja baada yake kutawazwa mchezaji bora wa mwaka Mwafrika aliyekuwa anacheza ligi za barani Afrika mwaka 2015.', 'Alishinda vikombe sita vikuu akiwa na TP Mazembe ikiwa ni pamoja na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015 kabla ya kuondoka.', 'Kufikia Machi mwaka huu, alikuwa ameichezea timu ya taifa ya tanzania mechi 44 na kuwafungia mabao 16 tangu alipowachezea mara ya kwanza mwaka 2011.', 'Samatta aliichezea Simba kabla ya kujiunga na TP Mazembe mnamo mwaka wa 2011.', 'Ingawa Mtanzania huyo amevuma sana msimu huu, ambapo alifunga mabao manane katika mechi 11 za kwanza, msimu uliopita hakufanya vyema sana. Alifunga mabao saba katika mashindano yote akichezea klabu yake msimu wa 2017/18.']
MICHEZO
USISHANGAE kuwaona akina fulani wanadumu kwenye uhusiano wao kwa muda mrefu huku kwa upande wako mambo yakiharibika. Usije kujiuliza ni vipi kwao tu, kwako mambo hovyo? Ni kwamba wenzako wanawekeza kwenye uhusiano, wakati wewe ukienda ilimradi siku zinakwenda. Kwa hakika hamuwezi kuwa sawa. Ndiyo sababu tunajifunza somo hili. Ni mada iliyoanza wiki iliyopita na leo tunamalizia sehemu ya mwisho. Tunaangalia ni mambo gani wanawake wanavutiwa zaidi kwa wanaume. Au niseme vitu gani ukivifanya kwa mwanamke wako hatafikiria kukuacha. Tuendelee na mada yetu.   KUMSIFIA Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Kumsifia mwanamke kuna nafasi kubwa sana kwake. Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.   MALENGO Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mwenzi wake basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika. Hii si sahihi. Mwenzako anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia. Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mwanamke kamili katika penzi lenu.   MPE KIPAUMBELE Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea akawa katika hali hiyo, msikilize. Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba yupo na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo. Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe. Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.   TENDO LA NDOA   Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.” Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara? Kuna kitu nimesahau? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Jiandae kupata kitabu changu kipya cha SIRI ZA MAISHA YA NDOA YENYE FURAHA kitakachokuwa mitaani hivi karibuni.
BURUDANI
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm, Meru alisema hayo leo wakati akizungumza katika maonesho ya kimataifa ya bidhaa mbalimbali kutoka nchini Uturuki.Dk Meru alitaka kampuni za Uturuki zifikirie kuwekeza nchini haswa katika viwanda vya uzalishaji, hususani katika viwanda vya nguo, ili Watanzania wengi wanufaike na teknolojia waliyonayo.“Fikirieni kuwekeza na kujiimarisha katika viwanda vya uzalishaji…Watanzania wanahitaji kupata faida, teknolojia pamoja na kukuza uchumi wetu,” alisema Dk Meru na kuongeza kuwa ingawa ziko kampuni chache kutoka Uturuki hapa nchini, lakini waongeze wigo.Akifungua maonesho hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk Reginald Mengi alisema kupitia maonesho ya Waturuki, Watanzania wajifunze kupitia bidhaa hizo kwa kuwa na ubora na bei rahisi.Alisema Watanzania wanahitaji kujifunza ujuzi kutoka Uturuki na kuutumia katika kuzalisha bidhaa zao na kuwa bora zenye kukubalika.
UCHUMI
LIGI Daraja la Kwanza imezidi kuchanja mbuga ikimalizika mzunguko wa sita, huku timu zikionesha ushindani mkubwa. Katika Kundi A, Mawenzi Market inaongoza ikiwa na pointi 10 sawa na Mlale FC, Namungo FC na Mbeya Kwanza zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Friends Rangers na Majimaji FC zina pointi tisa kila moja, Mufindi United ina pointi nane, Reha FC ina pointi saba, Ashanti United ina pointi sita, Kiluvya United ina pointi tano, Njombe Mji ina pointi nne na Dar City ina pointi tatu. Pamba FC inaongoza Kundi B ikiwa na pointi 11, sawa na timu za Boma FC na Arusha United, lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.Geita Gold na Rhino Rangers zina pointi 10 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa, Polisi Tanzania ina pointi tisa, Green Warriors na Dodoma FC zina pointi nane nazo zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.Transit Camp ina pointi saba, Mashujaa FC ina pointi sita, Arusha FC ina pointi tatu na Mgambo Shooting ina shika mkia ikiwa na pointi mbili. Kila timu itakayokuwa inashika nafasi ya kwanza itapanda Ligi Kuu moja kwa moja, huku mshindi wa pili akichezeshwa pamoja na timu, ambazo zitashika nafasi ya 17 na 18 katika Ligi Kuu baada ya msimu kumalizika ili kupata timu mbili zitaungana na mshindi wa kwanza wa kila kundi kupanda Ligi Kuu.
MICHEZO
Na AGATHA CHARLES WATUMISHI wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wamekamatwa katika operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kusaidia kupitisha kemikali bashirifu za ephedrine zinazotumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya heroine. Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizoko Upanga, Dar es Salaam, Kamishna wa Operesheni hiyo, Mihayo Msikhela, alisema pamoja na hao, wapo watumishi wengine wawili wa TRA ambao nyendo zao zinafuatiliwa. “Wakati wa kukabidhiwa majina ya watu wanaojihusisha na dawa hizo nilitamka kuwa wapo watumishi wa umma wanaosaidia kuingiza hasa kemikali bashirifu,” alisema. Kuhusu watumishi hao waliokamatwa ambao hata hivyo hakuwa tayari kuwataja kwa majina, alisema taratibu zinafanyika na wakati wowote watafikishwa mahakamani. Kamishna Msikhela alisema tayari operesheni hiyo inayofanyika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kwa kukamata wasambazaji, wauzaji, watumiaji na kuharibu dawa za kulevya zilizoko mashambani, imeonyesha mafanikio ndani ya siku nne za mwanzo.  “Dawa za kulevya ziko katika makundi mawili, kundi la kwanza ni dawa za kulevya zilizoko mashambani na kundi la pili ni dawa za kulevya za viwandani. Na dawa za kulevya za mashambani kwa kiwango kikubwa ndio kero iliyopo kwa wananchi wetu. Matokeo haya ni operesheni ya siku nne tu hadi jana (Alhamisi),” alisema Kamishna Msikhela. Alisema Mkoa wa Simiyu umeongoza kwa kuteketeza ekari 40 za bangi ukifuatiwa na Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya kwa ekari 36 huku Lindi ukiongoza kwa kukamata dawa za viwandani aina ya heroine ambazo ni kete 50. Kamishna Msikhela alitaja mikoa mingine iliyofanya vyema katika operesheni hiyo kuwa ni Tanga ambayo ilikamata mirungi kg 44, bangi puli 3, Morogoro (bangi kg 18, heroine kete 3),  Shinyanga (bangi kg 10 na gramu 136), Kagera (bangi ekari 14, mirungi ekari 1), Njombe (bangi nusu ekari na gramu 20), Songwe (heroine kete 274, mirungi kg 3), Tabora (bangi kilo 6, mbegu kg 18),  Singida (bangi misokoto 203, heroine kete 1), Rukwa (bangi kete 105), Mbeya  (bangi kg 5), Kigoma bangi nusu ekari na Ruvuma bangi gramu 300. Kamishna huyo alisema watuhumiwa hao ni wengi na wanaendelea kuhojiwa ambapo baadaye utafanyika utaratibu wa kisheria kuwafikisha mahakamani. “Kama tutaendelea na mlipuko huu ambao umeongezewa mafuta, nina uhakika dawa za kulevya mashambani zinaweza kupungua kwa kiwango kikubwa. Tuunganishe nguvu na kuhakikisha vita hii inapiganwa kila sehemu,” alisema Kamishna Msikhela. Akijibu swali la waandishi kuhusu kutaja na kushughulikia majina 97 wakiwemo wanaodaiwa kuwa ni vigogo na watoto wa vigogo, Kamishna Msikhela alisema kila aliyetajwa ataguswa. “Yeyote aliyetajwa kwenye orodha hiyo ambayo ni orodha yenye fumbo ataguswa, hatutazami kwamba kigogo ni yupi na yupi si kigogo, yaliyomo mle ni majina ya wahalifu kama wahalifu wengine,” alisema Kamishna Msikhela. Alisema orodha hiyo ambayo haina muda mrefu tangu ikabidhiwe kwao, ufuatiliaji umeanza na hivyo atatoa taarifa. Akijibu swali lingine kuhusu orodha za awali zilizowataja kwa majina watuhumiwa huku ile ya majina 97 wakifichwa, Kamishna Msikhela alisema ni mfumo unaotumika. “Ni mfumo uliotumika, yapo makosa ya mtaani hayaendelei kusumbua tena. Yapo makosa yaliyo wazi na yapo makosa yaliyojificha. Kwa hiyo yaliyo wazi tutajua yalikuwa katika hatua ipi na yaliyojificha yako kwenye hatua ipi na yanafanywa vipi,” alisema Kamishna Msikhela. Kamishna Msikhela alisema: “Vita ina mifumo mbalimbali ya upiganwaji, kwa hiyo mifumo yote itatumika ilimradi itakupelekea kwenye mafanikio na ukatoka umetangazwa you’re a hero (shujaa) yote huwa inatumika.” Alisema vita ya dawa za kulevya ilianza miaka ya nyuma na kinachofanyika hivi sasa ni mwendelezo kama ilivyo upambanaji duniani kote. “Huu ni mwendelezo kama ilivyo dunia nzima inavyopiganwa na sisi tunawajibika kupigana hii vita mpaka dunia itakapoweza kuipunguza kabisa au kuimaliza,” alisema Kamishna Msikhela.   Kamishna Msikhela alisema pamoja na Mamlaka hiyo iliyotangazwa hivi karibuni, lakini pia kuna vyombo vya ulinzi na usalama na hasa Jeshi la Polisi ambavyo utaratibu wa kuripoti na kufanya majukumu yake uko pale pale.
KITAIFA
Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike mwaka jana lakini baadhi ya wanachama walimwomba Mwenyekiti anayemaliza muda wake Yusuf Manji kuendelea kuwania tena nafasi hiyo kitu ambacho kilimlazimu kuwaomba wanachama hao asogeze mbele uchaguzi ili apate muda wa kufikiria ombi lao.Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili, aliwataka watu mbalimbali wenye mapenzi ya dhati na klabu hiyo kujitokeza kuwania nafasi hizo kwa lengo la kuipa mafanikio zaidi klabu hiyo.“Jambo hili ni la kikatiba na wala halina mjadala, tunataka Yanga iwe na viongozi ambao watatokana na utashi wa Wanayanga ni matumaini ya Kamati ya Uchaguzi kwamba hapatatoka mtu mwingine wa kutaka kuvunja misingi ya Katiba,”alisema Kaswahili.Alisema lengo la kutangaza tarehe ya uchaguzi mapema ni kutaka kupata viongozi wapya ambao watapata muda mzuri wa kuiandaa timu kwa ajili ya kutetea ubingwa wao wa bara msimu ujao na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ambayo mwakani.Kaswahili alisema fomu za kuwania uongozi kwenye klabu yao zitaanza kutolewa keshokutwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zitawekwa kwa nia njema ya kuhakikisha klabu yao inapata viongozi bora.Mara ya mwisho Yanga ilifanya Uchaguzi wake Mkuu Julai 18,2010 ambapo Lloyd Nchunga alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Delvis Mosha alichaguliwa katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti huku wajumbe wakiwa ni Charles Mgondo, Ally Mayay, Mzee Yusuf na Theonest Rutashobolwa, Titus Ossoro, Sara Ramadhani, Mohamed Binda na Salum Rupia.Lakini baadhi ya viongozi hao walijiuzulu nyadhifa zao na hivyo ikalazimika kufanyika uchaguzi mdogo Julai 15,2012 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na Manji alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Clement Sanga akichaguliwa kama Makamu Mwenyekiti na nafasi za Wajumbe wakachaguliwa Aaron, Nyanda, George Manyama, Abdallah Bin Kleb na Valentine Katabalo.
MICHEZO
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kusimamia utendaji kazi katika maeneo yao ili kuendana na kasi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.Majaliwa ametoa agizo hilo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa umma katika ziara yake mkoani Tabora, ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuziba mianya yote ya uzembe kutoka kwa watendaji na ikibidi kuchukua hatua pale inapostahili.Amesema kila kiongozi aliyepewa dhamana katika serikali hii ya awamu ya tano anapaswa kuwa makini katika kusimamia majukumu aliyopewa ili kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, tofauti na hayo atakuwa anakwenda kinyume na hivyo kutakiwa kuwajibishwa kama hatoweza kujiwajibisha yeye mwenyewe.Amesema serikali iliyopo madarakani hivi sasa chini ya Rais John Magufuli inafanya kazi huku ikiweka kipaumbele cha kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia matakwa ya uadilifu na weledi mkubwa kwa kila mtumishi wa umma, na kwamba haitokuwa tayari kuwaona watumishi wazembe, wala rushwa au wabadhirifu wa mali za wananchi wakipata nafasi ya aina yoyote.“Ili kuleta tija ya kiutendaji wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri mnapaswa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri zenu, ikiwemo kusikiliza na kutatua kero za wananchi, hakikisheni mnakuwa na mpango kazi wa kila siku ili kuharakisha maendeleo,” amesema Majaliwa.Pamoja na hilo pia aliwataka viongozi na watumishi wa umma kuwahudumia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao wala uwezo wao kifedha.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema wilaya zote zinatakiwa zihakikishe zinakuwa na angalau na shule moja ya kidato cha tano na sita katika kila tarafa nchini na kwamba Serikali itapeleka walimu.Amesema uwepo wa shule hizo utaamsha ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii, jambo litakaloongeza idadi ya wanafunzi watakaoendelea na masomo ya kidato cha tano na sita huku akitaka kuwekwa mkazo zaidi katika usimamizi wa watoto wa kike ili waweze kumaliza masomo yao salama."Huu ni mkakati wa Taifa tunataka watoto wa kike wote walindwe ili waweze kumaliza shule na marufuku kukatisha elimu yao, iwe kwa kuwapa ujauzito au kuwaoa, adhabu yake ni kali, na hili naomba mlisimamie kikamilifu” aliongeza Waziri Mkuu.Mbali na hatua hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya kuwanyonya wananchi kwa kupiga dili na kujinufaisha wenyewe na kwamba kama wanataka kwenda na tabia hiyo, ni vyema wajiondoe mapema.Alisema viongozi wanaowaumiza wananchi wanaovuja jasho lao wasidhurumiwe wapewe haki zao kutokana na shughuli wanazozifanya ambazo zitawaletea manufaa katika maisha yao na waweze kufikia malengo yao.Amesema wapo baadhi ya viongozi wanaowaumiza wananchi wanaovuja jasho lao wakifanya hivyo kwa tamaa zao, akiwataka kuacha tabia hiyo na badala yake wawape wananchi haki zao kutokana na shughuli wanazozifanya ambazo zitawaletea manufaa katika maisha yao na waweze kufikia malengo yao.Majaliwa amebainisha kuwa serikali imeandaa utaratibu wa hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika kuwaumiza wananchi ambao wakulima na kupiga dili kujinufaisha wenyewe na kama wanakwenda kwa lengo hilo wajiondoe mapema.Hata hivyo, alisema ushirika utakaotunza mali za wakulima ili aweze kunufaika kwa kazi zao ili waondokane na hali ya ugumu wa maisha na waweze kuzitunza familia zao vizuri.Kadhalika Waziri Mkuu amewaahidi wananchi wa manispaa hiyo ya Tabora kuwa atamuagiza Waziri wa Ardhi, William Lukuvi afike kutatua migogoro ya ardhi na kuimaliza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wengi wa mkoa huo kuwa wamedhulumiwa.Alibainisha kuwa Waziri wa Ardhi, Lukuvi ana uwezo mkubwa wa kuwatendea haki wananchi kwa kuhakikisha wanapata haki zao za msingi kwa wale wote walidhurumiwa.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri aliwataka watumishi wa umma katika mkoa wake kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali kila mtu atambue ni nini serikali ya awamu ya tano inataka na hivyo watekeleze wajibu wao kikamilifu.
KITAIFA
Timu za taifa za Para Taekwondo na Taekwondo zilizoondoka nchini mwishoni mwa wiki na kwenda Morocco kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika ya Taekwondo.Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Machi 28-30 wakati yale ya Para Taekwondo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu, itaanza siku moja baadaye.Rwanda ambao walikuwa wenyeji wa mashindano ya Para Taekwondo mwaka jana, walimaliza kileleni katika msimamo wakiwa na medali sita, zikiwemo mbili za dhahabu tatu za fedha na moja ya shaba.“Baada ya miezi mitatu ya mazoezi ya nguvu, sasa tuko tayari kwa ajili ya kusaka medali nchini Morocco," alisema Bagire siku moja kabla timu haijaondoka kwenda Morocco.Aliongeza kusema: “Wachezaji wangu wana uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ambao nina uhakika utatuongoza sisi katika ushindi. Tutacheza dhidi ya baadhi ya wachezaji bora Afrika lakini sisi ni mabingwa watetezi wa Para Taekwondo na tunatakiwa kuonesha kuwa ushindi wetu wa mwaka jana hatukubahatisha.Ikishika nafasi ya nane katika ubora wa mchezo huo Afrika, kwa mujibu wa Shirikisho la Dunia la Taekwondo (WTF), Rwanda itakuwa ikisaka mafanikio ya kutetea taji lao la Afrika walioutwaa mwaka jana mjini hapa.Katika mashindano hayo ya Afrika, Rwanda itakuwa na timu iliyokamilika ya wachezaji 14, nane katika taekwondo na sita katika Para Taekwondo. Wapambanaji wa Rwanda watakutana na ushindani mkali kutoka kwa wenyeji Morocco, Misri, Algeria, Tunisia na Gabon.Timu kamili: Para Taekwondo: Jean de la Croix Nikwigize, Consolee Rukundo, Jean Claude Niringiyimana, Jean Marie Vianney Bizumuremyi, Parfait Hakizimana na Jean Pierre Manirakiza Taekwondo: Benoit Kayitare (captain), Savio Nizeyimana, Vincent Munyakazi, Moussa Twizeymana, Delphine Uwababyeyi, Raissa Umurerwa, Aline Ndacyayisenga na Benise Uwase.
MICHEZO
JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma hatahudhuria mazishi ya mwanaharakati wa kuipinga serikali ya ubaguzi wa rangi Ahmed Kathrada kwa ombi la familia yake. Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu mwaka uliopita, kufuatia kashfa za ufisadi. Aidha mke wa Kathrada, Barbara Hogan anafahamika kuwa mkosoaji mkubwa wa Zuma. Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa ataiwakilisha serikali kwenye mazishi hayo. Kathrada (87) aliyefariki dunia juzi, alifungwa pamoja na shujaa wa Afrika Kusini Nelson Mandela kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi. Alitumikia kifungo cha miaka 26 gerezani kabla ya kaachiwa huru mwaka 1989. Baadaye alihudumu kama mshauri Rais Mandela, kwenye serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia. Zuma alikuwa ameagiza bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo chake, na kuahirisha mkutano wa mawaziri ili maafisa wapate kuhudhuria mazishi yake.
KIMATAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, alisema mwishoni mwa wiki kuwa ni vizuri wafanyabiashara mkoani humo na Watanzania kwa ujumla wake, wakachangamkia fursa hizo na kuufanya mkoa huo eneo la kuvutia wawekezaji.“Dodoma ya leo siyo ya miaka ishirini iliyopita, kwani ina mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii pia ni kitovu cha elimu, hivyo mna kila sababu ya kujipanga nakuangalia ni namna gani mnaweza kuifanya Dadoma kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji hapa nchini,” alisisitiza.Akizindua Baraza la Biashara la Mkoa huo (RBC), Gallawa alisema Baraza kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, linapaswa kutangaza vivutio vilivyopo Dodoma kwa lengo la kupata wawekezaji ili kupiga hatua kiuchumi.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi alisema amefurahishwa kwa mwitikio mkubwa wa wadau katika ufunguzi wa baraza hilo na kuwataka kutumia uwepo wa baraza katika kujadiliana juu ya fursa zilizopo na namna ya kuboresha mazingira ya biashara.Alisema umuhimu wa baraza hilo ni kutatua matatizo yanayowakabili wafanyabiashara hivyo ni jukumu la sekta za umma na binafsi kukaa pamoja na kujitathmini ili kufikia lengo la kukuza uchumi wa mkoa na maendeleo kwa ujumla.
UCHUMI
SIMBA tayari imemaliza kazi moja na inatarajia kuanza nyingine mpya kabisa. Ndiyo, wamemaliza vyema safari ya kupambana na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika! Simba imeingia hatua hiyo baada ya kucheza mechi nne za kimataifa na sasa inatembea kifua mbele ikitamba kila kona, si wachezaji wala viongozi.Siyo mashabiki wala wanachama lakini pia hata watanzania wenye mapenzi ya kweli na soka la nyumbani wamekuwa na msisimko wa kutosha kwa Simba kufika hatua hii. Si kwamba wekundu hao wamebahatisha kupata mafanikio hayo kidogo ambayo ni makubwa kwa sasa ukilinganisha na mara ya mwisho timu za Tanzania kufika hatua hiyo. Nitakwambia kwa nini? Ila kwa faida yako mara ya mwisho Tanzania kufikia hatua hii ilikuwa 2003 na Simba hii ndiyo ilipindua meza kibabe.Kwanza, ilimnyoosha bingwa mtetezi wa wakati huo, Zamalek ya Misri na kutinga hatua ya makundi na sasa imerudia tena makali yake hayo baada ya kupita miaka 15 bila Tanzania kuonekana katika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu Afrika. Turejee kwa nini Simba haikubahatisha kufanya hivyo. Msingi wa timu hiyo, tangu inaanza kufanya mabadiliko ya uongozi, wimbo wao mkubwa ulikuwa ni kufika hatua kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.Bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’ambaye ni mwekezaji mwenye hisa asilimia 49 kwa klabu hiyo alipambana kwa kila namna pamoja na viongozi wengine wa timu hiyo kuhakikisha wanakuja wachezaji wakali na wanapata wanachokihitaji ili mambo tu yaende sawa. Haikuishia hapo, benchi la ufundi la timu hiyo lilipigwa msasa wa kutosha kama siyo kusafishwa vyema ili tu apatikane mtu sahihi atakayewaongoza kufika nchi ya ahadi ambayo sasa Simba ipo.Ilianza mtihani wake wa kwanza kwa timu ngumu ya eSwatini, Mbabane Swallows ingawa safari hii ilionekana kuyumba na Simba ikatumia mwanya huo bila ya kupoteza muda na kuifumua mabao 4-1 katika mechi ya kwanza ailiyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao yalifungwa na John Bocco, Clatous Chama na Meddie Kagere. Katika mechi ya pili iliyopigwa kwenye ardhi ya Mfalme Mswati, Simba iliamua kufanya maajabu hukohuko ugenini kwa kuwabubujua wapinzani wao kwa mabao 4-0.Katika mechi hii, Chama aliweka mabao mawili murua na kisha Emmanuel Okwi na Kagere wakakandamiza moja kila mmoja. Hatua iliyofuata, wakakutana na Nkana FC kutoka Zambia. Hapa haikuwa shughuli nyepesi na hapa ndipo Simba ilipoonesha kwa kiasi gani ilikuwa na kiu ya mafanikio ya kufika katika hatua ya makundi. Ilianza kwa kipigo kule Kitwe, Zambia kwa kuchapwa mabao 2-1.Licha ya Simba kukukuruka na kupambana kutengeneza nafasi nyingi lakini Nkana walisimama imara katika ardhi yao ya nyumbani na mwisho Simba ikaondoka Zambia kichwa chini. Hazikuwa hisia nzuri kwa watanzania hasa mashabiki wa Simba, waliamini hawana chao na shughuli ndiyo imeishia hapo. Historia ya Nkana dhidi ya Simba haikuwa nzuri hata kidogo. Hapo awali Simba haikuwahi kukutana na Nkana na ikatoka salama na mara zote wamekuwa wakizidiwa bao moja tu katika matokeo ya jumla mwisho kutupwa nje ya mashindano.Lakini safari hii, historia haikufanya kazi na hisia mbaya pia hazikuwa na nguvu zaidi ya matumaini na mapambano ya kweli yaliyojaa mioyoni mwa wachezaji wa timu hiyo, ndicho kilichoirejesha Simba kwenye ramani ya soka la Afrika. Mechi ya pili iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa z utata huo. Maelfu ya mashabiki walijitokeza kuipa nguvu timu yao ingawa mapema walianza kukatishwa tamaa na kuamini hawana chao baada ya dakika ya 17 ya mchezo, Walter Bwalya kuipatia Nkana bao la kuongoza na kuifanya mechi kuwa ngumu zaidi. Katika mechi hiyo, Simba ilihitaji ushindi wa bao 1-0 pekee ili isonge mbele kwa kuwa walikuwa wakilindwa na lile bao moja la ugenini walipofungwa 2-1.Lakini kwa bao la Bwalya, Sasa Simba ilihitaji ushindi wa mabao kuanzia matatu huku wakiwa hawajaruhusu jingine ili ikate tiketi ya kuingia makundi. Simba ilijitutumua na kuamini bado wana nafasi. Jonas Mkude aliyelelewa na kukulia katika timu ya vijana ya Simba kwa muda mrefu akiwa hajaifungia bao timu hiyo, siku hiyo ndiyo ilikuwa wakati wake wa kulipa fadhila kwa kupiga shuti nje ya 18 na kumzidi mlinda mlango wa Nkana na mpira kujaa wavuni dakika ya 29. Shangwe zenye matumaini finyu zililipuka na Simba wakacharuka wakitandaza kabumbu huku wakilisakama lango la wapinzani hao na zikiwa zimesalia sekunde chache kwenda mapumziko, Kagere akaiandikia Simba bao la pili.Kazi ikawa imelainika lakini ikahitajika shughuli ya ziada ili kuwa na uhakika juu ya hilo. Baada ya vuta nikuvute, wengi wakiamini mshindi ataamuliwa kwa matuta kama ilivyotokea mwaka 2003 wakati Simba inaingia hatua ya makundi kwa mara ya mwisho, Clatous Chama akaiandikia Simba bao la tatu dakika ya 88. Lilikuwa bao safi, litakalobaki kwenye kumbukumbu ya watanzania wengi kwa miaka mingi kuliko unavyofikiri. Alifunga kwa kisigino chepesi akiwahadaa kipa na beki wa Nkana baada ya kupokea pasi ndani ya 18 kutoka kwa Hassan Dilunga.Huo ukawa mwisho wa Nkana katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ukawa mwanzo mpya kwa Simba katika michuano hiyo. Jana ndiyo droo ilitarajiwa kupangwa mjini Cairo, Misri. Timu zilizofuzu hatua hiyo ni Al Ahly ya Misri, TP Mazembe (Congo DR), Wydad AC (Morocco), Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates (Afrika Kusini).AS Vita Club (Congo DR), CS Constantine na JS Saoura (Algeria), Ismaily SC (Misri), Lobi Stars (Nigeria), FC Platinum (Zimbabwe), Horoya SC (Guinea), CA African (Tunisia), Asec Mimosas (Ivory Coast) hizi ndiyo timu zinazotarajia kuumana na Simba katika makundi. Hakuna timu ya kubeza hapo. Hakuna timu nyepesi, wote hawa ni wazoefu na wamejipanga kila kona kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ‘ndoo’.Hiki ni kipimo halisi cha Simba yenye malengo na inayojitutumua kuandika kwa wino mwekundu jina lake katika ramani ya soka la Afrika. Inawezekana popote na muda wowote kama kweli Simba itayavaa mashindano hayo kikamilifu na kuendeleza kile ilichoanza kukifanya tangu katika mechi za awali. Simba hii ina kikosi kipana na chenye kutafuta matokeo kwa machozi, jasho na damu. Inaweza kupambana kwa ajili ya nembo yao kubwa lakini pia ikiiweka begani Tanzania na kudhihirisha Afrika Mashariki sio ya kinyonge! Kila la heri Simba katika mapambano yenu, ni wakati wenu kuudhihirishia ulimwengu wa soka juu ya nini Simba imedhamiria kufanya, inataka kuonesha nini na imepanga kulitawala soka la Afrika.
MICHEZO
NA MWANDISHI WETU MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amezindua studio ya kisasa ya Kaburu Record iliyogharimu Sh milioni 130. Mmiliki wa studio hiyo iliyopo Sinza Palestina ametakiwa na mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anakuza vipaji vya wasanii wachanga ili wafikie mafanikio. Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika juzi, Hapi alisema Serikali inaunga mkono uwekezaji uliofanywa na vijana hao na kwamba ni wakati sasa wa wenye vipaji kupata ajira kupitia vipaji vyao ili wajikwamue kimaisha,” alisema. Kwa upande wa Mkurugenzi wa studio hiyo, Msafiri Peter ‘Papa Misifa’, alisema: “Najivunia kufanyakazi na wasanii wenye majina makubwa kwa sasa katika muziki nchini akiwemo Diamond, Rich Mavoko, Timbulo, Dayna na wengine hivyo tutaiendesha ili kutimiza malengo na mafanikio ya wasanii wanaochipukia,” alisema.
BURUDANI
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuwa tayari amepata dawa ya kumaliza tatizo la safu ya ulinzi kuruhusu kufungwa mabao kabla ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo keshokutwa.Katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha Simba na Azam FC ambao ulimalizika kwa wekundu hao wa Msimbazi kushinda 4-2, safu yake ya ulinzi ilionekana kufanya makosa ya wazi hali iliyotia hofu kwa baadhi ya mashabiki juu ya mchezo wao dhidi ya UD Songo.Katika mchezo wa kwanza Simba na UD Songo zilimaliza dakika 90 bila kufungana hivyo ili Simba isonge mbele inahitaji kupata ushindi wa aina yoyote.Akizungumzia hali ya maendeleo ya timu yake kocha huyo raia wa Ubelgiji alisema kuwa, baada ya mchezo wa Azam alianza kulifanyia kazi tatizo hilo na tayari ameshalimaliza, Alisema kulikuwa na makosa kadhaa yaliyokuwa yakifanyika sio tu kwa mabeki bali timu nzima hivyo yote ameshayarekebisha.Aliongeza kuwa mchezo huo ni muhimu kwa timu yake hivyo amejaribu kuiandaa timu kuepuka kufanya makosa yatakayoigharimu timu.“Tunajaribu kadiri tuwezavyo kurekebisha makosa yetu tuliyoyabaini katika mechi zilizopita, wengi wanaona tatizo kubwa ni safu yetu ya ulinzi lakini nilichokifanya ni kuiboresha timu yote. “Kwenye mpira timu inapofungwa makosa huwa yanaanzia mbali, ushambuliaji kiungo na kumalizikia kwa mabeki,” alisema Aussems.
MICHEZO
MAMLAKA ya Manunuzi ya Vifaa vya Umma (PPDA) imetaka muongozo unaoweka bayana kuwa asilimia 30 mikataba ya mafuta nchini Uganda iende kwa wakandarasi wa ndani ya nchi, ili kuimarisha uwezo wa wananchi wa Uganda. Mkurugenzi Mkuu wa PPDA, Benson Turamye alisema muongozo huo wa asilimia 30 kwa wakandarasi wa ndani tayari unafanya kazi katika bodi za manunuzi katika wizara mbalimbali, vitengo na mashirika ya umma.“H ata ikiwa ni katika nyanja za kimataifa lazima kuwe na chombo kinachochunguza usawa katika mikataba hasa katika kuhakikisha kuwa asilimia 30 inakuwepo kwa ajili ya wakandarasi wa nyumbani,” alisema. Turamye aliyasema hayo katika kikao kazi cha masuala ya mafuta na gesi kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Mkaguzi wa H esabu za serikali, Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini pamoja na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ ).Suala la asilimia 3 0 lipo katika skimu ya P P DA iliyowekwa mwaka jana kwa lengo la kuwainua wakandarasi wazawa katika manunuzi ya umma. Turamye alisema kutokana na hali hiyo pindi wakandarasi wa kimataifa wanapopewa kandarasi lazima kuwe na nia ya makusudi ya kuwalazimisha kushirikiana na wakandarasi wazawa ama kwa kuwapa sehemu ya mikataba au kuungana nao.
KITAIFA
APRILI 26, 2018. Ni siku ya historia kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa jumla. Hii ni baada ya Rais John Magufuli kuitangaza Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji la Dodoma.“Nimejaribu kuangalia majiji yaliyopo nikaona kuna Jiji la Dar es Salaam, Jiji la Tanga, Jiji la Mbeya, Jiji la Mwanza, na kwa mamlaka niliyonayo kuanzia leo natangaza Dodoma siyo Manispaa tena, bali linakuwa jiji na kuanzia leo tarehe 26 mwezi huu na mwaka huu aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa atakuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,” anasema Rais Magufuli.Siku hiyo hiyo, Rais Magufuli anaahidi kwenda kukutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ili kuzungumza naye kwa ajili ya kupata fedha za kufanya miradi ya maendeleo kwa bajeti ya jiji badala ya kupata fedha za miradi yenye sura ya manispaa. Huo ni mwaka 2018 ulioipandisha hadhi Dodoma na kuifanya kuingia katika urithi wa matukio ya kihistoria Tanzania.Bunge lapitishaSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anakaririwa na HabariLeo akisema: “Bunge litahakikisha linatengeneza Sheria ya Tamko la Dodoma kuwa Makao Makuu ambayo haitakuwa rahisi kukanyagwa kanyagwa na kubadili.”“Haijalishi kama sheria itakuwa na ukurasa mmoja, jambo la msingi kuwe na kipengele kinachotamka Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi kisheria. Suala hili limekuwa kwenye Ilani ya CCM (Chama Cha Mapinduzi) kwa miaka mingi sana, hivyo tunataka kutunga sheria ambayo siyo tu kwamba siyo rahisi kukanyagwa kanyagwa, bali pia ambayo ni vigumu kuibadili.”Huo ndio mwaka 2018 unaoelekea ukingoni. Itakumbukwa kuwa, serikali iliwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018 uliolenga kulifanya Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Tanzania. Kupitia kwa muswada huo kunafanya sasa kuwepo Sheria ya Tamko la Makao Makuu ya Mwaka 2018 ambayo madhumuni yake ni kutangaza Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya Tanzania.Sheria hiyo inatambua Tamko la Aprili 26 mwaka huu la Rais John Magufuli alipotangaza Manispaa ya Dodoma ambayo ni Mji Mkuu wa Tanzania kuwa Jiji la Dodoma. Pia inatambua uamuzi wa mwaka 1973, ambapo Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alitangaza Manispaa ya Dodoma kuwa makao makuu wa chama tawala; CCM na serikali. Kutungwa kwa sheria hiyo kunaifanya azma ya serikali kuhamia Dodoma kutimia na kuwa ndoto ya kweli.Asili ya Dodoma kuwa mji wa SerikaliKumbukumbu zinaonesha kuwa safari ya serikali kuhamia Dodoma ilianza tangu mwaka 1970. Lengo la safari hii lilikuwa kuutumia mji huu ulio katikati ya nchi kuwa kituo cha kuhudumia Watanzania wote au kutoa fursa kwa wananchi kutoka pande zote nchini kupata huduma za kiserikali bila kusafiri umbali mrefu. Mwaka 1973, Serikali inaamua kuanzisha Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na kuundwa Programu ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma, ili kukidhi vigezo muhimu vya kuwa makao makuu ya nchi.Kimsingi, historia ya serikali kuhamia katika mji huyo ni ndefu na inaanza kuonesha matunda yake kamili mwaka 2016, ikiwa ni zaidi ya miaka 40, baada ya Rais John Magufuli kuweka bayana maamuzi na nia ya kutekeleza kwa vitendo azima ya serikali kuhamia Dodoma. Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani katika anatangaza wazi kuwa Serikali itahamia Dodoma ifikapo 2020. Hatua hiyo inaondoa sintofahamu ya muda mrefu pamoja na kuwapo juhudi za serikali za kuwezesha uhamishaji makao makuu kupitia maamuzi mbalimbali ya chama tawala, Baraza la Mawaziri, nyaraka na miongozo ya serikali na matamko ya viongozi wakuu wa kitaifa.Hadi Desemba 8 mwaka huu, takwimu zinaonesha kuwa watumishi 6,531 kati ya watumishi takribani 7,000 wa wizara zote, walikuwa wamehamia Dodoma ikiwa ni sawa na asilimia 87.5 huku kundi la mwisho la watumishi 400 lilitarajia kuhamia kabla ya mwaka huu kuisha. Awamu ya kwanza ya watumishi 1,789 walihamia Dodoma mwaka 2016 wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Kisha, ikafuata awamu ya pili kati ya Novemba, 2017 ambapo watumishi 2,130 walihamia Dodoma wakiongoza na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na tayari awamu ya tatu kati ya Machi na Juni ni watumishi 2,612.Matarajio ni hadi mwisho wa mwaka 2018 zoezi la kuhamishia watumishi Dodoma liwe limekamilika na kuendelea na utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Aidha, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi anabainisha kuwa hakuna mtumishi aliyehamia Dodoma ambaye anaidai serikali fedha za uhamisho.Mji wa SerikaliSerikali inajenga mji wa serikali katika eneo la Mtumba kilomita 7 nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Ujenzi wa Mji wa Serikali unatekelezwa ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kuhakikisha watumishi wa serikali Dodoma ili wafanye kazi katika mazingira mazuri na yenye miundombinu yote itayorahisisha utendaji kazi wa kila siku. Serikali imeshatoa takribani Sh bilioni 1 za awamu wa kwanza kwa ajili ya ujenzi wa ofisi kwa ziara zote na kazi hizo kupewa vyombo vya ulinzi na usalama, jambo ambalo linao. Wizara 21 zimeanza hatua za awali za ujenzi ikiwemo kusafisha maeneo yao, kuweka mipaka, kuchimba misingi, kumwaga zegi na wengine uwekaji wa nondo na matofali ili kuanzia Januari, wizara kadhaa zianze kuhamia katika eneo hilo.Akizungumza katika ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipotembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali katika eneo la Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Maimuna Tarishi anasema hatua ya serikali kuhamisha ofisi zake katika eneo hilo ina tija hasa ukizingatia kuwa tayari asilimia 87.5 ya watumishi wameshahamia Dodoma.Mpango wa utekelezaji wa ujenzi huo kwa awamu ya kwanza umefikia asilimia 82 na unatarajiwa kukamilika Januari 2019 ambapo viongozi na baadhi ya watumishi wanapaswa kuwa wamehamia katika eneo hilo mapema mwakani. Azma ya serikali ni kuhakikisha inajenga majengo bora yenye kuzingatia mahitaji yote muhimu ikiwemo miundombinu ya umeme, maji safi na taka, teknolojia ya habari na mawasiliamo (Tehama), mawasiliano na barabara katika mji wa Serikali Ihumwa.BaloziUjerumani imekuwa nchi ya kwanza kufungua ofisi ndogo mjini Dodoma itakayofanya pia shughuli za kibalozi. Pia Umoja wa Mataifa umeshafungua ofisi yake ya mawasiliano jijini hapa. Rais Magufuli alikabidhi hati miliki za viwanja kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yenye makazi yake hapa nchini kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi jijini Dodoma. Hatimiliki zilizokabidhiwa ni 62 za balozi za nchi mbalimbali na 5 ni za mashirika ya kimataifa. Kila kiwanja kina ukubwa wa ekari 5.Hivyo Serikali kuhamia Dodoma kutoka Jiji la Dar es Salaam ni tukio la kihistoria linalopaswa kuandikwa katika vitabu na kumbukumbu za nchi yetu ikiwa ni wazo lililoanzishwa na Baba wa Taifa (Nyerere) lililoanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2016 Serikali ilipohamia rasmi Dodoma na “limetiwa mhuri mzito’ Aprili 26, mwaka huu Rais Magufuli alipoipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji la Dodoma.
KITAIFA
Chanzo cha picha, Getty Images Nyota wa Uingereza Jude Bellingham amekataa uwezekano wa kuhamia Chelsea au Paris St-Germain, kulingana na ripoti za Express. Kiungo huyo wa kati wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuhama msimu wa joto, huku Liverpool, Manchester City na Manchester United zote zikihusishwa naye, pamoja na wababe wa La Liga Barcelona na Real Madrid. Thamani ya Bellingham ilipanda wakati wa Kombe la Dunia, huku mchezaji mwenzake wa Uingereza Phil Foden akisema "atakuwa kiungo bora zaidi duniani" kufuatia kutumika kwake katika ushindi wa 3-0 wa Three Lions dhidi ya Senegal katika hatua ya 16 bora. Chanzo cha picha, Getty Images Manchester United wamehusishwa na mshambuliaji wa Barcelona Ansu Fati wiki hii lakini rais wa klabu hiyo ya Catalan Joan Laporta amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania hauzwi kwa sasa. "Hatufikirii kuhusu kuondoka kwake. Siwezi kutabiri siku zijazo lakini tuna matumaini makubwa kwake," Laporta aliambia mkutano wa wanahabari siku ya Alhamisi. Chanzo cha picha, Getty Images Bruno Fernandes kuhusu kurejea kwa mabao ya Jadon Sancho katika safu ya Manchester United : "Ni muhimu kwa kila mtu kwa sababu tunataka wachezaji wengi iwezekanavyo kwa ajili ya timu. "Jadon anarejea, anapata dakika zake, na amepata lengo lake. "Tunatumai itakuwa msaada mkubwa kwake na kwa timu kwa msimu mzima kwa sababu tunahitaji kila mtu katika ubora wake. Chanzo cha picha, Getty Images Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes aliulizwa kama ana wasiwasi kuhusu uwezekano wa Leeds kupata meneja mpya, iwapo watapata mbadala wa Jesse Marsch kabla ya mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu katika Elland Road. "Hapana, sina wasiwasi kabisa," alisema. "Pamoja na timu hii, na tabia tuliyo nayo katika timu hii, shauku, hamu, umoja tulionao, hatuogopi kwenda popote kucheza dhidi ya mpinzani yeyote. Chanzo cha picha, Getty Images Julien Lopetegui anasisitiza kuwa anataka kuwa bosi wa Wolves kwa "muda mrefu" huku akifurahia "changamoto ya kusisimua" ya kuwaweka kwenye Ligi ya Premia. Lopetegui amesimamia ufufuo katika klabu ya Molineux tangu aanze kuinoa mwezi Novemba na klabu inayoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza. Ushindi wa 3-0 wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Liverpool uliwapandisha hadi nafasi ya 15.
MICHEZO
RAIS John Magufuli amekabidhi zaidi ya hati 1,000 kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, baada ya kufanyiwa urasimishaji kwenye maeneo yao ambapo hati hizo zitawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha na kujikomboa kiuchumi.Hati hizo zimekabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi, Dk Angeline Mabula kwa niaba ya Rais Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Mtaa wa Mecco katika Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela na katika mtaa wa Nyangulugulu katika Kata ya Mahina katika Halmashauri ya jiji la Mwanza.Akikabidhi hati hizo kwa wananchi hao, Dk Mabula alisema rais amesikia vilio vya muda mrefu vya wananchi hao juu ya changamoto za ardhi zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kuporwa viwanja vyao.Aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati zenye umri wa miaka 99, kutosahau kulipa kodi ya serikali, ambayo ndiyo inaiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo miradi mikubwa ya kitaifa.Alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinapima maeneo yote ambayo hayapo kwenye mpango wa urasimishaji, kuwapatia wananchi leseni ya makazi itakayotozwa Sh 5,000 katika kipindi cha mpito cha miaka mitano na baadaye makazi yao yataingizwa kwenye mfumo rasmi wa urasimishaji makazi na kuwapatia hati za umiliki wa maeneo yao.Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hosiana Kusiga alisema urasimishaji katika jiji la Mwanza umefanyika na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, ambapo jumla ya viwanja 19,635 vimepimwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuondokana na ujenzi kwenye makazi holela katika halmashauri hiyo.Amesema halmashauri yake ilikuwa na lengo la kupima jumla ya viwanja 24,000 kupitia mradi huo wa urasimishaji makazi, ambapo viwanja 25,766 ikiwa ni sawa na asilimia 107.3 vimepimwa katika kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, Kishiri na Nyegezi.Kusiga aliongeza kuwa kazi ya upimaji wa viwanja bado inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Kishiri na Luchelele, ambapo jumla ya viwanja 19,635 upimaji wake umekamilika ikiwa ni sawa na asilimia 80.
KITAIFA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Jennifer Omollo amesema, Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Pwani ni fursa kwa halmashauri hiyo kwa kuwa viwanda kwenye eneo hilo vinahitaji soko la bidhaa.Amesema ofisini kwake mjini Kibaha kuwa, pia wajasiriamali wadogo wanahangaika kupata soko la bidhaa zao hivyo wakikutana na wenzao wenye viwanda vikubwa wanaweza kuuza wanachozalisha.Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.Maonesho hayo ya pili ya viwanda mkoani Pwani yatafanyika kuanzia Oktoba Mosi hadi saba kwenye viwanja vyaa CCM Sabasaba Picha ya Ndege, na Kongamano litafanyika Oktoba tatu.“Kwa hiyo kongamano hilo kwa mji wa Kibaha ni fursa kubwa kwa sababu wananchi pia wataona ni jinsi gani Serikali inawekeza katika eneo la viwanda lakini pia wataona maendeleo ambayo Halmashauri ya Kibaha na Mkoa wa Pwani imepiga katika masuala mazima ya viwanda” amesema Omollo.Amesema, Halmashauri hiyo ina miradi kadhaa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na kujenga soko kubwa katikati ya mji lenye uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 4,000.“Tunawaalika, ni vizuri watu wakaja wakapata maeneo katika lile soko ili weweze wakafanya biashara…lakini pia Halmashauri inajenga machinjio ya kisasa kwa mpango wa miradi mkakati” amesema na kuongeza kuwa fedha za miradi hiyo zimetoka Serikali kuu.
UCHUMI
WASHINGTON, MAREKANI MTOTO mkubwa wa kiume wa Rais wa Marekani Donald Trump, amekiri kuonana na mwanasheria mmoja mwenye ukaribu na Ikulu ya Urusi, Kremlin. Donald Trump Junior alikiri kuonana na mwanasheria huyo, Natalia Veselnitskaya muda mfupi baada ya baba yake kuidhinishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican. Kwa kufanya hivyo, alikuwa na matumaini ya kupata taarifa zinazoweza kumsaidia baba yake katika kampeni za uchaguzi. Likiwanukuu washauri wa Ikulu ya Marekani, gazeti la New York Times liliripoti kwamba mtoto huyo alikubali kukutana na Veselnitskaya baada ya kuahidiwa taarifa dhidi ya aliyekuwa mgombea wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton. Mkutano huo uliofanyika Juni mwaka jana kwenye jengo la Trump Tower, ulihudhuriwa pia na shemeji yake Jared Kushner na Paul Manafort aliyekuwa wakati huo mwenyekiti wa kampeni ya Rais Trump. Msemaji wa kundi la wanasheria wa Trump, Mark Corallo amesema ‘Rais hakuwa na taarifa kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea na wala hakuhudhuria mkutano huo.’ Tuhuma hizo zinajiri wakati Trump akiendelea kuchunguzwa kuwa alishinda uchaguzi wa urais wa Marekani dhidi ya Clinton kwa msaada wa Urusi, kitu ambacho anaendelea kukikana.
KIMATAIFA
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Alexander Kyaruzi amesema bodi hiyo itatoa ushirikiano wa asilimia 100 kwa shirika hilo katika kutekeleza miradi ya kimkakati ya umeme ambayo itachangia kufikia Tanzania ya viwanda na hatimaye kufanya biashara ya umeme.Dk Kyaruzi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kutembelea miradi ya kimkakati wa kujenga njia kuu ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 na upanuzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Zuzu.Alisema kwa sasa kazi inayofanyika ni kutekeleza miradi ya kuongeza uzalishaji wa umeme, kuboresha na kujenga njia kuu za kusafirisha umeme na miradi ya kusambaza umeme.Bodi alisema inaisaidia Tanesco kutekeleza vipaumbele vya taifa vya kuhakikisha nchi inakuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda ambao unatengemea uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha.Kuhusu kusambaza umeme, Dk Kyaruzi alisema kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita yamefanyika marekebisho ya usambazaji umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro na kuwa juhudi hizo zimeelekezwa katika mikoa mingine ili kupunguza wasiwasi wa umeme kukatika katika.Kuhusu maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Zuzu, Dk Kyaruzi alionesha kufurahishwa na hatua iliyofikia na kuwa kukamilika kwake kutasaidia Jiji la Dodoma kuwa na umeme wa uhakika.Naye Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kilovolti 400 kwa ajili ya kuunganisha mfumo wa Gridi ya Taifa na zile za Kenya kwa upande wa Kaskazini na Zambia kwa upande wa Kusini, Peter Kigadye alisema hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo ni kujenga vituo vinne vya kupoozea umeme wa kilovolti 400.Alisema vituo hivyo ni Dodoma, Singida, Sinyanga na Iringa ambavyo vitagharimu dola za
UCHUMI
Na TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM KUMEKUWAPO na dhana kwamba baadhi ya shule binafsi zinafanya udanganyifu katika matokeo ya mitihani ya Taifa. Dhana hii inatokana na ukweli kwamba wamiliki wa shule hizi ni wafanyabiashara hivyo hulazimika kuzitangaza shule zao kwa kuonesha zinafanya vizuri katika mitihani ya Taifa. Baadhi ya shule zimekuwa zikifanya udanganyifu huu kutokana na ukweli kwamba hawakuwa na maandalizi ya kutosha sambamba na kutokuwa na mitihani ya kujipima kabla ya mtihani ya kuhitimu. Interschool examination ni mradi ulioandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia masuala ya elimu ya Teacher’s Junction ambayo iliandaa mitihani kwa shule binafsi za mikoa ya Arusha na Dar es Salaam. Ofisa Mradi wa Interschool exam, Njama Salum anasema huo ni mradi shirikishi uliobuniwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule binafsi. Anasema shule nyingi binafsi zimejikita katika ushindani huku wakitupilia mbali ubora wa taaluma wanazotoa. “Baadhi zimefikia hata kufanya udanganyifu katika mitihani ya Taifa ili waonekane wanafundisha zaidi bila kujali taaluma wanazowapa wanafunzi. Anasema kwa kuliona hilo wao wameamua kubuni mradi wa kuwapima wanafunzi wa shule za msingi binafsi kabla ya mitihani ya Taifa. Njama anasema walimu wa shule husika hutunga mitihani kwa masomo yote kwa darasa la saba na nne kisha kuikabidhi kwao ili kuiboresha. “Tunapoipokea mitihani hii, tunaichuja na kuandaa mtihani wa pamoja ambao hufanywa na shule zote kwa siku moja, ambapo hufanywa kwa usimamizi mkubwa. “Hii inawasaidia wanafunzi kujipima na kuwajengea hali ya kujiamini katika ufanyaji wa mitihani, pia kuwaondoa hofu,” anasema Njama. Anasema faida za mitihani hii ni pamoja na kuwasaidia walimu kutambua upungufu unayopatikana katika ufundishaji wao. “Inawasaidia walimu kujua uwezo wa uelewa wa wanafunzi walionao ili waweze kuangalia mbinu mpya za kufundisha,” anasema. Anasema baada ya mitihani huandaa ripoti ya mitihani na kuzipeleka katika shule zilizoshiriki. “Timu ya Interschool exam wakiongozana na shule zilizofanya vizuri huzitembelea shule ambazo hazijafanya vizuri na kuwapa ushauri,” anasema Njama. Kwa upande wake Mkuu wa shule mstaafu, Athman Ahmed anasema mitihani hiyo itawajengea wanafunzi kujiamini zaidi katika kufanya mitihani na hivyo kuinua taaluma nchini. “Nitoe rai kwa wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu na wamiliki wa shule katika kukuza taaluma ya watoto wetu,” anasema Ahmed. Anasema hizi ni juhudi binafsi zilizoanzishwa mahususi kuinua elimu hivyo ni vema kuziunga mkono. “Niwapongeze walioanzisha wazo hili kwa kuwa ni juhudi za dhati kuinua taaluma inayotolewa na shule binafsi,” anasema Ahmed. Mwanafunzi wa darasa la nne aliyefanya vizuri na kutunukiwa, Hanspoppe Jeremia kutoka shule ya msingi Sakana, anasema juhudi binafsi zimemsaidia kufika hapo alipo. “Huwa najisomea usiku ninapokuwa nyumbani, hii hunisaidia kukumbuka ninapokuwa katika mitihani,” anasema Hanspoppe. Naye mshindi wa jumla kwa darasa la saba kutoka katika shule ya Green Acre, Nakiye Mwinuka anasema amefurahishwa na mashindano ya mitihani hiyo kwani itamsaidia kujiimarisha kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba. “Ninafuraha kushinda katika mitihani hii, naamini itaniongezea hali ya kujiamini katika mitihani ya mwisho,” anasema Nakiye. Anawaomba wanafunzi wenzake kujituma na kutumia muda wao vizuri ili waweze kufikia malengo wanayoyataka. Mkuu wa shule ya msingi ya Sakana ambayo alitokea mshindi wa jumla kwa darasa la nne, Johansen Rwebugisa anasema amefarijika kutoa mwanafunzi bora kwa mikoa miwili. “Lengo la walioanzisha Interschool ni zuri kwa kuwa tunaweza kuinua kiwango cha elimu kwa kuongeza ushindani kwa shule zetu,” anasema. Akizumgumzia maisha ya shule ya mwanafunzi aliyefanya vizuri, Hanspoppe Jeremia anasema ni kijana anayejituma. “Hanspoppe ni kijana anayejituma na anapenda kutunza muda na mwanafunzi mwenye nidhamu ya hali ya juu,” anasema Rwebugisa. Naye Gracian Mbelwa ambaye ni mmiliki wa shule ya Mothers’ of Mercy anasema amefurahishwa na tukio hilo ambalo litawawezesha kutambua uwezo wa wanafunzi walionao. “Tukiendelea na utaratibu huu tunaweza kuinua kiwano cha elimu kwa shule zetu kwani kwa sasa ushindani utaongezeka,” anasema Mbelwa. Anatoa wito kwa shule nyingi kuingia katika mitihani hiyo ili kuongeza ushindani kwa wanafunzi. Katika mitihani hiyo jumla ya shule 13 zilishiriki na kupata washindi wa kila shule na washndi wa jumla. Shule hizo Dar es Salaam ni Sakana, mothers of Mercy, Green Acre Mabibo, Green Acre Mbezi, Bright View,Emmy na Grace. Kwa Arusha shule zilizofanya mitihani hiyo ni Tumaini,Upendo friends, Kilimanjaro, Dominion, Mecson na Marian.
AFYA
SHULE zote za msingi nchini Uganda, Januari mwakani zitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili na baadae kufanya mitihani kwa lugha hiyo.Hatua hiyo imeelezwa ni mkakati wa nchi hiyo, kutaka kujitanua katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuona nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo na nje ya jumuiya zimeitangaza lugha hiyo kuwa rasmi na kuwekwa kwenye mitaala. Mbali na hatua hiyo, Uganda pia imeanzisha Baraza la Kiswahili, huku kikianza kusambaa kwa kasi mashuleni.Nchi nyingine za Afrika Mashariki ambazo zinakitambua Kiswahili kama lugha rasmi ya taifa ni Tanzania, Kenya na Rwanda, huku Burundi na Sudan Kusini zikiingiza lugha hiyo adhimu katika mitaala yake ya shule. Wizara ya Elimu Uganda imesema nchi hiyo imejiandaa kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili shuleni, baada ya kufanyika majaribio na kwamba itaanza kufundishwa kuanzia darasa la nne mpaka la saba.Kamishna Msaidizi wa Elimu ya Msingi Uganda, Dk Tony Mukasa alisema hayo wakati wa mkutano wa maofisa tawala uliofanyika juzi nchini humo.Alisema tayari wameshambaza vitabu vya Kiswahili shuleni, huku walimu wakiwa wamepata mafunzo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.“Lengo ni kukukifanya Kiswahili kuwa lugha ya pili ya taifa kutokana na kuwa inatumika kwa kiasi kikubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema.Dk Mukasa alisema alitahadharisha kuwa shule ambazo hazitatekeleza sera hiyo, zitapata shida miaka mitatu ijayo, kwani wizara inatarajia kuwa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi utakaoandikwa kwa Kiswahili.“Katika siku za baadaye tunatarajia kukifanya Kiswahili lugha itakayofanyiwa mtihani na kusimamiwa na Bodi ya Taifa ya Mitihani Uganda katika elimu ya msingi,” alisema.Miaka ya hivi karibuni, serikali Uganda iliaidi kuanza kutekeleza utoaji mafunzo ya lugha hiyo shuleni, lakini ilichukua muda kutokana na kutokuwa na sera maalum ya maendeleo ya lugha hiyo.Mwakilishi wa Chama cha Walimu Uganda na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kisugu iliyopo Kampala, James Jjuko, alisema hajui mipango hiyo ya serikali na kwamba shuleni kwake wana vitabu vya lugha ya Kiswahili, lakini hawana mwalimu wa kufundisha lugha hiyo. Kauli hiyo iliungwa mkono na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Triple P, Plan Virginia, aliyesema serikali imekuja na sera hiyo bila mpangilio hivyo inaweza kusababisha migogoro.Septemba mwaka huu serikali ilipitisha kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Kiswahili Uganda, ikiwa ni maandalizi ya a kutangazwa kuwa lugha rasmi ya pili ya taifa. Akizungumzia hatua hiyo ya Uganda, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita), Dk Selemani Sewange, alisema ni takwa la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuzitaka nchi wanachama kutambua Kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa. Alisema itifaki ya Kamisheni ya Kiswahili EAC, inasema kila nchi inatakiwa kuwa na Baraza la Kiswahili na baadaye lugha hiyo kupanuliwa kwa kufundishwa shuleni.
KITAIFA
Christian Bwaya PAMOJA na faida zake, maendeleo yanaweza kubadili kwa kiasi kikubwa mfumo wa malezi uliozoeleka. Kwanza kabisa, majukumu ya kijinsia yaliyozoeleka katika jamii yanabadilika. Mama aliyezoeleka kuwa mlezi anapoingia kwenye soko la ajira, anaacha nyumbani swali gumu: Nani atabaki na mtoto yeye akiwa kazini? Swali hili ni gumu kwa sababu hata ule utamaduni wa familia tandao nao umeanza kupotea. Shauri ya maendeleo, uwezekano wa ndugu kama shangazi, mama mdogo, wifi, shemeji, binadamu kukaa pamoja unakuwa mdogo na hivyo ule msaada uliozoeleka unakosekana. Matokeo yake inabidi sasa wazazi ambao kwa kawaida wanahitaji kuendelea na shughuli za uzalishaji watafute malezi mbadala. Mojawapo wa mbadala huo ni binti wa kazi maarufu ‘house girls’. House girl, kwa kawaida, ni watoto au vijana wadogo waliokulia katika mazingira ya kawaida, mara nyingi kijijini tena bila elimu kubwa, wanaoajiriwa na wazazi kwa lengo la kuwasaidia kumtazama mtoto wakati wa kazi. Sambamba na malezi, wasichana hawa hufanya kazi za ndani. Walezi hawa hupatikana kwa utaratibu usio rasmi unaotegemea mfumo wa kufahamiana na ndugu, jamaa na marafiki wanaoweza kuwaunganisha wazazi wenye uhitaji na msichana anayetafuta kazi. Hakuna utaratibu rasmi unaowawezesha waajiri wenye uhitaji kuwa na uhakika na historia yake, ujuzi wake pamoja na tabia zake kwa ujumla. Hata hivyo, hutokea wakati mwingine wakapatikana kupitia kwa watu wanaofahamika. Ingawa utaratibu huu wengine huuchukulia kama namna nyingine ya usafirishaji wa binadamu, lakini umekuwa ukiwasaidia wazazi kuwa na uhakika na wapi hasa watoto hawa wanatoka. Mara nyingi, mabinti hawa huajiriwa bila mikataba inayoeleweka na hulipwa kiasi kidogo cha fedha. Hata hivyo, nje na malipo ya fedha taslimu, wazazi wengi huwapa marupurupu kama chakula, matibabu na huduma nyingine za msingi. Ratiba zao za siku hujaa shughuli nyingi zisizolingana na kipato chao. Wengi wao huwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala. Waajiri wao huwa na matumaini makubwa kupindukia. Pamoja na kazi kubwa wanayofanya, yamekuwapo matukio ya wasichana hawa kuonewa na waajiri wao kwa namna mbalimbali. Wapo wanaotendewa kama watumwa wasiostahili heshima kama binadamu wengine. Wengine hunyimwa haki zao za msingi. Katika mazingira haya, wasichana hawa, wakati mwingine hujenga tabia zisizofaa ambazo huzorotesha uhusiano na waajiri wao. Hali ya kutokuelewana kati ya mwajiri na mtoto huyu wa kazi husababisha hasira, uchungu na visasi ambavyo mara nyingi huishia kwa mtoto asiye na hatia. Ikumbukwe kuwa wasichana hawa ambao mara nyingi ni watoto, huwa hawana uzoefu na malezi. Utendaji wa wengi wao hutegemea maelekezo ya kila mara kutoka kwa waajiri wao ambao wakati mwingine ni watu wenye uwezo mdogo kiuchumi lakini wenye matarajio makubwa. Tunaposikia matukio ya akina dada hawa kuwafundisha watoto tabia zisizofaa, kuwaonea watoto na kuwatendea vitendo visivyofaa, tunaumia kwa sababu tunafahamu waathirika wakuu ni watoto wasio na hatia wanaolelewa na wasichana hawa ambao wakati mwingine huyafanya yote wayafanyayo kulipa kisasi kwa waajiri wasiojali haki zao. Katika makala ijayo tutatoa mapendekezo matano ya namna tunavyoweza kupunguza changamoto hizi na hivyo kumsaidia mzazi kuwa na amani anapoendelea na shughuli zake za uzalishaji kazini. Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Twitter: @bwaya, Simu: 0754 870 815
AFYA
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM MWILI wa binadamu hupitia mabadiliko mbalimbali katika ukuaji wake, kipindi hicho huitwa balehe ambapo uhusisha mabadiliko yote ya kimwili – kimawazo na kihisia. Mabadiliko hayo huwapata jinsi zote yaani ya kike na kiume. Ni katika kipindi cha mabadiliko ya mwili ambapo msichana huanza kupata damu ya hedhi. Hatua hiyo muhimu huitwa kupevuka  au kuvunja ungo kama inavyojulikana, ni kipindi maalumu katika maisha ya mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa. Hedhi hutokeaje Zipo ovari mbili (vifuko vya mayai) katika mwili wa mwanamke, moja upande wa kushoto na nyingine kulia ambazo hutengeneza mayai ya uzazi ambayo husafirishwa hadi katika mji wa mimba kupitia mirija ya uzazi. Kila mwezi ovari moja huachia yai, mchakato ambao huitwa kitaalamu ovulation na wakati huo mabadiliko ya homoni huuandaa mji wa mimba (uterus) kutengeneza ukuta mpya uitwao endometrium kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mapokezi ya mimba inayoweza kutungwa. Yai linalofika katika uterus iwapo halitarutubishwa na mbegu ya mwanamume, ukuta huo humeguka na kutoka nje ya mji wa mimba kupitia ukeni ukiwa pamoja na damu. Zamani wanawake wengi wamekuwa wakitumia vipande vya khanga kujihifadhi wakati wa hedhi. Lakini kukua kwa teknolojia kukasababisha kutengenezwa taulo za kisasa za kutumia na kutupa ambazo huuzwa kwa bei tofauti tofauti madukani. Ni changamoto kwa wasichana Nchini Tanzania suala la hedhi salama kwa wasichana hasa waliopo shuleni linatajwa kuwa bado ni kitendawili na changamoto kwa walio wengi hususan vijijini. Hali hiyo inasababishwa na hofu ambayo huwakumba wakiwa katika kipindi hicho ya kuchafua sare za shule, kuchekwa na kutaniwa na wanafunzi wenzao hasa wa kiume walio chini kiumri. Tafiti mbalimbali ikiwamo ya Haki Elimu ya mwaka 2013, unasema kutohudhuria kwao masomo huchangia kuzorotesha kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi husika. Abuni taulo za kufua Hali hiyo ndiyo iliyomchochea mjasiriamali Jenipher Shigoli, kufanya utafiti akiwa na nia ya kuja na mbinu itakayowasaidia wasichana kutohofia na kuhudhuria masomo yao pasipo kujali kipindi cha hedhi. “Kitaaluma ni mwanasheria pia ni mwanadiplomasia lakini napenda mno ujasiriamali, nimekuwa nikijihusisha na utengenezaji wa bidhaa za usafi tangu mwaka 2013. Kupitia biashara hiyo nimeweza kupata tenda za kusafisha vyoo vya shule mbalimbali nchini kupitia kampeni ya choo salama inayoendeshwa na kampuni ya Malikia ambayo mimi ndio mkurugenzi wake,” anasema. Anasema kupitia kampeni yake hiyo ameweza kufika katika shule nyingi za Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Iringa. “Nikiwa katika shughuli hizo za kampeni ya choo salama, ndipo nikagundua kwamba wasichana wengi hasa kwa shule za kule vijijini hushindwa kuhudhuria masomo wakiwa katika kipindi cha hedhi kwa hofu ya kuchafuka na kuchekwa,” anasema. Kilichomsukuma kubuni taulo hizo Shigoli anasema alipata nafasi ya kuwahoji baadhi ya wanafunzi ambao walimueleza kuwa ili kujihifadhi hutumia manyoya ya kuku, udongo, magunzi ya mahindi, ugali au soksi. “Wapo ambao walinieleza huwa wanatumia vitambaa vya khanga au vitenge lakini wataalamu wa afya wanasema si salama kwa afya kwani rangi inayotumika kutengeneza bidhaa hizo kwa kawaida huchuja zinapokuwa zimelowa majimaji. “Walimu nao walinieleza kuwa baadhi ya wanafunzi huacha masomo na kuamua kukaa nyumbani kwa sababu ya hedhi, kwani hata wale wanaovaa vitambaa huwa hawajiamini, hali ambayo huwaathiri kisaikolojia,” anasema na kuongeza: “Kwa kuwa wengi wanashindwa kumudu gharama za kununua taulo za kutumia na kutupa nilipata wazo la kutengeneza taulo za kutumia zaidi ya mara moja,” anasema. Alivyofanikisha wazo lake Anasema baada ya kupata wazo hilo aliwashirikisha watu mbalimbali wakiwamo wataalamu wa maabara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shirika la  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambao walimsaidia. “Walinishauri na tulichukua muda wa miezi sita kukamilisha bidhaa hizo,” anasema. Malighafi ni pamba halisi Shigoli anasema taulo hizo zimetengezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kwa kutumia pamba halisi, kitambaa na nailoni maalumu ambayo huweza kupokea damu ya hedhi hadi kiwango cha mililita 30 hadi 40. “Uwezo huo unalingana na ule wa taulo zingine zinazouzwa huko madukani na huweza kuvaliwa kati ya saa sita hadi saba. Baada ya saa hizo unalazimika kuifua na kuianika ikauke vizuri kwa ajili ya kuitumia tena na hudumu hadi mwaka mmoja,” anasema. Atunukiwa tuzo Anasema kupitia bidhaa yake hiyo aliweza kuibuka mshindi katika shindano la kusaka wabunifu barani Afrika mwaka jana linalosimamiwa na taasisi ya ‘African Entrepreneur Award’. “Niliibuka mshindi wa kwanza na nilizawadiwa Dola za Marekani 150,000 sawa na Sh milioni 300 za Kitanzania,” anasema. Serikali yampa eneo la kiwanda, mtaji Jenipher anasema anaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kwa kumpatia mtaji wa Sh milioni 30 ili kukuza biashara yake. “Kupitia wizara hiyo, nimepewa eneo la kutosha kujenga kiwanda huko Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizi tunatarajia kukizindua ifikapo Machi, mwaka huu,” anasema. Anasema tayari pia ameshapeleka barua Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwamba anatarajia kupata ushirikiano wa kutosha katika kuisaidia jamii. Jenipher anawasihi Watanzania hasa wanawake kutokuwa na wasiwasi juu ya taulo hizo alizobuni. “Nimepitia taratibu zote kisheria, zimepimwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zimeonekana zina ubora, nimeenda pia Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) nimepewa ‘certificate’ na kama nilivyoeleza awali kuna wataalamu ambao nashirikiana nao kutoka UDSM na SIDO,” anasema. Simulizi ya Monica Monica Elius (si jina lake halisi) anasema ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu aanze kutumia taulo hizo za kufua na kwamba amebaini tofauti kubwa ikilinganishwa na zile za kutumia na kutupa. “Sikujua kama kuna mbunifu Mtanzania ambaye ameanza kuzitengeneza pia taulo za aina hii nchini, maana nilianza kuzitumia muda mrefu sasa umepita na nilikuwa najua kwamba zinatoka nje na kuletwa kama msaada. “Nina dada yangu ambaye mume wake alikuwa akifanya kazi katika kambi ya wakimbizi iliyopo Ngara mkoani Kigoma, wanawake na wasichana waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo walikuwa wakigawiwa na mashirika ya misaada,” anasema. Alianzaje kuzitumia “Awali nilikuwa natumia taulo za kawaida zinazouzwa madukani, lakini kila nilipotumia nilikuwa napata muwasho mkali mno, hali yangu ilikuwa mbaya,” anasema. Anasema alikuwa analazimika kwenda hospitalini kupima na kupewa matibabu kila mara ingawa haikugundulika tatizo lilikuwa nini hadi anapatwa na hali ya namna hiyo. “Nakumbuka kuna wakati nilikuwa mkoani Morogoro nilitokewa na hali hiyo nikaenda katika zahanati moja na kumuelezea daktari niliyemkuta, alinipima na kugundua kuwa nina mzio na hizi taulo za kawaida. “Hivyo, alinishauri ninunue khanga mpya nikate vipande vya kunitosha au ninunue gozi (kitambaa maalumu ambacho hutumika kufunga vidonda) pamoja na pamba ili nijitengenezee taulo zangu mwenyewe,” anasema. Gozi ni gharama kubwa Anasema; “… nilishindwa kumudu hilo kwani nilikuwa natumia fedha nyingi kununua gozi ambalo huuzwa kati ya Sh 25,000 hadi 30,000 na pamba ni kati ya Sh 25,000 hadi 30,000 kwa hiyo nilihitaji Sh 60,000 ili niweze kupata bidhaa hizo na kutengeneza taulo za kutumia miezi mitatu hadi minne, ni gharama kubwa mno. Anasema siku moja akiwa na dada yake huyo alimshangaa kuona anahangaika kutengeneza vitambaa vya kujihifadhi jambo ambalo lilimlazimu kumsimulia sababu za kufanya hivyo. “Alinishangaa, ikabidi nimsimulie ndipo akaniambia atanipatia hizo taulo za kufua, sikuamini kama zipo hadi siku aliponiletea,” anasema. Anasema taulo hizo huuzwa kati ya Sh 5,000 hadi 8,000 na kwamba tangu ameanza kuzitumia ameondokana na ile adha ya kupatwa muwasho katika sehemu zake za siri. “Unaona kama hii niliyobeba (akimuonesha mwandishi wa makala haya) ina mwaka sasa lakini bado naitumia, haijachoka kama unavyoiona,” anasema. Uzoefu wake Monica anasema taulo hizo zimetengezwa na malighafi ya pamba pekee na kitambaa maalumu hali ambayo inaifanya kuwa laini na murua wakati wote anapokuwa ameivaa. “Yaani ni laini kiasi kwamba unajisikia raha ukiwa umeivaa hakuna michubuko wala huwezi kujihisi harufu mbaya unapokuwa umeitumia, hata ukipata muwasho si kama ule unaotokea ukiwa umevaa taulo zile za kutumia na kutupa,” anasema. Zinafuliwaje? Anasema suala la usafi wa taulo hiyo ni wa muhimu kuuzingatia ili mtumiaji asipate matatizo mbalimbali ya kiafya kama vile muwasho na hata harufu mbaya. “Huwa nafulia sabuni ya unga, naona ndiyo inafaa zaidi kuliko zingine. Hii unapaswa kuifua na kuisuuza vizuri kwa maji mengi, ukisuuza na maji kidogo ikikauka unaikuta ina alama za mistari zimekatisha katikati. “Alama hizo hufanya muonekano wake kuwa wa kuudhi, uzuri ni kwamba unapoifua na kuianika kukiwa na jua kali haichukui zaidi ya saa mbili unaikuta tayari imekauka na unaweza kuivaa tena,” anasema. Anaongeza kuwa ukiwa safarini na ukawa umetumia taulo hii ni tofauti na zile za kutupa, ukijisafisha hubaki na harufu, unahifadhi vizuri taulo yako na kwenda kuifua nyumbani pindi unapofika,” anasema. Anasema taulo hizo zinasaidia kupunguza gharama kwani mtu anaponunua huweza kukaa nazo hadi mwaka mzima. Daktari Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kinamama na Uzazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Belinda Balandya anasema kipindi cha hedhi ni muhimu kwa afya ya mwanamke. “Mwanamke anapokuwa katika siku zake hulazimika kutumia taulo hizo ambazo kazi yake kuu ni kupokea ile damu inayotoka, kama hatavaa maana yake ni kwamba itapitiliza kuchagua nguo zake. “Taulo za kutumia na kutupa jinsi zilivyotengenezwa zina ‘layer’ maalumu kwa ndani ambayo hufyonza damu ya hedhi, hulazimu kubadili mara nyingi (kiasi cha kila baada ya saa nne) hasa inapokuwa inatoka kwa wingi,” anasema. Athari Daktari huyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) anasema kuna athari kubwa iwapo mwanamke hatazingatia usafi akiwa hedhi. “Kwa kuwa inanyonya damu maana yake ni kwamba hufika wakati unakuwa kama vile umevaa kitu kibichi, hivyo ngozi huanza kupata michubuko. Kwa wale ambao ngozi yao ni ngumu kidogo huwa si rahisi kuona michubuko hiyo lakini wanapojisafisha kwa maji na sabuni huhisi maumivu,” anasema. Anaongeza kuwa damu ni sehemu ambayo bakteria huota kwa urahisi kwa sababu wanakuwa wanapata chakula wanachohitaji kwa urahisi, mtu anaweza kuendelea kuvaa kwa sababu hajui jambo hili lakini ni hatari. Kuhusu taulo za kufua “Sijaziona, sijawahi kuzisikia, wewe ni wa kwanza kunieleza, lakini zamani mabibi na wazazi wetu walikuwa wakitumia vitambaa… sijui hizo zipoje. “Kumbuka kwamba nimesema bakteria huzaliana kwa urahisi kwenye damu, sasa kama itafuliwa, isikauke na kubaki na unyevunyevu maana yake ni kwamba bakteria waliozaliwa watabaki na kuendelea kukua hivyo muhusika atakuwa amejiweka kwenye hatari ya kupata tatizo,” anasema. Akizungumzia taulo za tampons zilizo tengenezwa mfano wa unene wa  kidole na imewekwa kamba kidogo, anasema ni mbaya zaidi. Anasema kuwa wanawake huzitumia kwa kuingiza ndani ya uke ili kufyonza damu na huitoa kwa kuvuta kamba hiyo inayokuwa imebaki nje ya uke. “Hizi ni taulo mbaya, wengine wanapoweka wakati wa hedhi chache hujisahau kuzitoa na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata madhara,” anasema. Anasema bakteria hao huenda kutengeneza kovu katika mirija ya uzazi mwishowe huziba kabisa na kwamba huweza kupenya na kuingia hadi katika mfumo wa damu na kuleta athari zaidi. Kauli ya TBS Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Egid Mubofu anasema ni kweli shirika hilo lilipokea maombi ya kupima taulo hizo za Elea. Anasema bidhaa hiyo bado haijaruhusiwa kuingizwa sokoni. “TBS tulipokea maombi kutoka kampuni ya Malkia ambao ni wazalishaji wa bidhaa za Elea. Upimaji wa awali wa bidhaa hiyo ulifanyika na matokeo yalionesha kuwa bidhaa hiyo haikidhi kiwango cha bidhaa husika ambacho ni TZS 1659:2014, hivyo mzalishaji akatakiwa  kufanyia marekebisho bidhaa hiyo,” anasema. Mubofu anasema mpaka sasa mzalishaji wa bidhaa hiyo hajafanyia marekebisho bidhaa hiyo, hivyoTBS bado haijathibitisha ubora wa bidhaa hiyo. “Bidhaa za pedi ziko katika orodha ya bidhaa za lazima, hii ni kutokana na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza endapo bidhaa hizo hazitakidhi matakwa ya kiwango husika. Hivyo basi, bidhaa za aina hii hazipaswi kuingizwa sokoni mpaka hapo ubora wake utakapothibishwa,” anasisitiza. Kauli ya wizara Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni EATV hivi karibuni, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema serikali inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kuna uwezekano wa kupata taulo za hedhi (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.
KITAIFA
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Barcelona, Samuel Eto’o, anaamini nyota mpya wa Real Madrid, Eden Hazard atakuja kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d’Or akiwa na kikosi hicho. Hazard amejiunga na Real Madrid wakati huu wa majira ya joto akitokea Chelsea kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 150, baada ya kuitumikia Chelsea kwa miaka saba. Hivyo Eto’o amedai mchezaji huyo ataacha historia nchini Hispania kutokana na uwezo wake. ‘Hazard atakuja kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or akiwa na Real Madrid, mwanzo hakuwa na thamani kubwa, lakini sasa thamani yake itakuwa kubwa sana kwa kuwa yupo katika moja ya timu kubwa hivyo macho ya wengi yatakuwa kwake kutokana na ujio wake,” alisema Eto’o. Hata hivyo Eto’o aliongeza kwa kumfananisha mchezaji huyo na nyota wa Barcelona na timu ya Argentina, Lionel Messi. Hazard na Messi sasa watakutana mara kwa mara kwenye Ligi ya nchini Hispania tofauti na ilivyo awali akiwa na Chelsea. “Hazard akiendelea kufanya vizuri ataweza kuwa kama Messi, ana nafasi kubwa ya kutengeneza jina zaidi katika timu hiyo ya Real Madrid,” aliongeza Eto’o. Eto’o alicheza jumla ya michezo 199 ndani ya Barcelona tangu mwaka 2004 hadi 2009, huku akiwa pamoja na Messi kwenye kikosi hicho. Hata hivyo aliwahi kucheza alicheza jumla ya michezo saba akiwa Madrid tangu mwaka 1997 hadi 2000. Maandalizi ya msimu mpya wa ligi, Real Madrid hawajaanza vizuri katika michezo yao ya kirafiki, huku mwishoni mwa wiki iliopita wakikubali kichapo cha mabao 7-3 dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid. Hata hivyo walipokea kichapo kingine kutoka kwa mabingwa wa nchini Ujerumani, Bayern Munich, lakini waliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Arsenal kwa mikwaju ya penalti. Kiwango hicho kilichooneshwa na Madrid kimewashangaza wengi hasa kutokana na kiasi kikubwa cha fedha walichokitumia kwa ajili ya kuongeza wachezaji wakati huu wa kiangazi.
MICHEZO
NEW YORK, Marekani NYOTA wa mbio za magari, Lewis Hamilton, amepigwa marufuku na mchumba wake, Nicole Scherzinger, kuendelea kuwasiliana na mwanamitindo na mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani, Rihanna. Kauli ya mwanadada huyo kumpiga ‘stop’ mpenzi wake huyo kunatokana na tetesi kwamba nyota huyo wa mbio za magari ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Rihanna. “Nimemwambia Hamilton akate mawasiliano na Rihanna na kama hataki akate mawasiliano na mimi ili wawe na uhuru. “Nimempa muda wa kukata mawasiliano na Rihanna, ikishindikana nitajua cha kufanya, sitaki kugombana na mtu ila nataka wawe waelewa,” alisema Nicole. Rihanna baada ya kuachana na mkali wa RnB, Chris Brown, amekuwa akitajwa kutoka na wanaume mbalimbali akiwemo mchezaji wa timu ya Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid, Karim Benzema na wengine wengi.
BURUDANI
NAIBU Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa amesema sehemu kubwa ya maisha ya utendaji wa kazi yake hautakuwa wa ofi sini badala yake, atahamia mashambani kwa wakulima.Nia ni kubaini changamoto zinazowakabili wakulima na kuzitafutia ufumbuzi ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.Alitoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa sekta ya pamba uliofanyika jijini hapa na kuhudhuriwa na wakuu wa mikoa, wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wanunuzi wa pamba na wakulima wa pamba.Mkutano huo uliokuwa na lengo la kujadili changamoto zinazomkabili mkulima na kutafuta mikakati ya kisayansi ili kulifanya zao la pamba kuleta tija kwa mkulima na kuinua uchumi wa nchi.Halikadhalika, Bashungwa aliwataka watendaji walio chini ya wizara yake kuhakikisha wanayashughulikia na kuyatafutia majawabu matatizo yanayowakabili wakulima nchini.“Mimi niwahakikishie katika kipindi changu sitakaa ofisini nitawafuata wakulima mashambani, tunao asilimia 65 ya Watanzania wanategemea kilimo, hivyo hatuwezi kufanya mzaha na kilimo wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Tano,” alisema.Katika kuhakikisha changamoto mahususi za wakulima kwenye maeneo yao zinatatuliwa, Bashungwa aliwataka wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi watendaji kuhakikisha kuwa wanatenga bajeti kwenye maeneo yao ili kuanza kushughulikia changamoto hizo badala ya kutegemea fedha kutoka serikali kuu.Akitoa mfano, alisema wizara ilifanya uchambuzi wa fedha zilizoombwa kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kujenga na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji ikagundua kuwa kiasi cha Sh trilioni 7 kinahitaji kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa nchi nzima.
KITAIFA
NA CHRISTOPHER MSEKENA BAADA ya kusambaa kwa picha za mwanamitindo Calisah Abdulhameed, akiwa amevaa viatu vya kike (High Heels), modo huyo amefunguka kuwa licha ya kitendo hicho kupokewa na jamii kwa mitazamo tofauti malengo ya kutangaza bidhaa hiyo yametimia. Akizungumza na MTANZANIA, Calisah alisema kwa mara ya kwanza alipopigiwa simu na jamaa anayeitwa Frank Knows anayewavalisha viatu mastaa wa kike kama, Jokate Mwegelo na Hamisa Mobetto ili afanye tangazo hilo alisita lakini baadaye alikubali baada ya kulipwa dau kubwa alilolitaka. “Frank Knows tayari amewavisha kina Jokate na Hamisa Mobetto lakini alikuwa hafahamiki sana ila nilipovivaa mimi vile viatu watu wengi wamemfahamu na kiukweli mpango  wa biashara yake umefanikiwa, nimepokea matusi mengi lakini ukweli ile ni kazi tu na mimi ni mwanamume kamili, nisihisiwe vibaya,” alisema Calisah. Modo huyo ambaye alijizolea umaarufu mwaka jana baada ya kutoka kimapenzi na Wema Sepetu aliongeza kuwa mashabiki wa mitindo wataelewa zaidi  baada ya tangazo la video kuanza kuonekana kupitia runinga zote.
BURUDANI
Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam HOSPITALI ya Regency ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Hospitali ya HCG Multi Specialty Ahmedabad ya India imeanza upasuaji wa magoti na nyonga nchini ili kuwasaidia Watanzania wasilazimike kwenda nje ya nchi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency, Dk. Rajni Kanabar, kuanza kwa upasuaji huo ni hatua nzuri itakayosaidia Watanzania wengi waliokuwa wakienda kutibiwa nje kutibiwa nchini. “Hadi sasa tumeshawafanyia upasuaji wagonjwa wanane ambao wamesharuhusiwa wakiwa hawana shida yoyote ile, haya ni mafanikio makubwa kwa hospitali binafsi kuanza kufanya upasuaji wa aina hii unaohitaji utaalamu wa hali ya juu,” alisema Dk. Kanabar. Pia alisema upasuaji huo umekuwa ukifanywa kwa ushirikiano baina ya madaktari bingwa, Dk. Deepak Dave na Dk. Yuvraj Lakum, wakisaidiwa na wahudumu wa afya wa Regency. Dk. Kanabar alisema upasuaji huo hufanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu kiasi kwamba mgonjwa anakaa muda mfupi hospitali na kuruhusiwa kwenda nyumbani tofauti na ilivyokuwa zamani. “Tunachukua wagonjwa wote kutoka kwenye kampuni zinazotumia bima na watu binafsi na kampuni kubwa na upasuaji kama huu utakuwa unafanywa kila baada ya wiki sita hapa Regency. Hii ni fursa ya kipekee kwa Watanznaia kufanyiwa upasuaji wa aina hii hapa hapa Tanzania badala ya kwenda nje,” alisema. Alisema uchunguzi wa wagonjwa wenye matatizo ya nyonga na magoti utafanyika kuanzia Oktoba 1-3, mwaka huu na upasuaji utafanywa kwa watakaochaguliwa na kuonekana wanahitaji huduma hiyo.
KITAIFA
Ngoma amejiunga na Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na tayari ameonesha uwezo mkubwa kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kuisaidia timu yake kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao.Mshambuliaji huyo aliyeifungia Yanga mabao 13 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, alisema sababu ya kutoa kauli hiyo ni kutokana na kiwango chake kuwa juu na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake waliopo kwenye kikosi cha kocha Mholanzi Hans Pluijm.“Ni michuano migumu hasa hatua tuliyopo hivi sasa, lakini Yanga ni timu kubwa, wachezaji lazima tuoneshe vipaji vyetu ili kuipa mafanikio timu hii na hatimaye tuweze kufikia hatua ya makundi au hata tucheze fainali mwaka huu,” alisema Ngoma.Mzimbabwe huyo alisema amejipanga kuhakikisha Yanga ya msimu huu inavunja rekodi kwa kuwatoa mabingwa wa zamani wa Afrika, Al Ahly kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo ya Afrika.Alisema anajua hiyo ni timu kubwa Afrika, lakini haoni sababu ya kuwahofia kwa sababu hata wao wana timu nzuri ambayo kama watacheza kwa kujituma wanaweza kuwatupa nje ya michuano hiyo na kujiwekea rekodi ya kuwatoa mabingwa hao wa zamani.“Nimesikia kuwa mara nyingi Yanga imekuwa ikitolewa kwenye michuano ya kimataifa na timu za kiarabu, nataka mwaka huu iwe tofauti kwa kufanya maajabu ya kuwatoa Al Ahly, kwa sababu tuna timu nzuri ambayo inaweza kufanya vizuri kama tutacheza kwa ushirikiano,” alisema Ngoma.Mshambuliaji huyo amelitaka benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzake kujiwekea mikakati maalumu kwa ajili ya mchezo huo ili waweze kufanya vizuri na kufanikisha kile ambacho wamekikusudia.
MICHEZO
TOKYO, JAPAN KIONGOZI wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis amewasili Japan anakotarajiwa kutoa risala kali ya amani dhidi ya nyuklia katika nchi pekee iliyowahi kuhujumiwa kwa mabomu ya atomiki. Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 82 anatekeleza dhamiri ya muda mrefu ya kuhubiri nchini Japan ambako miaka kadhaa iliyopita alitarajia angekuwa mmisionari. Amewasili Tokyo na mvua kali na upepo, huku kofia yake nyeupe ikipeperushwa alipokuwa anateremka ngazi za ndege ya shirika la ndege la Thailand, akitokea Thailand. Ziara yake ya siku nne itaanzia Nagasaki na Hiroshima, miji inayofungamanishwa daima na mabomu ya nyuklia yaliyodondoshwa mwishoni mwa vita vikuu vya pili vya dunia na kuangamiza maisha ya watu wasiopungua 74,000 Nagasaki na 140,000 Hiroshima.  Katika miji yote hiyo miwili Papa Francis atazungumza na wahanga wa mashambulio ya mabomu ya atomiki.  Papa Francis atahutubia mbele ya kumbusho la amani mjini Hiroshima-ushahidi wa shambulio la bomu la nyuklia lililodondoshwa  Agosti 6 mwaka 1945. Katika ujumbe wake kwa wananchi wa Japan kupitia kanda ya video kabla hajaondoka Vatican, Papa Francis alikosoa vikali “matumizi mabaya ya silaha za nyuklia.” “Pamoja nanyi, naomba Mungu silaha za maangamizi za nyuklia hazitotumika tena katika historia ya binadamu” alisema kiongozi huyo wa waumini bilioni 1.3. Papa Francis amewasili Tokyo akitokea Thailand ambako alihubiri uvumilivu wa kidini na amani.  Anatarajiwa kutoa nasaha kama hiyo nchini Japan yenye waumini 440,000 tu wa kikatoliki kutoka jumla ya wakazi milioni 126. Jumatatu Papa Francis atakutana na wahanga wa majanga ya kimaumbile, “matetemeko ya ardhi,Tsunami na kuvuja mionzi ya nyuklia mwaka 2011” tukio lililoathiri sehemu kubwa ya kaskazini mashariki mwa Japan. Amepangiwa pia kukutana na mfalme mpya Naruhito na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe pamoja na kuhutubia katika uwanja wa michezo mjini Tokyo.
KIMATAIFA
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amesema kuanzia sasa Mkuu wa Idara ya Ardhi atakayekutwa amekaa na hati ya ardhi kwa muda mrefu bila kuipeleka ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda kukamilisha taratibu za utolewaji hati hiyo, basi ataondolewa katika nafasi yake.Dk Mabula alisema hayo juzi alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.Kauli yake inatokana na kukuta baadhi ya hati katika halmashauri hiyo zikiwa kwenye masijala ya ardhi tangu mwaka 2017 bila kupelekwa ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.Alisema baadhi ya halmashauri alizozitembelea wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi, amebaini wakuu wengi wa idara ya ardhi wakiwa na hati ofisini kwa muda mrefu bila kufanya jitihada zozote za kuhakikisha hati hizo zinaenda ofisi ya kamishna kukamilishwa na hati kutolewa.Kwa mujibu wake, ucheleweshaji utoaji hati miliki za viwanja na mashamba siyo tu unawakera wananchi, bali unaikosesha serikali mapato ya kodi ya ardhi kwa kuwa wananchi wanakuwa hawajamilikishwa ardhi kisheria.Naibu Waziri ametoa onyo kali kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa kukaa na hati kwa zaidi ya miaka miwili kwenye ofisi yake bila kuwasilisha hati hizo ofisi ya Kamishna Msaidizi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa na hatimaye kukabidhiwa kwa wahusika kwa haraka na wakati.Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wa miji ya Kyaka na Mtukula wilayani humo kuchangamkia kazi ya urasimishaji makazi holela ambayo imeonekana kusuasua katika miji hiyo.Akizungumza na wakazi wa Kyaka na Mtukula kwa nyakati tofauti, Dk Mabula alisema haridhishwi kabisa na namna kasi ya urasimishaji inavyoendelea katika miji hiyo ambapo takwimu zinaonesha wananchi waliojitokeza kwenye kazi hiyo ni ndogo ukilinganisha na wakazi wa miji hiyo.
KITAIFA
LONDON, ENGLAND BAADA ya klabu ya Arsenal kutolewa katika michuano ya Kombe la FA juzi dhidi ya Watford, mashabiki wa klabu hiyo ya jijini London wamemjia juu kocha, Arsene Wenger na kumtaka aondoke. Arsenal walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo, lakini wameshindwa kulitetea na kukubali kichapo hicho cha mabao 2-1 na kuwafanya mashabiki kumtaka Wenger afungashe virago vyake. Mashabiki hao wamemshambulia kocha huyo kupitia mitandao ya kijamii, lakini amewataka kuwa wavumilivu na kuiunga mkono timu yao hasa katika michezo ijayo. “Arsenal imepoteza michezo mingi na imetolewa kwenye michuano ya Kombe la FA, mashabiki wanatakiwa kuvumilia na kuangalia michezo ijayo ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. “Hii ni timu yao wanatakiwa kukubaliana na chochote kinachotokea sio siku zote tutakuwa na furaha, kuna wakati mambo yanakuwa magumu lakini tunatakiwa kuwa pamoja katika kila mchezo, najua inauma sana hasa unapopoteza mchezo ukiwa nyumbani ila ndivyo soka lilivyo,” alisema Wenger. Wenger anaamini nguvu zake anazielekeza katika michuano ya Ligi Kuu nchini England na Ligi ya Mabingwa, ambapo kesho klabu hiyo itashuka dimbani kupambana na mabingwa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp, huku mchezo wa awali Arsenal wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha mabao 2-0.
MICHEZO
  MARTIN  MAZUGWA NA MITANDAO, HATIMAYE bondia Manny Pacquiao ameomba pambano dhidi  ya bingwa wa ngumi mchanganyiko, Connor  McGregor, ambaye anakuja juu na kuwa tishio. Emmanuel Dapidran Pacquiao, bondia mkazi wa Manila, Ufilipino, mwenye  majina mengi kama vile Pac Man, The Destroyer, Manni Pakyyao, The Mexicutioner, Mp na mengine mengi,  lakini wengi  hupenda kumuita Manny  Pacquiao, ni kati ya mabondia bora zaidi hivi sasa duniani kutokana na rekodi zake. Bondia huyo, ambaye amecheza jumla ya mapambano 67, huku akiwa amepoteza mara sita na kushinda mapambano 38 kwa KO, si wa kubezwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kurusha makonde, huku mkali huyo akiwa ni bondia mwenye spidi zaidi ya kurusha ngumi. Pac Man (38), mwenye urefu wa futi tano pamoja na uzito wa kilo 144, amekuwa nje ya ulingo tangu Novemba 5, mwaka jana, aliposhinda pambano lake dhidi ya Jesse Vargas, lililofanyika jijini Las Vegas, nchini Marekani. Mkali huyo amechoshwa na tambo za Mc Gregor, raia wa Ireland, ambaye amekuwa akijisifu kuwa yeye ni bora na hakuna bingwa yeyote anayeweza kumdondosha ulingoni hivi sasa kutokana ubora wake. Tambo hizo zimekuwa zikiwafanya wakali hao wa mchezo wa masumbwi kumtaka ulingoni mapema mbabe huyo na kumaliza utata baina yao. Kuonyesha kuwa amedhamiria juu ya jambo hilo, tayari promota wake, Bob Arum, ameongea na waandishi wa habari kuthibitisha taarifa hizo, akisema kuwa, anafahamu kuwa mkali huyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya bingwa asiyepigika, Floyd Mayweather, ambaye wamekuwa wakitupiana vijembe mara kwa mara katika mitandao ya kijamii, lakini pia mteja wake anatamani kupanda ulingoni dhidi yake. Arum anasema kuwa, Pacquiao hatakuwa na pambano jingine mara baada ya kupanda ulingoni dhidi ya bondia anayefanya vizuri hivi sasa raia wa Australia, Jeff Horn, litakalopigwa katika Ukumbi wa Suncorp Stadium Julai 2, hivyo utakuwa wakati sahihi kwa yeye kupanda ulingoni dhidi ya mbabe huyo wa ngumi mchanganyiko. Promota huyo alisema hayo akihojiwa na kituo cha TMZ kuwa McGregor anapaswa kupanda ulingoni na Pacquiao kama pambano lake dhidi ya bingwa asiyepigika litashindikana. "Pacquiao anatarajia kuwa na pambano gumu mbele ya bingwa huyo wa Australia, lakini si kigezo cha kushindwa kupanda ulingoni dhidi ya Mc Gregor. "Mara baada ya pambano la Julai litakalofanyika hapa United States, iwapo kama McGregor bado atakuwa akisubiri kupata mpinzani katika mchezo wa masumbwi, Manny Pacquiao atakuwapo kwa ajili yake," alisema Arum. "Kwa upande wa McGregor, tayari tumemalizana kila kitu kimekwenda sawa, hivi sasa naanza mazungumzo na kambi ya Mayweather, ambayo pia ina hati miliki yake," alisema bosi wa UFC, Dana White, alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha TNT. McGregor, bingwa asiyeisha vituko, tayari amethibitisha kusaini mkataba wa kucheza mchezo wa masumbwi na kuweka rekodi ya aina yake katika mchezo wa ngumi mchanganyiko. "Ni jambo la heshima kusaini na kuweka rekodi ya aina hii, hakika ni furaha kubwa kufanya hivi nikiwa karibu na mshauri wangu, Zuffa LLC,” alisema McGregor. Iwapo mipango itakwenda kama ilivyopangwa, huenda pambano hilo likapigwa Septemba 16, mwaka huu, ikiwa ni tarehe iliyopendekezwa na upande wa Pac Man ambao ndio walioomba pambano hilo.
MICHEZO
NEW YORK, MAREKANI BAADA ya penzi la Wiz Khalifa na Amber Rose kuyumba, kwa sasa wawili hao wameonekana kulidumisha penzi hilo kwa kufanya mitoko mbalimbali ya wazi. Tangu warudi kwenye uhusiano miezi miwili iliyopita, kwa sasa wamekuwa wakiwa pamoja mitaani na mtoto wao kwa ajili ya kulitangaza penzi lao jipya. “Ni furaha kubwa kuona familia ikiweza kulea mtoto, sikukuu hii tumeweza kutoka na mtoto wetu kwa ajili ya kuonesha upendo, tunaweza kuwa familia ya mfano bora,” aliandika Amber Rose. Wawili hao walirudiana baada ya Wiz kuachia wimbo wake wa ‘See You Again’ ambapo Amber Rose alikuwa anashindwa kuzuia hisia zake kila anapousikia wimbo huo.
BURUDANI
Chanzo cha picha, Getty Images Baada ya kukosekana kwa miaka 11, Koffi Olomide alitarajiwa kutumbuiza katika ukumbi wa Paris La Defense Arena, mojawapo ya kumbi kuu za burudani barani Ulaya, akirejea Ufaransa. Msanii huyo maarufu nchini Congo na Afrika, ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa, ni miongoni mwa Waafrika ambao wameuza albamu nyingi zaidi barani Ulaya na anaendelea kuwavutia wengi kwenye kumbi za burudani. Lakini katika siku za hivi karibuni amerejea kwenye vyombo vya habari kwa makala nzito. Kesi ya "le Grand Mopao" wanenguaji wa kike wanne wa zamani wa dansi. Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 65 alihukumiwa kifungo cha miaka minane jela na Mahakama ya Rufaa ya Versailles mjini Paris mnamo Jumatatu, Oktoba 25. Anashtakiwa kwa kuwadhulumu kingono na kuwabaka wanenguaji wanne wa kike waliokuwa wakicheza dansi wakati walipofanya naye kazi kwenye tamasha nchini Ufaransa. Hukumu ya kwanza ya mashtaka, iliyopewa jina la "hatari," sasa inataka hukumu nzito zaidi kwa "mtu mwenye nguvu" maarufu duniani kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu mashtaka dhidi yake. Mnamo 2009, Koffi alikimbilia DR Congo lakini aliahidi kujitetea dhidi ya madai hayo. Mnamo 2012, Antoine Agbepa Mumba, ambaye jina lake halisi lilihojiwa kuhusu ubakaji wa wacheza dansi wanne, hakufungwa lakini baadaye mahakama ya eneo hilo ilimhukumu kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la "kumnyanyasa kingono mtoto wa miaka 15". Mwimbaji huyo aliamriwa kulipa faini ya euro 5,000 na riba kwa mmoja wa wacheza dansi wake. Mahakama ya Nanterre pia ilikuwa imemuamuru kulipa faini sawa na hiyo kwa kuwasaidia wanawake watatu kuingia Ufaransa kinyume cha sheria. Wizara ya Utawala, ambayo ilikuwa imeomba afungwe kwa miaka saba, ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Koffi Olomide ambaye mara kadhaa amekuwa akisema hadharani kuwa ananyanyaswa, anaendelea kukanusha tuhuma za ubakaji. Mnamo mwaka wa 2019, aliiambia TV5 Monde: "Mradi nikumbuke kuwa nimekosea na ninatumai kuwa siku moja wanawake hawa watakuja na kusema kwamba wamedanganya kuhusu madai hayo." Mashtaka dhidi yake yanawezekana kuwa yalifanyika wakati wa matamasha nchini Ufaransa kati ya mwaka 2002 na 2006. Wanawake hao wanamshutumu kwa kuwapa hifadhi katika nyumba iliyo karibu na Paris na kuwalazimisha kufanya naye mapenzi, ili baadhi yao waweze kudumu kukaa hapo. Mbele ya majaji, Koffi alikanusha mashtaka hayo waziwazi, akidai kuwa wanawake hao "walisafiri kwenda na kutoka Champs-Élysées", na wakati mwingine "walidai wasindikizwe". Waendesha mashtaka wanasema walisindikizwa kwa nguvu. Koffi alithibitisha kuwa ana "haki ya kuwasimamia" walipoondoka, ili kuhakikisha kuwa hawatoroki Ufaransa kutokana na kazi waliyokuwa nayo. Kwake, madai hayo yametungwa na wanawake hao wanne wanaotafuta namna ya kuendelea kuishi Ufaransa. Kuhusu jinsi wanawake waliotoroka kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na kwenda kuandamana, mwimbaji huyo alijibu, "Hiyo ni sinema tu ... muda wao wa kurudi Kongo kulikuwa karibu, walijua kabisa kwamba wanarudi Kongo." Kwa hivyo walitaka kukaa Ufaransa "kwa gharama yoyote," alisema. Wanawake hao wanasema hawajaweza kurejea Kongo kwa kuhofia kulipizwa kisasi. Chanzo cha picha, Getty Images Koffi Olomide pia alikanusha madai ya ubakaji. Wanawake hao wanasema wakati fulani aliwaalika hotelini, wakati mwingine katika studio ya muziki, na kuwalazimisha kufanya naye mapenzi. Koffi alisema, "hapana, sijawahi kuwa peke yangu na hawa wasichana, unawezaje kufanya mapenzi studio? Siwezi kuwafikia! "Hakuna ushahidi wa kuunga mkono madai yaliyotolewa na washtaki hawa." Mahakama ilisema itatangaza uamuzi wake mnamo Desemba 13. Unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto wa miaka 15. Chini ya sheria ya makosa ya jinai , nchini Ufaransa, ni kosa kwa "kitendo cha mtu mzima, kutumia au kufanya ngono na mtoto wa miaka 15, bila ubakaji wowote au nguvu yeyote." Mfungwa huyo anahukumiwa kifungo cha miaka saba jela na faini ya Euro 100,000 . Kwa mujibu wa sheria, "umri wa miaka 15" inamaanisha ni mtoto aliye chini ya miaka 15. Chanzo cha picha, Getty Images Koffi ana kesi nyingine zinazomkabili nchini Ufaransa , mwaka 2012 alifungwa gerezani kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kushtakiwa kumpiga na kumuumiza mtayarishaji wa muziki. Kufuatia shutuma za mtengeneza filamu Harvey Weinstein, kuhusu shutuma za ubakaji ambazo zilitikisa ulimwengu. Tangu kampeni ya #MeToo ilipomalizika, kumekuwa na kampeni nyingine ambazo ziliwataka wanawake kupinga unyanyasaji wa kingono na kuwashtaki wahusika. Kuanzia mtayarishaji filamu Bill Cosby mpaka msanii R. Kelly wengi wametulia na wameharibu ajira zao. Lakini madai mengine bado hayajapata suluhu, kwa kukosa ushahidi wa kutosha. Kwa upande wake, Koffi Olomide, kwa upande mwingine, alielezea kuwa ni uzushi, mara nyingi kurudia , "Sijawahi kumpiga mtu au kumbaka mtu au kubaka watu." Kesi yake ambayo itasikilizwa Desemba 13, inaweza kuathiri kazi yake ya muziki, mwanamuziki huyo mwenye miaka 65- ambaye anakabiliwa na kesi kadhaa nchini Ufaransa. Chanzo cha picha, Koffi Mwaka 2018, Zambia alishtakiwa kwa kumuacha mpiga picha wake Mwaka 2016, alikamatwa Nairobi na kurudishwa kwao baada ya kumpiga mnenguaji wake wake wakati anawasili Kenya. Video ilisambaa mtandaoni , na kuwakasirisha wengi wakitaka kazi yake isitumike. Mwaka 2012, DRC mtayarishaji wa muziki alimfunga kwa kipindi cha miezi mitatu gerezani. Mwaka 2008, alishutumiwa kwa kumpiga mpiga picha wa kituo cha televisheni RTGA kilichopo DR Congo na kuharibu kamera yake lakini lakini baadae walipatana nje ya kesi. Koffi alitarajiwa kuwa na tamasha tarehe 13/02/2021 mjini Paris huko La Defense Arena na kupelekwa mpaka tarehe 27/11/2021, "kwasababu ya janga la corona haswa kutokana na marufuku ya kimataifa," kwa mujibu wa waandaaji , wametangaza.
BURUDANI
Upendo Mosha, Kilimanjaro Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi, umewasili Kilimanjaro tayari kwa mazishi yatakayofanyika kesho Alhamisi Mei 9, kijijini  kwake Nkuu Sinde, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Mwili wa Mengi uliwasili leo Jumatano Mei 8, saa 3:30 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokewa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro. Mughwira amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo jirani. Mbali na kiongozi huyo pia Spika wa Bunge, Job Ndugai, wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, mabalozi pamoja na viongozi wa dini wanatarajiwa kushiriki katika mazishi hayo. “Hadi sasa nimepata taarifa kwamba Rais atatuma Mwakilishi ambaye ni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa atashiriki katika mazishi japo sijapata uthibitisho… pia Spika wa bunge letu atakuwepo pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali na dini,” amesema.
KITAIFA
KATIKA kuhakikisha inakamata fursa za kibiashara ndani na nchi jirani upande wa Kusini, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeelekeza nguvu katika mradi wa upanuzi wa bandari ya Mtwara wenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 137.Tayari mradi huo unaokwenda sambamba na maboresho mengine, umeshafikia asilimia 25 ukihusisha ujenzi wa gati mpya, ujenzi wa gati kubwa, uchimbaji wa sehemu ya kugeuzia meli na ununuzi wa kitambo ya kisasa kwa ajili ya kuhudumia meli kubwa kwa kiwango cha kimataifa.Mbali ya kuhudumia mikoa ya Kusini, bandari hiyo iliyoanza kurejesha kasi ya kupokea shehena na meli kwa wingi, pia inahudumia nchi za Malawi, Zambia, Msumbiji na sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).Akizungumzia maboresho na mafanikio ya bandari hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, Meneja wa Bandari hiyo, Nelson Mlali, alisema bandari ya Mtwara kwa sasa inafunguka zaidi kuliko kipindi cha nyuma kutokana na maboresho na utafutaji wa masoko.Alisema upanuzi wa bandari hiyo iliyokuwa na gati moja lenye urefu wa meta 385, ulichagizwa na ongezeko la shehena za mizigo inayohudumiwa bandarini hapo hadi kukaribia uwezo wa juu wa bandari hiyo pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali za kiuchumi unaoendelea katika mikoa ya kusini.“Bandari yetu kwa sasa ina uwezo wa kuhudumia tani 400,000 kwa mwaka na kwenye msimu wa korosho uliopita ambao ulikuwa na mavuno mengi uliongeza shehena hadi tani 377, 590, ambayo ukiangalia inakaribia uwezo wetu, hivyo tukaona uhitaji wa upanuzi ili tuendane na jitihada za serikali za kuvutia uwekezaji ambao kwa kiasi kikubwa utahitaji bandari kusafirisha mizigo na malighafi,” alisema Mlali.Aliongeza kusema, wanategemea bandari ya Mtwara miaka kadhaa ijayo itakuwa na mizigo mingi kutokana na uwekezaji unaotarajiwa kufanyika katika mikoa ya kusini ikiwemo uzalishaji wa mpunga Kilwa, uzalishaji wa korosho, uchimbaji wa madini aina ya graphite na kilimo cha mihogo kwa ajili ya utengenezaji wa wanga ambapo zaidi ya hekta 3,000 zimetengwa.Makaa ya mawe yanatarajiwa pia kusafirishwa kwa wingi kwenda nje kupitia bandari hiyo inayogeuzwa kuwa ya kisasa zaidi, maboresho yanayokwenda sambamba na bandari nyingine zilizo chini ya usimamizi wa TPA, zikiwemo za Tanga na Dar ea Salaam.Alisema maboresho hayo yataiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa za kimataifa zenye urefu wa hadi mita 211 kutokana na kuwa na gati imara itakayoweza kuhudumia tani 65,000 kwa wakati mmoja. Aliongeza kuwa upanuzi huo wa bandari utaipa uwezo wa kuhudumia hadi tani milioni moja kwa mwaka ambayo ni karibu mara nne ya uwezo wa sasa.Akizungumzia mafanikio yaliyotokana na mabadiliko ya uendeshaji katika miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano, Mlali alisema Bandari ya Mtwara imeongeza kasi ya ukuaji katika kuhudumia shehena za mizingo na kufikia asilimia 16 kwa mwaka kutoka asilimia 13 kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Akizunguzia ulinzi na usalama bandarini hapo, Mlali alisema katika bandari hiyo kuna ulinzi imara wa mizigo ya wateja, usalama wa eneo hilo pamoja na ulinzi wa miundombinu ya bandari.
KITAIFA
Mwandishi wetu -Dar es salaam MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Usalama wa Taifa (TISS), Apson Mwang’onda (75), amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Akithibitisha kutokea kwa msiba huo, mtoto mkubwa wa marehemu, Thomas Mwang’onda, alisema baba yao alipatwa na mauti jana majira ya saa 5 asubuhi. “Ni kweli mzee ametutoka na inaumiza kupoteza mzazi, ilikuwa kwenye saa tano asubuhi wakati wadogo zangu wanamsindikiza mama kwenda Airport wakapigiwa simu kuwa warudi haraka hospitali. Na walipofika walikuta tayari mzee amefariki. “Kwa sasa msiba upo nyumbani Mbezi Beach, ila kesho ndio tutajua utaratibu wa namna ya kuuleta mwili wa mzee hapa nyumbani kwa taratibu za mazishi,” alisema. Thomas ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, alisema kuwa wakati wa uhai wake, baba yao aliwahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini. “Mwenyewe baba huwa nakaa naye ambapo hupata nafasi ya kunihadithia maeneo kadhaa ambayo alifanya kazi. Nakumbuka aliniambia kuwa aliwahi kufanya kazi Shirika la Mafuta la wakati huo la TP, pia alikuwa JKT katika kambi ya Kaboya mkoani Kagera na baada ya hapo alikuwa mkuu wa kambi ya JKT Mgulani ambako hapo ndipo jicho la Serikali lilimuona zaidi na kumpa kazi nyingine hadi anastaafu,” alisema. Septemba 5, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli alimjulia hali Mwang’onda, ambaye alikuwa akipatiwa matibabu hospitali Dar es Salaam. Hata hivyo hali ya mzee Apson ilibadilika na familia kwa kushirikiana na Serikali iliamua apatiwe matibabu nchini Afrika Kusini kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. ALIPOKUTANA NA MAGUFULI Desemba 6, 2018 Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Apson, Ikulu Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo hayo Apson alimshukuru Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kumuona. Pia alipongeza uongozi wa Rais Magufuli kwa kuchochea kasi ya maendeleo, hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Apson aliitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wa uzalishaji wa umeme wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji, ujenzi wa madaraja na barabara ambazo licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. “Mabadiliko ni makubwa sana ambayo yametokea, kuna miradi mikubwa mingi inafanyika sasa hivi, kwa hiyo mabadiliko ni makubwa kusema kweli na yote hayo ni kwa manufaa ya nchi. Kwa hiyo ninachoweza kusema amefanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi,” hiyo ndiyo iliyokuwa kauli ya Apson hadharani katika mkutano wake na Rais Magufuli Alistaafu Agosti 21, mwaka 2006 kwa mujibu wa sheria na nafasi yake aliteuliwa Rashid Othman, ambaye naye alistaafu rasmi Agosti 19, mwaka 2016. Apson ni Mkurugenzi Mkuu wa nne wa Usalama wa Taifa kushika nafasi hiyo kwa muda mrefu akiwa amekaa kwa miaka kumi (1995-2005). Hadi sasa anayeshikilia rekodi ya kukaa katika nafasi hiyo muda mrefu zaidi ni Emilio Mzena aliyetumikia miaka 15   kutoka mwaka 1961 hadi 1975. Wa pili ni Luteni Jenerali Imrani Kombe aliyekaa miaka 12 kutoka mwaka 1983 hadi 1995 na wa tatu ni Othman Rashid aliyekaa miaka 11 kutoka mwaka 2005 hadi 2016. WALIOWAHI KUONGOZA USALAMA Kwa miaka kadhaa idara hiyo iliongozwa na vigogo waliobobea katika masuala la ulinzi na usalama, wakiwamo Mzena, Lawrance Gama na Hans Kitine ambaye alipoondoka nafasi hiyo ilikamatwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga. Mbali na hao, nafasi hiyo ilishikiliwa pia na Kombe, Mwang’onda na Othman.
KITAIFA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kitaifa katika kukusanya mapato katika mwaka wa fedha 2017/18.Amesema, Halmashauri hiyo imekusanya mapato kwa asilimia 218.Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati anatoa taarifa ya makusanya ya mapato kwenye Halmashauri katika mwaka wa fedha 2017/2018.Jafo amesema, Geita imefuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani iliyokusanya kwa 165%.Kwa mujibu Waziri Jafo, Halmashauri ya Mpingwe mkoani Katavi imeshika nafasi ya tatu kwa kukusanya kwa asilimia 162.Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe amesema, viongozi wa Halmashauri zilizopata makusanyo makubwa zaidi kwenye mwaka wa fedha 2017/2018 watabanwa waeleze ilikuwaje wakapata mapato hayo.Iyombe amesema, haiwezekani Halmashauri hizo zipate mapato hayo kama kulikuwa na mipango mizuri.Kwa mujibu wa kiongozi huyo, huenda pia baadhi ya Halmashauri zilijiwekea malengo madogo ili zionekane zimekusanya mapato makubwa.Waziri Jafo amesema, kiwango cha ukusanyaji mapato katika mwaka wa fedha 2018/2019 kitakuwa kigezo kikuu cha kupima utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri.
KITAIFA
WAANDISHI wa habari barani Afrika, wamehimizwa kuandika kwa usahihi habari zinazohusu bara hilo ili kuweka kumbukumbu na marejeo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Akitoa mhadhara jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Rais wa Taasisi ya Waandishi wa Habari Tanzania (TAJOA), Simon Mkina amesema waandishi wengi nje ya Bara la Afrika, mara nyingi wamekuwa wakiandika kwa kupotosha habari zinazohusu maendeleo, watu, mazingira na masuala mengine ya bara hilo.Katika mhadhara huo, unaohudhuriwa na waandishi wabobezi wa habari za uchunguzi Afrika, Mkina amesema wakati umefika kwa waandishi kuunganisha nguvu ili kuwa na sauti ya pamoja kujenga taswira sahihi ya Afrika.“Nguvu ninayohimiza hapa ni kuandika mazuri kuitetea kwa wale wanaopotosha habari zake na kuandika mabaya yanayofanywa na baadhi ya Waafrika kulingana na nafasi na dhamana walizonazo katika jamii,” amesema Mkina katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.Mkina amesema nguvu ya pamoja kuandika kuhusu Afrika, haina maana ya kuficha maovu na mabaya, ila ni kuyaweka kwa usahihi na si kuyakuza wala kupotosha, na kuyafanya matukio hayo kuwa jumuishi kwa kila nchi.Amesema habari nyingi zinazoandikwa na vyombo vya habari nje ya Afrika, zinajumuisha kila tukio la baadhi ya nchi ya Afrika kuwa la bara zima.“Kuna matukio kwa baadhi ya nchi za Afrika kuwa na viongozi wanaopenda kung’ang’ania madaraka, kukumbatia rushwa, kuonea raia, kuminya demokrasia na kudhibiti vyombo vya habari, sasa wenzetu nje ya bara hili wakiandika, wanapotosha kana kwamba matukio ya namna hiyo yapo kwa kila nchi ya Afrika, jambo ambalo siyo sahihi,”amesema.Mkina alitumia mhadhara huo wa siku tatu, kukumbusha umuhimu wa vyombo vya habari kwa maendeleo ya Afrika na watu wake.Alisema kwamba bila vyombo vya habari makini na vyenye uzalendo kwa bara hilo, historia iliyondikwa wakati wa ukoloni kuhusu bara hilo itaendelea kujirudia.
KITAIFA
TUHUMA nne zimemtia hatiani Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (pichani), ambapo yeye amesema ‘Maji yamenifi - ka shingoni’.Tuhuma hizo ni zilizotajwa kwenye ripoti, iliyowasilishwa jana na kusomwa na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana, inayotaka kumng’oa madarakani meya huyo. Mwita ni Diwani wa Kata ya Vijibweni wilaya ya Kigamboni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ripoti hiyo imemtia hatiani kutokana na kukabiliwa na tuhuma nne, ambazo ni kutotumia Sh bilioni 5.8 za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).Fedha hizo ni asilimia 51 ya hisa zilizotolewa na Kampuni ya Simon Group, kama sehemu ya ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za UDA. Tuhuma nyingine ni kutumia vibaya gari ya ofisi, ambalo alipata nalo ajali, kushindwa kuongoza kikao cha Baraza la Madiwani na kusababisha Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kugombana na Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo na kudaiwa kuwapendelea baadhi ya mameya kuingia kwenye kamati za fedha.Akisoma ripoti hiyo, Liana alisema kamati imemkuta na hatia meya huyo wa Dar es Salaam, kwa makosa yote anayotuhumiwa nayo. Mkutano huo maalumu, uliokuwa na ajenda ya kupokea Taarifa ya Timu Iliyochunguza Tuhuma dhidi Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama Paul Makonda, ulifanyika katika Ukumbi wa Karimjee jana.Kikao hicho kiliketi na kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya huyo, kwa mtindo wa kusimama. Kikao hicho kikiongozwa na Naibu Meya, Abdallah Mtinika na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Liana. Meya huyo alipinga mchakato mzima wa kura, ulivyoendeshwa wa kutokuwa na imani naye.Mwita alisema “Kiukweli sasa maji kwangu yapo shingoni, mbele sioni wala nyuma sioni, ila naamini Mwenyezi Mungu atasimama.”Aliongeza kuwa: “Umeya wangu sasa unapimwa, ikiwa imebaki miezi mitatu kabla hatujavunja Baraza la Madiwani. Hivi karibuni nimeanza kupata wakati mgumu kwenye kiti change. Naomba viongozi wa dini waniombee.”Gari layeyuka, amuangukia Rais Magufuli Katika hali asiyoitarajia, Meya huyo wa Jiji la Dar es Salama alipigwa na butwaa baada ya kufika eneo la maegesho, lakini hakulikuta gari aina ya Prado, alilokuwa akilitumia katika shughuli zake za kila siku, ambalo alipewa kutokana na nafasi hiyo.“Nashangaa nimenyang’ nywa gari na bendera imeshushwa. Nawaambia mimi bado ni meya. Namuomba Rais Dk John Magufuli aingilie kati suala hili, kwa sababu wakati naingia madarakani ilikuwa hivi hivi.“Sio gari tu, hata ofisi imefungwa. Sielewi kinachoendelea dhidi ya wadhifa wangu. Nasisitiza mimi bado meya wa jiji hili, kwa mujibu wa Kanuni Ibara ya 82 (2) meya ataondolewa kwa kura mbili ya tatu (theluthi mbili) “alisema Mwita Alisema mahudhurio yalikuwa watu 16, ambapo kati yao 13 ndio walipiga kura za kutokuwa na imani naye.Wawili walipinga suala hilo na mmoja hakupiga kura, hivyo akidi hiyo haikutimia kumuondoa. “Sisi kama Watanzania tumeapa kulinda Katiba yetu, kanuni na miongozo. Tusitie aibu. Mimi ni mmoja tu, sing’ang’anii kuwa meya ila taratibu zifuatwe. Sitaacha kupigania haki yangu. Namuomba Rais Magufuli aingilie hili. Namuomba sana Rais,”alisisitiza Mwita.Makonde yazuka Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga alimtwanga makonde Naibu Meya, Abdallah Mtinika baada ya kusoma matokeo ya Azimio la wajumbe waliopiga kura ya kutokuwa na imani na Mwita. Mtinika aliyekuwa akiongoza kikao hicho, alisema idadi ya waliopiga kura, kwa kusimama kwenye viti vyao ni 16.Assenga alimtwanga makonde hayo ya nguvu Naibu Meya, kwa kile madai ya kuchukizwa na matokeo aliyotangaza ya kutokuwa na imani na Mwita. Makonde hayo yalifanya askari kutumia nguvu na kumkwida mzobe mzobe Assenga mpaka kwenye gari defender ya Polisi, ambapo walimpeleka Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Dar es Salaam. Hali ilikuwa hivi kabla ya Naibu Meya kusoma matokeo.Alianza kwa kusema “Naomba nisome uamuzi wa mwanasheria wetu wa jiji la Dar es Salaam, kuhusu uamuzi wa kutokuwa na imani ya meya.“Kura zilizopigwa ni 16 na mjumbe mmoja ameomba udhuru na wawili hawakupiga kura, uamuzi wenu umepitishwa, baada ya hapo nafunga kikao”.Hata hivyo, Mtinika hakusema kama Mwita ameondolewa katika nafasi, badala yake alisema ni uamuzi wa wajumbe 16 ambao ni wa CCM. Baada ya kutoa uamuzi huo, wajumbe wa Chadema walionekana wakishangilia na kusema: “Hoja yenu imeshindwa, kwisha habari yenu.” Waliendelea kushangilia na kudai kuwa Mwita bado ni meya wa jiji hilo.Hata hivyo, vurugu zilitamalaki katika ukumbi huo, kwa Assenga kuchukuliwa na Polisi. Vurugu ukumbini Awali, kabla ya kupiga kura kuanza, kuliibuka vurugu katika Ukumbi wa Karimjee. Msingi wa vurugu hizo ni baada ya Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kudai kuwa kuna saini feki ya jina la mjumbe, Kassim Mshamu kwenye kikao hicho. Alishika kitabu cha mahudhurio na kunyoosha juu, huku akisema kuna saini feki.“Usinisumbue, usiniguse, acha kunisukuma” Jacob alimwambia askari aliyemfuata kutaka kumshika, wakati akipaza sauti kuwaeleza wajumbe kuhusu saini hiyo feki. Wakati Jacob akipaza sauti, ukumbi ulikuwa unazizima kwa kelele na kutoelewana, huku wajumbe wa Chadema wakionekana kupandwa na hasira.Kesi yake Kisutu Wakati yanatokea hayo ukumbini, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kutoa uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita aliyeomba mahakama hiyo itoe amri ya kusitisha mchakato wa kung’olewa kwenye nafasi hiyo hadi maombi ya msingi yatakaposikilizwa. Wakati askari wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega aliahirisha shauri hilo hadi leo saa 5:00 asubuhi kwa sababu hajamaliza kuandika uamuzi huo.Shauri hilo lilipoitwa upande wa wajibu maombi, waliwakilishwa mahakamani hapo na jopo la mawakili wa serikali, likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Tango huku upande wa mleta maombi, ukiwakilishwa na Wakili Hekima Mwasipo na wenzake wawili.Mwita amewasilisha maombi hayo dhidi ya Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda, Halmashauri ya Jiji hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Wakili Mwasipo aliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura na yanalenga kuwazuia Mkuu wa Mkoa na Halmashauri hiyo, kujihusisha katika mchakato wa kumng’oa kwenye nafasi ya Umeya wa jiji hilo.
KITAIFA
 FARAJA MASINDE– DAR ES SALAAM WAZIRI wa Nishati, Dk. Merdad Kalemani, amesema Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) halina mpango tena wa kutumia mitambo ya IPTL, Aggreko na Symbion katika kuzalisha umeme kwa kuwa ilikuwa ikisababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara ya Sh milioni 439 kwa mwaka. Alisema, walipoondoa mitambo hiyo ya ufuaji umeme shirikahilo lilikuwa likiokoa karibu kila mwezi Sh bilioni 6.9 zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kuendeshea mitambo hiyo kupitia kununua mafuta mazito. Dk. Kalemani aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akiainisha mafanikio ya Wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ya Uongozi wa Rais Dk. John Magufuli. Alisema, awali Tanesco ilikuwa inanunua umeme kwa bei ya juu hatua ambayo ilikuwa ikichochea gharama za umeme kuongezeka kwa watumiaji, jambo ambalo serikali imelipiga marufuku. “Hivyo, tumeondoa pia mitambo mikubwa ya IPTL uliokuwa na megawati 103, mtambo wa Aggreko uliokuwa na megawati 48 na Symbioni megawati 129 ambapo kwa kufanya hivyo tumeokoa fedha Sh bilioni 138, haya ni mafanikio makubwa ya utendazaji wa njia za kusambaza umeme. “Kutokana na huduma hizo kupatikana hapa nchini, ikiwamo kuimarika kwa miundombinu na ukarabati uliofanyika, kupitia upya matumizi ya Shirika, tulibaini kuwa lilikuwa likipata hasara ya Sh milioni 439 kwa mwaka, hivyo kwasasa halina hasara kutokana na juhudi ziliofanyika.  “Hasara hizo zilikuwa zinatokana na kutumia mafuta mazito ya kuendeshea umeme wa IPTL wa kuzalisha umeme megawati 103, hivyo unanunua mafuta ya Sh bilioni moja unauza umeme unaotokana na fedha hiyo unapata Sh milioni 800, unapata hasara ya milioni 200 jambo ambalo lilikuwa likisababisha hasara kubwa, hivyo tumekataa kuendelea na utaratibu huo wa hasara,” alisema Dk. Kalemani. Alisema baada ya kufanyika kwa uamuzi huo kumechochea sasa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida kubwa hatua mbayo itachochea kusukuma zaidi maendeleo.  “Hatua hiyo sasa imefanya Shirika kujiendesha kwa faida hivyo kuchochea kutoa gawio kwa serikali la Sh bilioni 1.43 kwa mwaka wa fedha uliopita, lakini pia kama Rais Magufuli alivyotuelekeza kujisimamia shirika kwasasa halipati ruzuku kutoka serikalini badala yake linajiendesha lenyewe na kwa faida kubwa,” alisema. Upatikanaji umeme nchini Akizungumzia hali ya upatikanaji umeme nchini, Dk. Kalemani alisema kuwa imekuwan ikiimarika siku hadi siku na kwamba kwa mwaka 2015 kulikuwa na megawati 1,038 katika gridi ya taifa huku mwaka huu ikifikia megawati 1,602.34 sawa na ongezeko la megawati zaidi ya 480. “Hii yote imechangiwa na kuwapo kwa miradi ya Kinyerezi I na II ambayo imekuwa ni kichocheo cha ongezeko hili, hatua ambayo imechagia kuwapo kwa umeme wa kutosha, pia tumekarabati mitambo ya Kitadu, Kihansi na Mtera. “Pia tumeimarisha miundombinu ya usafirishaji umeme nchini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mikoa yote inaunganishwa kwenye gridi ya taifa, mfano njia ya kutoka Mbagara hadi Mtwara ambao ni umbali wa kilometa 512 za umeme wa Kilovolt 132, kwani mikoa ya kusini haikuwahi kuunganishwa na gridi ya taifa kwa miaka yote hivyo ni jambo la kujivunia,” alisema Dk. Kalemani. UPATIKANAJI WA VIFAA Alisema mwaka 2015 transfoma zilizokuwa zimefungwa nchini zilikuwa ni 12,200 na kwamba kwasasa zimefika 23.000 sawa na asilimia 100, hatua ambayo imesaidia kupatikana kwa umeme wa kutosha. “Maeneo mengi kwasasa umeme haukatikin kutokana na kuboresha teransfoma na kuondoa zilizochoka, sawa na eneo la nguzo ambalo nalo limeimarika kwa kuwa sasa zinapatikana nchini hatua mbayo imeokoa fedha Sh bilioni 162 na hakuna upungufu wa nguzo. “Hilo pia tumelifanya kwenye eneo la mita za luku ambapo hadi sasa tuna viwanda vitatu vinavyoweza kuzalisha mita zaidi ya milioni 2.5 ikilinganishwa na mahitaji yetu ambayo ni milioni 1.6. “Hata Bwawa la Mtera maji yameongezeka na kufikia mita za ujazo zaidi ya 696.7 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa, hivyo hali ya umeme uliopo unatosha kwasasa na kunaziada ya megawati 280 hadi 300 kwa siku,” alisema Dk. Kalemani na kuwahimiza wakandarasi kusambaza umeme kwa wakati ili kuwaondoa wananchi gizani. Alisema hadi kufikia Juni 31, mwakani vijiji vyote nchini vitakuwa vimeunganishwa na umeme na kuwa nchi ya kwanza kwa Afrika Mashariki kufikia hatua hiyo. Aidha, aliwataka wawekezaji waonajenga vituo vya mafuta kuhakikisha kuwa katika kila vituo vitatu wanavyojenga kimoja kinakuwa kijijini ili kusaidia nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana kuendelea kufanya shughuli zao huko waliko pamoja na kuondoa tabia ya vijana kuuza mafuta kwenye chuoa za maji. Kuhusu akiba ya mafuta, Dk. Kalemani alisema kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta yote ikiwa ni pamoja na mafuta ya Petroli, Dizeli, Ndege na mafuta ya taa.
KITAIFA
SERIKALI ya Oman imetenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la maajabu ya historia ya mambo ya kale 'Beit-al-Jaib' lililopo eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar, ili kulirudisha katika uhalisia wake wa awali.Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka kujua maendeleo ya kazi hiyo.Alisema hatua ya kwanza zilizochukuliwa ni kulihami jengo ili lisiporomoke imekamilika na sasa jengo lipo salama na tishio la kuanguka zaidi katika kipindi hichi cha mvua za masika.Alisema jengo hilo kwanza lilihitaji kuzuiliwa na kuwekewa vyuma ili matengenezo madogo yafanyike ambapo jumla ya Sh milioni 250 zilitumika ambazo zimetolewa na serikali ya Oman.Alizitaja hatua zinazoendelea kuchukuliwa kwa sasa ni kufunguliwa kwa kwa zabuni ya tenda ya ujenzi wa jengo hilo kazi ambayo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwezi huu.Alisema baada ya hapo mjenzi wa kufanya ukarabati huo atapatikana ambaye atashirikiana na kampuni moja kutoka Oman itakayosimamia kazi hizo kwa kuishirikisha Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar.''Mheshimiwa Spika nataka kusema kwa ufupi kwamba kazi za ukarabati wa jengo la ''Beit-al Jaib'' unaendelea hatua kwa hatua.....hiyo kazi haijasimama ambapo wenzetu wa Oman wametenga fedha nyingi kwa ajili ya kazi hiyo,'' alisema.Alisema Serikali ya Oman kupitia viongozi wake mbalimbali waliotembelea Zanzibar mwaka huu, imeahidi pia kulifanyia ukarabati jengo la kasri la makao makuu ya wafalme waliopita People Palace liliopo Forodhani mkabala na bandari ya Malindi.Alisema ukarabati huo ni muhimu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutunza historia ya Zanzibar ya watawala mbali mbali waliopata nafasi ya kuongoza visiwa vya Unguja na Pemba.''Tumezungumza na ujumbe wa Oman ambao pia umekubali kulifanyia ukarabati jengo la People Palace ambalo lilikuwa makao makuu ya watawala wote waliotawala Zanzibar tangu mwaka,'' alisema.Mwaka 2017 ujumbe wa ngazi za juu kutoka Oman ukiongozwa na Waziri wa Mafuta na gesi, Dk Mohamed Hamad Al-Rumhy alitembelea Zanzibar na kuahidi kufanyika kwa ukarabati wa jengo hilo akisema ni utambulisho wa Mji wa Zanzibar kimataifa.Aidha, mwaka jana ujumbe wa Oman ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale, Salum Mohamed Al-Mahrooq ulitembelea Zanzibar na kuonana na viongozi wa ngazi za juu huku kiongozi wa ujumbe huo akiahidi kutekelezwa kwa mradi wa jengo hilo ambalo lilijengwa karne ya 17.
KITAIFA
Chanzo cha picha, Getty Images Tottenham wamedhamiria kuzima majaribio ya Manchester United ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 29, msimu huu wa joto, huku mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akigoma kumuuza Kane kwa timu pinzani ya Ligi kuu England. (Mirror) Erik ten Hag ana imani kuwa anaweza kumshawishi kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 ajiunge na Manchester United kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake kwenye usajili wa majira ya joto. (Telegraph) Bayern Munich wako tayari kulipa pauni milioni 95 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, huku timu hiyo ya Ujerumani ikiwa na nia ya kuipiku Arsenal katika kuinasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mirror) Paris St-Germain wana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 24. (Mail) Chanzo cha picha, Getty Images Tottenham, Newcastle na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vya Ligi kuu ya England vinavyomtaka James Maddison wa Leicester. Kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 26 anaweza kununuliwa kwa takriban £40m. (Mirror) Crystal Palace wamemtafuta mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter kuziba nafasi ya kocha iliyo wazi, huku Nice pia ikimtaka Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 48. (Footmercato) Liverpool wamekataa ofa ya kudumu ya uhamisho kutoka nje ya nchi kwa kiungo mshambuliaji wa Ureno chini ya umri wa miaka 21 Fabio Carvalho huku klabu hiyo ya Merseyside ikifikiria kumtoa kwa mkopo tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Athletic) West Ham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua James Ward-Prowse, huku Southampton wakisema thamani ya kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 28 ni pauni milioni 40. (Sun) Chanzo cha picha, Getty Images Newcastle wana imani kuwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 25, atasaini kandarasi mpya huko St James' Park licha ya kutakiwa na Barcelona. (90Min) Mshambulizi wa Brazil Roberto Firmino, 31, ambaye ataondoka Liverpool msimu huu wa joto, anasubiri kuona kama atafaa kwenye mipango ya Real Madrid kabla ya kuchukua uamuzi wa kuhamia Hispania. (Mail) Kocha wa Barcelona Xavi amekiri kuwa yuko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina na Paris St-Germain Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35 kuhusu kurejea Camp Nou msimu wa joto. (Standard) Chanzo cha picha, Getty Images Everton inamtaka mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure mwenye umri wa miaka 21 baada ya kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Almeria siku ya Jumapili. (Mail) Chelsea wameanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uruguay na Sporting CP Manuel Ugarte, 22. (90Min) Crystal Palace wanafikiria kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Chelsea na England wa chini ya umri wa miaka 19 Lewis Hall, 18. (Mail)
MICHEZO
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM KITENDO cha mama kumnyonyesha mtoto mdogo huku akiwa amekunywa pombe, kinatajwa kuwa ni hatari kwa afya. Kitendo hicho kinatajwa kuwa ni hatari kwa sababu mtoto hunyonya kilevi hicho kupitia maziwa ya mama yake na baadaye huathiri afya ya ubongo wake. Hayo yalisemwa na bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Plaxeda Swai wakati wa mahojiano na MTANZANIA Jumapili mapema wiki hii.  “Unywaji pombe ni hatari kwa mjamzito na mama anayenyonyesha, mjamzito haruhusiwi kutumia kilevi cha aina yoyote, pombe huathiri afya ya mtoto aliyepo tumboni na anaweza akazaliwa akiwa na hitilafu kuanzia mfumo wa fahamu, kuzaliwa na uzito mdogo, kichwa kidogo na madhara mengine mengi. “Wapo wanaofikiri kwamba madhara hujitokeza wakati wa ujauzito pekee na wanapojifungua hawajali wakati wa kunyonyesha wanalewa, mama anayenyonyesha akiwa amelewa, mtoto wake naye hulewa kwa sababu hupata pombe kupitia maziwa ya mama yake.  “Hatua hiyo ni mbaya kwa afya ya mtoto, kwa sababu kilevi huenda kuathiri afya ya ubongo wa mtoto na matokeo yake anaweza hata kupata mtindio wa ubongo,” alisema Dk. Swai. Alisema unywaji wa pombe kupita kiasi hasa zile zilizo kali, ni hatari kwa afya ya mtumiaji kwa sababu anakuwa katika uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la kifafa baadaye katika maisha yake. “Asilimia nne ya watu wanaokunywa pombe kali huishia kupata kifafa, asilimia 50 hadi 75 ya watu wanaokunywa vilevi kupita kiasi huishia kupata matatizo ya kiakili na asilimia 20 hadi 25 ya watu wenye matatizo ya akili huwa wametumia aina moja au nyingine ya kilevi,” alisema Dk. Swai. Pia alishauri watu waliofikia hatua ya utegemezi wa vilevi na wanahitaji kuondokana na hali hiyo ni vema wakawahi mapema kufika hospitalini kwa matibabu. “Tafiti zinaonyesha asilimia 80 ya watu ambao wamefikia kiwango cha utegemezi wa pombe hupata tatizo la sonona na hofu iliyopitiliza,” alisema.
KITAIFA
SWAGGAZ RIPOTA AGIZO la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu kuchunguzwa kwa nyota wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, kama anatumia bangi au laa ili aweze kukamatwa, limenifikirisha vitu vingi na kufanya nianze kutazama kwa ukaribu mwenendo wa hivi karibuni wa memba huyo wa WCB. Licha ya mazuri mengi ambayo amekuwa akiyafanya kama vile kusaidia walemavu, kutoa mitaji kwa wanawake na vijana wajasiliamali, kufanya shoo kubwa zinazoacha gumzo pamoja na kuzidi kupaa kimuziki, Harmonize amekuwa tofauti kitabia na yule wa kipindi kile anaatoka. Ukitazama ukurasa wake wa picha ambao mpaka sasa una wafuasi zaidi ya milioni 2.9, utagundua mambo kadhaa ambayo hapo awali hakuwanayo. Mengi ni mabaya yanayofunika mazuri, jambo linalowaumiza wanaopenda mafanikio yake. TABIA YA KUVUTA SIGARA Katika agizo la mlezi wa WCB, Paul Makonda alilolitoa juzi katika kikao chake na wasanii, alisema tabia ya ajabu ni miongoni mwa sababu zinazokwamisha wasanii wengi kupata dili kwa kuwa kampuni nyingi zinataka mtu safi asiye na uchafu mbele ya jamii. Ndiyo maana akiwa kama baba wa WCB, alimwomba gavana wa Accra, Ghana amchunguze kijana wake Harmonize kama anachovuta hadharani ni sigara au bangi ili kama ni dawa za kulevya basi akitua Bongo, aweze kuwekwa rumande na kufunguliwa kesi kama ile ambayo ilimkuta mrembo Wema Sepetu. Hiyo yote imetokana na tabia mpya ya staa huyo, kuvuta sigara hadharani jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya vijana wadogo wanaomtazama kama kioo pia hata kwa afya yake akiwa kama msanii wa muziki anayeiwakilisha vyema Tanzania huko ulimwenguni. MGUU NDANI MGUU NJE WCB? Harmonize kwa sasa ni msanii mkubwa. Ukitazama msafara wake wenye walinzi mbavu nene wapatao wanne utagundua jamaa siyo wa mchezo na tayari ameanza kujijengea ‘empire’ au utawala wake akiwa bado ni memba wa WCB. Licha ya mambo kadhaa yanaonyesha, Harmonize bado ni msanii wa WCB, kuna tetesi zilizotokana na mwenendo wa msanii huyo na  viongozi wa WCB kuwa kwa sasa Konde Boy, mguu mmoja ndani na mwingine upo nje ya lebo hiyo kubwa Afrika. DIAMOND ASHANGILIA AGIZO LA MAKONDA Wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akitoa kauli ya Harmonize kushughulikiwa kutokana na tabia yake ya kuvuta hadharani kitu kinachotoa moshi unaofanana na bangi, Diamond Platnumz alionekana akipiga makofi. Hiyo ni ishara kuwa anapongeza na amefurahishwa na agizo hilo ambalo kama ni kweli linakwenda kumtia matatani Harmonize ambaye ni msanii wake. SAPOTI IMEKUWA NDOGO Tetesi zimeendelea kudai kuwa huwenda Harmonize hayupo sawa na Diamond Platnumz au viongozi wake kutokana na sapoti ndogo ambayo amekuwa akipewa hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Mfano wimbo Paranawe wa Harmonize aliofanya na Rayvanny, Diamond Platnumz, hakuwahi kuuposti katika ukurasa wake wa Instagram kama ilivyokawaida yao kusapotiana. Hata mameneja wao kama Sallam Sk, Babu Tale na Mkubwa Fella hawakuupa sapoti mtandaoni wimbo huo kama ambavyo wanawapa kina Rayvanny, Mbosso, Lavalava na wasanii wengine. Hali kadharika hivi karibuni Harmonize, anaachia albamu yake fupi (EP) inayoitwa Afro Bongo. Hii ni albamu kubwa inayotarajia kusumbua chati mbalimbali za muziki Afrika akiwa ameshirikiana na staa wa Nigeria, Burna Boy. Jambo la kusangaza, Harmonize amekuwa akiipa promo yeye mwenyewe bila sapoti ile kubwa ambayo tumezoea kuioa WCB wakipeana. HARMONIZE ANAKWAMA WAPI? Hakuna anayeweza kubisha kuwa Harmonize ni msanii bora zaidi kwa sasa, tazama nyimbo zake zinavyoweka rekodi kubwa, fuatilia shoo zake anazofanya, utagundua ni msanii ambaye atadumu kwa muda mrefu kwenye muziki. Harmonize, anakwama pale ambapo anaanza kulewa sifa kipindi hiki ambacho Afrika imempokea vizuri na tayari ameanza kuuwakilisha vyema ukanda huu wa Afrika Mashariki kama mwenyewe anavyojiita ‘East African Young Star’. Anaweza asione mapungufu hayo lakini ni vizuri akasikia kelele za mashabiki wanaompenda, wakimuonya kuwa siyo vizuri kwa afya yake kutumia moshi, siyo jambo jema  kujikweza ila vizuri kujilinda, kuwekekeza kwenye kazi na kusaidia jamii ili aendelee kudumu miaka na miaka.
BURUDANI
SERA ya Uchumi wa Kati kupitia ujenzi wa viwanda, umepata msukumo baada ya Kampuni ya IPP kuingia ubia wa kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari kutoka Jamhuri ya Korea maarufu kama Korea Kusini, kinachotarajiwa kuzalisha magari 1,000 kwa mwaka.IPP imeingia ubia huo na Kampuni ya Youngsan wenye uwekezaji wa kiasi cha zaidi Sh bilioni 22, sambamba na kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi 500, idadi inayotarajiwa kuongezeka kadri ya muda unavyokwenda. Ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kurasini, utaanza mwanzoni mwaka ujao na uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza kati ya Septemba na Oktoba mwaka huo.Makubaliano ya uanzishwaji wa kiwanda hicho yalifikiwa jijini Dar es Salaam kati ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Song Geum-young ambao kwa pamoja walisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, kumelenga kuunga mkono juhudi za maendeleo nchini.Akizungumzia hatua hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, ilikuwa moja ya ndoto zake kama hatua ya kuitikia mwito wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, inayosisitiza kasi ya ujenzi wa viwanda nchini.“Hakuna kinachoshindikana ukiwa na nia, hata Rais wetu anapambana katika mambo ambayo wengi waliona yanashindikana, amenunua ndege na kufanya mengine mengi..hii ni hatua kubwa katika kukuza maendeleo yetu,” alisema Mengi.Alisema kiwanda hicho kikianza kazi, kitatoa ajira kwa Watanzania, pia kitasaidia kuongeza mzunguko wa biashara katika Afrika Mashariki na Kati na kuiingizia mapato serikali kupitia kodi mbalimbali.Aidha, alisema mipango yake ya baadaye ni kuhakikisha wanajenga kiwanda chenye uwezo wa kutengeneza magari kuanzia mwanzo hadi inapokamilika kutoka katika hatua hiyo ya uunganishaji, jambo alilosema litazidi kuitangaza Tanzania.Magari yanayotarajiwa kuunganishwa kupitia kiwanda hicho ni mabasi, malori na magari madogo, ambapo kwa mujibu wa Balozi wa Jamhuri ya Korea, magari hayo ni ya kisasa. Alisema Jamhuri ya Korea imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa magari na kwamba anaamini kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho nchini, kutasaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda na kuleta tija kimaendeleo.
KITAIFA
Mkutano huo ambao umeandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kwa kushirikiana na kampuni ya ushauri na lengo lake ni kuwasaidia wawekezaji wa hapa nchini, ambao hawana mitaji mikubwa ya uwekezaji waweze kuingia kwenye biashara kwa kushirikiana na wawekezaji wa nje ya nchi.Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, alisema jana kuwa taasisi yake, inachofanya ni kutaka kuinua sekta binafsi nchini kwa kuwakutanisha na wawekezaji wenye fedha nyingi kutoka nje ya nchi na wafanyabiashara wa ndani, wajadiliane kwa pamoja na waone namna ya kufanya biashara kwa ubia.“Kuna watu wana fedha nyingi huko nje hawajui pa kuzipeleka, tumewaalika na kwenye mkutano wa kesho (leo) watakuwepo na lengo letu tunataka wawekezaji wa ndani waongee nao na hatimaye waingie ubia wa kibiashara ili kutunisha mitaji yao,” alisema.Alisema ikiwa Watanzania wataingia ubia na wawekezaji hao wa nje, taasisi yake itakuwa imefanikiwa kukuza mitaji ya ndani, ambayo kwa sasa ndio malalamiko makubwa ya wawekezaji wa ndani.Simbeye alisema lengo la mkutano huo ni majadiliano ya kina, ambapo Watanzania wanapaswa kuwaeleza wawekezaji hao ni miradi gani waliyonayo ambayo wanaona kuna haja ya kuingia ubia na watu wa nje na kila upande ukafaidika.Mkurugenzi huyo alisema tayari wawekezaji 50 wako tayari kukutana na wawakilishi wa kampuni za hapa nchini.Aliwataka Watanzania wote ambao wanatafuta fursa ya kutunisha mitaji yao, wajitokeze kwa wingi katika mkutano huo.
UCHUMI
['Bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Eliud Kipchoge Ijumaa wiki hii ametangazwa mwanamichezo bora katika hafla ya kufana iliyofanyika katika uwanja wa Mombasa Sports Club.', 'Kipchoge pia alichaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa kitengo cha wanaume naye bingwa wa dunia, Hellen Obiri akatwaa tuzo la wanawake.', 'Baadhi ya wanamichezo ambao Obiri aliwabwaga ni Brigid Kosgei ambaye anashikilia rekodi ya dunia na bingwa wa dunia wa marathon Ruth Chpngetich.', 'Miongoni mwa wanamichezo Kipchoge aliwaangusha ni bingwa wa dunia mbio za mita 1,500, bingwa wa Olimpiki na wa dunia mbio za mita 3000 kuruka vizuizi na maji, Conseslus Kipruto.', '"Nafurahia sana kushinda tuzo hii, inamaanisha watu wametambua niliyofanya Vienna kwa kukimbi chini ya saa mbili katika marathon. Napenda kuwaambia watu kuwa hazikua mbio ya ushindi ila kutuma ujumbe ya kwamba hakuna lisilowezekana dunia," anasema Kipchoge.', 'Timu bora kwa wanaume ilikua ni klabu ya mpira ya Bandari na Malkia Strikers kwa wanawake.', 'Malkia Strikers ilishinda taji la voliboli katika michezo ya mataifa ya Afrika nchini Morocco na hatimaye ikashiriki kombe la dunia nchini Japan.', ' "Ushindi huu wa tuzo la timu bora umetuongezea motisha sana. Tunajiandaa sasa kwa michezo ya Olimpiki. ', 'Huko tunaenda kubeba kombe," anasema nahodha wa Malkia Strikers Mercy Moim ambaye anafanya kazi na idara ya Magereza.', 'Mkufunzi wa Malkia Strikers Paul Bitok alishinda tuzo la kocha bora.']
MICHEZO
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia alitoa kauli hiyo bungeni mjini hapa jana akijibu swali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM).Ndassa ambaye ni mwanachama wa Simba aliuliza swali la nyongeza akitaka kufahamu kauli ya serikali kuhusu uozo wa rushwa ndani ya Fifa ambao umesababisha Rais wake, Joseph ‘Sepp’ Blatter kujiuzulu.Nkamia alisema Tanzania kama mwanachama wa Fifa, haifurahishwi na kinachotokea Fifa na inalaani matukio ya rushwa yanayoibuliwa sasa katika chombo hicho cha juu cha uendeshaji wa soka duniani.“Tunafahamu kuwa kuna uchunguzi unaoendelea, na Tanzania itatoa msimamo wake baada ya uchunguzi huo kukamilika,” alisema Nkamia na kuongeza: “Hii ni kashfa nzito, Tanzania tunalaani kwa sababu suala la rushwa halikubaliki siyo tu katika Fifa, bali hata katika michezo yetu yote hapa nchini.”Nkamia alisema zipo taarifa kwamba katika mpira wa miguu nchini, kuna klabu na wanamichezo wanajihusisha na rushwa na kueleza kuwa serikali haikubaliani na hilo, na inakemea kwa nguvu zake zote.Fifa imegubikwa na matatizo ya rushwa katika miaka ya karibuni katika utawala wa Blatter aliyeingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1998.Siku chache kabla ya kuchaguliwa kwa muhula wake wa tano Mei 29, mwaka huu, maofisa 14 wa Fifa walikamatwa na wengine kufunguliwa mashitaka kwa tuhuma za rushwa ndani ya shirikisho hilo.Licha ya kelele za watu mbalimbali kumsihi Blatter aachie ngazi kabla ya uchaguzi huo, Kanali huyo wa zamani wa Jeshi la Uswisi, aligoma na kuchaguliwa kwa muhula wa tano akimshinda Prince Ali bin Hussein wa Jordan.Hata hivyo, juzi Jumanne usiku, Blatter alitangaza kuwa anajiuzulu wadhifa huo kwa madai kuwa amegundua ushindi wake kwa sasa hauungwi mkono na wapenda soka wengi duniani, jambo ambalo si zuri.
MICHEZO
Ramadhani Hassan -Dodoma KAMPUNI ya Starpeco Limited ya Dar es Salaam, imeanza ujenzi wa barabara darasa jijini hapa kwa kutumia teknolojia ya lami baridi huku Wakala wa Huduma za Barabara Vijijini (Tarura) ikisema iwapo teknolojia hiyo itaonekana kufanya  vizuri  watairuhusu iweze kutumika maeneo mbalimbali nchini. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Meneja wa Tarura Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Mohammed Makwata  wakati akifungua semina ya wanafunzi  wa vyuo vya ufundi stadi (Veta) nchini ambao walikuwa wakipewa uelewa kuhusu teknolojia ya lami baridi. Semina hiyo iliandaliwa na Kampuni ya Starpeco ambayo inajishughulisha na ujenzi wa barabara kwa kutumia lami baridi. Makwata alisema iwapo  teknolojia ya lami baridi itaonekana kufanya  vizuri,  watairuhusu iweze kutumika maeneo mbalimbali nchini kwani wana mtandao mkubwa wa barabara. “Teknolojia hii ikionekana kufanya vyema basi itatumika katika ujenzi wa barabara zetu. Tarura ina barabara nyingi zinazohitaji kujengwa na kutumika nyakati zote kwa maendeleo ya uchumi wa nchi,” alisema Makwata. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Starpeco, Gratian Nshekanabo, alisema kampuni yake  imeweza kuweka  viraka katika barabara ya Changanyikeni na barabara ya Uvumbuzi zilizopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na kumwaga lami mpya katika barabara ya Kileleni yenye urefu wa kilomita 120. Pia alisema teknolojia ya lami baridi imetumika katika ujenzi wa barabara ya Bagamoyo, Tazara Flayover na Ubungo Flyover na kwa sasa wanakarabati barabara darasa katika Jiji la Dodoma. Alizitaja barabara hizo ni zile zenye majina ya viongozi wakuu wa nchi ambazo ni Magufuli na Samia zilizopo Area C jijini hapa. Nshekanabo alisema teknolojia hiyo ni nzuri kwa kuwa ni rafiki kwa mazingira, ni rahisi na gharama zake ni ndogo, hivyo aliitaka Serikali kuitumia katika ujenzi wa barabara zake. “Ujenzi wa lami  baridi kuna faida nyingi na ni rafiki kwa mazingira, ni rahisi. Tuache mazoea kwani  mambo yamebadilika, tunaweza tukawa tunawalalamikia wakandarasi wakati hawatakiwi kulalamikiwa,  tubadilike tutumie lami baridi,” alisema Nshekanabo. 
KITAIFA
Matayo Kudenya, kijana aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la tende ya korodani , hatimae amepata msaada wa kufanyiwa upasuaji bila gharama kwa udhamini wa hospitali ya Decca iliyopo jijini Dodoma. Jopo la madaktari bingwa wanne, madaktari wawili wa usingizi wawili na wauguzi wawili wameshiriki katika upasuaji huo ambao umechukua jumla ya saa tatu na dakika arobaini na tano na kufanikisha kuondoa uvimbe wa kilo 25 zilizokuwa katika korodani ya Matayo. DKt Martin Singani ndie aliyekuwa daktari kiongozi wengine wakiwa ni Dkt Gustavus Deusdedith, Dkt. Charles Abeid na Dkt Ambilikisye Kajange Dkt Gustavus Deusdedith, mmoja wa madaktari amemwambia mwandishi wetu Aboubakar Famau kwamba mgonjwa anaendelea vizuri. Video ya wito uliotolewa na Kudenya akizungumza na BBC Daktari amesema, katika uchunguzi wao wa kitaalamu, wamebaini kuwa Matayo, alisumbuliwa na matende kama ya juu ya mguuni na sio ngiri maji kama alivyoeleza mwenyewe hapo awali. Kwa upande wake, Steven John ambae ni mjomba wa Matayo amesema, ameguswa sana na msaada huo ana anashukuru sana. "Sina la kusema kwa msaada huu. Machozi yananitoka," amesema John. Kutokana na ukubwa wa upasuaji wake, Matayo aliwekewa chupa 15 za maji na tatu za damu Itambukwa kuwa, BBC ndio iliyorusha taarifa za Matayo akiomba kusaidiwa, hivyo kupelekea kupata msaada huo. Wataalamu wanasema inaweza kumchukua Matayo kuanzia siku 10 mpaka 14 kupona.
AFYA
WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha mchezo wa timu ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho katika mbio za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, Azam FC bado ni zaidi ya Simba na Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. Taifa Stars itakwaana na Lesotho katika mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu kwa Afcon mwakani nchini Cameroon utafanyika Novemba 18 ugenini. Kwa sasa timu hiyo imepiga kambi ya mazoezi Afrika Kusini ikiendelea kuzoea hali ya hewa ya Lesotho, huku kocha wake, Mnigeria Emmanuel Amunike akisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri kwa ajili ya mpambano huo muhimu. Kwa upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC kwa muda sasa iko kileleni ikiwa na jumla ya pointi 30, baada ya kushuka dimbani mara 12 wakati mabingwa watetezi Simba pamoja na watani zao Yanga, wenyewe wana pointi 26 kila moja lakini wakicheza mechi pungufu. Simba, wenyewe wameshuka uwanjani mara 11 wakati Yanga wamefanya hivyo mara 10, hivyo ni matarajio ya timu hizo kutumia vizuri viporo vilivyobaki ili kuifikia na kuipita Azam FC katika mbio za kusaka ubingwa na nafasi ya kuliwakilisha taifa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwakani.Licha ya ligi kutofikia hata katikati ya msimu, lakini dalili zimeanza kuonekana kuwa mbio za kuwania taji hilo zitakuwa za timu tatu za Azam, Simba na Yanga, huku Mtibwa Sugar ikifuatiwa, licha ya kutokuwa tishio sana katika mbio hizo kutokana na rekodi yake. Mtibwa Sugar ndio wawakilishi wa Tanzania Bara katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la FA. Timu za Biashara United ya Musoma, Tanzania Prisons ya Mbeya, African Lyon ya Dar es Salaam, Lipuli, Alliance ya Mwanza, Ndanda ya Mtwara, Mwadui ya na Stand United za Shinyanga haziko katika nafasi nzuri, kwani wakati wowote zinaweza kushuka au kupanda katika msimamo kutokana na jinsi zitakavyochanga karata zao. Kiujumla mbio za kuwani ubingwa bado mbichi, lakini biashara siku zote ni asubuhi na jioni huwa ni kazi ya kuhesabu mapato, hivyo Azam FC kama itakwenda na mwendo huu wa kushinda mechi zake licha ya kupata ushindi mwembamba, inaweza kufika mbali na kufanya makubwa. Azam na Yanga ndio timu pekee ambazo hadi sasa hazijafungwa, lakini Simba pamoja na kufungwa ndio wenye kuonekana kuwa na safu kali ya ushambuliaji baada ya hadi sasa kutupia jumla ya mabao 23 ikifuatiwa na Yanga yenye mabao 17 na Azam 15.
MICHEZO
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), akilia baada ya kutakiwa apite kwenye migongo ya wanawake waliolala chini, wakati akielekea jukwaani kuwahutubia wananchi wa jimbo hilo jana. Na Florence Sanawa – Lindi ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema matendo ya utekaji nyara wananchi yasipotatuliwa yatakipa shida Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Nape alitoa kauli hiyo jana, ikiwa ni siku chache baada ya hivi karibuni kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa kama si kuingia msituni kwa miezi 28, CCM ilikuwa inaelekea shimoni. Akiwahutubia wananchi wa jimbo lake la Mtama jana, Nape alitaka hatua zichukuliwe za kukomesha tabia ya utekaji nyara wananchi, huku akikumbushia tukio la kada wa Chadema, Ben Saanane, ambaye amepotea miezi mingi iliyopita katika mazingira ya kutatanisha.  “Naomba hatua zichukuliwe tukomeshe hii tabia, Ben Saanane amepotea miezi mingi na mazingira ya kupotea ni ya kutatanisha. Matendo haya yasipotatuliwa na kukomeshwa, tutapata shida sana 2020,” alisema. Aliongeza kwa kusema kuwa matendo ya kuwateka nyara akina  Ben Saanane, Roma Mkatoliki, na wengine yanamjengea chuki Rais Dk. John Magufuli dhidi ya wananchi. Katika muktadha wa hoja hiyo, alilijumuisha tukio la mtu aliyemtishia bastola hivi karibuni wakati akitaka kufanya mkutano na wanahabari Dar es Salaam, kumshukuru Rais Magufuli kumteua na kisha kumwondoa katika wadhifa wa uwaziri aliokuwa anautumikia. “Shida niliyonayo huyu aliyetoa silaha vyombo vya dola vinafanya nini? lazima hatua zichukuliwe, Siamini alitumwa kutoa silaha, lakini alifanya upuuzi wake, ndiyo maana sikutishika, niliona kama anatoa ‘mice’… na mimi nilikuwa na bastola kubwa kuliko yake. “Nilivyofika yule kijana mpuuzi mliyemuona, akasogea karibu yangu. Nikamnong'oneza tuko moja kwa moja na vyombo vya habari vinaangalia,” alisema Nape. Akizungumzia uvamizi katika kituo cha Clouds, ambao wengine wanahusisha hatua alizozichukua ndizo zilizogharimu uwaziri wake, Nape alihoji akisema: “Wengine wamevamia kituo cha utangazaji, kama siyo yule tunayemwona kwenye kamera basi ni nani? “Wengine wamevamia studio na kuwachukua watu akiwamo Roma, watu wanapotea kama nzi.” Aliongeza kwamba Rais anapaswa kuingilia kati vitendo vya utekwaji watu vinavyofanywa pasipo kuchukuliwa hatua yoyote. Alisema hatua hiyo inaweza kusababisha watu wabaya kuendeleza matukio hayo kwa kuwa yamekuwa hayachukuliwi hatua. “Rais achukue hatua ili matendo haya yasijirudie, unajua dawa ya moto si moto, wakati mwingine unaweza kuuzima kwa maji. “Kifua changu kina mengi sana, siwezi kuyasema, lazima mkumbuke kuwa Rais Magufuli nimemtafutia kura mimi mwenyewe,” alisema Nape. Akizungumzia uamuzi wa Rais Magufuli kumtengua katika wadhifa wa uwaziri, Nape alisema uamuzi huo ni mabadiliko ya kawaida kwa mujibu wa katiba ya nchi.  “Nilitumia nguvu zangu zote kuhakikisha dhamana niliyopewa naitendea haki, Rais Magufuli alisema amefanya mabadiliko ya kawaida na ni kwa mujibu wa katiba yetu. Mara nyingi ukiwa na mchezaji mzuri na amefunga magoli mengi, unampumzisha ili acheze kesho. “Wapo waliosema Nape usiende kuzungumza Mtama, lakini siwezi kuwaacha wananchi wangu na maswali yasiyo na majibu… tusimnunie kocha aliyebadilisha wachezaji,” alisema Nape. Hata hivyo, Nape alikwenda mbali zaidi kwa kuwasihi wananchi wasiyumbishwe na cheo. Katika hili, alisema ni bora kuyumbishwa na msimamo ambao umewekwa na wananchi. Zaidi aliwaasa vijana kusimama imara kuusemea ukweli. Alisema Tanzania bado itakuwa salama kama vijana watasimama kuusemea ukweli. Katika hatua nyingine, Nape alizungumzia uhusiano wake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisema wao sasa ni kitu kimoja. “Kama mimi na Lowassa tuna kunywa chai sasa, nyie mnanuniana nini? Sisi ni kitu kimoja,” alisema Nape. Kauli hiyo ya Nape inatoa tafsiri ya kwenda kinyume na mrengo wake wa siku nyingi wa kutomkubali Lowassa kwa jambo lolote. Wakati akitumikia wadhifa wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape alisikika mara kadhaa akitoa kauli chafu dhidi ya Lowassa na mara nyingi alisikika akimfananisha na Oil chafu au marehemu anayetembea. ALIVYOPOKEWA Nape alipokewa na umati wa wananchi waliokuwa wakiburudishwa kwa wimbo wa ‘Nyota na ing’are’ wa Peter Msechu. Katika mapokezi hayo ya aina yake, Nape alitembea kwa kupita juu ya migongo ya akina mama  zaidi ya 10 waliokuwa wamelala  kifudifudi chini kwenye njia ya kuelekea jukwaa kuu. Wakati Nape akipita juu ya migongo ya akina mama hao, alishindwa kujizuia na badala yake alijikuta akibubujikwa na machozi hali iliyoibua tafsiri ya aidha alikuwa na furaha au hasira.
KITAIFA
WASHINGTON, MAREKANI MWANADIPLOMASIA wa Marekani nchini Ukraine, William Taylor, jana ametoa ushahidi mbele ya kamati ya ujasusi ya baraza la wawakilishi katika mchakato wa uchunguzi dhidi ya rais wa nchi hiyo Donald Trump. Kesi hiyo imesikilizwa kwa mara ya kwanza jana kwa njia ya televisheni, kwa nia ya kumshitaki Trump bungeni. Taylor alimhusisha moja kwa moja Trump na shinikizo la kampeni dhidi ya Ukraine ili kufanya uchunguzi utakaomnufaisha yeye binafsi. Taylor na mwanadiplomasia mwingine George Kent walitoa ushahidi juu ya shinikizo lililotolewa na Trump na washirika wake, dhidi ya Ukraine kumchunguza hasimu wake wa Democratic, Joe Biden kuhusu shughuli za kibiashara za mwanae wa kiume nchini Ukraine. Taylor aliliambia baraza la wawakilishi kwamba, wafanyakazi wenzake walisikia mazungumzo ya simu mnamo Julai 26 kati ya Trump na Gordon Sondland, ambapo Trump alimuuliza kuhusu uchunguzi huo na kujibiwa kuwa Ukraine wako tayari kuendelea.
KIMATAIFA
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru wa asilimia tano kwa bidhaa zote zinazotoka nchini Mexico, ili kuishinikiza nchi hiyo kuchukua hatua kali zaidi kuwazuia wahamiaji haramu kuingia Marekani.  Ushuru huo utaanza kutozwa rasmi kuanzia Juni 10 mwaka huu na unaweza kupanda mpaka asilimia 25 hadi tatizo hilo la wahamiaji litakapokuwa limedhibitiwa.  Uamuzi huo wa Trump unaonesha kuwa, Serikali ya Marekani itachukua hatua mpya za kuongeza mbinyo kwa Mexico kama ilivyokuwa kwa China kuchukua hatua hata kama zitahatarisha vipaumbele vya sera nyingine kama za makubaliano ya biashara huru kati ya Marekani, Mexico na Canada, ambayo ni msingi wa ajenda ya Trump bungeni na yanayoweza kumnufaisha katika juhudi zake za kuchaguliwa tena.
KIMATAIFA
Hiyo ni mechi ya pili ya kirafiki kwa Stars baada ya ile ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Botswana ambapo Stars ilishinda mabao 2-0.Stars ipo kwenye maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ na ile ya wachezaji wa ndani ‘Chan’ na Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga alisema mechi ya leo ni maalumu kwa Chan.“Kikosi changu kimejiandaa kushinda na mechi ya kesho (leo) nawapa zaidi nafasi vijana ili kupata mwanga wa kikosi ambacho kitashiriki kwenye michuano ya Chan,” alisema.Taifa Stars na Burundi zinakutana zikiwa na wachezaji baadhi ambao wanafahamiana kwa vile wanacheza wote kwenye Ligi Kuu Bara.Mmoja wa wachezaji hao ni mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo ambaye leo atawaongoza wenzake kwenye mechi hiyo.Hata hivyo timu hizo leo zinakutana zikiwa na vikosi tofauti za vile vilivyozoeleka kwa miaka miwili iliyopita kutokana na makocha wa timu zote kufanya mabadiliko.Stars ya sasa chini ya Kocha Mayanga amekuja na falsafa yake akijaribu kuwapa nafasi zaidi vijana kuliko mwanzo ambapo sura nyingi zilikuwa zikijirudia kwenye timu hiyo.Stars na Burundi ziliwahi kukutana chini ya Kocha Mart Nooij ambaye baadaye alitimuliwa na hakuna mchezo hata mmoja iliyoshinda mwaka juzi.Mchezo wa kwanza ilikuwa Aprili 2014 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kama sehemu ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Burundi ilishinda mabao 3-0.Pia, mwaka huo walirudiana mjini Bujumbura ambapo Stars ilifungwa mabao 2-0. Burundi sio timu ya kubeza, ina wachezaji wengi vijana wazuri na wenye uwezo akiwemo Mavugo ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akifanya vizuri.Pamoja na hilo, katika viwango vya soka vilivyotolewa na Fifa mwezi huu, Burundi ni ya 138 na Tanzania ikishika nafasi ya 158. Kocha wa Burundi, Alain Niyungeko alisema wamejipanga vizuri na wanatarajia kupata ushindi.“Tunajua Tanzania ina wachezaji wazuri, tunamjua Samatta (Mbwana anayecheza soka ya kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji) pia ni mchezaji mzuri lakini lengo letu ni kupambana na kupata ushindi ,”alisema kocha huyo.
MICHEZO
LOS ANGELS, MAREKANI MWANAMITINDO  wa Marekani, Kim Kardashian, ameendelea kuwa sehemu ya mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii baada ya kumkingia kifua mumewe Kanye West, kuhusu ahadi ya kufoji ya fedha katika taasisi ya kifedha ya Nonda House. Mbali ya kuwa na uwezo wa kusimama na kumtetea mumewe pia Kim amekuwa na upendo wa dhati kwa familia ya Kardashian. Kim jana aliposti tena katika ukurasa wake wa Twitter akimvaa rapa Rhymefest ambaye alionyesha kuingia mambo yaliyokuwa yakiendelea dhidi ya mumewe yalitokana na taasisi ya kifedha ya Donda House ambayo ilikanusha Kanye kuahidi kuweka fedha kwa ajili ya Kim. “Huna haki ya kuzungumza kwanza umefukuzwa studio kwa kuvaa Yeezy ya kufoji,” aliposti Kim katika ukurasa wake wa Twitter.
BURUDANI
MADRID, HISPANIA MASHABIKI wa klabu ya Real Madrid, wamekuja juu kwenye mitandao ya kijamii huku wakitaka mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, afungiwe michezo kadhaa kutokana na kumshika bega mwamuzi. Staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, Jumanne wiki hii aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa huku akifunga mabao mawili peke yake. Kwenye mchezo huo, Messi alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 54, baada ya kumshawishi mwamuzi wa mchezo huo atoe kadi ya njano kutokana na kuchezewa vibaya, hata hivyo mbali na kumshawishi mwamuzi atoe kadi, alionekana akimshika bega mwamuzi kumlazimisha atoe kadi. Hata hivyo, mwamuzi aliamua kumwonesha Messi kadi ya njano badala ya mchezaji ambaye alimchezea vibaya mshambuliaji huyo. Katika sheria za soka nchini Hispania, zinadai kuwa mchezaji akimfuata mwamuzi na kumsukuma au kumshika kwa lengo la kumshawishi jambo lolote uwanjani, anastahili kufungiwa michezo minne hadi 12. Mwezi uliopita mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, alifungiwa michezo mitano kutokana na kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo wa Kombe la Supercopa, huku Madrid ikishinda mabao 3-1. Mchezaji huyo awali alioneshwa kadi ya njano kutokana na kushangilia huku akiwa amevua jezi na baadaye alioneshwa kadi ya pili ya njano na nyekundu baada ya kujiangusha kwenye eneo la 18 akimshawishi mwamuzi Ricardo de Burgos Bengoetxea, ampe penalti. Ronaldo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu, aliamua kumsukuma mwamuzi huyo jambo ambalo lilimpelekea kufungiwa michezo mitano kutokana na sheria ya soka nchini humo. Mbali na mchezaji huyo kufungiwa michezo mitano, lakini alitakiwa kulipa faini ya Euro 800 ni sawa na Sh 2,116,750 za Kitanzania. Kutokana na hali hiyo, mashabiki wa Real Madrid, wamedai kitendo alichokifanya mshambuliaji wa Barcelona, Messi ni sawa na Ronaldo, hivyo anatakiwa kuchukuliwa hatua. Ronaldo juzi alirudi dimbani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuisaidia timu yake kushinda mabao 3-0 dhidi ya Apoel Nicosia, huku mchezaji huyo akipachika mabao mawili peke yake na bao lingine likipigwa na Sergio Ramos. Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa juzi ni pamoja na Liverpool wakitoka sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla, Porto wakipigwa 3-1 dhidi ya Besiktas, Tottenham ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Dortmund, wakati huo Maribor ikitoka sare 1-1 dhidi ya Spartak Moskva na RB Leipzig wakitoka 1-1 dhidi ya Monaco.
MICHEZO
Akaunti ya Akiba ya Malengo ni akaunti za akiba ambazo zimeanzishwa rasmi kusaidia wateja kufikia malengo yao ndani ya kipindi maalumu.Kampeni itadumu kwa muda wa miezi mitatu kutoka Februari 4 mpaka Aprili 30 mwaka huu.Katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya kampeni, wateja wanaoweka fedha watafaidika na kiwango cha kuvutia cha riba na kuwa katika nafasi kubwa ya kushinda gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser Prado .Lengo la kampeni ni kujenga uelewa wa umuhimu wa kuhifadhi kwa ajili ya baadaye ili kufikia malengo, alisema Musa Jallow, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja za kibenki na kuongeza kuwa kitu kinachotakiwa ili kuwa katika nafasi ya kushinda ni kufungua akaunti ya Mango ya akiba kwenye tawi lolote la NBC nchini kote.
UCHUMI
DAKAR, SEGENAL           |            KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani nchini Senegal na Meya wa zamani wa Jiji la Dakar, Khalifa Sall ambaye yuko gerezani kwa sasa, ametangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2019. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AfricaNews, Sall ametangaza nia ya kuwania urais kwa njia ya barua licha kutumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya kujipatia dola milioni 3.24 kwa njia za udanganyifu na kughushi nyaraka, tuhuma ambazo alikanusha na sasa anakamilisha mchakato wa kukata rufaa. “Ni kweli, mimi ni mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Februari 24, mwaka 2019,” amesema Sall katika barua yake. Haijafahamika kama Sall ambaye amekuwa mwanasiasa nyota anayemchachafya Rais wa sasa wa Senegal, Macky Sall, ataendelea na mpango wa kugombea iwapo rufaa yake itagonga mwamba mahakamani hali itakayomlazimu kubaki gerezani. Rais Sall na Khalifa Sall hawana undugu wowote licha ya kufanana majina ya ukoo. Hata hivyo, inadaiwa Sall anao wafuasi watiifu, hususan katika Jiji la Dakar, huku wengi wakiamini kuwa kukamatwa kwake na kufungwa kulichochewa na mbio za urais wa mwakani.  Serikali imekanusha kuhusika na tuhuma hizo. Kutokana na hali hiyo heshima ya Senegal katika demokrasia ipo majaribuni iwapo Khalifa Sall ataendelea kuzuiliwa gerezani hadi wakati wa uchaguzi mkuu. Licha ya sifa kubwa ya uchaguzi wa kidemokrasia mwaka 2012, Senegal imedaiwa kuingia kwenye mtikisiko wa kisiasa baada ya kukumbwa na matatizo makubwa ya ufisadi na kukosa uvumilivu wa kisiasa. Karim Wade ambaye ni mtoto wa zamani wa Rais Abdoulaye Wade, anatumikia kifungo cha miaka mitatu jela kutokana na makosa ya ufisadi, ikiwemo kuficha fedha ughaibuni kupitia kampuni mbalimbali zilizosajiliwa katika visiwa vya Virgin, nchini Uingereza pamoja na kashfa ya Panama papers.
KIMATAIFA
Upendo Mosha -Siha ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, amewaonya wachungaji, watumishi na waumini wa kanisa hilo wasijifanye mabwana, na wasitake kujipatia fedha kwa njia za aibu. Aliyasema hayo juzi, wakati wa ibada maalumu ya kumstaafisha mchungaji wa kanisa hilo na kuwaingiza kazini baadhi ya wachungaji katika Usharika wa Oshara, Jimbo la Siha, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. Alisema kujipatia fedha kwa njia za aibu ni jambo ambalo halipendezi na ni chukizo mbele za Mungu. NENO LA SHUKRANI Akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa kuliongoza tena kanisa hilo, Dk. Shoo alisema; “imempendeza Mungu kuliongoza kanisa hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne, na kwamba uchaguzi ulifanikiwa kutokana na maombi na si kwa nguvu zake mwenyewe. “Nimshukuru mwenyezi Mungu kwakuwa yeye ametutendea mambo makuu sana… Mungu kwetu ni kimbilio la nguvu, tena msaada utakaoonekana wakati wa mateso, hakika tumeona mkono wake Mungu na uweza wake. “Mungu alisema hata kama maadui wakijiinua namna gani yeye aliahidi atatuokoa… napenda kuwashukuru wana KKKT wote kwa maombi yenu na ushirikiano wenu na mshikamano wenu, maana hata katika hili tulilolisikia mkutano mkuu, mlinionyesha mshikamano… Mungu awabariki.” Dk. Shoo aliwataka viongozi wa dini na Wakristo nchini kusimama pamoja na kuzingatia wito wa Mungu ili kuendelea kuwa kielelezo duniani. “Tuelewe wito huu kwa unyenyekevu, kila mmoja ameitwa kwa nafasi yake… kipekee sisi ambao tumepewa dhamana ya kulichunga kundi la Bwana, tunapaswa kulichunga kwa uaminifu wote kwa bidii na kwa moyo wa upendo na unyenyekevu,” alisema. WAKATI MWAFAKA Mchungaji mstaafu wa kanisa hilo, Jeremiah Kileo, alisema ni wakati mwafaka wa waumini kusimama imara na kuliombea kanisa hatua ambayo itasaidia kuepusha changamoto mbalimbali zinazohusu shetani. “Kwa umoja wetu tunapaswa kuliombea kanisa ili tusiyumbishwe na yule adui muovu shetani. Pia tusimamie imani zetu bila kuyumbishwa,” alisema. Dk. Shoo alitangazwa mshindi usiku wa kuamkia juzi dhidi ya wagombea wengine katika uchaguzi huo na ataliongoza kanisa kwa kipindi cha miaka minne. Alipata kura 144, huku mshindani wake wa karibu, Dk. Abednego Keshomshahara akipata kura 74 kati ya 218 zilizopigwa mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wao wawili.
KITAIFA