text
stringlengths 5
25.1k
⌀ | label
int64 0
5
|
---|---|
Na MAREGESI PAUL – DODOMA BOMOABOMOA inayoendelea nchini kwa wananchi waliojenga katika maeneo ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), imewakera baadhi ya wabunge. Wabunge hao walionyesha hali hiyo bungeni jana wakati walipokuwa wakichangia Muswada wa Sheria ya Reli ya Mwaka 2017, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. Katika mchango wake, Mbunge wa Kaliua, Magdallena Sakaya (CUF), alionyesha kutoridhishwa na bomoabomoa hiyo kwa kuwa baadhi ya wanaovunjiwa majengo, walianza kuyamiliki miaka mingi iliyopita. Kwa upande wake, Mbunge wa Moshi Mjini, Jafary Michael (Chadema), pamoja na kulalamikia bomoabomoa hiyo, alitaka viongozi waliosababisha wananchi wakajenga katika maeneo ya reli, kuchukuliwa hatua. “Hii bomoabomoa inaumiza wananchi na kwa kuwa inaonekana baadhi ya waliojenga katika maeneo hayo walikuwa na vibali vya Serikali, basi waliotoa vibali hivyo wachukuliwe hatua kwani wamesababisha wananchi wapate hasara bila sababu,” alisema Michael. Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM), alisema kuna haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuwafidia waliovunjiwa nyumba zao kwa kuwa baadhi waliuziwa viwanja na Serikali. Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alilalamikia bomoabomoa hiyo na kusema mkoani Tabora kaya zaidi ya 500 zitavunjiwa nyumba, akiwamo kikongwe mwenye miaka zaidi ya 70 ambaye alianza kumiliki eneo lake miaka mingi iliyopita. Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), alisema nyumba zaidi ya 3,244 zitabomolewa na kwamba kuna haja watakaobomolewa, kulipwa fidia ili wakajenge makazi mapya. Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM), alitaka Serikali iimarishe ulinzi wa reli ili kudhibiti majangiri wanaong’oa mataluma kwa lengo la kupora mali za abiria. | 1 |
Na RAMADHAN LIBENANGA-MOROGORO
WAFUGAJI wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, wamesema wamekuwa wakitumia fedha nyingi kununua mihtasari ya vikao vya vijiji ili kuzionyesha mamlaka mbalimbali jinsi walivyoruhusiwa kumiliki ardhi waliyonayo.
Hayo yalielezwa jana na mchungaji Joseph Sepuke, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibaoni wilayani Mvomero.
“Wamasai wanapata mihtasari ya kijiji kwa gharama kubwa na viongozi hawa hawa wa vijiji ndio wanaowauzia hii mihtasari ili waweze kumilikishwa maeneo.
“Kwa hiyo, tunaomba gharama za mihtasari hiyo zipunguzwe ili tuweze kuzipata kwa urahisi zaidi,” alisema Sepuke.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kibaoni, Fabian Beatus, alisema kijiji chao kimegundua kuna baadhi ya wananchi walioghushi mihtasari ya vijiji na kufanikiwa kupata ardhi.
“Kuna watu wameghushi mihtasari kwa sababu sharti kuu linalomwezesha mwananchi kumiliki ardhi ni kuwa na muhtasari unaoonyesha vikao halali vya kijiji vilikaa kumjadilli na kuridhia kumpa eneo,” alisema.
Akizungumza katika mkutano huo, mfugaji mwingine wa jamii ya kimasai, Songambili Mfaume, aliwatupia lawama baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kwa kusema wamekuwa wakimfuata awape milioni mbili ili wampe muhtasari aweze kumilikishwa eneo lake.
Hata hivyo, tuhuma hizo zilikanushwa na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Stephano Udoba ambaye alisema wamekuwa wakifuata taratibu wakati wa kuwamilikisha wananchi ardhi.
Akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na Mradi wa Kuendeleza Kilimo katika Safu za Milima ya Uluguru (UMADEP) unaotekelezwa chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Ofisa Miradi wa UMADEP, Pesa Kusaga, alisema SUA inashirikiana na Serikali kuhakikisha migogoro ya ardhi inamalizika mkoani Morogoro.
| 1 |
Na Said Ameir, MAELEZO KUWAPATIA wananchi dawa zenye viwango bora, salama na ufanisi ni moja kati ya malengo makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha afya za watu. Pamoja na lengo hilo, utekelezaji wake mbali ya kukabiliwa na chagamoto za kibajeti, changamoto nyingine kubwa ni upungufu wa wataalamu wa ukaguzi na kudhibiti ubora na usalama wa dawa. Kwa mujibu wa takwimu za miaka ya hivi karibuni, soko la dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linategemea bidhaa hiyo kutoka nje kwa kati ya asilimia 70 na 75 hivyo uzalishaji wa ndani ni kati ya asilimia 30 na 25. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki anasema Tanzania huagiza nje ya nchi asilimia 80 ya mahitaji yake ya dawa. Nchi nyingine zinazoagiza dawa nje ya nchi ni Rwanda asilimia 90, Uganda asilimia 90, Burundi asilimia 100, Zanzibar asilimia 100 na Sudan Kusini asilimia 100. Katika nchi wanachama wa Jumuiya hii, ni Kenya pekee ambayo imepiga hatua katika utengenezaji dawa ambapo takwimu zinaonesha kuwa inatengeneza karibu asilimia 25 ya mahitaji ya soko la nchi wanachama. Mbali ya Jumuiya kuwa na mpango maalumu wa muda mrefu kuwezesha nchi wanachama kutengeneza zaidi dawa kuliko kutegemea watengenezaji wa nchi za nje, lakini pia imeweka mkazo katika kuwapatia uwezo na ujuzi wa udhibiti na ukaguzi wa viwango vya ubora na usalama wa dawa wataalamu wa nchi wanachama. Mkakati wa Jumuiya katika kujenga uwezo wa wataalamu wa nchi wanachama umejikita katika kuhakikisha dawa zinazotengenezwa katika nchi wanachama na zile zinazoingizwa toka nchi za nje zinakidhi viwango vya ubora unaotakiwa. Nchi hizo zimekubaliana kuwianisha viwango vya dawa ili dawa zinazotengenezwa na kuingizwa katika Jumuiya ziwe na viwango vinavyofanana ubora, usalama na ufanisi. Hivi karibuni, Jumuiya hiyo kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shule ya Famasi ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi za Afya Muhimbili (MUHAS) waliendesha mafunzo maalumu kwa wataalamu wa udhibiti na ukaguzi wa dawa kutoka nchi wanachama. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki, kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili yaliendeshwa kwa pamoja na wataalamu wa TFDA, MUHAS, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na mtaalamu mbobefu kutoka Bodi ya Dawa ya Uholanzi. Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2014 na kuanza shughuli zake mwaka 2015 na kinaendeshwa kwa pamoja kati Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA na Shule ya Phamasi ya Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili. Mafunzo hayo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa kituo hicho ambapo mafunzo ya kwanza yalifanyika mara tu kilipoanza kufanya kazi mwaka 2015. Ni vyema kubainisha kuwa katika programu ya uwianishaji wa dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA ndio taasisi kiongozi ya uratibu na usajili dawa. Hii inadhihirisha uwezo mkubwa wa kitaalamu na kitaasisi ilionao TFDA katika masuala hayo katika nchi wanachama wa jumuiya. Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo anaeleza kuwa moja ya majukumu ya mamlaka za udhibiti wa dawa katika nchi wanachama ni kufanya tathmini ya dawa kabla hazijaingia katika soko kuhakikisha kuwa zinakidhi viwango vya ubora, usalama na ufanisi vilivyokubalika kisheria. “Mafunzo haya ni sehemu ya uwezeshaji wa utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka za Udhibiti na Usimamizi wa Dawa katika nchi zetu, pia ni sehemu ya mpango wa uwianishaji wa dawa wa jumuiya ili kujenga uwezo kwenye ngazi ya nchi za ukanda huu kwa kufanya tathmini ya maombi ya usajili wa bidhaa za dawa,” anafafanua Sillo. Akizungumzia tathmini ya mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo Mhadhiri Mwandamizi na Meneja wa Maabara ya Utafiti na Maendeleo, Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, Profesa Eliangiringa Kaale anasema yana umuhimu mkubwa katika kulinda afya ya wananchi wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Kama takwimu za uingizaji dawa katika nchi wanachama zinavyoonesha, ni vyema kueleza kuwa kiwango hicho kikubwa cha dawa kinachoagizwa kutoka nje kinalazimu nchi wanachama kushirikiana kwa karibu kwa sheria, kanuni na viwango vinavyofanana ili ukanda wote uwe salama katika suala la dawa. Kama inavyoeleweka biashara ya dawa na vifaa tiba ni moja kati ya biashara inayonyemelewa na kushamiri kwa udanganyifu, hivyo ushirikiano wa karibu ni kitu muhimu katika udhibiti. Ukaguzi wa mipakani na ukaguzi wa mara kwa mara kwenye soko ndio utakaowalinda wananchi. Zaidi, uwezo mkubwa wa kitaalamu, rasilimali na kimiundombinu ndio silaha madhubuti kukabiliana na udanganyifu huo ambao Jumiya imekuwa ikichukua hatua kuimarisha uwezo wa wananchama wake wa usimamizi, ukaguzi na kudhibiti. | 5 |
MWILI wa binadamu na viumbe wengine kama vile wanyama, una mfumo unaosaidia kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali. Mfumo huu wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kwa kitaalamu huitwa ‘Immune system.’ Pamoja na mwili kuwa na mfumo wa kujilinda dhidi ya magonjwa, kuna nyakati ambazo kinga hii ya mwili inakuwa haijakomaa mfano kwa watoto. Pia kutokana na tafiti mbalimbali za kitabibu juu ya afya na uwezo wa mwili kujilinda, imesababisha kuwapo umuhimu wa kuimarisha kinga ya mwili kupitia matumizi ya chembe chembe ambazo hujulikana kwa jina la chanjo au kwa kitaalamu ‘Vaccine.’ Chanjo au ‘Vaccine’ ni chembechembe ambazo huandaliwa kupitia viumbe au bakteria wasababishao magonjwa (microbes), au chembechebe zinazoandaliwa kwa kutengenezwa (synthetic) ili kutumika katika kuuandaa mwili au kuamsha kinga ya mwili iweze kupambana na ugonjwa au magonjwa mbalimbali. Kutokana na aina ya matumizi, chanjo zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Makundi hayo ni chanjo itokanayo na bakteria au virus ambao wameondolewa uwezo wao wa kusababisha ugonjwa (An attenuated vaccine) na kundi lingine ni chanjo ambayo hutokana na bakteria au virus ambao tayari wameuliwa/hawana uhai (Inactivated vaccines). Miongoni wa chanjo ambazo zimekuwa zikitolewa kwa binadamu ni pamoja na chanzo dhidi ya magonjwa kama vile surua, tetenasi, polio, homa ya ini (Hepatitis A and B) pamoja na chanjo ambayo imezinduliwa hivi karibuni nchini, Tanzania, chanjo ya kumkinga mwanamke dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi (Human papilloma virus (HPV) vaccine). Chanjo imekuwa na umuhimu mkubwa katika mnyororo wa tiba za magonjwa mbalimbali. Baada ya kinga ya mwili kuamshwa na kuimarishwa, athari za magonjwa mbalimbali kwa binadamu zimekuwa zikipungua, mfano ulemavu (kupooza kwa viungo), magonjwa ya ini na vifo vimepungua. Sababu kubwa ya matumizi ya chanjo au utoaji wa chanjo ni kufanya mwili uweze kuzalisha kinga dhidi ya ugonjwa husika (Specific antibodies to each individual disease). Je, chanjo hutolewa kwa kundi lipi la watu? Kama ambavyo nimetangulia kwa kufafanua maana ya chanjo, kuwa ni chembechembe ambazo zinatokana na aina ya viumbe au bakteria wanaosababisha magonjwa, kuna tahadhari katika makundi ya watu ambao watakuwa na sifa ya kupatiwa chanjo husika. Kwa mtu ambaye tayari analo tatizo husika, mfano mtu mwenye tatizo la homa ya ini (Hepatitis A au B), hatopatiwa chanjo ya ugonjwa huo, kadhalika na magonjwa mengine. Si salama kumpatia mtu chanjo wakati tayari analo tatizo au ugonjwa husika. Kumpatia mtu chanjo huku akiwa na tatizo au ugonjwa husika, kunaweza kusababisha tatizo likawa kubwa zaidi hatimaye kuhatarisha afya na uhai wa mgonjwa. Pia, chanjo zimekuwa zikitolewa kulingana na umri wa mlengwa/mteja. Baada ya chanjo kutolewa, kwa baadhi ya nyakati pia zimekuwa zikisababisha maudhi madogo madogo kwa mtumiaji. Mfano kwa watoto wadogo zimekuwa zikisababisha joto kupanda, usumbufu katika kusikia, maumivu sehemu iliyo chanjwa mfano sehemu ya mkono au paja. Maudhi haya madogo madogo siku zote yamekuwa si lengo kuu la chanjo, bali hujitokeza kwa baadhi ya watu. Matibabu ya maudhi haya yanategemeana na aina ya usumbufu ambao umejitokeza kwa mtu, si matibabu ya jumla kwa watu wote. Miongoni mwa matibabu au msaada wa kitabibu ambao umekuwa ukitolewa kwa watu ambao wamepatwa na matatizo baada ya kupatiwa chanjo ni pamoja na matumizi ya dawa za kushusha joto au homa, dawa za kuondoa degedege (convulsions) pamoja na matibabu mengine kutegemeana na namna ambavyo yamejitokeza. Ili kuepukana na magonjwa mbalimbali pamoja na athari zake kiafya na kijamii, ni vyema walengwa wote wakapatiwa chanjo kulingana na miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya. | 5 |
Na WAANDISHI WETU – ZANZIBAR/DAR ES SALAAM
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema iwapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaikatia umeme Zanzibar kutokana na deni wanalodaiwa, wataweza kurudi katika matumizi ya asili ambayo ni kutumia vibatari kupata mwanga.
Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amaan Abeid Karume, akitokea nchini Indonesia katika mkutano maalumu aliomuwakilisha Rais Dk. John Magufuli.
Kauli hiyo imekuja wakati Tanesco jana ikiwa imetoa siku 14 kwa wadaiwa wote sugu, ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), linalodaiwa Sh bilioni 127, kulipa deni hilo ndani ya muda huo kabla ya kukatiwa umeme.
Wiki iliyopita, Rais Magufuli aliiagiza Tanesco kukata umeme kwa wadaiwa wote sugu, akisema hata kama Ikulu ya Magogoni inadaiwa, nayo pia ikatiwe nishati hiyo.
Jana mara baada ya Dk. Shein kuwasili, alizungumzia mafanikio ya safari yake ikiwa ni pamoja na mipango ya viwanda, kauli iliyofanya waandishi kuuliza viwanda hivyo vitaendeshwa vipi ilihali Tanesco imetangaza kuikatia umeme Zanzibar.
Kutokana na swali hilo alisema: “Naamini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Serikali ya kiungwana, inayojali watu wake, hivyo haiwezi kufanya hivyo kwenye suala hili la kuzima umeme visiwani Zanzibar na iwapo ikitokea umezimwa, Zanzibar watakuwa tayari kurudi kwenye matumizi ya vibatari.”
Alisema akiwa safarini alisoma magazeti mawili yaliyoandika juu ya Zanzibar kukatiwa umeme, lakini haamini kama taarifa hizo zina ukweli, huenda waandishi walinukuu vibaya vyanzo vya taarifa hiyo.
“Siamini kama umeme wanaweza kuzima, lakini natungojee wazime tuone,” alisema Dk. Shein.
Alisema atashangazwa iwapo umeme utakatwa, ikizingatiwa mahusiano mazuri yaliyopo baina ya pande mbili hizi zinazounda Tanzania.
Alieleza kwa kipindi cha miaka mingi, ikiwa ni pamoja na wakati yeye akiwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Zanzibar imekuwa ikidaiwa na Tanesco na wamekuwa wakilipa kwa utaratibu maalumu.
Alisema suala la kudaiwa si geni na lipo kwa muda mrefu na wao kama Serikali hawajawahi kukataa kulipa, hivyo ni utaratibu maalumu ambao unapaswa kutumika ili kuondoa hali hiyo.
SIKU 14
Wadaiwa sugu wa Tanesco, wakiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), wizara na taasisi za Serikali, wamepewa siku 14 kulipa madeni yao kabla kukatiwa huduma.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana.
Katika mkutano huo uliohusisha vyombo vichache vya habari – televisheni moja binafsi, moja ya Serikali, magazeti ya Serikali na ya kampuni moja binafsi, Dk. Mwinuka alisema hadi sasa shirika hilo linadai zaidi ya Sh bilioni 275 kwa Zeco, Wizara, Taasisi za Serikali na makampuni ya watu binafsi.
Dk. Mwinuka alisema jambo hilo limechangia kurudisha nyuma utendaji wa shirika hilo katika kusambaza huduma ya umeme nchini.
Alisema kutokana na hali hiyo, baada ya muda waliotoa kwisha bila deni hilo kulipwa, Tanesco itachukua uamuzi mgumu wa kuwakatia umeme wadaiwa hao.
Katika deni hilo, Zeco inadaiwa Sh bilioni 127, mashirika ya serikali, wizara na taasisi Sh bilioni 52, huku kampuni binafsi na wateja wadogo wakidaiwa Sh bilioni 94.
“Tumetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu wote wa Tanesco, wakiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) ambao tunawadai Sh bilioni 127 hadi Januari mwaka huu, wizara na taasisi za Serikali ambazo na zenyewe tunazidai, wanapaswa kulipa deni lao ili kuepusha usumbufu wa kukatiwa umeme,” alisema Dk. Mwinuka.
Alisema hadi sasa wameshatoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa hao ili waweze kulipa madeni yao na watakaoshindwa kufanya hivyo, watakuwa wamekaidi notisi hiyo.
Dk. Mwinuka alisema malimbikizo ya madeni hayo yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya shirika hilo.
Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa uendeshaji wa shughuli mbalimbali, ikiwamo matengenezo ya miundombinu na utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Dk. Mwinuka alisema mkakati wao ni kuhakikisha wanakusanya madeni hayo na fedha zitakazopatikana zisaidie kufanya shughuli za usambazaji umeme ili huduma hiyo iwafikie watu wengi zaidi.
Alisema upatikanaji wa umeme utasaidia kuchochea maendeleo na kusaidia ukuaji wa sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme.
Taarifa hii imeandaliwa na MUHAMMED KHAMIS (UOI – ZANZIBAR) na PATRICIA KIMELEMETA (DAR ES SALAAM) | 1 |
Alitoa pongezi hizo alipozindua rasmi hatua ya benki hiyo, Mwalimu Commercial Bank (MCB) kujiorodhesha DSE mwishoni mwa wiki Dar es Salaam tayari kwa kuanza kuuza hisa zake. “Soko la hisa ni njia mpya ya kuwakwamua walimu kiuchumi na kuzidi kujiendeleza kimaisha,” alisema Majaliwa.Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuendeleza elimu ikiwamo kuboresha maslahi ya watendaji wake na kwamba hatua iliyofikiwa na CWT ni chachu ya kufikia malengo hayo ya maendeleo.“Chama kimepiga hatua kubwa ya kuanzisha benki kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali, wanachama kuhamasika kuchangia fedha kwa kununua hisa za benki na hatimaye leo kujiunga na soko hili,” alisema Waziri Mkuu.Pia aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko na Mitaji kwa kutoa mwongozo hadi benki ya chama hicho kufikia hatua ya kuuza hisa kwa walimu Machi mwaka huu.“Mimi ni mwalimu na kwa kweli walimu tupo wengi nchini, majengo ya chama cha walimu yaliyopo mikoani pia yatumike katika kufungua matawi ya benki ili kuwafikia walimu wote na wadau mbalimbali,” alisema Majaliwa.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Walimu, Herman Kessy alisema mafanikio ya benki yaliyopatikana yanatokana na wanahisa wakiwemo walimu wote wa Tanzania, Mfuko wa pensheni wa PSPF, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wanahisa wengine wote wa benki.“Tumekusanya mtaji wa shilingi bilioni 31 na matarajio yalikuwa kupata bilioni 25,” alisema Kessy na kufafanua kuwa walikusanya zaidi ya matarajio yaliyokuwepo kupitia wanahisa 235,494.Katibu Mkuu wa CWT, Yahaya Msulwa alisema maandalizi ya awali ya kuanzisha benki hiyo yamefikia hatua nzuri kwani wamepata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania na wanatarajia itafunguliwa rasmi Mei mwakani. | 0 |
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM TEKLA (si jina lake halisi), ni mwalimu katika shule moja ya msingi jijini Dar es Salaam. Katika harakati za kutafuta maisha amekumbana na changamoto nyingi ambazo kama si mama yake kupambana huenda leo angekuwa na maisha mabaya zaidi. Tekla anasema alikuwa akiishi na mama na baba yake wa kambo na kwamba mara nyingi mama yake alikuwa akiingia kazini usiku na kurudi asubuhi. “Wakati nikiwa kidato cha tatu, siku moja wakati nimelala baba alinifuata na kunitongoza. Nilikataa na kukimbia kwenda kukaa nje hadi asubuhi alipoondoka kwenda kazini ndio nikarudi ndani kujiandaa na kwenda shule. “Tulikuwa tumepanga vyumba viwili hivyo mimi nilikuwa nalala sebuleni halafu wazazi wangu chumbani, siku nyingine baba akaja tena akiwa ameshika panga. Niliogopa sana nilijua ataniua hivyo nikajikuta nimefanya naye mapenzi,” anasema Tekla. Anasema baba yake huyo aliendelea kumfanyia vitendo hivyo huku akimpa vitisho na kwamba hakuwahi kumwambia mama yake. “Wakati naendelea na masomo nikashtukia nimepata ujauzito, sikumwambia mtu niliendelea kwenda shule hadi mimba ilipofikisha miezi saba. Niliongeza kipimo cha sketi nikawa navaa na sweta kila siku ili kuficha tumbo,” anasema. Anasema wakati mimba ilipofikisha umri wa miezi saba ilikuwa ni Desemba na baada ya kufunga shule alimuomba mama yake amruhusu asafiri kwa ajili ya likizo. Anasema alikwenda kwa bibi yake mkoani Dodoma na alipofika aliamua kumweleza ukweli bibi yake huyo. “Mama alitaarifiwa na kuja Dodoma, sikuwahi kusema kama baba ndiye aliyenipa ujauzito ule nilikuwa naogopa sana. Nilikaa Dodoma hadi Februari nilipojifungua…nilijifungua mtoto wa kiume lakini alifariki dunia baada ya siku mbili,” anasema. Mwalimu huyo anasema alipumzika kwa bibi yake na baada ya likizo ya Aprili aliamua kurudi shule lakini akamuomba mama yake asomee huko huko mkoani Dodoma ambapo aliamua kurudia kidato cha tatu. “Niliumia sana kwa sababu mama yangu ndiye alikuwa anahangaika kwa kila kitu na kunitafutia ada halafu baba akaja kunibaka…sitaki kukumbuka, namshukuru sana mama yangu hakunifukuza wala kunichukulia hatua yoyote ile na hata nilipotaka kurudi tena shule alikubali. “Nilisoma kwa bidii na nilipomaliza kidato cha nne nilifaulu vizuri kwa kupata daraja la nne na alama 27, nilienda kusomea ualimu na baada ya kumaliza nikaajiriwa kuja kufundisha hapa Dar es Salaam. Kisa cha Tekla ni mfano wa matukio mengi yanayowakumba wasichana nchini, wako wanaobakwa bila kutaka na kulazimika kuacha shule kutokana na sheria kutoruhusu kuendelea na masomo. Kitendo cha ukatili kama alichofanyiwa Tekla kinamnyima fursa ya kupata haki zake kama vile ya elimu. Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto uliozinduliwa Jumanne wiki hiii, jijini Dar es Salaam unasisitiza juu ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kimwili kwa wanawake na watoto kwani vinaleta kikwazo katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2015. Tafiti zinaonyesha sababu nyingi zilizochangia wasichana kupata mimba na kukatisha masomo yao zinahusishwa pia na vitendo vya ukatili. SABABU ZA KUPATA MIMBA Faustin Mroso ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kwamatuku iliyoko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, anasema wazazi wengi pia wamekosa mwamko wa elimu na hata shule ikipeleka taarifa za kutooneka kwa mwanafunzi wazazi huwa hawatoi ushirikiano. Pia wazazi wanalaumiwa kwa kushindwa kuwatimizia watoto wa kike mahitaji yao ya msingi ya kimasomo. Mmoja wa wanafunzi katika shule moja ya sekondari mkoani Dar es Salaam, anasema amejikuta akianza uhusiano wa kimapenzi ili kupata fedha za kujikimu. “Mama yangu ni mfanyabiashara ndogondogo na baba yangu ni mtumishi wa umma, kila mwezi baba hunipa Sh 50,000 kwa ajili ya nauli na mahitaji mengine ya shule. Lakini baba akishanipa mama hunifuata na kuniomba zile fedha ili aongezee katika mtaji wake. “Huwa naingiwa na huruma na kumpa kwa jinsi ninavyoona anavyohangaika kwa sababu aliwahi kuniambia baba huwa hatoi fedha za matumizi ya nyumbani, anachojua ni kulipa ada na mahitaji mengine ya shuleni,” anasema mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto sita wa familia hiyo. Anasema alilazimika kuanza uhusiano wa kimapenzi na kwamba mwanamume aliyekuwa naye alikuwa akimpa Sh 3,000 kila alipokuwa akikutana naye kimwili. Naye Mwalimu…ansema kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kumechangia wanafunzi wengi kushindwa kupokea mabadiliko ya makuzi kwa umakini. HALI ILIVYO Kila mwaka zaidi ya wasichana 8,000 huacha shule kutokana na mimba. Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi za mwaka 2010 zinaonesha katika shule za sekondari wanafunzi waliokatisha masomo walikuwa 66,069. Katika shule za msingi waliokatisha masomo kwa sababu ya utoro (baadhi ni watoro kwa sababu ya mimba) walikuwa wanafunzi 76,246 na waliofukuzwa kwa sababu ya mimba ni 1,056. Shule ya Sekondari Nanyamba iliyoko mkoani Mtwara ni miongoni mwa shule zilizokumbwa na tatizo hilo ambapo kwa mwaka huu wanafunzi wanane wa kidato cha pili na nne wamepata mimba. Pia katika Shule ya Sekondari ya Kwamatuku iliyoko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, wanafunzi sita wamepata mimba. Mkoani Kilimanjaro wanafunzi 238 wa shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, anasema Wilaya ya Rombo ndiyo inaongoza ambapo wanafunzi waliopata ujauzito ni zaidi ya 60. Kulingana na Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 kifungu 35 na kanuni zake za mwaka 1978 na marekebisho ya 1995 na 2002, mtoto wa kike akipata mimba ni ushahidi tosha kuwa amefanya vitendo vya ngono vilivyo kinyume na sheria za shule hivyo anafukuzwa shule. MJADALA WARUDI SHULE, WASIRUDI Kumekuwapo na malumbano ya muda mrefu kuhusu wanafunzi wanaoapata mimba kama waendelee na masomo baada ya kujifungua au la. Kumekuwa na hoja zinazopingana na kukinzana juu ya suala hilo huku nyingi zikitawaliwa na hisia, mitazamo na imani bila kuwapo na ushahidi wa kisayansi. Watoto wanaendelea kuteseka, wanapata mimba na kukatisha masomo, wanaathirika kisaikolojia, wanajikuta wakianza majukumu ya ulezi wangali bado wadogo na kubaki wajinga. Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na masuala ya elimu (Hakielimu), mwaka 2011 lilifanya utafiti juu ya suala hilo na kupendekeza njia za kufuatwa ili kufikia mwafaka wa jambo hilo. Chapisho la Hakielimu la mwaka 2011 linaonyesha hakuna ushahidi wa wazi ndani ya jamii unaoonesha kuwapo kwa faida za kuwafukuza shule wasichana waliopata mimba. Kulingana na chapisho hilo, maamuzi ya kuwafukuza shule wasichana yanawasukumia kwenye umasikini wa kudumu watoto wanaozaliwa na wasichana hao na hivyo kuendeleza duara la umaskini kwenye familia zao na taifa kwa ujumla. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Hadija Telela, anasema kuruhusiwa kwa jambo hilo kutasababisha mmomonyoko wa maadili na hivyo kushusha ubora wa elimu nchini. “Mimi naona wasirudi shule kwa sababu wakiruhusiwa vitendo vya ngono vitaongezeka na kutakuwa na upotovu mkubwa wa nidhamu,” anasema Mwalimu Telela. Naye Sheikh Khalifa Khamis anapinga hoja hiyo kwa sababu mafundisho ya dini hayaruhusu ngono kabla ya ndoa. “Dini zote haziruhusu ngono kabla ya ndoa hivyo, ukiruhusu watoto waendelee na masomo maana yake unahalalisha ngono kabla ya ndoa,” anasema Sheikh Khamis. Naye mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Zawadi Fundiyaya, anashauri watoto wanaopata mimba wakiwa shuleni wasamehewe na kuruhusiwa kuendelea na masomo kwa sababu wengi wanakuwa bado hawajapevuka kiakili. WAZIRI WA AFYA, ELIMU Waziri Ummy Mwalimu wakati anazindua Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, alipaza sauti na kutaka wanafunzi wanaopata mimba wafikiriwe kurudi kuendelea na masomo. “Tufikirie watoto wa maskini wanaopata mimba shuleni waendelee na masomo kwa sababu wa kwangu mimi na wewe tutampeleka private (shule binafsi) wataendelea na masomo. “Elimu kwa watoto wa kike ndiyo mwarobaini wa kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto,” anasema Mwalimu. Anasema wataanzisha sehemu rafiki katika shule za msingi na sekondari ili mtoto atakapofanyiwa jambo baya la ukatili aweze kupata msaada wa haraka. “Kutakuwa na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto wa kike katika kila mtaa na kijiji na pia utaanzishwa mtandao wa wanaume katika kila kata ili kulinda vitendo vya ukatili,” anasema. Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya, anasema “Suala la mwanafunzi kupata ujauzito akiwa shuleni ni jambo zito tunaliangalia kwa umakini na kipekee. Tutalifanyia kazi liweze kupata ufumbuzi, liangaliwe kwa mapana utekelezaji wake usiwe na athari kwa maeneo mengine. Pia baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo wanapendekeza ziwepo shule maalumu za ufundi stadi ambazo watapelekwa wasichana waliojifungua kuendelea na masomo na kupata ujuzi wa kimaisha. Mwalimu mlezi wa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari ya Kwamatuku, Christina Kavishe, anashauri kuwekeza kwenye elimu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwani pia kutasaidia kunapunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi. “Changamoto zingine zinazoathiri makuzi ya kimaadili kwa vijana ni kutopewa maarifa na taarifa sahihi jinsi ya kutumia miili yao bila kuathiri ndoto zao,” anasema Mwalimu Kavishe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq, anasema “Kuna mila ya kupeana jani linaloitwa Mashale na kusuluhishana, mila hii ni potofu na inawakandamiza watoto wa kike wanaopewa mimba na wale wa kiume ambao hulawitiwa. Jambo hili linasababisha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika mazingira magumu sana. Elimu inabaki kuwa kitovu cha maendeleo ya binadamu popote alipo hivyo cha msingi ni kufanya utafiti kubaini ukweli na uhalisia wa jambo hilo ili tuwe na mtazamo wa kujenga na wala si kubomoa. | 1 |
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi wakati alipokutana na Watumishi wa Halmashuri ya Mji wa Makambako, alisema mradi wa Liganga na Mchuchuma utatoa ajira zaidi ya 30,000, zikiwepo za wazawa na wageni.Aliwataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya ardhi kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.Mipango hiyo ni pamoja na kupima viwanja kuwavutia wawekezaji mbalimbali katika ujenzi wa hoteli za kisasa na halmashuri kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya maji na barabara.Dk Nchimbi alisema mpaka sasa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), limeanza mchakato wa uthamini wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia kupisha mradi huo.Aliwataka wananchi wa Makambako na Njombe kujiandaa na ujio wa wageni mbalimbali kwa kufuga kuku, ng’ombe na mifugo mingine kuuzia wageni hao ili kuongeza kipato cha familia.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako, Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa wanajiandaa kupokea wageni hao kwa kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi katika eneo la Makambako. | 0 |
MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba, wameialika Asante Kotoko ya Ghana kucheza nayo mechi ya kirafiki katika kilele cha maadhimisho ya Simba Day Agosti 8, mwaka huu.Simba hufanya tamasha hilo Agosti ya kila mwaka ambapo kabla ya kufikia kilele tarehe nane, hufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kumalizia na kucheza mechi ambapo pia hutambulisha kikosi chake pamoja na jezi watakazotumia kwa msimu mpya.Akizungumzia mechi hiyo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema wamechagua Asante Kotoko kutokana na historia yake ya kufanya vizuri ukanda wa Afrika Magharibi na michuano ya Klabu bingwa Afrika.“Hii ni timu kubwa Afrika na inatajwa kuwa klabu namba moja kwa Ghana, na namba mbili kwa Afrika katika karne ya 20 nyuma ya Al Ahly ya Misri,” alisema.Alisema timu hiyo iliwahi kucheza na Yanga mwaka 1969 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kutoka sare mechi zote mbili nyumbani na ugenini.Pia, iliwahi kuchukua mataji mawili ya Afrika mwaka 1970 na 1983 na Ligi Kuu ya Ghana mara 24, mara ya mwisho ilikuwa msimu wa mwaka 2013/2014.Kwa sasa wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Uturuki na wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki hii tayari kwa tamasha hilo.Kuhusu tamasha la wiki ya Simba, Mratibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajula alisema watatumia wiki hii kutambulisha jezi za nyumbani na ugenini keshokutwa.Amesema pia, maveterani wa klabu hiyo watawatembelea wenzao wa Yanga na kuchangia damu kwenye matawi, kutembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada na shughuli nyingine mbalimbali.Kajula amesema, baada ya mchezo siku hiyo ya tamasha kutakuwa na hafla ya chakula cha jioni itakayohudhuriwa na mashabiki, wachezaji na wadau kwa ajili ya kuwashukuru wachezaji. | 2 |
WIKI iliyopita, nilianza makala haya yanayolenga kuwahimiza Watanzania wenzangu kumsaidia Rais wetu, John Magufuli, kutekeleza ahadi yake kubwa kwa Watanzania ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati ifi kapo mwaka 2025.Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hatuna rais mwingine zaidi ya Magufuli aliyechaguliwa kidemokrasia na Watanzania na hivyo hata ambao hawakumchagua wanapaswa kumuunga mkono kwa sababu hakuna namna nyingine na siku rais atakapochaguliwa kila Mtanzania atapaswa kumuunga mkono pia.Ili kufikisha ujumbe wangu sawia, katika makala haya nimewagawa Watanzania katika makundi manne ambayo kila kundi lina nafasi muhimu sana katika kuchagiza maendeleo ya nchi yetu.Tumeshaangalia kundi la kwanza la viongozi au wasaidizi wa karibu wa Rais kuhusu mambo ambayo wanapaswa kuzingatia katika usaidizi wao huo utakaoharakisha nchi yetu kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda. Kwa muhtasari nilisema kwamba watanzania wenzetu hawa wenye mamlaka ya kuongoza na kutoa uamuzi wanapaswa kumwelewa Rais anataka nini na hataki kitu gani, kuzifahamu kwa uhakika wake sheria, sera, kanuni na miongozo mbalimbali wanayopewa, kuwa wabunifu, kuwa wacha Mungu na kadhalika na kadhalika.Leo tutaendelea na makundi mengine ambayo ni ya wanasiasa wa kambi ya upinzani, wafanyakazi walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi na watanzania wenzangu ambao hawana kazi ya kuajiriwa au kujiajiri.Nikianza na wanasiasa wa kambi ya upinzani ni muhimu kwao pia kuunga mkono mambo mazuri yanayofanywa na serikali iliyoko madarakani na kuonesha penye upungufu kama upo wakilenga kuboresha zaidi mambo kwa faida ya wananchi na siyo vinginevyo. Kinacholeta mushkeli ni hulka yao ya kupinga kila kitu, kukatishana tamaa na kuvizia makosa ya kibinadamu yanayofanywa na viongozi wetu na kuyavalia njuga badala ya kufanya ukosoaji wenye kujenga.Yaani wapinzani wetu ni kama vile wanaombea kila mara viongozi wetu wakosee kama si kuiombea nchi mabaya! Ni kweli kwamba nchi haiongozwi na malaika na kama ndivyo, huwezi kutotegemea waliopo madarakani wasifanye makosa kama binadamu, lakini kinachotakiwa ni kukosoa kwa njia yenye staha na stara.Lakini tunachoshuhudia kwa wapinzani wetu ni kutounga mkono hata mambo mengi mazuri yanayofanywa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kufua umeme (Stiegler’s Gorge) utakaoihakikishia nchi yetu umeme wa uhakika, ununuaji wa ndege ili kuboresha utalii wetu na kadhalika na kadhalika. Sijawahi kusikia hata siku moja mpinzani akipongeza yale yanayofanywa na serikali ya JPM hata yale ambayo huko nyuma walikuwa wakiyapigia kelele kama vile kupambana na ufisadi, kudhibiti rushwa, kuhimiza uwajibikaji katika sekta ya umma, kudhibiti mapato ya serikali na kudhibiti ubadhirifu.Matarajio ya wengi ni kwamba upinzani ungekuwa unaunga mkono yanayofanyika na kisha kutoa mapendekezo kwa ukijipigia debe kwamba pamoja na mazuri hayo, wenyewe ungekuwa madarakani ungefanya vizuri zaidi na kueleza njia mbadala ambazo wangetumia. Katika siku za karibuni tumemsikia kiongozi mmoja wa upinzani akiwa nje ya nchi akishambulia serikali na kuipaka matope kadri anavyoweza ili ionekane haina hata moja la maana walilofanya kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.Katika hali kama hii huwezi kusema kuna mchango wa maana unaofanywa na upinzani hata kama ni jicho mbadala (watch dog) katika kuiletea nchi maendeleo. Kundi la tatu ambalo ningependa kulielezea, kwa jinsi gani lina nafasi adhimu katika kuchangia maendeleo ya nchi yetu kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati ni la wafanyakazi wa nchi hii; walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi.Hawa ndio wazalishaji wakubwa na watoa huduma muhimu kwa Watanzania. Ni kundi ambalo linahusisha pia wakulima wa nchi hii. Jambo muhimu kabisa kufanywa na kundi hilo ni kuchapa kazi kwa bidii kwa maana ya kuwajibika ipasavyo kuanzia asubuhi hadi jioni. Walioko maofisini, hususani katika sekta ya umma, hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea na wanapaswa kumwelewa Rais anataka nini kwao kupitia falsafa ya hapa kazi tu.Kwa wale wanaojishughulisha na kazi katika sekta zisizo rasmi ili kujipatia riziki zao, mbali na kuchapa kazi kwa bidii wanao wajibu mwingine muhimu wa kulipa kodi stahiki, kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za nchi. Ni kwa kulipa kodi wataiwezesha serikali kuboresha huduma muhimu kwa wananchi na ambazo ni muhimu katika kuchagiza maendeleo ya nchi yetu.Kundi hili linapaswa kujiepusha na aina yoyote ya uhujumu uchumi au kuhujumu mipango mingine ifanywayo na serikali au kuleta upinzani dhidi ya mikakati mbalimbali inayosimamiwa na Serikali iliyopo madarakani. Kundi hili linapaswa pia kuendeleza kielimu na kiujuzi ili kuzalisha zaidi na kujiandaa kwa ajili ya Tanzania ya viwanda. Watanzania hawa walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi wanapaswa kuwa tayari kutoa taarifa zozote zinazohatarisha amani ya nchi kwa uongozi husika.Lakini pia wanapaswa kujiepusha na upinzani wowote usio wa msingi dhidi ya mikakati ya maendeleo, inayobuniwa na kusimamiwa na serikali iliyopo madarakani. Hata kama wao ni wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa vya upinzani, wasipige siasa katika masuala ya msingi ya maendeleo ya nchi yetu au kuikwaza serikali isifanikiwe katika malengo yake bali wapige siasa zenye maendeleo.Washiriki kwa kila lenye manufaa kwa nchi yao na hususani nyakati maalumu za uchaguzi ili kuchagua viongozi bora wanaowataka na siyo bora viongozi. Kundi la mwisho kwa mtazamo wangu ambalo nilipenda kulizungumzia katika makala haya ni la Watanzania wenzangu ambao hawana kazi ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Hawa ni Watanzania tegemezi.Kundi hili kwa kiasi kikubwa linahusisha wanafunzi walio katika ngazi mbalimbali kuanzia shule za msing hadi vyuo vikuu. Ni kundi pia linalohusisha walemavu wa aina mbalimbali, wazee, watoto, akina mama wasiojishughulisha zaidi ya kuwategemea waume zao na wale ambao bado wanahangaika kutafuta kazi na kadhalika. Nianze na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na wanavyuo (hususani waliokwenda vyuoni wakitokea mashuleni).Kundi hili linalo nafasi ya kumsaidia Rais kutimiza ndoto zake kwa kutimiza majukumu yao ya kujifunza kwa bidii, kwa umakini ili kuelewa kwa uhakika wanachofundishwa. Inaelezwa na wataalamu kwamba hakuna uwezekaji muhimu kwa nchi kama wa kuwekeza katika rasilimali watu ambao ni msingi mkubwa wa maendeleo ya taifa lolote. Ni katika muktadha huo serikali hii imeamua kurejesha utaratibu uliokuwepo wakati wa serikali ya awamu ya kwanza wa kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.Watanzania hawa walioko mashuleni na vyuoni sasa, ndio wanaotarajiwa kuungana na wenzao walioko makazini muda huu katika kujenga uchumi huo wa kati unaojikita katika maendeleo ya viwanda. Hivyo wanafunzi na wanavyuo, mbali na kutumia muda wao vizuri katika masomo, wanatakiwa kumsaidia Rais kwa kutii na kusikiliza maelekezo yote halali yatolewayo na viongozi wao, na kuyatekeleza kwa muda mwafaka.Kwa wale walioko kwenye taasisi za umma wanapaswa kutumia mali za shule na vyuo kwa uangalifu na kwa usahihi. Kwa kutekeleza haya na mengine mengi watakuwa wametimiza wajibu na majukumu yao vema, hivyo kwa namna moja au nyingine kumsaidia Rais kutimiza azma yake ya kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati. Kwa wale wasio na ajira ya aina yoyote nao wanayo nafasi adhimu ya kutekeleza majukumu na wajibu wao mbalimbali katika sehemu zao wanamoishi. Kwanza kwa wale wenye uwezo wa kufanya kazi watafute kazi badala ya kujibweteka.Katika jamii yetu, mbali na kilimo zipo shughuli nyingi za kufanya na mtu kujiingizia kipato. Lakini kama ilivyo kwa makundi mengine, hawa wanapaswa pia kuwa waaminifu na kutii maagizo na miongozo ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo yao, kutoshiriki katika uhalifu au matukio ya uvunjifu wa amani na sheria, kusikiliza maelekezo mbali mbali kutoka kwa viongozi wao na kuyatekeleza kwa uaminifu.Inawezekana yapo makundi niliyoyasahau lakini kama nilivyosema mwanzo, baada ya John Magufuli kuchaguliwa kuwa rais na Watanzania walio wengi, ndiye sasa rais wetu watanzania wote kwa sababu hiyo ndio demokrasia na hivyo hatuna budi kumuunga mkono hadi atakapochaguliwa rais mwingine.Ni kwa mantiki hiyo, kila mtanzania anao wajibu na jukumu la kumsaidia kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika serikali yake, kwa kutekeleza majukumu, wajibu na kutii sheria za nchi. Waswahili wanasema usione vyaelea vimeundwa na hivyo tunavyoona mataifa makubwa yameendelea, tusidhani maendeleo yale yalishuka kutoka mbinguni bali wananchi waliwaunga mkono viongozi wao kwa hali na mali. Shime kila mtanzania amuunge mkono Rais kwa nafasi yake. Mwandishi wa makala haya ni msomaji na mchangiaji wa gazeti hili. | 1 |