text
stringlengths
1
24.2k
label
int64
0
5
SERIKALI imewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya watoe taarifa kama maeneo yao yana upungufu wa chakula na ni kiasi gani kinahitajika.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema leo bungeni mjini Dodoma kuwa, wizara ya Kilimo ikipata taarifa hizo itaratibu vizuri na kuona namna ya kufikisha chakula kwa wananchi kwa kuwauzia ili zipatikane fedha za kununua chakula kingine kiwekwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chemba (CCM) Juma Nkamia aliyetaka kauli ya Serikali kwa kuwa baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dodoma, Manyara na Singida ina tatizo kubwa la chakula na huenda baadhi ya wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hawatoi taarifa sahihi kwa sababu ya woga.“Upungufu wa chakula upo kwa baadhi ya wilaya na maeneo mengine na huu ulitokana na tatizo la hali ya hewa kwamba yapo maeneo msimu uliopita hayakupata mvua ya kutosha. Jambo hili linapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi…”amesema Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo hapo kutoka kwa wabunge wa Bunge la Tanzania.“Inapotokea kama hali ya hewa imekuwa mbaya Mkuu wa Wilaya akieleza atakuwa anaeleweka kwa sababu pia baada ya kutoa taarifa hiyo timu ya Wizara ya Kilimo itakwenda kuona hali halisi na kuweza kuzungumza na ile mamlaka kuweza kupelekewa chakula kwa bei nafuu” amesema.Amesema jambo hilo limetolewa ufafanuzi mara nyingi na kwamba, Rais John Magufuli hajazuia kutolewa kwa taarifa za upungufu wa chakula isipokuwa kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa na kila mmoja ana nafasi ya kulima au kufanya kazi lakini yana upungufu wa chakula.“Viongozi waliopo kwenye maeneoi hayo wanao wajibu wa kusimamia kila mmoja anafanya kazi pamoja na kulima mazao ya chakula na biashara ili waweze kujipatia tija inapofikia kipindi kama hiki kila mmoja anakuwa na akiba yake” amesema.Ametoa mwito kwa wafanyabiashara watumie fursa ya tofauti za hali ya hewa kwenye maeneo kuuza chakula sehemu zenye upungufu.Amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wakutane na wafanyabiashara wawashawishi wapeleke chakula kwenye maeneo yenye upungufu ili kuongeza vipato vyao.
1
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa taasisi za kutoa huduma wezeshi kwa wateja kufanya hivyo kwa wakati na kuacha urasimu ili kutowakatisha tamaa wabunifu wakati huu wa uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda hapa nchini.Waziri Majaliwa alisema hayo kwenye viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha wakati wa kufunga maonesho ya Wiki ya Viwanda na kusema kuwa kuchelewa kutoa huduma kwa wakati ni kuzorotesha kasi ya uanzishwaji wa viwanda.Majaliwa alisema kwa kuwa serikali imeweka mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda, hakuna sababu ya kuchelewesha utoaji wa vibali vya wateja ambao wanataka huduma kwenye taasisi wezeshi.Moja ya taasisi hizo ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo linadaiwa kumchelewesha mteja ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Budget Motorways ya wilayani Kibaha ambayo ilikuwa na mpango wa kuanzisha utengenezaji wa mabasi, lakini amesubiri kibali mwaka mzima. Alisema kuwa kama tayari mtu keshasema ana uwezo wa kutengeneza kitu fulani, ni kwanini TBS isivipime vifaa vinavyozalishwa na kampuni hiyo kama vinakidhi vigezo au la, kuliko kutofanyia kazi suala hilo na kutoa majibu.“Mnachopaswa ni kumfuata na kupima vipuri anavyozalisha kuona kama vina uwezo wa kuundwa hayo magari kama havina uwezo waambiwe kuliko kukaa kimya muda mrefu kiasi hicho, kwani mnawakatisha tamaa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda,” alisema Majaliwa.Aidha alisema kuwa mpango wa serikali ya Awamu ya Tano ni kuwa na viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini ili kuachana na uagizaji wavifaa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuinua uchumi wa nchi na kupunguza gharama za uagizaji kutoka nje ya nchi. Alimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa na kupata ufumbuzi haraka.“Waziri Mwijage una wajibu kuhakikisha suala hili linakwisha ili kumwezesha huyo mtu anayetaka kuanzisha kiwanda cha kutengeneza magari aweze kupata vibali vinavyostahili na kama vigezo havipo basi ijulikane kuliko kutotoa majibu yoyote, hii haijakaa sawa, shughulikia suala hilo. Haya ndiyo tunayoyataka, watu wenye mawazo mazuri lazima yafanyiwe kazi,” alisema Majaliwa.Alibainisha kuwa serikali imezielekeza taasisi za fedha kutoa fedha za mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji kwa wajasiriamali ambao watakuwa na vigezo kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda ambavyo vitaongeza wigo wa mapato na kutoa ajira kwa watu wengi.“Tutahakikisha tunakabiliana na changamoto ambazo zilisababisha viwanda kufa ili hivi vinavyojengwa viweze kudumu kwani vitasaidia ukuaji wa uchumi pia mkoa wa Pwani ambapo ni kinara wa kuwa na viowanda vingi uendelee kuhimiza uanzishwaji wa viwanda,” alisema Majaliwa. Kwa upande wake, Waziri Mwijage alisema kuwa mkoa wa Pwani umefanya mageuzi makubwa ya viwanda kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta hiyo na kuufanya uongoze kwa kuwa na viwanda vingi na maonesho hayo watayafanya yawe ya kimataifa ili kuhamasisha wawekezaji.Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alisema ili kuhamasisha mikoa itekeleze kwa vitendo sera ya uanzishwaji viwanda watafanya mashindano kwa mikoa ili kuangalia ni mkoa gani umetekeleza na ulioshindwa.Jafo alisema mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo imetekeleza kwa vitendo sera ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda ambavyo vitaifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda. Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema kuwa lengo la kuanzisha maonesho hayo ambayo yatakuwa ni endelevu ni kutambulisha bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo pia kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.Ndikilo alisema lengo lingine ni kuzitangaza bidhaa zao ambazo zinakosa soko kutokana na kutojitangaza, hivyo watu kutojua bidhaa zao pia ni kuwatafutia masoko kwa wananchi na sehemu mbalimbali za nje ya nchi mkoa huo una viwanda 429 vikubwa vikiwa ni 109 na vidogo 320. Maonesho hayo yalifunguliwa Oktoba 29 na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
1
“Hatua hii ya Brela ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,” alisema Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.Pongezi za Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini, ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi.Akithibitisha maendeleo hayo, mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Vibindo, alisema hivi karibuni alifanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu. Brela imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.Mteja wa Brela anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.Anatakiwa kuingia katika mtandao wa Brela ambao ni www.brela. go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.
0
ASHA BANI-DAR ES SALAAM MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali 258 yamefutwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kutokana na kufanya majukumu kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs). Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Emmy Hudson, alisema kufutwa kwa NGO hizo kwenye muunganisho wa wadhamini wa taasisi zenye kufanya shughuli zilizoainishwa kwenye sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali sura namba 56, ni kufuatia mabadiliko madogo ya sheria. Alisema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika katika sura ya 318 kupitia sheria ya marekebisho mbalimbali Na.3 ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa Juni 30 mwaka huu. “Kuanzia sasa jukumu la kusajili muunganisho wa wadhamini utafanyika kwa taasisi zile tu ambazo zitakuwa katika utaratibu maalumu, ikiwa ni pamoja na taasisi ambazo usajili wake wa awali umefanyika kwa mujibu wa sheria nyingine, lakini zinahitajika kupata utu wa kisheria. “Taasisi hizo ni pamoja na vyama vya siasa, mashirika na taasisi za kidini na vilabu vya michezo,’’ alisema. Aliongeza kuwa taasisi ambazo usajili wake moja kwa moja hufanyika Rita ni zile zinazofahamika kama mifuko inayotoa huduma bila ya kupata faida na usajili wake unafanyika chini ya sheria ya muunganisho wa wadhamini sura ya 318. Pia alisema taasisi ambazo usajili wake umetokana na maelekezo ya kisheria moja kwa moja au maamuzi ya kimahakama yanayoelekeza kuanzishwa kwa muunganisho wa wadhamini wa taasisi hiyo. Emmy alisema taasisi zinazojihusisha na masuala ya kilimo ambazo hazijasajiliwa katika sheria yoyote ya Tanzania na zinahitaji usajili kwa ajili ya kupata utu wa kisheria.  “Hivyo basi kuanzia siku ya tangazo hili, ofisi ya Mtendaji Mkuu  haitasajili tena muunganisho wa wadhamini wa taasisi yoyote ambayo inafanya  shughuli zilizoelekezwa kwa mujibu wa sheria ya NGO. “Ijulikane kwamba kwa taasisi zile ambazo zilishasajiliwa Rita ambazo baada ya marekebisho ya sheria hizo zitafutwa rasmi katika daftari la muunganisho wa wadhamini katika ofisi ya Rita, wadhamini watapaswa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha wanalipia madeni yote wanayodaiwa katika marejesho ya wadhamini kila mwaka kwa kipindi ambacho hawakulipa madeni yao walipokuwa Rita,’’ alisema. Pia alisema wanatakiwa kurejesha hati halisi ya usajili wa wadhamini ambayo walikabidhiwa wakati wa usajili. Baadhi ya mashirika hayo ni Muungano wa Wafugaji na Wawindaji nchini, Maarifa Media Trust (Mamet), Saint Anne Maria, Comprehensive Community Based  Rehabiliation in Tanzania (CCBRT), Mviwata Trust Fund na Human Right Resources Center of Tanzania.
1
NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, amesema ofisi yake ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), inapata misukosuko inapochukua sampuli za vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto au wazazi. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili ofisini kwake Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Manyele, alisema mara nyingine wakati wa upimaji kipimo hicho hutokea vurugu, hivyo kulazimika kuwatoa wahusika nje kwa nguvu ili shughuli zao za kiofisi ziendelee. “Kuna wakati baadhi ya wapenzi au wanandoa ulazimika kufikishwa ofisini chini ya ulinzi wa polisi, huku wengine wakikataa kukubaliana na matokeo, hivyo kusababisha vurugu,” alisema. Profesa Manyele alisema kutokana na hali hiyo, upimaji DNA huchukua karibu asilimia 90 ya kazi za GCLA na hivyo kuwapa wakati mgumu katika utendaji kazi zao. Alisema kwa kawaida ofisi hiyo uchukua sampuli za upimaji wa DNA kwa wazazi na mtoto wakiwa pamoja, lakini inapokuwa vinginevyo inaleta shida. “Hivi vipimo kuna muda mwingine tunapata shida kuvipata kwa sababu hatuwezi kumpima mmoja mmoja, lazima wahusika waje kwa pamoja. “Upimaji unakuwa mgumu na kuibua vituko na misukosuko mzazi mmojawapo anapokuwa hayupo tayari… Unakuta mtu wakati mwingine hataki kupima, hivyo hulazimika kuletwa chini ya ulinzi wa polisi,” alisema. Profesa Manyele alisema ili kuepusha hali hiyo, ofisi hiyo huwa inawashauri wanaosimamia vipimo hivyo kuhakikisha wanawaandaa wahusika kisaikolojia ili wawe katika maelewano mazuri kabla uchukuaji wa sampuli zao haujafanyika. Pia alisema wapo watu wanaoshindwa kwenda kupima jambo ambalo ofisi yake inalazimika kutuma wataalamu na kuwafuata walipo ili kuchukua sampuli zao. Alisema wazazi wengine wanafika katika ofisi hiyo na kuanza kulalamikia matokeo ya vipimo yanapotoka tofauti na matarajio yao. “Unakuta mzazi katika hisia zake ameshajihakikishia kuwa huyo mtoto si wake, au wengine wanadhani ni wa kwake. “Sasa ikitokea majibu yakatoka tofauti, mtu anakasirika, anakuja hapa anagonga mlango wa ofisi huku akilalamikia matokeo ya DNA,” alisema. Alisema mara nyingi watu wanaofanya hivyo wanaenda kinyume cha utaratibu kwa kuwa mtu anayepaswa kulalamikia matokeo ni aliyepeleka sampuli za vipimo hivyo. Profesa Manyele alisema kutokana na unyeti wa vipimo vya DNA, ndiyo maana vinafanyika kwa usimamizi wa vyombo vilivyotajwa katika sheria, ikiwamo mahakama, ustawi wa jamii, hospitali, manispaa au mkuu wa wilaya, wakili wa kujitegemea, polisi na vituo vya utafiti. Pia alisema yapo makosa yanayofanywa na watendaji wa manispaa, wilaya na mikoa kwa kushindwa kutunza vizuri matokeo ya DNA baada ya kuyapokea. “Utakuta mhusika anaenda katika ofisi za wilaya au manispaa anamkuta ofisa anamuulizia kuhusu karatasi ya matokeo, anakuwa hajui alipoiweka, akiitafuta unamwona anaitoa chini ya uvungu, unashangaa anawezaje kuweka vile nyaraka muhimu kama ile,” alisema Profesa Manyele na kuongeza: “Kinachotokea watu wanapokea matokeo yale bila kufuata taratibu za kiofisi. Mtu analetewa matokeo hakuna sehemu ambayo anasaini wala kuandika kama amepokea kitu. Kwa kifupi hakuna usiri wa matokeo katika ofisi hizo.” Alitaja makosa mengine wanayoyafanya watendaji ni kusoma au kutoa taarifa za matokeo ya vipimo hivyo mbele ya mtoto husika jambo ambalo si sawa. “Mtoto hatakiwi kujua haya mambo. Waachwe wazazi wenyewe wasikilize. Ikitokea mzazi amekuja na mtoto kuchukua matokeo, watendaji wanapaswa wahakikishe wanamshauri wakati mtoto hayupo. Hii itasaidia kwa ustawi wa mtoto husika,” alisema. Profesa Manyele aliendelea kusema kuwa watendaji wanapaswa kuhakikisha wanawaelimisha wahusika wachukuliwe vipimo kuondoa dhana potofu ya kufikiri  kuwa kipimo hicho pia kinapima Virusi vya Ukimwi (VVU) jambo linalosababisha watu kuogopa. Mbali na kujua uhalali wa watoto au wazazi, pia alitoa sababu za watu kupima DNA kuwa ni pamoja na kutatua malalamiko ya kesi za urithi na kutambua ndugu halali. Alisema pamoja na kesi za watoto wanaopata mimba za utotoni kuwa nyingi, lakini ofisi hiyo haipokei kwa wingi malalamiko hayo kutokana na wahusika kutojua kama chombo hicho kinaweza kuwasaidia. “Maofisa elimu na walimu inabidi wafahamu kuwa ofisi ya mkemia mkuu ina nafasi kubwa sana ya kutatua migogoro ya mimba za utotoni baada ya mtoto kujifungua. Hivyo inakuwa rahisi kwa mhusika kuchukuliwa hatua,” alisema Profesa Manyele.
1
Vinara hao wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 21, wanaikaribisha kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hiyo ya Shinyanga ambayo iko katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 28. Imecheza mechi 22.Mwishoni mwa wiki, Yanga ilikumbana na Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.Huenda hasira zao za kushindwa kupata ushindi watazihamishia katika mchezo huo ili kuwafurahisha mashabiki wake ambao walitegemea timu hiyo ingepata ushindi mkubwa katika mchezo huo wa kimataifa.Katika mchezo wa raundi ya kwanza, Yanga ilishinda Stand United mabao 3-1 mjini Shinyanga. Mchezo wa leo utakuwa ni muhimu kwa Yanga kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi, kwani ina pointi 46 ikitofautiana pointi nne na mabingwa watetezi Azam FC wenye pointi 42.Ikishinda mchezo huo na mingine miwili inayokuja dhidi ya Ruvu Shooting na Polisi Morogoro itatwaa rasmi taji hilo. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, wachezaji wote wako vizuri kwa mchezo huo na wamejipanga kuondoka na pointi tatu.“Wachezaji wote wanaendelea vizuri, Telela (Salum) ambaye alikuwa ni majeruhi pia ameimarika na huenda leo akawepo katika kuiua Stand United, jambo la muhimu ni mashabiki wasichoke waje kutuunga mkono,” alisema Muro.Kwa upande wa Stand United, bado ina wakati mgumu kwani inahitaji ushindi kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri. Msemaji wa Stand United, Isaac Edward alitabiri mchezo huo na ujao dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC kuwa migumu kwao ambao wanatafuta nafasi ya kupambana ili wasirudi Daraja la Kwanza baada ya kupanda msimu huu.Edward alisema kikosi chake kiko vizuri na tayari kwa mchezo huo kuhakikisha kinaonesha juhudi kupata pointi tatu. Ligi hiyo inayoelekea ukingoni, itaendelea kesho kwa michezo miwili ambapo Simba itacheza na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa na Polisi Morogoro wataikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.Simba imetoka kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki hii jijini Mbeya, huku msemaji wao, Haji Manara akijifariji kuwa timu hiyo imedhamiria kuondoka na ushindi katika uwanja wake wa nyumbani.Katika mechi za juzi za ligi hiyo, Mtibwa Sugar iliibana Prisons nyumbani kwake Sokoine jijini Mbeya na kwenda sare ya bao 1-1 wakati Ruvu Shooting iliifunga Mgambo JKT mabao 2-1.
2
Mwandishi Wetu -Malinyi WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemwondoa madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa kosa la kupuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa. Licha ya kumwondoa katika nafasi hiyo, Lugola amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara yake, kumchukulia hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa maofisa wengine wa trafiki mikoa mingine. Alisema ameshuhudia video ambayo ilikuwa inasambaa mitandaoni, Bukombe akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na pia kugoma kuyatekeleza akiwa katika mkutano jijini Arusha. Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa mji wa Malinyi mkoani Morogoro jana, Lugola alisema yeye hatoi maagizo ya kisiasa, bali yatakayomsaidia rais kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na umasikini na ajira. “Namwagiza katibu mkuu achukue hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kumwondoa u-RTO afanye shughuli zingine za kipolisi na wengine ambao mkono wangu haujafika kwenu, nimeanza kuwaona hamsimamii vizuri maagizo yangu. “Wapo  ambao wanaendelea na uonevu, wapo baadhi ya askari wanaendelea kuchukua rushwa barabarani,” alisema Lugola. Pia Lugola alitoa onyo kali kwa wakuu wa trafiki wa mikoa ya Morogoro na Mara na kuwataka wachukue fursa ya kujitathmini katika utendaji wao kabla hajawachukulia hatua. “Wapo baadhi ya askari waonevu, wanaendelea kuchukua rushwa, wajitathmini katika utendaji wao kabla sijawachukulia hatua kali za kinidhamu,” alisema. Lugola ambaye alihutubia mikutano mingi kwa nyakati tofauti jana, alisema Serikali ni sikivu na haitaki kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki wasiokuwa waaminifu. Kutokana na hali hiyo, alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi nchini, kwamba bodaboda zinazotakiwa kuwapo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu; zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali. “Bodaboda hizo ndizo zinapaswa kuwapo vituoni, lakini kuziweka ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku, nataka polisi nchi nzima mnielewe,” alisema Lugola. Aliwataka waendesha bodaboda mjini Malinyi na Tanzania kwa ujumla, wafuate sheria za usalama barabarani ikiwamo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. Pia alipiga marufuku tabia ya baadhi ya askari kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za jeshi, akisema kufanya hivyo kunaleta kero kwa madereva na pia anayekamatwa anaweza akadhaniwa kuwa ni jambazi. Lugola anaendelea na ziara yake mkoani Morogoro na anatarajia kumaliza ziara hiyo Wilaya ya Ulanga.
1
LIGI Kuu ya wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo minne katika viwanja vinne tofauti.Vinara wa ligi hiyo Alliance Girls yenye pointi 13 wataikaribisha Baobab ya Dodoma yenye pointi moja katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza. Panama Queens yenye pointi tatu itacheza na bingwa mtetezi JKT Queens ambayo ina pointi tisa katika nafasi ya nne, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Samora, Iringa.Katika Uwanja wa Gwambina, Mwanza, TSC Queens yenye pointi sita itacheza na vibonde Tanzanite Queens ambayo haina pointi ikiwa imefungwa mabao 23. Akizungumza jana Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo alisema michezo mitatu imesogezwa mbele kwa sababu mbalimbali.Mchezo wa Simba Queens na Sisterz ya Kigoma ambao ulikuwa uchezwa leo umesogezwa mbele hadi keshokutwa kutokana na Sisterz kuchelewa kufika Dar es Salaam kwa sababu walisafiri kwa treni toka Kigoma, hadi jana ilisemekana walikuwa Kilosa, Morogoro, na ilishindikana kuendelea na safari kutokana na kuwepo ajali ya treni ya mizigo.Pia mchezo wa Mlandizi Queens dhidi ya Marsh na Ruvuma Queens dhidi ya Yanga Princess zitachezwa Jumanne ijayo badala ya leo, michezo hii imesogezwa mbele kutokana na timu hizi kuwa na wachezaji katika kikosi cha timu ya Taifa ya U-20 kilichopo Algeria.
2
 NEW YORK, MAREKANI KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres ameonya kuwa mlipuko wa sasa wa virusi vya corona (Covid 19) ndiyo changamoto kubwa kwa ulimwengu tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WWII). Amesema mlipuko huo unaweza kuleta kushuka kwa uchumi “ambayo labda hauwezi kufananishwa katika siku za nyuma za hivi karibuni”. Akiongea katika makao makuu ya UN huko New York wakati wa uzinduzi wa ripoti juu ya athari kubwa ya kiuchumi ya mlipuko huo, Guterres alisema ugonjwa huo mpya wa corona unashambulia jamii kwa kwa kishindo, kusabbisha vifo vya watu na kuathiri maisha yao. Alisema nchi zote ulimwenguni zimeweka safu za uchukuaji hatua, ikiwa ni pamoja na kuzuia atu kutembes na kukusanyika na kufunga biashara nyingi, ili kupunguza kuenea kwa virusi hivyo. Ripoti ya UN inakadiria kwamba hadi kazi milioni 25 zinaweza kupotea ulimwenguni kote kama matokeo ya kuzuka. Pia miradi inayokadiriwa kufikia asilimia 40 inayofadhiliwa katika nchi mbalimbali kwa ajili yakuchochea uchumi inatarajiwa kuporomoja. “Covid-19 ni mtihani mkubwa kabisa ambao tumekabili pamoja tangu kuumbwa kwa Umoja wa Mataifa. Tunahitaji mwitikio wa afya ulioratibiwa mara moja ili kukomesha maambukizi na kumaliza janga,” alisema. Onyo lake linakuja wakati wa utabiri mkali juu ya uwezekano wa athari za kiuchumi za hatua zilizowekwa kupambana na virusi hivyo.Idadi ya kesi zilizothibitishwa ulimwenguni kote sasa inakaribia 860,000, na zaidi ya vifo 42,000. Idadi ya vifo nchini Marekani tayari sasa ni zaidi ya 4,000 zaidi ya idadi ya waliouawa nchini China, ambapo ugonja huo ulianzia mwishoni mwa mwaka jana. Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimesema watu 865 walikuwa wamefariki dunia katika masaa 24 yaliyopita nchini Marekani na kwa watu wote zaidi ya 189,000 nchini humo wameambukizwa. Wakati huo huo, Hispania inaikaribia Italia kwa idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya kushuhudia vifo 849 katika masaa 24 kufikia jana, idadi kubwa zaidi ambayo imekuwa nayo katika siku moja. Nchini Uingereza, jumla ya watu 1,789 wamefariki dunia, ikiwa ni ongezeko la watu 381, maofisa wanasema. Kati ya waathiriwa ni kijana wa miaka 13, kwa mujibu wa Hospitali ya Trust King’s College ya mjini London.
3
['Vioja vya shabiki sugu wa timu ya taifa Tanzania katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika - Bongo Zozo amewaacha wengi hoi katika mitandao ya kijamii nchini humo baadhi wakiguswa na ushabiki wake kwa timu hiyo.', ' Ametoa matumaini kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo licha ya kipigo cha 2-0 walichopokea Taifa Stars katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.', 'Bongo Zozo, kama anavyojiita katika mitandao ya kijamii ikiwemo You Tube, anaonekana katika mojawapo ya kanda ya video iliosambaa mitandaoni akitembea mjini Cairo akiwa amevaa jezi huku akipeperusha bendera ya Tanzania huku akizungumzwa kiswahili na mashabiki wengine wa Tanzania.', 'Nchini kwenye Tanzania kwenyewe, picha zake zimesambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo hata makundi ya Whatsapp.', 'Baadhi wakifurahia namna Bongo Zozo anavyozungumza kiswahili na kuimba wimbo wa taifa.', 'Ni swali wanaloniuliza watu wengi "Mzungu mswahili ametuzidi uzalendo" baadhi wakiandika katika mitandao ya kijamii.', 'Bongo Zozo - ambaye jina lake halisi ni Nick Reynolds - alizaliwa Zimbabwe na kuwahi kuishi Tanzania kabla ya kuhamia Uingereza.', 'Ameeleza kwamba anazipenda Tanzania na Zimbabwe mataifa yalio karibu sana moyoni mwake.', '"Mimi ni shabiki wa timu mbili Ya Zimbabwe na timu ya Tanzania\'', 'Anasema anaishabikia Zimbabwe sababu ndiko alikolizaliwa Zimbabwe, na Tanzania kwa upendo alio nao kwa taifa hilo. ', "'Napenda na navutiwa sana na mpira wa Afrika lakini sanasana mpira wa Tanzania, sababu kuna fujo isiyoumiza. Yaani watu tuna kelele sana kuliko (mashabiki wa timu nyingine) watu.'", 'Hatahivyo anaongeza kuwa Kenya pia ni timu anayoishabikia kwasababu zote ni timu za Afrika mashariki kiashiria cha kwamba watu wote ni wamoja.', '"Nimeishi Tanzania kwa muda wa miaka kumi na minane tangu mwaka 98 hivi, nilikutana na mwanamke nikamuoa alafu basi nimekuwa Mtanzania," amesema.', 'Anasema anafurahia sana Tanzania kufuzu katika mashindano ya kombe la mataifa mwaka huu baada ya kusubiri kwa miaka 39."', 'Je kura anaitupa wapi katika mpambano wa Alhamisi wa Taifa stars dhidi ya Harambee stars ya Kenya?', "'Tanzania lazima tuwakung'ute (Kenya)'.", "'Sema nitalia machozi hata ya damu kama ni droo - sababu kama tunashindwa kuwafunga Kenya, naombeni mutufunge sababu ikiwa droo basi hatufuzu sisi (Tanzania) na Kenya haiwezi kufuzu' anaeleza Nick."]
2
NA VALERY KIYUNGU IKIWA Tanzania inaadhimisha miaka 17 toka Rais wa Kwanza, Julius Kambarage Nyerere afariki dunia mwaka 1999, huku kwenye muziki wa dansi, hasa kwenye safu hii ya Old Skul tunapata wasaa wa kumtazama Baba huyo wa Taifa kwenye suala la kuuendeleza muziki huo. Enzi za uhai wake, hayati Baba wa Taifa alikuwa chachu ya ukuaji wa muziki wa dansi, kwani alihamasisha na kuwezesha wilaya karibu zote Tanzania kuwa na bendi ya muziki, hali kadhalika aliagiza kuanzisha bendi kwenye viwanda na mashirika ya umma. Kufuatia agizo hilo, ziliibuka bendi nyingi zilizokuwa na wanamuziki mahiri, bendi hizo zilizopata kuvuma zilipewa majina kutokana na mahali ambapo zilitokea, mfano mzuri ni Kilombero Jazz, Kilosa Jazz, Kilwa Jazz pamoja na Butiama, ambayo ilipewa jina hilo kwa heshima ya kijiji alichozaliwa Julius Nyerere, ingawa ilikuwa na makazi yake Ifakara, mkoani Morogoro. Baada ya kuanzishwa kwa bendi za wilaya ambazo zilifanya kazi nzuri, wanamuziki wakongwe na mahiri wa bendi hizo kila mmoja kwa uwezo wake alifanya kile alichoweza, kama kutunga, kupiga vyombo au kutunga nyimbo. Maudhui yaliyokuwa yanazibeba nyimbo zilizotungwa na bendi hizo yalilenga zaidi kuwasifu wanasiasa na kuongeza hamasa kwa zile nchi tano zilizokuwa mstari wa mbele katika kuupigania ukombozi wa bara la Afrika. Nyimbo kama Mwenyekiti, ulioimbwa na Urafiki Jazz, uliotungwa na Juma Mrisho, Nyerere Baba wa Taifa ulioimbwa na waimbaji wa DDC Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’,  utunzi wake Joseph Mulenga pamoja na ule uitwao Mwalimu Nyerere ulioimbwa na bendi ya National Panasonic Sound uliotungwa na Maurus Mzelu mwaka 1982, nyimbo zote hizo zililenga kusifia mambo mbalimbali aliyoyafanya Nyerere. Lakini licha ya uhusiano mkubwa wa Mwalimu Nyerere na muziki wa dansi, alipofariki hakuna bendi wala wanamuziki wakongwe waliomkumbuka kwa kutunga nyimbo za kumuenzi ambapo siku kama ya jana zingeweza kuchezwa. TATIZO NI NINI? Baadhi ya wanamuziki wakongwe waliozungumza na safu hii walidai kuwa, siku hizi gharama zimekuwa kubwa tofauti na miaka mingi ya nyuma, hivyo wangepata mfadhili wa kuwapa fedha za kurekodi jambo hilo lingewezekana. KING KIKI AFUNGUKA Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya La Capital, Mzee King Kiki, ameiambia Old Skul kuwa wanamuziki inawawia vigumu kutunga nyimbo za kumbukumbu ya mtu aliyefariki kwa kuwa mtunzi anakuwa hana jambo jipya la kumsifu kwa kuwa matendo ya mlengwa yanakuwa yamekoma. CHAMUDATA  NAO VIPI Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata), Juma Ubao, anasema kuwa ni gharama kubwa kutunga nyimbo za siasa na matukio ya kumbukumbu kama ya kifo cha Nyerere, hivyo wanahitaji kuwezeshwa ili wafanikiwe kumuenzi Mwalimu. “Wanamuziki tunahitaji msaada wa kifedha kutoka kwenye Wizara yenye dhamana na muziki, tunapenda kuwatungia nyimbo za kumbukumbu viongozi wetu, kinachotushinda ni gharama, ni kubwa mno,” alisema Juma. Maoni yako yaweke hapa 0714288656
4
NA ESTHER GEORGE, RAPA mkali katika muziki wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’, amesema matumizi ya dawa za kulevya yamempa mafunzo makubwa na itabaki kuwa historia kwake. Chid Benz aliliambia MTANZANIA kwamba dawa za kulevya zimeharibu maisha yake kwa kiasi kikubwa na yamemdhalilisha yeye na familia yake na watu wake wa karibu hivyo hatathubutu kurudia kama baadhi ya wasanii walioacha na kurudia kama Rehema Chalamila ‘Ray C’. “Dawa za kulevya kwangu zinabaki kuwa historia, sitaki hata kuzisikia zimeniumiza sana kimawazo, zimenidhalilisha na zimepoteza mwelekeo wa maisha yangu, sina hamu nazo tena nina hasira nazo siwezi kuzirudia kama baadhi ya wengine walivyorudia kwa sasa naangalia maisha yangu mapya katika muziki,” alijieleza Chid Benz. Chid Benz anaeleza kwamba waliomshawishi kuingia katika matumizi ya dawa hizo ni marafiki zake katika makundi aliyokuwa akibadilishana nao mawazo ambao wengi wao walimshawishi kwamba akitumia dawa hizo atakuwa na nguvu zaidi ya kuimba na kufanya makubwa jukwaani lakini ikawa tofauti na matarajio.
4
Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakuwa wakijifua mara mbili kwa katika Uwanja wa Karume katika kujiweka sawa na maandalizi ya mchezo huo.Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezaji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Ajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).
2
WANAWAKE wametakiwa kuacha tabia ya kudai talaka wakati inapoibuka migogoro majumbani, kwani kufanya hivyo ni kuongeza matatizo na kusababisha kuwepo wimbi la watoto wa mitaani waliokosa matunzo.Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Wanawake, Watoto na Wazee Mouldin Castico wakati wa uzinduzi wa jengo la Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa huko mjini Unguja. Alisema njia pekee ya kuleta ufumbuzi wa migogoro ya ndoa ni usuluhishi wa pande zote mbili kwa kutumia wazee na viongozi wa dini ikiwemo makadhi.Alifahamisha kwamba migogoro ya ndoa kwa kiasi kikubwa imesababishwa na kusambaratika kwa familia na kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wa mitaani ambao hukosa haki ya msingi ya elimu. ‘’Njia pekee sahihi za kumaliza migogoro ya ndoa majumbani ni kufanya suluhu kwa kutumia wazee na viongozi wa dini,’’alisema. Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu alisema kazi kubwa inayofanywa na mahakama mbalimbali ikiwemo ya kadhi ni kuzifanyia ufumbuzi haraka wa kesi za ndoa.Alisema katika kipindi cha mwaka jana, jumla ya kesi za migogoro ya ndoa 767 ziliwasilishwa katika mahakama mbalimbali za kadhi Unguja na Pemba, kusikilizwa na kutolewa maamuzi. ‘’Kesi za migogoro ya ndoa ikiwemo zinazohusu talaka tumezipa kipaumbele cha kwanza kwa ajili ya kusikilizwa na kupatiwa ufumbuzi katika mahakama za kadhi zilizopo Unguja na Pemba,’’alisema.Kadhi dhamana wa Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa, Kassim Ali alisema jamii inahitaji kupewa elimu zaidi kuhusu ndoa kabla ya kuingia katika makubaliano hayo. ‘’Kesi za migogoro ya ndoa na kudai talaka zimekuwa zikiongezeka katika Mahakama ya Kadhi ambapo moja ya tatizo kubwa ni kukosekana kwa maadili na misingi ya ndoa katika jamii,’’alisema. Mahakama za kadhi zilizopo Zanzibar hutumiwa na jamii ya Waislamu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi kesi za talaka, matunzo ya watoto pamoja na urithi.
1
Msanii wa bongo fleva mashuhuri Faustina Mfinanga ambaye jina la jukwaani tunamfahamu kama Nandy amefunguka namna ambavyo dereva taksi alimpa dili kubwa. Nandy amesema kuanzia sasa anaviheshimu vyombo vya usafiri kama bodaboda, taksi na bajaji kwakuwa vina nafasi kubwa katika mziki wa bongo fleva. Amesema dereva mmoja wa taksi alijikuta akimla dili kubwa lililomlipa kuliko madili yote bila kujua, kwa kupiga nyimbo zake mfululizo akiwa amewabeba watu ambao baadaye walimtafuta Nandy na kumpa dili. Jana nimejifunza kitu kikubwa sana kwenye mziki!! Hivi vyombo vya uasafiri tunavo panda kama TAX, UBER, BAJAJI, PIKIPIKI, DALADALA ni vitu vya kuviheshimu sana hasa kwa sisi wasanii! Huwa tuna enjoy wanavokuwa na flash wanapiga nyimbo zetu ila kuna zaidi ya hilo na huwa wanafikisha mziki wetu mbali! Sababu wanapakia abiria tofauti tofauti kutoka nchi mbali mbali!…. imagine me kupata hii show naweza kiri ndo show niliyo pokea pesa iliyo pitiliza hata rate yangu ya show ya sasa kwa kupitia usafiri wa UBER!!! Hawa wafaransa walinisikia kwenye UBER na kwa jinsi walivokuwa wanasema uyo dereva popote alipo nakushuru alikuwa ana rudia rudia nyimbo zangu nakunisifia kweli!!! Basi hawa ikabidi wanifatulia kiundani ndo wakaona kumbe nina potential ndani yangu! Since izo siku ni mwaka sasa tangia wanijue wakawa wananifatilia na kuwa ma big FAN🔥… jana nimeimba kwenye sehemu ya kampuni yao wakiwa wao tu STAFF ONLY! nakuelezea hii historia walivyo nijua nilishangaa sana!! Kinacho nifurahiaha zaidi hii show imezaaa matunda zaidi ya nilivo tegemea kwao!! Me niseme asante sana @samaniconceptstore @samaniconceptstore we are now family i cant wait for the big things 2020🙏 . . A post shared by Faustina Charles Mfinanga (@officialnandy) on Dec 22, 2019 at 6:27am PST
4
KISWAHILI ni lugha iliyotoka mbali na ina historia ndefu tangu kuanza na kuenea kwake sehemu mbalimbali duniani inapozungumzwa kwa ufasaha, ikiwa miongoni mwa lugha zinazotambulika kitaifa na kimataifa.Jitihada nyingi zilifanyika katika kukienzi Kiswahili katika kukifundisha, kujifunza, kupitia wataalamu, waandishi mbalimbali wa vitabu vya tamthilia, riwaya na ushairi wanaolenga kuikuza lugha hii kwa kukizungumza na kukiandika kwa ufasaha. Kwa sasa lugha hii ya Kiswahili inachukua nafasi ya tatu barani Afrika kama lugha kwa kuzungumzwa na watu wengi na ni moja kati ya lugha kumi katika orodha ya lugha za kimataifa ulimwenguni hali inayofanya Kiswahili kitambulike zaidi duniani kote.Akizungumza katika uzinduzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (Chaukidu) lililofanyika mjini Unguja hivi karibuni, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anasema: “Kiswahili ni lugha yetu na ni lugha ya taifa letu, hivyo tunapaswa kukiheshimu na kukizungumza kwa ufasaha na kujivunia kwa vitendo.”Kongamano hilo linahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) akiwamo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Karume, Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Mohammed Seif Khatib, na wadau wengine mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.Makamu wa Rais anawahimiza Watanzania kujivunia lugha hiyo kwa kuacha kinachochanganya na maneno ya lugha nyingine ili kiwe lugha isiyo tegemezi na inayozidi kuimarika. Anatoa mfano wa maneno yanayotumika kwa kuchanganywa Kiswahili na Kiingereza kuwa ni pamoja na “kuji- giftisha” na “ku-stop-isha”.Samia anasema ili Kiswahili kiendelee kuwa na hadhi yake kama lugha ilivyo, jamii haina budi kujitathmini inapotaka kukitumia na kuzingatia uasili unaoendana na mila, silka na tamaduni ikiwemo kanuni za lugha ili kuepuka kukiharibu katika mazungumzo.Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, asili na hadhi ya Kiswahili inajulikana hasa katika historia; kwamba ni lugha yenye malengo na hadhi yake inazidi kuonekana katika nyanja mbalimbali siku hadi siku hali inayokifanya kiendelee kuwa lugha endelevu na lugha ya taifa (Tanzania) na Afrika ya Mashariki kwa jumla. Anasema hata Benki ya Afrika imeiona thamani ya Kiswahili na kuamua kutoa\ chapisho la Afrika kwa kutumia lugha hiyo adhimu na kwamba, hii ni ishara kwamba Kiswahili ni lugha inayojitegemea na inayokubalika Afrika na duniani kote.Anakipongeza: Chaukidu kwa kulenga kueneza Kiswahili ili kitumike kwa ufasaha katika mataifa mbalimbali na kuwa lugha moja, lengo moja na mawasiliano kwa wote. Uchunguzi wa makala haya kupitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa, watu wengi wamekuwa wakivutiwa na Kiswahili na kukizungumza siyo tu barani Afrika, bali hata kwa mataifa mengine kama Marekani, Burundi, Austria, Pakistani na Ujerumani.Ndiyo maana Makamu wa Rais anawasisitiza walimu na wadau mbalimbali kukitumia ipasavyo katika kuelimisha na kutumia juhudi zote kukifanya kuwa lugha endelevu zaidi. Anawaomba wanachama wa Chaukidu kuwaelimisha na kuwakumbusha viongozi na wanahabari umuhimu wa kuzungumza lugha hii kwa ufasaha ili wengine wajifunze zaidi kutoka kwao.Profesa Abdulaziz Yussuf Lodh wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (Suza) anasema Kiswahili ni lugha inayowaniwa kuzungumzwa katika mataifa mbalimbali hali inayomaanisha kuwa, Kiswahili sasa ni lugha muhimu duniani. Profesa Lodh anazitaja baadhi ya nchi duniani zinazozungumza Kiswahili kuwa ni Oman, Abudhabi, Somalia, Rwanda, Burundi na Kongo. Anasema kwa mujibu wa historia, Kiswahili kilitumika kama sehemu ya biashara kikitumika pia kutafsiri masuala ya dini katika maeneo mbalimbali muhimu kwa wakati huo.Kadhalika anasema, Kiswahili pia kimekuwa ni lugha inayotumika katika Umoja wa Afrika na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) huku kwa Tanzania ikiwa ni lugha ya taifa. Kutokana na umuhimu wake duniani, Profesa Lodh anasema nchi ya Marekani nayo imekuwa miongoni mwa ya nchi zinazotoa taaluma ya Kiswahili kupitia vyuo vikuu takribani 50 vinavyofundisha Kiswahili.Profesa Lodh katika kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo: “Lugha Yetu, Umoja Wetu kwa Maendeleo Yetu,” anasema Kiswahili kimekua na kukomaa zaidi hasa kwa vile kinatumika katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya jamii na taifa kama vile kutungwa kwa katiba ya nchi yetu kwa lugha ya Kiswahili kutunga mitihani inayohusu lugha ya Kiswahili, ikiwamo ya Somo la Kiswahili na kutunga vitabu mbalimbali kwa kutumia lugha hiyo.Naye Makamu Mkuu wa Suza, Profesa Idris Rai anawashukuru wadau wa Chaukidu na kumpongeza mtunzi maarufu wa vitabu, Wallah bin Wallah kutoka Kenya kwa maelezo yake ya kueleza jamii kwamba Zanzibar ndiyo asili ya lugha fasaha ya Kiswahili, hali inayowapa nguvu kuimarisha mikakati ya kukuza zaidi lugha hiyo. Profesa Idris anasema tangu mwaka 2011 Suza imefanikiwa kufundisha walimu wengi wasiojua kuzungumza Kiswahili kupitia Taasisi ya Kiswahili na Lugha ya Kigeni ikilenga kuimarisha, kueneza na kukifanya Kiswahili kizungumzwe hata na mataifa mengine duniani.Mdau, mtunzi na mwandishi wa vitabu ndugu Idd Mwimbe anasema ni thamani kwa Tanzania kupata fursa adhimu ya kufanyika kongamano hilo la kimataifa lililojumuisha mataifa mbalimbali hali inayowafanya watu waungane na kujuana ni lugha ya kujivunia na kuzingatiwa kwa faida ya wote. Anasema kongamano kama hili ni fursa na ni chachu hata kimaendeleo katika sekta ya utalii na kuingiza pato la taifa ikwemo fedha za kigeni na kwamba katika hili, kila mmoja anapaswa kuwa wakala kwa kuwafahamisha wanajamii ambao hawakuhudhuria kongamano hilo kuhusu kuhamasisha namna nzuri zaidi ya kutumia Kiswahili kwa ufasaha.
1
Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM VIGOGO wa soka nchini, timu za Simba na Yanga, leo zitashuka katika viwanja tofauti kusaka pointi tatu katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Yanga itakuwa nyumbani ikiikaribisha Singida United katika Uwanja Taifa, Dar es Salaam, huku, Simba wakiwa ugenini dhidi ya Mwadui FC, katika Uwanja wa Mwadui Complex, mjini Shinyanga. Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi tisa, baada ya kucheza michezo mitatu bila kupoteza, wakati Singida United inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi saba,  baada ya kucheza michezo mitano, ikishinda miwili, sare mmoja na kupoteza miwili. Katika msimu uliopita, timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare katika michezo yote miwili. Tangu Singida United wapande daraja msimu wa mwaka 2017/18, imepoteza mechi moja tu kati ya nne ilizokutana na Yanga msimu uliopita. Mchezo huo pekee waliopoteza ni ule wa kirafiki ambao Yanga iliibuka na ushindi wa  mabao 3-2 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga itashuka dimbani bila beki wake kisiki, Kelvin Yondani, ambaye ana kadi tatu za njano alizopata katika michezo iliyopita. Simba inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi saba baada ya kucheza michezo minne, ikishinda miwili, sare mmoja na kupoteza mmoja, wakati Mwadui wanashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi mbili, baada ya kucheza michezo minne, ikitoka sare miwili na kupoteza miwili. Kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi kitashuka kuikabili Mwadui kikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka Mbao FC katika mchezo uliopita, katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Simba iliambulia pointi nne msimu uliopita katika michezo miwili dhidi ya Mwadui, ikianza kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam, kabla ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Shinyanga. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema wanataka kushinda mchezo huo ili kuendelea kuzichanga vema karata zao katika michezo ya nyumbani. “Kila siku nawapanga wachezaji wangu wafanye mazoezi kwa nguvu na kufuata kile ambacho nawaelekeza, kwani nimefurahi kupata ushindi kwa mechi zote tatu na ninahitaji kuendeleza ushindani. “Najua mchezo hautakuwa rahisi, kwani Singida United nao wamejipanga, hivyo watakabiliana nao kwa tahadhari ili kuhakikisha wanatoka na matokeo mazuri,” alisema. Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Singida United, Hemedi Morocco, alisema anahitaji kushinda mchezo huo ili kujiongezea pointi tatu. “Najua tunakutana na Yanga, ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja, tunajua ubora wao, lakini tumejipanga kuhakikisha  tunaondoka na ushindi katika mchezo huo. “Tunataka kuhakikisha tunapambana kushinda ili kumaliza hasira za kupoteza mchezo uliopita, tunajua ni timu yenye wachezaji wazuri, lakini kwetu sisi hatuangalii hilo, bali tunahitaji ushindi,” alisema Morocco. Mbali na mchezo huo, ligi hiyo itaendelea katika  viwanja vingine, Kagera Sugar itakuwa ugenini kuikabili Mbeya City, katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Azam FC pia itakuwa ugenini katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuikabili Alliance.
2
Na PETER FABIAN-MWANZA MBUNGE wa Misungwi Mkoa wa Mwanza, Charles Kitwanga, amesema ataondoa shilingi katika bajeti ya Wizara ya Maji ili kuishinikiza kutekeleza ahadi ya Rais Dk. John Magufuli ya kuupatia maji ya Ziwa Victoria mji wa Misungwi. Akizungumza na wananchi kutoka Kata za Fela, Koromije na Lubili wilayani humo, Kitwanga alisema amesikiliza kero za wananchi na kuwaomba wawe na uvumilivu wakati anajiandaa kuwasilisha hoja mbili binafsi ya njaa na maji kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea Mjini Dodoma. “Hii kero ya majisafi nimeisikia na imenigusa, inaninyima usingizi kutokana na jiografia ya Jimbo na Wilaya ya Misungwi kuwa na baadhi ya maeneo yenye ukame kila mara inafikirisha, lakini hili la kukosa maji kiasi cha wananchi kuhangaika na kuchangia maji na mifugo katika malambo linaumiza zaidi. “Lakini kwa hili ninaenda kuondoa shilingi kwenye bajeti ya Wizara ya Maji hadi wanipe uhakika wa maji katika wilaya hii, katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita, Rais Magufuli aliwaahidi wananchi kwamba suala la maji wasinisumbue akasema akichaguliwa kuwa rais maji yatafika Misungwi,” alisema. Alisema anakwenda bungeni na atakumbushia suala hilo ambapo asipopata majibu ya kuridhisha kuhusu kadhia wanayopata wananchi wake ataondoa shilingi katika bajeti hiyo. Mbunge huyo pia alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke, kushirikiana na wataalamu wake kupita vijiji vyote na kufanya tathmini upya ikiwamo kuvikagua visima vya majisafi ili kuona kama vinatoa maji na kama havitoi ili waweze kuanza mkakati wa kuvitengeneza ikiwa ni pamoja na kutafuta wafadhili wa kusaidia kupata visima vingine kusaidia kupunguza kero hiyo.
1
WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema litaanza kulipa madeni ya waamuzi kuanzia Jumatatu wiki ijayo, wakitumia fedha walizopokea kutoka Shirikisho la Sika la Kimataifa (FIFA). Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, wakati akitolea ufafanuzi mambo mbalimbali ya shirikisho hilo moja kwa moja kupitia mtandao wao. Kati ya mambo aliyozungumza kubwa ni kuhusu fedha walizopokea kutoka FIFA, ambazo zimekuwa zikijadiliwa na baadhi ya wadau wa soka kutaka kujua matumizi yake. Kidau alisema kati ya changamoto zitakazotatuliwa kupitia fedha hizo ni kulipa madeni ya waamuzi wanaodai kwa muda mrefu. Alisema waamuzi wakataolipwa kupitia fedha hizo ni wale wanaochezesha Ligi Kuu ya Wanawake, Ligi Daraja la Kwanza na la pili, huku wale wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakisubiri vyanzo vingine vya mapato. “Ndani ya wiki moja hii tumekuwa tukiangalia ukubwa wa madeni na jinsi gani tunaweza tukalipa, lakini niwahakikishie kuwa kwa kuanzia tutawalipa waamuzi wa Ligi ya Wanawake, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili. “Naamini malipo yataanza kufanyika Jumatatu kwa sababu tumeangukia wikiendi, hivyo kuanzia wiki ijayo kila kitu kitakuwa sawa,” alisema. Alifafanua kuwa kwa mwaka TFF inapata dola milioni moja sawa na bilioni 2.3 za Kitanzania  ambazo zinatolewa kwa awamu mbili, Januari na Julai. Kidao alisema kutokana na changamoto ya  janga la Corona, FIFA  imeamua kutoa mapema fedha hizo baada ya kubaini wanachama wake wameathirika na ugonjwa huo. “Fedha za FIFA huwa zinatoka endapo taasisi husika itakuwa imekidhi vigezo vinavyotakiwa, vigezo hivyo ni pamoja na vile vilivyoanishwa katika uendeshaji wa shughuli kwa kutumia fedha hizo,”alisema. Alieleza kuwa fedha zinazotoka Januari, mwanachama anatakiwa vigezo vya ukaguzi vya mwaka uliopita, tofauti na zinazotoka Julai. “Vigezo vingine tofauti na ukaguzi ni  lazima timu ya taifa  iwe imecheza mechi za Kimataifa zisizopungua nne, kuwe na timu za vijana mbili kila moja icheze mechi nne. “Pia timu za wanawake mbili, nazo zicheze michezo minne ya kimatifa kila moja, kuwepo Ligi za vijana, wanawake ambazo zitachezwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita,” alifafanua Kidao. Alisema pia zifanyike program za waamuzi zisizopungua 10 kwa mwaka, kingine kuhakikisha mwanachama ana mfumo wa usajili uliounganishwa na FIFA. Kuhusu kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema wanaendelea na vikao kuweka mipango sawa, huku wakisubiri kauli ya serikali. “Tangu kusimamishwa kwa Ligi, tumekua tukifanya kazi na serikali kwa ukaribu, kuangalia hali inaendaje pia tunatengeneza mipango kuona tutakapo ambiwa turudi tujue tunafanyaje,” alisema. Aliongeza kwa kusema, walipokea kwa furaha kauli ya Rais wa Tanzania, John Magufuli, kufikiria kurejesha Ligi kwa sababu hata FIFA imewaambia wadau wake kuwa kurudi kwa Ligi kutategemea na kauli ya serikali husika.
2
Na FERDNANDA MBAMILA SERIKALI inaendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwapatia huduma bora iwe za kiuchumi au kijamii kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Yote hayo yanafanikiwa kutokana uwapo wa taasisi imara za umma kama Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) ambalo wajibu wake ni kuhudumia wananchi kwa kutoa huduma bora huku likitambua umuhimu wa upatikanaji wa uhakika wa huduma ya maji. Ili kufanikiwa katika azma ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda, huduma ya uhakika ya maji ni nyenzo muhimu kwani itasaidia uwapo wa uhakika wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama vile uzalishaji wa umeme, viwandani na kwa matumizi ya kawaida ya binadamu. Kutokana na ukweli huo, Serikali ina malengo ya kuwapatia maji ya uhakika wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa jirani, Pwani, maeneo ambayo pia yana shughuli nyingi za kiuchumi kama vile viwanda na biashara nyingi na kubwa kubwa. Ili kuwa na uzalishaji wa uhakika viwandani huduma ya maji ni muhimu sana, jambo ambalo linaifanya serikali ya awamu ya tano kuipa umuhimu wa kipekee sekta hiyo. “Viwanda vingi, watu wengi wanahitaji uwepo wa huduma ya maji ya uhakika, hivyo juhudi za serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha maji yanapatikana kwa muda wote zitasaidia kujenga uchumi wetu,” anasema Juma Ali, Mchumi na mkazi wa Gongo la Mboto. Anasema wakazi wa jijini na maeneo mengine ya nchi yetu wanahitaji huduma ya uhakika ya maji ya bomba kwani huduma hiyo ni rahisi na pia salama kwa afya ya watumiaji. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Cyprian Luhemeja anasema amejipanga kikamilifu kuwatumikia wananchi lengo likiwa ni kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda na uchumi wa kati. Anasema uamuzi huo unalenga kuwawezesha wananchi ambao tayari walipoteza matumaini ya kupata maji kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama ya kuunganishiwa. “DAWASCO tumedhamilimia kuwajibika kikamilifu na kutimiza kauli mbiu ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ya “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani. “Tuko hapa kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania wote na kuhakikisha kwamba wanapata maji ya uhakika na salama kwa muda wote,” anasema Luhemeja. Mhandisi Luhemeja anatoa wito kwa wananchi ambao hawajaunganishiwa huduma hiyo kwenda katika ofisi za DAWASCO zilizoko karibu yao ili kupatiwa huduma hiyo. “Natoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na jirani zetu wajitokeze kwa wingi waweze kuunganishiwa huduma hiyo ili kila mtu afaidi matunda ya serikali yake bila kubughudhiwa,” anasema. Anasema yeye na timu yake wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu ili kuhakisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa wakati na uhakika. Anasema kwa kuchapa kazi mabadiliko yametokea kwani upatikanaji wa huduma hiyo umekuwa ni wa uhakika. “Dar es Salaam ilikuwa na uhaba wa maji, lakini baada serikali kubuni na kuanzisha miradi mikubwa ya maji, hali hiyo inaweza kuwa historia katika kipindi kijacho cha mwaka mmoja kuanzia sasa,” anasema. Anafafanua kuwa maji si tatizo isipokuwa watumiaji ndio tatizo -si maji bali watu. “Naweza kusema kuna baadhi ya watu kushindwa wenyewe kuomba kuunganishiwa huduma hiyo,” anasema. Anasema shirika lake limeimarisha kutoa huduma ya maji na kwamba kila siku lina uwezo wa kuzalisha lita milioni 483 jambo ambalo halikuwapo siku za nyuma. Mhandisi Luhemeja anasema awali Dar es Salaam ilikuwa ikitegemea vyanzo vikuu vya maji kutoka mitambo ya Ruvu Juu ambao kwa siku unazalisha lita milioni 82, Ruvu Chini unazalisha lita milioni 270. Mtoni unazalisha lita milioni 9 na visima virefu 106 ambavyo vinazalisha jumla ya lita milioni 106 kwa siku. Anasema vyanzo vyote hivyo huzalisha wastani wa lita milioni 371 kwa siku ambazo zilikuwa zikitosheleza asilimia 75 ya mahitaji ya wananchi ambapo sasa imeongezeka hadi zaidi ya asilimia 80. Kuhusu huduma ya maji taka, Luhemeja anasema imepiga hatua ya kuridhisha tofauti na awali kwani shirika lake limekuwa likikarabati miundombinu ya majitaka, hivyo kuweza kudhibiti kuvuja kwa baadhi ya mabomba. “Hali hii tumeidhibiti na kuepusha milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu na matumbo ya kuhara,” anasema Luhemeja. Hii inaonyesha dhahiri kuwa, maji yanayozalishwa bado hayatoshelezi wakazi wa mji huu lakini, Serikali inajitahidi kwa hali na mali, kuwasaidia wananchi wake kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama. Katika kutekeleza kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” ya Rais Dk Magufuli aliagiza kuwa, ifikapo Juni mwaka huu wateja 400,000 wa Dar es Salaam wawe wamepatiwa huduma ya maji safi na salama. Ili kutekeleza agizo hilo, DAWASCO imeamua kugharamia uunganishaji wa huduma hiyo kwa wakazi wake ambapo gharama hiyo ilikuwa ikilipwa na mteja mwenyewe. Akielezea utaratibu huo wa kugharamia uunganishaji wa huduma ya maji kwa wateja, anasema utakuwapo kwa kipindi maalumu cha miezi miwili. Anasema baada ya hapo mteja atawajibika kurudisha gharama za uunganishaji kidogo kidogo kila mwezi kwa muda wa miezi 12. Fursa hiyo imesaidia hata kwa wananchi wenye kipato cha chini kuweza kuunganishiwa huduma ya maji na hivyo kuepuka kunywa maji yasiyo na viwango ambayo ndio chanzo cha magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu. Malipo ya kuunganishiwa maji hayana riba bali mteja anahitajika kulipia gharama za uvutaji wa bomba kama zilivyoainishwa na utaratibu wa malipo unaunganishwa na bili ya kawaida ya maji inayopelekwa kwa mteja kila mwezi. Uondoaji wa kero ya maji umesaidia nguvu nyingine na muda uliokuwa unatumika kwa ajili ya kutafuta maji, kutumika kwa shughuli nyingine za uzalishaji mali. Sehemu nyingi za makazi ya watu katika jiji la Dar es Salaam, walikuwa wakipata huduma ya maji kwa kununua kutoka sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye visima, ambayo si salama kwa kunywa. Pia maji ya visima katika baadhi ya maeneo yana chumvi kiasi cha kufanya nguo zifubae na unywaji maji au matumizi katika mapishi kuwa magumu. Mbali na hilo, gharama ya kununua maji ilikuwa kubwa kuliko gharama ya chakula na wananchi wengi walikuwa wakitumia muda wao mwingi kuhangaika kutafuta maji jambo ambalo lilikuwa likikwamisha kutekeleza majukumu mengine ya kujenga nchi. Katika kero hiyo ya uhaba wa maji, waathirika wakuu walikuwa kina mama. Hivyo basi, mkakati wa DAWASCO wa kusambaza huduma ya maji safi kwa wananchi utasaidia kupunguza kero hiyo kwa kiasi kikubwa.  
5
NA MWANDISHI WETU MSHAMBULIAJI wa Yanga, Obrey Chirwa na kiungo wa Singida United, Deus Kaseke, wako huru kuendelea kuzitumikia timu hizo baada awali kusimamishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na tuhuma za kumfanyia  vurugu mwamuzi Charles Ludovic.   Chirwa, Kaseke na winga Simon ambaye kwa sasa anaichezea Difaa Al Jadid ya Morocco, walidaiwa kumfanyia vurugu mwamuzi huyo wakati wakiichezea Yanga, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita dhidi ya Mbao FC, uliofanyika Mei 21 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   Kamati ya Nidhamu ya TFF iliwasimamisha wachezaji hao kushiriki mashindano ndani ya Tanzania.   Katika mchezo huo, Mbao  iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kujinasua katika hatari ya kushuka daraja. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Peter Helam, akizungumza na  waandishi wa habari jana, alisema baada ya kupitia mkanda wa video wamejiridhisha Chirwa na Kaseke hawakutenda kosa.   Hata hivyo, alisema kamati hiyo imemtia hatiani Msuva kuwa ndio alihusika kumsukuma mwamuzi huyo, hivyo wamemwandikia barua na kumpa onyo kali. “Kamati ya nidhamu ya TFF imekutana jana kusikiliza shauri la wachezaji, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Simon Msuva. “Chirwa na Kaseke walikuwepo na walihojiwa kikaoni lakini Msuva hakuwepo, kupitia mkanda wa video kamati imejiridhisha kuwa hawakufanya kosa ila Msuva amepatikana na hatia,” alisema Helam. Kaseke alijiunga na Singida United wakati wa dirisha la usajili wa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kushindwa kuafikiana dau na Yanga. Tayari Kaseke na Chirwa wamekosa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.   Kufunguliwa kwa wachezaji hao kutaimarisha vikosi vya timu hizo katika ushiriki wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatabiriwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
2
Ramadhan ambaye pia ni mfanyabiashara wa bidhaa mbalimbali, pamoja na gari hiyo pia alijishindia zawadi kutoka Samsung ikiwa ni pamoja na kompyuta mpakato, mashine ya kufulia nguo, jokofu, simu ya Galaxy Tab 10.1, jiko la kupashia chakula, luninga ya LED 32’, deki ya DVD na muziki wa nyumbani zilizokuwa zimewekwa ndani ya gari hiyo.Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Sylvester Manyara alisema kwamba, lengo lake lilikuwa ni kujiweka karibu na wateja wao sambamba na kutoa elimu juu ya umuhimu wa bidhaa halisi ili kuwaepusha na hasara.“Pambika na Samsung ilikuwa ni promosheni ya wiki saba ambayo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi Novemba ikiwa na lengo kuu la kuwazawadia wateja wa Samsung wanaonunua bidhaa halisi za Samsung na kuzisajili kwenye mfumo maalumu wa dhamana.“Lakini si hilo tu bali ujumbe wa kampeni ulikuwa pia ukitoa fursa na kuwahamasisha Watanzania kuangalia uhalisia na uhalali wa bidhaa wanazonunua katika maduka mbalimbali ili kuepuka bidhaa zisizo na ubora,” alisema Manyara.Alisema katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi jana, mbali na kutoa elimu hiyo kwa wananchi mbalimbali pia wamewazawadia wateja 15 katika droo za kila wiki katika kipindi cha wiki saba kabla ya jana kutoa zawadi hiyo ya gari.
0
Simba inashika nafasi ya pili baada ya jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipokonya Azam pointi tatu baada ya kumchezesha Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano walipocheza dhidi ya Mbeya City.Simba kwenye msimamo ikiwa na pointi 58, katika michezo 26 waliyocheza itashuka dimbani Jumapili kuumana na Mwadui FC, ya Shinyanga.Akizungumza na gazeti hili, Mayanja alisema hana budi kuwapongeza Yanga kwa sababu mpira siyo vita na siku zote uadui wa soka upo ndani ya dakika 90 baada ya hapo watu wote watu hugeuka marafiki na kusahau yaliyotokea ndani ya mchezo.“Najisikia vibaya sana kuona malengo niliyotarajia kupata nikiwa na Simba msimu huu yapo ni vigumu kutimia, lakini sina budi kuwapongeza Yanga ambao ndiyo wanaoonekana kuwa katika nafasi nzuri ya ubingwa na hiyo inatokana na kazi nzuri waliyoifanya bila kujali upinzani wetu nao,” alisema Mayanja.Kocha huyo raia wa Uganda, alisema ingawa wapo katika matumaini madogo ya kubeba ubingwa lakini bado mikakati yao ni kushinda mechi zao nne zilizobaki ili angalau waweze kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili licha ya kwamba haina nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.Mayanja alisema kitu kizuri kwao ni kuona wanapambana hadi mechi ya mwisho bila kukata tamaa na mwisho wa msimu watajua wamemaliza wapi na kujitathmini mapungufu waliyokuwa nayo ambayo yalisababisha kushindwa kufikia malengo waliyojipangia.“Kama timu hatupaswi kukata tamaa, nimewaambia wachezaji wangu lazima tupambane hadi siku ya mwisho kuhakikisha tunashinda mechi zilizobaki ingawa nafasi ya ubingwa kwetu ni ndogo, lakini siyo mbaya hata tukimaliza nafasi ya pili kwani tunajiwekea rekodi nzuri kwa siku zijazo,” alisema.Mayanja ametua Simba mwishoni mwa mzunguko wa kwanza msimu huu akichukua nafasi ya Dylan Kerr, na aliweza kuibadilisha timu hiyo kwa kushinda mechi saba mfululizo na kufanikiwa kuongoza ligi lakini baadaye mambo yalikuwa tofauti katika mechi za mwishoni.
2
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna takwimu zisizo za kuridhisha za kiwango cha wananchi wasiotumia huduma za fedha za kibenki na jambo hilo linatokana na watoa huduma za fedha kutoa huduma zisizoendana na mahitaji halisi ya watumiaji wa huduma hizo.Alisema hayo jana mjini hapa wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki ya Biashara Mkombozi na kuongeza kuwa Tanzania imepiga hatua katika upatikanaji wa huduma jumuishi za kifedha, kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha ulifikia asilimia 65 wakati kiwango cha utumiaji wa huduma zisizo rasmi za kifedha ulipungua kutoka asilimia 29 hadi asilimia saba mwaka 2017.“Pamoja na mafanikio haya, bado takwimu si za kuridhisha kwani kiwango cha wananchi wasiotumia huduma za fedha bado ni kikubwa, kwa mujibu wa utafiti wa Finscope wa mwaka 2017, asilimia 28 ya Watanzania hawatumii huduma za fedha, sehemu kubwa ya hao ni wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, wakulima wadogo, vijana na wanawake,” alisema.Samia alisema utafiti huo ulibainisha changamoto kubwa ni ya watoa huduma za fedha kutoa huduma zisizoendana na mahitaji halisi ya watumiaji. “Watoa huduma za fedha kwenye mabenki wanatoa huduma zisizoendana na mazingira halisi, jitihada za mabenki kwenda kushawishi watu wajue watu wana changamoto ya kuelewa lugha ikiwezekana mtumie hata lugha zao za asili ili kukuza uelewa wao, mnawashawishi watu wanapokuja kufungua akaunti wanakutana na fomu yenye lugha ya kiingereza, kuna haja ya kuzingatia lugha mnapokwenda kushawishi watu,” alisema.Makamu wa Rais alisema pia bado kuna changamoto kubwa ya kuwafikia na kuwashawishi Watanzania hususan walio maeneo ya pembezoni mwa miji na vijiji kutumia huduma za fedha za kibenki.Aliwataka kuendelea kutumia tafiti mbalimbali kubuni huduma ili ziendane na mahitaji halisi ya wananchi walio wengi. Alisema benki hiyo ilianza kufungua tawi la kwanza jijini Dar es Salaam ikiwa ni miaka 10 sasa na imeendelea kupanua wigo na shughuli zake kutokana na kuendelea kukua na mtaji wake kutoka ule wa Sh bilioni sita mwaka 2009 hadi kufikia Sh bilioni 20 mwaka 2019 na kuiwezesha benki kufungua matawi mbalmbali nchini.Naibu Waziri wa Fedha, Ashatu Kijaji alisema serikali inasimamia sekta ya fedha ili kuchochea uwekezaji na kuhakikisha benki za biashara zinakuwa na ukwasi wa kutosha ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Thomas Enock alisema benki hiyo imebeba dira ya benki itatoa huduma za kibenki zenye suluhisho sahihi kiuchumi kwa jamii pana hapa nchini.“Leo benki inafungua tawi hili likiwa ni tawi la 10, benki imepata mafanikio ya kuridhisha katika kipindi kifupi ambapo imepokelewa vyema na wananchi wa kada zote, wameendelea kujipatia huduma za kibenki kutoka viunga vyote vya Jiji la Dodoma,” alisema. Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Profesa Marcelina Chijoriga alisema tangu kufunguliwa kwake benki hiyo imetoa fursa mbalimbali kwa jamii na taifa kwa ujumla.
2
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
0
LAGOS, Nigeria STAA wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘WizKid’ amefanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya Sony Music kwa ajili ya kusimamia kazi zake za muziki. Dili hilo limekuja mara baada ya msanii huyo kufanya vizuri katika muziki nchini humo na duniani kote, hasa kutokana na kazi ambayo ameifanya na Drake, wimbo ambao unajulikana kwa jina la "One Dance". Mkataba huo utamfanya msanii huyo kusimamiwa kazi za albamu zake duniani kote kama ilivyo kwa wasanii wengine ambao wamefanya kazi na kampuni hiyo ambao ni Chris Brown, John Legand, Tyga na wengine wengi. “Ni ngumu sana kwa upande wangu kuamini kile ambacho ninakifanya, lakini ninaamini watu wanaona na ndiyo maana wananipa dili kubwa, nawashukuru sana Sony pamoja na RCA Records kwa kunipa dili la kusimamia kazi zangu, kikubwa ni kuzidi kukazana ili niweze kufika mbali zaidi,” alisema WizKid.
4
RAIS wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani barani Afrika( AGRA), Dk Agnes Kalibata ametaka elimu zaidi kutolewa kwa wakulima, ili kufanya kilimo cha ushindani kitakachohimili mabadiliko ya soko duniani. Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea maeneo ya mradi wa kuwaleta wadau wa kilimo katika jukwaa moja la Ihemi-Ludewa, wakiwamo wakulima, wauza pembejeo na wanunuzi wa mazao ya wakulima.Ziara yake hiyo ambayo ameifanya baada ya mkutano mkubwa ulioshirikisha mataifa 11 yanayowezeshwa na AGRA katika miradi mbalimbali, uliofanyika mjini Iringa, alisema kwamba bila kuwaandaa wakulima, watakuwa wanakata tamaa na kuona kilimo chao hakilipi. Wataalamu walioshiriki mazungumzo hayo kutoka katika makundi ya wakulima, wafanyakazi wa serikali kutoka nchi hizo 11 zikiwemo za Tanzania, Msumbiji, Mali, Burkinafaso, Ghana, Nigeria, Ethiopia na Rwanda walikiri kwamba ipo haja ya watu wa masoko kuifanya zaidi ili kushawishi ukuaji wa kilimo.Akizungumza baada ya kutaka kununua soya kutoka kwa mkulima, Victory Mhanga wa Magulilwa Halmashauri ya Iringa, mkoani Iringa ambaye alitaka kumuuzia bei ya Sh 2,000, Dk Kalibata alisema kwamba bei hiyo ni kubwa kulinganisha na soya inayolimwa Brazil. Aidha wataalamu wa masoko waliokuwapo katika ziara hiyo walisema kwamba bei ya juu ilikuwa Sh 800 katika mnada wa Songea uliofanyika hivi karibuni, ingawa bei ya rejareja Dar es Salaam ni Sh 2,500.Alipouliza zaidi sababu ya bei hiyo kubwa wakati katika Soko la Dunia ni dola za Marekani 0.63, aliambiwa kwamba mkulima huyo anauza kwa nguvu ya soko inayomzunguka na kwamba hana tatizo la soko katika eneo lake.
0
Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM WADAU wa habari nchini wamepinga hatua ya Serikali kupitia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kulifungia gazeti la kila wiki la Mawio kwa muda wa miezi 24. Wameitaka Serikali kutengua  uamuzi wake wa kulifungia gazeti hilo kwa vile  umekwenda kinyume na Katiba ya nchi  na Sheria ya Huduma kwa Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambayo haimpi mamlaka ya kufungia chombo cha habari waziri mwenye dhamana. Wakizungumza   na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, wadau hao kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania (UTPC), walisema   kufungiwa kwa vyombo vya habari si mara ya kwanza licha ya sheria kutotoa fursa hiyo. Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo, alisema si mara ya kwanza kwa waziri mwenye dhamana kutumia sheria kandamizi ikiwamo ya Magazeti ya mwaka 1976 iliyofutwa mwaka 2016 na kuridhiwa na sheria ya huduma za vyombo vya habari ya 2016. Alisema kwa mujibu wa kumbukumbu,   baadhi ya magazeti  yaliyowahi  kufungiwa ni Mwananchi, Mawio, Mwanahalisi na Mtanzania huku   Mawio ikiwa ni mara ya pili. Alisema Januari 15, mwaka jana gazeti la Mawio lilipigwa marufuku  na kuamua kuishitaki Serikali kwa kufungua kesi mahakamani  na hatimaye lilishinda kesi. “Itambulike  kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukipinga utaratibu wa  sheria wa kumpa Waziri mamlaka makubwa katika sekta ya habari   kulifungia gazeti   kwa makosa atakayoyaona yeye kwa sababu ni kinyume na maslahi ya umma. “Sheria hii mpya imeendelea kumfanya waziri awe Mhariri Mkuu, mlalamikaji, mpelelezi, mwendesha mashtaka na hakimu kwa wakati mmoja,’’ alisema Nsokolo. Mratibu wa   Mtandao waWatetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),  Onesmo Olengurumwa, alisema  kifungu kilichotumika kulifungia gazeti hilo, cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari kwa madai ya kuchapicha picha za viongozi wastaafu, ni kinyume na maslahi ya umma. Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania Watanzania wana uhuru wa kutoa maoni na kupashana habari kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao. Pia alisema kitendo cha kuzuia watanzania au vyombo vya habari visichapishe picha za viongozi wastaafu hasa katika mijadala ya taifa ambayo inahusu mambo yaliyotekea wakiwa madarakani ni kuwaziba watanzania midomo katika suala  la vita dhidi ya wizi wa madini . Katika kosa la pili gazeti hilo lilitumia makala ya mbunge mmoja na mtaalamu wa sheria za madini nchini yenye maelezo juu ya mambo muhimu katika kumsaidia Rais katika vita dhidi ya uporaji wa rasilimali madini. “Tumeshangazwa kuona waziri ambaye kwa taaluma ni mwanasheria ametumia agizo la rais kama sheria kitendo ambacho ni hatari kwa mustakabali wa taifa… kama kila kitakachoagizwa na kiongozi mkuu kitachukuliwa kama ni sheria. “Hata hivyo kwa mujibu wa Mawio, agizo la rais kuhusu kuzuia marais wastaafu wasitajwe au kujadiliwa kwenye suala la madini, lilitoka wakati tayari gazeti hilo  limekwisha kuchapishwa na kusambazwa kwa mawakala nchi nzima,’’ alisema Olengurumwa. Kaimu Katibu Mtendaji  Baraza la Habari Tanzania (MCT),  Pili Mtambalike aliitaka Serikali itengue uamuzi wake wa kulifungia gazeti la Mawio kwa sababu ni   kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  a na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 ambayo kimsingi haimpi mamlaka waziri kutoa adhabu aliyoitoa. Alisema juhudi  za Serikali katika kuhakikisha uchumi unakua   na kupambana na rushwa lazima ziende sambamba na viongozi kuwa wavumilivu na kukubali kukosolewa kwa  mambo ambayo ni muhimu katika kufikia malengo na matarajio.
1
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza viongozi wa Jiji hilo kukamata mifugo yote inayozurura hovyo makazi ya watu na kuwatoza faini wamiliki.Aliagiza hayo baada ya kukutana na makundi ya ng’ombe wakizagaa hovyo kwenye makazi ya watu kwenye mitaa jijini humo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa.Alisema hivi sasa Dodoma ni Jiji linatakiwa kuwa safi na mazingira yake kutunzwa bila kuharibiwa na mifugo, hivyo viongozi wa jiji wanatakiwa kuhakikisha hakuna mifugo inayofugwa hovyo katika makazi ya watu.“Kama kuna mtu anataka kufuga mifugo lazima awe na banda la kulishia mifugo hiyo ndani, badala ya ufugaji huo wa kutembeza mifugo hiyo kwenye makazi ya watu,” alisema.Alisema ni marufuku kuendesha ufugaji wa mifugo katika makazi ya watu, barabarani na maeneo mbalimbali kwani linatakiwa kuwa safi.Dk Mahenge alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Petrobas Katambi kukamata mifugo na kuwatoza faini wanaofugia makazi ya watu kwa kutumia sheria ndogo za halmashauri ya Jiji zinazoruhusu kukamata mifugo na kuchukua hatua dhidi ya wanaofugia makazi ya watu.Mkuu wa Wilaya, Katambi aliyekuwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Hidaya Maeda waliahidi kutumia sheria ndogo kuwachukulia hatua wale wote wanafugia mifugo katika makazi ya watu.Katambi amesema wanalichukulia agizo hilo la Mkuu wa Mkoa kwa uzito mkubwa na hivyo watatumia sheria ndogo katika kukamata mifugo yote inayofugwa makazi ya watu.
1
Na ELIUD NGONDO – SONGWE WANANCHI wa Vijiji vya Ndalambo na Mengo, Kata ya Ndalambo wilayani Momba mkoani Songwe, wamewataka wanasiasa kutekeleza kile walichoahidi kwenye kampeni zao.   Wananchi hao wameeleza msimamo huo jana mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Momba, Twaha Masoud, kwenye mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea udiwani wa CCM, Flavian Sichizya.   Walisema wanayo kero kubwa na ya siku nyingi ya kupata maji safi na salama ingawa waliahidiwa kutatuliwa kero hizo na wanasiasa, huku wakisisitiza kuwa hadi sasa hakuna ahadi yoyote iliyotekelezwa na viongozi waliopo madarakani.   Osea Mgala, mkazi wa Kijiji cha Ndalambo, alisema wanakatishwa tamaa na viongozi ambao hawatekelezi ahadi zao kama ambavyo waliahidi wakati wakitafuta madaraka ya kutawala.   “Wanasiasa walitoa kauli ya kuaminiwa lakini hadi sasa hakuna hata dalili ambazo zinaonyesha kutekelezwa kwa ahadi hizo, tunaendelea na shida zetu za kukosa maji safi na salama ambacho ndicho kilio chetu,” alisema. Godfrey Mwanguku alisema katika vijiji hivyo wameshindwa hata kufanya shughuli za maendeleo kutokana na shida ya upatikanaji wa maji. Akijibu hoja hizo, Masoud alisema wananchi wanatakiwa kuwaamini viongozi wanaotumia Katiba ya chama kuahidi na si wanaotumia majukwaa pekee. Alisema mwanasiasa akitumia katiba ya chama ni rahisi kutekelezwa ahadi alizoziahidi kutokana na utaratibu ulivyo, lakini wale wanasiasa ambao huongea majukwaani bila kuwa na Katiba ni waongo. “Ukitoa ahadi kwa wananchi kwa kuongozwa na katiba ya chama chako lazima utaitekeleza tu, kwani sheria itakubana lakini kama hakuna katiba yoyote ni rahisi kudanganywa na kutochukuliwa hatua yoyote,” alisema Masoud.   “Wananchi wanatakiwa kuiamini CCM kutokana na kuongea mambo ambayo yameandikwa ndani ya Katiba yake, hivyo kuna baadhi ya vyama havina hata katiba hali ambayo wananchi hawawezi kuvibana,” alisema Masoud.
1
Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Joackim Tiganga amewataka mahakimu wanawake nchini kutambua masuala ya msingi yanayosababisha ukiukwaji wa maadili na mgongano wa maslahi na kutakiwa kuchukua tahadhari kubwa.Tiganga amesema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mahakimu wanawake wa jiji la Dar es Salaam na kuongeza kuwa idadi ya wanawake wanaotoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa maadili ni asilimia moja tu.Kuhusu mgongano wa maslahi amesema suala hilo ni nyeti na pana na sio Tanzania peke yake ambayo inakabiliana na changamoto ya tatizo hilo, bali ulimwengu mzima na hata nchi kubwa zilizoendelea.“Tatizo la mgongano wa maslahi lina athari kubwa kwa maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, hutokea pale ambapo kiongozi mwenye dhamana anapofanya maamuzi na kutumia nafasi yake kwa maslahi yake binafsi au ndugu ama jamaa,” alisema.Alisema maamuzi yanapofanywa kulinda maslahi ya mtu fulani ni wazi hatua hiyo ni kujiingiza katika mgongano wa maslahi.Mafunzo hayo yameandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Tiganga alisema mgongano wa maslahi husababisha watu kukosa haki na fursa sawa hivyo jambo hilo lisipodhibitiwa linasababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya utoaji haki.“Tunaambiwa haki isitendeke tu bali ionekane kuwa imetendeka, kiongozi mwadilifu lazima azingatie huu umuhimu wa utoaji haki,” alisema na kuongeza kuwa katika mafunzo hayo wataweza kuelekezwa namna ya kupunguza uwezekano wa uwepo wa mgongano wa maslahi katika maeneo yao ya kazi.Alisema ni vyema kiongozi kuepuka hali hiyo na kufanya uamuzi kwa kuzingatia matakwa ya sheria zinazohusika bila upendeleo na ubaguzi ili kujenga Taifa lenye maendeleo endelevu kwa wote.Kuhusu mafunzo hayo kwa Mahakimu wanawake, alisema utafiti wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwaka 2015, unaonesha wanawake wanaotoa taarifa za ukiukwaji maadili ni asilimia moja.“Idadi hiyo ni ndogo, tutumie vyema fursa hii ya mafunzo ili kuwa chachu ya kuongeza idadi ya wanawake wanaoshiriki katika kukuza na kusimamia maadili nchini,” alisema Tiganga.Alisema mafunzo hayo kwa Mahakimu wanawake inalenga kujenga msingi wa uzingatiaji maadili na kuwawezesha viongozi kutojiingiza katika masuala ambayo yanakiuka sheria.Tiganga alisema mafunzo yanawawezesha kuelewa misingi ya tabia na mwenendo wa kimaadili kwa viongozi wa umma unaokubalika katika utendaji kazi za umma unaopaswa kuzingatiwa, huku Mahakama za Tanzania zikiwa katika kampeni ya kuhubiri na kusimamia maadili kwa viongozi na watumishi wake.Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha, alisema wanawake wanaojihusisha na kutoa taarifa za maadili ni wachache, hivyo wanajengewa uwezo wasaidie kukuza maadili na kuongeza idadi ya wanawake wa kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa maadili.Alisema mafunzo yanawataka kuwa mabalozi, sehemu zao za kazi ili kuongeza wigo wa wanawake kushiriki ipasavyo katika kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili.
1
Hitmaker wa UNO Harmonize amesema kuwa yupo tayari kufanya kazi na msanii yoyote ndani na nje ya nchi hata Ali Kiba ambaye ni mpinzani mkubwa wa aliyekuwa na bosi wake wa zamani wa label ya WCB, Diamond Platnumz Harmonize ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake na wandishi wa habari wakati anatambulishwa kuwa balozi wa kinywaji cha Sayona kinachozalishwa hapa nchini “Mimi ni msanii naweza kufanya kolabo na msanii yoyote Sina shida wala tatizo na msanii yoyote ndo maana nasema konde boy is for everybody, na nadhani kitu kinachoinua muziki wa afrika magharibi ni kolaba, siraha pekee itayo inua muziki wetu ni kufanya kolabo sisi kwa sisi“ amesema Harmo
4
WASHIRIKI zaidi ya 800 kutoka asasi za kiraia zaidi ya 400, wanatarajia kushiriki Maonesho katika Wiki ya Asasi za Kiraia, ambayo yanatarajia kufunguliwa leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Wiki ya Asasi za Kiraia inatarajia kuanza leo jijini Dodoma hadi Oktoba 26, mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation For Civil Society, Francis Kiwanga amesema lengo la maonesho hayo ni kuonesha mafanikio yao katika maendeleo ya Taifa na kuona namna asasi za kiraia zitachagiza azma ya serikali ya Tanzania ya Viwanda.Alisema kuwa The Foundation For Civil Society imepata mafanikio mengi hapa nchini katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.Alisisitiza kuwa asasi nyingi zimefanya vizuri na kutimiza malengo ya kusaidia jamii.Alisema katika maonesho hayo, pia wataangalia namna gani wanaweza kushiriki katika kuchangia mkakati wa Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025.“Pia tutatumia wiki hii kuwa karibu na viongozi wa Serikali, Bunge, Taasisi Binafsi na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu nini tunafanya na kuondoa dhana ya kuwa asasi za kiraia zipo kwa ajili ya manufaa binafsi,” alisema.Kiwanga alisema kwenye maonesho hayo, watatoa elimu kwa umma na kufanya midahalo inayolenga ushirikishwaji wa wananchi na asasi za kiraia katika Tanzania ya viwanda.“Tunalenga kutoa nafasi kwa sekta ya asasi za kiraia kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki kwenye juhudi za serikali na wadau wengine za kujenga uchumi wa viwanda.“Pia tunalenga kuhamasisha ujenzi wa jamii inayoheshimu haki za watu na kuwashirikisha raia wake katika michakato ya mustakabali wa maisha yao,” alisema.Mratibu HakiRasilimali, Rachel Chagonja amesema, kutakuwa na utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya mafuta, madini na gesi na kuangalia namna ya rasilimali hizo zitakavyosaidia kufikia azma ya viwanda hapa nchini.“Tumeona baadhi ya nchi rasilimali hizi badala ya kuwaletea manufaa wameingia kwenye migogoro, sasa ni lazima tuangalie manufaa yake hasa katika kufikia Tanzania ya viwanda na pia kuhakikisha nchi haiingii kwenye matatizo kama yalivyo nchi zingine,” alisema.
1
Na ELIYA MBONEA -ARUSHA USHIRIKINA na ulevi unaochangia watu kutokuwa makini kwenye mgodi wa Moramu uliouwa watu watatu na kujeruhi wanne, unadaiwa kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea kwa miaka tofauti nyakati za Pasaka. Mwaka 2013 siku ya Jumatatu ya Pasaka machimbo hayo yaliuawa watu 13, na Aprili 23, mwaka huu ajali hiyo imetokea tena ikiwa ni   Jumanne, siku moja baada ya Jumatatu ya Pasaka.  Baadhi ya mashuhuda na wakazi wa eneo hilo waliliambia MTANZANIA jana kwamba zipo sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia machimbo hayo kuendelea kuua watu vikiwamo ushirikina na ulevi. Mkazi wa Sekei Moivaro tangu mwaka 1976, Zelothe Mollel alisema  wameshangaa kuona tukio la ajali kwenye machimbo hayo likitokea Sikukuu ya Pasaka.  “Ajali ya mwaka 2013 ilitokea siku ya Pasaka ya Pili (Jumatatu ya Pasaka) na ajali ya juzi tena imetokea Jumanne siku moja baada ya Jumatatu ya Pasaka. “Tukio hili lingetokea Jumatatu ya Pasaka ila tu kwa sababu kuliwekwa sheria hapa kwamba siku za mapumziko mgodi huwa unafungwa hakuna kufanya kazi, “Jumatatu ya Pasaka hawakuingia, Serikali haiamini nguvu za giza lakini wananchi tunaamini kuna nguvu za giza ziko hapa. Kwa nini kila Pasaka damu za watu zinamwagika hapa?     “Hawa waliofunikwa walishindwa kukimbia manake unaweza kukuta mtu kalewa jana yake hivyo kukimbia haraka akawa ameshindwa,” alisema Mollel.   Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqarro akizungumzia mazingira na usalama wa eneo hilo, alisema umewekwa ulinzi mkali kwenye machimbo hayo  kuzuia watu wasiendelee kuchimba.  “Miili ya marehemu watatu ilipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa taratibu nyingine ambako gari liliharibika kabisa,” alisema DC Daqarro na kuongeza: “Kikao cha Kamati ya Usalama ya wilaya cha dharura kitakaa na kujadili juu ya mchimbo yaliyopo wilayani kwetu ambako wataalamu wa madini watashiriki kujadili kwa kina na kuona nini kifanyike”.
1
MANCHESTER, ENGLAND KLABU ya Manchester United, inaongoza kwa utajiri katika klabu za nchini England, huku thamani yake ikiwa imeongezeka kwa asilimia saba tofauti na msimu uliopita. Kwa mujibu wa jarida la Forbes, klabu hiyo imeendelea kuongoza kwa utajiri ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.32, sawa na pauni bilioni 2.52. Hata hivyo, hii ni kwa upande wa nchini England, lakini katika soka klabu ambayo inaongoza duniani kwa utajiri ni klabu ya Real Madrid, yenye thamani ya dola bilioni 3.65 sawa na pauni bilioni 2.77, ikifuatiwa na Barcelona yenye thamani ya dola bilioni 3.55 sawa na pauni bilioni 2.67. Hata hivyo, klabu ya mchezo wa NFL ya nchini Marekani, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake duniani ikiwa ni dola bilioni 4 sawa na pauni bilioni 3.03. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi soka kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011. Inadaiwa kwamba utajiri wa klabu ya Manchester United imezidi kuongezeka mara baada ya kusaini mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, ambao ulikuwa na thamani ya pauni milioni 750. Chakushangaza ni kwamba, Manchester United ina fedha nyingi lakini imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
2
ZIKIWA zimebaki siku 97 kukamilika kwa muda uliotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili wananchi kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mbinu za kufanikisha kazi hiyo. Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ihakikishe wananchi hasa walioko vijijini wanapata angalau namba za utambulisho wa usajili wao kabla ya muda wa usajili wa laini za simu haujamalizika. Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Hospitali ya Wilaya ya Geita iliyopo kwenye Kijiji cha Nzela. Alisema kuwapatia namba za utambulisho wa usajili wananchi ambao hawajapata vitambulisho vya uraia kutawasaidia kuingia katika orodha ya wanosubiri kusajiliwa hata muda wa usajili ukiisha. Mwisho wa muda wa usajili ni Desemba, mwaka huu. Alisema serikali imewapa NIDA vifaa vya kisasa vya kielektroniki ili wafanye kazi zao kwa haraka na ufanisi, lakini hali hairidhishi kwani wananchi wengo hawajapata vitambulisho na kasi ya usajili wa laini za simu inalalamikiwa katika meneo mengi. “NIDA mnalalamikiwa, nimeenda Morogoro Vijijini NIDA mnalalamikiwa hivi utendaji wenu ukoje? Kwa nini mnachelewa ?” alimuuliza Ofisa Msajili wa NIDA Wilaya ya Geita, Paschal Saro aliyejibu wamesajili laini za simu 340 na namba za usajili 330 zimeshatolewa. Saro alimwambia Waziri Mkuu utata wa uraia kwa baadhi ya wananachi wanaoomba vitambulisho vya NIDA ni moja ya sababu zinazochelewesha usajili wa vitambulisho. Waziri Mkuu, Majaliwa aliwasihi wananchi wote kuwa walinzi wa nchi yao kwa kutoa taarifa za watu wanaomba vitambulisho vya uraia wa Tanzania wakati si raia. Aliwataka watoe taarifa mara moja kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuwa kuna raia wa nje wanafanya mchakato wa kupata vitambulisho hivyo. Alisema katika baadhi ya mikoa ya mipakani yenye wakimbizi, Serikali imekamata silaha ambazo raia hawaruhusiwi kuzimiliki, zimeletwa na raia wa nje wasio waaminifu.Hali ilivyo hadi sasa Licha ya watu zaidi ya milioni 44.2 kutumia simu nchini, hadi Agosti, mwaka huu watu milioni 5.2 sawa na asilimia 12 ndio waliosajili laini kwa mfumo wa alama za vidole. Pamoja na kusalia miezi mitatu ya kukamilika usajili mpya, watu 39,035,916 ambao wanatumia simu hawajasajili laini zao katika mfumo huo wa kielektroniki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upatikanaji Vitambulisho vya Taifa na kusubiri mwishoni. Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mkuu wa Mawasiliano wa TCRA, Frederick Ntobi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usajili kwa njia ya alama za vidole kati ya kampuni za mitandao ya simu na TCRA. Ntobi alisema tangu kuanza kwa usajili huo Mei Mosi, mwaka huu, ni Watanzania 5,222,721 waliosajiliwa huku wanaotumia simu ni watu 44,258,637. Alisema takwimu za watu waliojisajili wamezipata kupitia kwa watoa huduma wa mitandao mbalimbali ya simu nchini. Pia alisema kutokana na uchache wa watu waliojisajili, kampuni za simu zimeahidi kuongeza vifaa na kuvisambaza wilayani usajili ufanyike kwa ufanisi kufikia malengo.“Kwa sasa usajili huu unaendelea katika maduka yote ya watoa huduma za mawasiliano na mawakala wenye vitambulisho maalum. Tunapenda kutaarifu umma kuhakikisha watumiaji wote wa mawasiliano wanasajili upya laini za simu kwa mujibu wa sheria kwani baada ya Desemba 31, mwaka huu laini zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa hazitaruhusiwa kutumika,” alisema Ntobi.Alieleza TCRA iliboresha kanuni za usajili ili kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi, kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli nyingine za usimamizi.
1
Mchezaji huyo pia jana alionekana kwenye mazoezi ya Simba yanayofanyika kwenye uwanja wa Sigara ingawa alikuwa akijificha ndani ya gari bila kujitokeza kwa mashabiki waliozingira gari hilo.Kiiza, ambaye aliachwa msimu uliopita na Yanga na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji wa Liberia Kpah Sherman, amesajiliwa kama mchezaji huru kwani hakuwa na timu yoyote baada ya kutemwa na vijana hao wa Jangwani.Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana msemaji wa Simba, Haji Manara alisema Kiiza kwa sasa ni mchezaji wao kwa vile wamekwishampa mkataba wa miaka miwili.“Kiiza amefuzu vipimo leo mchana (jana) kwa hiyo tumempa mkataba wa miaka miwili, ni mchezaji wetu halali, tunategemea atakiongoza kikosi cha Simba kufanya vizuri msimu ujao,” alisema.Aidha, katika uwanja wa Sigara Kiiza alijitokeza huku mashabiki wa Simba wakionesha shauku ya kutaka kumsalimia lakini alijificha katika gari bila kushuka na baadaye alisalimia huku akiwa ndani ya gari bila kushuka.Kwa mujibu wa mtandao wa Simba, Kiiza alisema amekuja na kitu tofauti kwa ajili ya wapenzi na wanachama wa klabu hiyo na hivyo wakae mkao wa kula kwa vile anaijua vizuri ligi ya Tanzania.“Nitashirikiana na wachezaji wenzangu kufikia malengo ya kutwaa ubingwa msimu ujao,”alisema.Wakati huo huo, Simba inatarajia kuweka kambi Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Simba, Collin Frisch alisema kambi hiyo wataitangaza wakati wowote na kwamba lengo ni kuhakikisha timu inajipanga na kufanya vizuri msimu ujao.
2
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amedai kuwa aliwahi kuambiwa na nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann, kuwa hampendi hata kidogo. Wawili hao walikutana katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Euro 2016, ambapo timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kutwaa taji hilo mbele ya wenyewe Ufaransa kwenye uwanja wa nyumbani. Ronaldo na Griezmann kila mmoja alitarajia kuisaidia timu yake lakini Ronaldo alifanikiwa kutoa mchango mkubwa ndani ya uwanja hadi nje, mara baada ya kutoka katika dakika 45 za kipindi cha pili kutokana na kusumbuliwa na goti ambapo mchango wake ulikuwa kama kocha. Ronaldo baada ya kuchukua ubingwa huo, alikwenda Miami nchini Marekani kwa ajili ya mapumziko, hivyo alikutana na Griezmann katika mgahawa akipata chakula na rafiki zake na ndipo mchezaji huyo aliinuka na kumfuata Ronaldo na kumwambia kuwa anamchukia. “Lilikuwa jambo la kufurahisha,” Ronaldo aliambia France Football. “Kwa sababu muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016, nilikwenda Miami kwa ajili ya mapumziko, nilikutana na Antoine Griezmann kwenye mgahawa akiwa na rafiki zake wakipata chakula. Alikuja hadi nilipo, huku akiwa anatabasamu na kuniambia Cristiano, nakuchukia,’ alisema Ronaldo. Hata hivyo, mchezaji huyo alikumbushia jinsi alivyojisikia baada ya kuumia katika mchezo huo wa fainali dhidi ya Ufaransa. “Nilikuwa katika wakati mgumu sana kwa kuwa nilikuwa na lengo la kuisaidia timu ila baada ya kuumia, nilijikuta ninalia kwa kuwa niliamini ndoto zangu za kuisaidia timu hiyo zimefikia mwisho baada ya kuisi maumivu makali, lakini daktari wangu aliniambia sijaumia sana,” aliongeza.
2
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM KUMRUSHA mtoto darasa kwa kisingizio kwamba ana uwezo mkubwa ni jambo la hatari na linaweza kuharibu akili yake kadri anavyoendelea kukua na kupanda darasa, imeelezwa. Mratibu na Mkufunzi wa Taasisi ya kutetea haki za watoto ya Tukumbushane Society, Celvin Shola aliwashauri wazazi  kuacha kuwapangia walimu darasa gani watoto wao wasome  kuondoa uwezekano wa kuwavuruga watoto wao kiakili. Alikua akizungumza kwenye  semina kuhusu mitaala mipya ya elimu ya awali kwa walimu wa shule za msingi wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Alisema hata kama mtoto ana kipaji na uelewa wa haraka si jambo jema kumrusha darasa ambalo si lake kwa sababu kila umri una tabia yake. “Tabia hii ya kuwarusha watoto darasa kwa kisingizio kwamba wana akili sana imeshamiri katika shule hizi za English Medium (shule zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza), huko baadhi ya wazazi wanapanga watoto wao wasome nini, waingie darasa lipi. “Kisaikolojia akili ya mtoto inatakiwa kusoma vitu vinavyoendana na umri wake, hata kama mtoto yuko darasa la kwanza na ana uwezo wa kufanya mtihani wa darasa la tatu na zaidi, tuwashauri wazazi wasione kurusha mtoto darasa ni jambo la sifa, mwisho wake si mzuri.”alisema Shola bila kufafanua.   Kuhusu elimu ya awali, Shola ambaye pia ni mkufunzi wa taasisi hiyo, alisema kwa kuwa Tanzania haikuwa na sera maalum na iliyokuwa  wazi kuhusu elimu ya awali, imejikuta hata walimu wa kufundisha elimu hiyo hawapo au ni wachache.   Alisema walimu wengi nchini hawajapitia taaluma ya namna ya kufundisha elimu ya awali matokeo yake  watoto wengi wanakosa haki ya msingi ya kujengwa  akili kuanzia ngazi hiyo. “Katika maeneo mengi ya vijijini elimu ya awali inafundishwa na walimu wenye umri mkubwa ambao wamestaafu au wanakaribia kustaafu na hawaendani kabisa na sifa zinazotakiwa katika kufundisha watoto wenye umri mdogo. “Watoto wa awali lazima watumie muda mwingi kucheza na kuimba, kuchora na vitu vingi vya kuwafanya wapende shule, sasa huyu mtu mzima atawezaje vitu hivi? Anaweza kuruka kamba au kukimbia na hawa watoto?“ alihoji Shola.
1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, watu waliokufa jana baada ya lori la mafuta kulipuka mjini Morogoro wameungua sana na huenda baadhi yao hawatatambulika.Amesema, miili ya marehemu hao itazikwa leo jioni baada ndugu, jamaa na waombolezaji wengine kupita kuona kama wataweza kuwatambua marehemu.Waziri Mkuu amesema mjini Morogoro kuwa tukio la jana si jambo dogo na kwamba, Serikali imeona ni busara kutoa nafasi kwa wananchi kupita mbele ya miili ya marehemu kuitambua kabla ya kuwazika.Amesema, hadi saa 10 jioni leo wananchi watakuwa na fursa ya kuitambua miili hiyo na baada ya hapo ataungana na waombelezaji kwa dua na sala kisha watakwenda makaburini.“Lakini kuanzia saa kumi sasa tutaruhusu wale waliotambuliwa na ndugu kuwapa nafasi ndugu ya kuamua kubeba mwili kupeleka nyumbani. Lakini hatukuzuii kama hamjajipanga vizuri kule nyumbani na ukaridhia kwenda kuzika huko huko. Basi tutauchukua mwili huo na wewe ukijua ndugu yangu ni huyu tutakwenda kumzika kwa pamoja kwa sababu kila mmoja tumeandaa kaburi lake”amesema.Majaliwa amesema, kifo cha aina yoyote ni tukio kubwa kwa kuwa inakuwa ni mara mwisho kuwa na marehemu kwenye jamii zetu hivyo Serikali inatambua huzuni waliyonayo wananchi kwa kuwapoteza wapendwa wao.“Nimepita hapo, hali sio nzuri, ndugu zetu wameungua sana na ipo hatari wengine tunaweza tusiwafahamu kabisa. Lakini hatutawanyima nafasi ya kwenda kushuhudia nyie wenyewe...“Tunatamani kila mmoja apite aone unaweza ukagundua angalau kwa alama aliyokuwanayo ndugu yako, jirani yako. Na kwa kuwa ndugu zetu hawa tulikuwanao mpaka jana asubuhi unaweza kutambua jana alivaa nini kama kipo, wapo wengine walivaa bangili bado zipo kama unatambua kwa alama hiyo itakuwa vizuri…”Majaliwa amesema, kama marehemu hao hawatatambuliwa, kuna utaratibu mzuri wa kisayansi uliotumika wa kuipima miili yote kipimo cha vinasaba.“Wapo wengine walivaa mkanda haujaungua basi kama unatambua kwa hilo basi itakuwa vizuri, wengine walivaa hereni hazijaungua kama unatambua kwa hilo, kwa hiyo kila alama iliyopo ni vema kila mmoja akajiridhishe ili tuweze kuwatambua”amesema.
1
LONDON, ENGALND BAADA ya klabu ya Arsenal kufanya vibaya katika michezo yake miwili ya mwanzo kwenye michuano ya Ligi Kuu England, mfanyakazi wa klabu hiyo ameamua kutangaza kujiuzulu kwa madai kwamba timu hiyo inafanya vibaya kwa kuwa haifanyi usajili wa maana. Katika mchezo wa mwanzo, Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 4-3 kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates, kabla ya kutoka suluhu dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Leicester City, matokeo hayo tayari yamewafanya mashabiki wa klabu hiyo kuanza kumtupia lawama kocha Arsene Wenger. Kocha huyo hadi sasa amefanya usajili wa baadhi ya wachezaji kama vile, Takuma Asano ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Sanf Hiroshima na Rob Holding ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Bolton, hata hivyo mashabiki wa klabu hiyo wamempigia kelele ya kutakiwa kusajili ili timu iweze kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu. Inasemekana klabu hiyo ina jumla ya wafanyakazi 600 ambao wameajiriwa, hivyo fedha nyingi zinatumika katika kulipa mishahara wafanyakazi hao na kushindwa kusajili wachezaji wazuri wanaoweza kutoa mchango mkubwa kwenye timu. Wenger amedai kuwa ana pauni milioni 300 ambazo anaweza kuzifanyia kazi ya usajili, lakini watu wanatakiwa kukumbuka kwamba katika klabu hiyo kuna wafanyakazi 600 ambao wanatakiwa kuwajibika. Kutokana na kauli hiyo ya Wenger, mfanyakazi mmoja wa klabu hiyo ambaye pia ni mwanachama, ametuma barua kwa uongozi wa klabu ya kutaka kujiuzulu kutokana na kauli ya kocha Wenger, mfanyakazi huyo amedai kuwa anaona bora ajiuzulu ili idadi ya wafanyakazi ipungue na klabu hiyo iwe na fedha za kutosha kwa ajili ya usajili. Amedai kwamba anaumia sana kuona klabu hiyo ikishindwa kufanya vizuri kwa muda mrefu na alikuwa hajui kama tatizo ni fedha za usajili, hivyo amechukua maamuzi ya kujiuzulu huku akiwa anasubiri majibu hadi ifikapo Septemba 9 mwaka huu. Kuondoka kwa mfanyakazi huyo sasa klabu hiyo itakuwa na jumla ya wafanyakazi 599. Usajili wa wachezaji katika kipindi hiki cha majira ya joto bado unaendelea hadi kufikia Agosti 31 mwaka huu, hivyo klabu hiyo bado ina nafasi ya kufanya usajili wa nguvu na kuwafurahisha mashabiki wao. Japokuwa mashabiki wengi wamekuwa wakimzoea kocha huyo kufanya usajili katika siku za mwisho za kufungwa kwa dirisha hilo, lakini sasa wameanza kumchoka na wapo ambao wanatamani kocha huyo ajiuzulu.
2
KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, amesema Benno Kakolanya hakwenda Simba kushindana naye ila kushirikiana kuifikisha klabu hiyo inapotaka kufika.Kakolanya amejiunga Simba SC msimu huu akitokea Yanga, hivyo kwa sasa makipa wa Simba ni Manula, Kakolanya na Ali Salim. Manula amesema jijini Dar es Salaam jana kuwa, Kakolanya ni kipa mzuri na amekwenda Simba waunganishe nguvu ili klabu hiyo ifanikiwe.“Kwa hiyo ujio wa Benny ni kitu kizuri na utaongeza nguvu kwenye timu yetu,” alisema kijana huyo aliyejiunga Simba akitokea Azam FC takriban misimu miwili iliyopita.Alisema anafurahi pia kuwa na Juma Kaseja Taifa Stars kwa kuwa miaka ya nyuma alimpa mbinu za kuwa kipa mzuri na sasa wapo pamoja. Kaseja aliyekuwa Tanzania one miaka iliyopita, ameitwa tena kwenye kikosi cha Stars hivi karibuni na kufanya vizuri kwenye mechi zote mbili za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika, Afcon. Aliyasema hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha kituo cha radio Clouds FM kinachomilikiwa na Clouds Media Group.Manula alisema, wakati Taifa Stars ikifundishwa na kocha Kim Poulsen, alikuwa akimuita ajifunze kwa aliowakuta ili awe kipa Taifa Stars baadaye. Miongoni mwa makipa wa Taifa Stars wakati huo alikuwa Kaseja.“Kwa hiyo leo hii mimi nakuwa na Kaseja kwangu mimi naona ni furaha, ni faraja kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa ananifundisha leo hii nacheza nae, nashindana nae kwenye nafasi,” alisema na kuongeza kuwa, anaamini Kaseja naye anafurahi kuwa naye Taifa Stars.Manula amemshukuru Mungu kwa kupata bahati ya kufundishwa na Kaseja na kwamba, miongoni mwa vitu alivyomfundisha ni namna ya kudaka mpira na kutoa pasi uwanjani. Amesema amekuwa na Kaseja kwa muda mrefu na hadi sasa wanakutana na kushauriana mambo mbalimbali na kwamba bado anajifunza kwa kipa huyo wa KMC.“Yaani kumuona Kaseja timu ya taifa kwangu najisikia faraja kwa sababu ukimzungumzia Kaseja kwenye nchi hii ni golikipa ambaye kafanya mambo makubwa sana...ninapopata muda tunakaa pamoja tunapiga stori ananiambia vipi mdogo wangu bwana labda kuna siku ulicheza mechi, labda usikate tamaa, ongeza juhudi hivi,” alisema.Manula alisema alikuwa akicheza kwa presha kubwa alipokuwa Azam FC kuliko Simba na kwa sasa amekomaa.
2
MOSCOW, Urusi RAIS wa Urusi, Vladimir Putin jana aliadhimisha siku ya kutimiza miaka  66  ya kuzaliwa kwake ambapo aliitumia kupumzika karibu na ndugu wa familia, marafiki na wasaidizi wake. Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Ikulu ya  hapa,  Dmitry Peskov   wakati wa mahojiano na Shirika la Habari la nchi hii, TASS tofauti na walivyo viongozi wengine ambao huwa wanafanya sherehea kubwa kiongozi huyo huwa anaitumia siku hiyo kwa kupumzika huku akipokea ujumbe mbalimbali wa kumtakia kila la kheri. Alisema kuwa kama jana kiongozi huyo alipokea salamu mbalimbali kutoka kwa viongozi wan je na miongoni mwa waliompigia simu ni Rais wa  Belarusi,  Alexander Lukashenko, Rais wa Azerbaijani,  Ilham Aliyev  na wa  Armenia, Armen Sarkissian. Alisema kwamba pia Waziri Mkuu,  Dmitry Medvedev  alimpigia simu Rais  Putin  akimtakia afya njema na mafanikio makubwa kwa kazi anayoifanya kwa ajili ya maslahi ya wananchi wan chi hii. Mwaka jana Rais  Putin aliitumia siku hiyo akiwa nje ya mji huu ambapo aliamua kukutana na maofisa wa  Baraza la Usalama mkutano ambao ulifanyika mjini  Sochi. Mwaka  2016, pia Rais Putin aliitumia siku kama hiyo bila kufanya shughuli yoyote ikiwa ni baada ya mwaka mmoja kwenda kushuhudia mechi ya mpira wa magongo na huku mwaka 2014 akiisherehekea akiwa ziarani nchini Siberian.
3
MADEREVA wa bodaboda kutoka kata nane za Manispaa ya Kinondoni wamepewa msaada wa kofia ngumu na Kampuni ya Mcheza ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa ya kujikinga na ajali za barabarani wao na abiria.Akizungumza kwenye Viwanja vya Biafra baada ya kukabidhiwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Bajaji na Bodaboda Kinondoni, Issa Mustapha alisema waliopewa kofia wengi ni viongozi wa vituo ambao pia ni madereva ili wakawe mfano kwa wenzao kuhamasisha kuvaa helmenti.“Tulipewa kofia ngumu 100, tuna madereva wa bodaboda na bajaji 7,000 lakini kwa sababu kofia tulizopewa hazitoshi kwa wote tukaona tuwape viongozi baadhi wa vituo wakawe mfano kwa madereva wao wakiwa kazini,” alisema Mustapha. Kwa upande wake, Balozi wa Mcheza, Edger Kibwana alisema huu ni utaratibu wao walioanzisha mwaka huu kuhakikisha usalama kwa madereva wa bodaboda unakuwa mkubwa sana wanapokuwa kazini kwa kuwapa vifaa hivyo vitakavyosaidia kutoa huduma bora kwa Watanzania. “Tunawasihi bodaboda kuendelea kuzingatia sheria za usalama kama wanavyoelekezwa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, na sisi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha usalama wao unakuwa mzuri, M cheza ipo pamoja nao Watanzania waweze kunuifaka na huduma yao,” alisema Kibwana.Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Mcheza, Moses Busaimoni alisema utoaji wa kofia hizo ni kuunga mkono juhudi za vyombo vya usalama za kuelimisha umuhimu wa madereva na abiria kuvaa kofia ngumu kujiepusha na hatari ya kupoteza maisha pindi wanapopata ajali. Alisema bado wataendelea kuwaunga mkono madereva hao ambapo hivi karibuni watakuja na shindano linalowahusu lenye lengo la kutoa zawadi za bodaboda kwenye kata mbalimbali. “Nawakumbusha madereva wa bodaboda kuwa tumeandaa shindano dhidi yao washindi watanyakua bodaboda, wajiandae utaratibu tutauweka hadharani hivi karibu ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono,” alisema.
2
NA PENDO MANGALA, ARUSHA MAHAKAMA ya Wilaya ya Kongwa   imemuhukumu kifungo cha miaka  30 jela, Lazaro Madeha (56) kwa kupatikana na hatia ya  kujaribu kumbaka mtoto  wake wa kambo wa miaka tisa. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,   Marry Senapee   alisema   Mahakama yake ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa. Alisema ndiyo sababu imetoa adhabu hiyo  iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za ukatili kwa watoto wadogo. Awali,  Mwendesha mashtaka wa    Polisi, Mkaguzi msaidizi, Kandoro Babile  alidai  mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 26 mwaka huu   katika Kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa. Alidai mtuhumiwa alimkamata  mtoto huyo na kumuingiza chumbani kwake. “Baada ya mtuhumiwa huyo kumuingiza mtoto huyo wa kambo  chumbani kwake alimvua nguo zote huku naye akiwa mtupu na kutaka kumbaka. “Mtuhumiwa Madeha alikuwa anataka kumbaka mtoto huyo baada ya mama wa mtoto kwenda kisimani kuchota maji  na aliporudi alimkuta mtuhumiwa akiwa mtupu kitandani  yeye pamoja  na mtoto akitaka kumbaka. “Mama huyo alipiga kelele na majirani walifika na kumkamata,”alisema. Mwendesha mashitaka   aliiomba Mahakama kumpa adhabu kali mtuhumiwa iwe fundisho kwa wengine weye tabia kama hizo.
1
MWENGE wa Uhuru umeingia Mwanza huku Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Charles Kabeho akionya mwenge huo hautafungua miradi iliyojengwa chini ya kiwango na isiyokidhi thamani halisi ya fedha iliyowekezwa.Ametoa onyo hilo baada ya mapokezi ya mwenge uliowasili kutoka mkoani Shinyanga.Kabeho amesema uzoefu wa baadhi ya miradi aliyofungua huko nyuma umeonesha haikidhi viwango na mingine haioneshi mtiririko mzuri wa thamani ya vifaa vilivyotumika kwa ujenzi.Baada ya kuanza mbio na kudhihirisha kauli yake, alikataa kuzindua kituo cha upashanaji habari za Kilimo na Mifugo kilichojengwa kijiji cha Mhande wilaya ya Kwimba kwa Sh milioni 69, akidai maelezo ya kina juu ya thamani halisi ya samani zilizonunuliwa na kuwekwa hapo."Mwenge hautafungua kituo hiki na ninaiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ifanye uchunguzi juu ya gharama zilizotumika kwa ununuzi wa samani," amesema.Taarifa iliyosomwa mapema juu ya ujenzi wa kituo hicho ilionesha samani zake ziligharimu zaidi ya Sh milioni 15 ingawa mwonekano wake ulimtia shaka kiongozi huyo na akaamuru uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ubadhirifu.Miradi 56 yenye thamani ya Sh bilioni 13 inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru ulioanza mbio zake mkoani Mwanza hapo jana.Mapema akisoma taarifa ya mkoa kwa kiongozi wa mbio hizo mpaka wa mkoa wa Mwanza na Shinyanga ulioko eneo la Kazizimba A kata ya Mande wilayani Kwimba jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema miradi 17 ya Sh bilioni 5.8 itawekewa mawe ya msingi.Alisema miradi 17 ya thamani ya Sh bilioni 2.8 itazinduliwa, 12 ya Sh bilioni 2.3 itafunguliwa na mingine 10 ya Sh bilioni 2.6 kukaguliwa."Miradi hii yote imegharamiwa na serikali kuu kwa Sh bilioni 5.8, halmashauri kwa Sh bilioni 1.3, nguvu za wananchi Sh bilioni 1.9 na wahisani mbalimbali Sh bilioni tano," alisema.Alisema serikali ikishirikiana na wananchi inawekeza ujenzi wa miundombinu na akataja mfano wa ukarabati wa majengo yaliyochakaa ya shule nne kongwe za sekondari Mwanza.Alitaja shule hizo ni Bwiru Wasichana, Bwiru Wavulana, Nganza na Sengerema zilizotumia zaidi ya Sh bilioni 3.7 kuzifanyia ukarabati.Sambamba na ukarabati huo, Mongela alisema Sh milioni 983 zimetumika kwa ujenzi wa hosteli za shule zenye kidato cha tano na sita za Nyehunge, Bukongo, Mwamashimba na Pius Msekwa wakati uwekezaji mwingine ni kwenye ujenzi wa matundu 276 ya shule za msingi 62. Mongella alisema ukarabati na uimarishaji wa miundombinu umeongeza idadi ya wanafunzi waliodahiliwa elimu ya msingi na sekondari.Alitoa mfano wa mwaka 2015 ambapo udahili ulikuwa wanafunzi 107,221 hadi 127,746 mwaka huu na sekondari kutoka wanafunzi 37,017 mwaka 2015 hadi 49,046 mwaka huu.Kwenye eneo la afya, Mongela alitoa taarifa mpya za maambukizi ya Ukimwi takwimu zikionesha yamepungua kutoka asilimia 15.1 mwaka 2016 hadi asilimia 8.1 mwaka huu.Akikabidhi mwenge huo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack alisema miradi 47 ya Sh bilioni 27.9 ilizinduliwa na kuwekewa jiwe na msingi huku watu 4,315 wakipima VVU.
1
LONDON, UINGEREZA KUNDI la wabunge 50 wa chama tawala cha Conservative wamekutana jana kujadili mchakato wa kumng’oa madarakani Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May. Kundi hilo ni lile linalopinga mpango wa May kuhusu mchakato wa nchi hiyo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU), maarufu kama Brexit. Hiyo ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuriwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambavyo havikutaka kujulikana. Vyanzo hivyo vilisema kundi hilo la wabunge ambao ni sehemu ya kundi la wanasiasa wanaopinga uhusiano wa karibu wa Uingereza na EU ndani ya chama cha May cha Conservative walikutana juzi usiku. Wanadaiwa walijadili wazi mustakabali wa May kama kiongozi. Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo wamesema tayari wamewasilisha barua za kusema hawana imani na May. Kwa mujibu wa kanuni za chama hicho cha kihafidhina, kiongozi anaondolewa madarakani iwapo asilimia 15 ya wabunge wa chama hicho watapiga kura ya kutokuwa na imani naye.
3
['Kuigeuza Everton kuwa klabu ya kugombea nafasi ya kucheza Champions League si jambo ambalo halitawezekana, anaeleza kocha mpya wa klabu hiyo Carlo Ancelotti.', 'Ancelotti, 60, ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na AC Milan ametia saini mkataba wa kuwanoa Everton mpaka mwaka 2024.', 'Kocha huyo mwenye mafanikio lukuki anaichukua timu hiyo ikiwa nafasi ya 15 kwenye jedwali la Ligi ya Primia, wakiwa na alama nne tu juu ya mstari wa kushuka daraja. ', '"Champions League ni mpango wetu wa muda mrefu," amesema na kuongeza. "Hakuna kisichowezekana katika mpira wa miguu."', 'Everton hawajamaliza katika nafasi nne za juu toka mwaka 2005, na kabla ya hapo ilikuwa mwaka 1988. ', 'Klabu pekee ambazo Ancelotti amefundisha na kukosa uwiano wa ushindi wa kufikia 50% ni klabu za Italia za Reggiana na Parma mwishoni mwa miaka ya 1990.', 'Ancelotti amesema kilichomvutia kujiunga na klabu hiyo ni: "Historia na utamaduni wa klabu. Ni moja ya klabu kubwa zaidi England."', 'Ancelotti ameshinda Champions League mara tatu kama kocha - mara mbili akiwa na AC Milan na mara moja na Real Madrid.', 'Pia ametwaa ubingwa wa Ligi ya Primia na Kombe la FA akiwa na Chelsea mwaka 2010 na ametwaa mataji wakiwa na Bayern Munich na Paris St-Germain.', 'Ancelotti ametua Everton siku chache baada ya kutimuliwa katika klabu ya Napoli ya nchini kwao Italia.', '"Ni kweli nimefunza klabu kubwa," amesema, "Mipango ya Paris St-Germain ilikwa mizuri. Naamini itakuwa hivyo na hapa pia. ', 'Nimeenda uwanja wa mazoezi jana. Mambo yalikuwa mazuri.', 'Mipango ya klabu kujenga uwanja mpya inaonesha kuwa klabu inataka mafanikio. ', '"Kukusanya mapato ni jambo kubwa katika mpira wa kisasa. Everton wanataka uwanja wao mpya ili uwasaidie kukusanya mapato na kuwa na ushindani mkubwa. ', '"Kwangu, itakuwa ni jambo zuri kuwepo hapa wakati uwanja mpya ukifunguliwa." ']
2
NAIROBI, KENYA KATIKA uchaguzi wowote wa kisiasa kura za maoni ni jambo muhimu sana. Mara nyingi kura hizo ni utafuti unaoendeshwa na taasisi mbalimbali ili kupata maoni ya wananchi juu ya wagombea mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu. Hali hiyo ndiyo imetokea nchini Kenya, ambapo kura za maoni zimewashtua wachambuzi wa masuala ya siasa nchini humo na kudai kuwa huenda ikawa kura halisi hapo Agosti 8 mwaka huu. Ripoti ya utafiti ya Infotrak iliyotolewa Ijumaa wiki hii imebainisha kuwa Uhuru Kenyatta anayo nafasi kubwa ya kumshinda mpinzani wake Raila Odinga, kutoka muungano wa vyama vya upinzani, NASA. Ripoti hiyo imesema endapo uchaguzi ungefanyika leo Uhuru Kenyatta angeshinda kwa asilimia 48 dhidi ya asilimia 43 za Raila Odinga. Ripoti hiyo imesema chama cha Jubilee kimekuwa maarufu zaidi  nchini Kenya huku muungano wa NASA ukishika nafasi ya pili kwa umaarufu. Kura za maoni zinaonyesha kuwa asilimia 50 ya Wakenya wanasema nchi yao inakwenda kombo hivyo ushindi wa Uhuru Kenyatta utaongeza matatizo zaidi kama atamshinda Raila Odinga. Hata hivyo Infotrack wamesema kuwa kuna maeneo mbalimbali ambayo yanaweza kuwaibua na kura nyingi wagombea hao. Mathalani wanasema Uhuru Kenyatta amekuwa maarufu zaidi kuliko Raila Odinga, ambapo anaungwa mkono zaidi katika maeneo ya kati ya Kenya. Aidha, Infotrack wanasema mgombea ambaye angeshika nafasi ya tatu Abduba Dida kwa kujizolea asilimia 0.5 ya kura zote. Wengine Ekuru Aukot, Cyrus Jirongo  na Joe Nyaga wanmgegawana asilimia 0.1. Kura hizo za maoni zilikusanywa na kati ya Juni 24 na 27, imebainishwa kuwa uchaguzi huo unaweza kuingia kwenye raundi ya pili na kuwakutanisha tena Uhuru na Raila. Sababu kubwa inayotolewa ni kwamba kila mmoja angetamba kuibuka na ushindi, lakini watalazimika kufikisha asilimia 50 ya kura zote. Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ataamuliwa kwa kura za jumla. Taasisi ya Infotrak imeeleza kutumia sampuli za wtau 2000 ili kupata matokeo yao. Idadi hiyo inawakilisha watu milioni 19.6 ambao wameandikishwa na Tume ya Uchaguzi (IEBC) kupiga kura mwaka huu. KURA ZA KENYATTA Takwimu za ripoti Infotrak zinaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta anaungwa mkono katika maeneo ya ukanda wa Kati kwa asilimia 90, Kaskazini Mashariki asilimia 75, Mashariki asilimia 58, na Bonde la Ufa asilimia 56. Hata hivyo Uhuru Kenyatta angepata kura chache mno katika maeneo haya Nyanza asilimia 14,  Magharibi asilimia 28, Pwani asilimia 29, na Nairobi asilimia 41. KURA ZA ODINGA Raila Odinga anaungwa  katika maeneo ya Nyanza asilimia 83, Pwani asilimia 61, Magharibi asilimia 53 na Nairobi asilimia 51. Naye Raila Odinga angepata kura chache kwenye maeneo haya; Kati asilimia 5, Kaskazini Mashariki asilimia 20, Bonde la Ufa asilimia 4  na Mashariki asilimia 37. Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa chama cha Jubilee ni maarufu zaidi nchini Kenya ambapo kinafahamika miongoni mwa wananchi kwa asilimia 47. Hilo ni tofauti na muungano wa upinzani NASA ambao unafahamika miongoni mwa wananchi wa Kenya kwa asilimia 43 Chama cha Jubilee ni maarufu zaidi katika maeneo ya Kati asilimia 88 na maeneo ya Nyanza asilimia 14, wakati muungano wa upinzani NASA unafahamika  maeneo ya Nyanza kwa asilimia 83 ambapo ni pungufu kwa asilimia 5. Pia NASA kinafahamika maeneo ya Kati-Kenya kwa asilimia 5 tu wakati Jubilee ni asilimia 88. Ni dhahiri utafiti huo umeonyesha tofauti ya vyama hivyo kwa kila eneo nchini humo. WANASIASA WATIWA KUFULI Wakati takwimu za uchaguzi mkuu zikitolewa na Infotrak, upande mwingine wanasiasa wametiwa kufuli  na mamlaka ya Mawasiliano nchini humo baada ya kupiga marufuku vyama vya siasa kutuma ujumbe mfupi kutumia lugha za makabila. Hatua hii imechukuliwa kupambana na lugha za uchochezi kipindi hiki cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu. Utaratibu huo uliotolewa na Tume hiyo ya Mawasiliano pamoja na Tume ya uwiano na utengamano, inavitaka vyama vya siasa nchini humo kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza pekee katika mawasiliano yake. Aidha, lengo la utaratibu huu mpya ni kuwazuia wanasiasa kuepuka kutumia lugha ya uchochezi kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Whats App, Twitter na YouTube. Kampuni za simu nchini humo sasa zitahitaji kupitia ujumbe uliotumwa na kuuwasilisha kwa mamlaka hayo ili kupitiwa kubaini ikiwa kuna matamshi ya uchochezi yanaendelea kutolewa. Hatua hii imetajwa ni kukomesha siasa za kikabila amabzo zimekuwa zikitawala chaguzi za Kenya kila mara.
3
Okwi anayechezea Simba, anatarajiwa kwenda nchini Denmark kufanya majaribio katika Klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu ya huko kuanzia kesho.Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya Klabu ya Simba jana, majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia kesho na baada ya hapo klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio hayo.Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Simba inafurahi sana kuona wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye viwango vya kimataifa zaidi, hivyo Simba inamtakia kila la kheri Okwi kwenye majaribio yake ya siku 14 kwenye Klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye ligi ya Denmark.”Okwi aliyezaliwa miaka 23 iliyopita nchini Uganda, aliwahi pia kucheza kwa muda mfupi katika Klabu ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia na baadaye kuichezea Yanga kabla ya msimu uliopita kurudi klabu yake ya Simba.Katika hatua nyingine, mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco mambo yake yamemnyookea baada ya Klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini kukubali kumsajili.Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari, Azam FC imekubali kumuuza mchezaji huyo na kinachosubiriwa ni timu hiyo kumalizana juu ya maslahi binafsi ili kuhamia katika timu hiyo.Kwa mujibu wa mtandao wa bongostaz, Azam FC imekubali kumuuza mshambuliaji huyo kwa kitita cha Dola za Marekani 80,000 ikiwa ni sawa na zaidi ya Sh milioni 160,000 kwa klabu hiyo.Na sasa kinachosubiriwa na Free State kumalizana na mchezaji juu ya maslahi binafsi ili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, ahamie Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.Mshambuliaji mahiri, Mrisho Ngassa aliyesajiliwa na Free State miezi miwili iliyopita baada ya kumaliza mkataba Yanga, anaeleza kuwa ndiye aliyempa ulaji huo Bocco kwa kuwapa viongozi wa timu hiyo mawasiliano ya Bocco.Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd kuzungumzia taarifa hizo, alisema hazina ukweli na kama zitakuwa na ukweli zitawekwa mara moja katika tovuti ya klabu hiyo.Bocco aliwahi kufanya majaribio Afrika Kusini katika Klabu ya Supersport na Algeria na kufuzu ila hakuuzwa kutokana na dau dogo
2
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana walizidi kuwapa presha mahasimu wao Simba baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC, huku Azam ikiiangamiza Mtibwa Sugar mkoani Morogoro. Kwa matokeo ya jana, Yanga iliyoikaribisha Mwadui katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilifikisha pointi 56 na kuzidi kuipumulia Simba huku Azam ikifikisha pointi 55 kutokana na ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Mtibwa katika Uwanja wa Manungu, Morogoro. Vinara Simba wanaoongoza kwa kujikusanyia pointi 57, wanazidi kupata mchecheto kutokana na mahasimu wao Yanga kubakiwa na mchezo mmoja wa kiporo wakati Azam wakiwa tayari wamemaliza baada ya kucheza mechi 24 sawa na Wekundu hao wa Msimbazi. Yanga wameendelea kutetea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakitofautiana pointi moja na vinara Simba, wakati Azam imebaki nafasi ya tatu kutokana na pointi 55 walizojikusanyia huku wakifuatiwa na Mtibwa wenye pointi 43. Katika mchezo wa jana, wenyeji Yanga ndio walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya tatu kwa bao safi lililofungwa na kiungo, Simon Msuva, aliyeunganisha krosi iliyochongwa na mlinzi, Oscar Joshua. Bao hilo liliwazindua Mwadui ambao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 13 kupitia kwa Kelvin Sabati aliyewazidi maarifa mabeki wa Yanga na kupiga shuti lililodakwa na kipa Deogratius Munishi na kumponyoka na kupata urahisi wa kufunga. Yanga waliendeleza mashambulizi langoni kwa Mwadui ambapo dakika ya 24 mshambuliaji, Donald Ngoma, alipata nafasi ya wazi kutokana na pasi ya Amissi Tambwe lakini alishindwa kuitumia baada ya kupiga shuti lililotoka nje. Dakika ya 70 mwamuzi Selemani Kinugani kutoka Morogoro alimwonyesha kadi ya pili ya njano na kumtoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji wa Mwadui, Iddy Mobby, baada ya kumfanyia madhambi Ngoma. Bao la pili lililoipa ushindi muhimu Yanga lilifungwa dakika ya 86 na kiungo, Haruna Niyonzima, kwa shuti kali baada ya kuunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Ngoma. Kwa upande wa Azam FC, bao pekee la ushindi liliwekwa wavuni na mshambuliaji, John Bocco, kwa mkwaju wa penalti.
2
FRANCIS  GODWIN, IRINGA WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya  Waziri Mkuu (Sera  ,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu  wenye  Ulemavu, Jenista Mhagama  ameagiza  ujenzi  wa  vituo  20 vitakavyotoa  huduma  za ugonjwa   Ukimwi kwa   wasafiri wa  masafa marefu vinavyojengwa chini ya Programu  ya Sattf   barabara kuu ya Dar es Salaam  kwenda nchi za  kusini mwa Tanzania kukamilisha ujenzi  huo ndani ya  mwezi mmoja. Alitoa  agizo  hilo juzi,baada ya kuwekaji wa jiwe la msingi  kituo cha afya  Ipogolo  mjini  Iringa  kwa niaba ya  vituo  vingine. Alisema hajafurahishwa na kasi  ndogo ya  ujenzi wa vituo  hivyo  ambavyo  kimsingi ujenzi  wake  ulipaswa  kukamilika tangu  Oktoba, mwaka huu. Alisema  ujenzi  wa  vituo   20  kutoka  Dar es Salaam  hadi  Tunduma – Momba mpakani  wa Tanzania na  Zambia,Serikali  imekwishatumia  Dola za  Marekani milioni 3,  japo  kasi ya ujenzi  inasuasua. Alisema  kutokana na  kasi ya Serikali uboreshaji wa  huduma  za  afya   ujenzi wa vituo  hivyo  utasaidia   kupunguza kasi ya maambukii ya  virusi vya ugonjwa huo kwa  wasafiri   wanaotumia barabara  hizo. Alisema kupitia   fedha  hizo pamoja na kukamilisha ujenzi  wa vituo, pia  zitawezesha  kununua vifaa vya  kisasa na kuweka mazingira  wezeshi ya  kufundisha  wataalamu 10 kila  kituo watapata mafunzo. Alisema lengo la kuwafundisha  wataalamu hao,  ni  kuondoa  usumbufu  wa  uhaba wa wahudumu katika vituo ili  wateja  watakapofika wapate huduma kwa wakati. Alimtaka   Mkurugenzi  Mkuu wa  Tume ya Kuthibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS )  kuangalia  uwezekano wa kuanzisha mpango wa ujenzi wa  vituo kama  hivyo maeneo ya mipakani. Alisema  ili  vituo  lazima  viweze endelevu na  kutoa  huduma  zake  kwa kipindi  kirefu zaidi ni  vizuri suala la  utunzaji  na usimamiazi wa miundombinu. Katika  hatua  nyingine,Waziri Mhagama  aliahidi  kuanzisha  ujenzi  wa chumba  cha upasuaji na chumba  cha uzazi  kituo cha afya Ipogolo  na yeye atachangia  mifuko 100 ya saruji na bati 100 kama  sehemu ya  kuunga mkono. ” Ninalazimika  kuchangia bati  na saruji  ili  kuanza  ujenzi  wa  chumba cha upasuaji na chumba  cha uzazi,  nimefurahi  kukutana na Rosemary  Mwenda  ambae  leo amepata mtoto  katika  kituo hiki tena mtoto wa  kike  ambae  nimempa jina la Jenista,mimi ni mama  yake wa hiari baada ya mzazi wake  kufikisha ombi la kujengewa  vyumba,”alisema. Kuhusu    kasi ya mambukizi ya virusi wa  vya  Ukimwi (VVU) mikoa ya  Njombe , Iringa na Mbeya, Mhagama  alisema   inatisha  na kuna haja ya  mikoa hiyo  kuweka mkakati wa  kupunguza kasi hiyo. Mkuu wa  Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema  mkoa huo umepatiwa  vituo vinne   Wilaya ya Kilolo,kimoja  na  Iringa  vituo  vitatu ambavyo  vitasaidia  kupunguza kasi ya maambukizi. Mkurugenzi  Mtendaji wa TACAIDS,Dk. Leonard Maboko  alisema  Tanzania ni miongoni mwa  nchi  za   kusini  mwa Jangwa la  Sahara  ambazo zinakabiliwa na kiwango kikubwa  na tatizo la ugonjwa huo,huku takwimu  zikionyesha  watu takribani milioni 37.9 wanaishi na maambukizi ya  VVU mwishoni  mwaka 2018 duniani , kati ya hao asilimia   53 wapo nchi  za  mashariki na kusini  mwa Afrika .
5
NAIROBI, KENYA WABUNGE wa Chama cha Jubilee wamedai kinara wa muungano mkuu wa upinzani wa NASA, Raila Odinga, anashirikiana na mataifa ya kigeni kula njama za kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa urais na kwenda kuapishwa nchini Tanzania. Hayo ni kwa mujibu wa wabunge watatu wa chama hicho na majimbo yao kwenye mabano, Muthomi Njuki (Chuka/lgambangombe), Moses Kuria (Gatundu Kusini ) Kimani Ichungwa (Kikuyu) na Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Tharaka Nithi, Beatrice Nkatha. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Chuka, Kaunti ya Tharaka Nithi, wabunge hao walisema lengo la Raila kutaka muungano wa NASA kuwa na kituo cha kuhesabu kura ni kujitangaza mshindi kisha aende kuapishwa katika nchi jirani ya Tanzania. Walionya hatua hiyo itazua ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 kama ilivyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Viongozi wa Jubilee wamekuwa wakipinga azma ya NASA kuwa na kituo cha kuhesabu kura wakisema ni Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pekee inayoruhusiwa kisheria kuhesabu na kutangaza matokeo. “Tunajua Odinga anapanga kujitangaza mshindi na kwenda kujiapisha Tanzania akishindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 8,” alisema Icungwa. Alisema kujitangazia matokeo ya uchaguzi mkuu ni sawa na uhaini kwa sababu hilo ni jukumu la IEBC pekee kufanya hivyo. Njuki alidai ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 zilisababishwa na kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu kulikofanywa na Odinga. Kuria alisema Odinga anahisi kushindwa na hivyo anatafuta njia za kupinga matokeo.
3
Kwa mujibu wa Komba, kikao hicho pia kitahusisha Wenyeviti wa Kamati za Uchaguzi za DRFA na TEFA.Komba alisema kikao hicho kitafanyika Jumanne, Septemba 15, kikiwa na lengo la kuchambua upya sifa za wagombea na wapiga kura wa uchaguzi wa TEFA.Komba alisema baada ya kupitia suala hilo, watapanga tarehe ya uchaguzi wa Tefa baada ya awali TFF kuusimamisha hivi karibuni kutokana na sintofahamu iliyotokea baada ya baadhi ya Wagombea kukatwa.
2
LONDON, ENGLAND ALIYEKUWA beki wa kati wa klabu ya Arsenal, Per Mertesacker, amefunguka na kusema, wachezaji walichangia kumwangusha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Arsenal Wenger, bila ya kujali ya kuwa mtetezi wao. Mertesacker amedai anajisikia vibaya kuwa miongoni mwa wachezaji ambao walishindwa kumpigania kocha huyo aendelee kuwepo, lakini aliungana na wachezaji hao kusababisha kocha huyo kufukuzwa. Wenger alifukuzwa mwishoni mwa msimu uliopita mara baada ya kuwa hapo kwa kipindi cha miaka 22, lakini uongozi ulidai kuwa, umefikia hatua ya kuachana na kocha huyo kutokana na kushindwa kutwaa mataji katika kipindi cha hivi karibuni. Mertesacker alisema Wenger alikuwa sahihi kuondoka kwa wakati huo, lakini wachezaji walisababisha kwa kiasi kikubwa. “Kilikuwa kipindi kigumu sana, ambapo Wenger alikuja kutuambia kuwa anaondoka, kwa kuwa nilikuwa na hisia kali, huku nikiamini nimekuwa mmoja wa wachezaji ambao wamechangia kuondoka kwake. “Wachezaji tulikuwa na kila sababu ya kupata matokeo mazuri, lakini tulishindwa kufanya hivyo na hatimaye kumsababishia kocha huyo matatizo, mara zote alikuwa pamoja na sisi katika kupigania haki zetu, lakini sisi tulishindwa kumpigania. “Ukweli ni kwamba nitaendelea kujilaumu katika maisha yangu, lakini ndiyo maisha ya soka yalivyo,” alisema beki huyo wa zamani. Mertesacker kwa sasa amepewa jukumu la kuwa kocha wa timu ya vijana ya Arsenal baada ya kuwa mchezaji wa klabu hiyo kwa miaka saba. Amecheza jumla ya michezo 156 ya Ligi Kuu na kufanikiwa kupachika mabao sita.
2
Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM BEKI wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Abdi Banda, anayecheza soka la kulipwa Afrika Kusini kwenye klabu inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, Baroka FC, amesema kucheza nje ya nchi kumemsaidia kukuza kiwango chake. Banda alisajiliwa na Baroka msimu huu baada ya kufuzu majaribio akitokea klabu ya Simba, mara baada ya kumaliza mkataba wake. Tangu mchezaji huyo asajiliwe na klabu hiyo licha ya kuchezea nafasi ya beki, amefanikiwa kufunga bao moja kati ya michezo mitano waliyocheza, ambapo timu yake inaongoza ligi kwenye msimamo ikiwa na pointi 15. Akizungumza na MTANZANIA jana, Banda alisema tangu ameanza kucheza nje ya nchi ameweza kujifunza mambo mengi kutoka huko, hali iliyopelekea kiwango chake kuongezeka tofauti na alivyokuwa Tanzania. “Mpira wa Afrika Kusini upo juu tofauti na Tanzania hivyo imenisaidia kipaji changu kukua zaidi tofauti na nilivyokuwa nikicheza timu ya Simba,” alisema Banda. Alisema anajitahidi kutumia nafasi yake vizuri ili azidi kung’ara kwenye timu yake ya Baroka na Taifa Stars ili azidi kuitangaza vema Tanzania. “Timu za nje hakuna kulala, unatakiwa kupambana na kujituma ili kiwango kizidi kuongezeka na mimi nitajitahidi kupambana kila nitakapopata nafasi ya kucheza ili kumshawishi kocha azidi kuniamini,” alisema.
2
MIRADI mikubwa mitatu ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano imewezesha kutoa ajira kwa Watanzania 15,009 hadi kufikia Oktoba mwaka huu.Miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza unaotekelezwa kwa awamu, Mradi wa Kufua Umeme wa Maji katika Maporomoko ya Mto Rufiji wa Julius Nyerere (JNHPP) na ununuzi wa ndege kwa ajili ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji ametoa takwimu hizo bungeni jijini Dodoma wakati akifafanua hoja za wabunge waliochangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mwongozo wa Bajeti ya Mwaka 2020/2021.Akitoa ufafanuzi huo juzi bungeni, Dk Kijaji alisema miradi hiyo mikubwa ya kimkakati imekuwa na faida ya moja kwa moja katika maendeleo ya kiuchumi nchini.Akitoa mifano na takwimu, alisema kwa upande wa SGR, hadi kufikia Septemba mwaka huu, mradi umetoa ajira 13,117 kwa Watanzania katika awamu ya kwanza.Pia umetoa fursa kwa makandarasi 640 wa nchini ambao wamefaidika na jumla ya Sh bilioni 664.7, huku bidhaa kama saruji, nondo na malighafi nyingine zikinunuliwa kutoka ndani ya nchi. “Asilimia 30 ya gharama za mradi huu zimetumika kununua bidhaa kutoka ndani ya nchi,” alisema.Aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaokoa Sh bilioni 6.7 ambazo zinatumika kwa matengenezo ya barabara kila mwaka nchini.Kuhusu Mradi wa Umeme wa Rufiji wa Julius Nyerere, alisema hadi kufikia Oktoba mwaka huu, mradi umetoa ajira 1,456 na wakandarasi wa ndani 10 wamenufaika kwa kupata kazi katika mradi huo utakaofua megawati 2,115 za umeme ndani ya miaka mitatu ijayo.Aidha, alisema mradi huo una ongezeko la matumizi ya bidhaa za ndani kama saruji, nondo, kokoto na vyakula, na mradi huo ni muhimu kwani bila umeme wa uhakika na bei nafuu, hakuna viwanda.Akizungumzia ununuzi wa ndege, alisema ndege ambazo zimeshaletwa nchini, zimewezesha kupatikana kwa ajira 436 kwa Watanzania hadi kufikia Septemba mwaka huu.Naibu Waziri aliongeza kuwa ndege hizo zimerahisisha huduma na kufikia vituo 11 nchini na sita nje ya nchi, huku zikiongeza mapato pamoja na idadi ya watalii wanaotembelea nchi.Akizungumzia kilimo, alisema serikali inafahamu umuhimu wake na itaendelea kutenga fedha zaidi kwa sekta hiyo ili kufikia Azimio la Maputo linalotaka nchi za Afrika kutenga asilimia 10 ya bajeti kwa kilimo.Kuhusu maji, alisema upatikanaji wake umezidi kuongezeka kwani kwa sasa kwa Jiji la Dar es Salaam upatikanaji ni asilimia 85, miji mingine asilimia 80, miji midogo ni asilimia 64 na vijijini ni asilimia 64.8.Alisema serikali imejipanga kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) na Mfuko wa Maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unaboreka.Akizungumzia maboma yaliyojengwa na wananchi katika sekta za afya na elimu ambayo hajakamilishwa, alisema serikali imekuwa ikitoa fedha kukamilisha maboma hayo.Alibainisha kuanzia Julai 2018 hadi Oktoba mwaka huu, serikali imetoa Sh bilioni 104 katika ujenzi huo sekta ya elimu na Sh bilioni 38.9 katika sekta ya afya kwa ajili ya kukamilisha maboma ya vituo vya afya.Pia imetoa Sh bilioni 29.9 kukamilisha madarasa 2,392 ya sekondari na Mpango wa Lipa Kutokana na Matokeo Makubwa (EP4R), Sh bilioni 32.2 zimejenga vyumba 2,760 na matundu ya vyoo 670 shule za msingi nchini.Amesema serikali imekuwa ikitekeleza mpango huo wa maendeleo kwa mujibu wa sheria na matokeo makubwa yanaonekana katika miaka hii minne.Amesema ni kwa msingi huo, Juni mwaka huu, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi ikitanguliwa na Djibouti, Ethiopia na Rwanda.Akihitimisha mjadala huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimsifu Rais John Magufuli,Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mawaziri kwa jinsi wanavyochapa kazi.
1
“NAIPONGEZA timu nzima ya Mkoa wa Arusha iliyobuni mtihani wa pamoja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa mkoani ambao sasa unasaidia wanafunzi kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kuongeza ufaulu zaidi.”Ndivyo anavyosema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anapozungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuboresha elimu mkoani humo, zikiwa ni juhudi za kusaidia mkoa huo kuendelea zaidi kielimu hali iliyouwezesha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2018.Katika mpango huo uliozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za binafsi na za serikali mkoani humo, watafanya mtihani mmoja unaofanana kwa shule zote kadiri ya madarasa yao. Mpango huo ni matokeo ya juhudi za mkuu wa mkoa huo, watendaji na wadau mbalimbali wa elimu mkoani humo kushirikiana kutatua changamoto za walimu wa shule za msingi na sekondari.Katika kufikia mafanikio hayo, mara kwa mara Gambo amekuwa akifanya vikao na walimu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro pamoja na maofisa elimu na waratibu wa elimu kata. Vikao hivyo na wadau wa elimu wa Mkoa wa Arusha vimekuwa vikilenga kuhakikisha hakuna mazingira yanayokwamisha walimu kufundisha darasani au watoto kutosoma masomo yote. Uchunguzi umebaini kuwa, juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa mkoa, ndizo zimewezesha Mkoa wa Arusha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega anasema mpango huo umesababisha kuwapo matokeo chanya ya darasa la saba mwaka huu. Mkoa huo wenye walimu wa shule za sekondari 4,950, mwaka 2017 ulishika nafasi ya saba katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi. Mwaka 2016 ulishika nafasi ya sita. Kwitega anasema mpango ulianza kutekelezwa mwaka 2017 kwa kuanzisha mtihani wa mihula kwa shule zote za sekondari na za msingi.“Tumejifunza mambo mengi katika mpango huu wa uboreshaji wa elimu na baadhi ya masomo vijana wanafaulu vizuri huku masomo mengine wakishindwa kufaulu kutokana na walimu kutofundisha vema,” anasema. Akizindua mpango wa kuboresha elimu uliobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na wadau wa elimu wakiwemo viongozi wa dini, Waziri Jafo anaupongeza mkoaa kwa kuzindua mpango wa uboreshaji wa elimu kwa shule za msingi na sekondari.Anasema kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba, ameandaa vyeti maalumu kwa mikoa mitatu iliyofanya vizuri ikiwemo wa Arusha ili kuwapongeza walimu na wadau wa elimu kwa kuuwezesha kuwa mkoa wa tatu kitaifa katika masuala ya elimu. Anawataka wadau hao kujipanga vema zaidi na kuongeza juhudi kuboresha elimu ili mkoa huo ushike nafasi ya kwanza kitaifa.Anasema uzinduzi wa mpango wa elimu ni ajenda ya kumkomboa mtoto masikini kwa kuwa Rais John Magufuli amekuwa akitoa Sh bilioni 23.5 kila mwezi kwa ajili ya elimu bila malipo akilenga kuwakomboa watoto wa Kitanzania. Anasema mitambo ya kuchapia mitihani ya pamoja iliyopo mkoani hapo, pia itasaidia kuondoa kero ya walimu kuandika mitihani ubaoni. Imebaini kuwa, mpango huo pia unaondoa majigambo ya baadhi ya walimu kudai wamefaulisha vizuri wanafunzi wao, na badala yake umewezesha shule mbalimbali kufanya vema katika kukuza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi.“Jambo hili likisimamiwa vizuri Mkoa wa Arusha utaacha mikoa mingine kwa ufaulu na nawaomba wakuu wa mikoa wengine kuiga mfano wa mkoa huu katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” anasema Waziri Jafo. Waziri anamhimiza Mkuu wa Mkoa (Gambo) kuainisha wanafunzi wanaofaulu vema sambamba walimu wanaofanya kazi vizuri ili wapewe zawadi za kiwilaya na kimkoa na kuwataka pia kuandaa siku maalumu ya elimu ili kuhamasisha elimu.Anasema walimu na madaktari ni watu muhimu katika jamii, hivyo hawana budi kupewa motisha sambamba na kuepushiwa adhabu zinazoshusha utu na ari yao ya kazi. “Mwalimu ndiye mtu anayemwandaa mtoto kiakili na anamjenga, hivyo lazima walimu wasikilizwe na wasaidiwe kutatua kero zao…” anasema. Anausisitiza Mkoa wa Arusha kubuni mkakati mwingine wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuandaa jukwaa maalumu la mjadala wa kimaarifa ili kushindana kihesabu, kisayansi na kihistoria, hali itakayochochea ongezeko la maarifa ya wanafunzi.Gambo anasisitiza kuwa, mpango wa kuboresha elimu mkoani Arusha umewezesha kutatuliwa changamoto za ufaulu wa mitihani, likiwamo suala la kutofundisha mada zote na kusisitiza walimu kutunga mitihani kulingana na silabasi wanazofundisha. Awali katika mitihani ya nusu muhula kwa kidato cha kwanza hadi cha tatu kila halmashauri ilionesha hakuna halmashauri iliyofikia asilimia 50 huku somo la Sayansi likiwa na wastani wa asilimia 30 na Fikizia wastani asilimia 44. Kwa somo la Hisabati kidato cha kwanza asilimia 20, kidato cha pili asilimia 13 na kidato cha kwanza asilimia 10.“Kama ungekuwa ni utafiti, tungesema wamefaulu katika utafiti, lakini kutokana na matokeo haya tunasema hapana lazima sasa tufanye jambo la kuboresha elimu kwa Mkoa wa Arusha,” anasema Gambo. Anasema siku ya Ijumaa, masomo huisha saa sita na yanapoisha, kila mwalimu mkuu na mkuu wa shule akae na walimu wa masomo yote kujua kwa nini mwalimu husika hajafundisha somo lake kama lipo. Anasema mwalimu akieleza sababu, lazima zitatuliwe ili kuboresha elimu na waratibu wa elimu kata waangalie changamoto za walimu na kuzitatua, ikiwemo kuziwasilisha kwa maofisa elimu katika halmashauri zote.“Maofisa elimu nendeni mkajue hao wengine wana changamoto gani maana kuna mahali utakuta shule haina vyoo, mazingira yake si rafiki sasa lazima uangalie tatizo lipo wapi na siyo suala la kusimamisha tu, walimu,” anasema Gambo. Anasema: “Mfano, katika Shule ya Msingi Mkonoo kulikuwa na ukosefu wa vyoo walimu walikuwa wakichangia vyoo na wanafunzi. Nilipofika pale Aprili mwaka huu kuangalia yale mazingira, nilihuzunika sana…” “Nilichofanya ni kumchukua Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni ili ajionee hali halisi ya maisha ya walimu hawa na ndipo nilipohakikisha Halmashauri ya Jiji inatenga milioni kadhaa kwa ajili ujenzi wa matundu ya vyoo zaidi ya 20 nimeongeza hapo.”Mchakato wa Mpango wa Elimu ulianza mwaka 2017 kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, hivyo badala ya kununua mashine kwa Sh milioni 20 tulinunua mashine 10 za kuchapisha mitihani kwa Sh milioni 7. Katibu Tawala wa Mkoa (Kwitega) anasema mkakati mwingine ni kuwezesha wazazi kuwa na utaratibu wa kusoma vitabu na watoto wao kwenye maktaba zilizopo mkoani humo.Theresia Mahongo kwa niaba ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, anasema awali aliona mpango huo hauwezekani, lakini kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, umefanikiwa na kuzaa matunda chanya. Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Dk Stanley Hotay anaiomba serikali kuhakikisha mitaala inayotolewa ya kuanzia elimu ya msingi na sekondari inamjenga na kumwandaa mtoto kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa. Mwalimu Ambrose Bashayija kutoka wa Shule ya Edmund Rice iliyopo katika Kata ya Sinon, anasema awali shule za binafsi zilikuwa zikikabiliwa na uhaba wa vifaa vya kuchapisha mitihani pamoja na udanganyifu wa ufaulu, lakini mpango huo utawezesha walimu kujulikana kama kweli wanafundisha vipindi vizuri darasani ama la.
1
WANANCHI wametakiwa kujitokeza na kutumia fursa za ufugaji wa mazao ya baharini ikiwamo majongoo na kaa ili kuongeza kipato.Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Mussa Aboud Jumbe amesema hayo alipozungumza na wafugaji wa mazao ya baharini kisiwani Pemba katika mafunzo ya kuwawezesha kubuni njia mpya za uzalishaji wa kilimo cha mwani.Jumbe alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha fursa za ubunifu wa mazao ya baharini ikiwamo kituo cha kimataifa cha uzalishaji wa vifaranga vya baharini.Alisema kama kituo hicho watakitumia kikamilifu, wafugaji wanayo fursa kubwa ya kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika uzalishaji wa mazao ya baharini.“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa imejikita katika kuwawezesha wafugaji wa mazao ya baharini uwezo wa kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo mwani, majongoo ya baharini na kaa,” amesema.Baadhi ya wafugaji na wazalishaji wa mazao ya baharini wameitaka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoa elimu zaidi kwa walengwa watumie mbinu za kisasa za ufugaji na kuongeza kipato.Mfugaji wa mazao ya baharini ya majongoo na kaa, Ali Hamadi alisema wanahitaji mbinu za kisasa ambazo zitaongeza uzalishaji ikiwamo kupatiwa vifaranga vyenye ubora.“Tunakosa mbinu za kisasa za elimu ya uzalishaji wa mazao ya baharini ambayo yataongeza mapato yetu.....wataalamu wa idara washuke chini kwa wananchi,” amesema.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezindua kituo cha kutotoa vifaranga kilichopo Beit-el-Ras nje kidogo ya mji wa Unguja ambacho kitakuwa kikizalisha vifaranga vya samaki wa aina mbali mbali ikiwemo majongoo na kaa.
0
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani, Donald Trump ametia saini sheria itakayoruhusu kuagizwa kwa dawa zinazohitajika kwa bei nafuu kutoka nje. Trump alitia saini maagizo manne yanayonuia kupunguza bei ya dawa kinyume na bunge ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic ambalo hadi sasa halijapitisha miswada kuhusiana na suala hilo.  Akizungumza kutoka ikulu, Trump alisema amechukua hatua hiyo ya ushupavu na kihistoria kupunguza bei ya dawa kwa ajili ya wamarekani wagonjwa na wazee.  Trump atakutana na wakuu wa kampuni za dawa siku ya Jumanne lakini baadhi ya wachambuzi wa masuala ya viwanda wamesema, hatua hiyo huenda isilete tofauti kubwa.  Katika taarifa, shirika la utafiti na utengenezaji dawa nchini Marekani limesema, serikali ya Trump imeamua kufuata sera hatari ya kudhibiti bei kulingana na viwango vinavyolipwa na mataifa ambayo Trump ameyataja kuwa ya kisoshalisti. Amesema sera hizo zitawaathiri wagonjwa kwa sasa na siku za usoni.
3
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Serikali imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu watatu kwa kosa la kukutwa na tausi watatu wanaodaiwa kuwa wa Ikulu. Washtakiwa hao David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally, wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 25, mbele ya Hakimu Mkazi Vicki Mwaikambo. Wakili wa serikali Mkuu Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon, wamedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Julai Mosi mwaka 2015 hadi Oktoba 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijihusisha na kuratibu mtandao wa uhalifu kwa kujihusisha na biashara ya ndege aina ya tausi bila kuwa na kibali kutola kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori. Imedaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walikutwa na tausi watatu wenye thamani ya Dola za Marekani 1500 sawa na Sh 3,444,150 mali ya serikali  bila ya kibali. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu aliwataka Washtakiwa hao kutojibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Kesi itatajwa Novemba 7 mwaka huu.
1
Na Fredy Azzah, Dodoma Mbunge Jimbo la Mbinga (CCM), Sixtus Mapunda, amesema wimbo ulioimbwa bungeni leo wakati wa kufungua mkutano wa 11 siyo ule rasmi. Akiomba mwongozo wa Spika, Mapunda amesema wimbo huo una makosa mengi kuanzia kwenye ala, mdundo na maneno na kwamba wimbo wa taifa unaoimbwa bungeni unatofautiana na ule unaoimbwa kwenye maeneo mengine ikiwamo kwenye shughuli muhimu ambapo alisisitiza wimbo huo si ule uliothibitishwa na mamlaka husika. Dk. Tulia, akijibu mwongozo huo amesema anahitaji muda akasikilize tena wimbo huo ili abaini tofauti hizo alizoziainisha mbunge huyo.
1
India Walimu wawili nchini India, wanatuhumiwa kumbaka msichana kipofu aliyekuwa akisoma katika shule ya watoto wenye ulemavu kwa muda wa miezi miwili. Walimu hao Chaman Thakor, (62) na Jayanti Thakor (30), inadaiwa walimbaka msichana huyo wa miaka 15 kwenye chumba cha muziki cha shule hiyo. Taarifa ya shambulio hilo ilibainika baada ya familia ya mwanafunzi huyo kukataa kurudi shule ya bweni huko Ambaji, Gujarat baada ya likizo ya Diwali mwezi uliopita. Mwanafunzi huyo alivunjika moyo na kumwambia shangazi yake, akielezea shida anazopata mikononi mwa walimu hao wawili ambapo shangazi yake huyo aliwasiliana na polisi na kuwaelezea. Aliwaambia alibakwa kwanza kwenye chumba cha muziki na Chaman Thakor miezi miwili iliyopita na kisha Jayanthi Thakor alidaiwa kumshambulia katika chumba kimoja siku tatu baadaye. Msichana alikuwa ameandikishwa katika shule ya bweni Julai mwaka huu kusoma muziki na alikuwa akisoma darasa la nane katika kijiji chake. Inspekta wa polisi, Ambaji, JB Agrawat, aliliambia gazeti la Times la India kwamba watu hao wawili walikimbia baada ya uhalifu wao kugunduliwa.
3
Simba ikiwa nyuma kwa mabao 2-0 iliibuka na kushinda mabao 3-2 katika dakika za majeruhi na kuwafanya kurudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 58, juu ya Yanga yenye pointi 56 ikiwa na mechi moja mkononi.Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa, Simba ilionekana kuelemewa karibu muda wote wa mchezo kabla ya kuzinduka dakika za mwisho na kupata mabao yaliyofungwa na Fredrick Blagnon na Mzamiru Yassin.Akizungumza baada ya mechi hiyo juzi, kocha Mayanja alisema mechi za Kanda ya Ziwa ngumu hivyo kuwataka wachezaji wake kupambana katika mechi yao ya mwisho kwenye ukanda huo dhidi ya Toto Africans itakayochezwa Jumamosi ya wiki hii.Kabla ya mechi dhidi ya Mbao, Simba ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba.“Sasa tumebakiza mechi moja huku (Kanda ya Ziwa) dhidi ya Toto na yenyewe tunaamini itakuwa ngumu pia, ni suala la wachezaji wetu kupambana kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu,” alisema.“Lazima tupambane na kuhakikisha tunashinda michezo yetu. Mechi za Kanda ya ziwa ni ngumu sana na timu zimejipanga kuhakikisha zinapata ushindi, Mbao FC walianza kucheza kwa kupania lakini mabadiliko ya Fredrick Blagnon alileta mabadiliko katika timu na kuwasumbua mabeki wa Mbao FC,jambo liliopelekea mabeki wao kuanza kubutua ovyo,” alisema Mayanja.Mayanja alisema wanao muda wa kutosha kujiandaa dhidi ya Toto kabla ya kurudi Dar es Salaam kumaliza ligi.Naye kocha mkuu wa Mbao, Mrundi Etienne Ndairagije alisema timu yake ilicheza vyema licha ya kupoteza mchezo huo dakika za mwisho.“Tulicheza mechi yetu vizuri sana na vijana wangu walicheza muda mwingi kwa kujituma. Mchezo ulikuwa mzuri sana sijaona makosa yoyote kwa timu yangu, ’’ alisema.Aidha aliwapongeza waamuzi wa mechi hiyo kwa kuchezesha vizuri pamoja na kikosi cha Simba kwa kutumia nafasi walizopata kuondoka na ushindi. Matokeo ya juzi yanaifanya Mbao kubaki kwneye nafasi ya 11 ikiwa na pointi 27 baada ya michezo 26.
2
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM MADAKTARI bingwa watatu wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu pamoja na magonjwa ya ndani wa Chuo Kikuu cha Kimataifa na Hospitali ya Peking, nchini China kwa mara ya kwanza wametua nchini katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI). Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk. Respicious Boniface alisema huo ni mwanzo wa ushirikiano na kwamba lengo ni kuimarisha ubingwa wa ndani ili kuendelea kusaidia watanzania. “Tumepokea ugeni wa mabigwa kutoka China, watarejea kwao Februari 26, mwaka huu, lengo hasa ni kushirikiano nao katika kujenga uwezo wetu wa ndani,” alisema. Dk. Boniface alisema kulingana na sensa ya watu na makazi inakadiriwa watanzania wapo takriban milioni 50 lakini mabingwa wa upasuaji ubongo wa ndani waliopo nchi nzima ni wanane pekee. “Tuna uhaba mkubwa wa wataalam ili kutosheleza mahitaji inahitaji wawe angalau 200, hapa MOI wapo watatu tu, na kwa siku katika kliniki yetu tunaona wagonjwa wapatao 500 hadi 600. “Kwa wastani daktari mmoja hapa MOI anaona wagonjwa wapatao 30 kati ya hao, watatu huwa ni wanaohitaji upasuaji wa ubongo, hii ni kazi ya kujitolea tunafanya wakati mwingine hadi muda wa ziada, hatuwezi kuwaacha wagonjwa, tunapata muda wa kupumzika, pindi tunapomaliza kliniki,” alisema. Alisema tayari wameshaandaa wagonjwa wanne watakaofanyiwa upasuaji na mabingwa hao siku ya jumatatu (Februari 25,mwaka huu). Alisema pamoja na uhaba wa wataalam bado pia wanakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba ili kuweza kutosheleza mahitaji. “Ndiyo maana tunaona ujio wao ni mwanzo wa ushirikiano mzuri kwani kwa wataalam tulionao wataweza kupata ujuzi zaidi utakaosaidia kuboresha huduma ya afya kwa watanzania,” alisema Dk. Boniface. Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, alisema ndani ya ushirikiano huo mabingwa wa chuo hicho watakuwa wakija nchini na mabingwa wa ndani watapata fursa ya kwenda China kujifunza zaidi. “Ushirikiano huu tuliuanza rasmi mwaka jana baada ya Rais John Magufuli kutuagiza twende katika hospitali hii huko China, tulikwenda mapema April, mwaka jana. “Tulikubaliana wataalam wao waje nchini kushirikiana nasi lakini pia wataalamu wetu watakuwa wanakwenda nchini mwao kujifunza zaidi,” alisema. Akizungumza, Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo wa Chuo Kikuu cha Kimataifa na Hospitali ya Peking, Profesa Yuanli Zhao alisema pindi watakaporejea nchini mwao wataishawishi serikali yao kusaidia upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba ili kuiongezea nguvu MOI. “Ni mara yangu ya kwanza kuwapo Tanzania, nina matumaini makubwa kwamba ushirikiano kati yetu utakuwa wa manufaa zaidi kwa watanzania,” alisema.
5
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewakaribisha makada wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa katika uchaguzi kujiunga na Chadema. Wiki iliyopita Kamati Kuu ya CCM na baadaye Halmashauri Kuu, vilipitia majina 1,400 ya walioomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya za CCM ambazo ni sawa na zile za kiserikali na kufanikiwa kuchuja hadi kufikia 161. Akitangaza maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alitaja wilaya tano, zikiwamo Siha, Moshi Mjini, Hai na Makete, kuwa hazikupata wagombea wenye sifa kutokana na kasoro nyingi za kimaadili na kikanuni zilizojitokeza. Kutokana na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi katika ngazi hiyo. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Lowassa alisema: “Nimesoma na kusikia baadhi ya waliokuwa viongozi katika Chama Cha Mapinduzi wamekatwa ama kutetea nafasi zao au kugombea, kwa sababu mbalimbali. Na jina langu limekuwa likiendelea kutajwa tajwa humo. “Mimi nawaambia hawa Watanzania wenzetu waliokatwa huko CCM nawakaribisha huku Ukawa wafurahie demokrasia. “Huku niliko kuna maisha mazuri ya kisiasa, uhuru wa fikra na demokrasia halisi,” alisema Lowassa, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema. Mbunge huyo wa zamani wa Monduli alisema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere alisema ni wakati mwafaka kwa Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi.  
1
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amesaini mkataba wa kufundisha klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda kucheza ligi kuu kuanzia msimu ujao. Zahera aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instragram majira ya usiku kuwa anarudi Tanzania kuungana na timu ya Gwambina ambayo itacheza ligi Kuu Tanzania bara Agosti 21, 2020. Novemba 5, 2017 Klabu ya Yanga ilivunja mkataba wa Zahera pamoja na benchi nzima la ufundi sambamba na kuvunja kamati ya mashindano. Zahera aliiongoza Klabu ya Yanga kwa miezi 15 akichukua nafasi ya ya Mzambia, George Lwandamina.   Kocha Mkuu wa zamani wa club ya Yanga SC Mwinyi Zahera usiku huu ametangazwa kupitia kurasa za instagram za Gwambina FC ya Misungwi Mwanza kuwa ameungana nao, Zahera anarudi Tanzania kuungana na Gwambina timu ambayo itacheza Ligi Kuu Tazania bara 2020/21 #MillardAyoSPORTS pic.twitter.com/dcDN4FSiI5 — millardayo (@millardayo) August 10, 2020
2
SERIKALI imesema katika mkataba wa kukarabati reli ya zamani (Meter Gauge) unajumuisha uletaji wa mabehewa mapya 44, lengo ni kuongeza mabehewa ya kubeba mizigo iliyopo Bandari ya Dar es Salaam ili kukuza uchumi haraka.Aidha, Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeshafanya ukarabati wa mabehewa 16 huku mengine 11 yakiendelea na ukarabati ambayo yanapita katika reli ya mitageji na kwamba wanatarajia kuongeza mabehewa kufikia 700 ili kuwa na uwezo wa kubeba mizigo mingi.Akizungumza wakati wa kukagua ukarabati huo jana, Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele alisema kuwa kazi ya kutoa mizigo bandarini ikifanywa kwa wakati itasaidia kuongeza mizigo mingi na nchi zinazopataka nazo, zitanufaika na bandari hiyo. Kamwele alisema ili kufikia malengo hayo ni lazima wahakikishe miundombinu inakarabatiwa na kwamba sasa hivi, wanaendelea na ukarabati wa bandari kuanzia gati namba moja hadi saba ili kuongeza kina cha bahari.Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa meli zenye uwezo wa kubeba kuanzia tani 60 zinaingia bandarini hapo ili kuongeza mzigo. “Meli ikiingia inatakiwa siku mbili iwe imekwisha pakua mizigo na ili kuondoa migongano katika bandari tunajenga bandari kavu eneo la Kwala. Hii itasaidia baada ya makontena kupakuliwa kwenye meli yatachukuliwa na treni kwenda Kwala ambako ni kilometa 115,” alisema Kamwele.Alisema pia kuwa wanataka bandari hiyo iwe wazi ili watu wanapoleta mizigo iweze kusafirishwa kwa haraka kupitia reli ya kati na kusisitiza kuwa mikataba mbalimbali imeingiwa ikiwa ni pamoja na ukarabati wa reli kilometa 970 na ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) ambapo mizigo itapitishwa kutoka bandarini na kwamba Februari mwaka huu mataruma pamoja na reli yataingia nchini. “Ukarabati wa reli hii utatumia Sh bilioni 690, mikataba tayari tumekwisha saini na kazi inaendelea na vifaa vipo majini mwezi wa pili vitaingia.Rais John Magufuli ametoa fedha Sh bilioni tano kwa ajili ya kukarabati mabehewa kwa sababu tumeona badala ya kununua mapya tunaweza kukarabati yaliyopo,” alisema Kamwele alisema mabehewa 16 yamekwisha kamilika, mawili yanapakwa rangi na 11 yanaendelea na ukarabati na kwamba TRC imeahidi kukarabati mabehewa 20 kwa mwezi na kuongeza kuwa mazingira mazuri ya usafirishaji nchini yatasaidia wafanyabiashara wengi kutumia bandari hiyo na kupitisha makontena kupitia reli zilizopo. “Tunaendelea kuhamasisha taasisi zote za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), TRC na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) waweze kufanya kazi kwa pamoja ili kuongeza chachu ya ukuaji wa uchumi.
1
Mwekezaji wa Klabu ya Simba ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo Mohammed Dewji almaarufu MO amekosa baadhi ya watu wanaotupa lawama kwa Taifa Stars kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza wa Kundi C dhidi ya Snegal, katika michuano ya Afcon 2019 huko nchini Misri. Katika mchezo huo, Taifa Stars ilipoteza kwa kufungw mabao 2-0. Katika mchezo huo, Stars sio tu walipoteza bali walizidiwa kwa kila kitu na wapinzani wao Senegal kutokana na uzoefu wa kikosi chao katika michuano mikubwa duniani. Takribani asilimia 100 ya kikosi cha Senegal kilichoanza, wachezaji wote wanacheza soka la ushinda katika vilabu vya Ulaya ukifananisha na Taifa Stars ambao ni wachezaji wachache tu wanaocheza Ulaya akiwemo nahodha Mbwana Samatta na pamoja na Adi Yusuf ambaye hata hivyo hakupata nafasi ya kucheza siku hiyo. “Ni rahisi kuchambua mapungufu ya #TaifaStars uwanjani lakini naomba tusilalamike sana. Hebu tutazame kikosi cha Senegal kisha tukitathmini na chetu. Wachezaji wao wapo Barcelona, Liverpool, Everton n.k. Ukiacha uwezo (skill) wenyewe, uzoefu (experience) na EXPOSURE ni kila kitu!” Ameandika Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter. Walistaili kutupiga hata 5.. — Chris Enock🍌 (@chrisenock93) June 24, 2019
2
JUBA, SUDANI KUSINI Maofisa wawili wa mabingwa wa soka nchini Sudan Kusini, klabu ya Atlabara, wameuawa na watu wasiojulikana kutokana na machafuko yaliyotikisa mji mkuu wa Juba wiki iliyopita. Shirikisho la Soka la Sudan Kusini (SFA), limetangaza kuwa maofisa hao walivamiwa na kupigwa risasi na watu wasiojulikana, usiku wa kuamkia Jumamosi. Rais wa SFA, Chabur Goc, aliwataja viongozi hao kuwa ni William Batista na Leko Nelson. “Shirikisho la soka nchini Sudan Kusini, linasikitika kutangaza vifo vya viongozi wa mabingwa watetezi wa klabu ya Atlabara, ambao wamepigwa risasi na watu wasiojulikana, ni jambo la kusikitisha, pia ni pigo kubwa kwa soka la Sudan. “Uchunguzi unaendelea kufanyika kuwatafuta wahusika wa tukio hilo, na tunaomba Mwenyezi Mungu awaweke mahali pema peponi,” alisema Goc. Kwa upande wao, uongozi wa Atlabara umesema kuwa umeguswa na vifo vya viongozi hao na kwamba wapo pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Batista alikuwa katibu mkuu katika klabu hiyo wakati huo Nelson alikuwa akihudumu kama meneja mkuu wa Atlabara. Mapigano nchini humo yamekuwa yakiendelea kwa siku za hivi karibuni kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa kwanza wa Rais Dk. Riek Machar.
2
Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Benedict Mashiba, ambapo amemtaka kuimarisha mahusiano baina ya nchi zote mbili. Alikutana na Balozi Mashiba jana katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi. Pia amemtaka kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususani katika sekta ya viwanda. Alisema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii, pia amemtaka kuboresha biashara baina ya Tanzania na Malawi kwa kutumia meli mbili za mizigo za Mv Ruvuma na Mv Njombe alizozizindua hivi karibuni. Hata hivyo, Waziri Mkuu amemtaka Balozi Mashiba kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio nchini Malawi na kuwasisitiza kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia kuwaunganisha pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini. Kwa upande wake Balozi Mashiba alisema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Malawi
1
PARIS, UFARANSA NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs, ameweka wazi kuwa atakimbilia nchini Ufaransa kwa ajili ya kuwa kocha mkuu katika klabu za nchini humo. Mchezaji huyo ambaye baada ya kustaafu soka alikuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo ya Man United, lakini alikuja kufukuzwa kazi baada ya kocha wa sasa, Jose Mourinho kujiunga na klabu hiyo wakati wa majira ya joto mwaka huu. Nyota huyo alikuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo kwa misimu miwili akiwa chini ya kocha Louis van Gaal, lakini ujio wa Mourinho ulimfanya awe katika wakati mgumu, ambapo Mourinho aliamua kuja na benchi lake jipya la ufundi. Giggs alihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Celtic baada ya kuondoka United, lakini hadi sasa hajafanikiwa kupata timu, ila anaamini kuwa baada ya kukosa nchini England basi ana nafasi kubwa ya kuwa kocha nchini Ufaransa. “Kuna klabu mbalimbali ambazo zimeonesha nia ya kutaka kufanya kazi na mimi, nimekuwa nikiangalia wapi sehemu sahihi kwa kuwa lengo langu ni kutaka kuja kuwa kocha mkubwa kama ilivyo kwa makocha wengine. “Si kila klabu ambayo inaonesha nia ni lazima nifanye nayo kazi, kikubwa ni kuangalia mipango ya klabu pamoja na manufaa yangu binafsi. “Nchini England kuna timu nyingi ambazo zilionesha nia ya kutaka kufaya kazi na mimi, lakini hatukufikiana mwisho, hivyo ni wakati sasa wa kugeukia nchini Ufaransa kwa ajili ya kuanza maisha yangu mapya. “Siangalii nitakuwa katika klabu gani, ila naweza kuwa katika klabu ya Ligi Kuu au Ligi daraja la kwanza, bila ya kujali Ligi lakini ninaamini nitakuwa nchini Ufaransa,” alisema Giggs. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, kwa sasa anafanya biashara zake pamoja na kocha wa timu ya taifa ya vijana, Gary Neville. Mbali na kufanya biashara, pia kwa sasa kocha huyo ni mchambuzi wa michezo.  
2
KIGALI, RWANDA MWANAMUZIKI maarufu nchini Rwanda, Ngabo Medard Jobert maarufu kama Meddy, amelazimika kusitisha ziara yake ya kimuziki katika nchi jirani ya Burundi kwa sababu za kiusalama. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa, RFI, imesema mwanamuziki huyo alitarajiwa kuwaburudisha wafuasi wa muziki wake jijini Bujumbura mwishoni mwa wiki hii, na sasa ziara hiyo kwa mujibu wa meneja wake, itafanyika wakati mwingine. Taarifa hiyo imeoneza kuwa uamuzi wa mwanamuziki huyo umechangiwa na hali iliyopo sasa ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili kuwa mbaya hivyo kuzua hofu  za kiusalama. Serikali ya Bujumbiura inawatuhumu viongozi wa Rwanda hususani Rais Paul Kagame mwenyewe kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kufanya kila wawezalo ili kumuondoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Madai ambayo Rwanda imetupilia mbali na kusisitiza kuwa tuhuma zinazotolewa na serikali ya Burundi ni mbinu za kutaka kujihusisha na mauaji ya kimbari dhidi ya wapinzani wake. Zaidi ya raia wa Burundi 250,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwezo Rwanda, kufuatia kuzuka kwa machafuko na mivutano ya kisiasa nchini Burundi. Machafuko nchini Burundi yalianza mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka 2015 kufuatia hatua ya Pierre Nkurunziza ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu. Licha ya kutekelezwa jitihada za kimataifa kwa minajii ya kuhitimisha mgogoro wa Burundi, lakini juhudi hizo hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda.
4
PYONGYANG, Korea Kaskazini KIONGOZI wa nchi hii, Kim Jong-un, juzi aliondoka kwa kutumia usafiri wa treni kwenda katika mji wa Hanoi kwa ajili ya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump. Mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano na Alhamisi katika mji huo mkuu wa Vietnam. Mkutano huu unakuja baada ya wa kwanza wa kihistoria uliofanyika mwaka jana nchini Singapore na macho yote yatakuwa yakitazama kama kuna hatua yoyote iliyopigwa tangu wakati huo kuhusu kuteketeza silaha za nyuklia. Taarifa zilizopatikana mji  hapa zinaeleza kuwa Rais Kim Jong-un amesafiri na dada yake, Kim Yo Jong na mmoja kati ya washauri wake muhimu, Jenerali wa zamani, Kim Yong Chol. ”Tulipendana,” Trump aliuambia mkutano Septemba mwaka jana kuhusu Kim.” Aliniandikia barua nzuri,” aliongeza kiongozi huyo. Hata hivyo, pamoja na maneno hayo mazuri, miezi kadhaa baada ya mkutano wa Juni mwaka jana, ilitawaliwa na kauli za msuguano na mahusiano yasiyoridhisha.  Mkutano huu unatarajiwa kuendeleza misingi ya mkutano uliopita kuhusu masuala ya silaha za nyuklia, ambapo wataalamu wanasema jitihada zilizofanyika ni kidogo na kwamba zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkutano huo wa Hanoi, ajenda zake hazijawekwa wazi. Wachungizi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba, licha ya mkutano wa Juni mwaka jana nchini Singapore kati ya viongozi hao kuwa ulikuwa ni wa kihistoria, lakini makubaliano waliyoyatia saini hayakuwa dhahiri na hatua kidogo zimechukuliwa kuhusu lengo la kukomesha silaha za nyuklia. Wanasema katika mkutano huo, Rais Trump aliahidi kukomesha vitendo vya majaribio ya silaha za nyuklia, akishirikiana na Korea Kusini ambavyo vimeighadhabisha Korea Kaskazini, lakini miezi imepita sasa wengi wakihoji yeye amefanya nini kwa upande wake.
3
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamepangwa na Le Messenger Ngozi ya Burundi katika mbio za kusaka taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika.Wakati Simba wakijiandaa na Warundi hao, wenzao wa Zanzibar JKU wenyewe watakuwa na kibarua kigumu baada ya kupangwa kuanza na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa mashindano hayo.Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Afrika, Caf, ratiba hiyo ilipangwa juzi usiku.Le Messenger FC ndio mabingwa wa Burundi kwa sasa na uwanja wake wa nyumbani ni ule wa Urukundo uliopo Bujumbura na una uwezo wa kuchukua watazamaji 5,400 kwa wakati mmoja.Timu hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na haina uzoefu mkubwa na mechi za kimataifa ukilinganisha na wapinzani wao Simba, mabo wamecheza mara nyingi mechi za Caf.
2
Akizungumza na gazeti hili jana kocha msaidizi wa timu hiyo, Charles Mkwasa alisema kuwa, hawana wasiwasi nao na watahakikisha wanaibuka na ushindi.Mkwasa alikiri kuwa Etoile ni kubwa barani Afrika, lakini alisema hilo haliwatii hofu kwani kikubwa ni kujiandaa vizuri na tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo.Akielezea ratiba ya kuanza na Etoile nyumbani kama ilivyo michezo miwili iliyopita, Mkwasa alisema hilo halina tatizo kikubwa ni kuhakikisha kuwa wanashinda kwa ushindi mkubwa kama ilivyokuwa kwa michezo mingine.Alisema kuwa wachezaji wake wanaendelea na mazoezi kama kawaida kwa kuwa wanashiriki kwenye michezo ya Ligi Kuu na wanazichukulia mechi hizo kama mazoezi ya kucheza na Waarabu hao.“Najua kwa sasa kuna ligi inaendelea na wachezaji hawa wanatumia michezo hii ya ligi kujiandaa kwa mchezo huo ujao pia, lakini labda kunakuwa na tu msisitizo wa hapa na pale katika kuwakumbusha kuwa haya yanayofundishwa kwenye michezo ya ligi yaendelee na katika mchezo huo wa kimataifa,” alisema kocha huyo msaidizi.Kwa sasa Yanga imefuzu hatua ya 16 bora Afrika baada ya kuitoa timu ya FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2, katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa 5-1 na baadae kufungwa 1-0 huko Bulawayo.Mkwasa aliwatoa wasiwasi mashabiki hao kwa timu yao kufungwa katika mechi za marudiano ugenini ikilinganishwa na ile ya hapa nyumbani.Alisema kuwa hali hiyo haina maana kuwa wachezaji wake wamekuwa wakishindwa ugenini kwa kutojiamini isipokuwa hiyo ni hali ya mchezo kama michezo mingine.
2
MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda amempatia siku saba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (DED), Missana Kwangura kuwasilisha polisi majina ya watumishi waliostaafu walioshindwa kukabidhi pikipiki kwa halmashauri hiyo ili wamakatwe na kushtakiwa . Aidha, amemwagiza Kwangura kuhakikisha katika kikao kijacho cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya anawasilisha hoja zote za mkaguzi wa ndani wa halmshauri hiyo zikiwa zimepatiwa majibu. Mtanda alitoa maagizo hayo jana wakati akiwasilisha kauli ya serikali katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kilichofanyika katika mji mdogo wa Namanyere.“Wapo watumishi wa halmashauri hii waliostaafu ambapo walikabidhiwa kwa ujumla wao pikipiki nane mali ya halmashauri, wapo waliouziana kwa bei chee, huku wengine wameshindwa kuzirejesha na kuzikabidhi kwa mwajiri wao baada ya kustaafu utumishi wa umma ..., Nampatia DED siku saba awe amewasilisha majina yao polisi ili wakamatwe na pikipiki hizo zirejeshwe halmashauri na kukabidhiwa watendaji wengine katika jitihada ya kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri hii,”alisisitiza. Alimtaka DED kusimamia maagizo hayo kwa vitendo ndani ya siku saba alizompatia kutekeleza agizo lake hilo. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Sumuni Mwamakula alimhakikishia Mtanda kuwa maagizo yake yatatekelezwa kama alivyoagiza huku akiwataka madiwani kuendelea kusimamia makusanyo ya mapato ya ndani kwa karibu kwa kuwa ndio uhai wa halmashauri hiyo.
1
Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM SUALA la Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, limechukua sura mpya baada ya meya huyo kuitwa  Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma na kutakiwa kujibu shauri lililofunguliwa la matumizi ya ofisi ya umma kwa shughuli za chama chake. Machi 22, mwaka huu Meya Jacob aliwasilisha mashitaka dhidi ya Makonda kwa Sekretarieti hiyo, akitaka achukuliwe hatua za  nidhamu kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kutumia vyeti feki na hivyo kukosa sifa ya kuwa kiongozi. Akizungumza na waandishi wa habari   muda mfupi baada ya kutoka katika mahojiano na sekretarieti hiyo jana, Jacob alisema sekretarieti hiyo imemwomba kujibu shauri hilo ikisema kwa kuwa hata yeye aliwahi kutumia Ofisi za Manispaa ya Ubungo kwa vikao vya chama chake. “Wameniomba kuondoa shauri hili kwa madai kuwa walipomwita Makonda alisema tuyamalize kwa kuwa hata mimi nilitumia ofisi ya umma kufanya vikao vya chama… mimi nimesema ruksa kunihukumu kama wana ushahidi wa kutosha,” alisema Jacob. Alisema uhalali wa Makonda kumhoji kuhusu kufanya vikao vya chama katika ofisi ua umma ndiyo mwanzo wa uhalali wa kumhoji mkuu wa nchi uhalali wa kufanya vikao vya chama Ikulu. “Hakuna kikao ambacho nilikiongoza mimi nikiwa na wafuasi wa chama, ninachojua nilitembelewa na Frederick Sumaye. Kiongozi wa Chadema akinitembelea nimkatae? “Lakini wenzetu wamefika mbali kwa kuvaa sare za chama na kuzungumza masuala ya chama,” alisema. Alisema wanaporuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kumuuliza kuhusu hilo walipaswa waanze kujitafakari kuwa kuna Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inafanyika Ikulu. Alisema walimwambia hakuna mtu aliyewahi kulalamika kwa nini mikutano ya CCM inafanyika Ikulu. “Sheria inasema wao waliposikia tu kuwa Makonda ana vyeti feki walitakiwa kumwita na si kusubiri mtu aende kushtaki. “Wao kama wasimamizi wa maadili ya umma wakiona mtu anarudisha fedha za rushwa benki hawakustahili kusubiri mtu wa Chadema kwenda kushtaki,” alisema Jacob. Jacob alisema alipewa dakika 10 za kuandika malalamiko   kwa nini CCM inafanyia vikao vyake Ikulu. “Nimewakabidhi ushahidi wa picha na video za vikao vya Chama cha Mapinduzi Ikulu,” alisema Jacob. Alisema lengo lake si kulalamika kuwa CCM inafanyia vikao vyake ikulu bali suala la vyeti feki ambalo anahitaji lifikishwe katika Baraza la Maadili.
1
BELFAST,IRELAND NYOTA wa mchezo wa tenisi, Andy Murray, ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa tenisi wa BBC baada ya kuwazidi wapinzani wake kwa kura nyingi. Tuzo hizo ambazo zilifanyika huko Ireland ya Kaskazini, Murray alifanikiwa kushinda kwa idadi ya kura 361,446, sawa na asilimia 35 dhidi ya Kelvin Sinfield ambaye alipata kura 278,353, sawa na asilimia 28 na Ennis Hill akipata kura 78,898, sawa na asilimia 8. Hii ni mara ya pili kwa Murry kuchukua tuzo hiyo, na mwaka huu ameonekana kuboresha kiwango chake na amefanikiwa kufikia fainali za mashindano ya Australia na fainali za Wimbledon. “Nashukuru sana kufanikiwa kuchukua tuzo hii kwa kuwa sikutegemea, lakini leo nina furaha kubwa na ninaamini kila kitu kinawezekana katika maisha. “Hii ni safari ya miaka mitano kwenye tenisi, nilianza kama utani nikishika nafasi ya mwisho, lakini leo hii najikuta nikishika nafasi ya kwanza, nashukuru sana,” alisema Murray.
2
Elizabeth Kilindi, Njombe CHANGAMOTO ya uwapo wa virusi vya corona imeathiri kwa kiasi kikubwa uchangiaji damu Wilaya ya Makete, mkoani Njombe, na kusababisha kutokufikia lengo lililokusudiwa. Kwa sasa, kiwango cha uchangiaji damu kimepungua kwa sababu wachangiaji wakubwa walikuwa ni wanafunzi wa sekondari na vyuo ambao wamerudi majumbani baada ya masomo kusitishwa kwa lengo la kuepuka msongamano unaoweza kuchangia maambukizi mapya ya virusi hivyo. Akizungumza na Mtanzania, Mratibu wa Damu Salama Wilaya ya Makete, mkoani Njombe, Sergio Mkwama, anasema ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona umeathiri kwa asilimia 80 suala la uchangiaji damu wilayani humo. “Hii ni kwa sababu yale maeneo ambayo tulikuwa tunatarajia kwa kiasi kikubwa kukusanya damu au kuhamasisha utoaji wa uchangiaji damu ilikuwa ni sehemu za shule na vyuo mbalimbali,’’ anasema Mkwama. “Sasa tangu ulipoingia huu ugonjwa hizi sehemu zimefungwa ili kuepuka mikusanyiko. Kwa hiyo, ile nafasi ya kwenda kuwafikia hao wachangiaji damu imekuwa ni ngumu, tunapata changamoto,’’ anasema Mkwama. Anasema njia wanayotumia kuhamasisha jamii ni kufika katika vituo vya afya ili kuweza kuchangia licha ya kuwa muitiko sio mkubwa kama ilivyokuwa hapo awali. “Njia ambayo tunahamasishana na jamii ni kufika kwa wataalamu kwenye vituo vya afya, wakifika pale wanaweza wakachangia damu kwa kufuata taratibu zote na Wizara ya Afya au mpango wa taifa wa kuchangia damu sambamba na serikali kufuata taratibu zote na kuchukua tahadhari zote kwa kufuata taratibu zote za uchangiaji damu salama kwa hiyo, watu wasiogope kwamba pengine nikifika kule ndio nitapata ugonjwa,’’ anasema Mkwama. Anaongeza: “Mchangia damu hawezi kupata ugonjwa wa corona kwa sababu mazingira ni salama na tahadhari zote zinachukuliwa kwa hiyo tunahamasisha wananchi wote kuona umuhimu wa kuchangia damu. “Tunapambana na corona ndio, lakini upande wa pili tunaathirika, kuna watu watakosa huduma ya damu kwa sababu ili ipatikane inatulazimu kwenda kuwahamasisha watu kuchangia kwa kufuata kundi au taasisi Fulani. Sasa hivi imekuwa ni shida kwa sababu mikusanyiko haipo kwa hiyo tunashindwa kuwapata watu kwa urahisi.’’ Anasema kufuatia hali hiyo imewalazimu kutembea katika taasisi mbalimbali ikiwamo makanisa. “Huko huwa tunapopata nafasi ya watu zaidi ya watano au watatu, tunatoa elimu ya kuhamasisha juu uchangiaji damu kwa wale wenye nafasi na afya njema wanaweza wakafika hospitalini na kuchangia. Kwa wale ambao hawana nafasi za kufika hospitalini tunafanya mawasiliano na wataalamu wa afya wanafika eneo ulilopo na tunafanya utaratibu wa wao kuchangia damu na zitaweza kufika hospitalini ili kuweza kusaidia watu,’’ anasema Mkwama. Mkwama anasisitiza kuwa hali ni mbaya kwa sababu wachangiaji damu hawapatikani. Kwa upande wake Yona Luvanda, anasema elimu ya uchangiaji damu itolewe kwa msisitizo kwa jamii kama ilivyokuwa vyuoni ili kusaidia makundi yenye uhitaji. “Elimu ya uchangiaji damu ihamie kwa jamii na kampeni hii iwe kama walivyokuwa wakifanya shuleni, jamii itajitokeza watachangia bila ya kujali tatizo hili la corona linalotukabili hivi sasa,’’ anasema Luvanda. Naye Mery Lwiva, anasema kutokana na uwapo wa virusi vya corona, watu wengi wamekuwa wakijilinda wao na kusahau wajibu wao. “Tumesahau wajibu wetu wa kuchangia damu, tunapojilinda sisi tukumbuke na makundi ambayo yalikuwa yakitutegemea kwenye suala la damu, tubadilike la sivyo tutasababisha vifo vya wajawazito, watoto wachanga na hata wale wanaopata ajali kutokana na kukosekana kwa damu,’’ anasema Mary.
5
NEW YORK, MAREKANI RAPA Jay-Z, amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa muziki nchini Uingereza, Amy Winehouse, akidai kuwa msanii huyo hakusikia ushauri wake. Amy alikutwa amepoteza maisha nyumbani kwake jijini London, Julai 23, 2011, kifo hicho kilitokana na matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya. Jay Z amedai kwamba, mara ya kwanza kukutana na msanii huyo jijini New York alimtaka kuungana pamoja, lakini Amy alionekana wazi kuwa hataki. “Mara ya kwanza kukutana naye niliamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kuimba, nilimwomba aungane na sisi lakini hakuonesha kukubali, nilikuwa na lengo la kutaka kumbadilisha ili aweze kuachana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe, lakini hakutusikiliza,” alisema Jay Z.
3
Mwandishi Wetu -Singida BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 katika wilaya kadhaa nchini. Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanya biashara humu nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu, inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama wa raia. Benki  ya NMB imeshatoa  msaada wa  vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mikoa ya Kanda ya Kati. Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani ingida, Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ya zaidi ya Sh milioni 200 iliyotolewa imelenga sekta ya elimu, afya  na majanga kwa mikoa mitatu ya  Kanda ya kati. Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewa na NMB zimetumika kununua madawati, viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya. Aidha, alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali. Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule, zahanati, hospitali katika mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara. Pia NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 29.5 kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo. Katika hatua nyingine, Benki hiyo imevipatia kituo cha Polisi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati 160 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa ajili ya kuezekea maboma. NMB iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wa kuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini, Meneja wa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus, alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi ya maendeleo. Baraka alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepa tamabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati 80.
0
MWANAMITINDO maarufu nchini Hispania, Georgina Rodriquez ambaye ni mchumba wa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, anatarajia kujifungua watoto mapacha. Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, mchezaji huyo ameweka wazi kwamba ameandaa nyumba yenye thamani ya Sh bilioni 13 kwa ajili ya kufikia watoto hao na pia ameweka vito mbalimbali vya thamani kwa ajili yao. Ronaldo ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr, ujio wa watoto hao utaongeza ukubwa wa familia yake lakini kwa mchumba wake huyo mwenye umri wa miaka 23 itakuwa ndio watoto wake wa kwanza. Kupitia akaunti ya Instagram, Georgina amedai kuwa familia hiyo kwa sasa ipo katika furaha kubwa ikiwa inatarajia kupata watoto hao wawili. “Muda mfupi ujao familia itakuwa kubwa na Cristiano Jr. anatarajia wadogo zake wawili, tuna furaha mno,” aliandika Georgina.
4
Na Hamisa Maganga, Bagamoyo Tanzania hutumia Sh trilioni 1.2 kwa ajili ya shughuli za kudhibiti Ukimwi kwa mwaka. Aidha, asilimia 93 ya fedha za kudhibiti Virusi vya Ukimwi (VVU) hutolewa na wahisani ambapo kati ya hizo asilimia 86 hutoka Marekani. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Yasin Abbas, amesema hayo leo Alhamisi Machi 8, wilayani Bagamoyo wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za VVU na Ukimwi. Amesema asilimia kubwa ya fedha hizo hutumika katika kununua dawa za kufubaza makali ya VVU (ARVs). “Asilimia 93 ya fedha hufadhiliwa na wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi, kati ya hizo asilimia 86 zinatoka Marekani kupitia programu yake ya PEPFAR na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund ATM). “Tanzania hutoa asilimia saba tu ya fedha zote. Hivyo, kupitia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF), tunatarajia kuongeza rasilimali za ndani kutoka asilimia saba mwaka 2015 hadi asilimia 30 mwaka huu,” amesema Abbas. Hata hivyo, amesema iwapo watafanikiwa kufikia lengo, Tanzania itaondokana na utegemezi kwa asilimia kubwa.
5
Ripoti ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, inasema mapigano ya kutumia silaha nzito na mashambulizi kutoka angani vimeendelea katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Libya, Tripoli na viungani. Ripoti inasema katika viunga vya Tripoli, katika maeneo ya Abusliem, Souq Jumaa na Hadbaa, makombora yamesababisha vifo vya watu sita wakiwemo wanawake wanne na kuwajeruhi watu wengine 20. OCHA inasema tangu kuanza kwa vurugu, inakadiriwa kuwa watu 80 wamejeruhiwa na wengine 20 wamepoteza maisha lakini wale ambao wamethibitishwa ni wananchi 54 kujeruhiwa na wengine 14 kupoteza maisha.   Ripoti ya sasa imeonesha ongezeko la wanaokosa makazi kwa siku, ambapo zaidi ya watu 4,500 ni watu wapya waliopoteza makazi kiasi kinachoongeza idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia 25,000. Wananchi wengi waliokwama katika maeneo yenye mgogoro wamejikuta katika sintofahamu ya kutokujua ikiwa wabaki katika majumba yao au waondoke kwa sababu ya hali mbaya iliyoko huko nje ya mapigano na mabomu. Hali hiyo ya sintofahamu inazidi kuongezeka kwani chakula na mahitaji mengine muhimu vinazidi kupungua. Mgogoro wa sasa umeongeza hatari zaidi kwa watu baada ya mgogoro wa miaka mingi, mgogoro wa kiuchumi na kijamii na upungufu katika huduma za kijamii ambazo tayari zimewaweka takribani watu 820,000 waakiwemo watoto 250,000 katika uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu.
3
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM SIKU chache tangu kutokea kifo cha mtoto Happiness Josephat (6), aliyekuwa amefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa betri ndani ya moyo wake, hali ya wasiwasi imetanda miongoni mwa wagonjwa waliopandikizwa kifaa hicho. Wasiwasi huo umetanda kutokana na taarifa zinazosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, watumiaji wa mitandao hiyo wakidai kifo hicho kimesababishwa na kifaa hicho kushindwa kufanya kazi. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba ni za upotoshaji. “Kwanza jamii ielewe kwamba, JKCI tumesikitishwa mno na kifo cha Happiness kwa sababu tulikuwa tukifuatilia maendeleo yake kwa ukaribu, na kifo chake kimetushtua kwani kimetokea ghafla. “Baada ya kifo kile kumekuwa na taarifa nyingi zinazosambazwa mtandaoni ambazo si sahihi na zimepelekea wagonjwa wetu tuliowafanyia upasuaji wa aina hiyo kuwa na hofu na wasiwasi. “Ukweli ni kwamba kifaa kile tulichomuwekea hakikuwa na tatizo lolote, kilikuwa kinafanya kazi sawa sawa nah ii ni kwa mujibu mama yake, Elitruda Malley ambaye tulihojiana naye kujua alipatwa na shida gani. “Akatueleza kuwa alianza kulalamika kuwa anasikia maumivu ya tumbo, akachukua kifaa cha kupima mapigo ya moyo ambacho tulimpatia, alipompima kifaa kilionesha kuwa yalikuwa sawa sawa. “Lakini akatueleza bado mtoto alilalamika tumbo linamuuma, akampeleka hospitali ya Selian lakini hawakugundua tatizo na wakampatia dawa ya diclofenac kutuliza maumivu,” alisema. Profesa Janabi alisema hata hivyo tatizo hilo liliendelea ambapo mama huyo alimrudisha tena mwanawe hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi. “Lakini bado tatizo halikuonekana, na alipokuwa akipimwa mapigo ya moyo kifaa kilikuwa kinasoma yapo sawa sawa, ripoti ya awali ya madaktari wa selian inaeleza kuwa alisumbuliwa na tumbo, tumeomba watupatie uchunguzi ufanyike kwa kina na watupatie taarifa kamili,” alisema. Dk. Janabi alisema wanataka kufanya uchunguzi zaidi kwani hadi sasa jumla ya wagonjwa 31 wamefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa kifaa na wanaendelea vizuri pasipo shida yoyote. “Happiness ndiye mtoto wa kwanza nchini kuwekewa kifaa hiki ndiyo maana tulisema ni upasuaji wa kihistoria, tumesikitishwa mno na kifo chake, taarifa zetu zinaonesha alizaliwa Desemba 16, 2012 huko Mbulu, Manyara na Julai 15, mwaka huu tulimfanyia upasuaji wa kumpandikiza kifaa hicho baada ya kugundulika kuwa alizaliwa na tatizo lijulikanalo kitaalamu ‘heart break’. “Mfumo wa umeme wa moyo wake haukuwa unafanya kazi sawa sawa kama inavyotakiwa, ndio maana mapigo yake yalikuwa kati ya mara 20 hadi 25, madaktari wa JKCI tulifanya upasuaji huo kwa kushirikiana na wenzetu wa marekani na aliruhusiwa wiki mbili baadae, Agosti mosi, mwaka huu. “Tulitamani hata tungeweza kuufanyia mwili wake ‘postmotum’, ili tujue nini hasa kimesababisha kifo chake ikiwa kifaa tulichomuwekea kilikuwa kinasoma mapigo ya moyo vizuri,” alisema. Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya simu, Elitruda alisema amesikitishwa na taarifa zinazoenezwa mtandaoni kwani si za kweli. “Mwanangu akuugua kifua, bali tumbo na alikuwa anatapika, kifaa kilikuwa kizima.. mimi ni muelewa, ni muuguzi,  alinifia mikononi mwangu, nasikitishwa na uzushi huo wa mtandaoni,” alisema. Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo Idara ya Watoto, Edwin Sharau alisema kila mwaka duniani watoto 22,000 huzaliwa na tatizo kama alilokuwa nalo marehemu Happiness. “Takwimu zinaonesha Tanzania kwa mwaka huzaliwa mtoto mmoja, hali hiyo hutokea pale nguvu ya kupigana na magonjwa ya mama wakati wa ujauzito ‘antibody’ zinapovuka kwenye kondo la mama kisha kuingia kwa mtoto akiwa tumboni. “Asilimia 70 ya watoto wanaokumbana na nguvu hiyo, hufariki dunia, asilimia 25 huzaliwa lakini hufariki katika miezi ya kwanza na asilimia 85 kati ya hawa asilimia 25 ambao huzaliwa hufariki kwa sababu moyo wao hushindwa kufanya kazi ipasavyo,” alisema.
1
Mwandishi wetu, Tanga WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shidakulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao. Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimukwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu kwa kukishirikiana namaafisa wa TRA mkoa wa Tanga. Maafisa hao waliwatembelea wafanyabiashara kwenye maduka yaoyaliyopo barabara za namba jijini Tanga kwa lengo la kuwaelimisha nakuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.Sambamba na hilo, maafisa hao pia waliweza kusikiliza kerozinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao kama mpango wa kutengeneza mazingira rafiki kati yao naTRA.Thabiti Salimu ambaye ni mfanyabiashara wa Ukwaju wa jumla na rejarejakatika eneo la barabara za namba amesema kuwa, atamshangaamfanyabiashara atayekwepa kulipa kodi hususani katika kipindi hikiambacho wameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kupitia kodi zao. “Rais Magufuli anatumia kodi zetu vizuri, tunaona utekelezaji wa miradimingi ya maendeleo hivyo lazima tuendelee kulipa kodi la sivyo kazi yautekelezaji wa miradi hii itakwama,” alisema Salimu. Naye Dina Mbenu, mfanyabiashara wa vipuli vya pikipiki amesema kuwa,ikiwa wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi watasababisha madhara yakiuchumi na kuathiri jitihada za serikali za kuboresha miundombinuikiwemo barabara. Amesema hatua ya maafisa wa TRA kuwatembelea kwenye maduka yaokwa lengo la kuwahamasisha kulipa kodi na kusikiliza kero na maoni yaoinawasaidia kutopoteza muda kwenye ofisi za TRA wakisubiri kuhudumiwa. Kwa upande wake Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Julius Mjenga amesemazoezi la kuwatembelea wafanyabiashara ni endelevu na kabla ya kufanyikaTanga, zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,Mbeya na Morogoro. Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutoa elimu ya kodi, kuwakumbushawafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kusikiliza maoni yao pamoja nachangamoto kwa ajili ya kuzitatua.Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure, aliwaombawafanyabiashara kuunga mkono zoezi linalofanywa na maafisa wa TRA lautoaji elimu ya kodi, kusikiliza maoni na changamoto zao kwa kuwa zoezi hilo linalenga kuboresha huduma kwa mlipakodi.“Niwaombe wafanyabiashara wote mkiwaona maafisa wanatembelea,msifunge maduka, wapokeeni na kuwapa ushirikiano kwa kuwa wanalengakuwaelimisha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenyebiashara zenu ambazo kwa pamoja tunaweza kuzitafutia ufumbuzi,”alisema Owure. Amesema zoezi hilo la utoaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiasharamkoani humo linatarajiwa kumalizika Juni 30, 2020 na kwamba lengo likiwani kutaka kuwafikia wafanyabiashara wengi mkoani hapo.
0
RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, wameeleza matumaini makubwa kuwa, ziara ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, itafanikisha kuleta amani nchini Sudan Kusini.Viongozi wanaovutana nchini Sudan Kusini ni Rais Salva Kiir na makamu wake, Dk Riek Mechar.Akizungumza na HabariLeo kuhusu ziara ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao, Askofu Nyaisonga alisema kupatikana kwa amani nchini humo kutakuwa na faida kubwa si kwa Sudan Kusini pekee, bali kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Alisema hakuna biashara inayoweza kufanyika wakati wa machafuko, hivyo utulivu wa Sudan Kusini utainua biashana na uwekezaji kwa nchi hiyo na Afrika Mashariki kwa ujumla.Kilaini alipozungumza na gazeti hili jana kuhusu umuhimu wa ziara hiyo ya Papa ambaye ataongozana na Askofu Mkuu wa Canterbury wa Kanisa la Aglikana la Uingereza, Justin Welby, alisema:“Kabla ya ziara hiyo, Papa Francis ambaye amejitolea kufanikisha mchakato wa amani nchini humo, aliwaita viongozi wakuu wa taifa hilo wanaovutana Rais Kiir na Dk Machar katika makao makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican mapema mwaka huu ili kuwapatanisha lakini viongozi hao wakaendelea na mvutano wao".Kuhusu ushawishi wa ziara ya Papa katika kuleta amani, Kilaini alisema ziara hiyo ina ushawishi mkubwa kwa sababu wananchi wote wa Sudan Kusini watamwona Papa Fransis kama kiongozi wao.Alitolea mfano Papa Yohane Paulo II alipofanya ziara nchini Poland ambayo ilikuwa nchi ya kikomunisti na serikali yake ilikuwa haiaminiki, lakini alipofika watu wote wakaenda kwa Papa na ukawa ndio mwisho wa ukomunisti nchini humo mpaka leo.
1
Na RAMADHANI MASENGA KATIKA dunia ya utandawazi hutakiwi kuwa na misimamo isiyobadilika( Rigid). Mbali na kuamini sana mambo fulani, kanuni fulani ama hisia fulani ila pia unatakiwa kujua wakati unataka nini na kitu gani ukubali ama ukatae. Katika dunia ya muziki kuna wasanii wa aina tatu. Kwanza kuna wasanii wakali. Pili kuna wasanii promo. Tatu kuna wasanii wanaojitahidi. Habari njema ni kwamba hawa wote ni muhimu kutokana na mahitaji ya wakati. Wasanii wakali wanajulikana. Katika kundi hilo wapo wakina Young Killer, Harmonize, Msami na kina Diamond. Wasanii wanaojitahidi ni kama wakina Snura, Shilole na Hemed Suleiman. Wasanii promo wako wengi mno, miongoni mwao wako akina Gigy Money na Lulu Diva. Hapa japo kila mmoja ana uwezo wake na umahiri wake ila pia wamezidiana sana. Mfano. Mbali na Msodoki kuwa msanii mkali na mwenye mashairi adimu ila amezidiwa sana na Hemed Suleiman namna ya kujiweka kisanii. Hapa sizungumzi muonekano halisi( natural physical appearance). Nazungumzia namna anavyojiweka ili popote awapo ama lolote analofanya liwe habari na kuweza kuweka jina lake juu zaidi. Hili msodoki mbali na kipaji kikali. Akili iliyotulia ila kitu hiki hana. Hata Rubby. Mbali na kuonekana na vituko fulani ila kuna kitu anakosa. Anakosa namna ya kujiwekea ushawishi binafsi kama msanii. Mbali na kuwa mbabaishji katika sanaa ila Gigy Money akituliza akili ana uwezo wa kuwa na kitu hiki na kukimbiza sana Rubby. Kuna mambo watu wanashindwa kuelewa kuhusu ukali wa Diamond Plutnumz. Mbali na kuwa na kipaji kikali ila Diamond ameweza kujitengeneza na kuwa msanii bidhaa. Hiki wasanii wengi wakali hawana. Barnaba hana, Ali Kiba hana, Amin hana na wengine pia hawana. Ndiyo maana mpaka sasa kuna baadhi ukiwaambia Diamond ni msanii mkali Afrika mashariki na kati wanashindwa kuelewa. Wanashindwa kuelewa kwa sababu kwao sanaa ama muziki unaishia katika sauti na na mashairi pekee. Hapana. Katika dunia ya sasa ya utandawazi sanaa ni zaidi ya hapo. Sanaa ni jumla ya unavyoishi wewe na kutengeneza jina lako. Kwa zaidi ya miaka nane sasa jina la Diamond liko juu sio kwa sababu ya nyimbo zake tu. Ni zaidi ya hapo. Hata namna anavyoachia nyimbo zake ziko katika hali fulani ya utata ambao inafanya wapenzi wa muziki wajawe na shauku kabla. Nilikuwa namsikiliza msanii fulani akijisifia maisha yake ya kukaa maskani kama zamani kabla hajawa msanii. Alisema yeye bado hajabadili maisha na hategemei kubadili misha yake. Kwake kufanya hivyo ndio ubinadamu. Ndiyo uungwana. Na ndiyo utanzania. Asichokijua ni kwamba ili thamani na hadhi yake ionekane juu ni lazima abadili mfumo wake wa maisha. Ni lazima aifanye jamii yake imuone yeye sio wa kawaida tena kama ilivyo kuwa manzo. Mbinu hii ndiyo inatumiwa na wasanii wengi wenye kujua mitikasi na mizungu ya biashara ya burudani. Hii ndiyo mbinu inayofanya Diamond kila siku aonekane mpya katika macho ya mashabiki wake na kufanya kampuni kubwa za biashara zimkimbilie. Angalia watu kama kina 20% na Afande Sele. Mbali na majina yao makubwa. Mbali na nyakati fulani kuweza kusimamisha nchi katika matembezi yao. Ila nini kiliwakwamisha kuwa wasanii bidhaa? Wasanii wenye kubabaikiwa na wadau na makapuni makubwa kwa ajili ya dili za matangazo? Ni usela wao uliokithiri uliofanya wajichanganye hovyo na kuonekana watu wa kawaida sana mbele ya macho ya wapenzi wa muziki. Gigy Money pamoja na ya hovyo yake usishangae akawa msanii mkubwa kuliko Ruby. Nasema usishangae. Kuna uchawi anaujua wengine hawaujui. Hata hii nyimbo yake mpya inayokwenda la Papa. Uchaguzi wa hilo jina uliona mbali kuliko kawaida. Alikua akitaka watu wapate shauku baada ya kusikia jina la nyimbo yake ili waweze kuisaka. Akili hii hata Ali Kiba mbali na uwezo wake mkubwa katika kuimba na kuandika ila hana.
4
MIONGONI mwa changamoto kubwa zinazokwamisha juhudi za wakulima kujiletea maendeleo hasa baada ya kuvuna mazao yaokatika nchi mbalimbali za Afrika ikiwamo Tanzania, ni kuwapo kwa uharibifu wa mazao wakiwemo dumuzi na fukuzi.Profesa Mshiriki katika Kituo cha Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambaye pia ni Mkuu wa Mradi katika Kituo Mahiri cha Mashariki na Kusini mwa Afrika kinachohusika na utafiti wa panya na matumizi yake katika unusaji, Apia Massawe anasema panya pia wamekuwa waharibifu na wanaosumbua wakulima.Profesa Massawe ambaye pia ni Mkuu wa Mradi unaofadhiliwa na serikali wa kupunguza matatizo ya wadudu katika maghala na nyumbani kwa wakulima wadogo wadogo, anasema wapo pia panya wanaokula mazao yakiwamo mahindi na hata kusababisha usumbufu mwingine kwa binadamu na wanyama.Mbobevu huyo katika utafiti wa panya ambaye amekuwa akifanya utafiti kuhakikisha hawaleti madhara kwa wakulima nyumbani na shambani, Mradi wa Hifadhi Bora wa Mazao kwa kutumia mifuko maalumu unaofadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ulianza mwaka 2012 na ulitarajiwa kuisha mwaka jana, lakini umeongezewa muda mpaka Machi mwakani. Katika mradi huo, Costech imetoa Sh milioni 89 kuwezesha watafiti hao wa SUA.Anasema utafiti huo umelenga kuangalia matumizi bora ya uhifadhi wa mifuko ya nafaka kwa wakulima wadogo. “Kama watafiti, tumehangaika kutafuta njia nyingi za kusaidia wakulima, ikiwa ni pamoja na kuweka kwenye vihenge ili kuzuia panya, lakini bado dumuzi na fukuzi wamekuwa wakisumbua,” anasema.Anasema ili kukabiliana na hali hiyo, wakulima wengi wamekuwa wakitumia viuatilifu kuua wadudu na mimea mbalimbali, lakini katika kuhifadhi bado ni tatizo. “Hizi dawa athari zake zimekuwa kubwa kwa wakulima.Unakuta mtu anasaga unga wa dona bila kuosha anakula anakuwa amekula sumu na madhara yake ni makubwa… Tukaangalia ni njia ipi itasaidia wakulima wengi kwani wapo waliojitahidi kutumia hata mapipa kuhifadhi lakini changamoto ipo kwenye nyumba zetu kwani mkulima ataweka mapipa mangapi ili ahifadhi?” Anahoji Profesa Massawe.Anasema waliona njia bora ni kutumia mifuko ya uhifadhi wa nafaka iliyobuniwa na Chuo Kikuu cha Pado-United State ili kusaidia Afrika Magharibi kuhifadhi mazao ya nafaka. Kwa mujibu wa Profesa Massawe, baada ya kugundua kuna kiwanda kinachotengeneza mifuko hiyo hapa Tanzania lakini wakulima hawana habari kuhusu kiwanda hicho, walijiuliza ni kwanini wakulima hawakitumii, ndipo walipofanya utafiti na kujua sababu.“Tukaona tunahitaji kufanyia utafiti ili tuone hiyo mifuko inafanyaje kazi ili wakulima waweze kuitumia,” anasema. Kama watafiti walipata fedha za utafiti kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kisha wakaanza utafiti ulioeleta matokeo mazuri. Mradi huo umefanyika Berega wilayani Gairo na katika Kijiji cha Mgugu mkoani Morogoro. Anasema: “Wakulima watanufaika sana kwa kutumia mifuko hii.Unapotumia na kufanya vizuri wadudu wanakufa na hakuna mdudu atakayeingia na kuharibu mazao ndani ya mfuko huo. Hata panya hana uwezo wa kutoboa mfuko huu kwa sababu hutoboa kitu baada ya kunusa, lakini ukihifadhi nafaka zako vizuri ndani ya mifuko mitatu hawezi kutoboa.”“Mkulima atakuwa na uhakika wa kupata chakula mwaka mzima, kama anataka kuuza, atauza wakati ambao bei inakuwa nzuri tofauti na wakati kabla ya kuanza kutumia mifuko hiyo walipouza ili nafaka zao zisishambuliwe na wadudu,” anasema.Profesa Massawe anasema kwa kuwa wakulima walikuwa hawana uhakika wa kuuza mazao yao, waliuza mapema kwa bei ndogo, lakini watauza kwa bei nzuri na hata matumizi ya mifuko hiyo yatapunguza utumiaji wa viuatilifu. Mwitikio ukoje? Baada ya utafiti wa mwanzo na kuanza kutangaza mifuko hiyo, mwitikio umekuwa mkubwa, ingawa upatikanaji wa mifuko hiyo ulikuwa ni mgumu kidogo.Profesa Massawe anasema, wao kama watafiti wa SUA wakiwa kiungo kati ya kiwanda na wakulima ili kuwezesha wakulima waipate kwa urahisi na hivi sasa wengi wao wanaitumia. Upatikanaji wa mifuko ulivyo Profesa huyo anasema wamezungumza na watu wa viwandani wa Pee pee Tanzania Limited na A to Z kama wanaweza kuzalisha kwa wingi ili wawauzie wakulima, lakini pia yapo maduka ya pembejeo yanayouza mifuko hiyo japo ni ghali kidogo kwani mmoja unauzwa kati ya Sh 5,000 na Sh 6,000. “Tunajaribu kuzungumza na viwanda kama wataweza kuzalisha kwa bei ya chini ili wakulima wote waweze kuitumia mifuko hiyo,” anasema.Anaelezea faida za mifuko hiyo mbali na kuhifadhi nafaka zisishambuliwe na wadudu, kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutumika hata mara tatu bila kuharibika. “Kwa kutumia hii mifuko hii, wakulima watakuwa wamepunguza gharama, pia hawatatumia sumu tena na hawatauza mazao yao haraka kwa kuhofia kuharibiwa na wadudu,” anasema.Anasema kama chuo kikuu, wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu kuhusu matumizi ya mifuko hiyo kwa njia mbalimbali ili jamii iweze kuitumia kwa ufasaha. Mtaalamu huyo anasisitiza kuwa, wataendelea kutoa mafunzo kwa mabwana shamba nchi nzima, ikiwa ni pamoja na kutoa vipeperushi vya kutosha ili ifikapo Machi mwakani kabla mradi huo, Watanzania wengi wawe wamepata elimu.Anasema baada ya utafiti huo kufanya vizuri, elimu kuhusu faida na utumiaji wa njia hiyo ni muhimu iwafikie watu wengi zaidi. Mwenyekiti wa Kijiji cha Berege, David Aron anasema wamenufaika na mradi huo kwa sababu hivi sasa hawaweki dawa kwenye nafaka zao, na badala yake wanahifadhi kwenye mifuko hiyo. “Kwenye mfuko mmoja unaweka mahindi debe sita, tofauti na viroba vya kawaida ambavyo ukiweka mahindi au nafaka nyingine inabanguliwa,” anasema.Mkulima kutoka Kijiji cha Berege, Jones Ngiga, anasema analima mahindi na mbaazi eka tatu na amepata magunia 30 anayohifadhi kwenye mifuko hiyo. Kwa maelezo yake anasema, amekuwa mhamasishaji kwa wakulima wenzake kuhusu kutumia mifuko hiyo kuhifadhi nafaka baada ya kuona mafanikio yake.Mkulima mwingine Betina Chibwaya anayeishi katika Mtaa wa Mlingoti A, kijiji cha Berege anasema ni mkulima wa mahindi na kipindi hiki mazao hayo hayana bei, hivyo ili hataki kuyauza kwa hasara, hivyo ameyahifadhi kwenye mifuko hiyo hadi bei itakapokuwa nzuri.Mkurugenzi Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu chuoni hapo, Dk Ladislaus Mnyone anasema wamekuwa na miradi miwili kutoka Costech, mmoja ukiwa huu wa kuhifadhi mahindi yasibanguliwe na wadudu waharibifu, na mwingine ni wa kutumia mkojo wa paka kudhibiti panya waharibifu.Anasema kumekuwa na matumizi makubwa ya kemikali katika nafaka hivyo kutumia mifuko hiyo, kutapunguza matumizi hayo ya dawa. Anasema anashukuru kituo chake kupata fursa ya kufanya utafiti wenye matokeo chanya kwa jamii, lakini pia ni vipaumbele vya taifa, ikiwa ni pamoja na watafiti kufanya kazi na watu wengine.
1
Aveline Kitomary -Dar es salaam MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila, Profesa Lawrence Museru, amesema hospitali hiyo ina madaktari bingwa 52 hali inayowezesha kutoa huduma nzuri za matibabu na kupunguza idadi ya vifo kwa wagonjwa. Ufafanuzi huo aliutoa jana Dar es Salaam, kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo Mloganzila, hali inayosababishwa na watoa huduma kuwa ni madaktari wanafunzi. Profesa Museru alisema kuwa madai hayo si ya kweli na watoa taarifa hiyo wana nia ovu iliyojificha. “Moja ya sababu ambazo zimeelezwa na mtoa taarifa kwamba madaktari wanaotoa huduma ni wanafunzi waliopo katika majaribio si za kweli, tuna madaktari bingwa 52, madaktari wa kawaida 50 na kwa sasa kuna madaktari tarajali 53,” alisema Profesa Museru. Alisema madaktari hao wanashirikiana na kutoa huduma na madaktari wengi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili – Upanga na wengine wawili wabobevu wenye hadhi ya uprofesa kutoka nchini Korea.  “Hivyo sio kweli kwamba madaktari ambao wapo mafunzoni wanafanya kazi bila usimamizi, kwani hospitali imeweka utaratibu wa kila mgonjwa anayefika kupata huduma anaonwa na daktari bingwa kwa ajili ya maamuzi. “Takwimu tulizonazo zinaonyesha kwamba wagonjwa wanaotibiwa Mloganzila wameongezeka katika makundi yote, wagonjwa wa nje wameongezeka kutoka 17,115 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia 25,493 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 48.8. “Wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa wameongezeka kutoka 1,459 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba mwaka 2018 na kufikia wagonjwa 2,795 katika kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 91.6. “Wakati huo huo idadi ya vifo (mortality rate) ikipungua kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 na kufikia asilimia 10.4 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 kwa upande wa Mloganzila,” alisema Profesa Museru. Akizungumzia upande wa Upanga, alisema takwimu zinaonyesha kwamba katika kipindi cha robo cha Julai hadi Septemba mwaka 2018 wagonjwa waliolazwa walikuwa ni 12,375 na kulitokea vifo 1,000 sawa na asilimia 8.1. “Vilevile katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 MNH Upanga ililaza wagonjwa 17,230 na kati ya hao vifo vilikuwa 1,673 ambayo ni asilimia 9.7 (mortality rate), hivyo basi takwimu kati ya MNH-Mloganzila na MNH-Upanga za asilimia ya wagonjwa waliofariki hazitofautiani sana ambapo MNH-Upanga ni asilimia 9.7 wakati MNH-Mloganzila ni asilimia 10.4 katika robo ya Julai – Septemba, 2019,” alisema Museru. Alisema malengo yao ni kuhakikisha huduma bora zitaendelea kupatikana, hivyo kuwataka Watanzania wenye jukumu la kuelimisha jamii kuzungumza na wataalamu ili waweze kutoa taarifa sahihi kwa jamii.
1
Mkurugenzi mtendaji wa Bundesliga Christian Seifert amesema ligi ya nchi hiyo inaweza kurejea kwanzia tarehe 9 mwezi ujao kama wataoata kibari cha serikali Seifert amesema kwa Upande wao kama bodi ya ligi wamejiweka sawa kwanzia mazingira ya uwanjani mpaka utaratibu wa mashabiki kuingia uwanjani Ligi ya ujerumani ilisimama mapema katikati ya mwezi Machi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19  unaosababishwa na virusi vya corona “Tayari temeshapeleka mapendekezo kwa serikali kilichobaki ni kwa serikali kuamua wakisema tuanze tarehe 9 mwezi mei tupo tayari na hata ikiwa baada ya hapo tutakuwa tayri zaidi na zaidi” amesema Seifert Kwa mujibu wa Skygermany mechi moja haitaruhusiwa kuwa na watu zaidi ya 300
2
MWANDISHI WETU NA MITANDAO NI miaka mitatu imepita tangu ulimwengu wa soka kuishuhudia timu ya taifa ya soka ya Ujerumani ikitawazwa mabingwa wapya wa Kombe la Dunia juu ya ardhi ya Brazil mwaka 2014, baada ya kuifunga Argentina bao 1-0. Michuano ya mwaka huo ilikuwa ni ya kufurahisha kama sio kushangaza, ikiwa na matokeo yaliyowaacha wengi midomo wazi na historia pia. Moja ya kitu cha kukumbukwa zaidi ni kichapo cha aibu walichokipata mabingwa mara tano wa kombe hilo na waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo, Brazil, cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani. Haikuwa siku nzuri kabisa kwa wananchi wa Brazil. Na sasa, kwa mara nyingine tena tutapata wasaa maridhawa wa kuishuhudia tena michuano hiyo ikirindima nchini Urusi mwakani. Msimu huu kuna timu ambazo zimefanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza lakini, nyingine zimerejea na nguvu mpya baada ya kupita miaka kadhaa bila ya wadau wa soka kuziona katika msimu mmoja au miwili ya michuano hiyo. Timu hizo ni Tunisia, Morocco, Senegal, Saudi Arabia, Sweden, Poland ambazo zote hizo hazikushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014, huku Iceland ikifuzu kwa mara ya kwanza katika historia yao ya mchezo wa soka. Morocco ndilo taifa pekee kati ya hayo yaliyofuzu ambalo halijashiriki michuano hiyo kwa muda mrefu, ambapo ilifuzu kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 19, mara ya mwisho wakishiriki michuano ya mwaka 1998 ambayo bingwa wake alikuwa ni Ufaransa. Hata hivyo, shukrani zimwendee kocha mwenye historia nzuri na timu za Afrika, Herve Renard, ambaye uzoefu wake wa kufanya kazi kwenye mazingira yenye changamoto nyingi za soka Afrika uliisaidia Morocco kurudi tena kwenye mashindano hayo makubwa. Renard anakumbukwa kwa kuzifanya Zambia na Ivory Coast kutwaa mataji ya kihistoria ya Mataifa Afrika katika miaka ya 2012 na 2015. Lakini, bila kujituma kwa mastaa wa timu hiyo wakiongozwa na nahodha Mehdi Benatia, Morocco ingetazama michuano hiyo kwenye runinga. Morocco walimaliza kundi lao na alama 12, ikishinda mechi tatu, sare tatu; ikifunga mabao 11 na bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa katika mechi sita za hatua ya makundi. Timu nyingine ambayo kwa muda mrefu haikuonekana katika michuano hiyo na imekuja kufuzu mwaka huu ni Senegal. Mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni mwaka 2002, walipotinga robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao. Hata hivyo, hatua hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa safari yao katika michuano hiyo ambapo walijikuta wakipoteza mchezo mbele ya Uturuki kwa bao 1-0 lililofungwa na Ilhan Mansiz dakika ya 90 na nne za nyongeza, katika mtanange uliolazimika kwenda hadi dakika 30 za nyongeza baada ya zile tisini kumalizika kwa suluhu. Senegal ya miaka hiyo ilikuwa si ya mchezo mchezo, ambapo wachezaji kama Papa Bouba Diop, Ferdinand Coly, Papa Malick Diop, El Hadji Diouf, Henry Camara na wengineo, na iliweza kuzisumbua timu kubwa duniani, lakini baada ya michuano hiyo haikuweza kufuzu kwenye misimu mitatu mfululizo ya Kombe la Dunia. Kurudi kwao kwa ajili ya michuano ya mwakani kunachangiwa na uwepo wa wachezaji wengi bora na vijana, wakiongozwa na kocha Aliou Cisse ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Senegal kilichocheza dhidi ya Uturuki mwaka 2002 akiwa nahodha. Unaweza pia kusema historia ya mafanikio ya kocha huyo Cisse yameisaidia Senegal kutinga kwenye michuano hiyo baada ya kukosekana kwa muda mrefu. Mataifa mengine ya Poland na Sweden, ambayo yanatoka katika ukanda wa Ulaya, pamoja na Saudi Arabia ambao wapo Asia nayo yalipambana vilivyo na kujihakikishia nafasi hiyo baada ya kupita miaka 11 ya kutoshiriki michuano hiyo, mara ya mwisho wakionekana mwaka 2006. Katika kipindi cha miaka yote hiyo, Poland na Sweden zilikumbwa na ugumu wa kuchuana na mataifa ambayo kimsingi yanajiweza duniani, kama vile Ujerumani, Hispania, England, Ureno na mengineyo. Kwa mapana, tumeziangazia zile timu ambazo zimefuzu kushiriki michuano hiyo lakini hatujazitupia macho timu nyingine ambazo zimekosa tiketi ya kushiriki michuano mwakani ambazo ni Chile, Uholanzi, Ghana, Algeria, Ugiriki, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Italia ambao ndio waliowaacha wengi midomo wazi kwani haikutegemewa kwa taifa lenye historia kubwa na michuano hiyo kushindwa kufuzu. Italia walipangwa Kundi G na nchi za Macedonia, Albania, Israel, Liechtenstein na Hispania, na kiukweli, timu iliyokuwa ikiwapa upinzani ilikuwa ni Hispania ambao walimaliza kundi hilo wakiwa nafasi ya kwanza na kuilazimisha Italia kucheza mechi ya mchujo ili waweze kwenda Urusi. Kwa mfumo wa kufuzu katika bara la Ulaya, ni mshindi mmoja tu kwa kila kundi anayekuwa na uhalali wa kushiriki michuano hiyo hivyo Italia haikuwa najinsi zaidi ya kuvaana na Sweden kwenye mechi hiyo ya mchujo (play off). Hata hivyo, Italia ilishindwa kufurukuta mbele ya Sweden na kukubali kichapo cha jumla ya bao 1-0, baada ya kucheza mechi hizo mbili dhidi ya Sweden. Lawama zote za matokeo hayo ya Italia kuikosa tiketi ya kushiriki michuano hiyo zilitupwa kwa kocha, Giampiero Ventura kwa kukosa mbinu za kiufundi kulingana na hadi ya timu hiyo ya taifa na kulifanya taifa hilo lianguke kwenye aibu kubwa ya soka. Vyombo vya habari viliyataja matokeo hayo kama ‘ngumu kumeza’ na kila kona ikihimiza kocha huyo abwage manyanga na hatua za lazima zichukuliwe ili kuirudisha Italia kwenye mstari ulionyooka. Tunapata funzo gani kama Tanzania na timu yetu ya Taifa Stars? Ni kwamba, hakuna mafanikio yanayopatikana kwa njia rahisi na ndiyo maana Iceland imefanikiwa kutinga michuano hiyo kwa mara ya kwanza kwenye historia yao ya soka kutokana na kutekeleza mipango yao kwa vitendo na sio maneno kama ilivyozoeleka hapa nchini. Aidha, inaweza kuwa ni kosa kuifananisha Iceland na Tanzania kutokana na maendeleo ya soka katika nchi za nje kuwa juu zaidi yetu kwa namna moja ama nyingine, lakini kwa kuzingatia misingi ya soka ambayo ni mipango madhubuti na kujituma kwa sana, hakutakuwa na sababu ya maana ya kujitetea kama tusipoona timu yetu ya Taifa Stars ikishindwa kufikia Watanzania wanapopataka.
2
KIGALI, Rwanda MWANDISHI wa  habari wa kujitegemea, Phocus Ndayizera ameonyeshwa mbele ya vyombo vya habari na polisi wa upelelezi nchini hapa  wiki moja baada ya kutoweka huku akidaiwa kujihususha na vitendo vya ugaidi. Msemaji wa idara ya polisi ya upelelezi nchini hapa alisema juzi kwamba  mwandishi huyo anatuhumiwa makosa ya ugaidi na  alikuwa akifuatiliwa. Mwandishi huyo ambaye amewahi kufanyia kazi vyombo vya habari mbalimbali na mara kwa mara amekuwa akiripoti pia katika Shirika la Utangazaji la Uingereza  (BBC),  Idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi,   alisema kwamba hajui kwa nini anashikiliwa. Mwandishi wa BBC   mjini hapa, Yves Bucyana, alisema    Ndayizera  alipoonekana mbele ya waandishi wa habari   makao makuu ya idara ya polisi inayohusika na upelelezi, alikuwa amefungwa  pingu na hali yake ilionyesha uchovu. Alisema, mwandishi huyo alifahamika katika vyombo vya habari mbalimbali na mara kwa mara aliifanyia kazi BBC idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi kama mwandishi wa kujitegemea. Alisema   mara ya mwisho kwa  Ndayizera   kuiripotia BBC ilikuwa   Juni mwaka huu. Alipotakiwa na polisi kuwambia waandishi wa habari tuhuma dhidi yake, Ndayizera alisema   hana habari yoyote kuhusu mashitaka dhidi yake. Ndayizera alisema   alikamatwa katika mtaa wa Nyamirambo jijini hapa  alipokwenda kumuona jamaa yake na kupelekwa sehemu isiyojulikana kabla ya kujikuta katika mahabusu ya polisi Kituo cha Remera. Msemaji wa Idara ya Upelelezi, Modeste Mbabazi aliwaambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi. Polisi wa upelelezi wamekiri kuwa ndiyo waliokuwa wanamshikilia mwandishi huyo kwa wiki nzima. Msemaji huyo wa Idara ya Upelelezi,  Mbabazi aliwaambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi. Kwa mujibu wa msemaji huyo, walikuwa na taarifa za mipango ya watuhumiwa   kuhatarisha usalama wa   Rwanda. Msemaji wa Polisi alisema walisubiri siku kadhaa kutangaza kumshikilia mwandishi huyo kwa sababu  makosa ya ugaidi yanafuatiliwa kwa njia ya  pekee tofauti na makosa mengine. Haijafahamika ni lini mwandishi huyo na wengine wanaotuhumiwa   watafikishwa mahakamani.
3
Mchezaji mpya wa Barcelona Frenkie de Jong yupo Bongo anakula maisha na mpenzi wake kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti katika kipindi hiki ambacho yupo mapumzikoni baada ya kumaliza majukumu akiwa na Ajax na baadaye timu ya taifa ya Uholanzi. Hiki ni kipindi ambacho wachezaji na makocha wengi hususan wanaokipiga barani Ulaya na Marekani hutumia kufanya ziara katika nchi mbalimbali za Afrika kwaajili ya kujipa mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi mbalimbali. Mbuga na Hifadhi za Wanyama ni sehemu ambazo wachezaji hupenda kutembelea kwaajili ya kujionea uzuri wa asili kutoka Afrika. Wameshakuja wachezaji mbalimbali hapa Tanzania. David Beckham amewahi kuja, Messi inaelezwa ameshawahi kuja kutembea Mlima Kilimanjaro, Mamadou Sakho na siku chache zilizopita inalezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Tottenham na Timu ya Taifa ya Ufaransa Moussa Cissoko alikuja kutembelea moja ya Hifadhi za Taifa hapa nchini.  
2
JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali itanunua dawa zinazotengenezwa na wawekezaji wa hapa nchini kwa kuzingatia ubora, usalama na ufanisi. Waziri Mwalimu alitoa masharti hayo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Maabara zinazohamishika uliofanyika kwenye ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Dar es Salaam. Alisema baada ya  Serikali kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini itaanza kununua dawa zinazotengenezwa na viwanda vya ndani lakini kwa wekezaji waliotimiza vigezo. Waziri Mwalimu alisema uzinduzi wa maabara hizo ni moja ya jitihada zinazofanywa na serikali kuondoa bidhaa na dawa bandia ili kuokoa maisha ya raia wake “TFDA imeendeleza mpango mahsusi wa uchunguzi wa awali wa dawa ulionza 2002 katika baadhi ya hospitali za mikoa na vituo vya forodha kwa dawa muhimu za kifua kikuu, dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) na viua sumu (antibiocs). “Hatua hii ya kununua maabara zinazohamishika 10 na kufikia 25 kote nchini inalenga kuimarisha nguvu katika kudhibiti ubora na usalama wa dawa zinazoingia na zilizoko sokoni. “Na niweke wazi kwamba Serikali haitanunua dawa za ndani ambazo hazikidhi vigezo,” alisema Mwalimu. Aidha Waziri Mwalimu aliitaka TFDA kutowaone aibu na kuwaogopa wawekezaji ambao wataleta dawa bandia bali iwachukulie hatua stahiki bila kujali gharama za mzigo wenyewe. “Wawekezaji walete dawa zenye ubora unaotakiwa hivyo TFDA hata mtu akileta mzigo wa bei ya juu kiasi gani kama hauna ubora msimwonee aibu. “Lakini pia TFDA msikwamishe wawekezaji bali muwe sehemu ya kuwezesha ufikiaji wa uchumi wa viwanda nchini,” alisema Mwalimu. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, alisema maabara hizo 10 zimegharimu Sh milioni 100 na kwamba hivi sasa maabara hizo zimefikia 25 kutoka 15 mwaka 2012/13.   Alisema maabara hizo zitapelekwa katika ofisi za kanda tatu za Tabora (Magharibi), Mbeya (Nyanda za juu Kusini) na Mtwara (Kusini) na vituo vya forodha Namanga, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA), Sirari na Mutukula na katika Bandari ya Dar es Salaam na kwamba maabara nyingine mbili zitapelekwa katika mikoa ya Geita na Katavi. “Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maabara hizo, uwezo wa kubaini dawa duni na bandia umeongezeka na imewezesha idadi ya dawa duni kushuka kutoka asilimia 3.7 2005 hadi chini ya asilimia 1 mwaka 2017,” alisema. Alisema TFDA ilimebaini dawa bandia zilizodaiwa kuwa na viambata vya Ampicillin, Erythromycin, Quinine Sulphate, Metronidazole na dawa ya mseto ya Metakelfin.  
5
KOCHA wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger, ameuponda uhamisho wa kiungo wa klabu ya Juventus, Paul Pogba, kujiunga na mashetani wekundu, Manchester United. Nyota huyo anatarajia kuvunja rekodi ya usajili duniani atakapofanikiwa kujiunga na klabu ya Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 100, ambapo kabla ya usajili huo, mchezaji ambaye anaongoza kwa kusajiliwa kwa kitita kikubwa ni Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa pauni milioni 86. Kwa sasa usajili ambao unasubiriwa na idadi kubwa ya mashabiki na wadau wa soka duniani ni juu ya kiungo huyo raia wa nchini Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. Kutokana na kiasi hicho cha fedha, Kocha Wenger amekiponda na kudai kwamba ni kikubwa na hakuna sababu ya kutumia fedha zote hizo kwa ajili ya kumsajili mchezaji mmoja. “Kwa upande wangu nitanunua mchezaji ambaye atakuwa na mchango mkubwa katika kikosi changu, kikubwa ninachokiangalia ni kupata mchezaji mwenye sifa zote, lakini si kununua kama wengine ambavyo wanafanya. “Hata ukiwauliza mashabiki ni mchezaji gani ambaye anaweza kufaa katika kikosi watakuambia, hivyo siwezi kutumia fedha nyingi kumnunua mchezaji mmoja kama ambavyo wanataka kufanya Manchester United kwa Pogba. “Timu ambayo inataka kushindana katika kumsajili Pogba ni ujinga, kwa kuwa fedha zinazotakiwa ni nyingi, lakini kama ipo klabu ambayo ina uwezo wa kumsajili basi inaweza kufanya hivyo, lakini kwa upande wangu siwezi kufanya hivyo,” alisema Wenger. Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba soka la sasa ni tofauti na miaka ya nyuma, hivyo kuna uwezekano wa kuzidi kuyaona mengi kwa miaka inayokuja katika biashara ya soka. “Kama leo hii mchezaji anauzwa pauni milioni 100, basi ninaamini ipo siku tutakuja kusikia thamani ya mchezaji ikifika pauni milioni 200 hadi 300 kutokana na ushindani. “Hii hali tutakuja kuiona miaka michache ijayo bila kujali uwezo wa mchezaji mwenyewe, ila kwa upande wangu siwezi kusema kama nitaweza kufanya usajili wa fedha kama hizo kwa mchezaji mmoja,” aliongeza. Arsenal kwa sasa inahangaika kutafuta beki wa kati ambaye atachukua nafasi ya Per Mertesacker, ambaye anadaiwa kuwa majeruhi, klabu hiyo inamuwinda beki wa Valencia, Shkodran Mustafi, mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa kwamba thamani ya mchezaji huyo ni pauni milioni 42.
2
UJENZI wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka mkoani Shinyanga mpaka Kigali nchini Rwanda, umeanza kupamba moto baada ya Rwanda kutangaza kuwa inahitaji dola za Marekani bilioni 1.3 kwa ajili ya reli hiyo itakayounganisha nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa, tofauti na ilivyobainika awali ambapo ilikuwa dola za Marekani bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ya kilometa 400 Januari mwaka huu.Waziri wa Uchukuzi wa Rwanda, Jean de Dieu Uwihanganye alisema utafiti wa ujenzi wa reli hiyo ya SGR kati ya Isaka Tanzania na Kigali Rwanda kwa kiwango cha SGR umekamilika.Akizungumza na redio moja nchini Rwanda alibainisha kuwa nchi inatafuta takribani dola za Marekani bilioni 1.3 ili kufadhili kwa sehemu yake ili kupunguza gharama kuboresha biashara na kurahisisha muingiliano wa watu kati ya nchi hizo mbili.Utafiti wa jumla ulionesha kuwa mradi huo kati ya Rwanda na Dar es Salaam, unatarajia kutumia wastani wa dola bilioni 2.5. Januari mwaka jana,Tanzania na Rwanda kupitia mawaziri wanaohusika na ujenzi, walisaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali.Tukio hilo liliwakutanisha mawaziri watatu wa Tanzania ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga na Waziri wa Ujenzi wa Rwanda, James Musoni huku wakiwa wameongozana na wataalamu mbalimbali wa miundombinu kutoka nchi hizo. Kabla ya kusaini makubaliano hayo, mawaziri walipokea rasimu ya ujenzi wa reli hiyo na kuijadili kabla ya kupitisha rasmi. “Reli hii ni biashara, lazima tufanye haraka, itasaidia kukuza uchumi nchini, kuongezeka fedha za kigeni, barabara zetu zitadumu, watu wetu watakuza biashara zao,” alisema Waziri Mpango.Kwa mujibu wa mapendekezo ya rasimu hiyo iliyoandaliwa na makatibu wakuu kutoka Rwanda na Tanzania, mradi huo ulioanza mchakato wake miaka mitatu iliyopita, sasa utaanza ujenzi wake rasmi, baada ya kuwekwa jiwe la msingi Oktoba mwaka jana na marais wa nchi hizo.Akiwasilisha rasimu hiyo kabla ya kupitishwa, Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Rogatus Mativila alisema rasimu imependekeza njia mbili za ufanikishaji wa mradi huo wenye urefu wa kilometa 521.Alisema njia ya kwanza ni kushirikisha sekta binafsi na njia ya pili ni kutumia bajeti za serikali mbili kwa kila nchi kugharamia kipande kilicho katika nchi yake.Zaidi ya Sh trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,190, ambapo benki hiyo itashirikiana na serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam- Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora-Mpanda-Kalemela- Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.
0
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) inatarajia kuendesha kampeni maalumu ya mfano, kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika eneo la mpaka wa Namanga unaoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.Kampeni hiyo inatarajiwa kuwa na matokeo chanya na kujenga uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko hasa kwa nchi hizo mbili.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Jumuiya ya Afrika Mashariki ilieleza kuwa kazi hiyo itafanyika kwa siku nne kuanzia Juni 11 hadi 14 mwaka huu.Kampeni hiyo itakayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kuwahusisha wadau 250 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wanaohusika na afya ya wanyama, afya ya binadamu, mazingira, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, waandishi wa habari, wananchi na viongozi wa kijamii.Wananchi wanafanya shughuli zao katika mpaka wa Namanga wilaya ya Longido Kaskazini mwa Tanzania na upande wa Kajiado nchini Kenya wameombwa kuwa watulivu kwa kipindi cha siku nne za majaribio na kutokuwa na hofu.Mwakilishi wa Shirika la GIZ, Dk Irene Lukassowitz alisema kama watu watakuwa na taarifa sahihi watajua jinsi magonjwa ya milipuko yanaambukizwa hivyo ni rahisi kujikinga.Alisema, “Hicho ndicho tulichojifunza kuhusu ugonjwa wa ebola huko Afrika Magharibi. Tunatakiwa kuunganisha nguvu na kufanya kazi pamoja ili kupambana na magonjwa haya, na ndio maana tunawaleta watu pamoja ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko,” alisema Dk Lukassowits.Katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuna magonjwa mengi ya kuambukiza yanayoathiri wanyama na binadamu kama vile homa ya bonde la ufa, ebola, kipindupindu na kichaa cha mbwa na ndio sababu jumuiya hiyo inaona upo umuhimu wa wadau mbalimbali kutoka eneo hilo kuunganisha nguvu kuyadhibiti.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Michael Katende alisema mpango huo unafuatia makubaliano ya mawaziri wa afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofikiwa mwaka 2015 ya kudhibiti magonjwa ya milipiko kwenye maeneo ya mipakani.Magonjwa hayo ya milipuko yanatajwa kuzikumba nchi nyingi hasa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara na kuua maelfu ya watu, kuathiri mifugo, makazi pamoja na uchumi.
1
Na Amina Omari – Tanga MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga imetupilia mbali rufaa ya kusikiliza upya shauri la mirathi ya marehemu Mohammed Shosi lililofunguliwa na Swabaha Mohamed Ali. Mwanzoni mwa mwezi huu, Swabaha aliyedai kuwa ni mke wa marehemu Shosi, aliibuka mbele ya Rais Dk. John Magufuli wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria na kulalamika kutaka kudhulumiwa haki yake ya mirathi. Rufaa hiyo uamuzi wake ulitakiwa kutolewa kesho, lakini hata hivyo ulitolewa juzi na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Amour Hamis. Katika kesi hiyo ambayo Swabaha aliifungua dhidi ya Saburia Shosi, ambaye ni mtoto wa marehemu Shosi aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu baba yake, Jaji Amour akitoa uamuzi alisema mahakama hiyo imeridhika na hukumu iliyokuwa imetolewa hapo awali na mahakama ya wilaya pamoja na ile ya mwanzo. Katika hilo, jaji huyo aliamuru taratibu nyingine za uendeshaji wa mirathi kuendelea kama ilivyokuwa imeamuliwa na mahakama ya mwanzo na ile ya wilaya. Katika kesi iliyofunguliwa na Saburia katika Mahakama ya Mwanzo Desemba 16, 2012, kuomba awe msimamizi wa mirathi, mahakama hiyo ilimruhusu. Hata hivyo, mwaka 2015 Swabaha alikata rufaa Mahakama ya Wilaya akifungua kesi ya kuzuia mali za marehemu, ambayo nayo upande wa akina Saburia walishinda huku mahakama ikimuamuru aendelee kuwa msimamizi wa mirathi. Katika umuzi wake wa sasa, Jaji Amour alisema kuwa pamoja na hukumu hiyo, Swabaha ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wake Ngomela, atatakiwa kumlipa Saburia gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo. Awali Jaji Amour alisema kuwa Swabaha aliwasilisha mahakamani hapo ombi la kukata rufaa nje ya muda baada ya kesi ya msingi kumalizika na hukumu kutolewa. Aidha alisema kuwa kesi ya msingi ilitolewa uamuzi katika Mahakama ya Wilaya Septemba 9, 2016 na Swabaha alikuja kukata rufaa nje ya muda, Novemba 14, 2016. Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, Saburia ambaye alikuwa akitetewa na Wakili Abdon Rwegasira, aliipongeza mahakama kwa kumaliza mapema shauri hilo ambalo lilikuwa likiwasumbua kwa muda mrefu. Saburia ambaye anadai kuwa ni miongoni mwa watoto tisa wa marehemu Shosi, alisema hukumu ya kesi hiyo ilipangwa kutolewa kesho, lakini juzi akiwa nyumbani alipigiwa simu kwamba anahitajika mahakamani. “Nilipigiwa simu kama saa nne hivi nikiambiwa nahitajika mahakamani, basi tukaenda, huwezi kujua pengine ndio mambo ya tume aliyosema rais, tukaambiwa kesi yetu inatolewa uamuzi na tunashukuru Mungu tumeshinda,” alisema. Saburia ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya familia yake, alisema kwa uamuzi huo sasa wataweza kuendelea na taratibu nyingine za mirathi. “Nimefurahishwa sana na uamuzi wa mahakama kwani haki imeweza kutendeka kwa wakati na sasa tunaweza kuendelea na mambo ya kugawana mali za marehemu baba,” alisema Shosi. MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Swabaha ili kuzungumzia uamuzi wa kesi hiyo na alisema ameupokea vizuri na kwamba kwa sasa anajiandaa kupeleka maombi Mahakama Kuu kufanya mapitio (review) ya hukumu mbili zilitolewa katika Mahakama ya Mwanzo na ile ya Wilaya. “Yalikuwa ni maombi ya kuingia kwenye rufaa na actually tulikuwa tumechelewa kukata rufaa, sasa ni nafasi ya mahakama kuangalia hukumu zile mbili, nitakwenda Tanga kati ya Jumatatu (kesho) au Jumanne (keshokutwa) kupeleka maombi hayo,” alisema Swabaha. Mjane huyo pia alikwenda mbali na kumtaja kwa jina askari mmoja (jina tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kitaaluma), kwamba katika siku za hivi karibuni amekuwa akimfuatilia kumchunguza. “Nashangaa alikuwa wapi muda wote, nimesikia amekwenda hadi Bakwata kufuatilia cheti cha ndoa yangu, na wakati alikwisha kwenda siku za nyuma, si hilo tu, amekwenda hadi Buguruni, sasa mimi nina uthibitisho wa kila kitu,” alisema Swabaha ambaye anadaiwa alifunga ndoa nyingine Buguruni. Kabla ya uamuzi wa sasa, Februari 4, mwaka huu, siku moja baada ya mama huyo mjane kutoka mkoani Tanga kuibuka mbele ya Rais Magufuli na kudai kudhulumiwa haki yake ya mirathi na vyombo vya sheria, gazeti hili lilizungumza na pande mbili zinazovutana katika sakata hilo la mirathi kabla ya baadae kufika yalikokuwa makazi ya marehemu Shosi Mohamed ambaye Swabaha anadai kuwa ni mume wake mkoani Tanga. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili baada ya kusambaa kwa andiko lililokuwa likieleza upande wa pili wa ‘mama huyo mjane’ likimtuhumu kama tapeli ambalo liliandikwa na rafiki wa karibu wa familia hiyo, mtoto wa marehemu Shosi, Saburia alisema madai yote yaliyotolewa na mama huyo mjane si ya kweli na hivyo kutamani Rais Magufuli asikilize upande wa pili unaotuhumiwa wa familia hiyo. Saburia ambaye alizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, kwa simu na baadae nyumbani kwao Tanga, alianza kueleza jinsi anavyomfahamu mama huyo mjane akisema ni dada yake na kwamba marehemu baba yake alikuwa akimwita mjomba. “Simfahamu kama mke wa marehemu baba, namfahamu kama dada, mama yake mzazi na baba yangu (Shosi) ni mtoto wa mkubwa na mdogo na kwa kabila letu Wagunya, aliyepaswa kuolewa na baba yangu ni mama yake ambaye ni shangazi yangu na si yeye,” alisema. Saburia alisema baba yake alioa wake watatu ambao ni Mariam Tayb ambaye ni mama yake mzazi aliyekuwa amezaa watoto saba, lakini walio hai ni wanne, Mariam Sadick anayeishi Mkumbara Korogwe na Methe Mwanga ambaye kwa sasa ni marehemu. “Kwa kifupi sisi tulikuwa hatumfahamu kabisa, tulimfahamu siku ya 40 baada ya baba kufariki na alikuwa amekuja kutupa pole tukiambiwa kuwa ni ndugu yetu kutoka Mombasa, sasa wakati tunaandaa muhtasari wa kikao tukashangaa anasema aliolewa na baba yetu. “Hebu jiulize, anasema baba alimuoa mwaka 1993, mwaka 2011 alikuwa Buguruni, Dar es Salaam eda baada ya kufiwa mume wake mwingine aliyekuwa akiishi naye huko, mwaka 2013 alikuwa anafuatilia mirathi ya huyo mume wake wa Buguruni, sasa mwanamke anawezaje kuolewa na watu wawili kwa wakati mmoja?” alihoji Saburia. Wakati akisema hayo, mama huyo mjane alikaririwa pia na vyombo vya habari akidai kuwa Saburia ni mtoto wa nje wa marehemu mume wake na kwamba amekuwa akitumia nguvu yake ya pesa za dawa za kulevya kutaka kumpora haki yake, jambo ambalo mtoto huyo wa marehemu amekuwa akilipinga. Akizungumza na gazeti hili, Swabaha ambaye mara ya kwanza alikataa kueleza kuhusu ndoa yake ya Buguruni, jana alikuwa tayari kueleza kuhusu jambo hilo. Alikiri alikuwa akishughulika na mirathi ya Buguruni, lakini alikana kwamba mtu huyo haliwahi kuwa mume wake. “Ni kweli nilikuwa nashughulika na mirathi ya Buguruni kwa sababu marehemu huyo nilikuwa nikimdai shilingi milioni 8.6,” alisema. Wiki kadhaa zilizopita gazeti hili lilifika yalikokuwa makazi ya marehemu Shosi, mkoani Tanga jirani na Hospitali ya Rufaa ya Bombo na kuzungumza na Marium Tayb ambaye anadai kuwa ni mke mkubwa wa marehemu.  Nyumba hiyo anayoishi Tayb kila upande unakiri kuwa yalikuwa ni makazi ya marehemu na shughuli zote za maziko zilifanyika hapo.  “Najua marehemu aliwahi kuoa wake watatu, lakini hakuwahi kusema kama ameongeza mke mwingine na kama angekuwa ameolewa tungeweza kujua kwani tungetambulishwa kwake,” alisema. Tayb alisema sakata la Swabaha kudai mirathi hiyo lilianza mwaka 2012 wakati wa kikao cha arubaini ya marehemu mumewe wakati wakili wao alipowasilisha nyaraka ya mirathi. Alisema Swabaha ambaye alikuwapo kwenye kikao hicho alijitambulisha kama mpwa wa marehemu na baada ya kusomwa wosia wa marehemu aliomba auone kwa ukaribu ili ajiridhishe na kilichoandikwa. “Alipopewa akasimama na kusema na yeye ni mke halali wa marehemu, hivyo anastahili kurithi mali za marehemu kwani na yeye ana haki na kisha kukimbia na wosia huo,” alisema Tayb. Alisema walijaribu kumfuatilia kupitia kwa ndugu pamoja na wazazi wake wanaoishi Mombasa kuomba arudishe wosia huo, lakini badala yake alikataa na kuamua kuwapa kopi. Tayb alisema kuwa ilipofika Desemba, 2012  Swabaha aliamua kufungua kesi ya kudai mirathi na kuweka zuio la mali zote za marehemu. Februari 4, mwaka huu, Rais Magufuli aliagiza mama huyo mjane apewe ulinzi, huku akimwagiza Jaji Kiongozi kuhakikisha analifuatilia suala lake na kulimaliza kwa taratibu za kisheria.
1