text
stringlengths 1
24.2k
| label
int64 0
5
|
---|---|
Arodia
Peter, Dodoma Hospitali ya Benjamini
Mkapa iliyopo jijini Dodoma, imefanikiwa
kupandikiza figo kwa wagonjwa nane kwa kipindi
cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Hayo yalisemwa na daktari bingwa wa figo hospitalini hapo Dk. Kessy Shija, jana Mei 4, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani humo. Dk. Shija alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo ya kibingwa
hospitalini hapo kumepunguza gharama kwa wagonjwa kwenda kupata matibabu hayo
nje ya nchi, hususani India. “Niwashauri Watanzania kujiunga na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, kwa sababu magonjwa ya
kudumu kama figo yanachukua wastani wa Sh, 200,000 hadi 250,000 kwa wiki ambazo
ni gharama za kusafishwa, ambapo kwa
matibabu ya kupandikizwa figo huchukua wastani wa hadi Sh, 6, 000, 000 kwa mgonjwa
mmoja,” alisema. Aidha Dk. Shija alisema mbali na figo, hospitali hiyo pia
inatoa matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa wa moyo kama ilivyo kwa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. | 5 |
LOS ANGELES, MAREKANI KWA mujibu wa mtandao wa HollywoodLife, staa wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, anadaiwa kufurahia mgogoro kati ya rapa Cardi B na Nicki Minaj. Chris Brown ambaye mwaka huu amekuwa kando kwenye migogoro, amedai muziki wa hip hop unataka ushindani wa aina hiyo, hivyo haoni tatizo kwa warembo hao kupishana kauli kila siku. “Chris hana tatizo na Nicki Minaj, pia ni shabiki mkubwa wa muziki wa Cardi B, hivyo anapenda kuona wawili hao wakiendelea kuwa na mgogoro ili waweze kuufanya muziki wao kuwa juu zaidi,” kilisema chanzo hicho cha habari. | 4 |
Habari za Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (VVU), kodi na manunuzi ya umma, habari za uchambuzi na matukio na kundi la Afya ya Uzazi kwa Vijana, zimeondolewa katika makundi yatakayowania Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari(EJAT) kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo rasilimali fedha. Tuzo hizo zimezinduliwa rasmi leo ambapo makundi makundi matano kati ya 19, yamepunguzwa kutokana na sababu hizo. Mwenyekiti wa maandalizi ya tuzo hizo zinazosimamiwa na Baraza la Habari nchini (MCT), Kajubi Mukajanga amesema mwaka huu kutakuwa na ushindani wa umahiri wa habari katika makundi 14 kati ya 19 yaliyokuwa yakishindaniwa mwaka jana. Amevitaja vipengele vilivyobaki katika tuzo hizo ni habari za afya, habari za michezo na utamaduni, habari za uchumi, biashara na fedha, na uandishi wa habari za biashara, kilimo, elimu, utalii na uhifadhi, uchunguzi, data, haki za binadamu na utawala bora, mpiga picha bora wa magazeti na runinga, mchoraji katuni bora, habari za jinsia, wazee na watoto na kundi la wazi. “Kazi zitakazoshindanishwa ni zile zilizochapishwa na kutangazwa kati ya Januari Mosi hadi Desemba 31 mwaka huu, na mwisho wa kuwasilisha kazi zao ni Februari 16, mwakani na tuzo hizi zitatolewa Aprili 27, mwakani,” amesema. | 1 |
BAADA ya miezi 12 ya kukaa katika Hospitali ya Kisarawe na Muhimbili na kushindwa kuendelea na matibabu, Rashid Mtepo (30) amewaomba wasamaria kumsaidia fedha za kulipa deni Muhimbili ili arejee kwa matibabu.Mtepo mkazi wa Mpingoni, Nanguruku wilayani Kilwa amesema tatizo la mguu wake lilianzia mwaka 2015 ambapo alipatiwa tiba ya takribani mwezi mmoja katika Hospitali ya Kisarawe kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo alikaa miezi 11 na kufanyiwa upasuaji wa kubadili ngozi ili kuziba eneo la kidonda. Tatizo lake lilianza kama jipu kabla halijasambaa katika mguu wake wa kushoto, kubabuka ngozi na kuzalisha kidonda kikubwa.Upasuaji ulifanyika Hospitali ya Muhimbili mwaka 2016 kama sehemu ya tiba, lakini baada ya kukaa miezi 11 ya matibabu alilazimika kuondoka hospitalini hapo kutokana na deni kubwa alilokuwa amelipata. Mpaka anaondoka deni lake lililikuwa Sh 961,042. Kutokana na hali yake kuwa mbaya alirejea nyumbani kwao Likawage wilayani Kilwa ambapo mpaka leo analazimika kutumia vidonge vya kupunguza maumivu vya diclopar mbili huku kidonda chake akikifunga na kitambaa cha kawaida ambacho hukifua kila mara.“Ni muda mrefu nashindwa kumudu kwenda hata kufunga kidonda kutokana na hali duni niliyonayo na kushindwa kutembea nalazimika kufunga tambala na kulifua kufunga tena” alisema.Hali yake ya sasa na umaskini wa familia yake unafanya ashindwe kupata msaada wa kurudi tena Muhimbili kukamilisha matibabu. Aliitaka jamii imsaidie kupata fedha za kumaliza deni Muhimbili na kuendelea na matibabu.“Mimi nahitaji msaada wa matibabu. Maisha yangu ya mbele hata siyaelewi. Naomba nisaidiwe matibabu. Namuomba kila mtu anayeweza kunisaidia. Naiomba wizara ya Afya, Namuomba Waziri wa Afya nawaomba wananchi wote watakaoguswa na hali yangu wanaotaka kunisaidia kwa chochote wanitumie katika simu ili niweze kupata matibabu” alisema Mtope ambaye namba yake ya simu kwa anayetaka kumsaidia ni 0659376885.Ofisa Ustawi wa Jamii, Bahiya Akida alisema kwamba Mtepo alifika ofisini kwao na hali yake hairidhishi waliweza kumsaidia walichoweza lakini akasema wasamaria wanaweza kusaidia ili kijana huyo aende kumalizia matibabu Muhimbili na kupona. | 1 |
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, ameweka wazi kuwa hana wasiwasi na maneno ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.
Nyota huyo amekuwa akishambuliwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kugoma kuongeza mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika 2018, hivyo wanaamini kuwa ataondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
“Bado nina mkataba na klabu ya Arsenal hadi pale 2018, hivyo kwa sasa siwezi kusema kama nataka kuondoka, lakini kila kitu kitakuwa wazi baada ya kumalizika kwa mkataba wangu, bado najitoa kwa ajili ya timu yangu.
“Soka sijaanza leo, hivyo nimekuwa nikikutana na changamoto mbalimbali na sishangai kuona baadhi ya mashabiki wa Arsenal wakionesha ubaguzi, hiyo ni karibu kila sehemu na kila klabu lazima utakutana na watu ambao wanakuwa tofauti na wewe, ninachokiangalia kwa sasa ni jinsi gani nitaisaidia Arsenal katika michezo yake na si kuwafikiria wanaonizungumzia,” alisema Ozil. | 2 |
Na DERICK MILTON – SIMIYU SIKU moja baada ya
kuripotiwa habari juu ya kuibiwa kwa mashine ya kupima magonjwa ya ndani mwa
mwili wa binadamu (ultrasound) katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa
Bariadi ya Somanda, Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga, ameagaza wafanyakazi wa
hospitali hiyo kujichangisha na kuinunua. Katika kikao chake
na watumishi wa hospitali hiyo, Kiswaga ametoa siku saba kwa watumishi wote
kuchanga kulingana na mishahara kwa kila mmoja kuhakikisha wananunua mashine
hiyo. Kikao hicho ambacho
kilifanyika jana katika ukumbi wa hospitali hiyo, Kiswaga alimtaka Mganga Mkuu
wa Halmashuari hiyo, Mkurugenzi wa Halmashuari kuhakikisha ikifika Agosti 21, wapeleke
mashine hiyo Ofisini kwake. “Kwa kuwa mashine
hii iliibiwa mchana na ikaibiwa na vifaa vyake vyote, inaonyesha kuwa
walihusika ni wataalamu na kwa maana hiyo watumishi wote 137 wa hospitali hii
mnahusika na wizi huu, hivyo nyie ni watuhimiwa wa kwanza wa wizi huu. “Kila mmoja kuanzia
kwa Mganga Mkuu wa Halmashuari mtachangia kulingana na kila mtu na mshahara
wake, nataka ndani ya siku saba nikabidhiwe hiyo mashine, ambaye atagoma
kuchangia huyo itakuwa halali yangu,” alisema Kiswaga. Pia alisema kuwa watumishi 17 ambao walikamatwa na
polisi kwa ajili ya uchunguzi, kesi yao itaendelea kufanyiwa kazi, huku
akimtaka Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) kukamilisha uchunguzi unakamilika haraka. Aidha Kiswaga
alimtaka Ofisa Utumishi wa Halmashuari hiyo kuorodhesha majina yote ya
watumishi hao kwenye karatasi kisha kumpatia kwa ajili ya kuangalia nani
atakaidi kuchanga ili mashine hiyo inunuliwe. Aidha alisema tabia
ya wizi katika hospitali hiyo imekuwa sugu ambapo wahusika wakuu wamekuwa
watumishi wake, hali ambayo alieleza hawezi kuivumilia kama kiongozi wa Wilaya. “Siyo mara ya
kwanza kutokea wizi kwenye hospitali hii, mlihusika na wizi wa darubini
(Microscope) ambapo baadaye ilipatikana ikiwa juu ya mti imeninginizwa, mkaiba
tena mashine ya kufulia nguo ambayo mpaka sasa haijapatikana na leo tena
Ultrasound hii haiwezekani na wala haikubaliki,” aliongeza Kiswaga. Alisema kitendo
hicho ni uhujumu uchumi hivyo watumishi wote lazima wahusike katika kuhakikisha
mashine hiyo inarudishwa kwa gharama zao. Kiswaga alisema
yuko tayari kufukuzwa kazi kwa hatua yeyote ambayo atachukua kwa watumishi hao
ikiwa watashindwa kuhakikisha wanarudisha mashine hiyo kupitia michango yao
ndani ya muda ambao ametoa. Awali akizungumza
katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashuari, Merkzedeck Humbe, alisema kitendo
hicho ni fedhea kwa halmashuari na Serikali hivyo alisema hatua kali
zitachukuliwa kwa wahusika. “Mashine hii
haiwezi kuibiwa na mtu yeyote kutoka nje bila ya kuwepo kwa ushirikiano kutoka
kwa watu wa ndani, lazima wahusika wapo humu humu, kama ambavyo mlirudisha
darubini basi fanyeni hivyo kwa mashine hii,” alisema Humbe. Awali akitoa
taarifa ya wizi huo Mganga Mkuu wa Halmashuari, Mike Mabimbi, alisema mashine
hiyo iliibiwa Agosti 5, majira ya mchana ikiwa kwenye wodi ya akina mama wajawazito
hospitalini hapo. Mabimbi alisema
baada ya kupata taarifa za wizi huo walitoa taarifa polisi ambapo, watumishi 17
walikamatwa na wamehojiwa ambapo uchunguzi dhidi yao bado unaendelea. Wakati huo
huo Mkuu huyo wa Wilaya ametaifisha pamba inayodaiwa kuwa ya magendo ikiwa ni
siku mbili baada ya kukamatwa kwa gari aina ya scania yenye namba za usajili
T917 BCN ikiwa na pamba tani zaidi ya 20. Pamba hiyo
ilikamatwa katika Kijiji cha Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 12,
saa tano usiku, ikisafirishwa bila kibali maalumu huku ikiwa haijulikani wapi
inapelekwa na wapi imenunuliwa. “Baada
ya wahusika kushindwa kujitokeza, sasa kama Mkuu wa Wilaya nachukua uamuzi wa
kuitaifisha pamba hii na tunaenda kuiuza kwenye viwanda vya kuchambua pamba leo
hii na fedha zote zitapelekwa kununua vifaa vya kukamilisha ujenzi wa bweni
katika Shule ya Sekondari Simiyu,” amesema Kiswaga. | 5 |
KAMANDA wa Polisi Mkoa (RPC) wa Dodoma, Gilles Muroto amewataka viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa, kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini wao katika suala la ulinzi na usalama kwenye kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Alitoa ushauri huo alipozungumza na viongozi wa madhehebu ya dini katika kikao cha pamoja kuhusu hali ya usalama katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya. Alisema kuwa viongozi wa madhehebu ya dini, wanayo nafasi kubwa ya kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini juu ya suala la ulinzi na usalama na maeneo yao yakawa salama na amani.“Jeshi la polisi kwa kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na waumini wakiwa kitu kimoja, kuna asilimia kubwa ya kuwepo kwa salama kwa kipindi hiki cha tunachoendea sikukuu,” alisema.Kamanda huyo alitoa tahadhari kwa waumini katika kipindi hiki cha sikukuu, kujiwekea ulinzi wa kutosha kwenye maeneo yao wanayoishi Kamanda huyo aliwataka viongozi hao wa dini, kuhakikisha nyumba zao za ibada wanafunga kamera, ambazo zitasaidia kudhibiti ulinzi wa maeneo yao.Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya dini ya Kikristo Mkoa wa Dodoma Askofu Damas Mukassa, alilipongeza jeshi hilo la polisi kwa kuwatambua viongozi wa dini kwenye mchango wao wa kushirikiana suala la ulinzi na usalama.Alisema viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na waumini wanaowaogoza, watashirikiana na jeshi hilo muda wote katika suala la ulinzi na usalama, bila kuangalia kama kuna sikukuu. Alisema moja ya majukumu ya viongozi wa dini ni kuhakikisha usalama unakuwepo. Alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama, vipo kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo. | 1 |
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa leseni za udereva na kusema jambo hilo limesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa utoaji leseni ambao hivi sasa unaboreshwa ili leseni ziwe imara na kwamba kazi hiyo itakamilika kabla ya mwisho wa mwezi huu.Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji wa kupewa leseni kwa madereva walioomba leseni kutokana mfumo wa sasa kubadilishwa. Aliongeza kuwa wataalamu hao wakandarasi wameshafika na wanaendelea kukamilisha kazi hiyo na kwamba ndani ya siku chache kuanzia sasa watakuwa wamemaliza na kuanza kutoa leseni kabla ya mwisho wa mwezi huu.“Nia ya serikali na TRA ni kuboresha leseni zetu ili ziwe imara na tumekubaliana na Jeshi la Polisi kwa sasa madereva waendelee kutumia leseni za zamani ili mradi tu anaposimamishwa aoneshe risiti ya malipo aliyolipia leseni mpya,” alisema Kayombo. Alisema lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kompyuta wa leseni ya kuendesha ni kuisaidia serikali kukusanya taarifa sahihi kuhusu dereva ambazo zitasaidia katika kufuatilia mienendo yao na kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato yake ya kutosha.Alisema matarajio ya serikali ni kwamba mfumo huo mpya wa kutoa leseni utapunguza ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva ambao hawana sifa za kutosha za kuendesha magari. Kayombo aliwataka madereva ambao wamelipia leseni na hawajazipata kuwa watulivu kwani maboresho hayo yanayofanywa ni katika kuzifanya leseni hizo mpya kuwa imara na kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia sasa zitaanza kutolewa. Alisema mfumo mpya wa leseni unachukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti. | 1 |
Safina
Sarwatt, Moshi Zaidi ya Dola za Marekani milioni 10, zimetengwa
na Shirika lisilo la kiserikali la Candy and Candy Group Limited, kwa ajili ya
kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake wajane, watoto waishio katika
mazingira magumu na vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo jana
mjini Moshi, Meneja wa shirika hilo, Fortunate Macha, amesema lengo la shirika
hilo ni kuwasaidia makundi hayo kujikwamua kichumi na kuondokana na hali ya
umaskini. “Shirika limetenga fedha hizo kwa makundi hayo
ili kuwasaidia kujikwamua kichumi na kuanzisha biashara mbalimbali itakayowawezesha
kuwaongezea kipato. “Mradi huo kwa mkoa Kilimanjaro unatarajia
kuanza katika vijiji vya Kata ya Pasua na Kahe wilayani Moshi na kuendelea,”
amesema. Kwa upande wake Ofisa Mradi wa shirika hilo, Elizabeth
Sabula, amesema mradi huo pia unatarajia kufikia vijana zaidia 200 wenye vipaji
vya uimbaji. Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa
wa Kilimanjaro, Gerald Sakaya, aliipongeza shirika la hilo kwa kutenga fedha
kwa ajili ya kuwasaidia makundi hayo kuondokana na umaskini. | 5 |
Na ELIYA MBONEA-ARUSHA
SHIRIKA la Mfuko wa Msamaria la Marekani linaloendeshwa na Frankline Graham, mtoto wa Muhubiri maarufu duniani, Bill Graham, limetoa ndege kubwa kwa ajili ya kubeba wanafunzi majeruhi watatu wa ajali ya basi la Lucky Vincent iliyoua watu 35.
Ndege hiyo DC 10, inatarajiwa kuruka usiku wa leo (jana) Alhamisi kutoka Uwanja wa ndege wa Charllote katika Jimbo la North Carolina, Marekani na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo.
Akizungumzia kukamilika kwa baadhi ya hatua za safari hiyo mjini hapa jana, mratibu wa safari hiyo, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, alithibitisha kukamilika maandalizi ya safari hiyo.
“Kuna mambo nimeamua kuyasimamia, nimewasiliana na Shirika la Mfuko wa Msamaria linasimamiwa na Frankilin Graham mtoto wa Bill Graham nimewaeleza kilichotokea kwa watoto wakakubali kutoa ndege,” alisema Nyalandu na kuongeza:
“Tunashukuru Mungu Hati za kusafiria zimekamilika kwa wazazi, madaktari na watoto maandalizi ya VISA yanaendelea kushughulikiwa safari hii tunatarajia itakuwa Jumamosi (kesho) endapo tu VISA itakuwa imekamilika”.
Alisema ndege hiyo DC 10 baada ya kutoka KIA itakwenda moja kwa moja hadi Uwanja wa ndege wa Charllotte, North Calorina.
Alisema baada ya kuwasili uwanjani hapo Shirika hilo la Msamaria limeandaa ndege nyingine maalumu (Air Ambulance) itakayoondoka uwanjani hapo hadi Hospitali ya Mercy iliyopo Jiji la Sioux katika Jimbo la IOWA. | 1 |
Na Christina Gauluhanga -Dar-es-salaam MANISPAA ya Ilala imetumia Sh milioni 86 kwa awamu mbili tofauti kudhibiti
homa za dengue na magonjwa mengine ya mlipuko ili kutokomeza maradhi hayo. Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake juzi, Mganga Mkuu Manispaa ya
Ilala, Dk. Emily Lihawa alisema jitihada zimefanyika kupuliza dawa sehemu
mbalimbali, hasa katika madimbwi. Alisema awali walitumia Sh milioni 52 kununua dawa ya kungamiza
viluilui wa mbu na awamu ya pili wametumia Sh milioni 34 kununua dawa nyingine
za kuua mbu pevu ambayo wamepiga katika shule mbalimbali ili kutokomeza ugonjwa
huo. Emily alisema pia tayari
wamehamasisha wananchi kupima ugonjwa huo ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii wameleta vifaa mbalimbali vya upimaji. “Ndani ya kata 36 tumejitahidi
kuhamasisha upimaji, usafishaji mazingira lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa
ya mlipuko ambapo takwimu halisi zitatolewa na wizara,” alisema Emily. Alisema hata hivyo ugonjwa huo kwa sasa umeshuka tofauti na miaka ya
2011 /2012 ambapo ulianza na kushambuliwa wananchi kwa kasi ikiwamo watumishi
wa afya. Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, alisema hali ni shwari
katika manispaa hiyo kwa kuwa kwa siku tano sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa. | 5 |
Na MALIMA LUBASHA – SERENGETI ZAIDI ya tani 4.1 za chakula zinahitajika wilayani ya Serengeti mkoani Mara ili kunusuru maisha ya kaya zaidi ya 32,000 kutokana na mahindi yao kukauka kutokana na ukame. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alisema hali ya chakula kwa mwaka huu sio ya kuridhisha kutokana na mvua vuli kutonyesha kwa wakati. Alisema wapo baadhi ya watu, wanakula mlo mmoja na wengine mitatu kwa siku na hakuna mtu wala mifugo iliyokufa kutokana na ukame, kwa sasa bei ya mahindi debe moja linauzwa Sh 15,000 ambapo upatikanaji wa chakula kwenye masoko wa kiwango kinachohitajika. Alisema wilaya bado inaendelea kufanya tathimini kwa kupita kila kaya ili kubaini hali ya chakula kwa wale wenye upungufu wa chakula, kaya zisizo na uwezo,zenye uwezo na zile zinazohitaji msaada wa chakula na tayari wameomba kibali ili wafanyabiashara waruhusiwe kuuza mahindi kwa bei nafuu. “Maofisa kilimo wamefanya tathimini kwenye kaya 32,055 zilizopo katika kata 22 kati ya 30,wamebaini kaya 8,582 ambazo ni maskini zinahitaji chakula cha bure tani 811, kaya 10,655 wenye hali ya nafuu wanahitaji tani 1,454.4 na kaya 12,818 zilizo na uwezo wa kununua kwa bei yoyote zinahitaji tani 1,749.7 za mahindi,” alisema Babu. Hata hivyo, Babu amewataka wananchi kuhifadhi chakula kilichopatikana na kuacha utamaduni wa kutumia nafaka kutengenezea pombe za kienyeji na kila familia iwe na ghala la kuhifadhi chakula. Alisema mbali ukame, mvua kutonyesha kutokana na mabadiliko ya tabianchi pia yapo malalamiko ya wananchi kuhusu tembo kuvamia mashamba yao na kula mazao yote na kueleza kuwa changamoto hiyo serikali inalifahamu na takwimu za uharibifu zilikwisha wasilishwa wizara ya maliasili na utalii ili kuli pa kifuta machozi kwa wote walioathirika. | 1 |
HIVI karibuni, Tanzania ilishitushwa na tukio la kutekwa nyara kwa mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Mohamed Dewji (MO). Tukio hilo liliwasikitisha Watanzania wengi, ingawa baadhi ya wanasiasa walitaka kulitumia kama mtaji wa kisiasa kwa kuwa lilikuwa na sura ya kulipaka matope taifa ili wasio makini kufikiri, wadhanii au waamini kuwa Tanzania sio salama.Wengine wameamua kulitumia kuumba maneno yanayofanana na ukweli mengi yakilenga kuipaka matope serikali. Wengine wakataka hata kujaribu kushinikiza Taifa liombe msaada wa wapelelezi kutoka nje ya nchi, huku wakijua wazi kabisa kuwa vyombo vya dola nchini vipo na vinaweza kufanya kazi zake kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha.Ndiyo maana Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Siro, alilihakikishia taifa kupitia vyombo vya habari kuwa, Jeshi la Polisi lipo makini, lina uwezo na litahakikisha MO anatafutwa na kupatikana. Bahati nzuri, ukweli huo ukathibitishwa kwa kupatikana kwa mfanyabiashara huyo.Ndiyo maana Watanzania wanalipongeza na kujivunia kuwa na jeshi lao makini na lenye uwezo wa kuwahudumia, licha ya changamoto kadhaa zinazoweza kujitokeza. UTEKAJI HAUJAANZA LEO Vitendo vya utekaji nyara mara nyingi hutumiwa na baadhi ya watu (wahalifu) kwa madhumuni kadhaa, mojawapo ikiwa ni kujipatia fedha kutoka kwa ndugu wa mtu aliyetekwa.Lakini pia hutumiwa kisiasa kwa maana ya kupunguza nguvu za wapinzani na wakati mwingine hutumiwa kuipaka matope serikali ili kudhoofisha nguvu za kiutawala. Hata hivyo, asilimia kubwa ya utekaji nyara huwa unalenga kujiingizia kipato kwa njia kudai kikombozi ili kumwachia mateka.Uhalifu huu ni kati ya matendo ya kale yaliyofanyika hata kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita kama yalivyo matendo ya rushwa, ugaidi, ukahaba, sanaa ya urembo, ujangili, uharamia, ujambazi, mihadarati na kadhalika.WATU MAARUFU WALIVYOATHIRIWAMtaalamu wa Kuzuia Utekaji El Nahual wa blogu ya Mexico Para los Mexicanos nchini Mexico akitoa maoni juu ya kutekwa Felix I Batista, mtaalamu wa kuzuia utekaji nyara wa Marekani alisema: “Jambo la kwanza kufanya ni kucheka; la pili linalonijia ni woga…Kama mtaalamu wa kijeshi mstaafu mwenye uzoefu wa miaka 24 katika nyanja ya usalama anaweza kutekwa, je, sisi wengine tuna nafasi gani ya kusema kwamba hatuwezi kutekwa?” Batista alitekwa na watu waliovaa vinyago usoni akiwa nchini humo kuendesha semina kama mtaalamu wa kukodiwa wa kampuni ya usalama yenye makao huko Texas ASI Global LLC.Blogu ya The Mex Files ilikuwa na maswali yafuatayo kuhusiana na tukio hilo: Kama Batista ni mtaalamu, imekuwaje akaruhusu atekwe yeye mwenyewe? Batista alikuwa mfanyakazi wa ‘kampuni ya usalama’ yenye makao yake huko Texas ASI Global.Imeelezwa kwamba alikuwa huko Saltillo kwa shughuli za kibinafsi. Je, alikuwa akimfanyia nani kazi huko? Je, kampuni ya ASI Global siyo moja ya kampuni za Kimarekani zinazopokea fedha kwa ajili ya ‘Mpango wa Merida’…Na hili linatuambia nini juu ya utendaji kazi wa wataalamu wake wa ukufunzi? Takwimu kadhaa zinaonesha kuwa utekaji unatokea kwa takribani mara mbili kwa siku na hasa katika majimbo ya mpakani kaskazini mwa nchi hiyo. Mexico ina wastani wa juu zaidi wa utekaji nyara ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.Matukio haya huathiri marafiki na familia za waliotekwa, kama alivyoathirika bloga Tony Scotti, Rafiki wa karibu wa Batista, Tonny alisema hivi: “Ninamfahamu Felix (Batista), ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuzuia utekaji nyara, Felix ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika shughuli za kuokoa mateka.”Akaendelea kusema: “Felix ni mtu anayejulikana, ambaye mara nyingi hunukuliwa kwenye magazeti na hata katika jarida la mwezi huu la Usalama. Kujulikana kwake kunaweza kuwa ndiko kulikomsababishia kutekwa.Baada ya kusoma magazeti ninaweza kuhisi kwamba Felix aliwekewa mtego, na aliwekewa mtego huo na mtu anayemuamini.” Julius Caesar Amiri jeshi aliyefanikiwa zaidi katika hitoria ya dunia, Julius Caesar, alitekwa nyara ili kupata fidia katika karne ya kwanza, ndivyo na Richard wa Kwanza (King Richard I), mfalme wa Uingereza mwenye roho kama simba alivyotekwa.Katika karne ya12 fidia kubwa zaidi iliyowahi kulipwa ilikuwa tani 24 za dhahabu na fedha ambazo Wainka walimpa mvumbuzi maarufu Mhispania Francisco Pizzaro asaidie kuachiwa huru kwa chifu wao Atahuallpa mwaka wa 1533.Hata hivyo, watekaji hao walimuu kwa kumnyonga. Aldo Moro Inaelezwa katika vyanzo mbalimbali kuwa, jambo lililoduwaza ulimwengu ni kutekwa nyara kwa Waziri Mkuu wa Italia, Aldo Moro.Waziri Mkuu huyo alikuwa mwanasiasa maarufu nchini humo aliyependwa sana na raia. Alihudumu kama Waziri Mkuu kati ya 1963-1968. Moro alikuwa ndiye waziri mkuu aliyekuwa amehudumu muda mrefu zaidi tangu wakati wa Vita Kuu vya Dunia.Kundi la Red Brigades lilifanya mashambulio mabaya, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara na mauaji ya Waziri Mkuu huyo wa mwaka 1978. Kundi hilo liliweza kuzuia msafara wa Waziri Mkuu huyo na kuwaua walinzi wake kadhaa na kufanikiwa kumteka nyara likidai Serikali kuwaachilia washirika wake.Serikali haikukubali matakwa hayo ndipo kundi hilo lilipomuua kiongozi huyo kikatili. Moro alikuwa mwanachama wa chama cha Kidemokrasia cha Kikristo cha Italia na alishika madaraka ya uwaziri mkuu kwa duru tano.Umaarufu wake na kupendwa na watu pengine vilisababisha kiongozi huyo kuwindwa na kundi hilo la Red Brigades. Machi 1978, wanachama wa kundi la wanamgambo wa Red Brigades, waliwaua walinzi wake watano na kumteka kwenye barabara moja jijini Roma, wakitaka kuachiliwa huru kwa wenzao 16 waliokuwa wanazuiliwa na serikali,.Moro alipigwa risasi mara kumi akiwa kwenye gari na kutelekezwa akiwa marehemu baada ya kuzuiliwa kwa siku 55. UTEKAJI NCHINI MEXICO Polisi wa mji wa Axapusco walifanikiwa kuwaokoa wahamiaji 103 waliokuwa wametekwa nyara wakiwa wanaelekea kuvuka mpaka wa Marekani katika jengo lililokuwa nje ya mji wa Mexico.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa kijiji hicho, waathirika wengi zaidi walitoka mji wa Guatemala na El Salvador walipofungiwa katika jengo hilo kwa muda wa siku 35.Mmoja kati wa wahamiaji hao alifanikiwa kutoroka na kukimbilia kituo cha polisi kilichopo kijijini hapo kutoa taarifa ya kutekwa kwao. Viongozi wa vikosi bora vya kukabiliana na utekajinyara nchini Mexico, Colombia na katika nchi zilizokuwa jamhuri za Sovieti walilaumiwa kwa kujihusisha na utekaji nyara huo. Naye Mtekaji nyara sugu wa Mexico alisema kuwa alizingirwa na ulinzi rasmi uliotokana kwa kuwahonga maofisa na waendesha mashtaka wa manispaa, jimbo na serikali.UTEKAJI NYARA NA MAUAJIUtekaji nyara na mauaji yanayofanywa na vikundi mbalimbali vya watu walioficha sura zao, limekuwa ni jambo la kawaida katika nchi za Amerika ya kusini. Watu wengi wasiokuwa na hatia wamekuwa wakiuawa. Inakadiriwa kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja, zaidi ya watu laki tano waliuawa na wahalifu; idadi hiyo ni kubwa kuliko ya watu waliouawa vitani.Mataifa mengine yanafika mbali na kuilaumu serikali ya Rais Hugo Chaves kuwa imelea magenge ya watekaji na mauaji. Kwa mujibu wa ripoti hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja, watu zaidi ya 100,000 waliuawa na wahalifu katika bara la Amerika ya Kusini.Nchini Brazili peke yake zaidi ya watu 50,000 waliuawa, nchini Venezuela na Honduras suala la mauaji kama hayo ni jambo la kawaida, kila baada ya dakika 9 hadi 10 utekaji au mauaji hutokea katika nchi hizo.Aidha Sheria ya Kimusa ilitoa adhabu ya kifo kwa watekaji nyara huko nyuma katika karne ya15 (Kumbukumbu la Torati 24:7 Ni kwa msingi huo, unapotokea uhalifu wa namna hiyo na mwingine wowote, wajibu wa raia ni kuvisaidia vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi kusaidia uhalifu usitendeke au kuwakamata wahalifu na sio kujaribu kuwakatisha tamaa watendaji wa vyombo hivyo na wengine kuvutumia kujitafutia umaarufu wa kisiasa. | 1 |
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba, leo watakuwa na kibarua kigumu cha kutaka kuendeleza ushindi katika mchezo wake na timu ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.Mchezo wa leo unatabiriwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na Simba kuhitaji ushindi ili iendelee kujiweka vizuri kwenye kutetea taji lake huku JKT ikihitaji kujiweka sawa ili ibaki kwenye ligi kwani haipo salama sana. Mechi hiyo ni ya pili kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri baada ya Simba kuufanya uwanja wake wa nyumbani kupisha matengenezo kwenye Uwanja wa Taifa. Simba inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na pointi 57 na ushindi wa leo unaweza kuisogeza mbali zaidi.Simba kwa sasa inajivunia kuwa na hazina ya mabao ya kufunga tofauti na timu zinazoshiriki Ligi Kuu kwa vile hadi sasa imefikisha mabao 41 wakati wapinzani wake wakuu Azam FC wakiwa na mabao 28 na Yanga ina mabao 26 ya kufunga. JKT ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi 31, kwa maana hiyo ushindi leo ni muhimu kwake. Kwa sasa timu hiyo inaongozwa na kocha Abdallah Balesi aliyekatishiwa mkataba wake na Prisons kutokana na kuwa na mwenendo mbaya kwenye ligi kabla haijakaa sawa baada ya kocha huyo kuondoka.Balesi amechukua mikoba ya Bakari Shime ambaye pia alikatishiwa mkataba na timu hiyo kutokana na kuwa na mwenendo mbaya. Mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, JKT Tanzania ilifungwa mabao 2-0 hivyo ni kazi kwao kubadili matokeo leo.Simba inatambia safu yake ya ushambuliaji na hivyo mabeki wa JKT watakuwa na kazi ngumu ya kuwazuia washambuliaji wenye uchu wa mabao kama Meddie Kagere na nahodha John Bocco aliyefunga mabao mawili mechi iliyopita huku Kagere akifunga bao moja. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems aliliambia gazeti hili kuwa anaichukulia mechi hiyo kwa uzito wa hali ya juu. Aussems alisema, kila mchezo wa Ligi Kuu kwao una umuhimu mkubwa katika kusaka ushindi utakaochangia kutetea taji lao. | 2 |
SERIKALI imebaini asilimia 88.6 ya waajiri ambao ni wamiliki wa vyombo vya usafi rishaji, hawatekelezi kikamilifu Sheria ya Kazi ikiwemo kutowapa kabisa madereva mikataba ya ajira na likizo ya mwaka. Pia, imebainika waajiri hao wamekuwa wakiwafanyisha kazi madereva kwa saa nyingi zaidi na kutowasajili kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati wa kikao cha mashauriano kati ya ofisi yake na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji. Alisema katika kushughulikia malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji (madereva) za kunyimwa haki zao za msingi na waajiri wao, serikali ilifanya ukaguzi maalumu uliolenga kubaini hali halisi ya utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.Mhagama alisema uchunguzi huo, uliofanyika kati ya Julai 15 hadi Agosti 26 mwaka huu, kwa kukagua kampuni au wamiliki wa vyombo vya usfirishaji 787 kutoka mikoa 24, ulibaini kuwa kati ya waliokaguliwa, ni waajiri 90 tu waliotekeleza kikamilifu sheria ya kazi. “Uchunguzi ulilenga kukagua kama madereva wana mikataba ya ajira, kukagua viwango vya mishahara kwa kulinganisha na Agizo la Serikali Namba 196 kuhusu mishahara ya sekta binafsi la mwaka 2013. Pia tulikagua kama madereva wamesajiliwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kupokea malalamiko ya madereva kuhusu masuala ya saa za kazi na mambo mengine ya ajira,” alisema. Jenista alisema kuwa, “Ukaguzi umebaini kuwa hali ya utekelezaji wa sheria za kazi na kanuni zake katika sekta ya usafirishaji si ya kuridhisha, hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na uelewa mdogo wa sheria za kazi miongoni mwa waajiri na wafanyakazi na hivyo kusababisha kuwepo kwa malalamiko na migogogoro ya mara kwa mara.” Kutokana na ukaguzi huo, serikali na vyama vya wafanyakazi madereva na waajiri walikutana juzi katika kikoa kilichochukua takribani saa sita na kufikia maazimio yaliyosainiwa na pande zote tayari kwa ajili ya utekelezaji. Akisoma maagizo ya kikao hicho, Jenista alisema Mkataba wa Ajira ulioboreshwa uanze kutumika na waajiri wote wawapatie madereva wao mkataba huo. “Mwaka 2017, serikali ilitoa maagizo ya madereva kupewa mikataba wa ajira ulioboreshwa, lakini utekelezaji wake haukuwa mzuri, kwa hiyo sasa ni lazima waajiri kutekeleza hili,” alisema na kuongeza kuwa pia wameazimia Kanuni zinazoandaliwa na Wizara ya Uchukuzi, zitengeneze mazingira yatakayoruhusu Sheria za Kazi kutekelezwa na waajiri. Pia wameazimia kutolewa kwa elimu ya Sheria ya Kazi itolewe kwa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji na vyama vya madereva. “Tunatakiwa kuanza kutoa upya elimu ya sheria za kazi kwa waajiri na waajiriwa katika sekta hii na itolewe kwa nguvu zote.”“Maazimio mengine ni kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo mimi nasimamia kuendela kusimamia kikamilifu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi,” alisema. Alisema pia wameazimia vyama vya wafanyakazi na waajiri, wapewe nakala ya taarifa ya ukaguzi uliofanyika Julai hadi Agosti 2019 ili viweze kujadilianna na wanachama wao na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto. Alisema kikao hicho kimeazimia kuendelea kuheshimu na kuthamini utu na heshima ya mtu kati ya madereva na waajiri na wameazimia kufanyika kwa kikao kitakachojumuisha wizara zote zinazogusa sekta ya usafirishaji na madereva. | 1 |
LONDON, ENGLAND NYOTA wa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Riyad Mahrez, amekata mzizi wa fitina na kuamua kumalizana na klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka minne. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anahusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal, lakini hadi sasa dili hilo linaonekana kufikia mwisho baada ya kumalizana na klabu hiyo ya King Power. Mkataba huo mpya utamfanya mchezaji huyo aendelee kuwa katika uwanja wa King Power hadi Juni 2020, huku akipokea kitita cha pauni 100,000 kwa wiki. Hata hivyo, mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, Jamie Vardy, ameonekana kufurahishwa na kitendo cha mpambanaji mwenzake kujitia kitanzi ndani ya klabu hiyo. Kwa upande mwingine kocha wa klabu hiyo, Claudio Ranieri, amezidi kupata nguvu baada ya kumalizana na mchezaji huyo huku akiwa tayari amemkosa mchezaji wake muhimu katika safu ya kiungo, N’Golo Kante, aliyejiunga na klabu ya Chelsea. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, alionesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini Ufaransa, akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, hivyo kuwashawishi Chelsea kuweka kitita mezani cha pauni milioni 32 katika kipindi hiki cha usajili. Mwenyekiti wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, amefanya mazungumzo ya kina na Mahrez na kumwambia kwamba klabu hiyo inataka kuwapigania wale wote ambao walipambana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, ili waweze kuendelea kukaa kwenye klabu hiyo kwa muda mrefu. Hata hivyo, mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Jeffrey Schlupp, ambaye alikuwa anawindwa na klabu ya West Brom, amekubali kubaki kwa mabingwa hao na yupo tayari kwa dili jipya. Mahrez, raia kutoka nchini Nigeria, alikuwa mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, aliyefunga mabao 17 na kutoa pasi za mwisho 11. Alijiunga na klabu hiyo mwaka 2014, akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa. | 2 |
NEW YORK, MAREKANI
NYOTA ya msanii wa filamu nchini Marekani ambaye ni mzaliwa wa Kenya, Lupita Nyong’o, inazidi kung’ara baada ya kuweka wazi kwamba yupo kwenye maandalizi ya kufanya filamu ya pamoja na nyota wa muziki wa RnB, Robyn Rihanna.
Inasemekana kuwa, wawili hao walikutana mwaka 2014 kwenye mashindano ya urembo yajulikanayo kwa jina la Miu Miu, kisha walipiga picha ya pamoja na baada ya hapo mazungumzo yao yaligusia masuala ya filamu.
Licha ya muda mrefu kupita tangu walipokutana, lakini Lupita alijikuta akimkumbusha Rihanna mbali pale alipoweka picha waliyopiga pamoja na Rihanna walipokutana mwaka huo 2014, huku mashabiki wao wakiwapongeza kwa kupendeza.
Baada ya picha hiyo na kujali kwa mashabiki wao, Rihanna alimtaka Lupita wafanye kitu cha pekee kitakachowaongezea furaha mashabiki wao.
Ndipo wawili hao wakafikia makubaliano ya kufanya filamu ya pamoja inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. “Picha ambayo niliiweka kwenye akaunti ya Twitter imetufanya mimi na Rihanna tufanye filamu, hivyo mashabiki wakae tayari kwa kazi yetu,” aliandika Lupita. | 4 |
BUNGE la Tanzania limeombwa kuunga mkono kampeni ya kuondoa mfumo dume unaowanyima haki ya kurithi ardhi wanawake wanapofi wa na waume zao.Ombi hilo limetolewa na asasi 12 zinazojishughulisha na kutetea haki za wajane kurithi ardhi kwenye mafunzo yaliyowakutanisha na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.Akitoa ombi hilo Ofisa Programu wa Asasi ya Tanzania Land Alliance (TALA), Jamal Kafumbee aliitaka kamati hiyo kuwatetea wanawake hasa wajane kumiliki ardhi baada ya kufiwa na waume zao.Kafumbee alisema sheria nyingi za kimila zimekuwa zikitoa ardhi kwa wanaume au watoto wa kwanza wa kiume, lakini hazitoi ardhi kwa wajane na hata watoto wa kike hata kama wanakuwa wa kwanza kuzaliwa.Alisema wakati wa ukoloni mfumo huo uliruhusu wanaume pekee kulimiki ardhi, lakini wanaliomba Bunge kupitia wabunge majimboni kusaidia kutoa elimu kwa viongozi wa kamati za vijiji kuwapa haki wajane na watoto wa kike katika kumiliki ardhi.Ofisa Programu Mwandamizi kutoka HakiArdhi, Joseph Chombola alisema baadhi ya sheria zinatoa haki upande wa kiume wala si wanawake kuhodhi ardhi ya ukoo zinatakiwa kuendelea kupigiwa kelele ili kuondoka miongoni mwa jamii kwani binadamu wote wana haki ya kumiliki ardhi.Alisema mila na desturi katika baadhi ya makabila zinapendelea wanaume na makabila machache kiasi cha asilimia 15 yanayoongozwa na wanawake ndiyo yanatoa nafasi kwa wanawake kusimamia ardhi.Alisema hali hiyo pia inachangiwa na tamko la kimila la mwaka 1964 ambalo linampa haki mwanaume kumilikishwa ardhi na mwanamke kunyimwa. Akizungumza Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul (CCM) alisema hivi sasa watoto wa kike wanatakiwa kupewa haki ya kumiliki ardhi alisema atashangaa kuona familia za wasomi wa karne hii wanashindwa kuwaridhisha ardhi watoto wao wa kike.Mbunge wa Korogwe Mjini, Timotheo Mnzava (CCM) alisema elimu inatakiwa kuendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali hasa katika ngazi za vijiji ambako mabaraza ya vijiji yamekuwa yakiwanyima haki wanawake pamoja na kuwapo wanawake wawakilishi.Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shaban Shekilindi (CCM) alisema wao kama wabunge wamesikia ombi la asasi hizo na watalifanyia kazi. | 1 |
Na ABDALLAH NG’ANZI (TUDARCo) KUNA wakati unatafakari namna mambo yanavyokwenda, hasa katika zama hizi za kidigitali. Moja ya jambo kuu linaloumiza vichwa vya wahitimu wengi ni ukosefu wa ajira. Ajira imekuwa changamoto si kwa Tanzania pekee bali duniani kwa ujumla. Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kuwa mwaka huu idadi ya watu wasio na ajira itaongezeka kwa asilimia 5.8(awali ilikuwa asilimia 5.7) na kufanya jumla ya watu wasio na ajira kufikia milioni 500.8 duniani . Hili si jambo zuri kulisikia likitamkwa kwani ndoto za wasomi wengi ni kujiajiri au kuajiriwa na kufaidi kile ambacho wamekitafuta kwa jasho kwa zaidi ya miaka 18. Binafsi nimegundua kuwa zipo sababu ambazo zinawakosesha ajira vijana wengi, mojawapo ni ujuzi binafsi wa mtu ukiachana na vyeti alivyo navyo. Kwa mfano, mhitimu akiulizwa mbali na elimu aliyonayo ni kipi cha ziada alicho nacho? Katika dunia ya sasa elimu si stashahada, shahada ya uzamili au uzamivu. Elimu ni namna gani unaweza kukabiliana na mazingira magumu ya ushindani. Kwa sasa kama Taifa tumeanza na soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) lakini pia sisi tukiwa sehemu ya Taifa tunachanganyika na watu wa mataifa mengine. Kuna fursa nyingi tu zinazoweza kubadilisha maisha yetu. Mathalani, mara nyingi watu wanauliza kozi gani inalipa. Ukweli ni kwamba kila kilichopo duniani ukiweza kukitumia vizuri na kwa maarifa kinalipa. Lakini pia lazima uelewe kuwa milango haipo wazi kana kwamba utaweza kupata kila kitu kama unavyotarajia, inahitaji uvumilivu na kuvuja jasho. Mambo yamebadilika, kuna wasomi wengi wenye sifa wanazurura, sasa mwenzangu uliyehitimu juzi tu kama unadhani umefika basi ukweli ni kwamba bado una safari ndefu. Soko la ajira la sasa haliangalii shahada wala stashahada, bali wewe ukiwa mwajiriwa utaleta mabadiliko gani chanya kulisaidia shirika au taasisi? Una ujuzi gani zaidi ya shahada yako? Ikifika hapo kuna mambo yanajitokeza Je, una kitu gani kinachokutofautisha na washindani wengine? Wasomi msibweteke, endeleeni kutafuta ujuzi ili kujiongezea thamani. | 1 |
RAIS mpya wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Wallace Karia (pichani) ameahidi kuimarisha na kuboresha michezo ndani ya nchi wanachama.Karia ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alichaguliwa bila kupingwa kuongoza Cecafa miaka minne katika uchaguzi mkuu uliofanyika Kampala.“Nitaboresha michezo kwa maana ya upatikanaji wa wadhamini kwa mashindano ya klabu, wanawake na yale yanayoshirikisha nchi pia nitaimarisha michuano ya soka la ufukweni na nitasimamia nchi waalikwa kushiriki kikamilifu kwenye michuano inayoadaliwa na Cecafa,” alisema Karia.Pia Karia alisema atahakikisha yanakuwepo mashindano yanayohusisha umri chini ya miaka 15 ili kuwa na timu bora za taifa za baadae.“Kwa sasa tuna mashindano kuanzia U-17 hadi timu za wakubwa nitahakikisha tunakuwa na mashindano ya U-15 kwa wanawake na wanaume ili baadaye tuwe na timu za taifa imara zitakazoweza kushindana,” alisema Karia.Karia ambaye atakuwa madarakani kwa miaka minne atakuwa na Makamu wa Rais wawili, Francis Amin kutoka Sudan Kusini na Esayas Jiro kutoka Ethiopia. Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuhudumu kwa miaka 20. | 1 |
WANAWAKE wawili Mwajuma Hussein (23) mkazi wa kijiji cha Ikongolo wilayani Uyui na Mwanza Kushaha (34) mkazi wa kijiji cha Kombe kata ya Igagala wilayani Kaliua wameuawa na waume zao kutokana na wivu wa kimapenzi.Ametoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Emmanuel Nley alisema Agosti 21, mwaka huu, majira ya saa 11.00 jioni kata ya Ikongolo wilayani Uyui Mwajuma aliuawa kwa kupigwa risasi na mume wake Saidi Ramadhani.Amesema mwanamke huyo alipigwa risasi idhaniwayo kuwa ya gobori huku taarifa za awali zikisema chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.Inadaiwa kuwa, mumewe baada ya kutenda unyama huo alikimbilia msituni na kujitundika juu ya mti na pembeni yake kukiwa na silaha ambayo katika uchunguzi ilibainika ndiyo iliyotumika kumuua mke.Kamanda Nley aliongeza kuwa tarehe hiyo hiyo majira ya saa 5:00 katika msitu wa Isawima kata ya Igagala wilayani Kaliua ulikutwa mwili wa Mwanza Kushaha ukiwa na majeraha kichwani na maeneo mengine ya mwili.Ameeleza kuwa uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa aliuawa na mumewe kwa wivu wa kimapenzi.Mume huyo Chuga Lutumbiga (46), mkazi wa Kaliua amekamatwa.Mtuhumiwa huyo alimuagiza mke wake kwenda kijiji cha Uganza kununua mahitaji na baada ya kuchelewa kurudi nyumbani alimfuatilia na kumkuta njiani akiwa anarudi, ndipo akaanza kumpiga.Aliongeza kuwa baada ya kipigo hicho alimwacha porini akiwa mtupu na kurudi nyumbani na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani ya kumtafuta mke wake.Amesema, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. | 1 |
Na AZIZA MASOUD -DAR ES SALAAM OFISI ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imeiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutenga bajeti kukarabati mitambo na majengo yake ambayo yamechakaa. Akizungumza katika ghafla ya kutoa zawadi kwa walimu wanne na wanafunzi 18 waliohitimu na kufanyaa vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwenye mitihani ya taifa kidato cha nne 2015 na sita 2016, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alisema moja ya changamoto inayoikabili ofisi hiyo ni uchakavu wa majengo ambayo yamejengwa tangu kipindi cha ukoloni. “Majengo yaliyopo mengi ni yale yaliyorithiwa kutoka ukoloni wa Kijerumani, zipo jitihada zinazoendelea za kurekebisha majengo haya, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti zinafanyika kwa kasi ndogo,” alisema Profesa Manyele. Alisema wakala pia ina changamoto ya ukosefu wa vifaa na mitambo ya kisasa na upungufu wa rasilimali watu unaotokana na ufinyu wa bajeti. Aliongeza kuwa ufinyu wa bajeti unatokana na wakala kutopata ruzuku kutoka serikalini na kulazimika kutumia mapato yake ya ndani kutekeleza vipaumbele vinavyotolewa na wizara. Akizungumzia lengo la kutoa zawadi hizo, alisema ni kuleta hamasa kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi nchini waweze kufikia malengo waliyojiwekea. Naye Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari, alisema mkakati wa wizara wa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) hauna budi kwenda sambamba na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika vyuo vya afya na ustawi wa jamii. “Wizara inaendelea na juhudi za kuhamasisha vijana wetu kupenda masomo ya sayansi na hatimaye waweze kuongeza idadi ya wanaodahiliwa katika michepuo ya masomo ya sayansi,” alisema Dk. Bakari. Wanafunzi wa kidato cha nne waliopata zawadi ni Marynas Duduye na Julieth Zannie kutoka Sekondari ya St. Francis, David Joseph kutoka Ilboru na Asha Mlanzi wa Jangwani. Wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika masomo hayo ni Sheikhas Rashid wa shule ya Feza Wasichana, Prisca Kyando kutoka Kilakala na Gastory Munishi wa Mzumbe. Mbali na wanafunzi, walimu waliokabidhiwa zawadi ni Vaileth Kalangali na Frank Mella wa Ilboru, Habil Selemani wa Feza Wavulana na Joram Yohana wa Uwata. | 1 |
Na Harrieth Mandari , Geita MWANAMKE mkazi wa Kijiji cha Buligi, Kata ya Senga, Wilaya ya Geita mkoani hapa, Happyness Shadrack (36), amedaiwa kufanya tukio la kinyama la kumuua kwa kumchinja mtoto wake wa kuzaa, Martha Yakobo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita na kisha kumkatakata vipande na kumpika. Tukio hilo limetokea Juni 21, mwaka huu saa nane mchana. Inadaiwa Happyness akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi, Ruth Shadrack, alimchukua mtoto huyo aliyekuwa amelala kitandani na kumkatakata vipande vidogo vidogo na kisha kumweka ndani ya sufuria. Kwamba baada ya kumkatakata mtoto huyo, aliwasha jiko na kuweka sufuria kisha kuanza kupika kama kitoweo. Mtoto wa pili wa mwanamke huyo, Doris Yakobo, alisema alimuona mama yake akiwa anaweka sufuria jikoni na kuendelea kuchochea moto lakini alipomuuliza alimjibu kuwa anachemsha maji na alipotaka kufunua kuangalia alimkataza. “Mimi ndiyo nilikuwa mara nyingi nakaa na kumwangalia mtoto (marehemu), na siku hiyo baada ya mtoto kusinzia nilimpeleka chumbani nikamlaza kitandani, mama naye alikuwa kwenye chumba hicho hicho akiwa amelala,” alisema Doris. Alisema baada ya kumlaza alitoka nje kwenda kulinda karanga za bibi yake ili zisiibwe na kumwacha mama yake akiwa na mdogo wake wamelala. Doris alisema baada ya muda alimuona mama yake akitoka na kuanza kuwasha moto, huku mkononi akiwa na sufuria iliyofunikwa ambayo aliinjika jikoni na kuanza mapishi. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buligi, Manyoni Manyoni (CCM), alisema kuwa alipata taarifa za mauaji hayo akiwa kwenye kikao ofisini kwake. Manyoni alisema alifika mwendesha bodaboda ofisini hapo na kumtafuta askari ambaye naye alikuwa katika kikao hicho. Alisema mwendesha bodaboda huyo, alitoa taarifa kwa askari huyo kwamba kuna tukio la mama kumchinja mtoto wake. “Baada ya taarifa hiyo, wote tuliokuwa kikaoni tulipatwa na mshtuko na tulilazimika kusimama na kwenda kwenye eneo la tukio ambako tulikuta unyama huo wa mauaji ya mtoto huyo umeshafanyika na mwanamke huyo alikuwa ameshakamatwa na polisi kwa hatua zaidi za mahoajiano na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema Manyoni. Ndugu wa mwanamke huyo, Amoni Mtani, alisema Happyness, amewahi kuathiriwa na ugonjwa wa malaria, hivyo anaamini kitendo hicho amekifanya kutokana na kutokuwa na akili ya kawaida. “Ndugu yangu Happyness (mtuhumiwa) alishawahi kuugua malaria kali sana sasa hatujui labda imeathiri akili hadi kufikia kutenda kitendo hiki cha kinyama, unachinja mtoto na kisha kumpika jamani jamani tumuogope Mungu wetu,” alisema Amoni. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Dismas Kisusi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na kushikiliwa kwa mtuhumiwa. “Ni kweli tukio hili limetokea Juni 21 na tayari Jeshi la Polisi tunamshikilia mwanamke huyo kwa uchunguzi zaidi. Na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mwanamke huyo ana historia ya kuwa na ugonjwa wa afya ya akili,” alisema Kamanda Kisusi Alisema uchunguzi utakapokamilika jalada la mtuhumiwa huyo litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kulipitia kabla ya kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. | 1 |
RAIS John Magufuli amekabidhi zaidi ya hati 1,000 kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, baada ya kufanyiwa urasimishaji kwenye maeneo yao ambapo hati hizo zitawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha na kujikomboa kiuchumi.Hati hizo zimekabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi, Dk Angeline Mabula kwa niaba ya Rais Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Mtaa wa Mecco katika Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela na katika mtaa wa Nyangulugulu katika Kata ya Mahina katika Halmashauri ya jiji la Mwanza.Akikabidhi hati hizo kwa wananchi hao, Dk Mabula alisema rais amesikia vilio vya muda mrefu vya wananchi hao juu ya changamoto za ardhi zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kuporwa viwanja vyao.Aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati zenye umri wa miaka 99, kutosahau kulipa kodi ya serikali, ambayo ndiyo inaiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo miradi mikubwa ya kitaifa.Alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinapima maeneo yote ambayo hayapo kwenye mpango wa urasimishaji, kuwapatia wananchi leseni ya makazi itakayotozwa Sh 5,000 katika kipindi cha mpito cha miaka mitano na baadaye makazi yao yataingizwa kwenye mfumo rasmi wa urasimishaji makazi na kuwapatia hati za umiliki wa maeneo yao.Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hosiana Kusiga alisema urasimishaji katika jiji la Mwanza umefanyika na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, ambapo jumla ya viwanja 19,635 vimepimwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuondokana na ujenzi kwenye makazi holela katika halmashauri hiyo.Amesema halmashauri yake ilikuwa na lengo la kupima jumla ya viwanja 24,000 kupitia mradi huo wa urasimishaji makazi, ambapo viwanja 25,766 ikiwa ni sawa na asilimia 107.3 vimepimwa katika kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, Kishiri na Nyegezi.Kusiga aliongeza kuwa kazi ya upimaji wa viwanja bado inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Kishiri na Luchelele, ambapo jumla ya viwanja 19,635 upimaji wake umekamilika ikiwa ni sawa na asilimia 80. | 1 |
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) lipo tayari kuingia kwenye mjadala na serikali kuangalia njia mbadala za kuwasaidia wakimbizi wanaohudumiwa hapa nchiniPia limeahidi kufuatilia kila aina ya mavazi yanayoingizwa nchini kuwasaidia wakimbizi ili kuhakikisha hayaingii mavazi yanayofanana na sare za wanajeshi kama ilivyotokea karibuni na kuleta mtafaruku.Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa UNHCR, Fillippo Grandi alisema Tanzania imekuwa ikisaidia wakimbizi kwa miaka mingi na kuna changamoto ambazo UNHCR imebaini na kuwa zinahitajia mjadala wa pamoja na serikali ili kuwasaidia wakimbizi waliopo nchini.Alizibainisha changamoto hizo kuwa ni pamoja na njia bora za kuwahudumia wakimbizi ambapo alisema kuwa wakimbizi sio lazima wakae kambini tu kama ilivyo ila wanaweza kufanya shughuli za kiuchumi. Alitolea mfano kwenye kambi ya Nyarugusu ambapo awali kulikuwa na soko lililokuwa likitumiwa na wakimbizi hao pamoja na wananchi wa eneo jirani kuuzia na kununua mazao kama njia mojawapo ya wakimbizi kujipatia kipato na kuwa kutokana na kufungwa kwa soko hilo baadhi yao sasa wameathirika.Pia alisema kwenye mfumo wa kuwapokea wakimbizi kuna changamoto za baadhi kukataliwa kuingia nchini wakati wengine ni wagonjwa. Alisema kuna haja ya kuwapokea kwanza wote wanaoomba kuingia. Aliongeza kuwa licha ya Tanzania kufanya kazi kubwa ya kuwapokea wakimbizi hao nchini na kuwasaidia kwa kila hali, imeonekana bado kuna changamoto ambazo UNHCR na wadau wengine wanalo jukumu la kusaidiana na Tanzania kuzitatua hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji. “Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa katika namna ya kuwapokea na kuwarejesha majumbani kwao wakimbizi.Sina maana ya kuwa haifanyi kazi nzuri ila ninachomaanisha kuwa kuwa kuna haja ya kuwa na mjadalana Serikali tena shirikishi kubainisha sababu za changamoto hizo na kuzitatua,” alisema. Pia alisema suala la wakimbizi kurejea makwao linatakiwa kuwa ni la hiari zaidi na sio lazima au mkimbizi kuwekewa mazingira yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi kurejea kwenye nchi waliyotoka.Aliongeza kuwa nchi ambazo wakimbizi wanarejea makwao pia zinapaswa kuandaa mazingira rafiki ya kiuchumi kwa wakimbizi ambayo yatawawezesha kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa muda mrefu. Kuhusiana na mavazi yanayofanana na sare za jeshi yaliyokamatwa kambi ya wakimbizi Kigoma, Grandi alibainisha, sio lengo la UNHCR kuziingiza nchini na kuwa zilitokana na misaada ya watu mbalimbali. Alisema kuna nchi ambazo mavazi ya aina hiyo ni kitu cha kawaida na ndio walisaidia kuyaingiza nchini.Hata hivyo, alikiri k hilo ni kosa kwa kuwa haitakiwi mavazi yenye kuendana na sare za kijeshi kupewa wakimbizi kwani haitakiwi kujihusisha na shughuli za kijeshi hivyo hata mavazi yanayofanana sio mazuri. Mkuu huyo wa UNHCR alipongeza juhudi za Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa za kupigania amani nchini Burundi na kutoa mwito kwa nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupigania amani kwenye nchi zao ili wakimbizi waliotoka huko warejee nchini mwao.“Nimekutana na Rais John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga na mawaziri wengine wanaohusika moja kwa moja na kuhudumia wakimbizi na nimefanya majadiliano yenye tija kubwa kwa faida ya wakimbizi. Ninaishukuru Tanzania kwa msaada wao mkubwa kwa wakimbizi hawa, “alisema. Grandi aliwasili nchini Jumanne wiki hii na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam ambapo alimwomba radhi kwa kupatikana kwa sare za jeshi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kigoma. | 1 |
Taarifa ya Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana, Alfred Lucas ilisema Mkude analazimika kubaki kutokana na ushauri wa Daktari aliyemtaka kupumzika kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali juzi.Nahodha wa Simba, Mkude alikuwa miongoni mwa abiria sita waliopata ajali wakitokea Dodoma kwenye mechi ya fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao juzi ambapo shabiki mmoja wa Simba Shose ‘Wazza’ Fidelis alifariki dunia.Simba ilishinda mabao 2-1. Stars inakwenda Misri kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Lesotho Juni 10, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, Dare s Salaam.“Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia Mkude kubaki na kusema kuwa ataungana na wenzake Juni 8 mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri. Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude,” alisema.Aidha, Mkude aliliambia gazeti hili jana muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu tangu juzi usiku kwamba ana majeraha kidogo shingoni lakini anaendelea vizuri.“Nashukuru Mungu naendelea vizuri, daktari aliniambia sina tatizo kubwa ni mshtuko wa ajali na kwamba naweza kuendelea na ratiba zangu ndio maana nilikwenda kambini kuungana na wenzangu,” alisema.Lucas alisema wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa wataungana na wenzao moja kwa moja katika kambi ya Misri.Katika mechi hizo za kufuzu, Tanzania imepangwa kundi L pamoja na Lesotho, Uganda na Cape Verde . Kikosi cha Taifa Stars kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC).Walinzi wa kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Agrey Morris (Azam FC) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa sasa.Viungo wa kushambulia ni Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting). Wasaidizi wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa, meneja wa timu, Danny Msangi, mtunza vifaa Ally Ruvu, Daktari wa timu Richard Yomba na Daktari wa viungo Gilbert Kigadya. | 2 |
WADAU wa maendeleo na wahisani wanaosaidia miradi ya afya nchini wamepongeza maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali nchini katika kuimarisha utoaji huduma, upatikanaji wa vifaa na dawa za kutosha hali inayochangia kupunguza vifo ikiwemo vifo vya wanawake wajawazito na watoto.Kauli hiyo ya wadau wa maendeleo imetolewa mjini Kigoma wakati wa hafla ya kufungwa kwa mradi wa miaka 13 wa afya ua uzazi, mama na mtoto uliokuwa ukilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua ambapo mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya mkoani humo na kuwezesha kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Engender Health Tanzania, Prudence Masako alisema kuwa pamoja na uboreshaji wa maeneo ya utoaji huduma uliofanywa kwa pamoja baina ya serikali na wadau, uhakika wa upatikanaji wa madawa na vifaa tiba lakini uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara umekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto mkoani Kigoma.Masako alisema kuwa dhana ya ujenzi wa uboreshaji wa vituo vya afya maeneo ya mbali na hospitali za wilaya na mkoa inatokana na miundo mbinu duni ambapo mama wajawazito na watoto walikuwa wakifia njiani hali ambayo kwa sasa ni tofauti ambapo mgonjwa anayehitaji rufaa anaweza kusafirishwa kwa haraka kwenda hospitali ya wilaya na mkoa kwa matibabu ya kitaalam zaidi.Mratibu wa Shirika la Bloomberg Philanthropies, ambao ndiyo wafadhili wa mradi huo, Dk Godson Maro alisema kuwa mradi umekuwa na mafanikio makubwa na hiyo inatokana na ushirikiano mkubwa ambao serikali imetoa katika utekelezaji wake kuanzia ngazi za zahanati hadi kwa waziri wa afya ambaye amesaidia sana mradi kutekelezwa hadi kufikia mafanikio yaliyopo sasa.Dk Maro alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa miaka 13 mkoani Kigoma jumla ya vituo vya utoaji huduma 100 vimeboreshwa kwa majengo, uwekaji wa vifaa tiba na elimu kwa watoa huduma 400 ambapo takwimu hizo zinaonyesha kuwa jumla ya vituo afya 13 vimepandishwa hadhi na kuweza kutoa huduma za dharula za upasuaji kwa mama wajawazito.Mratibu wa Miradi ya Afya ya Uzazi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamad Makuwani alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa na kuwa serikali imetekeleza ujenzi wa vyumba vya upasuaji wa dharula kwenye vituo vya afya nchi nzima lengo ikiwa kusaidia kuokoa vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua. | 1 |
WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga wamewataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia timu yao ‘ikipindua meza kibabe’ wakati wakirudiana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika hatua ya makundi.Yanga ambao wanashika mkia katika Kundi D wakiwa na pointi moja tu, wanaikaribisha Gor Mahia iliyopo katika nafasi ya pili katika msimamo huo, mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo katika mitaa ya Twiga na Jangwani, msemaji wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa timu yao itashinda baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa mwanzo.Mbali na kutamba kulipa kisasi, Yanga pia ilitangaza viingilio vya mchezo huo, ambavyo ni Sh 10,000 kwa VIP A wakati VIP B na C ni Sh 7,000 huku mzunguko ni Sh 3,000.Aliwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, ambao umepangwa kuanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Tayari Yanga katika mechi tatu ilizocheza hadi sasa za Kombe la Shirikisho imefungwa mabao manane baada ya kufungwa 4-0 na kutoka suluhu na Rayon Sports ya Rwanda.Yanga iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika katika. | 2 |
Aidha, imeahidi pia kutoa zawadi ya dola za Marekani 20,000 kwa mshindi wa kwanza na dola 10,000 kwa mshindi wa pili kwa wauzaji hao.Hayo yalibainishwa jana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania, Wang Guang Jun wakati akizungumza katika mkutano na wasambazaji wa simu za mkononi na kuwaeleza mipango ya kampuni hiyo.Katika mkutano huo, Huawei Device Tanzania waliweka msisitizo katika haja ya kusaidia ukuaji kwa kutoa motisha kubwa ambapo Wang alitangaza kuwa asilimia 10 ya mapato ya kampuni hiyo yatatengwa kama uwekezaji wa kimasoko ili kuongeza na kuboresha bidhaa za Huawei.Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam na kuwashirikisha wasambazaji wa simu za mkononi. | 0 |
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KOCHA wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amewafunda wachezaji wa Tanzania na kuwataka kujituma wanapokuwa uwanjani ili wapate soko la kimataifa na kufikia hatua kama ya Mbwana Samatta, anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji. Kocha huyo raia wa Uganda alisema hayo mara baada ya kushuhudia mchezo wao uliopita dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo wachezaji wa timu pinzani walikuwa wakitumia muda mwingi kulinda lango lao na kushindwa kupambana ili kupata mabao. Akizungumza jana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyokuwa yanafanyika katika Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini hapa, Mayanja alisema ni vema mchezaji akaonyesha kiwango chake vizuri pindi anapopata nafasi ya kucheza ili aweze kujitangaza zaidi. “Wachezaji wanatakiwa kubadilika na kuangalia zaidi mbele ili wafanikiwe kama wenzao ambao wanacheza soka la nje, mfano mzuri ni Samatta ambaye kwa sasa anaendelea kuipaisha Tanzania Ulaya, hivyo wanatakiwa kufahamu wanapocheza watu wengi wanawaangalia huo ndio mwanzo wa kuvitangaza vipaji vyao,” alisema. Akizungumzia mchezo unaowakabili dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kocha huyo alisema wanataka kuvunja mwiko kwa kuamini kuwa timu kubwa lazima zifungwe na timu hiyo wanapokutana katika uwanja wao. Alisema mpira wa sasa hauna desturi ya kufungwa ugenini, isipokuwa kila mtu anakuwa na mipango yake itakayomfanikisha kupata ushindi, kitu ambacho wao wamejiwekea ili kupata pointi tatu muhimu ili waendelee kupeta kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara. “Tunatarajia kuondoka Alhamisi au Ijumaa kuelekea Tanga, ila kwa sasa kikosi kipo vizuri tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya kupambana katika mchezo huo na majeruhi wanaendelea kuimarika,” alisema. | 2 |
KAIMU Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah amesema hivi sasa mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo inatembelewa na takribani Watanzania 1,500,000.Tuma ametoa maelezo hayo kwa washiriki takribani 400 walioishriki kwenye Jukwa la Biashara mkoani Geita mwishoni mwa wiki, hivyo kuwataka kufanya kazi na taasisi hiyo.Ameitaja mitandao hiyo kuwa ni DailyNews digital ambayo huendesha mtandao wa Youtube, Twitter, Facebook, Instagram na pia habari kupitia tovuti yake. TSN pia huchapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo.Tuma ametoa mwito kwa Watanzania kutumia vyombo vya TSN ambavyo amesema haviripoti mambo ya kuzua isipokuwa kuandika ukweli kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.Amesema kutokana na mapinduzi ambayo TSN imekuwa ikifanya, kwa sasa mbali na habari pia hutengeneza makala za video (documentaries) na kwamba tayari mashirika kadhaa yamefaidika na kazi hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).Pia amesema TSN inafanya kazi ya kutafsiri, hususani kutoka Kiswahili kwenda Kingereza au kutoka Kingereza kwenda Kiswahili pamoja na uchapishaji wa vitabu na mabango.Kuhusu Jukwaa la Biashara, aliwataka wananchi wa Geita kufanyia kazi yote yaliyojitokeza kwenye jukwaa hilo.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Jim Yonazi, aliushukuru Mkoa wa Geita hususani Mkuu wa Mkoa huo, Robert Gabriel, kwa namna ulivyolipokea Jukwaa hilo.Dk Yonazi ambaye alikuwa Mhariri Mtendaji wa TSN kabla ya hivi karibuni kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, ameipongeza pia idadi ya watu waliojitokeza kwenye jukwaa hilo jana hadi watu wengine kukosa viti.“Mwitikio huu unaonesha kuwa wana-Geita tuko tayari kupokea mabadiliko,” amesema.Dk Yonazi ambaye ndio mwanzilishi wa Majukwaa ya Fursa za Biashara, alishukuru taasisi kadhaa zilizojitokeza kudhamini jukwaa hilo.“Wengi wametupokea na kuwa tayari kufanya kazi na sisi katika kufanikisha majukwaa haya toka tumeanza,” amesema Dk Yonazi na kutaja baadhi ya taasisi hizo ambazo zilikuwepo jukwaa hilo la Geita ni GGM, NBC, CRDB, TIRA, TRA, TCRA, TBC, Busowala Mining, TAGB (Benki ya Kilimo), Waja General, Rex Energy, ATCL na SSRA. | 1 |
Akizungumza na gazeti hili, baada ya mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Taifa, Mkwasa alisema kikosi chake kipo tayari kutetea bendera ya Taifa, kwani wameshafanyia kazi upunguzo waliouona katika mchezo wa kwanza.“Timu ipo vizuri na wachezaji wote wapo isipokuwa Mbwana Samatta ambaye anatarajiwa kuwasili kesho (jana) kuungana na wenzake na kama ulivyoona morali ipo juu, nina uhakika wa kushinda ili kujiweka nafasi nzuri,” alisema Mkwasa.Mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwepo mazoezini juzi. Katika mazoezi hayo, Mkwasa alionekana kutilia mkazo zaidi safu ya ushambuliaji akiwasimamia Elias Maguli, Ulimwengu na John Bocco.Mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani kutoka Kundi G unatarajiwa kuwa na ushindani, kwani Misri wana pointi saba na Taifa Stars ina pointi moja.Misri utakuwa mchezo wao wa mwisho, wakati Taifa Stars baada ya mchezo huo itabakisha mchezo mmoja ugenini dhidi ya Nigeria. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na mwamuzi Meya Bastred akisaidiana na Mihndou Gauthar na Vinga Theophil na mwamuzi wa mezani ni Oboga Eric wote kutoka, Gabon.Katika kundi hilo, Misri ndiyo wanaongoza wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Nigeria wenye pointi mbili Tanzania na Tanzania ya tatu ikiwa na pointi moja. Kundi lina timu tatu tu baada ya Chad kujitoa. Wakati huo huo, msafara wa watu 60 wakiwemo wachezaji, viongozi na mashabiki wa Misri uliwasili Dar es Salaam jana tayari kwa mchezo huo. | 2 |
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema kabla ya kufanya uchaguzi huo mashirikisho hayo yanatakiwa kulipa ada zao ili kuwa hai kwa ajili ya uchaguzi huo.“Ieleweke kwamba hakuna chama au shirikisho litakaloruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi bila kuwa hai kwa maana ya kulipa ada zote kama zinavyoelekezwa,”alisema.Mngereza alisema uchaguzi ufanyike mara moja kabla ya Februari mwaka huu viongozi wapya wawe wamekwishapatikana.Pia, alizungumzia umuhimu wa wasanii kuhakikisha wamesajiliwa, kuwa na vibali vya kufanya kazi za sanaa na kushiriki kikamilifu kujenga mfumo wa utawala katika sekta ya sanaa utakaokuwa unatumika kama mfumo sahihi na rasmi wa mawasiliano baina ya serikali na wasanii.Alisema kutokana na huko nyuma serikali kupata ugumu wa kuwasiliana na msanii mmoja mmoja, wanahamasisha umuhimu wa kuanzishwa vyama na mashirikisho ya wasanii na kuwalekeza kujiunga katika umoja huo kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa sekta hiyo.Alitaja mashirikisho baadhi yaliyoundwa kuwa ni shirikisho la wasanii wa muziki, ufundi, maonesho na filamu.“Mashirikisho yote haya yanajumuisha tanzu zote za sanaa na yanaundwa na vyama wanachama ambavyo kimsingi vinaundwa na vikundi vya wasanii na mmoja mmoja kulingana na fani husika,” alisema.Alisema licha ya kuwa wasanii huhamasika kuunda mashirikisho hayo, bado idadi kubwa ya wasanii hasa wenye majina makubwa wameendelea kuwa nje ya mfumo huo wa utawala katika sekta ya sanaa hali ambayo sio tu imeyafanya maslahi yao kukosa sauti ya pamoja bali pia kudhoofisha juhudi. | 2 |
JAKARTA, INDONESIA IDADI ya watu waliokufa kutokana na matetemeko ya ardhi na kimbunga cha tsunami nchini Indonesia imefikia 1,424. Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la kuratibu majanga, karibu watu 2,550 wamejeruhiwa vibaya. Msemaji wa shirika hilo, Sutupo Nugroho ametoa takwimu hizo jana wakati akizungumza na waandishi habari mjini Jakarta. Nugroho amesema bado kuna watu wengine waliofukiwa katika udongo na vifusi vya majengo yaliyoporomoka. Wakati huo huo, shirika la kimataifa la msaada kwa watoto, Save the Children limesema kiasi ya watoto 600,000 wametenganishwa na wazazi wao kutokana na majanga hayo na wamepatwa na mshtuko. Shirika hilo limesema watoto wengi wanalala mitaani na wengine kuachwa yatima na kwamba mashirika ya misaada yanashirikiana kwa karibu na serikali ili kuwatambua na kuwaunganisha watoto hao na ndugu zao. | 3 |
MBUNGE wa Kwanza wa Jimbo la Kondoa Kusini (1985 -1990) Shaban Muyombo, amesema serikali inakwenda kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la Farkwa ambayo ilikuwa ni ndoto ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.Akizungumza jana wakati wa mahojiano na gazeti hili, Muyombo alisema sasa, ndoto hiyo inatimia baada ya serikali kutoa fedha za kulipa wananchi ili kupisha ujenzi wa bwawa hilo.Alisema wazo hilo lilitolewa kabla ya uhuru na liko kwenye mpango wa mji wa Dodoma kuwa maji yatatoka katika chanzo cha Mzakwe na bwawa la Farkwa.“Tunafurahi kuona kuwa ndoto za Mwalimu zinakwenda kutekelezwa kwenye serikali ya awamu ya tano baada ya serikali kuwa na vyanzo vingi vya mapato pamoja na Rais mwenye nia ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,” alisema.Alisema vijiji vya Bubutole na Mombose vinapitiwa na mto bubu ambao unaanzia milima ya Hanang mkoa wa manyara na sasa utamwaga maji bwawa la Farkwa. Alisema miaka ya 1974 wachina walifanya mradi wa visima katika kijiji cha Jogolo kwa kutoboa maji ambayo yanatumiwa na wananchi na uwepo wa mradi wa ujenzi wa bwawa la Farkwa utasaidia sana upatikanaji maji katika wilaya za mji wa Dodoma, Serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vya Mombose na Bubutole wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ili wapishe ujenzi wa bwawa hilo.Wananchi zaidi ya 2,868 wataanza kulipwa kuanzia Oktoba 15 hadi 31 mwaka huu. Bwawa hilo linatarajia kumeza vijiji viwili. Hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitilya Mkumbo alitoa mwito wa serikali kwa wananchi hao baada ya kulipwa fedha hizo wapishe maeneo hayo.“Viongozi lazima mkawaeleze wananchi ukweli wakishalipwa lazima wapishe eneo, tukishakulipa uondoke ili kazi ya ujenzi ianze,” alisema.Alisema bwawa hilo baada ya kukamilika litakuwa likisambaza maji katika Jiji la Dodoma na wilaya za Chamwino, Bahi na Chemba. Profesa Kitilya alisema mradi huo upo kwenye vitabu vya bajeti na upo katika kipaumbele cha juu na serikali inaendelea kufuatilia fedha za ujenzi na kujenga miradi mingine. Alisema bwawa hilo litakuwa ni fursa kwa wananchi na litaleta fursa nyingi za kiuchumi na kijamii. | 1 |
Na Mwandishi Wetu Mafuriko
yaliyosababishwa na mvua kali maeneo ya kusini na magharibi mwa Irani yameua takriban watu 23
na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyombo
vya habari. Awali,
Wizara ya Mambo ya Ndani iliwashauri watu wa Irani kuahirisha safari zao lakini
pia kufuata onyo lilitolewa kwa uzito na Shirika la Usimamizi wa Maafa ambalo lilitoa
ujumbe wa maandishi ili kuwaonya watu kuhusu kutumia njia ambazo zinaweza
kukabiliana na mafuriko, ikiwa ni tahadhari pia kwa wale waishio katika milima
na mabonde ya mto. Janga
hili limetokea kipindi hiki wakati wa Mwaka Mpya wa Irani, Nowruz, pia ni
likizo, ,uda ambao Waislamu wengi wanasafiri nchini. Kulikuwa
na mvua nzito za dakika 15 ambazo zilisababisha mafuriko kuenea katika jiji
hilo lakini pia yasemekana idadi ya majeruhi ingekuwa chini endapo wtu
wngefuata tahadhari iliyotolewa kabla ya mafuriko. | 3 |
LISBON, URENO MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo,
amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuumia mapema wiki hii akiitumikia
timu ya taifa Ureno kwenye michuano ya kuwania kufuzu Euro 2020. Katika mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya
bao 1-1, lakini mchezaji huyo hakumaliza dakika 90 kutokana na kuumia nyama za
paja na kuwaweka wasiwasi mashabiki wa Juventus kuelekea michezo yao mbalimbali
ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba,
japokuwa alitolewa kwenye mchezo huo, lakini hana tatizo kubwa la kutisha na
kumfanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. “Sina wasiwasi kwa kuwa ninaujua vizuri mwili
wangu, haya yanatokea kwenye soka, hivyo ninaamini ninaweza kuwa nje ya uwanja
kwa wiki moja au mbili, nitakuwa imara. “Najua mashabiki wana hofu, lakini nataka
kuwatoa wasiwasi kwamba nitarudi viwanjani siku za hivi karibuni,” alisema
mshambuliaji huyo. Ronaldo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya
Juventus tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid mwishoni mwa msimu
uliopita. Mchango wake umeifanya Juventus kuingia hatua
ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwaondoa
Atletico Madrid. Mchezo wa kwanza Atletico Madrid walifanikiwa kushinda mabao
2-0, huku mchezo wa mwisho wa marudiano Ronaldo aliifungia Juventus mabao
matatu katika ushindi wa 3-0 na kuifanya timu hiyo kufuzu, ambapo inatarajia
kukutana na Ajax, Aprili 10, mwaka huu. Endapo hali ya mchezaji huyo itakuwa bado
haiko sawa ndani ya wiki mbili, basi ataukosa mchezo huo wa kwanza wa robo
fainali dhidi ya Ajax. Timu hiyo ya Ajax imefanikiwa kuingia hatua hiyo baada
ya kuwaondoa wababe wa michuano hiyo Real Madrid, hivyo timu hiyo inaonekana
kuwa tishio kubwa msimu huu. | 2 |
KATIKA simulizi nilizowahi kuzisikia kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam ni kuhusu eneo la Gongo la Mboto. Simulizi hii nilisimuliwa na jirani yangu zamani kwenye miaka ya 1998 alipokuwa akinielezea asili ya maeneo kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam na mengine ya mikoa kadhaa. Wakati huo, nilikuwa makini zaidi kwa Mkoa wa Dar es Salaam labda kwa sababu naishi hapa na nayafahamu. Miongoni mwa maeneo hayo ni Gongo la Mboto ambapo nilielezwa kuwa asili ya jina hilo ni mkulima mmoja aliyekuwa maarufu akiitwa Mboto. Alikuwa na tabia ya kutembea na gongo. Siku moja wakati alipokwenda shambani kwake kulima, hakurudi nyumbani nyakati za jioni kama kawaida yake.Ilipofika siku ya pili hakurudi nyumbani hadi mchana, taarifa ikatolewa, watu wakakusanyika kumtafuta.Hali ikawa ngumu kidogo kwa sababu wakati ule kwenye maeneo hayo kulikuwa hakujachangamka yaani hakuna makazi kama sasa, mapori na vichaka vilikuwa vingi na kuleta hali ya giza. Msako ule ulifanyika siku kadhaa na baadaye walikuta nyayo za mnyama mkubwa ambaye hakufahamika ni mnyama gani zaidi ya kuhisi labda chui au simba na kwa kuangalia vichaka, wakabaini kulitokea purukushani fulani hivi. Aidha,walikuta gongo la Mzee Mboto ambalo siku zote hutembea nalo. Kutokana na ishara hizo na kupatikana kwa hilo gongo, wakahisi Mzee Mboto ameshafariki dunia na atakuwa ameliwa na mnyama mkali na mkubwa. Tangu siku hiyo eneo hilo likaitwa Gongo la Mboto na mwili wa Mzee Mboto haukuwahi kuonekana hadi leo. Hiyo, ndiyo sababu ya eneo hilo kuitwa Gongolamboto Imeandikwa na MAULID AHMED | 1 |
Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’ Etienne Ndayiragije amesema hakuna kikwazo kitakachokizuia kikosi chake hicho kuibuka na ushindi kitakaposhuka dimbani leo kuumana na Burundi ( Intamba m’Urugamba), katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. Pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa litapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulipigwa kati kati ya wiki hii jijini Bujumbura, ambapo Stars ililazimisha sare ya bao 1-1. Ili kusonga mbele hatua ya makundi, Stars italazimisha kusaka sare ya aina yoyote au ushindi, huku wapinzani wao Burundi wakihitaji ushindi pekee ili kupiga hatua nyingine mbele. Faida iliyonayo Stars kuelekea mchezo huo ni akiba ya bao moja la ugenini ililolipata katika mchezo wa kwanza nchini Burundi. Kikosi hicho cha Stars kitashuka kuikabili Burundi kikijiamini kutokana na rekodi nzuri inapokutana na timu hiyo nyumbani. Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hizo katika ardhi ya Tanzania, Stars imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja. Hata hivyo, rekodi za jumla pia zinaibeba Stars inapokuana na Burundi. Kwa ujumla timu hizo zimekutana mara 19, Stars imeshinda 11, sare tatu na kupoteza mitano. Mara ya mwisho zilikutana Machi 28, 2017. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Taifa na Stars kushinda mabao 2-1. Ushindi wa mwisho wa Burundi dhidi ya Stars iliupata Novemba 28, mwaka 2012. Katika mchezo huo wa michuano ya Chalenji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Burundi ilitakata kwa bao 1-0. Kocha Mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije akizungungumzia maandalizi ya kikosi chake alisema wamejiandaa kiasi cha kutosha kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele. Alisema imani aliyonayo inatokana na sehemu kubwa ya kazi waliifanya ugenini hivyo leo watamalizia ungwe iliyobaki kwa kuibuka na ushindi. “Mchezo wa marudiano utakuwa wa kufa au kupona kwa sababu ndio utakaamua mustakabali wetu, lazima tutumie vema uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo mazuri na kusonga mbele. “Kasoro tulizoziaona katika mchezo wa kwanza tumezirekebisha, lakini hata yale mazuri tuliyoana pia tumeyaboresha zaidi mazoezini, vijana wameahidi kukata kiu ya Watanzania kwa kupata ushindi, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” alisema Mgunda. Mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva ambaye alifunga bao la kusawazisha la Stars kule Burundi alisema kwa upande wao wa wachezaji wamejiandaa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. “Tunashukuru tulikuwa na mchezo mzuri ugenini, tumerudi nyumbani kwa ajili ya kumaliza kazi, sisi kama wachezaji tuko tayari kujitoa kwa hali yeyote, Huu ni mchezo muhimu kwa Watanzania wote hivyo ni muhimu kuwa na mshikamano ili tufanikishe lengo kwa pamoja,” alisema Msuva. Naye mshambuliaji Adi Yussuf alisema baada ya kuanza vizuri ugenini watahakikisha wanamaliza kazi nyumbani. “ Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza ugenini, wachezaji walijituma , tunakila sababu ya kushinda kwani tutakuwa nyumbani huku tukipata sapoti ya Watanzania wenzetu,” alisema mshambuliaji wa Blackpool ya Ligi Daraja la Kwanza England. | 2 |
ELIZABETH HOMBO NA HARRIETH MANDARI, DAR ES SALAAM
RAIS Dk. John Magufuli amemwomba Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kumsaidia namna ya kuzungumza na Umoja wa Nchi tano zinazochipukia katika uchumi (Brics), ili apate mkopo wa riba nafuu utakaosaidia kujenga reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge).
Pia amesema wamekubaliana na Rais Zuma kuwa atapeleka walimu wa Tanzania kwenda Afrika Kusini kufundisha Kiswahili.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Ikulu Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kutia saini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Rais Zuma ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku mbili, kabla ya kutiliana saini hizo, aliteta na Rais Magufuli kwa saa takribani mbili.
Hati hizo ni pamoja na muhtasari wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya marais, makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya bioanuwai na uhifadhi na makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi.
Viongozi hao pia walizindua rasmi Tume ya Pamoja ya Marais (Bi- National Commission- BNC), kwa kufanya kikao cha kwanza cha tume hiyo tangu ianzishwe mwaka 2011, huku wakipokea makubaliano yaliyofikiwa katika kikao cha tume ngazi ya mawaziri.
Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake na Rais Zuma, alimweleza kuhusu ujenzi wa reli ya kati, mradi wa Liganga na Mchuchuma na kuwataka wafanyabiashara wa nchi hiyo kuwekeza nchini.
“Nimemuarifu Rais Zuma kuhusu miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), mradi wa Liganga na Mchuchuma na nimewakaribisha wawekezaji kutoka Afrika Kusini.
“Nimemwomba kupitia zile nchi zenye utajiri unaoinukia, Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini kutusaidia kupata mkopo wa riba nafuu utakaotusaidia kujenga Standard Gauge. Najua yeye hatashindwa akitia neno.
“Pia tumekubaliana na Rais Zuma kuwa Tanzania itapeleka walimu wa Kiswahili ambacho kinazungumzwa na watu takribani milioni 120 duniani wakafundishe lugha hiyo katika vyuo vya nchi hiyo,”alisema Rais Magufuli.
Alisema kwa kuwa Tanzania imefanya mengi katika ukombozi wa nchi hiyo, hivyo waifikirie namna ya kuisaidia.
Alisema hivi sasa biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini kwa mwaka ni Sh trilioni 2.4, uwekezaji wa Afrika Kusini nchini ni Dola za Marekani milioni 803.15 uliozalisha ajira 20,916 na kwamba kiwango hicho kinaweza kuongezeka.
Pia alimshukuru Rais huyo wa Afrika Kusini kwa mchango wa madawati 1000 yaliyotolewa na Serikali ya nchi hiyo wakati wa kampeni za kuchangia madawati.
Rais Zuma
Naye Rais Zuma alitoa pole kwa Watanzania kuhusiana na ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vicent, walimu wawili na dereva wa basi mkoani Arusha.
“Napenda kutoa pole kwa vifo vya watoto iliyotokana na ajali huko Arusha. Tunaungana na Watanzania kuwalilia hawa watoto ambao wamepoteza maisha yao wakiwa wadogo,”alisema Rais Zuma.
Rais Zuma ambaye alifuatana na mawaziri sita na wafanyabiashara zaidi ya 80 wa nchi hiyo, alimpongeza Rais Magufuli kwa kuanza ujenzi wa reli ya kati huku akiahidi kuunga mkono juhudi hizo.
Alisema anatambua kuwa ujenzi wa reli ya kati utaleta manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi za Maziwa Makuu hivyo atahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi yake kushirikiana kufanikisha mradi huo.
“Pia nimefurahi tumekumbuka tulikotoka katika uhusiano wetu, nimekumbuka Mazimbu mkoani Morogoro hatuwezi kusahau pia Dakawa.
“Jana nilipofika wakati natambulishwa viongozi, mmoja akasema katokea Kinondoni nikasema kanikumbusha mbali,”alisema Rais Zuma.
Rais Zuma alimwalika Rais Magufuli kufanya ziara nchini humo kuendelea kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.
WAFANYABIASHARA A. KUSINI
Wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini wamesema wamewashauri Watanzania kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kuuuza nchini mwao kuinua uchumi kati ya nchi hizi mbili.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Uwekezaji Afrika, Kitengo cha Biashara na Viwanda Afrika Kusini, Zanele Mkhize wakati wa mkutano kati ya wafanyabiashara Tanzania na Afrika Kusini, Dar es Salaam jana.
Akieleza umuhimu wa uhusiano wa uchumi endelelvu kati ya nchi hizo mbili, alisema ingawa kwa sasa bado idadi ya wawekezaji Watanzania nchini Afrika Kusini ni ndogo, ipo haja ya wengine kuendelea kuwekeza nchini humo. | 1 |
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hatarajii kuona 'disco-toto' ikifanyika popote pale jijini katika kuadhimisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Ameeleza kuwa hadi sasa hakuna aliyepeleka maombi kwa jeshi hilo ili kutoa huduma hiyo kwenye siku za sikukuu, ili ukaguzi wa kina ufanyike kwenye kumbi hizo kwa ajili ya usalama wa watoto.Amesema hayo alipofanya mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake, asubuhi ya leo, Jumamosi.Kamanda Mambosasa pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusherehekea sikukuu hizi ili kuepusha matukio ya watoto kupata ajali, kupotea na kuzama kwenye fukwe, kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma."Jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kulinda raia na mali zao kwenye siku za sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya ikiwa ni pamoja na mikesha yake," alieleza.Kamanda Mambosasa ametia wito pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote katika maadhimisho ya sikukuu hizo ili kuwepo na amani na usalama. | 1 |
Tanzania inatarajia kupata Dola za Kimarekani milioni 75 (takribani Shilingi bilioni 172.5) kwa ajili ya kuboresha elimu ya ufundi stadi.Fedha hizo zitatolewa na Benki ya Dunia (WB) kupitia mradi wake wa mafunzo ya ufundi kwa nchi za Afrika Mashariki (EASTRIP) utakaozinduliwa rasmi mwezi Juni, nchini Ethiopia.Haya yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alipozindua awamu ya kwanza ya programu ya Stadi za Ajira Tanzania (SET) leo, Ijumaa, itakayoratibiwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).Amesema mradi huo unashirikisha nchi tatu ikiwa ni pamoja na Kenya na Ethiopia na lengo kuu ni kuboresha mafunzo ya ufundi kwenye nchi zilizoteuliwa.“Mradi huu utaunga mkono juhudi za serikali kuboresha elimu ya ufundi kwa Watanzania ili kufikia lengo la kuwa uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” aliongeza. | 1 |
Na BENJAMIN MASESE MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, amewatahadhirisha wananchi kutodhubutu kupewa pipi na mtu yeyote ndani ya gari binafsi au basi la abiria. Amesema baadhi ya pipi hizo hupakwa dawa za kulevya na kusababisha kupoteza fahamu. Amesema tayari madhara ya ulaji wa pipi yalimkuta mtumishi mmoja wa Serikali ambaye alipewa pipi ndani ya basi na kujikuta akizinduka akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekeo Toure, akipatiwa matibabu. Tahadhari hiyo aliitoa alipozungumza na wananchi wa Kata za Igoma na Kishili kuhusu mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya ya Nyamagana. Tesha ambaye hakutaka kutaja jina lake la mtumishi huyo aliyekula pipi lakini alidokeza cheo chake kuwa ni mkurugenzi. Alisema alipewa pipi na abiria mwenzake aliyekuwa jirani na muda mfupi alisinzia na kupoteza fahamu. “Naombeni wananchi tuwe na tahadhari sana juu ya ulaji wa vitu ndani ya vyombo vya usafiri, hili nalisema wazi kwani limekuwa likijitokeza. “Hivi karibuni kuna mtumishi mmoja alikuwa anasafiri ambako alipopewa pipi na abiria mwenzake kumbe ilikuwa imepakwa dawa za kulevya. “Mtumishi huyo ambaye tena ni mkurugenzi alijikuta akizindukia Sekeo Toure, hajui alifikishwa vipi katika hospitali hiyo. “Epukeni ulaji wa pipi pia kwa sababu umekuwapo utapeli kwa njia ya simu nao umeendelea kutikisha nchi na watu kuibiwa mamilioni ya fedha,”alisema. Tesha alizungumzia suala la wana wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba akiwaonya wazazi watakaoshindwa kuwapeleka kuanza kidato cha kwanza watafikishwa mahakamani. Alisema ifikapo Januari 31, 2017 ataanza ziara ya kutembelea shule zote ndani ya Nyamagana kubaini wanafunzi walioshindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kuwachukulia hatua wazazi wao. Wananchi wa Igoma na Kishili walimweleza DC kwamba kumekuwapo na kero ya kukatika daraja la Fumagila linalounganisha wilaya za Misungwi na Nyamagana na kusababisha wananchi kushindwa kwenda shule hasa mvua inaponyesha. Akitoa majibu, alisema tayari Serikali imetenga Sh milioni 300 kwa ajili ya kujenga daraja la Fumagila na kuwataka wazazi kuwasindikiza wanafunzi na kuwavusha upande wa pili mvua inaponyesha. | 1 |
ASHA BANI-DAR ES SALAAM
WAUAJI wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ‘wamembipu’ Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, kwa kuua mtu mwingine usiku wa kuamkia jana katika Kitongoji cha Kazamoyo Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini wilayani humo.
Wauaji hao walivamia kijijini hapo na kumpiga risasi shingoni, Erick Mwarabu (38) ambaye ni fundi rangi.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mwarabu akiwa nyumbani kwake saa 8.00 usiku juzi, wauaji hao walifika na kumpiga risasi shingoni ambayo ilitokea kichwani upande wa kulia kati ya jicho na sikio na akafariki dunia papo hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo, aliithibitishia MTANZANIA kwa simu kwamba tukio hilo la mauaji lilitokea usiku wa kuamkia jana.
Alisema tayari mwili wa marehemu umekwisha kufanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa mazishi.
Kifo cha Mwarabu kinafanya idadi ya watu waliouawa hadi sasa katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani kufikia 30.
Kutokana na vitendo hivyo vya mauaji, hivi karibuni IGP Sirro, alitangaza mkakati wake ikiwamo jinsi ya kukomesha mauaji katika maeneo hayo.
IGP Sirro aliapa kupambana na wauaji hao huku akiahidi donge nono la Sh milioni 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kukamatwa wauaji hao.
Alisema polisi wanaendelea na operesheni mbalimbali kuhakikisha vitendo hivyo haviendelei na kwamba lazima watafanikiwa kubaini mzizi wa mauaji hayo.
Mei 21 mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alitembelea eneo hilo na kuteta na askari wa operesheni maalumu ya kuwasaka wauaji wilayani Kibiti.
Alisema mauaji hayo sasa yametosha akisisitiza Serikali haitakuwa tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea kama ilivyo Somalia.
Ziara hiyo ya ghafla ya Waziri Nchemba ilitokana na mauaji ya mara kwa mara ya raia ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana.
Akizungumza baada ya kuwatembelea polisi katika kambi maalumu ya operesheni ya kusaka wahalifu katika Kata ya Bungu, alisema Serikali imejipanga kukomesha hali hiyo kwa sababu kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama.
“Tunaendelea kufuatilia kazi mnayoendelea kufanya, tuendelee kusonga mbele. Nikiziangalia takwimu na mwenendo, nazidi kupata maswali na naendelea kuona kuwa kuna kamchezo kanachezwa.
“Mauaji haya waliyoyafanya inatosha. Lazima tuwatie nguvuni, hatuwezi kuruhusu jambo hili likaendelea na kamchezo haka kakaendelea.
“Anayefanya mauaji haya, anayeshirikiana na anayeshangilia hiki kinachofanyika wote tunawaweka katika kundi moja. Kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama,”alisema.
Nchemba aliwataka polisi hao kukaa kimkamkati kuwakamata wauaji hao.
Alisema ni muhimu polisi waondokane na dhana kwamba wametokomea kusikojulika bali wawakamate. | 1 |
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati na 217,016 wameshahudumiwa. Kaimu Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI, Dk Angela Swai, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.Alisema wagonjwa hao wamepatiwa huduma hiyo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wapo wagonjwa kutoka Zimbabwe, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Ethiopia na hata katika visiwa vya Comoro ambao wamekuwa wakipatiwa huduma hapa ikiwamo za shida za mishipa ya moyo iliyoziba.”“Gharama sio kubwa sana hata kwa wagonjwa wanaotoka nje ya nchi, hatujazitofautisha sana na wagonjwa wa ndani, gharama hizo ni sawa na zile anazotoa mgonjwa anayetibiwa katika hospitali za binafsi,” alisema.Alisema ni muhimu wananchi wakatambua huduma za moyo zinazotolewa katika taasisi hiyo na kuchukua hatua pindi wanapobaini kuwa na shida za aina hiyo. Dk Angela alisema tangu kuanzishwa kwa JKCI Septemba 2015, imekuwa ikihudumia wagonjwa kutoka mikoa yote nchini ambao wamekuwa wakipewa rufaa kutoka hospitali za mikoa kwa ajili ya kupata huduma ya kiwango cha juu cha tiba ya moyo.“Wagonjwa katika taasisi hii hupata huduma za matibabu za kibingwa za magonjwa yote ya moyo zikiwamo za upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua, urekebishaji wa mfumo wa umeme wa moyo, tiba ya mishipa ya damu na utayarishaji wa wagonjwa wanaokwenda kupandikizwa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema.Kuhusu viwango vya vifo katika taasisi hiyo kila upasuaji unaofanyika, alisema JKCI hufanya uchunguzi kwa mwezi kwa wagonjwa waliofariki, jambo ambalo huwasaidia kujitathmini zaidi kiutendaji. Lengo la tathmini hii ni kujipima katika ufanisi wa utoaji wa huduma za upasuaji wa moyo na kuweza kujipanga zaidi kwa huduma zilizo bora kwa kipindi kingine.Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Moyo katika taasisi hiyo, Dk Tulizo Sanga, alitoa mfanokuwa, kwa kipindi cha miaka mitatu imeweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje ya nchi 217,016, huku waliolazwa wakiwa ni 11,587 na waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua ni 1,098.Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa huduma madhubuti zinazotolewa na wataalam wazalendo wanaofanya kazi ya kuwahudumia wananchi wenye matatizo na wasio na matatizo ya moyo kwa kutoa mada mbalimbali zinazowasaidia kujikinga na maradhi hayo. | 1 |
NA OSCAR ASSENGA KUNA usemi unaosema ukicheka na nyani utavuna mabua, hali hii inajidhihirisha katika matukio ya wanafunzi wa kike kukatishwa masomo kutokana na kupata ujauzito na kusababisha kushindwa kufikia ndoto zao za kupata elimu bora ambayo inaweza kuwa mkombozi kwa maisha yao. Licha ya kuwapo kwa sheria kali za vifungo vya miaka 30 kwa watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine kuwapa hali hizo wanafunzi hao, lakini suala hilo limekuwa wakati mwingine likimalizwa kienyeji na mamlaka husika kutokana na wahusika au jamii fulani inayotajwa kwenye jambo hilo kuamua kukaa na kuyaongea na hatimaye kuweza kuyamaliza. Jambo hilo limeleta manung’uniko kwa watendewa kwani ni wazi kuwa baada ya kutokea hali hiyo msingi mzima wa maisha yao unakuwa umepotea na kujikuta wakishindwa kujua wafanye nini baada ya kujikuta wakiingia kwenye majukumu ya kuitwa mama bila kutarajia. Licha ya Serikali ya kuonekana kulipa uzito jambo hilo, lakini yapo baadhi ya maeneo nchini ambayo vitendo hivyo vinatokea na baadaye wahusika kuamua kukaa pamoja na kufikia mwafaka, huku mtendewa akiendelea kubaki hana la kufanya kutokana na ndoto yake kukwamishwa. Nasema hivyo kwa sababu kama hatua kali zingekuwa zinachukuliwa ipasavyo, hili ambalo limejitokeza kwa Mkoa wa Tanga kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata mimba yaani mimba za utotoni 261, lisingejitokeza kwa kiasi hiki. Takwimu hizo zilizotolewa hivi karibuni na Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Tanga, Wiliam Mapunda, zinaonyesha idadi kubwa ya waathirika wa jambo hilo ni wanafunzi wa shule za sekondari ambapo 206 waliripotiwa kupata ujauzito wakiwa mashuleni. Huku kwa shule za msingi walioripotiwa walikuwa 55, jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa taaluma ya elimu mkoani hapa, lakini linaweza kukwamisha nyuma juhudi zinazoweka iwapo halitapatiwa ufumbuzi haraka. Ni dhahiri kabisa vitendo hivyo iwapo vitafumbiwa macho vinaweza kukatisha ndoto za wanafunzi wengi ambao wanatarajiwa kufanikiwa kupitia elimu hata kuiongoza jamii ya Watanzania. Wapo baadhi yao walikuwa na ndoto za kuwa siku moja mawaziri, mabalozi na hata viongozi ambao wangeweza kuisaidia jamii kuinuka kiuchumi, hivyo mambo yanapokuwa kinyume chake kutokana na kupata ujauzito ni kuzima malengo yao muhimu. Lakini sababu kubwa ambayo huenda ikawa inachangia kutokea matukio kama haya ni uwepo wa ngoma za usiku maarufu kama baikoko na vibanda vya video, jambo ambalo limekuwa hatari kwao kutokana na vishawishi. Jambo kubwa na la msingi ambalo linaweza kusaidia kuondokana na kadhia hiyo ni utungwaji wa sheria kali itakayosaidia jamii hiyo kuweza kusoma bila kuwepo kwa vipingamizi vya aina yoyote ile. Kwani ni ukweli usiopingika leo hii kwenye maeneo ya vijiji mbalimbali hapa nchini wapo wanafunzi ambao hivi sasa wanajuta kutokana na kukatishwa masomo kutokana na kupata ushawishi kujiingiza kwenye mapenzi na hatimaye kujikuta wakipata ujauzito ambao unakwamisha ndoto zao. Sambamba na kuchukuliwa hatua kali wahusika, lakini pia lazima kuwepo na sheria ambayo itawabana wanafunzi watakaobanika kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, huku wakijua kuwa bado hawajafikia wakati wa kufanya hivyo ili kukomesha tabia hiyo. Kwani tunaweza kuwakamata vijana ambao wana mahusiano na wanafunzi kumbe ukakuta wao wenyewe ndio washawishi wakubwa kutaka mambo hayo, jambo ambalo linaweza kukwamisha juhudi za kuwaepusha na madhila hayo. Kama hatua zinachukuliwa kwa wahusika na kuachwa wanafunzi ambao wamekubali kuingia kwenye mahusiano na dhahiri jambo hili hatutaweza kulimaliza. Lakini pia lazima jamii itambue kuwa jambo kama hilo linapotokea kwenye jamii zao na kuamua kulifumbia macho kwa kuyazungumza kifamilia au kindugu, inachangia mambo ya aina hiyo kuendelea kutokea. Suala kubwa ambalo limekuwa likiziponza familia nyingi hasa za vijijini kwani wanaona wakimpelekea Polisi muhusika atafungwa miaka 30 na wazazi watamhudumia mtoto, kutokana na hali hiyo wazazi wanaona ni bora vijana hao waoane ili waweze kukaa pamoja na kuwatunza watoto wao, hivyo lazima Serikali ione namna ya kufikisha elimu kwenye maeneo hayo ili vitendo hivyo vimalizike. | 1 |
Vijana, licha ya kufungwa na Pazi vikapu 82-76 bado inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 ikifuatiwa na JKT yenye pointi 13, ambayo iliifunga Jogoo kwa vikapu 68-55 lakini pia ikafungwa na Ukonga vikapu 54-47.Oilers inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo sita na kushinda yote, ABC ambayo iliifunga Mabibo vikapu 60-50 inashika nafasi ya tano baada ya kucheza michezo saba, ikishinda mitano na kupoteza miwili.Ukonga Kings inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo saba, ikishinda mitano na kufungwa miwili, Jogoo inashika nafasi ya nane licha ya kufungwa na Kigamboni vikapu 71-63 ikiwa imecheza michezo saba, kushinda minne na kupoteza mitatu na kujikusanyia pointi 11.DonBosco Youngstars inashika nafasi ya tisa ikiwa imecheza michezo sita na kushinda minne na kufungwa miwili na ina pointi 10, Mabibo Bullets inashika nafasi ya kumi baada ya kucheza michezo saba, ikashinda mitatu na kufungwa minne na kukusanya pointi 10.Kurasini Heat inashika nafasi ya 11 ikiwa imecheza michezo nane, ikashinda miwili na kufungwa michezo sita na kukusanya pointi 10, Magnet ipo nafasi ya 12 ikiwa imecheza michezo saba, ikashinda mitatu na kufungwa minne na kujikusanyia pointi 10 Kigamboni inashika nafasi ya 12 ikiwa imeshuka dimbani mara nane na kushinda mchezo mmoja na kukusanya pointi nane, UDSM Insiders ambayo iliifunga Tanzania Prisons vikapu 66-56 ikiwa ni ushindi wa kwanza baada ya kucheza michezo saba ina pointi nane na Magone inaburuza mkia ikiwa na pointi nane baada ya kucheza michezo nane na kufungwa yote.Kwa upande wa timu za wanawake, Ukonga Queens inaongoza msimamo ikiwa na pointi nane, DonBosco Lionesses inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi saba sawa na JKT Stars, Jeshi stars ina pointi tano sawa na Oilers Princesses na Vijana Queens inaburuza mkiwa ikiwa na pointi nne. | 2 |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeelezea masikitiko yake kutokana na kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ikisema ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mihayo Juma N’hunga wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika duniani kote jana. N’hunga alisema Dk Mengi atakumbukwa kwa mambo mengi mema akiwa miongoni mwa wawekezaji wa mwanzo kuitumia fursa ya kuanzishwa vyombo vya habari nchini.Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa imesaidia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo ajira kwa waandishi wa habari wanaomaliza elimu kwa viwango mbalimbali. “Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar natoa salamu za masikitiko kufuatia kifo cha mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi ambaye ametumia muda wake mwingi katika kuwekeza kwenye sekta ya habari na ajira,” alisema Naibu Waziri N’hunga.Aliwataka waandishi wa habari na wawekezaji wengine kuiga mfano wa Mengi aliyetumia utajiri wake kwa ajili ya uwekezaji na kutoa ajira kwa watu wengine. “Watu wengine ikiwemo matajiri waige mfano wa Mengi katika kutumia utajiri wake kwa ajili ya kuwanufaisha wengine,” alisema. Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Hassan Mitawi alisema baraza litamkumbuka Mengi kwa ushirikiano wake mkubwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vimetoa mchango wa hali ya juu katika uhuru wa vyombo vya habari.Alisema wakati waandishi wa habari wakiadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wanatakiwa kukumbuka mchango wa Dk Mengi aliyesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini. “Mengi tutamkumbuka kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini sambamba na uhuru wa taaluma hiyo ikiwemo kutoa ajira kubwa kwa waandishi wa habari,” alisema. Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, Dk Mzuri Issa alisema taaluma ya uandishi wa habari imepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Dk Mengi. | 1 |
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. | 0 |
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake. | 0 |
Na CHRISTOPHER MSEKENA STAA wa filamu za Kibongo Irene Uwoya, ameendelea kugonga vichwa vya habari za burudani baada ya mume wake, Hamad Ndikumana aliyefunga naye ndoa ya Kikristo kufariki dunia mapema wiki hii akiwa nyumbani kwake, Kigali nchini Rwanda. Kwa wiki tatu mfululizo Uwoya amekuwa hakuauki kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa tukio aliloliita ni ndoa ya Kiislamu aliyofunga na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, ndoa ambayo Janjaro alithibitisha siyo filamu, licha ya Uwoya kudai ni filamu. Mfululizo wa tukio la ndoa mpya na msiba wa mume wake, Ndikumana yamepokewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wake. Wapo waliompa pole huku wengine wakimtusi. Wanaomtusi wanahusisha tukio lake la ‘ndoa tata’ na Janjaro kuwa huenda limemuumiza Ndikumana kiasi cha kupata mshtuko wa moyo na kupoteza maisha. Hata hivyo, kwa jumla wengi wameonyesha kuguswa na msiba huo na kuonyesha hisia zao. Katika kundi hilo ambalo lina watu wengi zaidi, wamekwenda mbali zaidi na kuumizwa kwa msiba huo kiasi cha kufananisha na pigo alilopata mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady baada ya kufiwa na aliyekuwa mumewe Ivan Don. NDOA Uwoya aliolewa na kocha huyo msaidizi wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda mwaka 2009 na katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Krish, ambaye amekuwa akiishi naye jijini Dar es Salaam. Upande wa Zari, naye alifunga ndoa ya kimila na mfanyabiashara wa Uganda, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ miaka mingi iliyopita na katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata watoto watatu wa kiume. CHANGAMOTO NDANI YA NDOA Mwezi uliopita, Uwoya na mzazi mwezake marehemu Ndikumana, walianza kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii ambapo Ndikumana alitoa malalamiko kwa mrembo huyo kuwa katika maisha yao hakuwa mkweli ikiwa ni pamoja na kumnyima haki ya kumsalimia mtoto wao, Krish anayeishi Bongo na yeye akiwa anaishi Rwanda. Malalamiko hayo, Uwoya aliyakanusha na zaidi aliendelea kufanya mitikasi yake ikiwa ni pamoja na kula bata nchini China hata aliporejea nchini, Octoba 27, mwaka huu akadai kufunga ndoa na Dogo Janja, jambo ambalo lilionekana kutomuumiza Ndikumana. Alichofanya Ndikumana ni kujibu mashambulizi kwa kumtangaza mpenzi wake mpya wa Kinyarwanda, aliyemtaja kwa jina la Asmah na kuendelea na maisha yake ya furaha huku akionyesha kutokuwa na presha na ndoa ya Uwoya na Dogo Janja kwani mrithi wake aliweza kurudisha tabasamu lake lililopotea. Hiyo ilikuwa Oktoba 31, mwaka huu. Upande wa Zari, raia huyo wa Uganda aliachana na mume wake Ivan Don mwaka 2014 baada ya kunasa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambapo mpaka sasa wamepata watoto wawili, Tiffah na Nillan. Zari alikuwa karibu mno na watoto wake aliozaa na Ivan Don licha ya vijana hao wa kiume kuishi na baba yao Uganda na Afrika Kusini lakini hakuwahi kuonyesha nia ya kumrudia mumewe zaidi ya kuboresha panzi lake jipya na Diamond Platnumz. Ivan Don kwa muda wote huo akiwa mbali na mke wake alionyesha kuwapenda watoto wake, kusimamia miradi yake iliyopo Afrika Kusini na Uganda pamoja na kula bata na kundi lake la Rich Gang bila kuwa karibu na mrembo mwingine. VIFO VYA WAUME ZAO Kifo cha Ndikumana kimetokea ghafla usiku wa kuamkia Jumatano ya wiki hii, akiwa nyumbani kwake. Inadaiwa alipata tatizo la maumivu ya kifua kabla ya mauti kumkuta. Siku nzima kabla ya kifo chake alikuwa mzima, hata jioni yake alikuwa mazoezini akiwanoa wachezaji na yeye mwenyewe akishiriki mazoezi. Afisa Habari wa klabu hiyo aitwaye Gwakaya alisema Ndikumana alipata maumivu makali ya kifua na akaomba soda ya baridi, alipomaliza kunywa kidogo akatapika kisha akakata kauli hivyo anadhaniwa amekufa kwa ugonjwa wa moyo. Ndikumana ni baba wa watoto wawili wa kiume Baasit na Krish. Alizikwa Jumatano kwenye mjini Nyamirambo, Rwanda. Kifo cha Ivan Don, kilikuja baada ya tajiri huyo kuugua na Zari kushiriki katika kumuuguza kwenye Hospitali ya Stive Biko Academy, Afrika Kusini mpaka alipofariki kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo, Mei 25, mwaka huu na kuzikwa Nakarilo, Uganda. UWOYA AVISHWA VIATU VYA ZARI Kama unavyoona hapo juu, matukio yaliyotokea kwenye maisha ya Zari yanawiana kidogo na yale yaliyomtokea Irene Uwoya kwa kuwa wote waume zao wamepoteza maisha baada ya ndoa zao kuvunjika. Mungu ailaze roho ya marehemu Hamad Ndikumana mahali pema peponi – Amina. | 4 |
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora inahitaji mwekezaji ajenge kiwanda cha tumbaku.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adam Malunkwi amesema ofisini kwake mjini Urambo kuwa, tumbaku ni zao mama na linalimwa katika kila eneo wilayani humo.Amewaeleza waandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, Halmashauri hiyo imetenga eneo la kujenga kiwanda hicho na linafikika kwa kuwa miundombinu ipo, na pia kuna umeme na maji.“Kwa hiyo tukipata mwekezaji anayeweza kusaidia kujenga kiwanda cha tumbaku utakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwenye wilaya yetu ya Urambo na maandalizi ya awali kama nilivyosema tulishayaweka vizuri. Kwa hiyo hilo ndiyo ningeomba liwe la kwanza katika vipaumbele vyetu kwa upande wa viwanda” amesema Malunkwi.Amesema, Urambo pia inahitaji mwekezaji wa pembejeo za kilimo kwa kuwa hilo limekuwa tatizo kubwa katika eneo hilo.“Upatikanaji wa pembejeo za kilimo kama tunaweza tukapata mwekezaji mzuri akadhamini jambo hili kwa uhakika katika mkoa wetu wa Tabora hasa wilaya yetu ya Urambo inaweza kutusaidia. Na pembejeo zinazosumbua ni hizo za zao la tumbaku na zao la mahindi”amesema.Makunkwi amesema, Urambo pia inahitaji mwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa maeneo yapo na kuna fursa za kutosha.“Kama tunaweza tukapata wawekezaji katika masuala ya umwagiliaji tuna imani kabisa masuala ya kilimo hasa mpunga tunaweza tukalima mara mbili kwa mwaka, watu wanaweza wakalima bustani za vitunguu, nyanya na mazao mengine ambayo yanaweza yakasaidia vipato kwa wananchi wetu wa wilaya ya Urambo” amesema.Kwa mujibu wa Malunkwi, Urambo pia imetenga eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo. | 0 |
Anna Potinus – Dar es Saaam Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), wametangaza kushirikiana na kampuni ya Wasafi Ltd katika kupeleka ujumbe kwa jamii kuhusiana na suala la afya kupitia tamasha la Wasafi festival ambapo wasanii watapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 10, katika ofisi za Tacaids zilizopo Posta jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi na mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’, amesema lengo kuu la ushirikiano huo ni kuangalia ni namna gani wasanii wanaweza kutumia vipaji vyao kuelimisha jamii. “Tuliona
tuandae tamasha la Wasafi festival ambalo litatukutanisha na kutumia sanaa yetu
katika njia zilizo sahihi hivyo tukaona sasa imefikia muda kutumia ushawishi
tulionao na katika kulifanikisha hilo tukasema tukishirikiana na Tacaids
pengine tutafikisha ujumbe mzuri zaidi,” amesema. “Hauwezi kutimiza ndoto zako kama hauna afya bora hivyo tukiwa kama wasanii ambao Mungu ametupa Baraka za ushawishi tunaweza tukafikisha ujumbe kwa wenzetu wakatuelewa hivyo tumeshirikiana na Tacaids katika kuwaelimisha vijana namna ya kutumianafasi tulizonazo katika njia chanya zitakazoleta maendeleo katika nchi yetu,” amesema. Naye Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Tacaids, Jumanne Issango, amesema vijana ndio kipaumbele
katika katika mapambano dhidi ya ukimwi na kwamba ndio kundi lenye kiwango
kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi “Utafiti
uliofanyika 2016/17 unaonyesha kwamba maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kundi
la vijana kati ya miaka 15-24 wanachangia asilimi 40 ya maambukizi mapya kati ya
maambukizi ya idadi ya watu 72,000 kitaifa kwa mwaka hivyo baada ya kuzindua
utafiti huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa Tume kutumia wasanii kufikisha
ujumbe na elimu ya VVU na Ukimwi na kuhamasisha suala la upimaji kwa vijana,”
amesema Issango. “Majukwaa
ya wasanii ni mengi lakini mwaka huu tumebahatika kushirikiana na Wasafi
tumeambiwa takribani wasanii 20 wana ushawishi hivyo tumeona ni fursa nzuri
katika kuwafikishia ujumbe vijana juu ya maambuziki ya virusi vya ukimwi, eneo
muhimu ambalo tutaliwekea msisitizo ni pamoja na matumizi ya Condom, upimaji na
sasa hivi vijana wako katika mtandao kwahiyo tutahakikisha tunatumia akaunti za
wasanii hawa kupitishia jumbe,” amesema Issango. Aidha Issango
amesema kupitia tamasha hilo wanatarajia kuwafikia vijana milioni 15 na
kutakuwa na utoaji wa elimu, ugawaji wa condom na vipeperushi vitakavyokuwa na
maelezo juu ya maambukizi hayo ambapo ametoa wito kwa wasanii wengine kufuata
mfano wa wasafi wa kutoa elimu juu ya maambikizi ya ukimwi. | 5 |
CHAMA cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) kimeibana serikali ya Afrika Kusini, kikiitaka iwalinde raia wa mataifa ya Afrika wanaoshambuliwa, kuuawa na kuharibiwa mali katika mashambulizi ya kibaguzi.Msimamo huo wa CPA ulitangazwa bungeni jana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alipozungumzia maazimio ya Mkutano wa Mabunge wanachama wa CPA uliomalizika Zanzibar hivi karibuni. Ndugai alisema wanachama na washiriki wa mkutano huo aliosema umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya washiriki kuliko miaka mingine, wamesaini azimio maalumu kuhusiana na msimamo wao huo.“Tumesaini andiko la pamoja lenye tamko ya kulaani na kupinga mauaji yanayofanyika Afrika Kusini yanayojulikana kama Xenophobia (Ubaguzi kwa wageni). Tumepinga vikali ukatili huu unaofanywa kwa Waafrika wenzetu. Tumewataka viongozi wa serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua za haraka za kuwalinda raia wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika,” alisema Ndugai. Alieleza kuwa jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa raia hao wa Afrika Kusini hawaui wazungu, wala wahindi au wageni wengine weupe bali walengwa ni waafrika.“yaani waafrika sasa tunauana wenyewe kwa wenyewe,” Alisema ukatili na unyama unaoendelea kufanywa na raia hao wa Afrika Kusini hauwezi kuachwa ukaendelea kuota mizizi na ndio sababu wabunge wa CPA wameamua kufikisha andiko lao kwa viongozi wa Afrika Kusini. | 1 |
KUTOKANA na kuongezeka kwa abiria katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kuanzia Jumatatu wiki ijayo, litaongeza safari za Dar es Salaam-Moshi kutoka nne kwa wiki (mbili kwenda na mbili kurudi) hadi sita.Hatua hiyo inatokana na mahitaji makubwa yaliopo tangu treni ya abiria irejee kufanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi Ijumaa Desemba 6, mwaka huu baada ya miaka 25 ya kusitishwa, ambapo kwa safari moja zaidi ya abiria 500 walisafiri.Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema jana kuwa mahitaji yameongezeka tangu kuanza kwa safari hizo, hasa kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka, hivyo wanaangalia namna ya kuongeza safari ili kukidhi mahitaji.“Mpangilio wetu tangu turejeshe safari za abiria ni kwenda Moshi mara mbili na Dar es Salaam mara mbili, inayofanya safari nne kwa wiki. Sasa tunataka iwe mara sita, ‘discussion’ (majadiliano) inaendelea hivi sasa,” alisema Kadogosa.Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRC, Focus Sahani alipoulizwa, alifafanua kuwa wanasubiri idhini ya mkurugenzi mkuu waongeze safari hizo Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kwa kuwa mahitaji yameongezeka na kufanya lazima ya ruti tatu kwenda na tatu kurudi kutoka mbili kwenda na mbili kurudi za awali.“Mahitaji yapo mpaka Kigoma na Mpanda katika sherehe hizi za mwisho wa mwaka. Lakini kwa hii ya kaskazini, tumepanga kuongeza ruti tatu badala mbili na mabehewa mawili kutoka tisa na tunasubiri idhini ya DG (mkurugenzi) malengo yetu ni kuanza next week (wiki ijayo) Jumatatu,” alisema Sahani.Sahani alifafanua kuwa ruti moja ya kulala inabeba abiria 72, na daraja la pili kukaa ni mabehewa mawili yanayobeba abiria 120 huku daraja la tatu likiwa na mabehewa matatu yanayobeba abiria 240 na kufanya idadi ya abiria 432.Alisema kuna behewa moja ambalo ni hoteli na baa. Hata hivyo, alisema abiria hupanda na kushuka njiani na abiria wa Moshi hawapendi kusongamana, hivyo abiria wengi hupenda kukaa na wachache wanaopanda njiani kwa safari fupi kama Pugu, Korogwe, Kidomole baadhi husimama na kufanya idadi kufikia kati ya 550 hadi 600 kwa ruti moja.Kuhusu mapato, Sahani alisema wanashirikiana na maofisa wa TRC wa Moshi na Dar es Salaam kuweka sawa hesabu. Aliahidi ataeleza mapato hayo tangu kuanza kwa safari leo.Alisema nauli ya kukaa ni Sh 16,500 ikilinganishwa na mabasi Sh 32,000 na daraja la kulala ni Sh 39,000 na daraja la tatu ni Sh 10,700. Usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, ulisitishwa mwaka 1994 na treni ya mizigo ya Dar es Salaam- Arusha ilisitishwa 2007 na kurejea Julai mwaka huu huku ya abiria ikirejeshwa Desemba 6, mwaka huu. | 1 |
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. | 0 |
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaponda wote waliokuwa mstari wa mbele kumshawishi Ramadhani Singano kuikacha timuhiyo na kuhamia Azam kufuatia mchezaji huyo kuwa kwenye orodha ya majina ya wachezaji wa Azam waliochwa msimu huu. Manara amesema Singano alishauriwa vibaya na kutoa onyo kwamba iwe funzo kwa vijana wadogo wanaonyanyukia kisoka ili kutengeneza mustakabli mzuri wa maisha yao ya baadaye. “Mguu wake wa kushoto ulikuwa kama kijiko,ni dribbler mzuri na ana akili nyingi but alishauriwa hovyo na wanaojiona wajuaji,matokeo yake leo Azam wanakwenda kumuacha (sio kosa lao).” “Iwe funzo kwa vijana wadogo wanaonyanyukia kisoka,hawa wajuaji sidhani hata kama wanajishughulisha nae tena!! Nikuombe dogo utulie naiamini miguu yako, soon utarejea ktk uwezo wako na cc klabuni tulishakusamehe kwa yale maneno uliolishwa utubeze na wajuvi feki,” ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Bado ni mchezaji mwenye akili nyingi, uwezo wake hasa wa kutumia mguu wa kushoto na maamuzi ya haraka, hivyo ni muda sahihi kutulia kabla ya kurejea kwenye ubora licha ya kuachwa na Azam FC,” amesema. Messi aliachana na Simba msimu wa mwaka 2014-15 na kujiunga na Azam FC ambapo usajili wake ulizua sintofahamu kutokana na mvutano uliokuwa baina ya mchezaji huyo na Simba, ikidaiwa kuwa bado alikuwa na mkataba na klabu hiyo. Maoni ya mashabiki na wadau mbalimbali | 2 |
NEW YORK, MAREKANI MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amesema mtoto wake, Royalty, amembadilisha kitabia na mfumo wake wa maisha kwa sasa. Awali msanii huyo alikuwa akitumia muda mwingi kufanya mambo yasiyo na maana kwa jamii na familia yake, lakini tangu alipoanza kumlea mtoto huyo amekuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yake. “Royalty amekuwa na mchango mkubwa wa kubadilisha maisha yangu, kutokana na hali hiyo ninatakiwa kumfanyia kila kitu ambacho anapaswa kufanyiwa. “Maisha yangu ya sasa yamekuwa ya kiutu uzima ila haya yote yanatokana na kuitwa baba,” alieleza Chris. Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Zero’, wiki iliyopita aliachia albamu yake mpya ‘Mix tap’ yenye wimbo alioshirikiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Rihanna. | 4 |
Derick Milton – Simiyu Meneja wa Wakala wa Mejengo ya Serikali (TBA), mkoani Simiyu Mhandisi Loishorwa Naunga amesema kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi majengo mawili ya upasuaji mkubwa mionzi na maabara katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo miezi miwili kabla ya muda wa mkataba wake ambao ni Oktoba mwaka huu. Akizungumza na Mtanzania leo Mei 23, Naunga mesema kuwa majengo hayo yanayojengwa kwa gharama za sh.Bilioni 3.5 ambapo mpaka sasa wamepokea kiasi cha sh. Bilioni 1.6 “Tunategemea kama serikali itatuletea kiasi cha pesa kilichobaki
tuna uhakika kuwa mwezi Agosti tutakamilisha ujenzi mzima kabla ya muda wa
mkataba, ” amesema. Mganga mafawidhi wa hospitali hiyo Dk. Matoke Muyenjwa amesema kuwa kasi
ya mkandarasi ni kubwa na wanategemea kukabidhiwa majengo mapema kabla ya muda
wa mkataba. Dk. Muyemjwa amesema kuwa katika jengo la maabara mkandarsi amekamilisha
ujenzi huku jengo la mionzi na upasuaji likiwa kwenye hatua za ukamilishwaji
wake. | 1 |
Mholanzi huyo amepoteza kazi saa chache baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na Uganda, The Cranes juzi katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN).Katika mechi hiyo ya kwanza ya kuwania kufuzu kwa fainali hizo za mwakani nchini Rwanda, Stars ilipoteza kwa kipigo hicho kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar mbele ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo ilikuwa na kikao chake cha kawaida saa chache kabla ya mechi hiyo iliyochezwa usiku.Saa chache baada ya mechi, TFF ilitoa taarifa ikieleza kuhusu kikao hicho na kwamba imeamua kusitisha ajira ya Mholanzi huyo aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuanzia Aprili mwaka jana.“Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo (jana) pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.“Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo; ajira ya Kocha Mkuu Mart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21 Juni, 2015,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa benchi lote la Ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia jana na punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa litatangazwa.Kabla ya mechi hiyo, baada ya kelele za wadau kuzidi, TFF ilimpa masharti kocha huyo kwa kueleza kuwa mechi dhidi ya Uganda ambayo marudio yatakuwa wiki mbili zijazo jijini Kampala, ilikuwa kipimo chake cha mwisho na akishindwa kuipeleka timu Rwanda 2016, atafukuzwa kazi.Hiyo ilitokana na Stars kupoteza mechi zote tatu za makundi za michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini ambako ilialikwa mwezi uliopita, na kipigo dhidi ya Misri katika kufuzu kwa Afcon 2017, kilifuatia matokeo hayo mabaya.Mechi ya juzi ilikuwa ya tano mfululizo kwa Nooij kupoteza na kufanya acheze mechi 18 tangu aajiriwe na kati ya hizo, ameshinda mechi tatu tu, akitoka sare saba na kupoteza mechi nane.Mholanzi huyo aliyezaliwa Julai 3, 1953 mjini Beverwijk, akiitwa Martinus Ignatius au maarufu kwa jina la Mart Nooij, aliwahi kuwa Mkufunzi wa Chama cha Soka cha Uholanzi, na amewahi kufanya kazi Marekani na Kazakhstan.Alikuwa kocha wa timu ya vijana ya Burkina Faso ya miaka 20 katika Kombe la Dunia mwaka 2003 kabla ya mwaka 2004 kuwa kocha msaidizi wa muda wa FC Volendam ya Uholanzi. Mwaka 2007, aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Msumbiji, na akiwa na timu hiyo ilifuzu kwa fainali za Afcon mwaka 2010 baada ya kuzikosa kwa miaka 12.Baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali za Afcon za 2012, Nooij alijiuzulu kazi hiyo Septemba 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani Gert Engels.Aprili 19, 2012, aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Santos, lakini akafukuzwa Desemba 18, mwaka huu.Novemba 2013, Nooij aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Saint George ya Ethiopia na miezi mitano baadaye, alikubali kuifundisha Tanzania kuanzia Aprili 25, 2014 akichukua nafasi ya Kim Poulsen wa Denmark.Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa anatajwa kuwa mrithi wa muda wa Nooij atakayeiongoza Stars katika mechi ya marudiano nchini Uganda, kabla ya kuteuliwa kwa kocha wa kudumu. | 2 |
WANANCHI wenye makazi na wanaofanya shughuli zao kwenye hifadhi za wanyama wilayani Songwe, wametakiwa kuhama kutoka maeneo hayo kwa kuwa si salama na yanahatarisha maisha yao kutokana na uwapo wa wanyama wakali. Kwa mujibu wa ofisa maliasili kata ya Kapalala, wilayani Songwe, Benard Nenje, kumekuwapo na matukio mengi ya wakazi wa maeneo yaliyo jirani na hifadhi kushambuliwa na wanyama sambamba na kuharibiwa mali zao ikiwamo mazao shambani.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Nenje alisema kwa mwaka jana pekee, wananchi 24 walipata madhara ya kuvamiwa na wanyama, ambapo kati yao 22 wanatokea kata ya Gua na wawili kata ya Ngwala ambao serikali ililazimika kuwalipa fidia kutokana na mazao yao kuliwa na tembo. Alisema kwa mwaka huu wananchi 30 wanatakiwa kulipwa fidia kutokana na tembo kula mazao yao na wengine kujeruhiwa na simba na fisi.Ofisa huyo alisema asilimia kubwa ya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi wanakuwa hawaelewi madhara yake hivyo kujikuta wakijenga makazi na kujishughulisha na kilimo bila kuujulisha uongozi wa kijiji pamoja na kata ili kupata utaratibu. “Watu hao wamekuwa wakijeruhiwa na wanyama wakali wakiwamo simba pamoja na mazao yao kuliwa na tembo jambo linaloigharimu serikali kuwalipa fidia kutokana na kosa walilofanya wenyewe,” alisema. | 1 |
VIONGOZI wa dini kwa pamoja na wadau mbalimbali katika ngazi tofauti tofauti jijini Dar es Salaam wamepewa elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola.Maeneo waliyojifunza ni namna ya kujikinga, kutoa taarifa na hata kutoa msaada kwa watakaokuwa wameathirika. Aidha chini ya utaratibu huo, wahudumu wa afya ngazi ya jamii, watapita nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya afya kwa ngazi ya jamii kuhusu athari za ugonjwa huo, ambao hadi sasa haujaingia nchini.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tafiti za Afya, mkoa wa Dar es Salaam na Msimamizi wa Uelimishaji wa Ugonjwa wa Ebola, Dk Ndeniria Swai alisema elimu hiyo kwa viongozi ni muhimu kwa sasa, muda ambao ugonjwa huo haujaingia nchini ili kuwa na utayari.Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na elimu hiyo kuratibiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu (Redcross) nchini.Akizungumza, Dk Ndeniria alisema mafunzo hayo yanalenga kufanya kazi kwa pamoja na kada mbalimbali ili kufikisha elimu kuhusu athari za ugonjwa wa ebola, namna ya kukabiliana nao pindi utakapotokea, ilikuepusha maambukizi kwa walio wengi.Shehe Seif Sadiki Muyenga kutoka Kigamboni, alisema elimu hiyo kwao ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na wao kama viongozi wa dini na wajumbe wa kamati ya amani ni lazima kulipokea hilo kwa mikono miwili na kulifanyia kazi .Muyenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Amani, mkoa wa Dar es Salaam, alisema mwili ukiumwa na akili ama nafsi lazima kukosa amani, hivyo baada ya kuelekezwa wataenda kuufanyia kazi kwa waumini na wengine wataendelea kupeleka taarifa hizo. | 1 |
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kupangwa kwa maeneo yote itakapopita Reli ya Kisasa (SGR), ili shughuli zitakazofanyika katika wilaya na vijiji inakopita reli hiyo kwenda sambamba na shughuli za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.Aidha, Lukuvi alisema wakati wa kupanga maeneo hayo, hakuna mwananchi yeyote atakayenyang’anywa eneo lake, bali maeneo hayo yatapangwa kimji na kuainishwa matumizi yake, kama vile ujenzi wa viwanda, mahoteli na maduka makubwa, hivyo kuwataka wananchiwanaotaka kufanya uendelezaji mdogo kusubiri mpango huo.Lukuvi alisema hayo jana katika vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Kibaha Mkoa wa Pwani, alipozungumza na wananchi wa maeneo hayo kuwaelezea mpango wa wizara yake kupanga na kupima maeneo yote inakopita SGR ili kuendana na fursa za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.“Wilaya na vijiji vyote reli ya SGR itapita ardhi yao itapangwa na wale wananchi walio kando ya reli itakapopita wasubiri wasiwe na wasiwasi ardhi ya maeneo yao itengenezewe mpango na muongozo kuhusiana na maeneo hayo utatolewa,” alisema Lukuvi.Alisema, lengo la serikali kupanga maeneo hayo ni kutaka mpango mzima wa uendelezaji ukanda wa kiuchumi katika maeneo hayo, ufahamike kitaifa na kimataifa ili kuvutia wawekezaji, watakaotaka kuja kuwekeza na kubainisha kuwa fedha kwa ajili ya mpango huo zishatengwa.Aliwatahadharisha wananchi wa vijiji hivyo kutokubali kuanza kuuza maeneo yao, kwa kuwa baada ya kupangwa kwa maeneo hayo thamani ya ardhi itapanda na tayari baadhi ya watu wajanja kutoka nje ya vijiji, hivyo washaanza kutafuta maeneo kwa ajili ya fursa hiyo.Alisema, si vyema kila wilaya ikawa na mpango wake wa uendelezaji maeneo itakapopita reli hiyo, bali serikali inachotaka ni kuwa na mpango wa kitaifa utakaotoa mwongozo kwa wilaya zote, kusisitiza kuwa ardhi katika maeneo hayo itasimamiwa na wilaya husika.“Tukiacha maeneo ya kandokando ya reli bila kupanga na kupima kutafanyika vitu vya ajabu, reli hii ina faida kubwa, hivyo lazima kupanga maeneo inakopita ili kwenda sambamba na shughuli za kiuchumi za maeneo hayo,” alisema Lukuvi.Kwa mujibu wa Lukuvi, kuna timu imeundwa kwa ajili ya Mpango wa Uendelezaji Ukanda wa Kiuchumi katika eneo inakopita reli ya SGR na timu hiyo inashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kama vile za nishati, uchukuzi, reli na mawasiliano, lengo likiwa kuwa na mpango utakaokidhi mahitaji ya uendelezaji ukanda kiuchumi katika eneo linakopita reli hiyo.Mapema akiwa katika eneo inapojengwa Bandari Kavu kijiji cha Kwala Kibaha Vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshana alimueleza Waziri Lukuvi kuwa wilaya yake ilipanga kuitumia fursa ya reli hiyo na Bandari Kavu katika eneo la Kwala kwa ujenzi wa hoteli, maduka makubwa (malls), nyumba za kupangisha (apartments) ili wale wote watakaoitumia bandari hiyo kutoka maeneo tofauti waweze kupata malazi.Akiwa katika Kijiji cha Soga, Lukuvi aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa, eneo lao lishapandishwa hadhi na kuwa mji, hivyo ujenzi holela hautaruhusiwa na hati miliki za ardhi zitakazotolewa eneo hilo ni miaka 99.Aliwataka wakazi wake kuitumia fursa ya reli ya SGR kujiendeleza kiuchumi. Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alimueleza Lukuvi kuwa kazi ya kuandaa mpango katika maeneo hayo, iende sambamba na uboreshaji miundo mbinu katika vijiji hivyo, ili kuwawezesha watu watakaoenda katika maeneo hayo, kutokumbana na changamoto kama vile barabara, maji na umeme. | 0 |
Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM KIUNGO wa zamani wa Simba, James Kotei, bado hajaisahau raha ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, baada ya kusema leo ataketi mahali tulivu kuufatilia ‘live’. Timu hizo zitaumana, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kuanzia saa 11 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kotei aliicheza Simba kwa mafanikio makubwa, akiisaidia kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, kabla ya kutimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kisha FC Slavia-Mozyr ya Belarus. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kotei alisema mchezo huo ni mkubwa hivyo ataungana na Wanasimba kuisapoti timu yake hiyo ya zamani. “Najua kama kesho ni mchezo wa ‘derby’ ya Kariakoo, nitaangalia mechi hii hapa hapa nilipo, nakumbuka shamrashamra zake, Simba Nguvu Moja. “Kitu kikubwa ninachokumbuka katika mchezo huu ni jinsi mashabiki wanavyoufanya mchezo huo kuwa na mvuto wa aina yake na ndicho kinanifanya niangalie,”alisema Kotei. | 2 |
Madini itaikaribisha Simba kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Machi 18 mwaka huu kucheza nayo mechi ya robo fainali.Akizungumza na gazeti hili kocha huyo wa timu hiyo ya ligi daraja la kwanza alisema timu yake inaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya mchezo huo.“Tutashinda kwani vijana wangu wapo katika kupambana na ninawashukuru mashabiki wa soka walivyojitokeza kutuunga mkono katika mechi dhidi ya JKT Ruvu tunawaomba wajitokeze tena kwani huo ndio uzalendo,” alisema Juma.Aidha, mashabiki wa soka mjini hapa wameeleza kufurahia ujio wa Simba kwenye mechi hiyo wakisema muda mrefu hawajaona timu kubwa mkoani mwao.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini hapa mashabiki hao walisema kuwa ujio wa Simba utavuta hisia za masabiki mbalimbali kutoka ndani na nje ya jiji.Mmoja wa mashabiki hao, Athuman Hassan alisema wakazi wa Arusha na vitongoji vyake hawajaiona timu kubwa kama Simba kwa takriban miaka saba sasa hivyo hiyo ni fursa adhimu kwao. “Imekuwa faraja kwetu kushuhudia tena Simba ikicheza kwenye uwanja huu, tunatarajia tutaona burudani safi siku hiyo,” alisema Hassan.Naye Elibarick Siyangi alisema mchezo huo utafanya mzunguko wa fedha kuongezeka Arusha kwani watu wengi watakwenda kuushuhudia.“Hii sasa ni changamoto kwa klabu zetu hasa vinazoshiriki ligi daraja pili na ligi daraja la kwanza ziache mazoea na zipambane zicheze Ligi Kuu,” alisema. | 2 |
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mwezi ujao na hivyo anatarajiwa kujiunga na timu hiyo kipindi hiki ambacho ligi imekwisha hadi msimu mpya ujao. Kocha wa muda wa Zimbabwe, Norman Mapeza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo huo wa Kundi G dhidi ya Liberia.Kumusoko anakuwa mchezaji pekee wa Zimbabwe aliyeitwa katika kikosi hicho cha taifa akiwaacha raia wenzake watano wanaocheza ligi ya Tanzania. Kikosi hicho ni makipa; Edmore Sibanda (CAPS United, Zimbabwe), Ariel Sibanda (Highlanders, Zimbabwe), Petros Mhari (FC Platinum) Mabeki: Denis Dauda (CAPS United, Zimbabwe), Partson Jaure, Qadr Amin (both Ngezi Platinum, Zimbabwe), Onesimo Bhasera (SuperSport United), Teenage Hadebe (Chicken Inn, Zimbabwe), Jameson Mukombwe (Black Rhinos, Zimbabwe), Erick Chipeta (Ajax Cape Town), Sydney Linyama (Black Rhinos).Viungo: Thabani Kamusoko (Yanga SC, Tanzania), Devon Chafa, Ronald Chitiyo (both CAPS United, Zimbabwe), Simon Shoko (FC Platinum, Zimbabwe), Kuda Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns), Marvelous Nakamba (Vittese Arnhem, Holland), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum, Zimbabwe), Ovidy Karuru (AmaZulu). Washambuliaji: Tendai Ndoro (Orlando Pirates), Evans Rusike (Maritzburg United), Knowledge Musona (KV Oostende) na Prince Dube (Highlanders, Zimbabwe). | 2 |
Anna Potinus Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka viongozi nchini kuachana na tabia
ya kujikweza mbele za watu na badala yake kuishi kama binadamu wa kawaida kwani
kwa kufanya hivyo hakuwapunguzii cheo walicho nacho. Amesema watanzania hatutakiwi kubaguana kwa dini wala kabila na kwamba
Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ukubwa aliokuwa nao kama rahisi alikuwa mtu wa
kawaida mbele ya watu wengine kwa namna alivyokuwa anahusiana na watu hali
iliyopelekea mtu akikaa naye hapati hofu ya kwamba amekaa na rais. Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza katika kongamano la
kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
lililofanyika jijini Dar es Salaam. “Ni jambo la muhimu viongozi kutambua kuwa kujishusha hakukufanyi usiwe
kiongozi wasababu una wakati wa kutimiza majukumu yako lakini unapokuwa na
binadamu wenzako wako kama wewe,”. “Orodha ni ndefu ya mambo ya mwalimu kwa sisi ambao tumebahatika kuwa
karibu naye ametuachia urithi wa mambo mengi muhimu katika nyanja zote za
maisha ya Watanzaniani sasa ni wajibu wetu kuutambua urithi huo na kuutunza, baadhi
ya mambo hayo yameshakuwa tunu za taifa na ndizo zinazolea taifa hili,”. “Watanzania wenzagu, wanachama
wenzangu wa CCM na vyama vingine vya siasa, wa rangi zote, makabila yote na
madhehebu yote ya dini tushikamane katika kusimamia tunu hii, amani na umoja hauna
kabila wala chama na mtu yeyote anayepuuza mambo haya haitakii mema nchi yetu
wala yeye mwenyewe,” amesema Dk. Kikwete. | 1 |
PARIS, UFARANSA MSHAMBULIAJI wa timu ya PSG, Neymar Jr, amefunguka na kusema kwa sasa ana
furaha na amani kuwa ndani ya kikosi hicho, hivyo yupo tayari kuipigania timu
hiyo. Mshambuliaji huyo raia wa nchini Brazil, kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili Septemba 2, alikuwa na lengo la kutaka kuondoka huku akihusishwa
kuwindwa na klabu yaka ya zamani Barcelona pamoja na mabingwa wa kihistoria wa
Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, lakini dili hilo lilishindikana. Kutokana na hali hiyo mashabiki wa PSG walikuwa wanamzomea mchezaji huyo mara
baada ya kurudi kikosini msimu huu, lakini aliweza kuwanyamazisha mashabiki hao
kwa kuifungia timu hiyo mabao manne kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu nchini
Ufaransa. Akizungumza na waandishi wa habari huko Rio nchini Brazil wakati wa
maandalizi wa mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Senegal, Neymar
alisema lengo lake kubwa kwa sasa ni kuisaidia PSG. “Kila mmoja ameona kilichotokea wakati wa soko la uhamisho majira haya ya
kiangazi, ukweli ni kwamba nilikuwa na lengo la kutaka kuondoka PSG. “Lakini baada ya kushindwa kuondoka bado nina furaha ya kuwa PSG, sisemi
haya kwa kuwa nipo na timu ya taifa, ila naongea hivyo nimeona msimu huu
umeanza vizuri kwangu, hivyo nipo tayari kuipigania kwa meno na kucha zangu. Nina
asilimia 100 ya kuwa na mafanikio makubwa msimu huu. “Kiangazi kilikuwa kirefu kwangu, lakini nilijiandaa kwa lolote, hivyo
ninamshukuru Mungu msimu umeanza vizuri kwangu, ninaamini hali hii itaendelea
hivi,” alisema Neymar. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alikuwa nje ya uwanja kwa miezi
mitatu katika msimu wa 2018-19 kutokana na kusumbuliwa na mguu. Hivyo anaamini
kwa sasa angekuwa bora zaidi endapo hasingepata majeraha hayo. | 2 |
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM WADAU mbalimbali wa mchezo wa soka nchini wameitaka Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutafakari upya vigezo wanavyotumia kumpata kocha sahihi wa kuifundisha timu ya soka ya Taifa. Hatua hiyo inatokana na matokeo mabaya ya timu ya Kilimanjaro Stars waliyopata katika michuano ya Kombe la Cecafa, yanayoendelea nchini Kenya. Kilimanjaro wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji, Kenya na kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi A, wakiwa na pointi moja katika mechi nne walizocheza, wakifungwa mechi tatu na kwenda suluhu mchezo mmoja, huku wakifunga mabao mawili pekee katika michezo yote. Wakizungumza kwa wakati tofauti na MTANZANIA jana, wadau hao walisema Kamati ya Ufundi iweke wazi vigezo vilivyotumika kumteua kocha wa timu, kutokana na ukakasi uliopo, kwa kile kilichotokea kwenye michuano ya Cecafa Kenya. Kocha wa zamani wa timu ya Mbeya City na Yanga, Juma Mwambusi, alisema wasiwasi wake upo kwa wahusika waliomteua kocha huyo ili kuifundisha timu ya taifa. “Mimi ni Mtanzania kama wengine, naumia nikiona hali hii kama ilivyo kwa wengine, TFF ndio wenye jukumu la kumteua kocha, ila sijui kama walitumia vigezo sahihi kumpata Ninje. “Timu ya taifa si ya kufanyia majaribio, hata kama alikuwa mchezaji wa zamani na alisomea ukocha je, anafahamu mazingira ya hapa nchini? Aliwahi kufundisha timu yoyote na alitambua utayari wa wachezaji aliokabidhiwa?” alihoji Mwambusi. Mchezaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay, alisema waliomteua Ninje kuwa kocha wa timu ya taifa walisahau mahitaji ya Watanzania. “Hatukwenda Kenya kujifunza, badala yake tulitaka kushinda taji kwa kuwa michuano ya Cecafa tunaimudu, tulifanya hivyo katika michuano ya mwaka 2010 na tulikuwa na uwezo wa kufanya tena mwaka huu, ndiyo maana kuna wachezaji wazoefu,” alisema Mayay. Kocha wa timu ya Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio‘, aliishauri Kamati ya Ufundi ya TFF kutojali zaidi vyeti, badala yake wajikite kwenye ubora wa kocha. “Kocha bora Tanzania kwa sasa ni Meck Maxime, lakini TFF hawakuliona hilo, wao wakavutiwa na kocha anayejua kuzungumza lugha ya Kiingereza. “Kwa hili TFF na kamati husika wanatakiwa wajitafakari upya na nitakwenda kumweleza Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi, bila kumwonea haya kwamba uteuzi wake haukuwa sahihi,” alisema Julio. Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime, alisema licha ya TFF kuwa na viongozi wanaofahamu mpira, wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa, kabla ya kuwapa makocha majukumu ya kitaifa. “Wahusika wanatakiwa kujifunza na kubadilika, makocha wanaofahamu mazingara ya hapa nyumbani wapo wengi, hao ndio waliotakiwa kutumiwa na si vinginevyo,” alisema Maxime. Kocha Ammy Ninje ana leseni ya ukocha daraja A la Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) na tayari ameshawaomba radhi Watanzania, akiahidi kutengeneza kikosi bora kitakachoshiriki michuano ijayo. Akizungumza baada ya kuondolewa katika michuano hiyo, Ninje alisema mpango wake ulikuwa kurudi na kombe hilo nchini, ila kutokana na matokeo hayo anarejea kujipanga upya michuano ijayo. “Tatizo lipo kwa wachezaji namna tulivyowalea, hawakuwa na kasi, ukiacha mchezo dhidi ya Zanzibar, iliyobaki yote tulicheza vizuri, ingawa hatukupata matokeo mazuri. “Tunaomba Watanzania watusamehe kwa kuwaangusha, kwani halikuwa lengo letu, tunawaomba waendelee kuisapoti timu yao na tunawaahidi kuboresha tulipokosea,” alisema Ninje. | 2 |
Yanga itakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) nusu fainali dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kutokana na mchezo huo muhimu, uongozi wa klabu hiyo uliamua kupeleka kikosi cha vijana kilichocheza dhidi ya Jeshi Kombaini na kutoka sare ya bao 1-1.Kitendo hicho cha kupeleka kikosi cha vijana kilimkasirisha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyetaka uongozi wa Yanga kwenda kutoa ufafanuzi, kwa nini haikupeleka kikosi cha kwanza kama walivyoahidi.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema juzi kuwa uamuzi wa kutopeleka kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo, ulikuwa ni kwa maslahi mapana ya Yanga katika kufanya vizuri michuano ijayo ikiwemo dhidi ya Mbao FC na ligi.Lakini pia, alisema kulikuwa na dosari kadhaa katika kufikia makubaliano ya ushiriki wa mechi hiyo hasa upande wa Yanga, upana wa kikosi, ukaribu wa mechi ya FA na kuwataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu hasa kipindi hicho cha mpito.“Niwaombe radhi wote waliosikitishwa na uamuzi huo japo una manufaa kwa klabu. Pia, naomba tushikamane tuwe kitu kimoja, kuelekea kutwaa makombe tunayoshiriki kwa sasa na kuendelea kuichangia Yanga,”alisema.Aidha, kikosi kilichowafuata Mbao ni Deogratius Munishi, Beno Kakolanya, Ally Barthez, Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Vicent Endrew, Said Juma, Kelvin Yondani, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko. Wengine ni Obrey Chirwa, Amis Tambwe, Geofrey Mwashiuya, Hassan Kessy, Emmanuel Martin, Juma | 2 |
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imewataka aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba, Hans Pope na mkurugenzi wa kampuni ya Ranky Infrastructure & Engineering, Franklin Lauwo, wajisalimishe wenyewe katika ofisi zao kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ya rushwa yanayowakabili. Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungu, amesema juhudi mbalimbali za kuwatafuta watu hao zimegonga mwamba hivyo wanatakiwa watii amri na kujisalimisha wao wenyewe. Naibu mkurugenzi huyo amesema Pope anatuhumiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuhusiana na malipo ya kodi. Kati ya Machi 10,2016 na Septemba 30, 2016, mshitakiwa huyo akishirikana na washitakiwa wenzake, Evans Aveva na Geofrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za TRA, kwamba klabu ya Simba imenunua nyasi bandia kutoka Ninah Guangzhou Trading Limited kwa thamani ya dola za kimarekani 40,577. “Ukweli ni kuwa nyasi hizo zilinunuliwa dola za kimarekani 109,499 lengo ikiwa ni kukwepa kulipa kodi ya mapato sahihi kwa TRA,” Ameeleza. Amesema kwa upande wa Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi na aliupata kwa njia ya rushwa kwa sababu hakuwa na sifa na sio mkandarasi ambae amesajiliwa na bodi ya makandarasi nchini. “Kati ya Machi na Septemba 2016, mshitakiwa alifanya kazi ya ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa klabu ya Simba uliopo Bunju, Kinondoni kwa thamani ya zaidi ya bilioni mbili wakati hajasajiliwa na bodi ya makandarasi, kisheria kufanya kazi hiyo,” amefafanua. Aidha Brigedia Mbungu ameongeza kwamba mtu yeyote atakayesaidia kutoa taarifa za ukweli zitakazosaidia kupatikana kwa washitakiwa hao atapewa zawadi nono. | 2 |
MKUTANO wa mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa unaanza leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, mkutano huo unawashirikisha mawaziri wa nchi 16 za SADC ukilenga kujadiliana namna bora ya kutekeleza sera, mikakati na programu zinazohusu sekta hizo.Programu moja wapo ni mpango wa kuongeza kasi ya mtandao wa intaneti kupunguza gharama za huduma za mtandao kwa kuunganisha watoa huduma za Tehama kwenda kwenye vituo vya kitaifa na kikanda (SADC Regional Internet Exchange points).Alisema maunganiko hayo yatawezesha mawasiliano ya intaneti yanayofanyika ndani ya nchi kubaki kwenye nchi husika wanachama wa SADC bila kwenda kwenye nchi nyingine na kupunguza umbali na gharama ya kusafirisha mawasiliano ya nchi husika.“Kwa upande wa Tanzania tayari tuna vituo sita vya maunganisho ya watoa huduma za intaneti yaani ‘Internet Exchange Point’,” alisema waziri huyo.Kwa mujibu wa waziri, maeneo yatakayojadiliwa katika mkutano huo unaotanguliwa na vikao vya wataalamu wa sekta hizo wa SADC ni pamoja na miundombinu ya mawasiliano, usalama wa mtandao, sera, utafiti katika sekta ya mawasiliano, masuala ya posta, habari na matumizi ya pamoja ya huduma za mawasiliano.Mengine ni sekta ya uchukuzi; hali ya hewa, usafiri wa anga, reli, barabara, bandari, ujenzi na kuhuisha sera, sheria na kanuni zioane kikanda; miundombinu ya mawasiliano na maunganisho yake na kutumia teknolojia ya kisasa kufanikisha utoaji wa huduma na usafirishaji wa bidhaa kwa kutumia biashara mtandao na ushirikiano wa kikanda.Kamwelwe alisema mkutano huo utaanza leo hadi Septemba 20 mwaka huu na pamoja na vikao vya wataalam pia Septemba 19 kutakuwa na Kongamano maalumu la Ubunifu na Teknolojia Zinazochipukia la mawaziri wa SADC wa sekta hizo pamoja na wadau wengine.“Vile vile nchi wanachama wa SADC waliandaa mwongozo wa sheria za mfano wa usalama wa mtandao.Madhumini ya kuwa na mwongozo huo ni kuhakikisha kuwa kila nchi inatunga na kusimamia utekelezaji wa sheria za usalama mtandaoni kwa kuwa masuala ya usalama wa mitandao hayatambui mipaka,” alisema Kamwelwe. | 1 |
Kavumbagu amekuwa na msimu mbaya chini ya kocha Stewart Hall, kiasi cha kumfanya kujutia maamuzi yake ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga.Akizungumza na gazeti hili, Kavumbagu raia wa Burundi, alisema benchi limemchosha na hayupo tayari kushawishika kuongeza mkataba kutokana na kuhofia kuua kiwango chake kwa kukaa benchi.“Nashukuru wachezaji wenzangu na uongozi mzima wa Azam kwa kipindi chote cha misimu miwili niliyochezea timu yao, kwa sasa mkataba wangu umekwisha na nimeona inatosha ni vyema nikasake changamoto sehemu nyingine nitakapopata nafasi ya kucheza na kuimarisha kiwango changu,” alisema Kavumbagu.Mshambuliaji huyo aliyeifungia Azam mabao msimu huu kwenye mechi za ligi, alisema hajajua ni timu gani ataichezea msimu ujao, lakini angependa kujiunga na timu kubwa za Yanga na Simba kama zitamuhitaji .Alisema amekuwa akivutiwa na timu hizo mbili nchini kutokana na namna zilivyo na ushindani mkubwa na mashabiki wengi ambao wanazipenda na alikuwa na wakati mzuri wakati akiichezea timu ya Yanga. | 2 |
WAZIRI wa Uwekezaji, Angellah Kairuki ameliambia Bunge kuwa mwaka ujao wa fedha nchi itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuvutia wawekezaji. Kairuki alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF).Katika swali la nyongeza mbunge huyo alisema nchi ina tatizo kubwa kwenye uboreshaji wa mazingira ya biashara kutokana na mfumo wa kodi uliopo na kuhoji ni lini serikali itaandaa mfumo rafiki wa kodi ulio wazi. Aidha, alisema kwa sasa Tanzania iko kwenye nafasi ya 144 ya uwezeshaji kibiashara lakini Rwanda ni nchi ndogo lakini iko kwneye nafasi nzuri ya 29 huku Kenya ikiwa nafasi ya 40 na kuhoji serikali haioni inapoteza wawekezaji kutokana na mfumo wa kodi usio rafiki.Akijibu swali hilo, Kairuki alimhakikishia mbunge huyo kuwa mwaka ujao wa fedha nchi itakuwa inafanya vizuri zaidi na hivyo wabunge na wawekezaji wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.“Lakini ukiangalia kwa sasa Juni hadi Julai mambo mengi yamefanywa na serikali na juzi tu nilikuwa na mkutano na Benki ya Dunia jijini Washington nchini Marekani na Dar es Salaam kuhakikisha tunawasilisha vilelezo vya kuonesha ni kwa namna gani kama nchi tumefanya maboresho mbalimbali na tumepiga hatua katika kuboresha viashiria 11 ambavyo vinatumika kupima wepesi wa kufanya baishara,” alisema Kairuki.Alisema katika mkutano huo aliongezewa muda wa kuwasilisha vilelezo vingine vya namna gani serikali imeboresha mazingira na mifumo ya biashara kwa wawekezaji na wafanyabiashara. “Maboresho tuliyofanya ni pamoja na kuanzisha biashara, taratibu za baishara mipakani hivyo niwatoe hofu watanzania na wabunge kila mmoja atimize nafasi yake ili kuona ni namna gani tunaboresha huduma hiyo na naamini ifikapo 2020/21 ripoti yetu na nafasi ya Tanzania tutafanya vizuri zaidi,” alisema.Awali akijibu swali hilo, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alimhakikishia mbunge huyo kuwa serikali imekuwa ikiweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi na ndio maana kwenye kila bunge wamekuwa wakipata matukio mbalimbali ya kodi ili kuendelea kuboresha mazingira yawe ya ushindani.“Nimhakikishie kuwa pamoja na changamoto zilizopo serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kodi na kumhakikishia kuwa mazingira ya biashara yataendelea kuboreshwa hivyo kuvutia wawekezaji,” alisema Ole Nasha. Katika swali la msingi, mbunge huyo alisema mazingira ya kufanya biashara nchini ni magumu kwa wafanyabiashara wa ndani na wa nje.Je, ni lini serikali itaondoa urasimu ili wananchi waweze kunufaika. Ole Nasha alisema serikali imekuwa ikibuni na kutekeleza mikakati na mipango mbalimbali kwa kuhakikisha uwepo wa mazingira bora ya ufanyaji biashara nchini. Alisema kwa mwaka 2017 serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ilifanya uchambuzi wa kina wa mazingira ya biashara nchini kwa sekta zote na kubaini changamoto mbalimbali zikiwemo mwingiliano wa sheria.Alibainisha kuwa kufuatia changamoto hizo serikali iliandaa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa mazingira ya biashara nchini ambao umeridhiwa na baraza la mawaziri kwa ajili ya utekelezaji. “Mpango huo utasaidia kuondoa muingiliano wa sheria na kupunguza urasimu kwa wafanyabiashara wakati wa kupata huduma katika taasisi mbalimbali za serikali. Mpango wa utekelezaji wa Blue Print umekamilika,”alisema. | 1 |
UWEZO wa madaktari wazalendo kufanya upasuji wa masikio yenye matatizo ya kusikia nchini umefi kia asilimia 90 huku uwezo wa kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia watoto waliopandikizwa vifaa kwa watoto waliozaliwa wakiwa hawasikii ukiongezeka na kufi kia asilimia 100.Daktari Bingwa wa Upasuaji Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila), Godlove Mfuko alisema hayo jana hospitalini hapo na kuongeza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, hospitali hiyo ilifanyia upasuaji watoto watatu huku wengine wawili wakiwashiwa vifaa vyao waweze kusikia sauti.Alisema jitihada za kuboresha sekta ya afya nchini, zimesaidia wataalam wazalendo kutoa huduma zao kwa ufanisi zaidi, vifaa na vifaatiba vikiimarishwa na kuongezwa. Dk Mfuko alisema tangu waanzishe huduma ya kuwekea watoto vifaa vya usikivu Juni 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), watoto 34 wamewekewa vifaa hivyo maalum vya kusaidia kusikia.Alisema kufanyika kwa huduma hizo nchini ni mwendelezo wa wataalam hao wazalendo kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuhakikisha wananchi wanafikiwa kwa urahisi na huduma za afya kule kule waliko.Alisema gharama za upasuaji mgonjwa au mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha masikioni kumsaidia kusikia ni Sh milioni 36 wakati akipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo hugharimu Sh milioni 80 hadi Sh milioni 100 mgonjwa mmoja. Alisema watoto wawili wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia MNH - Mloganzila na wamewashiwa vifaa hivyo waweze kusikia sauti mara ya kwanza tangu wazaliwe.Aidha, mtoto Uebert Kigala amerekebishiwa sauti kifaa alichopandikiziwa ili kumsaidia kusikia ikiwa ni mwendelezo wa wataalam kufuatilia maendeleo yake ili kuhakikisha kifaa kinafanya kazi kwa ufanisi.“Hawa watoto hawajawahi kusikia sauti tangu wazaliwe hivyo leo wataanza kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’ alisema Dk Mfuko. Dk Mfuko alitoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao kwa sababu asilimia 20 ya watu wenye tatizo la usikivu nchini ndio wanaoenda hospitali huku asilimia 80 wakidaiwa kubaki majumbani. | 1 |
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa ya wizi wa kompyuta katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Kanda ya Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema wamepokea taarifa hiyo Jumanne asubuhi (Oktoba 15, mwaka huu).Kamanda Mambosasa alisema mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa wizi huo ambao hata hivyo hakuwa tayari kutaja ni kompyuta ngapi zimeibwa. Alipopigiwa simu, DPP Biswalo Mganga kuhusu wizi huo, alisema yupo kwenye kikao na hajui atazungumza muda gani kwa sababu ana mambo mengi.Kutokana na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), haijajulikana kama kompyuta hizo zimewahi kuhifadhiwa kesi zinazoendelea katika mahakama mbalimbali. Tukio hilo la wizi limetokea ikiwa ofisi hiyo iko katika mchakato wa kujadiliana na kuingia makubaliano na washitakiwa mbalimbali wa kesi za uhujumu uchumi.Miongoni mwa kesi ambazo ziko katika hatua ya makubaliano ni kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili vigogo wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IndependentPower Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sethi na James Rugemalira wanaodaiwa kusababisha hasara na utakatishaji zaidi ya Sh bilioni 309.Washitakiwa wengine ambao wako kwenye makubaliano ni Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera anatuhumiwa kukwepa kodi na kutakatisha jumla ya Sh milioni 173 na mwingine ni Yusuf Ally maarufu ‘Mpemba wa Magufuli’ anayekabiliwa na mashitaka ya kusafirisha nyara za serikali zenye thamani zaidi ya Sh milioni 200.Miongoni mwa washitakiwa ambao tayari wameshahukumiwa kwa kutumia utaratibu huo wa makubaliano ni wafanyabiashara wawili ambao ni Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga ambao wameingiza serikalini Sh bilioni moja baada ya kukiri kufanya biashara ya upatu.Wengine ni mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiibia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mohamed Yusufali (39) Sh milioni saba kila dakika na wenzake kuingiza serikalini Sh 24,303,777,424.70 pamoja na kutaifisha nyumba nne zinazomilikiwa na Yusufali. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Arifal Paliwalla (44) na Sameer Khan (40) ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya I& M. Washitakiwa hao mpaka sasa wamelipa Sh 1,201,000,000.Pia yupo Mkurugenzi Mkuu wa Benki M (Tanzania), Sanjeev Kumar (63) ametakiwa kulipa fidia ya zaidi ya Sh bilioni sita ndani ya miezi 24 ambapo mpaka sasa tayari ameshalipa Sh milioni 690. Wengine ni vigogo sita wa Kampuni ya Six Telecom akiwamo Wakili maarufu, Dk Ringo Tenga ambao wametakiwa kulipa fidia ya Dola za Marekani 3,748,751.19 sawa na Sh bilioni nane na tayari wamelipa Dola za Marekani 150,000 pamoja na kutaifisha nyumba ya washitakiwa iliyopo Mikocheni.Mbali na Tenga, wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha, Kampuni ya Six Telecoms na Frank Mwalongo. | 1 |
*Mahakama Kuu Dar yatengua hukumu yake ya miezi sita baada ya kubaini hati ya mashtaka dhidi ya warufani, ilikuwa na upungufu
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam
MBUNGE wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema) aliyehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero kwenda jela miezi sita bila faini, ameachiwa huru na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa yake huku akiwa amekaa gerezani siku 79, ambazo ni takribani miezi mitatu.
Lijualikali (30) ambaye hukumu iliyompeleka jela ilitikisa nyanja za siasa na sekta ya sheria, aliachiwa huru jana baada ya mahakama kubaini hati ya mashtaka iliyomtia hatiani awali ilikuwa na upungufu mkubwa.
Mahakama hiyo ilimuachia huru jana baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na mrufani aliyewakilishwa na Wakili Tundu Lissu, Fred Kiwelo na Enock Edwin.
Mwingine aliyeachiwa pamoja na Lijualikali baada ya hukumu yake kutenguliwa ni Stephano Mgata (35) aliyepewa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi sita.
Lijualikali na mwenzake huyo, awali walitiwa hatiani kwa kosa la kufanya vurugu na kusababisha taharuki wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Ifakara.
Uamuzi wa kuwaachia huru warufani hao ulitolewa na Jaji Ama-Isario Munisi, baada ya kukubaliana na hoja za warufani kwamba hati ya mashtaka dhidi yao ilikuwa na upungufu mkubwa usioweza kurekebishika katika hatua ya rufaa.
“Ushahidi uliotolewa na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Kilombero haujitoshelezi kuweza kuwatia hatiani washtakiwa hao.
“Upungufu katika hati ya mashtaka ni mkubwa hivyo mahakama inatengua adhabu za vifungo walizopewa washtakiwa na inaamuru waachiwe huru,”alisema Jaji Munisi.
Awali Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilombero, Timothy Lyon, aliwatia hatiani Lijualikali na mwenzake na kuwapa adhabu walizokuwa wakizitumikia.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa Januari 11 mwaka huu, Hakimu Lyon, alisema Mahakama inawatia hatiani washtakiwa kwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Lijualikali alikuwa na kesi tatu huko nyuma ambazo alitiwa hatiani na kuhukumiwa, mahakama ilimuona ni mkosaji mzoefu hivyo kumuhukumu kwenda jela miezi sita.
Kesi ambazo mbunge huyo alitiwa hatiani na kuhukumiwa ni kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014.
Mshitakiwa wa pili
Mahakama hiyo ilimwona mshtakiwa wa pili Mgata kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza hivyo kumuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na ndani ya kipindi hicho hakutakiwa kutenda kosa lolote la jinai.
Adhabu hiyo ilipingwa, kupitia mawakili wao walikata rufaa ambayo ilisajiliwa na kupewa namba 60 ya mwaka 2017, wakipinga adhabu hiyo wakiwa na sababu tano ikiwemo hati ya mashtaka ina upungufu mkubwa ambao hauwezi kurekebishika.
Walidai hati hiyo ya mashtaka ilikuwa haiendani na maelezo ya kosa, hivyo washtakiwa walitiwa hatiani kwa kitu ambacho hakipo.
Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ambaye alipinga hoja hizo za rufani akidai hati ya mashtaka ilikuwa inakubalika kwa mujibu wa sheria na makosa yaliyoko yanarekebishika.
Alidai ushahidi uliotolewa Mahakama ya Kilombero ulijitosheleza kuwatia hatiani washtakiwa.
LISSU
Siku moja baada ya Lijualikali kuhukumiwa Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, alisema hukumu hiyo inatokana na vita vya kisiasa kati ya Chadema na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Lijualikali na Lema (Godbless-Arusha Mjini) kwa sasa yuko nje kwa dhamana baada ya kukaa mahabusu miezi mitatu kutokana na kunyimwa dhamana akituhumiwa kutoa lugha ya uchochezi, wote hawa ni wafungwa wa kisiasa.
“Adhabu ya kifungo bila faini imetolewa kwa sababu za kisiasa. Kwanza walimshitaki mara mbili, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu ili wamfunge na asiweze kuendelea na kampeni. Haikuwezekana kumfunga na alishinda ubunge.
“Baadaye walimfungulia kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu ambako nako tuliwashinda vibaya. Wamekata rufaa Mahakama ya Rufani ya Tanzania nako tutawashinda na wanajua hivyo,” alisema Lissu.
Alisema waliamua kumfunga mbunge huyo bila faini wakiamini kuwa uamuzi huo utamfanya akose sifa za kuwa mbunge.
Huku akinukuu Ibara ya 67 (2) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Lissu alisema adhabu hiyo haina athari yoyote, kwa maelezo kuwa mtu anakosa sifa za kuwa mbunge iwapo atafungwa gerezani zaidi ya miezi sita.
“Si kifungo tu cha miezi sita, pia lazima awe amekutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
“Adhabu ya kifungo aliyopewa Lijualikali haijazidi miezi sita. Pia kosa la kumpiga askari polisi, hata kama lingekuwa la kweli si kosa la utovu wa uaminifu,” alisema. | 1 |
Mwandishi Wetu -Singida BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 katika wilaya kadhaa nchini. Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanya biashara humu nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu, inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama wa raia. Benki ya NMB imeshatoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mikoa ya Kanda ya Kati. Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani ingida, Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ya zaidi ya Sh milioni 200 iliyotolewa imelenga sekta ya elimu, afya na majanga kwa mikoa mitatu ya Kanda ya kati. Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewa na NMB zimetumika kununua madawati, viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya. Aidha, alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali. Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule, zahanati, hospitali katika mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara. Pia NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 29.5 kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo. Katika hatua nyingine, Benki hiyo imevipatia kituo cha Polisi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati 160 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa ajili ya kuezekea maboma. NMB iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wa kuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini, Meneja wa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus, alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi ya maendeleo. Baraka alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepa tamabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati 80. | 0 |
DERICK MILTON NA SAMWEL MWANGA, ITILIMA SERIKALI imeanza
ujenzi wa hospitali mpya ya kisasa katika eneo la kijiji cha Nguno katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi
ya kutembea
umbali mrefu kutafuta huduma za afya. Akizungumza kwenye ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo uliofanywa
wilayani humo baada ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru, Mganga Mfawidhi, Anorld Musiba
amesema zoezi hilo litasaidia kupunguza changamoto wanazopitia wananchi hao.
“Mwaka jana vimetokea vifo vya watu watano, mwaka huu mpaka sasa
vimetokea vifo vya watu wawili na vyote ni akina mama wajawazito, serikali
imeamua kujenga hospitali wilayani hapa ambapo ujenzi wake unaendelea na
utakamilika Juni 30, mwaka huu. “Ujenzi huu utahusisha majengo saba na utagharimu kiasi cha
shilingi bilioni 1.5, hadi sasa gharama
zilizotumika ni shilingi bilioni 2.1 sawa na asilimia 81 ya
utekelezaji, tunategemea ujenzi huu utasaidia kumaliza vifo vya kina mama
wajawazito na tunatarajia hospitali hii itahudumia wananchi zaidi ya 300,000. Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge, Mkongea Ali amesema
ameridhishwa na ujenzi huo na ametaka kuongezwa
kwa kasi ya ujenzi huo kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha. Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo walishukuru serikali kwa
kuwaletea hospitali ambapo wameomba kuharakishwa kwa ujenzi wake ili kuanza
kupata huduma mapema. “Tulikuwa tunateseka sana kwenda Bariadi, ukiangalia huku ni
vijijini na miundombinu ya barabara ni mibovu tumekuwa tukitumia muda mrefu
kupata matibabu,” amesema Janeth Saguda. | 1 |
Tayari Yanga ilitua Mbeya kwa ndege kwa ajili ya pambano hilo la kuthibitisha ubingwa baada ya juzi Yanga kutoshuka dimbani licha ya kupewa ubingwa baada ya Simba kulambwa 1-0 na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa.Baada ya kipigo hicho cha Simba na ushindi wa Azam FC wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba ilishushwa katika nafasi ya pili na kuangukia ya tatu.Tayari Yanga imeshacheza michezo 27 na kufikisha pointi 68 ikiwa na michezo mitatu mkononi ambazo kama Simba itacheza michezo mitatu iliyobaki bado haitamfikia kwa kuwa itafikisha pointi 67 na Azam FC ikimaliza michezo miwili iliyobakiza itafikisha pointi 66.Pia, inakutana na Mbeya City ambayo hata ikishinda haina nafasi tena ya kuchukua ubingwa wala ikipoteza haitaweza kushuka daraja, kwani ina pointi 33 na inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi. Iwapo itashinda mchezo wa leo na miwili iliyobaki itaendelea kujitengenezea rekodi yake ya kipekee kwa kufikisha pointi 71 na zaidi.Hata ikipoteza michezo yote iliyobaki haina hasara yoyote kwa kuwa wameshatetea ubingwa wao. Kikosi cha Kocha Mkuu Hans Pluijm baada ya mchezo huo wa Mbeya, Mei 14 kitasafiri hadi Mtwara ambako watacheza na Ndanda ambako pia watakabidhiwa mwali wao.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, Yanga ilitangaza ubingwa juzi jioni baada ya Simba kupoteza mchezo wake dhidi ya Mwadui, muda ambao haukutosha kwa maandalizi ya kutawazwa sherehe za kukabidhiwa kombe. Alisema kuwa Yanga itakabidhiwa ubingwa huo katika mchezo dhidi ya Ndanda FC mwishoni mwa wiki hii. | 2 |
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu. | 0 |
Na JUSTIN DAMIAN,
SHIRIKA la Maendeleo la Ufaransa (AFD), lipo katika majadiliano yatakayoiwezesha Serikali kupata mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 65 (zaidi ya Sh bilioni 150) kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini, Emmanuel Baudran, aliliambia MTANZANIA katika kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa linaloendelea jijini Dar es Salaam, kuwa mkopo huo unalenga kuboresha uwanja huo – terminal 2, ili uweze kuendana na ongezeko la abiria.
Baudran alisema majadiliano hayo yapo katika hatua nzuri na kuongeza kuwa mkataba wa mkopo huo unaweza kusainiwa mwezi ujao.
“Tunaamini kuwa usafiri wa anga ni kichocheo muhimu cha maendeleo na Tanzania imekuwa ikipokea watalii wengi. Biashara kati ya mkoa mmoja na mwingine zinakua pia na kwa kuwa nia yetu ni kusaidia sekta zenye mchango kwa maendeleo, tunaona eneo hili ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,” alisema Baudran.
Alisema shirika hilo lipo katika majadiliano na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo wa masharti nafuu kukarabati viwanja vingine vya ndege vilivyopo katika mikoa mbalimbali.
“Tanzania ina viwanja vya ndege zaidi ya 15, ikiwa ni pamoja na vikubwa na vidogo. Baadhi ya viwanja hivi havipo katika hali nzuri na AFD ipo tayari kusaidia ukarabati wake,” alisema.
Alisema katika mpango wa ukarabati wa viwanja 11 vya ndege ambao Serikali inao, shirika hilo lipo tayari kufadhili baadhi ya viwanja ambavyo Serikali itatoa kipaumbele na kutaka fedha kwa ukarabati na upanuzi. | 1 |
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kwamba ameshitushwa na uwezo wa nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, aliouonesha juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, ambapo alipachika mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-2. Kutokana na kiwango hicho, Wenger amedai kwamba hakutarajia kuona uwezo mkubwa ambao aliuonesha mchezaji huyo. “Kwa upande wetu, tulishindwa kuwa na mipango mizuri ya kutafuta mabao kutokana na nafasi ambazo tulizipata, lakini katika mchezo huo nilikuja kushangazwa na uwezo wa nyota mpya wa Man United, Rashford. “Nadhani haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa kila mmoja kushangazwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili, alikuwa na akili ya kwenda na mchezo na kujua wapi sehemu sahihi ya kukaa. “Ninaamini atakuja kuwa na uwezo wa hali ya juu endapo ataendelea na aina ya mchezo ambao anacheza na kama hatalewa sifa,” alisema Wenger. Nyota huyo alianza kuonesha uwezo wake wa kupachika mabao katika mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Midtjylland, ambapo katika mchezo huo alifanikiwa kupachika mabao mawili. | 2 |
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda pamoja na timu nzima ya Wizara ya Kilimo, wamefanya ziara kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kufuatilia sakata la ununuzi wa korosho.Viongozi hao walioapishwa juzi Ikulu Dar es Salaam na Rais John Magufuli, walilazimika kusafiri juzi usiku hadi kwenye mikoa hiyo ili kuhakikisha agizo lilitolewa na Rais kuhusu serikali kununua korosho zote linatekelezwa.Wakizungumza kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1) jana mchana, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa alisema ziara yao hiyo imewapa fursa ya kujiridhisha kiwango cha korosho kilichopo, zipo kwenye hali gani pamoja na kuona kama kuna ziada pia.Bashungwa alisema uamuzi wa serikali wa kununua korosho hizo umeungwa mkono na kufurahiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa mikoa hiyo ya kusini.“Serikali ya Rais Magufuli inataka kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.Kiwanda hiki cha kubangua korosho cha BUCCO kilikuwa kimefungwa, lakini baada ya kauli ya Rais, kimefunguliwa,” alieleza Naibu Waziri Bashungwa. Kwa upande wake, Waziri Kakunda aliwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi na kuvitaka viwanda vinavyochakata mazao ya wananchi kuzingatia hilo.Alisema uamuzi wa Rais Magufuli kukikabidhi kiwanda cha BUCCO kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni kwa sababu wanajeshi ni wazalendo, waadilifu na waaminifu. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alisema mpaka jana jumla ya tani 4,453 za korosho zilikuwa zimeshapokewa kwenye maghala.Zambi alisema kazi ambayo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepewa na serikali ni kulinda maghala ya korosho, kusafirisha korosho hizo kutoka kituo kimoja hadi kingine, na kuendesha kiwanda hicho.“JWTZ hawanunui korosho, kazi ya kununua korosho inafanywa na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kupitia vyama vikuu vya ushirika, na vyama hivyo vya ushirika ndivyo vinavyowalipa wakulima,” alieleza Zambi.Wataalamu wa uchumi na biashara, walisema kushindwa kwa wanunuzi binafsi kununua korosho kwa bei elekezi ya serikali, ni kutokana na kubadilika kwa bei katika soko la kimataifa.Mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Razack Lokina alisema serikali siyo tu ina uwezo wa kununua kwa bei iliyoipanga, lakini pia ina uwezo wa kuzihifadhi korosho hizo na kuziuza wakati wowote ambapo bei ya soko iko vizuri. Profesa Lokina alisema uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa unamlinda mkulima asipate hasara.Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Mchungaji Silver Kiondo, alisema mkulima anapaswa kulindwa na uamuzi huo wa serikali wa kuzinunua korosho hizo ni sahihi.Mchungaji Kiondo alisema kwa kuwa haieleweki sababu iliyowafanya wanunuzi hao kushindwa kununua korosho hizo, ni vyema ukafanyika utafiti ili kujua sababu iliyowafanya washindwe kuzinunua kwa bei elekezi ya serikali. | 1 |
NA GEORGE KAYALA MWIMBAJI chipukizi katika muziki wa Injili nchini, Mary Msigwa, amelalamikia wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kutowathamini, vyombo vya habari na wadau wa muziki huo pindi wanapotaka msaada kwa ajili ya kukuza muziki wao. Msigwa alilalama kwamba nyimbo za wasanii chipukizi hazipewi nafasi ya kuchezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila sababu za msingi. Mary alisema changamoto nyingine zinazowakabili waimbaji wachanga ni kukosa fedha kwa ajili ya kurekodia, kushindwa kujitangaza kiasi kwamba wanashindwa kutambulika kwa jamii. “Wasanii chipukizi hatuthaminiwi na hii imesababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kuendelea na huduma hii kwani hata kama ukifanikiwa kurekodi kwa kujibana shida inakuwa kwa watangazaji wa redio na televisheni ambao huwa hawazipi nafasi nyimbo zetu na hii inasababisha tushindwe kufahamika kwenye jamii,” alisema mwimbaji huyo. | 4 |
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM), amesema anakusudia kuwasilisha muswada binafsi bungeni utakaoweka sharti la kurejewa mjadala wa Katiba Mpya. Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema muswada huo atauwasilisha katika kikao cha tisa cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Novemba 7 mwaka huu mjini Dodoma. Alisema Katiba ya nchi ni mkataba wa wananchi ambao utadumu kwa miaka mingi hivyo hautakiwi kufanywa kama dharura au kuogopwa bali unahitaji umakini. “Mchakato ulianza ukatumia fedha nyingi na kuhusisha watu wengi lakini haukukamilika, na hapa katikati ulighubikwa na sintofahamu nyingi. “Na kwa namna yoyote ile ili tuweze kuwa na Katiba bora itakayohusisha wadau wote kwa maana ya wananchi, viongozi wa vyama vya siasa na upande wa serikali itakuwa ni muhimu mchakato uanze kwa kuzingatia rasimu ya katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba,” alisema Nyalandu. Alisema anatarajia kuwa wabunge wa chama chake na wabunge wa upinzani watamuunga mkono hoja hiyo iweze kurudi upya na wadau wote wapate fursa ya kujadili ipatikane Katiba Mpya. “Wabunge tuna nafasi yetu ya kujadili na kupeleka maoni ya binafsi na yale ya pamoja. “Katiba imempa nafasi mbunge mmoja mmoja bila kujali ametoka chama gani, hivyo mimi naona ni hoja ambayo ni lazima ipate nafasi kama hoja nyingine na kufanyiwa kazi. MATOKEO YA TWAWEZA Wakati huohuo, Taasisi ya Twaweza jana ilitangaza matokeo ya utafiti ambayo yanaonyesha Watanzania wawili kati ya watatu wanahitaji Katiba Mpya. Utafiti huo uliopewa jina la ‘Zege Imelala’ ulilenga kupata maoni ya wananchi kuhusu kukwama kwa mchakato wa kuunda Katiba Mpya. Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema ulifanyika kati ya Juni hadi Julai mwaka huu na kuhusisha watu 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara. “Asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata katiba mpya na nusu ya wananchi wanasema mchakato wa katiba uanze upya na tume mpya,” alisema Eyakuze. Kulingana na utafiti huo, asilimia 49 ya wananchi wanafahamu juu ya mchakato wa kukusanya maoni uliofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba na asilimia 21 wanafahamu kuwa vipengele vya rasimu ya Warioba viliondolewa na Bunge Maalumu la Katiba kupitia Katiba Inayopendekezwa. “Wananchi hawakubaliani na mabadiliko mengi yaliyofanywa na BMK chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba Mpya, Andrew Chenge,” alisema. POLEPOLE Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, alikiri kuwa inahitajika Katiba Mpya lakini kwa sasa wameamua kushughulikia kwanza shida za wananchi. “CCM inaamini katika utafiti kama nyenzo ya kutuarifu juu ya yale tunayoyatenda. Hata mimi na serikali ya CCM inataka Katiba, lakini kwa sasa tumeamua kushughulika na shida za watu suala la katiba litakuja baadaye. “Tuna miaka mitano kupanga ni kuchagua, mageuzi ya katiba yatafanyika pale ambapo tumefanikiwa kufanya mageuzi ya taasisi za siasa, jamii na serikali…itaandikwa pale ambako nidhamu ya viongozi na watumishi itakuwa imenyooka,” alisema Polepole. Alisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa BMK lakini walikwama kwa sababu kulikuwa na masilahi binafsi ya viongozi wa vyama vyote ambao walishindwa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya nini Watanzania wanataka na muafaka na maridhiano pia havikuwapo. ACT WAZALENDO Katibu wa Itkiadi na Uenezi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, alisema katiba mpya bado ni kipaumbele cha Watanzania na kuinyoosha nchi bila katiba ni kazi bure. ASASI ZA KIRAIA Mwakilishi wa Asasi za Raia, Deogratias Bwire, alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kumshauri Rais Dk. John Magufuli aupe kipaumbele mchakato wa Katiba Mpya. “Serikali inafanya mambo mengi mazuri kama vile ya kulinda rasilimali za nchi je, haya yote yanalindwa kwenye nyaraka gani. “Tunapotaka kunyanyua maisha ya mtu mnyonge halafu mwisho wa siku hakuna sehemu anapoweza kwenda kuidai haki yake tunakuwa tunamdanganya,” alisema Bwire. CHADEMA Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu, aliishauri Serikali isikilize maoni ya wananchi. | 1 |
NA JOSEPH SHALUWA NI mrefu, mwenye ngozi yenye rangi ya dhahabu. Ana macho meupe, pua fupi, midomo minene iliyofunika meno yaliyopangika vyema kinywani na kutengeneza mwanya mdogo wa kichokozi katikati. Sauti yake nyembamba ni kivutio kingine, shingo ndefu kama ya twiga ni kati ya sifa zinazomuacha kwenye orodha ya warembo wa Tanzania wenye mvuto kwa mwaka wa kumi sasa. Usisahau kwamba mwaka 2013 alishinda Tuzo ya Msichana Mwenye Mvuto Zaidi (Sexiest Girl Award) ya gazeti moja la wiki nchini akiwamwaga washiriki wenzake waliongia fainali, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Nelly Kamwelu, Jacqueline Wolper na Jokate Mwegelo. Wema Isaac Sepetu ni kati ya warembo wachache nchini kutokea Miss Tanzania wenye kismati cha aina yake. Wamepita warembo wengi sana tangu yalipoanzishwa mashindano hayo mwaka 1994, lakini wengi wameshapotea kwenye ramani. Achana na walioshinda nyuma yake, tangu aliposhinda Wema mwaka 2006, warembo wengine takribani wanane waliomfuata, wengi wamesahaulika kabisa. Nitakukumbusha mwishoni. Ni rahisi kusema mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa bahati kwa washiriki na hasa wale walioshinda nafasi za juu. Kati ya warembo watano waliongia Tano Bora, wanne mpaka sasa wanaendelea kutesa kwenye sanaa mbalimbali. Nyuma ya Wema kuna Jokate Mwegelo ambaye ni modo, mwigizaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lisa Jensen – mwanamitindo na mwigizaji na Irene Uwoya aliyechukua namba 5 akitesa kwenye filamu za Kibongo.
Pamoja na kwamba warembo wote wanne kutokea Miss Tanzania 2006 wapo kwenye game, Wema anaonekana kukubalika zaidi na mashabiki. Hiyo ni nyota ya ajabu kwa mlimbwende huyu. Kwa lugha nyepesi, naweza nikasema Wema ni brand – bidhaa. Ni taasisi kubwa ambayo inaweza kutengeneza fedha nyingi. Wema ni utajiri. Kupitia kipaji chake, anaweza kupata fedha nyingi mbali na umaarufu ambao pengine unamsaidia mambo mengi. Nimesukumwa kuandika makala haya ili kumuibua usingizini na kama alikuwa analitambua hili, basi ajue kuwa wapo wanaliona hilo kwa jicho pana, hivyo ingekuwa bora na faida kwake kama akianza haraka mapema ili kutengeneza umilionea. MVUTO WA WEMA Kama unabisha kuwa Wema siyo brand, hakubaliki na hana kismati, fanya uchunguzi mwepesi ambao utakupa majibu ya haraka. Andika chochote kuhusu Wema mtandaoni ukimsema vibaya, uone kazi ya mashabiki!
Wema hana sababu ya kujibu chochote. Hata ukimchafua kwa staili gani, wapo mashabiki zake huko, watasimama kwa ajili yake. Wema anapendwa, anakubalika.
Kingine kinachomsaidia kukubalika na kupendwa ni namna anavyoguswa na mambo mbalimbali ya kijamii. Amewasaidia wengi wakiwemo mastaa. Kajala Masanja ni miongoni mwao.
Wakati akiwa kwenye sakata la kwenda jela au alipe faini, ni Wema ndiye aliyotoa Shilingi milioni 13 kumsaidia kurejea uraiani na kupishana na mateso ya nyuma ya nondo. Wema hachafuki! NINI KIMEMPATA WEMA? Wakati anaanza alijitahidi kuonyesha nia ya kusaka mafanikio, lakini kwa sasa spidi yake imepungua. Wema alikuwa na kasi ya kucheza sinema. Alikuwa miongoni mwa wasanii wa kike wanaolipwa ghali zaidi.
Katika kundi hilo walikuwemo Aunt Ezekiel, Rose Ndauka, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Shamsa Ford. Mwaka 2013, Wema alifungua kampuni yake ya utayarishaji filamu, Endeless Fame Films. Lilikuwa wazo zuri la kibiashara.
Lakini wazo hilo hakulitendea haki, kwani mwaka mmoja baadaye alifunga ofisi hiyo. Nini kimetokea? Wema anapaswa kujitazama upya na kuangalia namna ya kusimama tena. Mtaji bado anao – ni jina lake tu. MANAGEMENT ZAIDI Wema anaweza kutengeneza fedha zaidi kama akiwa na uongozi imara zaidi. Haina maana kwamba, Martin Kadinda siyo meneja mzuri, la hasha! Kadinda ni kijana mjanja, mchakarikaji na mbunifu.
Ndiye aliyeharakisha na kushughulikia wazo la bidhaa ya lipstick yenye jina la Kiss by Wema Sepetu. Duka linalouza bidhaa hizo lipo Mwenge jijini Dar es Salaam. Hongera sana Kadinda.
Lakini tukiangalia mafanikio ya mastaa wengi, si ya kutegemea meneja mmoja. Unaweza kuwa na mmoja anayesimamia jumla, lakini wengine wawili au watatu wakawa wa kubuni idea zaidi za biashara na kutoa ushauri.
Sipati picha, ikiwa watu kama Ruge Mutahaba, Said Fella au Babu Tale wangekuwa kwenye crew ya management ya Wema ingekuwaje! Naamini tungekuwa tunamwongelea Wema mwingine.
Si dhambi kuwa na meneja zaidi ya mmoja. Mwangalie Diamond anavyotusua kimafanikio, ni kwa sababu amezungukwa na mameneja wanaoshindana kuumiza vichwa kubuni mawazo ya biashara ya kumpaisha zaidi na zaidi.
Hata Wema pia anaweza kutumia mbinu hiyo ili kutumia jina lake kujiweka pazuri kimafanikio. Kama kuna mtu amepata kumwambia kuwa eti jina lake limeanza kuchuja, anamdaganya sana. Muda bado unao Wema. Ni wewe tu. | 4 |
Na
MWANDISHI WETU SELIMUNDU (sickle cell) ni ugonjwa wa kurithi ambao hutokea
baada ya mwili wa binadamu kuwa na upungufu katika umbile la seli, ambapo
hubadilika na kuwa nusu duara au umbile la mundu (zana ya mkulima) badala ya
mduara. Hali hii ya umbile la seli kufanana na mundu, ndio
iliyosababisha iitwe iitwe selimundu au kwa jina la kitaalamu sickle cell. Ni ugonjwa unaorithishana vizazi kwa vizazi, lakini endapo mzazi
mmoja tu akiwa na vinasaba vya ugonjwa huu basi huwa ni vigumu kusababisha
mtoto kuvipata, bali endapo wazazi wote wawili ikitokea wana vinasaba hivyo. Kwa Afrika, Nigeria ni nchi ya kwanza kuwa na idadi kubwa ya
watoto wanaozaliwa na selimundu huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu, ambapo
kila mwaka watoto takribani 11,000 huzaliwa na matatizo hayo. Kutokana na kuongezeka kwa tatizo hilo, wataalam kutoka Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) wameamua kufanya utafiti na
kutafuta njia ya kuutibu ikiwa ni pamoja na kupandikiza uboho (born marrow) na
vinasaba kwenye mifupa. Kwa kawaida, chembe nyekundu ya damu ni
mviringo, husafiri kupitia mishipa midogo kabisa ya damu kwa urahisi na kwa
wagonjwa wenye selimundu, chembe zao za damu huvunjika na kupoteza umbo
hilo la mviringo na kuchukua umbo la ndizi au mundu. Chembe hizo nyekundu za damu zenye umbo la
mundu hukwama katika mishipa midogo ya damu mwilini na mtiririko wa damu kwenda
sehemu fulani ya mwili unapopungua huku hewa safi ya oksijeni ikizuiwa na
kusababisha maumivu makali ya ghafla. Kutokana na hali hiyo, husababisha maumivu
makali katika mifupa na vifundo, maumivu yasiyotabirika ambayo yanaweza kutokea
mara chache au mara nyingi kama kila mwezi kwa mgonjwa mwenye matatizo hayo. Dalili Dalili ya kwanza huanza kuonekana kwa mtoto pindi anapotimiza umri wa miezi
sita tangu kuzaliwa kwake. Huanza kuugua mara kwa mara, kuvimba miguu, kuishiwa damu pamoja
na ubongo wake kushindwa kukua ipasavyo. Hali hiyo inapotokea, mzazi anashauriwa kumpeleka hospitalini
ili aweze kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema ili kupunguza ukubwa wa
tatizo. Daktari Akizungumzia ugonjwa huo, Daktari wa Watoto kutoka Hospitali ya
Rufaa ya Mloganzila, Moses Karashani, anasema sasa hivi kuna ongezeko la rufaa
kwa watoto wanaougua selimundu. Anasema watoto hao ni wale wenye umri kuanzia miezi sita hadi
miaka 14 ambapo kati yao nusu ni wale walio chini ya miaka minane. Anasema mara baada ya kuonekana kwa dalili zilizopo hapo juu,
mtoto anapaswa kufikishwa hospitali mapema ili aweze kupata huduma za matibabu
kwa haraka. “Mtoto ambaye wazazi wake wote wawili (baba na mama) wana
vinasaba vya selimundu, kuna uwezekano wa asilimia 25 kupata ugonjwa huo na
mtoto ambaye mzazi mmoja hana vinasaba hivyo hawezi kurithi,” anasema Dk. Karashani. Anaongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, walimua kuanzisha kliniki ya watoto wanaosumbuliwa
na ugonjwa huo siku ya Jumanne na Alhamisi hospitalini hapo ili waweze kupata
huduma bora za matibabu. Anasema watoto waliopewa rufaa kutoka hospitali mbalimbali
nchini zikiwamo za Mkoa wa Dar es Salaam, wanafikishwa hospitalini hapo kwa
ajili ya kupatiwa huduma za matibabu. Anasema pia wamekuwa wakipokea watoto wenye ugonjwa huo kutoka majumbani,
jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa. Anasema katika siku hiyo, zaidi ya watoto 20 wanafika hospitalini
hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu kuanzia umri wa miezi sita hadi
miaka 14, ambapo kati yao, nusu yake ni wale wenye umri chini ya miaka minane,
jambo ambalo linadhihirisha ukubwa wa tatizo. Anasema licha ya jitihada mbalimbali zinazotolewa na serikali
katika kuhakikisha watoto wanapata huduma bora za matibabu, hadi sasa idadi ya
watoto wanaougua ugonjwa wa selimundu ni kubwa. “Idadi ya wagonjwa wa selimundu inaongezeka siku hadi siku,
juhudi za ziada zinahitajika ili kuhakikisha wanapatiwa matibabu bora,”
anasema. Anasema watoto wanaougua ugonjwa huo, baadhi yao wanapitia
changamoto nyingi ikiwamo kukimbiwa na mzazi mmoja au unyanyapaa. Anasema wazazi wengine huamua kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji
wakiamini kuwa wamerogwa, jambo ambalo si kweli. Anasema hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya watoto
wanaofikishwa hospitalini kulelewa na mzazi mmoja. “Kwa sababu ugonjwa huu unahusisha udumavu wa ukuaji wa
ubongo na maradhi ya mara kwa mara, baadhi ya wazazi wanaamua kuwakimbia wake
zao na wengine kuwapeleka kwa waganga. Hii imechangia wengi wao kuletwa
hospitali wakiwa kwenye hatua mbaya,” anasema. Anasema katika za Marekani na India, mtoto mara baada ya
kuzaliwa anafanyiwa vipimo maalumu ‘screening’ ili kubaini matatizo aliyonayo, hii
huwasaidia kuanza matibabu mapema pindi anapobainika kuwa na matatizo. Dk. Karashani anasema Chuo cha Afya ya Tiba Muhimbili (Muhas)
walifanya utafiti kuhusiana na vipimo hivyo maalumu ‘screening’ katika
hospitali za Temeke na Mwananyamala na kufanikiwa. “Kwa mfano, baadhi ya hospitali binafsi nchini, wanaweka
‘full package’ ya mjamzito na gharama za malipo yake ikiwamo ya kumfanyia
‘screening’ mtoto mara baada ya kuzaliwa, hali ambayo inasaidia kujua matatizo
yanayomsumbua,” anasema. Anasema vipimo hivyo ni muhimu kwa sababu vinasaidia kujua
maradhi ambayo mtoto anaweza kuzaliwa nayo. Dk. Karashani anasema ili waweze kupiga hatua zaidi ya kuwatibu
watoto, Serikali inapaswa kuboresha sera zake na kuanzisha mpango maalumu wa
kuwafanyia vipimo maalumu watoto hao mara baada ya kuzaliwa. Anasema kuboreshwa kwa sera hizo kutasaidia kuwalazimisha
wajawazito kulipia gharama za matibabu zikiwamo za kuwafanyia screening watoto
wakiwa wachanga. Anasema hiyo itasaidia kutambua matatizo ya mtoto kuanzia
tumboni hadi anapozaliwa, jambo ambalo pia linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo. Anasema lakini pia serikali inapaswa kuanzisha utaratibu wa
utoaji wa elimu kwa wagonjwa wa selimundu kuanzia ngazi ya mtaa ili kuhakikisha
elimu ya ugonjwa huo inawafikia watu wengi zaidi. Hii itapunguza unyanyapaa na kuondoa imani potofu na kudhani
kuwa wamerogwa. Mmoja wa wazazi aliyezungumza na gazeti hili, Amina Omary,
ambaye mtoto wake wa umri wa miaka mitano anasumbuliwa na maradhi haya, anasema
awali alikua hajui kama ana ugonjwa huo hivyo alimpeleka kwa mganga wa kienyeji
ili kupatiwa matibabu. “Nilipojifungua mwanangu alikuwa anaumwa mara kwa mara
pamoja na kukaukiwa damu, nilidhani amerogwa, nikaanza kuhangaika kwa waganga
tofauti ili kutafuta tiba, lakini hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya mtoto
kuendelea kuugua,” anasema Amina. Anaongeza kuwa, wakati anaendelea kuhangaika kutafuta tiba ya
mtoto wake, mzazi mwenzie aliamua kumkimbia hivyo akawa katika mazingira magumu
huku akihangaika mwenyewe ukizingatia kuwa hana kipato cha kutosha. Anasema mwishowe aliamua kurudi hospitali na kuanza vipimo,
ndipo mtoto wake alipogundulika kusumbuliwa na selimundu, akatakiwa kuanza
matibabu haraka kwa sababu alikuwa amechelewa. “Mimi na familia yangu tulidhani mwanangu amerogwa hivyo
nikaamua kwenda kwa waganga, tuliposhindwa tukarudi hospitali na kuanza vipimo
ndipo alipogundulika kwamba anaumwa selimundu,” anasema. Anasema katika kipindi chote hicho, baadhi ya ndugu, jamaa na
familia walikuwa wanamnyanyapaa mtoto wake kwasababu ya maradhi yanayomsumbua. Anaiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuanzia ngazi ya
vijiji ili kila mmoja aweze kuujua ugonjwa huo na dalili zake, hii itasaidia
kuwafikisha watoto mapema hospitalini. Naye Mariam Hussein ambaye mwanawe hana ugonjwa huo, anasema
elimu kuhusu selimundu haijatolewa vya kutosha, ndio maana wananchi hukimbilia
kwa waganga wakidhani wamerogwa. “Mimi mwenyewe sina elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo,
ndio maana tunapoona mtoto anaugua mara kwa mara tunaamini karogwa,” anasema. Anaongeza: “Ikiwa watapatiwa elimu ya kutosha, itasaidia wazazi
wengi kuwahi hospitali na wanaume kushindwa kuwakimbia wake zao.” | 5 |
Vijana hao wa Hans van Pluijm na Charles Boniface Mkwasa, wanashuka dimbani wakitoka kuifunga Coastal Union mabao 8-0 katikati ya wiki hii na kujiwekea historia ya kufunga ya kuwa timu iliyoshinda mechi moja kwa mabao mengi katika msimu huu wa 2014/15 unaoelekea ukingoni.Yenyewe Mbeya City yenye makazi yake jijini Mbeya, katika mchezo wake dhidi ya Azam FC katikati ya wiki, ililazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na leo ita kuwa Uwanja wa Taifa, kusaka pointi tatu za kuiweka pazuri zaidi kuliko ilivyo sasa.Aidha, Yanga na Mbeya City zinakutana kwa mara ya pili, baada ya mzunguko wa kwanza kukutana kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.Mbeya City ni timu ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa inaongoza kwa sare 10 baada ya ndugu zao, Tanzania Prisons kuongoza kwa sare 11 kabla ya michezo ya jana.Wakati Yanga ikiongoza kwa pointi 43, Mbeya City wana pointi 25 wakiwa katika nafasi ya nane, lakini timu hiyo ya Mbeya ikiwa mbele kwa kucheza michezo 21 huku Yanga wakicheza 20.Timu zote mbili zimelenga kushinda mchezo wa leo ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri. Mbeya City ambao walianza vibaya msimu huu, kwa sasa wako vizuri na waliwabana mabingwa watetezi Azam FC kwenye uwanja wao wa nyumbani kwani wamekuwa wakionesha hamu ya kutaka ushindi.Itaingia Uwanja wa Taifa ikipania kushinda, lakini itakuwa na kazi ngumu dhidi ya Yanga iliyo katika kiwango bora kwa sasa huku wachezaji wake wa safu ya ushambuliaji Simon Msuva, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima wakiwa katika viwango vyao vya ubora.Katika kiungo, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’ wako vizuri, sawa na safu yao ya ulinzi chini ya nahodha Nadir Haroub na kipa wao, Ally Mustapha ‘Barthez,’ hivyo Mbeya City ambayo msimu uliopita iliingia ligi kwa kishindo na kumaliza nafasi ya tatu, itabidi ifanye kazi ya ziada kutokana na pointi Taifa leo.Mchezo wa leo utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ambao wanatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho mwishoni mwa wiki ijayo dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia kwenye Uwanja wa Taifa.Mechi nyingine itakayochezwa leo ni Stand United wakiwakaribisha maafande wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Katika mchezo wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.Polisi Morogoro ambao walianza vizuri Ligi Kuu, kwa sasa hawako katika hali nzuri, hadi kusababisha aliyekuwa kocha wake, Mohamed Rishard ‘Adolf’ kutimuliwa.Ni timu ambayo iko katika hatari ya kushuka daraja kwani inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 21 wakati Stand United inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 24, nayo ikiwa haina uhakika wa kubaki Ligi Kuu. | 2 |
Na Tiganya Vincent SERIKALI mkoani Tabora imeliagiza jeshi la polisi kuendesha ukaguzi wa magari yote yanayotoa huduma za usafirishaji wa abiria kuhakikisha mabovu yanazuiwa kutoa huduma hiyo. Kauli hiyo ilitolewa wilayani Sikonge baada ya ajali mbili za basi la Kampuni ya Adventure iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na la Kampuni ya HBS. Ajali hizo zilitokea hivi karibuni. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema hatua hiyo itasaidiz kuzuia ajali zinazototokea kutokana na ubovu wa vyombo hivyo. Alisema baada ya kuangalia gari la HBS namba T960 AHH, bodi yake ilionekana imechakaa ingawa lilikuwa linaendelea kutoa huduma ya usafiri. Alimwagiza Kamanda wa Polisi Usalama wa Barabarani Mkoa wa Tabora (RTO) kuanza mara moja ukaguzi wa magari yote ya abiria kila siku. Mwanri alisema haiwezekani magari mabovu yaendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na kuendelea kuhatarisha maisha ya watu. Alisisitiza kuwa gari lisiruhusiwe kusafiri likiwa bovu hadi litakapofanyiwa maboresho ya kuondoa ubovu huo. Ilielezwa kuwa ajali ya basi la HBS ilisababishwa na uzembe wa dereva ambaye alijaribu kulipita gari jingine katika upande usioruhusiwa na kujikuta akiingia katika daraja na basi kupinduka. Tukio hilo lilisababisha abiria zaidi ya 20 kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge. Mmoja wa majeruhi wa gari hilo, Sada Shabani alikiri dereva wa gari lao hakuwa makini alipokuwa anapishana na gari jingine na kujikuta akiingia katika daraja, Alisema ajali hiyo ingeweza kuepukika kama dereva huyo angesubiri lori la mafuta lipite na yeye aendelee na safari yake. Wakati huohuo, Mwanri aliagiza jeshi la polisi kuwatafuta madereva wa mabasi yote mawili waliosababisha ajali na kukimbia ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria. | 1 |
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata na kumfi kisha mahakamani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (Chadema) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh milioni mbili kati ya Sh milioni 10 alizoomba.Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla mtuhumiwa huyo hajafikishwa mahakamani jana, Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali alisema Kimbe alikamatwa na maofisa wa Takukuru juzi katika Hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa.Kimbe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Isakalilo mjini Iringa, anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa mzabuni wa manispaa hiyo, Nancy Hassan Nyalusi anayefanya kazi ya kukusanya ushuru katika stendi ya mabasi ya mjini Iringa.Kilimali alisema Meya huyo alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa kwenye gari yake aina ya Nadia yenye rangi ya maroon ikiwa na namba za usajili T456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegeshea magari ndani ya hoteli hiyo ya Gentle Hills.Katika hatua nyingine, Kimbe aliyekuwa akishikiliwa na Takukuru tangu akamatwe juzi jioni, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa jana majira ya saa saba mchana.Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Liad Chamshana, mwanasheria wa Takukuru, Lestituta Kessy alisema Kimbe (42) anatuhumiwa kwa mashtaka mawili ya rushwa kinyume na Kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.Alitaja shitaka la kwanza kuwa ni kushawishi kiasi cha Sh milioni 10 kutoka kwa Nancy Nyalusi kama zawadi ya kumpatia mkataba wa kukusanya ushuru katika maeneo ya stendi kuu ya mabasi mjini Iringa kitu ambacho kina mahusiano na kazi za mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.Katika shitaka la pili, Kimbe anatuhumiwa kama Meya wa Manispaa ya Iringa kujipatia Sh 1,990,000 kutoka kwa Nancy Nyalusi kama zawadi baada ya kumpatia mkataba wa kukusanya ushuru katika stendi ya mabasi. | 1 |
Mkuu wa Upelelezi wa wilaya, Charles Chalula, alipoulizwa juu ya tukio hilo jana alikiri taarifa kufika ofisini kwake, na tayari jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo mhudumu wa hoteli hiyo. Pia alisema atawasiliana na mkurugenzi wa hoteli hiyo, aliyemtaja kwa jina moja la Haule ili aweze kurudisha fedha za wachezaji, ambazo walilipa kukaa hapo hadi Mei 2 mwaka huu michezo itakapokamilika.“Ni kweli wachezaji wamekuwa na hofu na usalama wao na mali zao, nitamtafuta mmiliki wake akiwezekana arudishe fedha zao leo hii hii (jana) ili waweze kuhamia hoteli nyingine, ila nitahakikisha suala la upelelezi tunalifanya haraka ili hivi vitu vilivyoibwa vipatikane haraka,” alisema Chalula.Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo gazeti hili, wizi huo ulitokea majira ya saa 10:00 jioni wakati wengi wa wachezaji hao wakiwa Uwanja wa Jamhuri kuishangilia timu ya soka soka iliyokuwa inapambana na CDA ya hapa. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.Mbali ya soka, wachezaji wengine wa Uchukuzi ni wa michezo ya kuvuta kamba, bao, drafti na karata. Mmoja wa wachezaji hao, Ally Suleiman katika chumba chake ameibiwa kompyuta mpakato yenye thamani ya Sh milioni 1.2, fedha taslimu Sh 120,000 na mashine inayohifadhia nyaraka mbalimbali yenye thamani ya Sh 180,000.Suleiman aliyefungua kesi ya wizi iliyopewa jalada namba IR/3844/2016 pia aliibiwa vitu mbalimbali ikiwemo kadi ya Bima ya Afya na leseni ya udereva.Mchezaji mwingine, Tracius Dionis alisema wezi hao waliingia chumbani kwake na kutawanya vitu kwenye begi lake, lakini hawakuiba chochote zaidi ya kuchukua seti ya televisheni, mali ya nyumba hiyo ya kulala wageni.Aliongeza kuwa, walifungua chumba cha mchezaji mwingine, Aminiel Ombeni ambaye amesafiri kwenda Moshi kuzika baada ya kupata msiba wa mama yake, na bado haijajulikana vilivyoibwa kwani begi lake lilikutwa katika chumba cha mteja aliyefika juzi mchana.Naye Katibu Mkuu wa timu ya Uchukuzi, Alex Temba alisema wamesikitishwa na tukio hilo kwani haijawahi kutokea katika mikoa yote waliyowahi kushiriki michezo ya Mei Mosi.Temba aliomba jeshi la polisi kuonyesha ushirikiano kama lilivyoahidi siku ya kwanza timu ziliporipoti mkoani hapa kuwa watatoa ulinzi mkubwa, basi watekeleze ahadi yao kutokana na wachezaji wote ni wageni mkoani hapa.“Suala hili limetusikitisha sana huyu ni mfanyakazi mwenzetu pamoja na kwamba tupo katika suala la michezo lakini aliendelea na kazi za ofisi na jana tu alikuwa akituma taarifa mbalimbali, basi tunawaomba polisi watusaidie hivi vitu vipatikane, na hata waongeze ulinzi kwani ni tukio la aibu kuwaibia wageni,” alisema Temba. | 2 |
OSCAR ASSENGA, TANGA Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema kuwa ifikapo Januari mwakani viwanja vyote nchini vitatumia mfumo wa kieletroniki katika ukataji tiketi za kuingia uwanjani. Karia amesema hayo leo Desemba 1 alipofungua mkutano wa baraza kuu la TPLB lililofanyika mjini Tanga. Amesema wataanza mazungumzo na Chama cha Mapinduzi pamoja na Halmashauri mbalimbali zinazomiliki viwanja ambavyo hutumiwa na baadhi ya timu za zinzaoshiriki Ligi kuu bara. “Labda niwaambie kwamba viwanja vyote hapa nchini ifikapo Januari vitatakiwa kuwa na mashine kwa ajili ya ukataji wa tiketi na zoezi hilo litaanza mazungumzo na halmashauri pamoja na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” amesema Rais Karia. Karia amesema zoezi hilo litafanyika kama linavyofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Uhuru, Chamazi na Taifa vya jijini Dar es Salaam. | 2 |
TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa sasa ipo nchini Misri ambapo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21. Kikosi kilikuwa na jumla ya wachezaji 39 awali ambapo mchujo wa kwanza ulichuja wachezaji saba na mchuju wa pili ulichuja wachezaji 9 na kufanya wachujwe jumla ya wachezaji 16 na kufanya wabaki wachezaji 23. Mchujo Wachezaji saba walioachwa kwenye kikosi kabla ya kukwea pipa ulikuwa namna hii 1. Ibrahim Ajibu- Yanga
2.Jonas Mkude- Simba
3.Ally Ally -KMC
4.Shomari Kapombe- Simba
5.Ayoub Lyanga- Coastal Union
6.Kenedy Wilson- Singida United
7.Kassim Khamis- Kagera Sugar Wachezaji tisa walioachwa kutoka kwenye kikosi kilichokwea pipa mpaka kambini nchini Misri ni:- 1. Claryo Boniphace – U20.
2. Selemani Salula – Malindi FC.
3. David Mwantika – Azam FC.
4. Abdi Banda – Baroka FC
5. Fred Tangalu – Lipuli FC.
6. Miraji Athuman – Lipuli FC.
7. Shiza Kichuya – ENPPI.
8. Shaban Chilunda – Tenerife.
9. Kelvin John – U17. Hawa hapa ndio watakaoshiriki Afcon | 2 |
Na CLARA MATIMO- MWANZA WATOTO 45 wamekatiwa bima ya afya na Shirika la Foundation Dart linalosaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mwanza. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi watoto hao bima hizo katika kituo cha afya Buzuruga jana, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dorocella Reuben, alisema hiyo ni zawadi muhimu kwa walengwa kwa kuwa sasa watakuwa na uhakika wa matibabu endapo wataugua. Alisema tangu shirika hilo lianzishwe mwaka 2012, limekuwa likitoa misaada mbalimbali kwa watoto wa kike ambao wanaishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kielimu kwa kuwanunulia vifaa vya shule, kuwalipia ada na mafunzo ya ufundi, lakini wanapougua huingia gharama kubwa kwa ajili ya kuwapatia matibabu. “Tulikaa na viongozi wenzangu tukatafakari tukaona ni bora tuwakatie bima watoto wetu hawa ili wawe na uhakika wa matibabu, tumeanza na hawa wachache lakini tutaendelea kuwakatia wengine kadiri Mungu atakavyotuwezesha, naomba Watanzania wenzangu wenye uwezo wawatafute watoto ambao familia zao hazijiwezi wawakatie bima. “Tumeamua kuwakabidhi leo hizi bima zao ikiwa tunaelekea katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpaya kama sehemu ya zawadi za shirika kwao, maana hakuna zawadi kubwa kama ya uhai, unapokuwa na bima una uhakika wa kuokoa maisha,” alisema. Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga, Dk. Masoud Masele, alipongeza shirika hilo kwa kuwakatia watoto hao bima hizo za afya zenye thamani ya Sh 180,000. Alisema hivi sasa watakuwa na uhakika wa kupata matibabu katika hospitali zilizo ndani ya Manispaa ya Ilemela. | 1 |
Mwandishi Wetu-Dodoma SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kuwa limefanikiwa kuokoa
zaidi ya Sh bilioni 23.5 ambazo zilikuwa zikitumika kila mwaka kuendeshea
mitambo ya umeme. Pia katika kipindi cha miaka minne shirika hilo limeweza kupata megawati
400 za ziada ambazo awali hazikuwepo. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dodoma kuhusu mafanikio ya
miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano,
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, alisema kuwa fedha
hizo zilikuwa zinatumika katika uendeshaji wa mitambo ya kusukuma umeme katika
vituo mbalimbali hapa nchini. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Mtwara, Tunduru, Namtumbo, Songea, Madaba,
Ruvuma na Liwale ambavyo vyote hivyo
awali vilikuwa vikitumia mafuta kupeleka umeme maeneo mbalimbali hapa
nchini. “Tunashukuru sasa hivi tumefanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha
tokea mwaka 2018, na tunaamini tutazidi kupiga hatua kwa hii miradi
tunayoifanya,” alisema Dk. Mwinuka. Alisema shirika hilo limeongeza ukusanyaji wa mapato hadi kufikia Sh trilioni
1.53. kutoka Sh trilioni 1.2 mwaka 2012/13. Dk. Mwinuka alisema mafanikio mengine waliyoyapata ni kwenye ufuaji wa umeme, ununuzi, usafirishaji
pamoja na eneo la uwekezaji. Alisema kuacha kufua umeme kwa kutumia mafuta, kumetokana na
uwekezaji ambao wameufanya ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta hiyo. Mbali na hilo, alisema ili kutatua changamoto za umeme Dar es Salaam
wamefanikiwa kuboresha kituo cha Ubungo cha kupooza umeme kutokana na kuzidiwa. “Hivi karibuni tumeboresha kituo cha Ubungo, kutokana na mahitaji ya
jijini kuwa makubwa na kusababisha kituo kuzidiwa na megawati 240, hii
imesaidia kutatua tatizo la umeme,” alisema Dk. Mwinuka. Alisema wamefanikiwa kufunga transfoma mpya ambayo ina wezo wa
kufanya kazi katika maeneo mbalimbali tofauti na ilivyokuwa awali. Dk. Mwinuka alisema kuwa mwaka 2015 mita zilizofungwa ni 1,648,386
ambapo hadi kufikia mwaka jana mita zilizofungwa ni 2,700,682 sawa na ongezeko
la mita 1,052,292 sawa na asilimia 63.84. Alisema Mtwara kulikuwa na tatizo la umeme na wameweza kuongeza
mitambo miwili ya gesi asilia yenye KV 4. Dk. Mwinuka alisema katika kipindi cha miaka minne wameweza kupata megawati
400 za ziada ambazo awali hazikuwepo. “Kwa ujumla kwa kipindi cha miaka minne tumeweza kupata megawati 400
za ziada ambazo hatukuwa nazo kabla ya 2015,” alisema Dk. Mwinuka. Alitaja mafanikio mengine ni kushuka kwa gharama za umeme kuanzia
mwaka 2016 katika maeneo ya malipo ya huduma pamoja na gharama za maombi. “Ilikuwa ukitaka kuomba umeme ilikuwa lazima ulipie, hata gharama ya
uniti moja iliteremshwa kutoka 2.4 hadi 1.5 kwa uniti na ilitegemea na mteja wa
aina gani na hilo ni moja ya fanikio katika huduma yetu ya umeme,” alisema Dk.
Mwinuka. | 1 |
Derick Milton, Simiyu Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amesema wamepata taarifa kuwa
baadhi ya wasambazaji waliopewa dhabuni
ya kusambaza viuatilifu vya kuua wadudu kwenye zao la pamba wanaihujumu
serikali. Bashe amesema kuwa wamegundua wasambazaji hao wamekuwa wakiuzia serikali
dawa hizo kupitia bodi ya pamba kwa bei kubwa kuliko wanavyowauzia watu wenye
maduka ya kuuza viuatilifu hivyo. Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akipokea chupa 13,000 za viuatilifu vya
pamba kutoka bodi ya pamba kwa ajili ya kuwapatia wakulima wa Mkoa wa Simiyu. Bashe amesema kuwa wamegundua kuwepo kwa hujuma hizo, kwani viuatilifu
hivyo vinavyouzwa kwenye maduka hayo bei yake imekuwa rahisi, kuliko
vinavyouzwa na bodi ya pamba nchini. Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri huyo ameiagiza bodi ya pamba, kufanya
operesheni kali kwenye maduka yote yanayouza dawa hizo kuangalia kama bei ya viuatilifu
inayotumika inalingana na ile ambayo wanatumia bodi. “Hatuwezi kuwa na wasambazaji wa aina hii, waliomba wenyewe tukawapa
masharti, lazima wayatekeleze, hatuwezi kuendelea kumkandamiza mkulima, bodi ya
pamba ifanye opereisheni kila duka kuangalia bei za uko,” amesema Bashe. | 1 |
Aidha uzinduzi huo umeenda sanjari na kutoa huduma stahiki na bidhaa halisi za kampuni hiyo zinazouzwa na kupata waranti ya miaka miwili endapo bidhaa hizo zitaharibika.Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo nchini, Mike Seo wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa bidhaa hizo pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa duka hilo.Alisema lengo la kufungua duka hilo ni kukidhi mahitaji ya wateja wa kampuni hiyo kwani Arusha ni mji wa kiuchumi, kitamaduni pia ni kitovu cha utalii na diplomasia Afrika Mashariki.Naye Mikidad Mubaraka ambaye ni moja kati ya wadau wa kampuni hiyo, alisema lengo la kuzindua kituo hicho jijini hapa ni kusogeza huduma karibu na wateja na kuboresha mahusiano ili wateja kununua bidhaa halisi badala ya kukimbilia bidhaa feki.Aliongeza kuwa teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu zaidi ya 236,000 kwenye inchi 79 na inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye teknolojia mpya ya matumizi ya simu za kisasa na luninga. | 0 |
IMEELEZWA kwamba, kitendo cha baadhi ya madaktari kukataa kutoa ushahidi mahakamani na polisi kushindwa kufanya uchunguzi unaojitosheleza ni miongozni mwa vikwazo kwa kesi za udhalilishaji wa kijinsia kushindwa kusikilizwa kwa wakati.Hayo yalisemwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makame Mshamba, baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa mikoa ya Kaskazini Unguja na Mkoani Pemba juzi.Alisema baadhi ya madaktari wamekuwa wakisumbua kutoa ushirikiano, huku wakikataa kufika mahakamani wakati wanapotakiwa kutoa ushahidi kwa mtu aliyefikwa na tukio la udhalilishaji wa kijinsia ikiwamo kubakwa au kulawitiwa. Alisema ni kosa kwa mtu anapoitwa mahakamani kutoa ushahidi kukataa wito huo na inachukuliwa ni sawa na kukwamisha Mahakama kutekeleza majukumu yake.“Madaktari wanatusumbua sana katika uendeshaji wa kesi zetu kwa sababu wamefanya kazi ya uchunguzi wa kitabibu kwa muathirika sasa wanapoitwa waje wathibitishe mahakamani hawataki, hii si sawa,” alisema.Alisema zipo baadhi ya kesi zimekwama kwa sababu ya kushindwa kupatikana kwa ushahidi kutoka kwa madaktari waliofanya kazi ya kupima mtu aliyedhalilishwa. Alipoulizwa kwa nini madaktari hao wanakataa kufika mahakamani kutoa ushahidi wa mtu waliyemfanyia uchunguzi, alisema wanadai kwamba hiyo si kazi yao.Naye ofisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Rashida Ahmed, alisema baadhi ya kesi zinazowasilishwa kutoka Jeshi la Polisi uchunguzi wake kwa kiasi kikubwa huwa haujakamilika huku ukiacha maswali mengi ya msingi yanayotakiwa kufanyiwa kazi.“Tunaletewa baadhi ya kesi za udhalilishaji wa kijinsia kutoka polisi lakini uchunguzi wake kwa kiasi kikubwa huwa haujakamilika na ndiyo maana tunazifuatilia zaidi kwa kutaka kujua mambo ya ziada,” alisema.Kwa mujibu wa taarifa fupi ya uchunguzi wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia iliyofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, matukio hayo yamekuwa yakiongezeka ukiwamo ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume na wanawake visiwani hapa. | 1 |
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Tava, Agustino Agapa alisema wachezaji wa wavu ufukweni hawana gharama kutokana na kuwa timu inaundwa na wachezaji wawili pekee.“Ni wakati muafaka kwa makocha wetu katika mikoa mbalimbali kutafuta vipaji ambavyo vitashiriki katika mchezo huu ambao ni mzuri kwa watalii kwa kuwa huchezwa ufukweni zaidi,” alisema.Alisema pia kuwa hata ikihitajika kusafirishwa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ni rahisi kuwamudu kwa gharama na kufanya vyema. Mwenyekiti huyo alisema katika kuhakikisha mpango wa kuibua vipaji unafanikiwa walifanya mafunzo hivi karibuni kwa makocha 27 wa Dar es Salaam na mikoani na kuwaelimisha kuhusu mchezo huo.Alisema makocha hao walielimishwa namna ya kufundisha mchezo huo, hivyo anaamini wataenda kutengeneza timu zitakazoleta ushindani katika ligi ya kitaifa.Agapa alisema mchezo huo bado ni mchanga lakini iwapo utatumiwa vyema ni sehemu ya kuvutia utalii hasa katika hoteli zinazojengwa katika fukwe mbalimbali. | 2 |